Ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kilele ni tarehe 8 ya mwezi Machi kila mwaka,wadau mbali mbali wamekutana jijini Dodoma kujadili na kutathimini mustakabali wa juhudi za ukombozi wa mwanamke nchini kuelekea miaka 25 ya mkutano wa Beijing mwaka 2020.
Warsha hiyo siku moja ambao iliyowakutanisha washiriki zaidi ya 100 kutoka kote nchini wakiwemo wadau mbalimbali likiwajumuisha wanawake kutoka wakiwakilisha makundi mbalimbali,wabunge,madiwani,wanasheria,waandishi wa habari pamoja na wanafunzi wa vyuo na sekondari,iliandaliwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na TAWLA, Landesa, Msichana Initiative, Haki Ardhi, Haki Elimu, Care International na TAMWA.
Katika kuhakikisha kila mshiriki anachangia mawazo,ilitumika njia ya kuwagawa katika makundi na kujadili maana,uelewa,umuhimu,mitizamo pamoja na changamoto la azimio la Beijing katika jamii na nchi kiujumla ambapo miongoni mwa hoja zilizoibuliwa katika kuboresha jitihada za kuleta usawa wa kijinsia ni pamoja na elimu juu ya azimio bado inahitajika sambamba na ushirikishwaji wa jamii yote kwa ujumla sambamba na kueleza faida ya usawa wa kijinsia kuanzia ngazi ya familia ili kutengeneza kizazi chenye kuelewa manufaa yake.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanasimamiwa na kauli mbiu inayosema “Badili fikra kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu”.
Sehemu ya washiriki wa warsha ya siku moja iliyolenga kutathimini mustakabali wa juhudi za ukombozi wa mwanamke nchini kuelekea miaka 25 ya mkutano wa Beijing mwaka 2020.
Mwenyekiti wa TGNP Mama Assen Muro akitoa rai kwa wadau wote kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi wa changamoto zinazosimama kama vikwazo ili wanawake waweze kupiga hatua katika kufikia maendeleo endelevu.
Mwenyekiti wa TGNP Mama Assen Muro akimueleza jambo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa alipowasili kwenye warsha hiyo.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa akizungumza na washiriki wa warsha hiyo ambapo aliwahimiza kutorudi nyuma katika jitihada za kutetea haki na nafasi ya mwanamke katika jamii.






Washiriki wakifuatilia kwa karibu mawasilisho.
Mdau wa masuala ya wanawake ambaye pia ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Rachel Chibwete akiwasilisha majibu kwa niaba ya kundi lililojumuisha wabunge,madiwani pamoja na waandishi wa habari.
Wanafunzi kutoka shule ya sekondari Manchali iliyopo Chamwino jijini Dodoma wakicheza kuashiria furaha yao kutokana na fursa ya kushiriki katika warsha hiyo.

Washiriki wakishikana mikono kama ishara ya umoja na mshikamano ambayo kwa pamoja waliafiki kuwa ni nguzo muhimu katika kufanikiwa kuitetea nafasi ya mwanamke katika jamii.
Sehemu ya washiriki wakipata picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa
0 comments:
Post a Comment