Monday 25 March 2024

KAMWE SITONUNUA TENA CHANGUDOA!



Jina langu naitwa Dulla kutokea Dar es Salaam nchini Tanzania, nilikuwa na tabia baada ya kulewa natafuta mwanamke changudoa naenda kulala naye, ulikuwa ni mtindo wangu wa maisha kwa miaka mingi tu.

Nakumbuka siku moja baada ya kupiga tungi maeneo ya Kirumba, alipita dada poa mmoja nikamuita, alipofika tukaelewana kwenda kumalizana kwa Sh50,000, basi tukaanza kunywa na kulewa, tulipomaliza tukaenda kulala.

Kwa kuwa nilikua nimelewa sana nilipofika ndani tu nikapitiwa na usingizi, kuja kushtuka ni asubuhi tayari na yule mwanamke ameiba pesa zangu zaidi ya Sh800,000, simu yangu, kadi ya benki na vitambulisho vyangu vya kazini na vingine vya muhimu.

Hakuniachia hata fedha ya kulipa katika nyumba ile ya wageni, nilichanyikiwa ukizingatia simu yangu ilikuwa ina vitu vyangu vingi vya muhimu.

Nilianza kumtafuta yule dada maeneo yale tuliyokutana kwa zaidi ya miezi miwili lakini sikufanikiwa kumpata kabisa, kuna jamaa yangu akaja kuniambia kuna mtalaamu wa tiba asilia anaitwa Kiwanga Doctor anaweza kunisaidia.

Akanipatia namba zake, nami muda huo huo nikaruka hewani na kuzungumza naye, basi akanifanyia ganga ganga zake na kunihakikishia vitu vyangu vyote vitapatikana.

Baada ya siku mbili nikiwa sehemu ile ile nakunywa nilimuona tena yule mwanamke anapita, nikamuita, alikua ameshanisahau hivyo alijua ni mteja mpya.

Alivyofika tu nikamshikilia nkamuambia anilipe vitu vyangu, ila alikataa katakata na kusema hakuchukua.

Kwa kua nilikua na uhakika ni yeye, nilimnyang’anya kila alichokua nacho na kumtishia kumpeleka polisi.

Ndipo akakubali akasema ni kweli alichukua, akapiga simu kwa rafiki yake mmoja na kuvileta vitu vyangu vyote na fedha zangu.

Tangu siku hiyo nimekula kiapo kuwa sitakuja kununua tena changudoa!.

Siku zote kumbuka Kiwanga Doctors anatoa huduma kama kusafisha nyota, kusuluhisha migororo ya ndoa, mahusiano, mapenzi na familia, kumfunga mume au mke asitoke nje ya ndoa, anatoa tiba kwa wanaotafuta watoto.

Vilevile anatoa huduma ya kukusaidia kupata kazi au ajira, kupandishwa cheo na mshahara kazini, kuwasaidia wenye urahibu wa dawa za kulevya, sigara na pombe, kwa wanaotafuta mume au mke pia anawasaidia tena ndani ya siku chache.

Anatibu magonjwa kama kisukari, msukumo wa damu (BP), upungufu wa nguvu za kiume, miguu kuwaka moto n.k, pia anaweza kuisadia biashara yako kunawiri, na huduma zote hizi unaweza kuzipata bila kufika ofisini kwake.

Basi chukua hatua ya kuwasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba; +254 769 404965.

Mwisho.

 


Share:

RAIS SAMIA AFANYA MAGEUZI MAKUBWA YA MIUNDOMBINU MKOA WA KATAVI

 


Katika kipindi cha Miaka Mitatu cha Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan madarakani, Serikali ya awamu ya sita imefanya mageuzi makubwa ya Miundombinu ya Ujenzi wa Barabara na madaraja Mkoani Katavi.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Wakala ya Barabara ( TANROADS) Mkoa wa Katavi Mha. Martin Mwakabende, alipozungumza na waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya sita katika ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja.


Amesema “ Tunampongeza kwa dhati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami Barabara ya Mpanda-Tabora (km 337.429),sehemu ya pili ni Komanga-Kasinde ( Km 108), pamoja na Barabara ya Kasinde-Mpanda (Km 105.389) ndani ya miaka mitatu.”.

Amesema, miradi mingine ya kimkakati na ya kitaifa inayoendelea kutekelezwa ni pamoja na Barabara ya Mpanda-Uvinza-Kanyani (km 250.44), Kibaoni- Sitalike, sehemu ya Kibaoni-makutano ya mlele (km50), Barabara ya Kagwira-Karema (km 110.29), ujenzi wa kitanda cha Daraja la Kavuu ( urefu wa mita 87.5)

Vilevile, Ujenzi wa Daraja jipya la Mirumba (mita 60), Daraja jipya la Mto Lugufu ( mita 42) ambalo kukamilika kwa Daraja hilo kutatatua changamoto ya muda mrefu ya wakazi wa Mishamo na Lukoma.


“ Miradi hii itakapokamilika itasaidia sana Wananchi wa katavi kwani itarahisisha usafiri na usafirishaji wa kutoka Katavi kwenda Kigoma, Mbeya na mikoa mingine kwa haraka zaidi kwani Serikali inaenda kufungua Mkoa wa katavi kwa miundombinu ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami.” Ameeleza Mha. Mwakabende.

Amesema katika kipindi hicho wamefanikiwa kufunga Jumla ya taa 719 sawa na asilimia 77.15 , na kufanya Mkoa wa Katavi Uwe na Jumla ya taa 932 zenye thamani ya Shilingi bilioni 2.

Pia, ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi kulinda Miundombinu ya barabara pamoja na hifadhi ya barabara kwani kufanya hivyo kutapelekea barabara zidumu kwa muda mrefu zaidi.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Miradi ya Maendeleo kutoka TANROADS Katavi, Mha. Albert Laiza amesema wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuwaletea fedha za kufanya Matengenezo ya barabara.

Naye Mkandarasi mzawa anayetekeleza ujenzi wa Daraja la Kavuu lenye urefu wa mita 87.5, Mha. Bernad Ngailo kutoka Kampuni ya Ngetijo Group Co. Ltd amesema katika kipindi hiki cha Miaka mitatu Serikali imeweza kuwajali na kuwaamini wakandarasi wa ndani kwa kupewa kujenga miradi mikubwa ya kimkakati.

Mkoa wa katavi unatekeleza miradi 8 kimkakati na ya kitaifa yenye Jumla ya shilingi bilioni 410.81 na pindi itakapokamilika mtandao wa barabara kwa kiwango cha lami utakuwa kilomita 548.45

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MACHI 25, 2024



Share:

Sunday 24 March 2024

MTANZANIA SIMON MNKONDYA APELEKA KILIMO CHA VANILLA KENYA


Mkurugenzi wa Vanilla International Limited wa Tanzania ameweza kufanikiwa kuanzisha mashamba ya Vanilla katika eneo la Kaunti ya Kilith Nchini Kenya ambapo mradi huo mkubwa wa kilimo cha vanilla uko katika mji mdogo wa Mariakani kilomita 40 kutoka jiji la Mombasa.

Mradi huu unafanyika kwa ushirikiano na Mabati Technical Training Institute na wadau wengine wa maendeleo wakiwemo Safaricom Foundation ya nchini Kenya.

"Safari ya kilimo cha Vanilla inaenda vizuri licha ya vikwazo vya hapa na pale vya kisiasa lakini kiukweli wakenya wamekipokea kilimo cha vanilla kwa jicho kubwa sana hususani wakenya wanaoishi katika nchi mbalimbali za ughaibuni", amesema Simon Mnkondya Mkurugenzi wa kampuni ya Vanilla International Limited yenye mashamba yake pia Nchini Tanzania katika eneo la Zanzibar , Arusha na Dodoma.

Kwa Upande wa wakenya wamesema mradi huo utakuwa mkombozi wa uchumi wa Kenya na chanzo kikubwa cha ajira na kutoa ahadi ya kuwa watatunza vanilla vizuri na kushukuru kwa elimu ya utunzaji wa vanilla kutoka Mkurugenzi wa kampuni ya Vanilla International Limited Simon Mnkondya (+255 629 300 200).

Share:

BARRICK YAWEZESHA DAWATI LA KIJINSIA NA WATOTO KUTOA ELIMU YA KUTAMBUA NA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto wilaya ya Kawe A​/NSP Frank Mnojela akitoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wanafunzi.
Polisi pia walitembelea waathirika wa madawa ya kulevya na kuwafikishia elimu hiyo.
Madereva wa kituo cha Africana wakipatiwa elimu ya utambuzi wa vitendo vya ukatili wa kijinsia na jinsi ya kupambana navyo.
Maeneo ya masoko wilayani Kinondoni pia wamefikiwa na elimu hiyo iliyotolewa na Dawati la Jinsia la kituo cha Kawe kwa udhamini wa Barrick.
Maeneo ya masoko wilayani Kinondoni pia wamefikiwa na elimu hiyo iliyotolewa na Dawati la Jinsia la kituo cha Kawe kwa udhamini wa Barrick.

Wavuvi nao walifikiwa na elimu hiyo

****

Wakati changamoto za kuwepo usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda kuhusishwa na ongezeko la ajali za barabarani, ipo changamoto nyingine kubwa ya madereva wa bodaboda kudhalilisha watoto wadogo wanaotumia usafiri huo kingono , hali inayohatarisha maisha ya watoto kiafya na tishio la kuongezeka kwa mimba za utotoni katika miaka ijayo.
Changamoto hiyo imebainika wakati wa kampeni ya kutoa elimu dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ya siku 8 iliyoandaliwa na Dawati la kijinsia na watoto la kituo cha Polisi cha Kawe Jijini Dar es salaam katika mwendelezo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa udhamini wa kampuni ya Barrick.

Baadhi ya madereva wa bodaboda wa kituo cha Africana kilichopo wilayani Kinondoni wakiongea baada ya kupatiwa mafunzo hayo walieleza kukithiri kwa vitendo vya baadhi ya madereva wenzao kudhalilisha watoto kingono na wameeleza kuwa chanzo ni wazazi ambao wanawakabidhi watoto wawasafirishe kwenda mashuleni katika mazingira yasio rafiki.

Walieleza kuwa watoto wadogo wa kike wamekuwa wakielekezwa na wazazi wao kuwakumbatia madereva wanapokuwa wamebebwa kwenye usafiri wa pikipiki hali inayosababisha watoto kuwazoea madereva hao na wasio na maadili hutumia nafasi hiyo kuwadhalilisha watoto sambamba na kuwaingiza katika vitendo vya ngono katika umri mdogo.

Akiongea wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo mwishoni mwa wiki , Mkuu wa Dawati hilo ASP Elizabeth Msabila, alisema mafunzo yamefanyika katika maeneo mbalimbali ya jamii na kufikia makundi mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara wa vyakula na wauza kuku katika soko la Kawe , wauzaji wa pombe za kienyeji na watumiaji wa madawa ya kulevya (mateja) katika eneo la Rungwe Bandani Mbezi . Kawe beach kwa vijana wa Beach boys, na Wanafunzi wa shule ya Sekodari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi Beach Mtongani.

Msabila, alisema katika utoaji wa elimu hiyo wamegundua kuwa taifa lipo kwenye hatari kubwa ya kupoteza nguvu kazi ya vijana wa kiuume amabo wengi wamejiingiza katika vitendo vya tabia za ushoga, uvutaji wa bangi na madawa ya kulevya.

Pia alisema wamebaini kuwa watoto wengi wamekuwa wakifanyiwa ukatili na kubakwa hasa na ndugu wa karibu na kuwaasa wazazi kuhakikisha wanawalinda watoto wao kwa kuwakagua mara kwa mara kwa kuwa watoto wanaofanyiwa vitendo hivyo vya ukatili wanatishiwa kuwa wakisema watauawa na watoto wao kubaki na woga wa kutoa taarifa kwa wazazi wao.

ASP Elizabeth Msabila, alisema ili uweze kumgundua mtoto aliyebakwa moja ya dalili zake anakuwa hapendi kuchangamana na wenzake pia anakuwa mnyonge hapendi kucheza na wenzake pia anatembea kwa kuchechemea.

Aliwashukuru wananchi kwa kuwa na mwitikio mkubwa kuhudhuria mafunzo hayo sambamba na kufahamu Dawati la jinsia na watoto linavyofanya kazi na aliishukuru kampuni ya Barrick kwa kufanikisha mafunzo hayo,

Kwa upande Mkaguzi wa jeshi la Polis Dawati la Jinsia na Watoto kwa kata ya Kawe -Mbweni , wake Inspekta Ambilike Kibangu alisema wametoa elimu ya jinsi madawati ya kujinsia yaliyopo chini ya Jeshi la Polisi yanayovyofanya kazi na jinsi yanavtyoshughulikia kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto na Wanawake

Pia walitoa elimu juu ya aina mbalimbali za ukatili wa kijinsia ambapo alibainisha kuwa kuna aina mbalimbali za ukatili ukiwemo ukatili wa kimwili kwa watoto , udhalilishaji wa mke au mme ,mashambulizi ya aibu pamoja na ubakaji na suala zima la ulawiti kwa watoto wa kiume na watoto wa kike.

Pia wametoa elimu kwa akina mama wanaopigwa na waume zao au wanaume wanaonyanyaswa na wake zao kwa kunyimwa haki zao za unyumba kwenda dawati ili wakapatiwe ushauri juu ya kukabiliana na changamoto hiyo.


Captions


1.



2.


4.


5.


6/9-

Share:

BENKI YA CRDB YAFUTURISHA WATEJA NA WENYE MAHITAJI MAALUM GEITA

Katika mwendelezo wa utamaduni wa Benki ya CRDB kuungana na Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoishiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan imejumuika na wateja pamoja na makundi  yenye uhitaji maalum katika futari waliyoandaa.

Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB imefanyika Ijumaa Machi 22,2024 katika ukumbi wa Otonde  mkoani Geita ambapo Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Said Juma Mkumba alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela huku  Menejimenti ya Benki  ya CRDB iliwakilishwa na  Mkurugenzi wa Rasimali Watu Godfrey Rutasingwa. 

Benki ya CRDB pia imekabidhi vitu mbalimbali kwa vituo vya watu wenye mahitaji maalum vitakavyowasaidia kukamilisha funga yao  katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Benki ya CRDB ambayo mwaka 2021 ilianzisha dirisha la huduma za kibenki ambazo zimefuata misingi ya dini ya kiislamu maarufu kama Al Barakah Banking, imekuwa na utaratibu kila mwaka wakati wa Ramadhan kushiriki Futari na wateja wake na kutoa Sadaka ya vyakula kwa watu wenye mahitaji maalum.
Mkurugenzi wa rasilimali watu Godfrey Rutasingwa  akitoa salamu za benki ya CRDB
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi ndugu Jumanne Wambura Wagana akitoa salamu za ufunguzi
Shekhe mkuu wa mkoa wa Geita Alhaj Shekhe Alhad Kabanju akitoa salamu na pongezi kwa CRDB.
Mkuu wa Wilaya ya Chato  Mh. Said Mkumba akitoa salamu kwa niaba ya mgeni wa heshima mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Sophia Jongo aliye mbele na akina mama wa Mkoa wa Geita wakati wa Iftar.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger