
' Biafra Stadium' Kinondoni.
Hapo wa pili kutoka kulia ni Brown Costa. Jamaa alikuwa mzuri sans uwanjani hadi akacheza ligi ya Zanzibar. Namwona anayefuatia ni Hamis Malumbo, mmoja wa magolikipa bora wa kiwango cha kuchezea ligi kuu. Hakukuwa na maskauti wa kumwona na kumsajili. Nawaona brothers Mwinyihamisi,ni akina Hoppa, Mohammed na Khatib.
Hapo wa pili kutoka kulia ni Brown Costa. Jamaa alikuwa mzuri sans uwanjani hadi akacheza ligi ya Zanzibar. Namwona anayefuatia ni Hamis Malumbo, mmoja wa magolikipa bora wa kiwango cha kuchezea ligi kuu. Hakukuwa na maskauti wa kumwona na kumsajili. Nawaona brothers Mwinyihamisi,ni akina Hoppa, Mohammed na Khatib.
Hawa
jamaa familia nzima walikuwa na kipaji cha kusakata soka akiwemo Mangapi
na mdogo wao mwingine jina limenitoka. Hapo kulikuwa na akina Abdul
Mweta tukimwita Abdu Kiwaka, huyu akaja kuichezea Simba Sc. Tulikuwa na
Amri Said, tukimuita ' Gotagota' .
Huyu
akaja kuwa beki imara wa Simba SC. Tulikuwa na Ladislaus Shawa. Huyu
aliwahi kuwashangaza watazamaji kwenye moja ya mechi zetu alipotoka
golini na mpira na kuwapiga chenga wachezaji wote wa timu pinzani na
hadi akabaki na kipa na kupachika bao.
Ladis,
ambaye alikufa kwa ajali ya pikipiki akaja kuichezea Sigara FC kwenye
ligi kuu. Naam, tulikuwa na wengi mahiri kiasi mwenyekiti wenu siku
nikiingizwa kutokea benchi, basi, hadi nyumbani niwaambie! Tumetoka
mbali.
Maggid.(P.T)
Maggid.(P.T)

Ndugu zangu,
Kuna wimbo huu wa mchakamchaka;
" Kambona , ah, ah!
Kambona, ameolewa!
Wapi?
Uko Ulaya!
Wivu?
Wamkereketa!"
Utotoni nilipata kuwasikia kaka zetu wakiimba wimbo huo wa mchakamchaka. Nikiwa shuleni nimesoma sana habari za siasa za wakati huo. Bado naendelea kusoma na kujifunza. Katika kusoma kwangu nimeona, kuwa suala la ugomvi wa Oscar Kambona na Julius Nyerere alikuwa rahisi vile kama tulivyoambiwa na hata kuimbiwa. Simulizi za Oscar Kambona zinabaki kwa wengi kuwa ni za upande mmoja.
Hakika, si wengi wenye kufahamu nini hasa kiliwatokea marafiki watatu hawa (Pichani) ; Julius Nyerere, Oscar Kambona na Rashid Kawawa. Kizazi hiki cha sasa cha Watanzania kinaweza kunufaika sana na uelewa wa yaliyojiri katika harakati za kisiasa za wakati huo zilizopelekea uhuru wa Tanganyika na baadae Oscar ' Kujivua' gamba kwa kutokubaliana na rafiki yake Julius juu ya Azimio la Arusha. Kuna maswali ya kujiuliza; Je, ugomvi wa Oscar na Julius ulianzia kwenye Azimio au kabla ya hapo?
Je, umma ulipotoshwa juu ya nini kilichotokea? Ikumbukwe, Oscar na Julius walikuwa marafiki wa kushibana kiasi cha Julius kuwa ' Mpambe' wa Oscar kwenye ndoa yake iliyofanyika London. Je, Rashid alichangia kwenye ' kutoswa' au ' kujitosa' kwa Oscar. Kwamba Oscar aliona hakupata kuungwa mkono na Rashid. Je, Oscar alifanya makosa kwa kuondoka nchini badala ya kubaki na kupambana kwa hoja na rafiki yake Julius?
Je, nianze kuwasimulia machache niliyojitahidsi kuyajua, au niwaache kwanza wengine msimulie mnayoyajua, maana, kuna wanaodhani wanajua na kuna wanaojitahidi kujua. Mie niko kwenye kundi hilo la pili!
Maggid,
Pesa zilizotumiwa kukarabati nyumba ya Zuma zilikuwa ni za mlipa kodi
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amerudisha pesa zilizotumiwa kukarabati nyumba yake binafasi jinsi ilivyoamriswa na mahakama.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anaripoti kuwa msemaji wa wizara ya fedha amethibitisha kuwa pesa hizo zimepokelewa.
Wizara ya
fedha nchini Afrika Kusini ilikuwa imependekeza kuwa Rais Zuma
alihitajika kurejesha dola 509,000 kwa serikali, pesa zilizotumiwa
kukarabati nyumba yake huko Nkandla.
Makao ya binafsi ya Zuma ya Nkandla
Mahakama
ya juu zaidi nchini humo ilikuwa imetoa uamuzi mapema mwaka huu, kuwa
Zuma alipe dola milioni 23 pesa za umma zizotumiwa kwa nyumba yake mwaka
2009.
Sakata ya Nkandla ilitishia wadhifa wake Zuma. Alikwepa hatua ya kumuondoa madarakani na shinikizo za kumtaka ajiuzulu.
Hata hivyo aliomba msamaha kwa njia ya runinga mwezi Aprili akisema kuwa suala hilo limeleta aibu.BBC
Mkurugenzi
wa kiwanda cha ukamuaji na usafishaji wa mafuta ya alizeti cha Mukta
Agro-Proccesing Co Ltd cha mjini Babati Mkoani Manyara, Bakari Mukta
akishika mwenge wa uhuru ulipofika kuzindua kiwanda hicho.(P.T)
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka mchana tayari kumwakilisha
Rais Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa
Sita wa Zambia Mhe. Lungu uwanja wa Mashujaa kesho Septemba 14, 2016
Baadhi ya
wafanyakazi wa TBL Group wakipokea tuzo kutoka kwa Ma Meneja wa viwanda
vya TBL Group walipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKN
wa jijini Dar es Salaam wakitokea nchini Afrika ya Kusini.
Baadhi ya
wafanyakazi wa TBL Group wakipokea tuzo kutoka kwa Ma Meneja wa viwanda
vya TBL Group walipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKN
wa jijini Dar es Salaam wakitokea nchini Afrika ya Kusini.
Ma Meneja na baadhi ya wafanyakazi katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa ndege wa Dar wa Salaam
-Bia ya Safari yatangazwa kinara kwa ubora barani Afrika
Kampuni
ya TBL Group imezidi kung’ara kimataifa kutokana na viwanda vyake vya
kutengeneza bia vilivyopo kwenye mikoa ya Dar es Salaam,Mbeya,Mwanza na
Arusha kushinda tuzo za juu za kimataifa za SABMiller kwa uzalishaji
bora ambapo pia bia aina ya Safari Lager imetangazwa kuwa ni bia bora
(Champion Beer) barani Afrika.
Kampuni
ya SABMiller imekuwa na utaratibu wa kushindanisha viwanda vyake
vilivyopo kwenye nchi mbalimbali na kutoa vigezo vya kushindania kigezo
kikubwa kimojawapo kikiwa ni ubora wa bidhaa zinazozalishwa .
Hafla ya
kutangaza viwanda vilivvoshinda na kuvipatia tuzo ijulikanao kama
SABMiller Africa Technical Awards ilifanyika jana nchini Afrika na
kuhudhuriwa na Maofisa waandamizi wa kampuni hiyo wakiwemo mameneja wa
viwanda vya bia kutoka kampuni zake tanzu.
Bia aina
ya Safari Lager iliyozalishwa katika viwanda vya TBL vya Dar na Arusha
ilitangazwa bia bora barani na kutunukiwa tuzo,kiwanda cha Dar kikiwa
kimeshika nafasi ya kwanza na Arusha nafasi ya pili.
Tuzo nyingine ambazo viwanda vya TBL Group vimeshinda ni tuzo ya uzalishaji wa bia bora ya Castle inayojulikana kama
Mick
Steward Castle Lager award ambapo kiwanda cha TBL Dar es Salaam
kimeshika nafasi ya kwanza,TBL Mbeya nafasi ya pili na TBL Arusha nafasi
ya tatu.
Nyingine
ni Tuzo ya Upishi Bora wa bia ya mwaka (Brewery of the Year
Award),ambapo kiwanda cha TBL Mbeya kimeshika nafasi ya kwanza na
kiwanda cha TBL Mwanza kimenyakua nafasi ya pili.Pia kampuni imeshinda
tuzo ya kufuata kanuni bora za Ununuzi na Ugavi (Supply Chain and
Planning award).
Mkurugenzi wa Ufundi wa TBL Group,Gavin Van Wijk amevipongeza viwanda vyote kwa kuibuka na ushindi wa tuzo kubwa za SABMiller.
“Ushindani
ulikuwa mkubwa ukihusisha viwanda vingine kutoka nchi mbalimbali
duniani,inafurahisha kuona viwanda vya Tanzania vinachomoza na kushinda
tuzo kama hizi,hii inadhihirisha kuwa TBL imejipanga kwenda sambamba na
mkakati wa serikali wa kuifanya Tanzania nchi ya viwanda kwa kuwa
mafanikio haya yanaletwa na watanzania wenyewe”.Alisema.
Wijk
aliwashukuru wateja wote wa bidhaa za TBL Group kwa kuiunga mkono
kampuni na aliahidi kuwa kampuni itaendelea kuzalisha bora wakati huo
huo ikishiriki kusaidia miradi mbalimbali ya kuboresha maisha ya
wananchi hususani katika sekta za kilimo,mazingira,elimu na afya.
Akiongea
kwa niaba ya Mameneja wa viwanda vya TBL Group vilivyoshinda tuzo,Meneja
wa kiwanda cha Dar es Salaam,Calvin Martin amesema wamefurahishwa kuona
viwanda vya Tanzania vinafanya vizuri na kutambuliwa kimataifa “Tuzo
hizi zinatokana na mchango wa kila mfanyakazi wa kampuni,tuzidi kuongeza
bidii katika kazi tutazidi kufanya vizuri zaidi na tunashukuru wateja
wetu wote kwa kutuunga mkono kwa kutumia bidhaa zetu ,tumejipanga
kuhakikisha wanazidi kupata bidhaa zetu kwa ubora mkubwa na kwa urahisi
popote walipo”.Alisema Calvin.
Wakati
huohuo,Mhandisi wa kitanzania,Richmond Raymond ,ambaye alikuwa ni Meneja
wa Kiwanda cha TBL cha Mwanza kwa sasa hivi akiwa amehamishiwa nchini
Afrika ya kusini kuwa Meneja wa Kiwanda cha bia cha Polokwane kilichopo
nchini Afrika ya Kusini ametunukiwa tuzo maalumu ya kutoa mchango
mkubwa kwa kampuni inaojulikana kama SABMiller Brewery Legend status
katika hafla hiyo.(P.T)
Wafanyakazi
wa Benki ya Azania tawi la Moshi ,wakishusha Mbuzi kwa ajili ya kutoa
zawadi ya siku kuu ya Idd kwa baadhi ya wateja wake pamoja na makundi
yenye mahitaji maalumu.
Meneja wa
Azania Bank tawi la Moshi ,Hajira Mmambe akimkabidhi zawadi ya Mbuzi
mwakilishi wa Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Jafary Michael , Bw ,Bashir
Seleman wa kampuni ya Zuhad kwa ajili ya siku kuu ya Idd.
Meneja wa
Azania Bank tawi la Moshi,Hajira Mmambe akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa
msimamizi wa kituo cha kulea watoto waishio kwenye mazingira magumu cha
Qadria kilichopo kata ya mji Mpya,Alhaji Taqdir Haji Amir kama sadaka
ya siku kuu ya Idd.
Baadhi ya watoto wa kituo cha kulelea watoto cha Qadria kilichopo kata ya Mji Mpya.
Meneja wa Azania Bank akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa mteja wa Benki hiyo Aman Idd Mushi kwa ajili ya siku kuu ya Idd.
Meneja wa
Azania Bank tawi la Moshi,Hajira Mmambe pamoja na wafanyakazi wa benki
hiyo wakikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa mwakilishi wa kampuni ya Ibra line
,Bi Mosi Shayo kwa ajili ya siku kuu ya Idd.
Meneja wa
Azania Bank tawi la Moshi,Hajira Mmambe akizungumza mara baada ya
kukabidhi zaadi ya Mbuzi kwa ajili ya siku kuu ya Idd kwa wateja wake
pamoja na makundi yenye mahitaji maalumu.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. (P.T)
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili
kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Airtel
Tanzania Bi. Beatrice Singano (wa pili kushoto) wakati akiwasili katika
Uwanja wa Karume kuhitimisha mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka
17 ya Airtel Rising Star Septemba 11, 2016 kushoto ni Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw. Jamali Malinzi.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na
wanamichezo, wadau wa michezo na wanahabari kabla ya kushuhudia fainali
ya mashindano hayo yiliyohitimisha mashindano hayo kwa Vijana chini ya
umri wa miaka 17 Airtel Rising Star katika Uwanja wa Karume Jijini Dar
es Salaam Septemba 11, 2016.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikagua
wachezaji wa timu ya Morogoro Boys kabla ya kuanza kwa fainali kati yao
na timu ya Ilala iliyofanyika katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es
Salaam Septemba 11, 2016.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikabidhi
kikombe kwa nahodha wa Timu ya wasichana ya Temeke walioibuka washindi
wa mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star
kwa upande wa wasichana katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam
Septemba 11, 2016.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akitoa hutuba katika swala ya Idd El Haji
iliyofanyika Viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi.
Swala ikiendelea.
Waziri Mkuu alivyojumuika na waislam wenzake katika swala hiyo.
Sheikh Abdu Kadri akiongoza swala ya Idd El Haji
Sheikh Nurudin Kishki akihutubia baada ya swala hiyo.
Waumini wa dini ya kiislam wakishiriki swala hiyo.
Waumini wa dini ya kiislam wakiswali.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062) (P.T)
More...
Tafuta Habari
Nafasi za Kazi & Masomo
Prev
Next
Video Gallery
Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.




Maoni ya Wanakijiji
-
TAZAMA MUONEKANO WA NDANI WA JENGO JIPYA LA J.K. NYERERE AIRPORT TERMINAL III JIJINI DAR
10.09Tuwe makini ku hakikisha habari Ki u ndani kabla hatuja tuma.. Hilo jengo sio la Airport ya Dar es ... -
Totoa kuku kwa mafuta ya taa tu! Oil Lamp incubator...
07.09Mnapatikana wapi na bei za mshine zikoje?. Niko kgm -
CUF Watoa Waraka Kwa Rais Magufuli
05.09Nadhani tatizo kubwa la hawa wanaopita wanasiasa nchini kwetu ni pale wanapowaona Watanzania ni watu ... -
Ama, Wahenga Walinena; Ndugu Wakigombana, Chukua Jembe Ukalime...!
29.08Mwenyekiti kuamini njia fulani katika kufika mahali fulani ni muhimu sana. Mosi hutakuwa mtu wa ... -
Mafunzo kwa picha: Nyonga na ndoto ya umbo lako
27.08Wow mafundisho ulio towa ya kutengeza umbo kwakweli nimeyapenda nimejaribu na yamenisaidia ni mazowezi ...























0 comments:
Post a Comment