Tuesday 28 November 2023

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU 'NBS' YATOA MAFUNZO YA USAMBAZAJI NA MATUMIZI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 KWA VIONGOZI NA MAKUNDI MBALIMBALI MANISPAA YA SHINYANGA



Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii kwa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ili kuwajengea uwezo wa kutafsiri, kuchambua na kuyatumia matokeo ya Sensa katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kuthamini utekelezaji wa sera na mipango ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu.


Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo leo Jumanne Novemba 28,2023 , Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi amesema mafunzo hayo yataongezea uelewa na ujuzi wa kutumia matokeo ya Sensa katika kufanya maamuzi yenye tija ya maendeleo ya wananchi.


"Naipongeza NBS kwa kazi kubwa wanayoendelea kufanya ya kusimamia kwa weledi utekelezaji wa shughuli za Sensa kwa mafanikio makubwa. Uwepo wenu hapa leo unadhihirisha mnavyotekeleza kwa vitendo dhamira za kweli za Serikali zetu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan; na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekirti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Viongozi wetu hawa, wameelekeza matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yawafikie wadau wote na yatumike kikamilifu ili kuchagiza na kuharakisha maendeleo ya nchi yetu",amesema Mhe. Samizi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.

"Kwa kuwa suala la kupanga mipango ya maendeleo ni shirikishi na linaanzia ngazi za chini hadi Taifa; sisi tunao wajibu wa kuratibu suala zima la upangaji wa mipango na programu za maendeleo kuanzia Mtaa au Kijiji, kata, halmashauri, wilaya na mkoa. Hivyo mafunzo haya yanatuongezea ujuzi na kupata uzoefu zaidi kutoka kwa wataalamu wetu namna bora ya kutumia matokeo ya Sensa katika kutekeleza majukumu yetu",ameeleza Mhe. Samizi.


Amefafanua kuwa Matumizi sahihi ya matokeo ya Sensa yatawezesha kuongezeka kwa ufanisi katika matumizi ya rasilimali za nchi kwa kuzingatia mahitaji halisi na mazingira wanamoishi wananchi. 

"Mafunzo haya yatatuwezesha pia kuhakikisha mipango yetu inakuwa jumuishi kama ujumbe wa kaulimbiu ya Sensa wa Awamu hii ya Tatu inavyosema “Matokeo ya Sensa ya Sita, Mipango Jumuishi kwa Maendeleo Endelevu, ameongeza.

Amesema baada ya mafunzo hayo wanatarajia pia watakuwa na mipango itakayotoa majibu ya changamoto mbalimbali za maendeleo zinazowakabili wananchi wa mkoa wa Shinyanga hususan mipango inayojielekeza katika kuondoa umasikini wa kipato na usio wa kipato na hatimae kuinua kiwango cha hali ya maisha kama inavyoelekeza Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020.
Mafunzo yakiendelea

Amebainisha kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekamilisha na kuzindua ripoti mbalimbali za Sensa ambapo Ripoti hizo zimebainisha hali ilivyo katika sekta mbalimbali kuanzia ngazi ya Taifa, mkoa, wilaya na nyingine hadi ngazi ya kata.


"Matumizi ya matokeo hayo ya Sensa yanatusaidia kufahamu tuko wangapi katika maeneo yetu kwa jinsi, umri, fursa za kiuchumi zilizopo pamoja taarifa nyingine za kidemografia, kiuchumi na mazingira. Matokeo ya Sensa yanabainisha hali halisi ya upatikanaji na ubora wa huduma za kijamii kama vile huduma za maji, miundombinu ya barabara, huduma za afya, elimu, nishati, masoko, mabenki na mawasiliano. Hivyo, matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ni nyenzo muhimu ya kisera katika kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi. Hatuna budi kuyaelewa na kufahamu matumizi yake kwani ni jambo la msingi ambalo litachochea kasi ya kutatua kero za wananchi katika mkoa wetu", ameeleza.


Amewasisitiza viongozi na watendaji wote kuwa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 pamoja na takwimu nyingine za kisekta zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu; ziwe ndio msingi wa kufanya maamuzi ya maendeleo katika mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati akifungua Mafunzo hayo.

Amesema wananchi wana matumiani kuwa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yatawezesha kuleta mabadiliko chanya katika maisha yao ya kila siku.

"Matumaini hayo yamejengwa na wito wa viongozi wetu wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye wakati wote wa utekelezaji wa Sensa hadi kuzinduliwa kwa matokeo ya mwanzo ya Sensa mwezi Oktoba Mwaka 2022 amekuwa akisisitiza umuhimu wa matumizi ya matokeo ya Sensa. Katika uzinduzi huo Mheshimiwa Rais alisisitiza kuwa, matokeo ya Sensa yanakwenda kuleta mabadiliko katika mwenendo wetu wa kufanya maamuzi, uandaaji wa sera, mipango, ufuatiliaji na ufanyaji tathmini wa utekelezaji wa sera na mipango yetu ya maendeleo",amesema.


"Hivyo, tunayo dhima kubwa ya kukidhi matarajio hayo ya wananchi wetu na pia kuhakikisha tunakwenda bega kwa bega na dhamira ya Rais wetu kwa kukakikisha tunatekeleza kikamilifu Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022",amesema Mhe. Samizi.
Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Benedict Mugambi ambaye ni Meneja Idara ya Shughuli za Kitakwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Benedict Mugambi ambaye ni Meneja Idara ya Shughuli za Kitakwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ameshauri Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa Makundi Mbalimbali katika Jamii pindi wanapohitaji takwimu kwenye maeneo yao waombe taarifa kwenye ofisi za NBS.

"Tunajua mna mahitaji mengi kwenye maeneo yenu kutokana na matokeo haya ya Sensa ya Watu na Makazi 2022, tunaomba kama kuna mnahitaji takwimu, tuandikieni barua kwenye ofisi za NBS, tutawapatia takwimu mnazohitaji kulingana na eneo unalohitaji",amesema Mugambi.

 Akitoa Wasilisho la Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2022, Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Mdoka Omary amesema mkoa wa Shinyanga una wakazi 2,241,299 ambapo halmashauri yenye watu wengi ni Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (watu 468,611) ikifuatiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ( watu 453,654) na halmashauri yenye  idadi ndogo ya watu katika mkoa wa Shinyanga ni Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga (watu 214, 744).

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii kwa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 28,2023 katika ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii kwa Manispaa ya Shinyanga 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii kwa Manispaa ya Shinyanga
Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Benedict Mugambi ambaye ni Meneja Idara ya Shughuli za Kitakwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza wakati wa Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii kwa Manispaa ya Shinyanga
Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Benedict Mugambi ambaye ni Meneja Idara ya Shughuli za Kitakwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza wakati wa Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii kwa Manispaa ya Shinyanga
Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Benedict Mugambi ambaye ni Meneja Idara ya Shughuli za Kitakwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza wakati wa Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii kwa Manispaa ya Shinyanga
Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Benedict Mugambi ambaye ni Meneja Idara ya Shughuli za Kitakwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza wakati wa Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii kwa Manispaa ya Shinyanga
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza wakati wa Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii kwa Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anold Mkombe  akizungumza wakati wa Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii kwa Manispaa ya Shinyanga
Mafunzo yakiendelea
Mafunzo yakiendelea
Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Mdoka Omary akitoa Wasilisho la Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2022
Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Mdoka Omary akitoa Wasilisho la Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2022

Mrasimu Ramani kutoka 
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Nolasco John akitoa wasilisho la matumizi ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2022 kwa njia ya ramani
Mafunzo yakiendelea
Mafunzo yakiendelea

Share:

VYAMA VYA SIASA VYAONESHA USHIRIKIANO UBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA TABORA


Mkazi wa Kata ya Ng'ambo aliyefika katika Kituo cha Kizigo Mzee Juma Rai Juya, akionesha kadi yake ya mpiga kura mara baada ya kukamilisha taratibu za kuboresha taarifa zake kwenye daftari la wapiga kura na Kukabidhiwa kadi yake mpya.

Afisa Mtendaji wa kata na Mwandikishaji Msaidizi Kata ya Ng'ambo, Rehema Midelo akizungumza na mwandishi wetu katika kituo cha Masempele kata ya Ng'ambo mjini Tabora wakati akielezea namna zoezi hilo linavyoenda kwa ufanisi mkubwa.

Wakala wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kituo Cha Kaze Shule ya Sekondari, Bw. Brayson Dickson akielezea namna zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wazpiga kura linavyoendelea katika kituo cha Shule ya Sekondari Kaze mjini Tabora.

Bi Leila Muhaji Kaimu Mkurugenzi Masidizi Habari kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kulia akifuatilia zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika kituo cha Kizigo kata ya Ng'ambo mkoani Tabora.

...........................

Vyama vya Siasa pamoja na Wakazi wa Kata ya Ng'ambo, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mkoa wa Tabora wameonesha ushirikiano mkubwa wa kushiriki katika zoezi la uboreshaji wa majaribio wa daftari la kudumu la wapiga kura linaloendelea katika Kata ya Ng'ambo.

Akifanya mahojiano na Mwandishi Wetu, Afisa Mtendaji na Mwandikishaji Msaidizi Kata ya Ng'ambo, Rehema Midelo, amesema kuwa mwitikio ni mkubwa na wananchi wameendelea kujitokeza kujiandikisha katika zoezi la uboreshajia wa majaribio wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Bi. Midelo amesema kuwa katika zoezi hilo mpaka Novemba 26, 2023 kuna wapiga wengi wamejitokeza katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

"Wananchi wa Kata ya Ng'ambo wana hamasa kubwa katika ushiriki wa shughuli za kijamii na maendeleo ikiwemo zoezi hili la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ambalo baadaye linawapa uhalali wa kushiriki kuchagua viongozi wao wakati wa uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani" amesema.

Amefafanua kuwa Kata ya Ng'ambo kuna mitaa 10, huku mtaa wa Kizigo ukiwa na idadi kubwa ya watu ambao wanajitokeza katika zoezi la uboreshajia wa daftari la kudumu la wapiga kura, Hii imepelekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuongeza mashine mbili zaidi za BVR Kit na kufikisha tatu katika kituo hicho hata hivyo inapofika jioni bado kuna watu wanabaki ambapo wanaelekezwa kurudi kituoni kesho yake ili kumalizia taratibu zilizobaki.

"Mtaa huu kuna wapiga kura wengi, lakini kuna changamoto ya baadhi ya watu kutoka kata, jirani wamekuwa wakijiandikisha na tukiwabaini tunawapa elimu na kuwarudisha katika maeneo yao na kuwaelimisha kuwa zoezi bado halijaanza rasmi na likianza watatangaziwa" amesema

Wakala wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kituo Cha Kaze Shule ya Sekondari, Bw. Brayson Dickson, amesema kuwa wanachama wa CCM wamehamasika kwa asilimia kubwa na walio wengi ni vijana ambao pamoja na kufanya mikutano ya kuwahamasisha lakini tulitenga muda wa kuwafuata vijana katika vijiwe vyao na kuwaelimisha kuhusu zoezi hili ndiyo maana unaona mwitikio ni mkubwa sana kwa vijana.

"Baada ya kutoa elimu mwitikio ni mkubwa sana, na kituo hiki hakuna changamoto yoyote, tuendelee kutoa elimu na kuhamasisha wananchi pamoja viongozi ili tuweze kufikia malengo kwa muda uliobaki," amesema Dickson.

Wakala wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika kituo cha Kizigo Jumanne Kishimba, amesema kuwa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga linakwenda vizuri.

"Hamasa inakwenda vizuri, hakuna shida, sisi CHADEMA tumehamasisha wanachama wetu kwa kuwapigia simu pamoja na kutembea nyumba hadi nyumba kwa ajili ya kujiandikisha," amesema

Naye Mkazi wa Kata ya Ng'ambo aliyefika katika Kituo cha Kizigo Mzee Juma Rai Juya, amesema kuwa zoezi linakwenda vizuri na kila mtu anayefika anapata huduma kwa wakati.

"Nimefika hapa kituoni wakaniuliza taarifa zangu na kujaza fomu za uboreshaji wa daftari, nikapigwa picha, pia nikachukuliwa alama za vidole kisha nikapewa kadi yangu mpya ya kisasa ya kupigia kura, naishukuru serikali kwa utaratibu huu mzuri wa kuboresha taarifa na nitaitunza kadi yangu mpaka uzeeni" amesema
Share:

MUME ALINIACHA KIJIJINI NA KWENDA KUTEKWA NA WANAWAKE WA MJINI

Jina langu ni Elizabeth kutoka katika kaunti ya Bungoma, tulikuwa kwenye ndoa na mume wangu Benson kwa muda wa miaka minne, tulikuwa na maisha mazuri kwani hakuna lolote ambalo likuwa kikwazo katika uhusiano wetu.

Baadaye alipata kazi mjini Nairobi, tulikubaliana kuwa aende kufanya kazi hiyo na mimi ningebaki kijijini na watoto, kila mwezi alikuwa akinitumia fedha za kufanya shuguli mbalimbali  pale nyumbani kwetu.

Nilimwamini kwani hakuna hata siku mmoja mume wangu alionekana kuwa na mpango wa kando, jambo hili lilipelekea na mimi kumuonyesha mapenzi ya dhati.

Kila baada ya mwezi mmoja alikuwa akija nyumbani kunijulia hali na hapo sikuwa na shaka ya uwepo wake mjini Nairobi, ila baada ya siku kupita tabia yake ilianza kubadilika.

Hakuwa akipiga simu tena kama ilivyokuwa kawaida yake kila siku, nilianza kushuku mienendo hii yake kwani fedha alizokuwa akituma kila mwisho wa mwezi zilipungua sana na wakati mwingine hakuma kabisa.

Wakati mwingine nilipompigia simu sauti ya mwanamke ilisikika kwenye simu yake, nilifunga safari na kwenda Nairobi kujua alipokuwa akiishi. Nilipigwa na butwa baada ya kumpata mwanamke mwingine kwenye nyumba yake, huyu mwanamke aliniambia yeye ni mke wake mume wangu!. 

Nilienda kulala kwa dada yangu usiku ule kwani sikutaka ugomvi na mtu, Dada yangu alinihurumia kwa mambo yaliyonikumba na hata akanipa ushauri kuwa kuna mtaalam wa tiba asilia anaweza kunisaidia.

Aliniambia mtaalamu huyu ni African Doctors ambaye amesaidia watu wengi sana, alinipatia namba zake, niliweza kuwasilina naye na baada ya wiki moja niliweza kufika ofisini kwake na kumueleza changamoto zangu zote na akanifanyia tiba zake.

Nilirejea nyumbani na baada ya siku tatu sikuyaamini macho yangu, mume wangu alikuja nyumbani akiwa mnyonge ajabu, aliniomba msamaha kwa yote yalikyokuwa yametokea. Nilimsamehea kwa kuwa nilikuwa mwenye mapenzi ya dhati kwake, baadaye tulienda pamoja mjini.

Tangu siku ile mume wangu amekuwa ni mtu mwaminifu ajabu kwenye ndoa, pongezi sana kwa African Doctors kwa huduma yako ambayo imekoa ndoa yangu ambayo ilikuwa inaelekea kupotea.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com

Mwisho.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 28,2023





Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger