Wednesday, 22 March 2017

Ripoti ya uvamizi Clouds hadharani: Makonda alitishia kuwaingiza kwenye skendo ya dawa za kulevya

...

Habari wakuu,
Ile kamati iliyoundwa na Nape Nnauye ya masaa 24 inawasilishwa leo, baada ya kuzungumza historia ya tatizo, msemaji anasema wamejaribu juhudi zote za kumpata mkuu wa mkoa wa Dar ikiwemo kumpigia simu na kumpelekea taarifa ofisi.



Kamati imesema waliitwa ofisi ya mkuu wa mkoa na kuelekezwa ngazi za kutumia, lakini mkuu wa mkoa alitumia ngazi nyingine kutoka ofisini kwake na kuwatoroka.

Amesema Makonda aliingia kwenye studio ambazo hakutakiwa kuingia, kamati imethibitisha kulikuwa na vitisho ikiwemo kushika silaha za moto na kuwatishia kuwafunga jela miezi sita.

Pia alitoa vitisho kuwa angewakagua kama wanahusika na dawa za kulevya au wadhamini. Alitoa vitisho kwa wafanyakazi waliokuwa zamu na kusisitiza iwapo wangesema kilichotokea, wangejua yeye ni nani.

Ni kweli kwamba Makonda ana kawaida ya kwenda Clouds, mgeni mwenyeji. Ameshawahi kukaa wakati wa kuandaa kipindi chake cha mwaka mmoja mpaka saa 10 alfajiri.

Kamati haikuona uthibitisho wa wafanyakazi kupigwa au kukatwa mitama isipokuwa waliolia walitishiwa kwenda jela miezi sita bila kupitia mahakama.

Paul Makonda anatakiwa kuomba radhi, Waziri Nape Nnauye awasilishe malalamiko kwa mamlaka yake ya uteuzi

Vyombo vya dola vichunguze askari wake kuingia studio na kuepusha tukio hilo kujirudia siku za usoni.

Clouds ipitie upya miongozo yake na kuzuia watu wanaoingia mara kwa mara chumba cha habari ilhali hawana taaluma ya uhariri.
==========

NAPE: Hata mimi nilikuwa napata presha kubwa, sikujua kama lingekuwa na presha kubwa hivi. Nitoe wito watanzania wakati mwingine kuwa wavumilivu, watu walisema mambo mengi sana jana.
Nimeipokea ripoti na kazi hii ina gharama sana ikiwemo ya kusimamia haki na ukweli.

Juu yangu kuna waziri mkuu, makamu na Rais mwenyewe, nitachofanya ni kukabidhi kwao wenyewe na kama kuna chochote cha kufanya, watafanya chochote. Tunalipwa kwa pesa za walipa kodi na wavuja jasho, niwaombeni wanahabari tuendelee kuwa wavumilivu, Rais ana nia njema na tasnia ya wanahabari na sheria ya vyombo vya habari imewezekana chini ya utawala wake.

Nina imani madhaifu yakitokea kwa mtu mmoja mmoja haiwi tope kwa serikali nzima. Nyinyi ni sehemu muhimu katika kufanikisha sera, tumuunge rais mkono.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger