Wanafunzi wote mliochaguliwa UDOM kwa masomo ya sayansi na hisabati bodi imefungua mlango,kwani mda wa kuomba mkopo umewekwa kuwa ni wiki 2,kuanzia tarehe 29,MPE TAARIFA MWENZAKO,SOMA TAARIFA HIYO HAPO CHINI,MASWAYETU BLOG TEAM TUNAWAPENDA SANA.
TAARIFA KWA WAOMBAJI WA MIKOPO WALIODAHILIWA KATIKA PROGRAMU MAALUM YA STASHADA YA UALIMU WA SAYANSI NA HISABATI
Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, itatoa mikopo kwa wanafunzi watakaodahiliwa katika programu maalum ya stashahada ya Ualimu wa Sayansi na Hisabati kuanzia mwaka wa masomo 2014/2015. Ili kutekeleza jukumu hilo, Bodi ya mikopo ilitoa mwongozo kwa waombaji hao na kuwataka kuomba mikopo hiyo kwa njia ya mtandao (http://olas.heslb.go.tz).
Hivyo, Bodi inapenda kuwakumbusha na kuwasisitiza waombaji ambao bado hawajafanya maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao kufanya hivyo ndani ya wiki mbili kuanzia tarehe 29 Septemba, 2014. Hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya muda huo kwisha.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
0 comments:
Post a Comment