Sunday, 31 March 2019

Video Mpya : VAN - BINAGA

Ninakualika kutazama video ya wimbo mpya wa msanii Van inaitwa Binaga...Itazame hapa chini...
Share:

Picha : TIMU YA WAKONGWE 'SHYTOWN VETERAN' YAZINDULIWA RASMI UWANJA WA CCM KAMBARAGE

Timu ya wakongwe (Shytown Veteran Sports Club) imezinduliwa rasmi kwenye Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mjini, kwa kufanya Bonanza la michezo ambalo limeshirikisha timu za wakongwe kutoka mikoa mitatu Tabora, Simiyu pamoja na wenyeji Shinyanga Veteran. Uzinduzi huo umefanyika leo, Machi 31,2019...
Share:

SIMBA SC WAITWANGA MBAO 3 - 0

Dakika 90 za mchezo wa Ligi Kuu kati ya Simba na Mbao zimekamilika uwanja wa Jamhuri, Morogoro, kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0. John Bocco alianza kufunga bao la kuongoza kwa Simba dakika ya 24 akimalizia faulo iliyopigwa na Mohamed Hussein. Bocco alipachika bao la pili kwa Simba kwa...
Share:

Picha : AGAPE YATOA MAFUNZO YA SHERIA KWA WASAIDIZI WA KISHERIA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WASICHANA KWENYE MASOKO

Jumla ya Wasaidizi wa Kisheria 36 katika Masoko ya Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa mafunzo ya sheria na Shirika la Agape AIDS Control Programme ili wakasaidie kutoa elimu hiyo kwa wafanyabiashara kwa lengo la kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wasichana na wanawake wafanyabiashara sokoni.  Mafunzo...
Share:

CAG AKABIDHI RIPOTI 17 ZA UKAGUZI KWA RAIS MAGUFULI

Ripoti 17 za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2018 zimekabidhiwa rasmi kwa Rais Dk. John Magufuli. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT), ripoti hiyo imewasilishwa na CAG...
Share:

ASKARI ANUSURIKA KUFA POLISI WAKIUA MAJAMBAZI WATATU KIGOMA

Na Rhoda Ezekiel Kigoma. Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limewaua watu watatu wanaosadikikiwa kuwa ni majambazi waliokuwa wamejipanga kufanya uporaji katika baadhi ya nyumba za wananchi wilayani Kibondo. Akizungumza katika eneo la tukio Mkuu wa Wilaya ya Kimbondo,Louis Bura ambaye ni Mwenyekiti wa...
Share:

NEC YAPULIZA KIPENGA UCHAGUZI JIMBO LA JOSHUA NASSARI...UCHAGUZI MEI 19

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema uchaguzi mdogo katika jimbo la Arumeru Mashariki ni Mei 19, 2019. Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Machi 31, 2919 mkoani Morogoro amesema tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Tanzania ambaye...
Share:

Uteuzi Mpya Uliofanywa na Rais Magufuli Lro Jumapili March 31

Rais wa Tanzania, John Magufuli amemteua Adolf Ndunguru kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango anayeshughulikia sera. Taarifa  iliyotolewa leo Jumapili Machi 31, 2019 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imesema Ndunguru ameteuliwa kushika nafasi hiyo kujaza nafasi iliyokuwa...
Share:

Lugola Atangaza Vita Dhidi Ya Matrafiki Wala Rushwa Akifungua Kongamano La Taifa La Usalama Barabarani

Na Felix Mwagara, MOHA. WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka Askari Polisi Kikosi cha Usalama barabarani nchini, kusimamia sheria kikamilifu na kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kuokoa maisha ya watu wasio na hatia ambao hufariki, kupata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali. Akizungumza...
Share:

Rais Magufuli Kuanza Ziara Ya Kikazi Mkoani Mtwara.

Na Bakari Chijumba, Mtwara. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Dkt.John Pombe Magufuli, anatarajia kufanya ziara ya kikazi mkoani Mtwara kuanzia 02 April hadi April 04, Mwaka huu wa 2019 . Akizungumza na wanahabari leo Jumamosi 30 Machi 2019, mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema...
Share:

Mkurugenzi TAMWA Awasihi Wazazi Kuacha Kuwahamasisha Watoto Kujifelisha Mitihani Kwa Makusudi.

Na Bakari Chijumba,Lindi. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari  Wanawake Tanzania (TAMWA) Bi Rose Reuben, amewataka wanawake wa Ruangwa kubadilika na waweke juhudi katika kupinga kuishi kwenye maisha ya ukatili wa kijinsia. Aidha amewataka wazazi kuacha kuwanyima watoto haki ya kupata...
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya March 31

...
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger