Thursday 25 April 2024

WANAGDSS WAICHAMBUA BAJETI YA OFISI YA RAIS (MIPANGO NA UWEKEZAJI) NA KUBAINI HAIJAZINGATIA MASUALA YA JINSIA



NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WADAU mbalimbali wa masuala ya Jinsia na Maendeleo wamekutana katika Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) na kuichambua bajeti ya Ofisi ya Rais (Mipango na uwekeshaji) na kubaini kuwa haijazingatia masuala ya jinsia.

Akizungumza leo Aprili 24,2024 jijini Dar es salaam, wakati wa semina ambazo hufanyika kila Jumatano katika Ofisi za TGNP Mtandao, Mhadhiri Chuo Kikuu Mzumbe Lihoya Chamwali amesema uwekezaji ambao umekuwa unafanyika kwa wanawake haukuzingatiwa hasa kufufua viwanda ambavyo wanawake wamekuwa wakishiriki.

Aidha ameishauri serikali kutoa elimu kwa wananchi kuhusu maswala ya uwekezaji kwani elimu hiyo imekuwa haijulikani kwa watu wengi hasa wanawake.

"Tunaishauri serikali iweke mifumo rafiki na elimu itolewe ili kila mwanamke ambae anaweza kuwekeza aweze kuingia kwenye mfumo na ndio maana tunasisitiza elimu itolewe kwani mifumo mingi ya uwekezaji inafanyika kielektroniki kitu ambacho wanawake wanawake wamekuwa wanaachwa kwa sababu wengi hawana ujuzi wa elimu hiyo". Amesema Chamwali.

Amesema bajeti ya mwaka huu imekuwa ndogo tofauti ya mwaka jana kwani mwaka 2023 bajeti ilikuwa bilioni30 lakini mwaka huu bilioni 17.

Amesema kufuatia na upungufu huo wa bajeti katika kupitia malengo wameona malengo mengi ya mwaka huu ni muendelezo wa malengo yaliyofanyika mwaka jana ikiwemo kupitia uundaji wa sera ya dira ya maendeleo 2050.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kituo cha maarifa kata ya Majohe Tabu Ally ametoa rai kwa serikali kuwaangali wanawake waliopembezoni ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa elimu bora ya uwekezaji.

Amesema changamoto kubwa inayowakabili wanawake waliopembezoni ni miundombinu ya barabara kwani wanazalisha lakini wanashindwa kufika sokoni kutokana na uharibifu mkubwa wa barabara hivyo inawalazimu kutumia ghalama kubwa ili kufika sokoni jambo ambalo linawarudisha nyuma kimaendeleo.

"Kila kitu ili kiende ni lazima barabara zipitike na hiyo ndio changamoto ambayo sisi tunalia nayo lakini hata tukiwezeshwa mitaji bado tutashindwa kutokana na hii moundombinu",Amesema Tabu

Naye,Mdau wa maswala ya jinsia kutoka Kigamboni Ayub Sharif amesema serikali inapaswa kutoa kipaumbele kwenye maeneo ambayo nguvu kazi kubwa inatumika ili kuongeza motisha ya ufanyaji kazi.

"Mimi naishauri serikali kuangali maeneo ambayo nguvukazi kubwa inatumia ndio uwezeshaji uanzie kwani tumeona katika sekta ya madini wanawake ndio wachenjuaji wakubwa lakini madini yakipatikana anaenufaika mwingine hii sio sawa serikali inapaswa kuangali swala hili kabla ya kuwekeza kwenye mitambo waweke mazingira mazuri kwa hizi nguvu kazi". Amesema.
Share:

Wednesday 24 April 2024

WADAU WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA KILIMO IKOLOJIA HAI


Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Kilimo, Obadia Nyagiro,akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa Kilimo Ikolojia hai kilichoratibiwa chini ya mwamvuli wa Taasisi za Kilimo Hai Tanzania (TOAM) kilichofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa TOAM, Dk.Mwatima Juma,akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa Kilimo Ikolojia hai kilichoratibiwa chini ya mwamvuli wa Taasisi za Kilimo Hai Tanzania (TOAM) kilichofanyika jijini Dodoma.

Paul Holmbeck kutoka Shirika la Biovision Foundation,akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa Kilimo Ikolojia hai kilichoratibiwa chini ya mwamvuli wa Taasisi za Kilimo Hai Tanzania (TOAM) kilichofanyika jijini Dodoma.


Baadhi ywa wadau wa Kilimo Ikolojia hai wakifatilia majadiliano mbalimbali wakati wa kikao hicho kilichoratibiwa chini ya mwamvuli wa Taasisi za Kilimo Hai Tanzania (TOAM) kilichofanyika jijini Dodoma.


Na.Alex Sonna-DODOMA

WADAU wa kilimo ikolojia hai wamekutana jijini Dodoma kutengeneza mpango kazi wa mwaka 2024/25 kwa ajili ya utekelezaji vipaumbele vya Mkakati wa kitaifa wa kilimo hai wa ikolojia wa 2023-2030 (NEOAS) utakaoleta mageuzi ya kilimo nchini.

Akizungumza kwenye kikao hicho kilichoratibiwa chini ya mwamvuli wa Taasisi za Kilimo Hai Tanzania (TOAM), Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Kilimo, Obadia Nyagiro, alisema kilimo hicho ni muhimu kwa watanzania kwa kuwa kitaleta tija kiuchumi, kulinda afya za walaji, afya ya udongo na kuongeza kipato.

Alisema mkakati huo unatokana na Sera ya kilimo kuelekeza masuala ya kuweka mfumo wa uzalishaji, upatikanaji wa masoko na kutambua bidhaa za kilimo hai.

“Mkakati wenyewe ulizinduliwa mwishoni mwa mwaka jana na upo tayari kwa utekelezaji, kilichotufanya tukutane ni namna ya kutekeleza mkakati huu kwa kuandaa mpango kazi kila mwaka kwa muda wa miaka saba ya huu mkakati wa kitaifa, kama tulivyowashirikisha kwenye maandalizi yake lazima tushiriki sisi wadau kwa kuweka malengo ya utekelezaji wake kila mwaka,”alisema.

Alisema serikali itaendelea kutoa ushirikiano ili kufanikisha uandaaji wa mpango huo kwa kuwa ni muhimu wadau kushiriki katika kilimo himilivu na endelevu kwa mazingira na afya ili kuleta tija kwenye sekta ya kilimo.

Alizitaka asasi za kiraia na sekta binafsi kuchangamkia fursa ya uwekezaji katika kilimo hicho kwa kuwa kina tija kubwa.

“Nihimize sekta binafsi na asasi za kiraia mpitie na kuona fursa ya kuwekeza katika eneo hili kwa kuwa tija yake ni kubwa ikiwamo kuongezeka kwa mapato, mkipitia nchi nyingine mtaona waliowekeza kwenye kilimo hiki na tija yake na ni muhimu mipango yetu izingatie kilimo himilivu kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchini,”alisema.

Naye, Mwenyekiti wa TOAM, Dk.Mwatima Juma alisema kilimo hicho kinalenga kuwa na uzalishaji wa kutosheleza, kulinda afya na udongo kwa kuondokana na matumizi ya kemikali.

“Kilimo cha kutumia kemikali kilianza miaka 100 iliyopita baada ya kuisha kwa vita kuu ya pili ya dunia ambapo utengenezaji wa mbolea za kemikali, viuatilifu vya kemikali ilionekana itatusaidia kuzalisha chakula zaidi, tulihamasika kuwa kutumika kemikali ndo ukisasa na kwa bahati mbaya tuliacha kilimo chetu cha asili ambacho mtu alikuwa akilima kahawa ndani yake ana kunde,maharage, mtama vyote vinazalishika vizuri na ana ng’ombe anatupia mbolea shambani kwake.”

“Tukahamasisha tuwe na mashamba makubwa tulime zao moja, tupulize dawa miaka imekwenda na tulipofika mimi binafsi nasema tuwaombe radhi wakulima kwa maeneo tuliyowapeleka hasa wakulima wadogo hapafai, kuna aina ya ukulima wanaweza kulima bila kupunguza uzalishaji, bila kupata shida kwenye chakula na kuuza kwenye masoko ya ndani na nje,”alisema.

Alibainisha kuwa kilimo hicho kitasaidia watanzania kuondokana na maradhi mbalimbali ikiwamo uzazi, saratani kwa kuwa yanatokana na matumizi ya kemikali kwenye kilimo.

Naye, Paul Holmbeck kutoka Shirika la Biovision Foundation akizungumzia mataifa mengine namna yanavyotekeleza kilimo hicho, alisema wanasayansi na mashirika ya kimataifa ya masuala ya kilimo yanahimiza kilimo hicho kwa usalama wa chakula na kuna tija kiuchumi ambapo serikali za nchi ambazo zinatekeleza kilimo hicho zinaweka malengo yake.
Share:

RC MACHA AFUNGUA RASMI SEMINA YA FAMILIA,MALEZI,BIASHARA NA HUDUMA ZA AFYA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO

 



Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,amefungua Rasmi Semina ya Familia,Malezi,Biashara na huduma za Afya, ambayo inaendeshwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Ukanda wa dhahabu Nyanza Gold Belt Field NGBF.

Semina hiyo imeanza kutolewa Aprili 2,2024 ambayo itakwenda hadi Aprili 27 mwaka huu Siku ya Jumamosi,imekutanisha watu mbalimbali ambayo inafanyika katika ukumbi wa Makindo.
Macha akizugumza wakati wa kufungua Semina hiyo, imelipongeza Kanisa la Waadventista Wasabato kwa kuendesha Semina hiyo ambayo inathamani kubwa kwa taifa, kwa kutoa masomo ya Familia na Makuzi,Afya pamoja na Biashara.

“Nalipongeza sana Kanisa la Waadventista Wasabato,ni Kanisa ambalo lenye Mahaghaiko makubwa katika kuhakikisha Makuzi ya Vijana yanakuwa kwenye Maadili mema, sababu sasa hivi hapa nchini kuna Janga la Mmomonyoko wa Maadili ya Vijana, na Taifa bora linajengwa na Malezi bora na Makuzi,”amesema Macha.
“Masomo haya ya Familia yanakumbusha wazazi kulea watoto wao katika Maadili Mema, na siyo kuwaacha wakijilea wenyewe na hatimaye kusababisha watoto kuwa na Maadili Mabovu,”ameongeza Macha.

Amesema kwa upande wa Masomo ya Afya, ameitaka jamii kuzingatia lishe bora, sababu Magonjwa mengine hasa yasiyo ya kuambukiza husababishwa na Mtindo Mbovu wa Maisha, na kwamba kupitia Mafunzo hayo yanaijenga jamii yenye Afya Bora.
Aidha, amesema kupitia Masomo ya Biashara,amewataka Wafanyabiashara wawe na hofu ya Mungu, na kufanya biashara zao kwa haki bila ya kuchakachua bidhaa, pamoja na kulipa Kodi ya Serikali.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa, ametoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa Amani, pamoja na Rais Samia na wasaidizi wake,ili awe na maono mazuri ya kuiongoza Nchi katika kweli na haki, sababu Nchi ikiwa na Amani itakuwa na Maendeleo.
Naye Askofu wa Jimbo la Ukanda wa dhahabu (NGBF) Kanisa la Waadventista Wasabato Enock Sando, amesema Kanisa hilo limeendelea kujipambanua katika ulimwengu kote na kugusa jamii, kuisaidia kujitegemea kupitia Semina za Biashara ili wawe na Fikra Chanya ya kujikwamua kiuchumi sababu Mungu hapendezwi na Umaskini.

Amesema Kanisa hilo pia lina amini katika Afya, sababu bila Afya hakuna Maendeleo, ndiyo maana katika Semina hiyo mafunzo ya Afya yanatolewa, pamoja na Masomo ya Kaya na Familia ili kuwe na Taifa lenye Umoja,Mshikamano na Mahusiano Mazuri.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza wakati akifungua Semina hiyo.
Askofu wa Jimbo la Ukanda wa dhahabu (NGBF) Kanisa la Waadventista Wasabato Enock Sando.
Awali Mchungaji Mstaafu Wilbert Nfumbusa akitoa Somo la Kaya na Familia.
Awali Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Shinyanga (TCCIA) Jonathani Manyama akitoa Somo la Biashara kwenye Semina hiyo.
Awali Afisa Muuguzi Sherida Madanka akitoa Somo la Lishe kwenye Semina hiyo.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Kwaya ya Lubaga Mara Nassa ikiimba kwenye Semina hiyo.
Kwaya ya SAC ikiimba kwenye Semina hiyo.
Kwaya ya Lubaga Mara Nassa ikiimba kwenye Semina hiyo.
Kwaya ya SAC ikiimba kwenye Semina hiyo.
Kamati ya Maandalizi ya Semina hiyo ikiimba kwenye Semina.
Picha ya pamoja ikipigwa kwenye Semina hiyo.
Picha ya pamoja ikipigwa ikipigwa Semina hiyo.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger