Tuesday 12 September 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 13,2023































Share:

DEREVA BODABODA AFARIKI KWA KUGONGANA NA MWENDOKASI, RC CHALAMILA AKEMEA

Mtu mmoja aliyekuwa akiendesha pikipiki amefariki dunia katika ajali kati ya pikipiki hiyo na Gari ya Mwendokasi baada ya kugonga basi hilo kwenye eneo la Lumumba,  mataa ya Kituo cha Mwendokasi cha Fire na DIT Jijini Dar es Salaam.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limethibitisha kifo cha dereva huyo aliyedaiwa kuingia katika barabara ya mabasi ya mwendokasi na kuwa watatoa taarifa kamili ya tukio hili hapo baadaye.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amefika katika eneo hilo na kukemea vikali watu wote kupita kwenye barabara za mwendokasi bila vibali huku akibainisha kujana na mpango mahususi kwa bodaboda zinazokatisha kwenye mwendokasi na kusababisha ajali mara kwa mara.



Share:

WANAFUNZI WALIOPANGWA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI,2023

Share:

MASWA YETU BLOG TUMERUDI UPYA,KIVINGINE ZAIDI

 Ile blog pendwa ya Maswa yetu blog sasa imerudi rasmi hewani


Sasa utapata habari zote zinazokuhusu kwa wepesi zaidi.


karibuni sana.

Share:

Saturday 2 September 2023

WASTANI WA KUISHI KWA MTANZANIA WAONGEZEKA KUTOKA MIAKA 45 HADI 65


 Mtakwimu Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt.Albina Chuwa akizungumza katika mkutano maalum uliohusisha pia Wakuu wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Agosti 31, 2023 Jijini Dar es Salaam.

****************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

UMRI wa Mtanzania kuishi umeendelea kuongezeka ambapo katika Sensa ya Mwaka 1978 umri wa Mtanzania kuishi ulikuwa miaka 45 wakati wa sensa ya mwaka 2022 umri wa Mtanzania kuishi umefika miaka 65.

Mtakwimu Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt.Albina Chuwa, amesema hayo Dar es Salaam, wakati akifunga mkutano wa kuwajengea wakuu wa mikoa uwezo wa kuzitumia takwimu za Sensa.

Akizungumza katika mkutano maalum uliohusisha pia Wakuu wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, leo Agosti 31, 2023, Mtakwimu Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt.Albina Chuwa, amesema mchakato wa Sensa uliopita umekuwa na mafanikio makubwa na haijawahi kutokea kuwa na ushirikiano wa juu kama uliioneshwa na watendaji.

“Watanzania wanaendelea kuishi zaidi kwa kuwa na wastani wa miaka 69 wakati kwa Wanaume ni wastani wa miaka 62. Wanawake wanaishi miaka mingi zaidi kutokana na sababu kadhaa ikiwemo za kibaiolojia.” Amesema

Ameongeza kuwa Nchi nyingi zinakuja Tanzania kujifunza juu ya mchakato wa Sensa ulivyofanyika.

Pamoja na hayo amesema kuwa kiwango cha elimu kimeongezeka, watu wanaojua kusoma na kuandika imefikia zaidi ya Asilimia 80, upande wa Bara ni zaidi ya Asilimia 90.

Naye, Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Mhe.Anne Makinda akizungumza katika mkutano huo amesema “Awamu ya kwanza ilikuw akufanya uchechemuzi, ya pili kuhesabiwa na ya tatu ni kupeleka elimu ya matokeo ya Sensa kwa wahusika.

“Bado tunawategemea ninyi (wakuu wa mikoa) kuchukua haya ya juu mkayapeleka kwa Wananchi.”
Mtakwimu Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt.Albina Chuwa akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano maalum uliohusisha pia Wakuu wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Agosti 31, 2023 Jijini Dar es Salaam
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Mhe.Anne Makinda akizungumza katika mkutano maalum uliohusisha pia Wakuu wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Agosti 31, 2023 Jijini Dar es Salaam





Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 2, 2023

 




















Share:

Friday 1 September 2023

EXTRA BINGO MCHEZO WA KENO ULIORAHISISHWA!!

 

Hapa tena Meridianbet kasino ya mtandaoni tunakuletea mchezo wa namba wenye bonasi kubwa na rahisi kucheza, mchezo wa keno ni moja ya michezo pendwa inayopatikana Meridianbet.

 

Extra Bingo ni mchezo wa kasino ya mtandaoni uliotengenezwa na gwiji wa michezo ya kasino ya mtandaoni Wazdan. Je, umechoka kusubiri mpaka kipindi fulani ili kupata droo inayofuata? Kuanzia sasa, unaweza kuchagua wakati wa kuanza kwa droo inayofuata mwenyewe.

 

Fahamu Kuhusu Extra Bingo

 

Extra Bingo ni mmoja wa michezo ya keno iliyozoeleka. Kuna namba 20 za kuchagua na inatoa namba 20 katika kila mzunguko.

 

Idadi ya chini ya namba unazoweza kucheza kwa kila mzunguko ni namba tatu. Lengo la mchezo ni kubashiri idadi nyingi ya namba kadri iwezekanavyo. Ikiwa utapatia namba zote ulizochagua, utapokea malipo ya juu kabisa kwa mchezo huu wa Extra Bingo kutoka kasino ya mtandaoni.

 

Unaweza kuchagua aina yoyote/mpangilio wowote wa namba, kuanzia namba tatu hadi namba 10.

 

Chini ya mipangilio ya mchezo huu wa kasino mtandaoni utaona uwanja wa menu na dau zinazowekwa kwa kila beti. Unachagua kiwango cha dau/beti kwa kubofya namba uzitakazo. Pia unaweza kubadilisha jukumu kwa kutumia vitufe vya kuongeza na kupunguza vilivyoko kwenye uwanja wa menu.

 

Mchezo huu unakupa chaguo la kucheza Automatic, kupitia chaguo hili unaweza kuweka hadi mizunguko 1,000.

 

Je, unapenda mchezo wako wa kasino ya mtandaoni uendeshwe kwa kasi kidogo? Hakuna tatizo. Unaweza kuendesha chaguo hilo kwa kubonyeza alama ya Turbo.

 

Kuna viwango vitatu vya kasi katika mchezo huu. La kwanza linawakilishwa na kobe, la pili ni sungura, na la tatu ni farasi.

 

Faida kuu ya Extra Bingo ni kwamba wewe kama mdau wa michezo ya kasino unaweza kuamua muda wa droo kuanza.

 

Malipo ya Ushindi

 

Kulingana na idadi ya namba unazozicheza, malipo yanatofautiana. Jambo zuri ni kwamba hauhitaji kuchagua namba zote ili upate malipo. Malipo ya ushindi ni kama ifuatavyo.

 

Ikiwa unacheza mchanganyiko wa namba tatu:

  • Kugonga mbili kunatoa dau mara mbili
  • Kugonga tatu kunatoa mara 50 ya dau

 

Ikiwa unacheza mchanganyiko wa namba nne:

  • Kugonga mbili kunatoa thamani ya dau
  • Kugonga tatu kunatoa mara 10 ya dau
  • Kugonga nne kunatoa mara 85 ya dau

 

Ikiwa unacheza mchanganyiko wa namba tano:

  • Kugonga mbili kunatoa thamani ya dau
  • Kugonga tatu kunatoa mara tatu ya dau
  • Kugonga nne kunatoa mara 20 ya dau
  • Kugonga tano kunatoa mara 200 ya dau

 

Ikiwa unacheza mchanganyiko wa namba sita:

  • Kugonga tatu kunatoa dau mara mbili
  • Kugonga nne kunatoa mara 12 ya dau
  • Kugonga tano kunatoa mara 60 ya dau
  • Kugonga sita kunatoa mara 550 ya dau

 

Mchanganyiko wa namba saba:

 

  • Malipo yanatofautiana na ushindi mkubwa unakusubiri pindi unapo bashiri kwa usahihi namba zote saba. Kisha utashinda mara 1,000 ya dau lako.

 

Kwa namba nane, malipo ni tofauti, lakini kiwango cha juu cha malipo hufanana, mara 1,000 zaidi ya dau/beti yako.

 

Malipo ya juu kabisa yanakusubiri ikiwa unacheza mchanganyiko na namba tisa au 10. Kulingana na idadi ya namba unazo bashiri kwa usahihi, malipo yanatofautiana.

 

Hata hivyo, kiwango cha juu ni sawa. Kupatia uchaguzi wa namba tisa au 10 kunakupatia mara 2,000 ya dau lako.

 

Michezo Ya Bonasi

 

Unaweza kuzidisha ushindi wako kwa msaada wa bonus ya Gamble. Unahitaji tu kuotea rangi ya kadi inayofuata itakayoonekana kwenye skrini yako.

 

Extra Bingo-bonus ya kamari-online casino bonus-wazdan Bonus ya kamari Unaweza kucheza kamari mara kadhaa mfululizo.

 

NB: Ukijisajili Meridianbet unapewa bonasi ya mizunguko ya bure kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni. Jisajili na Cheza.

 


Share:

SERIKALI YAKERWA UTOROSHAJI WA MIFUGO NCHINI KENYA


Naibu Katibu Mkuu wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo),Dkt Daniel Mushi akiongea na uongozi na wafanyakazi wa kiwanda kikubwa cha kuchakata nyama cha Eliya Food Overseas Ltd kilichopo wilayani Longido mkoani mkoani Arusha alivyofanya ziara ya kikazi jana akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo


Na Woinde Shizza, LONGIDO


Serikali imeuagiza uongozi wa wilaya ya Longido mkoani Arusha kuhakikisha unadhibiti vitendo vya utoroshaji wa mifugo kwenda nchini Kenya vilivyokithiri na kuathiri uzalishaji katika kiwanda kikubwa cha kuchakata nyama cha Eliya Food Overseas Ltd kilichopo wilayani humo, kiasi kwamba uongozi wa kiwanda hicho umetishia kupunguza wafanyakazi kwa asilimia 50.


Akiongea kiwandani hapo jana, katika ziara yake akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo na bodi ya Nyama ,Naibu Katibu Mkuu wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo),Dkt Daniel Mushi aliutaka uongozi huo unakomesha mara moja vitendo vya utoroshaji wa mifugo kwa kuimarisha vikosi vya doria.


Awali kabla ya kufika katika kiwanda hicho kilichojengwa eneo la mauzo ya nje (EPZ) kwa thamani ya sh, bilioni 17 na kuzinduliwa na rais Samia Suluhu oktoba 18,2021


Naibu katibu mkuu alizungumza na wafanyabiashara wa mifugo katika mnada wa Ng'ombe wa Meserani na baadhi yao walikiri kupeleka mifugo nchini Kenya kwa njia za panya wakidai ni hatua ya wao kufuata soko zuri tofauti na wanalopata hapa nchini,hata hivyo walimhakilishia kuwa iwapo kiwanda hicho kitapandisha bei ya kununua mfugo kwa kilo watapeleka kuuza mifugo yao kiwandani hapo.


Dkt. Mushi aliwataka wafanyabiashara hao kuacha kutorosha mifugo nje ya nchi na kuwaeleza athari za kiuchumi ikiwa ni pamoja na kilikosesha taifa mapato,kukosa ajira pamoja na kukosa fedha za kigeni kupitia uuzaji wa nyama nje ya nchi unaofanya na mwekezaji wa kiwanda hicho cha Elia Food.


Alisema mwekezaji wa kiwanda hicho amekuwa akilalamika kukosekana kwa mifugo ya nyama wanaoletwa kiwandani katika kipindi cha zaidi ya miezi miwili kutoka mbuzi na Kondoo 4000 hadi kufikia mbuzi na kondoo 500 kwa siku na hii ni kutokana na mifugo mingi kupelekwa nchi jirani ya Kenya.


"Sisi kama serikali tunaowajibu wa kumlinda mwekezaji kwa nguvu zote kuhakikisha mifugo isitoroshwe na hapa niagize uongozi wa wilaya kupitia mkurugenzi awezeshe kikosi cha kuzuia utoroshaji wa mifugo (SPU)kiweze kufanya doria mara kwa mara na kwa ufanisi mkubwa"


Aidha Naibu katibu mkuu aliutaka uongozi wa wilaya hiyo kuwatumia viongozi wa kimila ,Laigwanani kuwaeleze athari zinazotokana na utoroshaji wa mifugo na kusababisha ukosefu wa ajira , fedha za kigeni na kukosa mapato ya serikali.


Akizungumzia suala la ukame aliutaka uongozi wa wilaya pamoja na mwekezaji kubuni njia mbadala ya chanzo cha maji ili wafugaji waache kuhamisha mifugo yao.


Awali mwekezaji wa kiwanda hicho,Irfhan Virjee alieleza kuwa wakati wanafungua kiwanda hicho mwaka 2019 walikuwa wakizalisha wastani wa mbuzi na Kondoo 300 kwa siku na baadaye walipandisha uzalishaji hadih tani 40 kwa siku sawa na wastani wa mbuzi na kondoo 4000 kwa siku.


Alisema hadi kufikia mwezi juni mwaka huu uzalishaji uliongezeka na kufikia tani 50 kwa siku,lakini baada ya hapo uzalishaji ulishuka kwa kasi kutoka mifugo 4000 kwa siku na kufikia mifugo 500 jambo ambalo limetokana na uhaba wa mifugo .


Alisema kiwanda kimekuwa kikiwalipa vizuri wauzaji wa mifugo ila changamoto kubwa, wafanyabiashara hao wanahitaji kulipwa fedha thasilim bila kupitia mfumo wa benki na hivyo kukwepa Kodi ya serikali kama ambayo wanafanya Nchini Kenya.

"Wakati tunapata changamoto ya mifugo tulifanya uchunguzi na kugundua mifugo mingi inapelekwa nchini Kenya kwa njia za panya ,na hivi sasa tunalazimika kufanyakazi siku tatu kwa wiki na hili tatizo ni zaidi ya miezi miwili sasa "


Aliongeza kuwa tatizo hilo limepunguza pia wastani wa mauzo kutoka dola za kimarekani milioni 3 kwa mwezi na kufikia wastani wa dola milioni 1 kwa mwezi.


Katika hatua nyingine Mkurugenzi mkuu wa kiwanda hicho,Shabir Virjee alipongeza uamuzi wa serikali kuingia ubia wa uwekezaji wa bandari kupitia kampuni ya kigeni ya DP World ya nchini Dubai akidai utakuwa msaada mkubwa kwao kwa kurahisisha usafirishaji wa mizigo.

"Kwa sisi wafanyabiashara tunaona ujio wa DP World utatusaidia kumaliza tatizo kubwa katika bandari ya Dar es Salaam kwani kwa sasa tunalazimika kutumia bandari ya Mombasa kutokana na ucheleweshaji wa mizigo",amesema

Share:

MBUNGE MTATURU AFANYA YAKE SEKTA YA ELIMU




MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu, ameshiriki mahafali ya darasa la saba ya Shule ya Msingi Mahambe na kukabidhi madawati 44 yenye thamani ya Shilingi Milioni 2.8 ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa samani shuleni hapo.

Mbali na madawati hayo pia amechangia Shilingi 500,000 ya kununua sinki la choo kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ,Shilingi 200,000 ya ufundi,gunia moja la mchele,sukari,jiko la gesi kwa ajili ya chai ya walimu asubuhi kama motisha na mipira miwili ya kuchezea wanafunzi netball na football.

Mh Mtaturu ametoa misaada hiyo kufuatia risala ya shule iliyosomwa na mwalimu Issa Omary.

“Maendeleo ya ufaulu ni mazuri ,lakini pamoja na mafanikio haya tunazo changamoto zinazowakabili wanafunzi na hivyo kuathiri maendeleo ya shule yetu,shule yetu inakabiliwa na uchakavu wa miundombinu ya shule,madarasa,nyumba za walimu na matundu ya vyoo,”ameeleza.

Amesema kama shule kwa kushirikiana na wazazi na wadau mbalimbali wamefanikiwa kutatua baadhi ya changamoto hizo kwa kuanzisha ujenzi wa matundu saba ya vyoo na sasa wapo hatua ya upigaji lipu na kuweka milango na masinki.

Amesema serikali kuu imewapeleka Shilingi Milioni 40 ili kujenga madarasa mawili na ofisi ujenzi ambao upo hatua ya Msingi.

Akikabidhi misaada hiyo Mtaturu amesema tangu anaingia bungeni aliweka bayana kuwa elimu ni kipaumbele chake cha kwanza na ndio maana amekuwa akijaribu kushirikiana na serikali kutatua changamoto zilizopo katika sekta hiyo.

“Niwapongeze sana kwa hatua mliyopiga ya kushiriki shughuli za maendeleo kwani maendeleo ni ya wananchi wenyewe,serikali inafanya kwa upande wake na jamii inao wajibu wa kushiriki kwenye miradi ya maendeleo ili kuimiliki na kuitunza,”amesema.

Amesema kazi ya kuhamasisha wanachi kushiriki shughuli za maendeleo aliianza mwaka 2016 na anafurahi kuona wananchi wameamua kuunga mkono serikali kutekeleza miradi ya maendeleo kinyume cha maneno ya awali kuwa serikali itafanya peke yake.

“Nimefurahi zaidi mmeweza kuchanga nafaka magunia 20 kwa ajili ya lishe shuleni,name nimewachangia mchele,sukari na gesi,niwaombe tuendelee kuiunga mkono serikali yetu ,”ameongeza.

Mtaturu amewahakikishia wananchi kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan itaendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia ili kuongeza ubora wa elimu na ufaulu sambamba na kuongeza idadi ya walimu kwenye shule zote.

Akiwa shuleni hapo Mtaturu amekagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa mawili na ofisi katika shule ya Mahambe ambayo serikali imepeleka fedha Shilingi Milioni 40.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi Diwani wa Kata ya Unyahati Abelly Suri amemshukuru Mbunge kwa kuendelea kuwa bega kwa bega na wananchi wakati wote.

“Mbunge umekuwa sauti yetu Bungeni kila mara tunakusikia ukitusemea,hata madarasa haya mawili tuliyoletewa ni matokeo ya kazi yako njema ya kutuombea fedha za miradi,tunaomba utufikishie shukrani zetu kwa Rais Samia kwani tunaona jitihada anazofanya katika kuwaletea wananchi maendeleo,”amesema.

Amesema wao Kata ya Unyahati ni mashahidi ,wamepokea fedha nyingi za miradi ya maendeleo ikimemo Shilingi Milioni 140 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule ya Msingi Matare.

“Tumepokea pia Shilingi Milioni 967 za ujenzi wa madarasa na bweni katika shule ya sekondari ya Unyahati na Shilingi Milioni 258 kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa maji kijiji cha Matare,hizi ni fedha nyingi zimetolewa na shukrani zetu ni kuzidi kumuombea awe na afya njema ya kuwatumikia watanzania,”ameshukuru.

Shule hiyo ilianzishwa mwaka 1979 na ina wanafunzi 467 walimu 8.
Share:

Thursday 31 August 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 1, 2023

















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger