Tuesday 28 November 2023
Monday 27 November 2023
TCRA CCC YAKUTANA NA WATOA HUDUMA ZA MAWASILIANO KUBORESHA HUDUMA KWA MTUMIAJI WA MAWASILIANO
ANDAENI WAINJILISTI WA KUDUMU WATAKAO FANYA KAZI YA KUENEZA INJILI - MCH. MWAZYUNGA
Na. Gideon Gregory, Dodoma.
Kiongozi wa Uinjilisti Kanisa la Moravian Nkuhungu Jijini Dodoma Mch. Boaz Mwazyunga ametoa wito kwa kanisa hilo jimbo la Kaskazini kuwa na mpango wa kuandaa wainjilisti wa kudumu ambao pamoja na kazi yao watafanya kazi ya kueneza injili ikiwa ni pamoja na kufungua na kupanda makanisa mapya vijijini.
Mch. Mwazyunga ametoa wito huo leo Novemba 26,2023 wakati akiongoza waumini wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Kaskazini ushirika wa Nkuhungu kuadhimisha miaka 16 ya kutoa huduma ya kiroho kwa waumini hao nakuongeza kuwa hapaswi kuogopa gharama na kuangalia nani yupo katika maeneo wanayokwenda pamoja na mazingira yaliyopo.
“Wito wangu ni kuona kuwa kanisa linatii agizo la Bwana Yesu Kristo alilosema, basi nendeni mkawafanye mtaifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la baba, na mwana na roho mtakatifu na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi na tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari (Mathayo 28:19-20),”amesema.
“Umefika wakati sasa wa kwenda maeneo ya pembezoni na vijiji kununua viwanja na mashamba ili tunapofanya uinjilisti wale tutakaowapa wawe na mahali pa kuanzia kuabudia,”ameongeza.
Awali akitoa mafundisho Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Kaskazini Mch. Isaac Siame ametoa rai kwa waumini kumruhusu Mungu awatumie katika utumishi wao na kuongeza kuwa wasikubali shetani akawatumia katika mipango yake hovu kwa wanadamu.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Wakili wa Ushirika 2023 Lilian Nzowa amesema tangu ushirika huo uanzishwe umefanikiwa kuongeza wakristo 170 kutoka 58 hapo awali wakati unaanzishwa ongezeko linalojumuisha watu wazima pamoja na watoto.
Sambamba na hayo maeongeza kuwa kwa mwaka 2024 wanatarajia kuanza ujenzi wa jengo la kuabudia linalotarajia kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 2 ambalo litakuwa na uwezo wa kuchukua jumla ya watu 800 kwa ibada moja.
Tanzia : MSANII MAARUFU WA NYIMBO ZA ASILI BHUHULU LUSAFISHA AFARIKI DUNIA
Sunday 26 November 2023
MAKATIBU WAKUU WAFANYA ZIARA HANDENI WANAPOHAMIA WAKAZI WA NGORONGORO
Na Mwandishi wetu - Tanga
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi Dkt. Yonazi amesema Serikali imejipanga katika kuhakikisha kuwa wizara zote za kisekta zinashiriki kikamilifu katika kuhakikisha kuwa miradi iliyopo katika Kijiji cha Msomera inakamilika kwa wakati ili kuwezesha wananchi wanaoendelea kujiandikisha kuhamia katika eneo hilo ili kuendelea shughuli zao.
Dkt. Yonazi aliyasema hayo wakati wa ziara ya kikazi ya Makatibu Wakuu wa Wizara za kisekta waliyoifanya katika Kijiji cha Msomera, Wilaya, Handeni mkoani Tanga kujionea hatua mbalimbali za ujenzi wa miundombinu kabla ya kuanza kwa awamu ya pili ya kuhamisha wananchi wanaoishi katika hifadhi ya Ngorongoro waliojiandikisha kuhama kwa hiari.
Amesema Makatibu Wakuu hao wamekagua ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali ikiwemo maji, umeme, madaraja, barabara, shule, Nyumba za makazi na uboreshaji wa huduma za mawasiliano.
“Niwaombe wanaohamia eneo hili waiamini Serikali kwamba inawatengenezea mazingira yaliyo bora sana hapa Msomera, nyumba zinazojengwa na huduma zote zina ubora ili wananchi wetu wanufaike na Serikali yao waachane na upotoshaji kwa sababu imewekeza fedha nyingi kuhakikisha wanaishi katika mazingira salama,”Amesema Dkt. Yonazi.
Naye Kamanda wa Kikosi Kazi cha Ujenzi wa nyumba 5000 kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema kila taasisi ya kisekta na Wizara zinawajibika ipasavyo kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati akisema kuwa licha ya changamoto za mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali lakini kazi inaendelea vizuri .
“Mpaka sasa ujenzi wa Msomera ambao tumeugawanya katika vitalu kuanzia A mpaka D tuko katika hatua mbalimbali za ujenzi nyumba 1000 katika eneo la Msomera B kitalu F viwanja 768 taratibu zake zimekamilika eneo liko tayari kwa ajili ya uchimbaji na kuanza msingi na kuendelea na hatua za ujenzi,”Ameeleza Brigedia Jenerali Mabena.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Albert Msando amewashukuru Makatibu Wakuu hao kwa kutembelea mradi huo hatua inayoongeza kasi yake kusonga mbele akiahidi kusimamia kwa karibu mradi huo ambao umefanyika kama hatua ya kuboresha maisha ya watanzania kila mwananchi kuishi katika hali ya ustawi pamoja na uwepo wa miundo mbinu muhimu pamoja na huduma za kijamii.
“Hii inaonyesha nia ya dhati ya Serikali ya kukamilisha mradi huu muhimu kwa wakati siyo tu kuhamisha watu lakini unaenda kuboresha maisha ya watanzania tunaendelea kuwaahidi kwamba tutasimamia kwa karibu tunajua unatekelezwa wakati wa mvua ambapo kwetu ni fursa ya kuona namna ya kuyavuna maji kwa ajili ya matumizi,”Amebainisha
“Hii kwetu ni neema kubwa sana Serikali inafanya kazi kubwa na niwaambie waliopo Ngorongoro wasikubali kupotoshwa na watu wachache wasio na nia njema kijiji cha Msomera ni kijiji mojawapo kati ya Vijiji 91 ndani ya Wilaya ya Handeni mradi huu umeleta faida kubwa kupitia wenzetu waliohamia kutoka Ngorongoro,”Amepongeza Mwenyekiti huyo.