Sunday 2 April 2023

BARRICK YADHAMINI KONGAMANO LA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU LILILOFANYIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA


Afisa Raslimali Mwandamizi wa Barrick Bulyanhulu,Renatus Malawa, akiongea na Wanafunzi katika kongamano la kuwajengea uwezo lililoandaliwa na taasisi ya AISEC Tanzania na kufanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Afisa Raslimali Mwandamizi wa Barrick Bulyanhulu,Renatus Malawa, akiongea na Wanafunzi katika kongamano la kuwajengea uwezo lililoandaliwa na taasisi ya AISEC Tanzania na kufanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Mkurugenzi wa elimu ya juu kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Dk.Kenedy Hosea ambaye alikuwa ni mgeni rasmi akiongea wakati wa kongamano hilo.
Wanafunzi wa UDOM na baadhi ya Maofisa wa Barrick wakifuatilia matukio wakati wa kongamano hilo.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, afande Maganga pia alipata fursa ya kuongea na Wanafunzi.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi, viongozi wa AISEC Tanzania, Jeshi la Polisi na wafanyakazi wa Barrick.
 ****
Kampuni ya Barrick Gold Corporation, imedhamini na kushiriki katika kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu lililoandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AISEC Tanzania) lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na kuwashirikisha wanafunzi,wahadhiri na wadau mbalimbali.

Kupitia kongamano hili ambalo hufanyika kila mwaka, wanafunzi huweza kufahamu jinsi taasisi mbalimbali nchini zinavyoendesha shughuli zake lengo kubwa ikiwa ni kuwajengea uwezo wa kujua vipaji walivyonavyo, kujifunza jinsi ya kujiamini na kukabiliana na ushindani katika soko la ajira, kujitambua uwezo wao ni jinsi gani wanaweza kushiriki kutoa mchango wa kuendeleza taifa pindi wamalizapo masomo yao.


Maofisa Waandamizi wa Barrick pia walishiriki katika maonesho na kongamano hilo ambapo walipata fursa kuzungumza na wanafunzi kuhusiana na kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ajira,kuendeleza vipaji vyao pia wanafunzi walipata fursa kuelewa jinsi kampuni ya kimataifa ya Barrick, inavyoendesha shuguli zake kwa kutoa kipaumbele kusaidia jamii sambamba na mpango wake wa kuibua na ukuzaji wa vipaji kwa vijana wa kitanzania na wafanyakazi wake.
Share:

BENKI YA CRDB YAWAPA SOMO WANAFUNZI WA CHUO KIKUU DODOMA


Kaimu Mkuu wa Kitengo cha mafunzo na uendelezaji wa wafanyakazi benki ya CRDB Edith Muyombela akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) alipoelezea huduma zinazotolewa na benki hiyo lililofanyika Aprili 01,2023 katika ukumbi wa CIVE Auditorium chuoni hapo Jijini Dodoma
Benki ya CRDB kwa imeshiriki katika Kongamano la kuwajengea uwezo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiuongozi pindi wamalizapo masomo, lililofanyika Aprili 01,2023 katika ukumbi wa CIVE Auditorium chuoni hapo.



Benki ya CRDB imekuwa ni moja ya benki kiongozi nchini katika kuhakikisha inashiriki kuelimisha makundi ya vijana wa vyuo mbalimbali nchini kupitia program mbalimbali yakiwemo Mafunzo kwa vitendo ‘Field attachmets’, Mafunzo kazini 'Ínternship’ na Programu maalumu ya Maendeleo ya wahitimu ‘Apprenticeship’ ambayo yalianzishwa mwaka 2020 kwa kuwachukua wahitimu 29 kutoka nchini Tanzania na 2 kutoka nchini Burundi.


Pia Benki ya CRDB kila mwaka huchukua kati ya wanafunzi 300 hadi 500 na kuwaunganisha katika vitengo mbalimbali vilivyopo ndani ya benki hiyo na kwenye matawi yake yaliyosambaa kote nchini ilikuweza kuwapatia mafunzo ya vitendo.


Kongamano hilo lililohudhuriwa na Mkurungenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ,Dk Kenedy Hosea, Benki ya CRDB iliwakilishwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha mafunzo na uendelezaji wa wafanyakazi, Edith Muyombela.


Wanafunzi wa vyuo nchini wamekuwa wakifurahia huduma mbalimbali za kibenki kutoka Benki ya CRDB ikiwa ni pamoja na upatikananji wa mikopo maarufu kama Boom Advance umekuwa ni mkombozi kwa wanafunzi wengi wanaotumia benki ya CRDB kwakujipatia mikopo rahisi hivyo kurahisisha kukabiliana na changamoto mbalimbali za kifedha.


Pia Benki ya CRDB imewatengenezea akaunti maalumu ya wanafunzi wa vyuo ambayo gharama zake za kufungua akaunti hiyo ni shilingi za Kitanzania Elfu Tano tu (5,000). wastani wa mikopo 20,000 inatolewa kila Mwezi kwa wanafunzi mbalimbali nchini, na wastani wa akaunti 50,000 zinafunguliwa kila mwaka na wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu nchini.


Kwa miaka kadhaa, Benki ya CRDB imekuwa Mshirika wa Umoja wa Taasisi za Elimu ya juu za wanafunzi nchini Tanzania ‘AIESEC’.

Mkurungenzi wa elimu ya Juu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ,Dk Kenedy Hosea (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Wafanayakazi wa Benki ya CRDB kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo alipotembelea banda la CRDB Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) lililofanyika Aprili 01,2023 katika ukumbi wa CIVE Auditorium chuoni hapo Jijini Dodoma Kaimu Mkuu wa Kitengo cha mafunzo na uendelezaji wa wafanyakazi benki ya CRDB .Edith Muyombela akiwa kwenye Banda la CRDB ambapo walikua wakielezea kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) huduma zinazotolewa na benki hiyolililofanyika Aprili 01,2023 katika ukumbi wa CIVE Auditorium chuoni hapo Jijini Dodoma
Share:

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA REA NA KUHAMASISHA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA ZA UMEME VIJIJINI


Veronica Simba na Issa Sabuni - REA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imesema imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini mkoani Singida na imewashauri wananchi wanaoishi vijijini waliofikiwa na huduma ya umeme, kuitumia nishati hiyo kwa matumizi yenye tija hususani katika shughuli za kujiongezea kipato na kukuza uchumi.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Irisya wilayani Ikungi, Mkoa wa Singida, wakati wa ziara ya Kamati hiyo kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili (R3R2), Aprili Mosi 2023, Makamu Mwenyekiti wa PIC, Augustino Vuma amesema lengo la Serikali kupeleka umeme vijijini ni kuwarahisishia wananchi kutekeleza kwa ufanisi shughuli mbalimbali za kiuchumi ili wajiletee maendeleo hivyo kutoitumia nishati hiyo ni kurudisha nyuma juhudi hizo za Serikali.

“Nitoe rai kwa wananchi kuitumia vizuri fursa hii ya uwepo wa umeme kwa kubuni shughuli mbalimbali za kiuchumi ili sasa ile dhana ya Serikali kuleta umeme hapa iweze kuonekana kwa maana ya kuchochea ukuaji wa uchumi na faida nyinginezo,” amesisitiza.

Aidha, Makamu Mwenyekiti amewaagiza Watendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuendelea kuwasimamia kwa ukaribu wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini ili kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuheshimu mikataba yao na kufanikisha azma ya Serikali kuwafikishia umeme wananchi wote waishio vijijini waweze kujikwamua kiuchumi.

Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti wa PIC ameeleza kuwa Kamati imeridhishwa na utekelezaji wa Mradi wa R3R2 huku akibainisha kuwa tayari manufaa yake yamekwishaanza kuonekana.




“Leo tumekuwa hapa katika Shule ya Sekodari Irisya na tumeshuhudia kwa macho yetu kwamba wanafunzi wameshaanza kunufaika kwani umeme umeingia kwenye Maabara na kufika katika madarasa hivyo kuwawezesha kujisomea hata nyakati za usiku.”

Akifafanua zaidi, amesema Kamati imeshuhudia uwepo wa umeme katika Maabara ya Fizikia na nyinginezo na kuwawezesha wanafunzi kusoma kwa vitendo. Amesema kuwa, kupitia uwepo wa umeme, matarajio ni kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wa masomo ya sayansi na kwamba ufaulu katika masomo yote pia utaongezeka kwani mazingira yameboreshwa.

Vilevile, ameongeza kwamba kuhusu manufaa kwa wananchi, umeme umeanza kuwafikia hivyo wataweza kufanya shughuli za kiuchumi ikiwemo kuanzisha viwanda vidogo vidogo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Janet Mbene pamoja na kuunga mkono uhamasishaji wananchi kuunganisha umeme katika makazi na shughuli za kiuchumi, amesema ni faraja kwa REA kuona umeme unaendelea kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali vijijini.

“Lengo letu ni lilelile, kuhakikisha kwamba kila kijiji kinapata umeme na hatimaye uwasaidie wananchi kiuchumi, kijamii na hata kimaendeleo kwa maana ya elimu na vitu vingine,” amesisitiza.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mbele ya Kamati ya PIC, Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Irisya, Ernest Edward wametoa shukrani kwa Serikali kupitia REA kwa kufikisha umeme katika kijiji hicho.

Awali, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini mkoani Singida kwa Kamati, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy ameeleza kuwa Serikali kupitia Wakala hiyo imetoa jumla ya shilingi bilioni 73.1 na Dola za Marekani 988,707.60 ili kuhakikisha miradi minne inayotekelezwa mkoani humo inakamilika na wananchi wanapatiwa huduma ya nishati hiyo ili kujipatia maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Aidha, ameeleza zaidi kuwa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika Wilaya za Ikungi na Singida unatekelezwa na Mkandarasi M/s Central Electricals International Ltd kwa gharama ya shilingi bilioni 26.3 na katika Wilaya za Iramba, Manyoni na Mkalama, unatekelezwa na M/s CRJE – CTCE Consortium kwa gharama ya shilingi bilioni 31.6




Amesema kuwa, maendeleo ya Mradi kwa wastani yamefikia asilimia 70.21 ambapo kwa Wilaya za Ikungi na Singida, Mkandarasi amefikia asilimia 77.54 na Wilaya za Iramba, Manyoni na Mkalama, Mkandarasi amefikia asilimia 62.87

Mkoa wa Singida una jumla ya vijiji 441 ambapo vijiji 287 vimekwishapatiwa umeme kupitia miradi ya umeme vijijini iliyotekelezwa awali. Vijiji 169 vilivyobaki vinaendelea kuunganishiwa umeme kupitia Wakandarasi waliotajwa.
Share:

DCEA KUANZA MSAKO KUDHIBITI BIASHARA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA



********** 

KAMISHINA Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya DCEA), Aretas James Lyimo ametaja malengo yake ambayo ameingia nayo ili kuhakikisha mamlaka hiyo inadhibiti kabisa biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Ameyasema hayo leo Aprili Mosi, 2023 mkoani Mtwara wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ambapo mamlaka hiyo inashiriki kikamilifu katika mbio za mwenge huku akiweka wazi mipango yake ya kuhakikisha wanakabiliana na changamoto hiyo.

"Kwa hiyo nitoe wito kwa watumiaji wa dawa za kulevya kuacha wenyewe kutumia dawa za kulevya, lakini pia kwa wale wauzaji na wasambazaji wa dawa za kulevya kuacha kabisa hiyo biashara ya dawa za kulevya, kwani kuanzia sasa tunafanya operesheni kabambe nchi nzima, lakini tutahakikisha vijiwe vote vya wauzaji, na watumiaji wa dawa za kulevya tunavisambaratisha.

Mbio za Mwenge kitaifa kwa mwaka 2023 katika uwanja wa CCM Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara leo Aprili Mosi, 2023 zimezinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri va Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

Aidha, Kamishana Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas James Lyimo amesema, ushiriki wao katika mbio hizo una umuhimu mkubwa.

"Tupo hapa Mtwara katika tukio hili la uwashaji wa Mwenge, kwa sababu Mwenge unatembea nchi nzima kwa ajili ya kukemea maovu, kuhakikisha kwamba, maovu yanaondoka kwenye jamii nchini, na sisi kama Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, dawa za kulevya ni sehemu moia wapo va maovu ambayo yanakemewa na Mwenge.
Share:

Saturday 1 April 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRILI 2, 2023























Share:

DKT. ABBASI: TUTAITANGAZA NCHI KWA VIWANGO VYA KIMATAIFA


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, amesema nia kuu ya Wizara hiyo kwa sasa ni kufanya uhifadhi na kutangaza utalii kwa viwango vya kimataifa.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Aprili 1, 2023 alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na kukutana na viongozi wa hifadhi hiyo iliyopo Morogoro ambapo pia aliendesha kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Mradi wa Kuendeleza Utalii wa Maeneo ya Kusini mwa Tanzania (Regrow).

“Tutahifadhi na baada ya kuhifadhi tutatangaza na maono ya viongozi wetu kwa sasa kupitia kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri wetu Mhe. Mohamed Mchengerwa ni kujipanga kuutangaza utalii wa Tanzania Kimataifa zaidi, niwaahidi tu kwamba hatutakiwa na jambo dogo,” alisema Dkt. Abbasi.

Ameongeza kuwa hizi ni zama za Royal Tour, akisisitiza kuwa kama Rais Samia alitoka na kuutangaza utalii wetu kwanini sisi tujifungie maofisini na kuwahimiza viongozi hao kutumia teknolojia za kisasa kuhifadhi na kutangaza utalii wetu.

“Kuna mtafiti mmoja pia ameonesha watu wengi nchini hawaendi kutalii kwasababu wana woga wa gharama na namna ya kufika kwenye maeneo husika.

“Tuanzishe vifurishi mbalimbali vya kuwavuta watalii wa ndani na nje, sikukuu zinakuja je tumejipanga vipi kutangaza vivutio vyetu, je watu wanajua bei zetu na kwanini tusiwe na vifurushi maalum kwa ajili ya hizi sikukuu, naamini tunaweza kupata watalii wengi kupitia hizi sikukuu,” alisisitiza.

Akiongoza Kikao cha ziada cha Kamati ya Uongozi ya Mradi wa REGROW, Dkt. Abbasi amesema mradi huo umechelewa kwa sababu mbalimbali na kuagiza kuwa kila taasisi husika ihakikishe kwa siku zilizobaki za mradi hakuna mkandarasi anaongezewa muda bila hoja zito na wasioweza waondolewe mapema kabla hata ya kusaini mikataba.

Share:

MALUNDE ASHINDA TUZO YA MTU BORA WA VYOMBO VYA HABARI 2022/2023 'BEST MEDIA PERSONALITY AWARD'


Mkurugenzi wa Mtandao Maarufu wa Malunde 1 blog www.malunde.com ndugu Kadama Malunde ametangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Mtu Bora wa Vyombo vya Habari Shinyanga 'Best Media Personality Awards 2022/2023' zilizoandaliwa na Taasisi ya Holysmile ambayo ni inatoa huduma za Sanaa, Utamaduni na Burudani pamoja na kutambua na kuthamini juhudi na harakati zinazofanywa na wadau wote wa maendeleo iliyosajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Kadama Malunde, ambaye ni Mwandishi wa Habari Mkoani Shinyanga ametangazwa Mshindi Mtu Bora wa vyombo vya habari 2022/2023/ Mtu Bora wa Vyombo vya Habari/Best Media Personality/ Mwandishi wa Habari Mwenye Mvuto na Ushawishi katika Media wakati wa tamasha la utoaji tuzo (SHINYANGA MDAU SHUPAVU AWARDS) lililofanyika Machi 31,2023 Mjini Shinyanga.
 


 

Share:

ZAIDI YA WAGONJWA 410 WAHUDUMIWA KATIKA KAMBI MAALUM MKOANI TABORA


Na Mwandishi wetu- Tabora

Zaidi ya wagonjwa 410 wamepata matibabu ya kibingwa na kibobezi katika kambi maalum ya siku 5 iliyofanyika katika hospitali ya Rufaa Nkinga, Tabora kwa ushirikiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na hospitali ya Rufaa Nkinga ambapo wagonjwa 20 wamefanyiwa upasuaji mkubwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Rufaa Nkinga Mr. Victor Ntundwe amewashukuru Madaktari bingwa, Wauguzi na Mtaalam wa usingizi wa Taasisi ya MOI kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha katika kambi hiyo ambayo imewajengea uwezo wataalam wa hospitali ya Rufaa Nkinga

“Tumepata shuhuda nyingi kutoka kwa wagonjwa mbalimbali ambao walikuwa hawana uwezo wa kwenda Dar es Salaam kuzifuata huduma hizo na wamefurahi sana kuona huduma hizo zinatolewa hapa hospitali ya Rufaa Nkinga ” Alisema Bw. Ntundwe

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amesema wamefanya kambi hiyo kwa lengo la kujengeana uwezo wa kutoa tiba bobezi ambazo zinapatikana katika hospitali ya MOI.

“Tunatekeleza kwa vitendo agizo la Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kusogeza huduma za kibingwa na kibobezi karibu na wananchi na kambi hii itakuwa endelevu kila baada ya muda Fulani wataalam wa MOI watakuwa wanakuja hapa” amesema Dkt. Boniface

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa hospitali ya Rufaa Nkinga Dkt. Tito Chaula amesema kulikuwa na uhitaji mkubwa wa huduma za tiba bobezi ukanda wa magharibi na zaidi ya wagonjwa 410 wametibiwa katika kambi hiyo na wagonjwa 20 wamefanyiwa upasuaji wa mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu.

Afisa Muuguzi kutoka kitengo cha upasuaji MOI Bi. Jane Mdalingwa amesema kwa muda waliokuwa pamoja wameweza kufundishana viwango ya chumba cha upasuaji inavyotakiwa ili mgonjwa anavyofanyiwa upasuaji asipate maambukizi yeyote na maandalizi ya mgonjwa kabla hajaingia chumba cha upasuaji.

Mkazi wa Geita Edina Joramu ameishukuru Taasisi ya MOI kwa kusogeza tiba za kibobezi mkoani Tabora kwani angetumia gharama Zaidi kwa kufuata huduma hizo Mwanza, Dodoma au Dar es Salaam.


Share:

DITOPILE AUNGANA NA WANA KONGWA KWA IFTAR, WAMUOMBEA DUA RAIS SAMIA


Katika Muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe. Mariam Ditopile ameungana na Waumini zaidi ya 500 katika Msikiti mkubwa Kata ya Mkoka, Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma katika Iftari na Dua Maalum ya kuiombea Nchi na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Kabla ya Dua hiyo Mhe. Mbunge alitembelea Shule ya Msingi Mkoka Kitengo Maalum cha Wanafunzi wenye mahitaji Maalumu(walemavu) na kuwapelekea sadaka, vitabu, kalamu na mahitaji ya shule mbalimbali.


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe Mariam Ditopile anaendelea kuwatakia Waislamu wote nchini Ramadhani njema.
Share:

SIMBA SC YASHINDWA KUFURUKUTA MBELE YA RAJA CASABLANCA, YANYUKWA 3-1



Simba SC imemaliza michezo ya hatua ya makundi kwa kufungwa 2-1 dhidi ya kinara wa kundi hilo, Raja Casablanca (Morocco) aliyeshinda michezo 5 na kusare 1 hivyo kupata alama 16.

Raja Casablanca ilianza kupata bao kupitia kwa Hamza Khabba kabla ya Simba Sc kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wao hatari raia wa DR Congo Jean Baleke.


Mabao mengine yalifungwa na Mohamed Boulacsou pamoja na Hamza Khabba ambaye kwenye mchezo huo aliweza kupachika mabao mawili na kuisaidia timu yake kuondoka na ushindi huo mnono.


Simba SC wapili akiwa na alama 9, AC Horoya ((Guinea) wa tatu akiwa na alama 7 ilhali Vipers FC (Uganda) imeshika mkia ikiwa na alama 2.


Raja Casablanca na Simba SC walishafuzu hatua ya robo fainali hivyo wanasubiri droo ambayo iyachezeshwa Jumatano Aprili , 2023 nchini Misri
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger