Thursday 4 April 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRILI 5,2024

Share:

DCEA YAFANIKIWA KUKAMATA JUMLA 54, 506.553 KG YA DAWA ZA KULEVYA

 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za DCEA leo  Aprili 4, 2024 Jijini Dar es Salaam.

*****************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imefanikiwa kukamata Kilogramu 4.623 za aina mpya ya dawa ya kulevya aina ya methylene dioxy pyrovalerone (MDPV) iliyokamatwa jijini Dar es Salaam ikisafirishwa na raia wa Comoro anayeitwa Ahmed Bakar Abdou (32).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 4, 2024 Jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema Methylene dioxy pyrovalerone (MDPV) ni dawa mpya ya kulevya iliyo katika kundi la vichangamshi inayotengenezwa kwa kutumia kemikali bashirifu.

"Dawa hii ina kemikali inayoweza kuleta madhara ya haraka kwa mtumiaji ikilinganishwa na dawa nyingine za kulevya. Pia, imeongezwa nguvu ya kilevi inayozidi cocaine, heroin na methamphetamine". Amesema

Amesema, dawa hiyo ya kulevya huuzwa kwa njia ya mtandao (internet) na husafirishwa kupitia kampuni za usafirishaji vifurushi na hufichwa kwa kuwekwa chapa za majina bandia kama vile bath salts, Ivory Wave, plant fertilizer, Vanilla Sky, na Energy.

Aidha amesema wamefanikiwa kukamata jumla ya Kilogramu 54,506.553 za dawa za kulevya za mashambani na viwandani pamoja na kuteketeza ekari 262 za mashamba ya bangi.

Amesema watuhumiwa 72 wamekamatwa kuhusika na dawa hizo na baadhi yao tayari wamefikishwa mahakamani.

"DCEA kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wakala wa misitu (TFS) tulifanya operesheni katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Iringa, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam na kufanikiwa kukamata dawa hizi". Amesema.

Amesema dawa zilizokamatwa ni bangi kilo 54,489.65, mirungi Kilogramu 10.3, heroin gramu 90.93, cocaine gramu 1.98 na Kilogramu 4.623 za aina mpya ya dawa ya kulevya inayoitwa methylene dioxy pyrovalerone (MDPV) iliyokamatwa jijini Dar es Salaam ikisafirishwa na raia wa Comoro anayeitwa Ahmed Bakar Abdou (32).
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za DCEA leo  Aprili 4, 2024 Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za DCEA leo  Aprili 4, 2024 Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za DCEA leo  Aprili 4, 2024 Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za DCEA leo  Aprili 4, 2024 Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za DCEA leo  Aprili 4, 2024 Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za DCEA leo  Aprili 4, 2024 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Share:

Ngoma Mpya : BHUDAGALA MWANAMALONJA - NZUNA WANE


Hii hapa ngoma Mpyaa kabisa ya Bhudagala Mwanamalonja inaitwa Nzuna Wane
 
Share:

DKT. TAX AELEZA MAFANIKIO YA WIZARA YAKE KWA KIPINDI CHA MIAKA 60 YA MUUNGANO





 Na Dotto Kwilasa,DODOMA

WAZIRI Wa  Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  Dkt. Stergomena Tax , amesema wizara yake kupitia JWTZ imechangia katika kulinda mipaka ya nchi pamoja na kujenga uchumi imara ambao umepelekea wananchi hujishughulisha na  uzalishaji mali bila hofu.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi Wa habari kuhusu mafanikio ya miaka 60  ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Amesema kwa kipindi cha miaka 60 ya muungano Serikali kupitia Wizara  hiyo imeendelea kutekeleza, na kuliimarisha Jeshi kwa kulipatia zana na vifaa bora na vya kisasa, rasilimali watu, na nyenzo za kufanyia mazoezi ili kuwa imara wakati wote.

"Mchango mwingine mkubwa wa Jeshi hilo  katika miaka 60 ya Muungano, ni ulinzi madhubuti wa mipaka yetu, uhuru, na katiba. Nchi imeendelea kuwa imara na yenye amani katika awamu zote;

Pia , katika miaka 60 ya Muungano, Wizara ya Ulinzi na JKT  Pamoja taasisi zake zimeendelea kufanya na kuendeleza tafiti na uhawilishaji wa teknolojia kwa ajili ya kuzalisha bidhaa na huduma kwa matumizi ya kijeshi na kiraia, "ameeleza Waziri huyo wa ulinzi. 

Licha ya hayo ametaja mafanikio mengine ya muungano kuwa ni pamoja na Serikali kuanzisha viwanda vya kijeshi likiwemo shirika la Tanzania Automotive Technology Centre (TATC) maarufu kama NYUMBU, pamoja na Shirika la MZINGA. 

"Katika kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, serikali kupitia wizara ya Ulinzi na JKT, imeendeleza pia kudumisha uhusiano na mataifa mbalimbali duniani, kupitia mafunzo na mazoezi ya kijeshi, misaada ya kitaalam, vifaa, zana na mitambo,

Pamoja na hayo tumefanikiwa pia kupitia ubadilishanaji wa wataalam, ubadilishanaji taarifa za uhalifu unaovuka mipaka, shughuli za ulinzi wa amani, mapambano dhidi ya ugaidi, uharamia baharini, uvuvi haramu, na usafirishaji haramu wa binadamu, .


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI APRILI 4, 2024


Share:

Wednesday 3 April 2024

Video Mpya : MJUKUU CHIGABILO - KAYA

Share:

Video Mpya : MAHILI NG'WANA LUSI - BINADAMU

 

Share:

UTUPAJI MPYA WA TAKA DODOMA, JIJI LATOA KAULI


Picha ikionesha moja ya chungu cha maua kilichowekwa kando ya barabara kikiwa kimewekwa uchafu ambao haukujulikana umewekwa na nani. 

Na Dotto Kwilasa,DODOMA

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma limedhamiria kushirikiana kwa ukaribu na watu wa usalama barabarani, polisi jamii,wasimamizi wa mandhari na watu wa sheria ndogo ndogo za uhifadhi katika kukabiliana na changamoto za uharibifu wa mazingira unaotokana na utupaji taka maeneo ya wazi na mengineyo. 

Hatua hii ni kutokana na kuwepo kwa tabia iliyoibuka ya kutupa taka kwenye maeneo ya wazi hususani kwenye vyungu vya maua vilivyowekwa  kwenye barabara kuu ya Nyerere (Kuu street ) kwa ajili ya kupendezesha  Mandhari ya jiji la Dodoma kugeuzwa kuwa sehemu ya kuhifadhia uchafu . 

Vyungu hivyo ambavyo vimezungushwa na kusambazwa kwenye Barabara hiyo vimeonekana kutotunzwa wala kuthaminiwa kutokana na hali hiyo ya kuenezwa uchafu kwa siri siku hadi siku. 

Akizungumza  jijini hapa,Afisa Mazingira wa jiji la Dodoma Dickson Kimaro amesema suala la uchafu linatia kichefuchefu kwani linaweza kusababisha magonjwa na kurudisha nyuma maendeleo na kuwataka wanaotupa taka bila utaratibu kuacha mara moja .

 Amesema kutokana na hali hiyo wamekuwa tukikamata wanaofanya uchafu na kuwapiga faini ya shilingi 300000 na kwa wanaobainika kuvigonga vyungu hivyo wanalipa faini ya shilingi 300000 na kutengeneza na kurudisha mmea au ua kama lilivyokuwa . 

Kimaro amesema  lengo la kuwepo kwa vyungu hivyo ni kupendezesha jiji la Dodoma  liwe jiji la kijani (Green city) lakini imetokea kwa baadhi ya wananchi kuvigonga usiku wakiwa wamelewa na wengine kutupa taka ndani ya vyungu hivyo jambo ambalo halifai.

"Hii tabia ni hatari ambayo hufanywa na wananchi wanaoishi au kufanya shughuli zao maeneo ya barabara wakiwemo madereva wa daladala, waendesha bajaji , pikipiki na watembea kwa miguu,lazima tujue kutunza Mazingira ili yatutunze ,tunapotupa chupa ya plastiki ndani ya mmea tambua unakwenda kuuua kwani chupa au uchafu unaoutupa ina  kemikali,"amesema

Sambamba na hayo ametoa wito kwa baadhi ya wafanyabishara hususani wanaokaanga Chipsi na mishikaka kuacha kutupa majivu ya moto kwenye vyombo vya kuhifadhia uchafu kwani wamekuwa wakisasabisha vyombo hivyo kuungua kutokana na material yake kuwa ya plastiki. 

Aidha amesema kutokana na tatizo hilo Serikali kwa kushirikiana na wadau wapo kwenye mpango wa kuhakikisha wanasambaza vyombo vya kuhifadhia uchafu vya chuma ili hata vikimwagiwa moto viweze kuhimili. 

 Mwenyemiti wa Mtaa wa Tofiki Alnoor Visram amezungumzia hali hiyo kuwa yeye kwa nafasi yake amekuwa akihimiza wananchi wake kuzingatia suala la usafi lakini imekuwa ni Changamoto kubwa .

"Ni kweli vyungu hivyo vimegeuzwa vibebeo vya uchafu na hiyo yote ni kutokana na eneo au Mtaa wake kuwepo katikati ya mji ambao una watu wenye tabia tofauti na kushindwa kutii kanuni za usafi,kwakweli ni aibu kubwa ukizingatia hii ndio barabara kubwa hapa mjini na tukiwa tumezungukwa na ofisi kubwa bila kusahau ofisi kuu ya  CCM,niombe kuwepo na utaratibu kwa watu kama hao kukamatwa na kuadhibiwa tena adhabu kali, "amesisitiza na kuongeza;

Sisi kama viongozi hasa wa Mtaa hatujapewa rugu la kuwakamata moja kwa moja na kuwawajibisha wale wote wanaoonekana kutupa taka hizo lakini tungepewa nafasi hii tunaimani mazingira yangekuwa safe,nitoe wito kwa Wananchi wa jiji la Dodoma kuheshimu sheria za utunzaji wa mazingira na kila mtu au Wananchi awe askari wa manzingira ili mwenzako asiweze kutupa uchafu hovyo, " amesema 

Kutokana na hayo ameiomba Serikali kuingilia kati suala hilo kwa kutoa kalipio kali kwa wote wataobainika kutupa uchafu hovyo ikiwa ni pamoja na kuwajibisha kisheria. 

Naye Jafary Mnyawi mkazi wa Dodoma Kata ya Miyuji amesema Licha ya Dodoma kuwa jiji lakini ukweli ni kwamba Dodoma ni chafu tofauti na majiji mengine hapa nchini. 

 "Nitoe ushauri kwa Serikali kuwepo na utaribu na sheria za kuwawajibisha wachafuzi wa mazingira wote, mtu akitupa taka akamatwe kama wanavyofanya katika mikoa ya Moshi na arusha ,Dodoma ni jiji hivyo ni lazima jiji liwe safi  na kupendeza, " Amesema mkazi huyo Mnyawi




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger