Friday 3 February 2023

TANZANIA GIRL GUIDES ASSOCIATION WAENDESHA KAMPENI YA UPANDAJI MITI SHULE YA MSINGI NDEMBEZI

 


Kampeni ya upandaji miti ikiendelea katika shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.


Na Marco Maduhu, SHINYANGA

CHAMA kisicho cha kiserikali Tanzania Girl Guides Association kimeendesha Kampeni ya upandaji miti katika shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na athari za mazingira.

Kampeni hiyo imefanyika leo Februari 3, 2023 ikiwa ni mwendelezo wa Kampeni ya kuhamasisha wananchi kupanda miti kwenye Kaya zao, pamoja na Taasisi za Serikali zikiwamo shule za Msingi na Sekondari, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Katibu Tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoani Shinyanga Beda Chamatata, akimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa huo.

Akizungumza kwenye Kampeni hiyo ya upandaji Miti Wakala Mtetezi wa Mradi wa Msichana na Mabadiliko ya Tabia nchi kutoka Tanzania Girl Guides Association, Joyce Maganga, amesema kampeni hiyo ya upandaji miti ilianza Rasmi mwaka 2021, na wameshapanda miti mingi katika shule za Msingi Manispaa ya Shinyanga.

Amesema upandaji miti katika shule hiyo ya Msingi Ndembezi ni mwendelezo wa Kampeni ambayo wamekuwa wakiiendesha mashuleni kupanda miti, ambapo wameshapanda pia miti 300 katika shule ya Msingi Ujamaa, Miti 200 shule ya Msingi Jomu.

“Leo katika Shule hii ya Msingi Ndembezi tumepanda Miti zaidi ya 1,000, na kampeni hii ni endelevu ili kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na athari za mazingira,”amesema Maganga.

“Nawaomba viongozi na watoa maamuzi katika vikao vyenu ajenga ya kuhamasisha wananchi kupanda miti hasa katika msimu wa mvua iwe ya kudumu, ili ipandwe miti mingi ya kutosha na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,”ameongeza.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, amepongeza kampeni hiyo ya upandaji miti ambayo itasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kupata mvua za kutosha na kuondokana na hali ya ukame.

Mgeni Rasmi Katibu Tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoani Shinyanga Beda Chamatata, akimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa huo, amewataka wanafunzi kuitunza miti hiyo ili ikue na kuwapatia faida mbalimbali ikiwamo kivuli na kuzuia mmomonyoko wa udongo.

Ametaja faida nyingine ya miti ni kuondoa hewa ya ukaa na kupata hewa nzuri, huku akiwaagiza viongozi kuwachukulia hatua kali wafugaji ambao wamekuwa wakipitisha mifugo kwenye maeneo yaliyopandwa miti.

Katibu Tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoani Shinyanga Beda Chamatata, akizungumza kwenye kampeni ya upandaji miti katika shule ya Msingi Ndembezi.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akizungumza kwenye kampeni ya upandaji miti katika shule ya msingi Ndembezi.

Wakala Mtetezi wa Mradi wa Msichana na Mabadiliko ya Tabia nchi kutoka Tanzania Girl Guides Association, Joyce Maganga, akizungumzia namna wanavyoendesha kampeni ya upandaji miti.

Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Mohamed Makana, akizungumza kwenye Kampeni ya upandaji Miti Manispaa ya Ndembezi.

Kamishina wa Skauti Bi. Suzani Kidima akizungumza kwenye Kampeni ya upandaji miti katika shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ndembezi Rubeni Dotto akizungumza kwenye Kampeni ya upandaji miti katika shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.

Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga akizungumza kwenye kampeni ya upandaji miti katika shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.

Mwanafunzi Noelina Busisi akitoa elimu ya umuhimu wa upandajimiti kwa wananafunzi wenzake ili wawe Mabalozi wazuri wa kupinga uharibifu wa mazingira.

Wakala Mtetezi wa Mradi wa Msichana na Mabadiliko ya Tabia nchi kutoka Tanzania Girl Guides Association, Joyce Maganga, akizungumzia namna wanavyoendesha kampeni ya upandaji miti.

Katibu Tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoani Shinyanga Beda Chamatata, akizungumza kwenye kampeni ya upandaji miti katika shule ya Msingi Ndembezi.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akipanda mti katika shule ya Msingi Ndembezi.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakipanda mti.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Katibu Tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoani Shinyanga Beda Chamatata, akizungumza kwenye kampeni ya upandaji miti katika shule ya Msingi Ndembezi, akiwa na Wakala wa Msichana na Mabadiliko ya Tabia Nchi Joyce Maganga, wakipiga picha na wanafunzi.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Kampeni ya upandaji miti.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Kampeni ya upandaji miti.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Kampeni ya upandaji miti.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Kampeni ya upandaji miti.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakitoa burudani kwenye Kampeni ya upandaji miti.

Walimu wakiwa kwenye Kampeni ya upandaji miti.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Kampeni ya Upandaji Miti.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Kampeni ya Upandaji Miti.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Kampeni ya Upandaji Miti.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Kampeni ya Upandaji Miti.

Katibu Tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoani Shinyanga Beda Chamatata, (kushoto) akipiga picha ya pamoja na Wakala Mtetezi wa Mradi wa Msichana na Mabadiliko ya Tabia nchi kutoka Tanzania Girl Guides Association Joyce Maganga.

Katibu Tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoani Shinyanga Beda Chamatata, (kushoto) akipiga picha ya pamoja na Wakala Mtetezi wa Mradi wa Msichana na Mabadiliko ya Tabia nchi kutoka Tanzania Girl Guides Association, Joyce Maganga.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura (kushoto) akipiga picha ya pamoja na Wakala Mtetezi wa Mradi wa Msichana na Mabadiliko ya Tabia nchi kutoka Tanzania Girl Guides Association, Joyce Maganga.

Picha na pamoja zikiendelea kupigwa.

Picha na pamoja zikiendelea kupigwa.

Picha na pamoja zikiendelea kupigwa.
Share:

TBS YATOA UFAFANUZI KUHUSU USALAMA WA JUISI YA AZAM EMBE







Share:

WANANCHI TABORA WAISHUKURU SERIKALI UJENZI WA VYUO VYA VETA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Hassan Suluhu akipata maelezo kuhusu ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Hudum cha Mkoa wa Kagera kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Anthony Kasore wakati wa makabidhiano na uzinduzi huo wa Chuo uliofanyika Oktoba 13, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu akiweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Chuo cha VETA Mbarali Agasti 8, 2022.

Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Igunga kilichojengwa na Chuo cha VETA Shinyanga.

Jengo la Utawala katika Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Uyui kiluchojengwa na Chuo cha VETA Tabora.

***************************

*Wadai kuwa Wilaya zimeongeza hadhi kwa kuwa na mafundi wenye ujuzi

Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv

Wananchi na wadau mbalimbali mkoani Tabora wameishukuru Serikali kwa ujenzi wa vyuo vya VETA vya Wilaya ambao umetoa fursa za Wilaya hizo kupaa kimaendeleo.

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inaendelea kukamilisha ujenzi wa vyuo 25 vya Wilaya kwa kutumia nguvu kazi ya ndani yaani force account.

Miongoni mwa vyuo hivyo vinajengwa katika mkoa wa Tabora ambapo Chuo cha VETA cha Wilaya ya Uyui kinajengwa na Chuo cha VETA Tabora pamoja na Chuo cha VETA cha Wilaya ya Igunga kinachojengwa na Chuo cha VETA Shinyanga.

Masele Paulo ni mkazi wa Igunga ambaye amesema kuwa ujenzi wa Chuo cha VETA Igunga umempatia fursa ya kushiriki kwenye kazi ya ujenzi wa chuo hicho kama fundi uashi na kujipatia fedha za kununua viwanja viwili pamoja na kuweza kumsomesha mtoto wake na kuboresha zaidi ujuzi wake.

“Nashukuru sana kutuletea hii VETA…hii VETA imeleta manufaa makubwa kwa wale ambao waliweza kujituma kufanya kazi hapa,” amesema

Mjasiriamali Yunisi Joseph mkazi wa Igunga amesema uwepo wa mradi huo katika eneo lao, umemsaidia kujiongezea kipato na kukidhi mahitaji muhimu kwenye familia yake.

Amesema tangu kuanza kwa mradi huo Aprili 2020, amekuwa akifanya kazi ya kuwapikia wafanyakazi wanaojenga chuo hicho na kwamba kipato alichokipata kimemsaidia kununua kiwanja na kusomesha watoto wake.

“Chuo hiki cha VETA kimetupa faida kweli…mara ya kwanza kabla ya chuo kuanza kujengwa kazi yetu ilikuwa ni kusanya kuni kupeleka kuuza mjini,”amesema Kwa upande wake Emmanuel Rubona mkazi wa Wilaya ya Uyui amesema ushiriki wake kwenye mradi wa ujenzi wa chuo cha VETA cha Wilaya ya Uyui kama fundi ujenzi kumemwezesha kuboresha ujuzi wake, kumjengea ari na kumwezesha kujiamini zaidi katika kazi.

Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus Ngassa amesema ujenzi wa chuo cha VETA Igunga umenufaisha wafanyabiashara kutokana na bidhaa za ujenzi kununuliwa wilayani hapo huku jamii ikinufaika kwa mtu mmoja moja kwa kushiriki katika shughuli za ujenzi.

Mhe. Ngassa amewataka vijana kujiandaa vyema kutumia fursa za mafunzo chuoni hapo na hatimaye kuwawezesha kupata fursa za ajira kwenye miradi mbalimbali inayohitaji wataalamu wenye sifa mbalimbali ikiwemo cheti cha VETA.

Amesema kuwa Igunga ni miongoni mwa Wilaya zinazopitiwa na bomba la mafuta kutoka Hoima - Uganda hadi Tanga na kwamba kazi mbalimbali kwenye mradi huo zinahitaji watu wenye ujuzi kwenye fani mbalimbali.

Pamoja na shughuli za ujenzi, VETA pia imetengeneza samani kwa ajili ya vyuo hivyo vipya vya Wilaya kupitia vyuo vyake vyenye fani za Useremala.

Mwalimu wa Useremala katika Chuo cha VETA Tabora Mwesigwa Rwezahula amesema kazi ya kutengeneza samani imesaidia kujiimairisha kwa chuo chake pamoja na wanafunzi na wahitimu wake katika kazi ya utengenezaji wa samani.

Mwanafunzi wa Chuo cha VETA Tabora Agustino Haonga amesema ushiriki wake kwenye mradi wa utengenezaji wa samani umeimarisha uwezo wake wa kufanya kazi kwa vitendo na kumfungulia fursa na matumaini zaidi ya kujiajiri pindi atakapohitimu.

Akizungumzia ujenzi wa vyuo vya VETA, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA. Anthony Kasore amesema VETA inajivunia kukamilisha kwa asilimia 97 ujenzi wa vyuo 25 vya Wilaya kwa kutumia nguvu kazi ya ndani yaani Force Account ambapo mafunzo kwenye vyuo hivyo vipya yanatarajiwa kuanza mwaka 2023 huku vyuo hivyo vikitegemewa kudahili wanafunzi 18,000.

Ametaja vyuo hivyo 25 kuwa ni vya Wilaya za Pangani, Mkinga, Korogwe, Kilindi, Uyui, Igunga, Ikungi, Kishapu, Rufiji, Mafia, Ukerewe, Kwimba, Masasi, Ulanga, Mbarali, Chunya, Butiama, Uvinza, Iringa Vijijini, Buhigwe, Chemba, Bahi, Monduli, Longido na Lushoto.

"Nichukue fursa hii kumshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika elimu na mafunzo ya ufundi stadi nchini ambayo anaamini ina mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi kiuchumi na kuwezesha vijana kujiajiri "amesema CPA Kasore na kuongeza kuwa Rais Dkt.Samia Hassan Suluhu ameonesha nia yake ya dhati ya kuhakikisha watanzania wanajipatia fursa zaidi za mafunzo ya ufundi stadi ili kuwawezesha kujipatia ujuzi utakaowawezesha kushiriki kikamilifu kwenye shughuli mbalimbali za uchumi.

Kwa mujibu wa CPA. Kasore, Serikali imeshatenga kiasi cha shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vyuo vingine 63 vya wilaya na ujenzi wa chuo cha ufundi stadi na huduma cha Mkoa wa Songwe.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARI 3,2023

 

V





Share:

Thursday 2 February 2023

SERIKALI YAAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA BINAFSI


Na Georgina Misama – MAELEZO.

Serikali kupitia Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara imeahidi kushirikiana na Sekta Binafsi katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo; katika kikao cha majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es salaam.

Akiongea katika mkutano huo, Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji alisema Serikali imeamua kuboresha mazingira ya Sekta binafsi ili kukuza mchango wake katika pato la taifa na kwamba ni wakati sasa wa wadau wote wa Sekta binafsi kutoa ushirikiano kwa kuwa wawazi, waadilifu, wakweli, wawajibikaji na wazalendo hasa wanapoombwa taarifa na Serikali.

“Kutokana na majadiliano yetu ya hapa leo, sote tunakiri uwekezaji, viwanda na biashara ndio msingi wa maendeleo wa taifa lolote Duniani hivyo ni muhimu tukaendelea kuimarisha, kama waziri mwenye dhamana, nawaahidi kwamba nimepokea michango yenu yote na kwamba nitaenda kusimamia na kutekeleza yote yanayowezekana na nawakaribisha milango iko wazi muda wowote, tuendelee kushirikiana,” alisema Dkt. Kijaji.

Alisema Sekta ya Umma na Sekta Binafsi zinategemeana na kwamba serikali itaanza kwa kuangalia sera, sheria, kanuni na taratibu ili kuingia kwenye utekelezaji wa azimio kubwa lililoamuliwa na kikao hicho la mpango wa kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji na kuwahakikishia wajumbe namna bora ya kushughulikia mambo yote waliyoyawasilisha kupitia kamati za kitaalamu chini ya baraza la biashara (TNBC).

Akijibu baadhi ya hoja za wajumbe zilizowasilishwa katika majadiliano hayo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Lawrence Mafuru alisema kuna faida zaidi ya wafanyabiashara wadogo kujiweka kwenye mfumo rasmi ikiwemo kupata fursa za mikopo na kutambulika na Serikali ambapo ni rahiusi kuwekewa mazingira rafiki ya kazi zao kuliko kutojiweka wazi.

“Mnaweza mkafikiri ni faida kukwepa kodi kwa kutojiweka kwenye mifumo rasimi lakini kuna faida nyingi mnazojikosesha kwa kutojiweka wazi ikiwemo kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za kifedha kwa ajili ya mitaji, ufahamu juu ya fursa za masoko, mitandao ya mafunzo ndani na nje ya nchi pamoja na kudorora kwa maendeleo ya nchi kwa kukwepa kulipa kodi,” alisema Mafuru.
Share:

SERIKALI YAANZA KUANGALIA DHAMANA KESI ZA ULAWITI NA UBAKAJI


Na Mwandishi wetu, Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalum imeanza kuangalia uwezekano wa kuondoa dhamana kwenye makosa ya ulawiti na ubakaji ili kukomesha vitendo hivyo vilivyokithiri nchini.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Patrobas Katambi ameyasema hayo bungeni leo Februari mosi, 2023 alipokuwa akijibu maswali ya Mbunge wa Viti maalum, Mhe. Judith Kapinga kwa niaba ya Wizara ya Katiba na Sheria.

Katika swali lake, Mbunge huyo amehoji serikali ina mkakati gani wa kurekebisha sheria ya ubakaji na ulawiti wa watoto ili kuwe na kifungu tofauti cha sheria.

Akijibu swali hilo, Mhe.Katambi amesema kukithiri kwa vitendo hivyo hakutokani na mapungufu kwenye sheria na kwamba uthibitishaji wa makosa ya jinai unatakiwa kufanyika bila kuacha shaka yeyote lakini ushahidi huharibiwa wakati wa upelelezi.

Naibu Waziri Katambi amempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuliona hilo na kuunda Tume maalum ya haki jinai.
Share:

DAWA YA MVUTO WA KIMAPENZI ILIVYONIPATIA MKE TAJIRI

Jina langu ni Majaliwa kutokea Mombasa nchini Kenya, ni Baba wa familia, mimi na mke wangu katika miaka sita ya ndoa yetu tumejaliwa kupata watoto wawili, mmoja wa kiume na mwingine wa kike. Tunawapenda sana, hawa ndio furaha yetu.

Kabla ya kuwa na mwanamke huyo, huko nyuma niliangaika sana kutafuta mwanamke mwenye mapenzi ya kweli na mimi ili niweze kumuoa na kuanzisha naye mahusiano na hatimaye ndoa na familia lakini sikuweza kufanikiwa licha ya kutia juhudi kubwa.

Sio kwamba nilikuwa na maisha duni sana, hapana!, maisha yangu yalikuwa na uhakika wa makazi na malazi, sio mtu wa kushindwa kumuhudumia mwanamke hata kidogo, sema tatizo kubwa kwangu lilikuwa ni kumpata huyo mwanamke.

Siku moja nilienda kumtembelea rafiki yangu ambaye mke wake alikuwa amejaliwa mtoto, katika mazungumzo yetu, ndipo akaniuliza ni lini nitaoa, ndipo nikamwambia mimi mwenyewe natamani kuoa hata leo lakini sijapata tu mwanamke wa kuoa.

Akaniambia kuna jambo moja napaswa kulifanya mara moja, nalo ni kuwasiliana na AfricanDoctors ambao wamekuwa wakitoa dawa ya mvuto wa kimapenzi na watu wengi ukanda wa Afrika Mashariki wamefanikiwa kupitia wao.

Ndipo akanipatia namba zao ambazo ni +254719153099, akaniambia nijaribu kuwasiliana nao wanaweza kunisaidia nami nikapata mwenza wangu maisha, nikawa kama wanaume wengine.

Basi baada ya kurejea nyumbani kwangu, nilichukua hatua muhimu sana, nayo ni kupiga namba ile, nashukuru ilipokelewa nami nikaeleza shida yangu; kuwa nataka kuwa na mvuto wa kimapenzi ili niweze kupata mke wa kuoa.

Ndani ya muda mfupi walinifanyia tiba na kuniambia haitachukua muda mrefu nitaanza kuona matokeo, basi nilikuwa nashauku kubwa kuona jambo hilo likitokea katika maisha yangu.

Siku chache nikiwa katika mizunguko yangu, niliweza kukutana na dada mmoja mrembo na kuniomba nimuelekeze eneo fulani, basi nikamuelekeza vizuri tu, akaniambia kama sitojali nimpe namba yangu ya simu ili ataposhindwa kutambua njia niliyomuelekeza anipigie.

Basi nilimpa namba ile, kesho yake alinipigia na kunishukuru kwa msaada wangu, kuanzia hapo tuliendelea kuwasiliana hadi mwisho wa siku tukaanzisha mahusiano.

Lakini kipindi ambacho penzi limekolea na tupo katika mchakato wa kuoana, nikaja kugundua kuwa yule mwanamke ni mtu ambaye anajiweza sana kiuchumi, ni mtu tajiri.

Basi mwisho wa siku tukaoana, na sasa tunaishi vizuri na maisha yetu yanaendelea vizuri na sasa tunaishi vizuri na familia yetu.

Wasiliana na AfricanDoctors kwa namba ya simu +254719153099.

Mwisho.
Share:

TBS YATOA ELIMU KWA WATOA HUDUMA YA CHAKULA KATIKA MIKUSANYIKO JIJINI DAR ES SALAAM

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Ashura Kilewela akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Uhamasishaji kwa Wauzaji wa chakula kwenye Mikusanyiko, Wasafirishaji wa chakula na wasagaji wadogo wa nafaka katika Mkoa wa Dar es Salaam ambayo yamefanyika leo Februari 2,2023.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Ashura Kilewela akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Uhamasishaji kwa Wauzaji wa chakula kwenye Mikusanyiko, Wasafirishaji wa chakula na wasagaji wadogo wa nafaka katika Mkoa wa Dar es Salaam ambayo yamefanyika leo Februari 2,2023.

***************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SAlAAM

Idadi ya watoa huduma ya Chakula katika mikusanyiko ambao wamekaguliwa maeneo yao na kupata vibali na Shirika la Viwango (TBS) si ya kuridhisha ikilinganishwa na idadi ya watoa huduma katika Jiji la Dar es Salaam.

Ameyasema hayo leo Februari 2,2023 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Ashura Kilewela wakati akifungua Mafunzo ya Uhamasishaji kwa Wauzaji wa chakula kwenye Mikusanyiko, Wasafirishaji wa chakula na wasagaji wadogo wa nafaka katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Amewataka wadau hao kuhakikisha wanasajili maeneo yao kwa mujibu wa sheria na pia kuwa mabalozi wema kwa wenzao wanaofanya shughuli hiyo kwenye maeneo mbalimbali.

Aidha Dkt.Kilewela amesema mafunzo hayo yamelenga kuwahamasisha wadau wao kwa Mkoa wa Dar es Salaam kuhusu kanuni, sheria na miongozo ya shirika katika kuhakikisha jamii inapata chakula bora na salama.

Share:

MREMBO ANG'ATA NYETI ZA BABA MKWE WAKE


Polisi katika kaunti ya Bungoma  nchini Kenya wanachunguza kisa ambapo mwanamke anadaiwa kumng'ata baba mkwe wake sehemu za siri wakati wa ugomvi.

Katika kisa hicho cha kustaajabisha ambacho kimeshtua familia na majirani, Vincent Simiyu mwenye umri wa miaka 78, kutoka kijiji cha Kimaeti eneobunge la Bumula, anauguza majeraha kufuatia kuumwa uume wake na mkaza mwana wake.

Kulingana na mashahidi, mshukiwa Everline Okelo, anadaiwa kukasirishwa na baba mkwe wake baada ya kupata fununu kwamba alikuwa anafahamu mwanawe alioa mke wa pili. Simiyu alisimulia kuwa Okelo alimpiga kwa jiwe na kuanguka chini na baadaye kumkalia kifuani huku akimshika uume wake alioweka mdomoni na kuuma.

"Alichukuwa mawe, akanipiga kwa mgongo nikaanguka chini nikakosa fahamu, bibi ya mtoto yangu akaniangukia anakikalia kwa kifua, akaniuma, nikamskuma, akanishika kwa long'i, akakunja sehemu nyeti akaweka kwa mdomo yake, akaniuma, nikalia ndio mtoto wangu akakuja kuniokoa," alisimulia babu. Zogo hilo lilivutia majirani ambao walimpa kichapo mwanamke huyo na mumewe na kumkimbiza mzee huyo hospitalini.

Kisha baadaye mwanamke huyo aliingia mafichoni na sasa nado anasakwa. Wazee wa Bukusu walisema mwanamke huyo ni lazima aadhibiwe kitamaduni kwa kuwa mila za jamii hiyo zinamzuia kukaribiana kimwili na wakwe zake. Kanuni, maadili na imani za ajabu ya ndoa ya Bukusu Jila jamii kote duniani ina maadili na imani zake, na hii inatimiza heshima katika kiwango fulani. Iwapo unatarajia kuolewa na jamaa kutoka katika jamii ya Bukusu, ni vyema kujifunza kuhusu kanuni kadhaa zinazoweza kusaidia maisha yako ya ndoa.

Bukusu ni kabila dogo la jamii ya Waluhya, ambalo ni mojawapo ya makabila makubwa zaidi katika Afrika Mashariki na Kati. Jamii hiyo inapatikana zaidi katika kaunti za Bungoma na Trans Nzoia. Jumuiya inajivunia desturi za kipekee za kitamaduni za kiasili ambazo zitakuacha uvutiwe. Moja ya tamaduni hizo ni kwamba baada ya kuingia katika nyumba wakwe, usifunge milango yoyote. Kimsingi mtu haruhusiwi kuwa katika nyumba moja na mama mkwe au baba mkwe wake na milango imefungwa hivyo milango yote yanatakiwa kuwa wazi wakati wanapokutembelea au unapowatembelea.
Share:

Wednesday 1 February 2023

WAKE WANNE WAMENIACHA NA KWENDA KUOLEWA TENA


Ukweli ni kwamba huku duniani kuna mikosi ya kila namna, mikosi ni mfululizo wa visa vibaya ambavyo vinaweza kuwa vinajirudia kila wakati na bila kujua sababu ni nini hasa.


Mathalani kuna mtu kila bishara anayofungua haiwezi kufikisha mwaka mmoja, mwingine kila gari analonunua lazima liibiwe, mwingine kila mtoto anayempeleka shule anafeli.

Au kuna familia unakuta mabinti wanazalia nyumbani tu bila kuolewa, ukichunguza unakuja kugundua hata mama yao naye alizalia nyumbani na hapo watoto wanapoishi ni kwa Babu na Bibi yao.

Hiyo ndio mikosi yenyewe, kipindi ambacho jamii zetu zinaheshimu mila na tamaduni kabla ya kuathiriwa na utamaduni za magharibi zilizoletwa na utandawazi, jambo kama hilo likitokea lazima wazee wakae na wafanye jambo.

Ila sasa hiyo imekuwa ni ngumu, watu wanapata mikosi kila siku, wanaumia, wanarudi nyuma kimaendeleo na kiuchumi, hakuna anaweza kujua kipi kifanyike kwa sasa.

Hata hivyo, kuna hawa AfricanDoctors, ni kiboko kabisa ya mikosi katika maisha, hawa ndio walioniondoa katika mkosi wa ndoa zangu kuvunjika.

Miaka ya nyuma kila mwanamke ambaye nilikuwa namuoa, baada ya miaka miwili, basi angechukua vitu vyake na kuondoka bila kusema sababu yoyote ile na mara moja angeolewa na mwanaume mwingine.

Wanawawake wanne ambao niliwaoa waliondoka na kwenda kuolewa na watu wengine, na kibaya zaidi walikuwa wanaondoka bila hata kunizalia mtoto.

Ndipo nilipopata tiba kutoka kwa AfricanDoctors na sasa mambo ni shwari kabisa, nimeoa na huu ni mwaka wa sita nipo kwenye ndoa na tumejaliwa kupata watoto wawili na mmoja tayari ameanza shule ya msingi.

Wasiliana na AfricanDoctors kwa namba +254719153099.

Mwisho.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger