Ajira Mpya za Walimu wa Sayansi ,Hisabati na Mafundi Sanifu
Walimu na mafundi sanifu watakao pokea posho ya kujikimu na baadae
kutoripoti na kuanza kazi katika vituo vyao vya kazi walivyopangiwa
watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene leo katika mkutano na
waandishi wa habari ofisini kwake mjini Dodoma juu ya ajira mpya za
walimu wa sayansi na hisabati awamu ya pili pamoja na mafundi sanifu wa
maabara kwa mwaka 2016/2017.
Alisema walimu hao na mafundi sanifu wa maabara ambao wamepangiwa
vituo vya kazi wanatakiwa kuripoti kuanzia tarehe 17 - 31 julai 2017
na kwa wale watakao pokea posho ya kujikimu na baadae kutoripoti
watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria .
� kumekuwa na tabia kwa baadhi ya watumishi wanaopangiwa vituo vya kazi
kupokea posho za kujikimu na kutokomea bila taarifa yoyote,hivyo basi
niwasihi wale wote waliopangiwa waripoti mapema ndani ya tarehe
hizo�alisisitiza
Waziri Simbachawene aliongeza kuwa watumishi hao wanatakiwa kufika
kwenye vituo vyao vya kazi wakiwa na vyeti halisi vya taaluma vya kidato
cha nne na cha sita,cheti halisi cha kitaalam cha kuhitimu mafunzo
katika ngazi husika na cheti cha kuzaliwa.
Vilevile alisisitiza kuwa walimu hao pamoja na wataalam wanatakiwa
kuripoti katika ofisi za Wakurugenzi wa Halmasahauri husika na baadae
kuripoti kwenye shule walizopangiwa na hakutakuwa na uhamisho ndani
ya Mkoa au Halmashauri.
Aidha Mhe. Waziri aliwataka Wakurugenzi wa Halmashauri ambazo walimu na
wataalam hawa wataripoti wawapokee kwa kuzingatia taratibu na kanuni
zote za utumishi na baadae kutoa taarifa mara baada ya tarehe ya mwisho
ya kuripoti.
Walimu hao pamoja na mafundi sanifu wa maabara wametokana na tangazo la
nafasi za kazi lilitolewa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia
mwezi aprili 2017 , ambapo kwa awamu ya kwanza walipatikana jumla
ya walimu 3,081 na kwa awamu hii Jumla ya walimu 381 na mafundi
sanifu wa maabara 137 wamechaguliwa .
Majina ya walimu na mafundi sanifu walioajiriwa yanapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI.
0 comments:
Post a Comment