Rais John Pombe Magufuli, anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa
barabara za juu (interchange), katika makutano ya Ubungo tarehe 20
Machi, 2017.
Rais wa Benki ya Dunia Mheshimiwa Dkt. Jim Yong Kim anatarajiwa
kushiriki katika sherehe hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la
‘interchange’ ya Ubungo.
Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imesema kuwa mradi huo wa ujenzi wa
barabara za juu katika makutano ya Ubungo utagharimu takribani shilingi
bilioni 188.71.
“Una lengo la kupunguza msongamano wa magari katika barabara za Morogoro, Nelson Mandela na Sam Nujoma,” ilisema taarifa hiyo
Mradi huu ni sehemu ya mradi wa uboreshaji usafiri Jijini Dar es Salaam
yaani (Dar es salaam Urban Transport Improvement Project),
utakaogharimiwa kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia na mchango wa Serikali
ya Tanzania.
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment