Saturday 29 July 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 29,2023



 


Share:

WAFANYAKAZI WA HOTELINI WAHIMIZWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII




Na Mwandishi Wetu, Arusha

Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imetoa wito kwa wafanyakazi wa hotelini kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ili kujiwekea akiba itakayowasaidia kwenye maisha yao.

Ofisa kutoka Idara ya Hifadhi ya Jamii wa Ofisi hiyo, Charles Liganya ametoa rai hiyo Julai 28, 2023 jijini Arusha alipokuwa akitoa elimu kwa wafanyakazi wa hotelini wanaopewa mafunzo ya kukuza ujuzi kwa uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi.

Liganya amesema wafanyakazi hao wanapaswa kujiunga na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili waweze kunifaika na Mafao yatolewayo na mfuko huo.

Pia amewahakikishia kuwa sekta ya hifadhi ya jamii kwa ujumla inasimamiwa vema na Ofisi ya Waziri Mkuu (Idara ya Hifadhi ya Jamii) na kama kuna changamoto ambayo haijatatuliwa na mfuko wawasilishe kwenye Idara hiyo ili kushughulikiwa.

Naye, Mkurugenzi Msaidizi wa Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi hiyo, Robert Masingiri, amesema suala la bima ya afya na pensheni ni kwa wafanyakazi hao ili kuwa na uhakika wa matibabu na maisha yao. Awali, Meneja Huduma kwa Wanachama kutoka NSSF, Robert Kadege, amesema mfuko una utaratibu wa kisheria wa kufuatilia michango ya mwanachama kwa mwaajiri wake ikiwamo kuwafikisha mahakamani ili kunusuru michango ya wafanyakazi ambao haijawasilishwa NSSF.

Share:

MKOA WA DODOMA WABAINIKA KUWA NA ORODHA YA MADINI MENGI ZAIDI YA MIKOA MINGINE


Kaimu Meneja Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Bw.Maswi Solomon,akimkabidhi kitabu cha Madini Yapatikanayo Tanzania toleo la tano kwa Mkuu wa Mkoa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule hafla iliyofanyika leo Julai 28,2023 jijini Dodoma.PICHA NA ALEX SONNA

Na.Samwel Mtuwa - GST

Utafiti umebaini kuwa Mkoa wa Dodoma una aina nyingi za madini kulinganisha na mikoa mingine nchini.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za madini zilizofanywa na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania(GST) zimeonesha kupitia kitabu kipya cha madini yapatikanayo Tanzania.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 28/7/2023 na Kaimu Meneja wa sehemu ya jioloji GST Maswi Solomon wakati akikabidhi kitabu cha Madini Yapatikanayo Tanzania toleo la tano kwa mkuu wa mkoa Dodoma Bi. Rose Senyamure.

yamesemwa na Mtaalam kutoka GST Bw. Maswi Solomon wakati akikabidhi Kitabu cha Madini Yapatikanayo Tanzania toleo la Tano kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule.

Akieleza sababu za mkoa huo kuwa na aina mbalimbali za madini Maswi amesema kuwa ni kutokana na Mkoa wa Dodoma kuwa kwenye Ukanda maalum wa jiolojia unaupitiwa na mabadiliko tofauti ya kijiolojia na kuufanya kuwa na orodha ya madini mengi ya aina mbalimbali kuliko Mikoa mingine yote ukifuatiwa na Mkoa wa Morogoro na Lindi.

Maswi alieleza kuwa baadhi ya madini hayo ni madini mkatakati kama vile Lithium, Nikel, Chuma, Urani, Shaba na Helium.

Aidha, baadhi ya madini mengine ambayo yametambuliwa kuwa Muhimu kwenye matumizi ya viwanda vya ndani ni pamoja na madini ya Chokaa, Jasi, Feldspar, Mfinyanzi, Quartz na Kyanite.

Madini mengine ambayo ni ya kipekee kwa sasa yanapatikanayo Tanzania tu ambayo ni madini ya Yoderite ambayo yako katika Mlima wa Mautia Wilaya ya Kongwa Mlima ambao GST imeshauri uhifadhiwa kwa ajili ya utalii wa jiolojia ikiwemo watafiti na wanafunzi kujifunzia na kushuhudia madini hayo.

Kitabu hiki kimekabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la Waziri Mkuu alilo litoa akiwa Mwanza kwenye Mkutano wa Femata mwaka 2023.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule,ameipongeza GST kwa jitihada za kutangaza fursa za madini nchini na kuahidi kutumia taarifa hizo kwa kuvutia uwekezaji katika mkoa wa Dodoma ambao unaongoza kwa wingi wa aina mbalimbali za madini.



Kaimu Meneja Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Bw.Maswi Solomon,akizungumza kabla ya kukabidhi kitabu cha Madini Yapatikanayo Tanzania toleo la tano kwa Mkuu wa Mkoa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule hafla iliyofanyika leo Julai 28,2023 jijini Dodoma.


Mkuu wa Mkoa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule,akizungumza mara baada ya kupokea kitabu cha Madini Yapatikanayo Tanzania toleo la tano hafla iliyofanyika leo Julai 28,2023 jijini Dodoma.


Kaimu Meneja Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Bw.Maswi Solomon,akimkabidhi kitabu cha Madini Yapatikanayo Tanzania toleo la tano kwa Mkuu wa Mkoa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule hafla iliyofanyika leo Julai 28,2023 jijini Dodoma.


Kaimu Meneja Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Bw.Maswi Solomon,akimuonesha Ramani Mkuu wa Mkoa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule sehemu yanayopatikana Madini mara baada ya kupokea kitabu cha Madini Yapatikanayo Tanzania toleo la tano kwa hafla iliyofanyika leo Julai 28,2023 jijini Dodoma.


Mkuu wa Mkoa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule akionyesha kitabu cha Madini Yapatikanayo Tanzania toleo la tano mara baada ya kukabidhi na Kaimu Meneja Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Bw.Maswi Solomon, hafla iliyofanyika leo Julai 28,2023 jijini Dodoma.


Mkuu wa Mkoa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa kitabu cha Madini Yapatikanayo Tanzania toleo la tano na Kaimu Meneja Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Bw.Maswi Solomon, hafla iliyofanyika leo Julai 28,2023 jijini Dodoma.
Share:

KAMATI YA USHAURI VIWANDA YAZINDULIWA NELSON MANDELA

Kamishna wa Elimu Lyabwene Mtahabwa (wa kwanza kushoto) akika utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kamati ya Ushauri wa Viwanda kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi yaani (Higher Education for Economic Transformation (HEET Project) leo tarehe 28 Julai,2023 jijini Arusha.
Kamishna wa Elimu Lyabwene Mtahabwa akisisitiza jambo katika hafla uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Viwanda kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi yaani (Higher Education for Economic Transformation (HEET Project) wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Afrika Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Anthony Mshandete akiongea na wajumbe waliohudhuria uzinduzi rasmi wa Kamati ya Ushauri wa Viwanda kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi yaani (Higher Education for Economic Transformation (HEET Project) wa taasisi hiyo leo tarehe 28 Julai,2023.
Kamishna wa Elimu Lyabwene Mtahabwa (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela mara baada ya uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Viwanda kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi yaani (Higher Education for Economic Transformation (HEET Project) leo tarehe 28 Julai ,2023. 

Na Mwandishi wetu

Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi yaani (Higher Education for Economic Transformation (HEET Project) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia imezindua Kamati ya Ushauri wa Viwanda kwa lengo la kuangalia mambo mbalimbali yatakayoinua uchumi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo leo tarehe 28 Julai, 2023 Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa alisema endapo wanasayansi wabobezi wakifanya tafiti vema wataweza kutatua changamoto za ajira ikiwemo kujua viwanda vinataka nini ili kuwezesha vijana kupata fursa za ajira na kujikwamua kiuchumi.

"Ukiwa mwanasayansi usiache mila na desturi za kitanzania,fanyeni bunifu zenu na kuleta maendeleo katika nchi ikiwemo kujua viwanda vinataka nini na ninyi kufungua fursa kwa vijana " alisema Kamishna Dkt. Lyabwene Mtahabwa

Naye Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Cha Nelson Mandela Profesa Anthony Mshandete alisema kamati hiyo italeta chachu katika utengenezaji wa mitaala na kujibu changamoto za viwanda na jamii, ambayo ni hatua kubwa ya kubadilisha fikra za watafiti.

"Zile bunifu na gunduzi zibadilishwe na kuwa biashara pamoja na bidhaa zinazozalishwa kutokana na utafiti lazima sasa chuo chetu kisonge mbele katika kukuza sekta ya ajira " alisema Profesa Anthony Mshandete

Wakati huo huo, Profesa Suzana Augustino ambaye ni Mkuu wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) aliongeza kuwa, mradi huo unalenga kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa elimu ya juu.

Profesa Suzana anazidi kueleza kuwa mradi huo unalengo la kubadili mitaala ili wataalam watakaozalishwa kutoa mchango kwa taifa na jamii, ikiwemo uboreshaji wa mifumo ya Tehama katika kufundisha na kufanya tafiti na kuleta maendeleo ya teknolojia na ubunifu nchini Tanzania.

"Tunataka mifumo yetu itoe shahada za uzamili na uzamivu kwa kutumia tehama popote mwanafunzi atakapokuwepo ndani na nje ya nchi, ikiwemo mageuzi makubwa katika maabara na kupewa udhibiti ili kupokea kazi zinazotoka nchi mbalimbali na kusaidia kuzichakata katika masuala nishati,udongo,tafiti na tehama"alisema Profesa Suzana

Aliongeza kuwa, kamati hiyo itatoa ushauri zaidi katika kufikia jamii hususani sekta binafsi viwandani ambapo kumekuwa na tofauti kubwa sana kati ya watafiti na kwenye viwandaili kuhakikisha teknolojia zinazozalishwa zinafika kwa jamii na sekta ya viwanda, katika kuchangia maendeleo ambayo taifa inahitaji katika kupata mpango mkakati wa maendeleo ifikapo mwaka 2050.
Share:

Friday 28 July 2023

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI WA MAJI SAFI BUGAYAMBELELE...BABU WA MIAKA 103 ATUMA SALAMU KWA RAIS SAMIA

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdallah Shaib Kaim amezindua rasmi Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) wenye thamani ya Shilingi 279,465,134.40.

Akizungumza leo Alhamisi Julai 28,2023 baada ya kukagua mradi huo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim ameipongeza SHUWASA kwa kutekeleza mradi wa maji kwa kiwango bora na thamani ya fedha imeonekana.


“Tumekagua mradi na nyaraka kwa kina, kazi nzuri imefanyika hivyo Mwenge wa Uhuru unazindua Mradi huu. Naipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa inayofanya katika utekelezaji wa miradi maji ili kumtua mama ndoo kichwani”,amesema Kaim.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA CPA Sarah Emmanuel amesema mradi huo unatarajiwa kunufaisha wakazi 10,165 kwa kuwawezesha kupata huduma ya majisafi na salama kutoka katika mtandao huo na kuwafanya waondokane na adha ya kufuata maji mbali kama ilivyokuwa hapo awali kwa kuongeza eneo la huduma na kuweka mabomba makubwa ya usambazaji wa maji.

Amesema kwa sasa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 100 ya utekelezaji wake na huduma inaendelewa kutolewa kwa wananchi.

Amesema Mradi huo wa Maji katika Kijiji cha Bugayambelele – Manispaa ya Shinyanga ulisanifiwa na Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) Shinyanga kwa kuongeza mtandao wa maji kilometa 8.041 ambapo awali RUWASA ilijenga kilometa 1.5 na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) ilijenga kilometa 6.459.

“Uongozi wa Mkoa wa Shinyanga unaendelea kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza Miradi ya Maji na kupunguza adha kwa wananchi ya kutopata majisafi, salama na yenye kutosheleza”,amesema.


Nao baadhi ya wananchi akiwemo Mzee John Maganga Midelo (103) na Fortunatha Allan Malongo wameishukuru serikali kuwa kuwapelekea mradi wa maji kwani walikosa huduma hiyo kwa muda mrefu na sasa wameanza kupata huduma ya maji safi na salama.

“Tunamshukuru sana Mhe. Rais Samia kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya kuleta maendeleo. Kiongozi wa mbio za Mwenge nakuomba upeleke salamu kwa Mhe. Rais Samia kwamba sisi tunampenda sana, aendelee kuchapa kazi ili kuwaletea maendeleo Watanzania”,amesema Mzee Midelo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akizindua rasmi Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga leo Julai 28,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim (katikati) akizindua rasmi Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga leo Julai 28,2023. Katikati ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini , Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim (kushoto) akimtwisha ndoo kichwani Fortunatha Allan wakati akizindua rasmi Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga leo Julai 28,2023. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim (kushoto) akimtwisha ndoo kichwani Fortunatha Allan wakati akizindua rasmi Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga leo Julai 28,2023. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim (kushoto) akimtwisha ndoo kichwani mkazi wa Bugayambelele wakati akizindua rasmi Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga leo Julai 28,2023. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim na viongozi mbalimbali wakipiga makofi wakati wa uzinduzi rasmi wa Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga leo Julai 28,2023
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim na viongozi mbalimbali wakipiga makofi wakati wa uzinduzi rasmi wa Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga leo Julai 28,2023
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akizungumza katika Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga leo Julai 28,2023
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akizungumza katika Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga leo Julai 28,2023
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA CPA Sarah Emmanuel akisoma taarifa ya ujenzi wa Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga leo Julai 28,2023
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA CPA Sarah Emmanuel akielezea kuhusu ujenzi wa Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga leo Julai 28,2023
Mkazi w Bugayambelele Fortunatha Allan akiishukuru Serikali kujenga Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA CPA Sarah Emmanuel akisoma taarifa ya ujenzi wa Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga leo Julai 28,2023
Viongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wakikagua nyaraka za ujenzi wa Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga
Muonekano sehemu ya mradi wa maji
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza katika Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga
Mzee John Maganga Midelo akiishukuru serikali kupeleka mradi wa maji katika Kijiji cha Bugayambelele. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini , kulia ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim
Mzee John Maganga Midelo akishika Mwenge wa Uhuru .Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini , kulia ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim
Mzee John Maganga Midelo akishika Mwenge wa Uhuru
Wafanyakazi wa SHUWASA wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga
Wajumbe wa bodi ya SHUWASA na viongozi wa RUWASA wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga
Wafanyakazi wa SHUWASA na RUWASA wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA CPA Sarah Emmanuel akisalimiana na Mzee John Maganga Midelo
Wafanyakazi wa SHUWASA wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye Mradi wa Maji Safi na Salama kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA CPA Sarah Emmanuel (kulia) wakipiga picha ya kumbukumbu
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA CPA Sarah Emmanuel (kulia) wakipiga picha ya kumbukumbu.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger