Monday 5 December 2022

WAZIRI DKT. GWAJIMA APANDA BASI LA WANAFUNZI MANISPAA YA SHINYANGA...AONYA USHOGA, ATAKA MFUMO KULINDA WATOTO


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akishuka ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa hatua mbalimbali inazofanya katika kutekeleza usimamizi wa kuzuia na kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kwa kununua magari mawili yanayobeba wanafunzi kuwapeleka shuleni na kuwarudisha karibu na makazi yao.


Waziri Dkt. Gwajima ametoa pongezi hizo leo Jumatatu Desemba 5,2022 wakati akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Town baada ya kupanda gari moja na wanafunzi hao kutoka majumbani mwao kuelekea katika shule hiyo iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia


“Nawapongeza sana Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ubunifu huu wa usafiri kwa gharama nafuu shilingi 200 kutoka nyumbani hadi shuleni, nina imani wanafunzi sasa watatumia muda mfupi kwenda shuleni na kuwaepusha na vishawishi mbalimbali wawapo njiani, lakini nimeshuhudia gari hili likiwa na Msimamizi wa wanafunzi ambaye ni Afisa Maendeleo ya jamii, hii ni hatua nzuri sana, ni vyema Halmashauri zingine zikaiga mfano wa Manispaa ya Shinyanga namna ya kusaidia wanafunzi, zisisubiri matamko”,amesema Dkt. Gwajima.

Katika hatua nyingine Dkt Gwajima amezitaka halmashauri na Mikoa yote nchini kuandaa mifumo ya upatikanaji wa haraka wa taarifa za kulinda watoto utaosaidia kufahamu taarifa za watoto.

"Mtengeneze na mifumo itakayogundua iwapo mtoto hayupo shuleni, iunganishwe kuanzia wazazi, walimu, polisi na jamii nzima. Endapo tutakuwa na mfumo wa kulinda watoto itatusaidia pia kudhibiti utoro shuleni, tutaweza kutambua kama mtoto yupo shule au la! Wazazi pia watasaidia kujua mtoto yuko wapi. Mfumo wa pamoja wa taarifa utasaidia kupata sulushisho la matukio ya ukatili katika jamii", amesema.

Katika hatua nyingine amewataka wadau kuendelea kupaza sauti juu ya vitendo vya jinsia moja huku akibainisha kuwa hatakubali kuona vitendo vya ushoga na vitendo vingine vya ukatili wa kijinsia kwenye vyombo vya usafiri vinavyobeba wanafunzi lakini pia shuleni.

"Suala la mapenzi ya jinsia moja halitafumbiwa macho kwa namna yoyote ile, watoto watalindwa kwa hali zote. Nawatangazia waovu wote wanaofundisha madarasa ya ushoga waache mara moja, hata huyo mwanaume aliyekamatwa huko Geita akifundisha watoto ushoga akiwa amevaa nguo za kike ‘sidiria’ na vitu vya kike kike ni lazima achunguzwe, tutalifuatilia hili jambo haiwezekani watoto wetu waharibiwe kwa kufundishwa mambo yasiyofaa, Hili la ushoga nitalifia. Tutawalinda watoto, na hayo madarasa ya ushoga yafe huko huko",amesema Dkt. Gwajima.

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo amesema ameahidi mkoa huo kuendelea kupambana na vitendo vya ukatili na kufuata maelekezo yote yaliyotolewa na kwamba wamejipanga kukutana na wadau mbalimbali ili kutengeneza mfumo wa kutoa taarifa kwa ajili ya kuwalinda watoto.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manipaa ya Shinyanga, John Tesha ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, amesema halmashauri hiyo inaendelea kutoa elimu ya kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto mara kwa mara katika ngazi ya jamii, kwenye nyumba za ibada na Shule za msingi , Sekondari na vyuo.

“Pia halmashauri imetumia nafasi ya utoaji mikopo kwa asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kama njia nyingine za kuzuia na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto”,amesema Tesha.

“Mfano mwingine wa namna mikopo ya asilimia 10 ilivyosaidia kwenye kuzuia na kutokomeza ukatili kwa watoto ni ule ambao mwezi Aprili 2022, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ilitoa mikopo yenye thamani ya shilingi Milioni 120 kwa vikundi viwili vya vijana. Vikundi hivyo tulivisimamia na kununua magari mawili (Moja ni Basi aina ya Tata na lingine ni Basi dogo aina ya Nissan – Civilian) yanayofanya kazi ya kubeba wanafunzi”,ameongeza Tesha.

Ameeleza kuwa Vikundi hivyo vya vijana vilipewa maelekezo na kusainiana mkataba na Halmashauri kuhakikisha nyakati za asubuhi kuanzia saa 12 hadi saa 2 asubuhi magari hayo yanabeba wanafunzi kuwapeleka shuleni na nyakati za jioni kuanzia saa 10 na nusu hadi saa 12 jioni magari hayo yanabeba wanafunzi kuwarudisha karibu na makazi yao kwa bei elekezi ya shilingi 200/= / 300/=.

“Lengo la kufanya hivi ni kuwahakikishia wanafunzi usalama wao wanapoenda shuleni na wakati wa kurudi nyumbani na kuhakikisha wanafunzi wanafika shuleni kwa wakati na siku zote za masomo hivyo kuwahakikishia ufaulu mzuri katika mitihani yao”,amesema Tesha.

Amesema upatikanaji na utumiaji wa magari hayo ya mkopo kwa vijana yamewapunguzia wazazi gharama za kuwasafirisha watoto kwenda na kurudi shuleni ambapo gharama za kumsafirisha mtoto kwenda na kurudi shuleni kwa siku ni kati ya shilingi 500/= - 600/= na kwa mwezi ni kati ya shilingi 10,000/= - 12,000/=

“Hii ni gharama nafuu ukilinganisha na gharama walizokuwa wanatumia wengi wao za kutumia baiskeli ambapo huwa ni shilingi 500/= hadi 1000/= kwa safari moja ambapo kwa siku ni shilingi 1000/= -hadi 2000/= na kwa mwezi ni shilingi 20,000/= hadi 40,000/=”,ameeleza.

“Kwa kutumia mikopo ya asilimia 10 pia Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imetoa Bajaji kwa watu wenye ulemavu kwa ajili ya biashara ya usafirishaji wa abiria ambapo pia waliokopa tumewaelekeza kubeba wanafunzi popote wanapowakuta kwa bei elekezi. Pia katika mwaka huu wa fedha 2022-2023 unaoendelea tumejipanga kutoa mikopo ambayo itawezesha kununua magari/ Hiace Sita ambazo zitawajibika kufanya biashara ya abiria ndani ya Manispaa na kuhakikisha zibabeba wanafunzi kwa bei elekezi”,amefafanua Tesha.

Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa Nancy Kasembo ameshukuru uongozi wa mkoa na Manispaa ya Shinyanga kwa ubunifu huo ambao utasaidia kupunguza utoro na mimba za utotoni kutokana na ukatili.

Akiwa mkoani Shinyanga Waziri Gwajima amezungumza pia na wananchi kupitia kituo cha Redio Faraja Fm, kufanya mazungumzo na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Mhashamu Liberatus Sangu pamoja na kutembelea Kamati ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto kata ya Ibinzamata sambamba na kutoa vyeti vya pongezi kutambua mchango wa baadhi ya taasisi na watu binafsi katika kushiriki mapambano dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto.


 Baadhi ya waliokabidhiwa vyeti hivyo ni Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale, Mwandishi wa Habari wa Azam Tv Kasisi Kosta ,  Chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club -SPC), ICS na kituo cha Redio Faraja Fm.

 ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akisalimiana na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Town Manispaa ya Shinyanga kabla ya kupanda kujionea namna Basi la Wanafunzi linavyosafirisha wanafunzi Mjini Shinyanga leo Jumatatu Desemba 5,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akisalimiana na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Town Manispaa ya Shinyanga kabla ya kupanda kujionea namna Basi la Wanafunzi linavyosafirisha wanafunzi Mjini Shinyanga. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manipaa ya Shinyanga, John Tesha ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manipaa ya Shinyanga, John Tesha  (kulia) ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga. Kushoto ni Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Shinyanga Elizabeth Mweyo anayesimamia wanafunzi katika Basi la wanafunzi.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akiwa ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari  Town ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akishuhudia wanafunzi wa shule ya Sekondari wakishuka ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akiwa ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akisalimianan na Dereva wa Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akishuka ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akisalimiana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manipaa ya Shinyanga, John Tesha ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manipaa ya Shinyanga, John Tesha ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga akizungumza katika shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manipaa ya Shinyanga, John Tesha ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga akizungumza katika shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akizungumza katika shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akizungumza katika shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza katika shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Tanzania, Nancy Kasembo akizungumza katika shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga wakisikiliza nasaha mbalimbali.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga wakisikiliza nasaha mbalimbali.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga wakisikiliza nasaha mbalimbali.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

RAIS SAMIA AELEKEZA FEDHA ZA SHEREHE ZA UHURU KUJENGA MABWENI

 


Na Dotto Kwilasa,Malunde 1Blog-DODOMA.

ZIKIWA zimesalia siku chache Tanzania kuadhimisha miaka 61 ya uhuru wake,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza  fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe za Uhuru mwaka huu zitumike kujenga mabweni katika shule nane za Msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum hapa nchini.  

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na Uratibu George Simbachawene amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa kuhusu Maadhimisho ya Sherehe za miaka 61 ya uhuru wa Tanzania Bara.

Amesema Rais Samia  ameamua fedha zote kiasi cha Shilingi Milioni 960 zilizokuwa zimetengwa na Wizara na Taasisi kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe za Uhuru mwaka huu 2022,zipelekwe Ofisi ya Rais – TAMISEMI ili zitumike kuwahudumia wenye mahitaji.

Simbachawene ameeleza kuwa Tanzania Bara ilipata Uhuru wake tarehe 09 
Desemba, 1961 na tarehe 09 Desemba, 1962 ikawa rasmi Jamhuri hivyo kila mwaka Tanzania Bara husheherekea Maadhimisho ya uhuru ambapo kwa mwaka huu yataazimishwa kwa kaulimbiu isemayo"Miaka 61 ya Uhuru:"amani na umoja ni nguzo ya maendeleo yetu".

"Kauli mbiu hii inaonyesha nia ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha uchumi unaojikita katika maendeleo ya watu kwa kufanya mabadiliko katika sekta zote za kiuchumi na kijamii ili kufikisha neema na Maendeleo kwa Wananchi wote wa Tanzania,"amesema Simbachawene.
 
 Simbachawene pia  "ameeleza namna yatakavyofanyika Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara mwaka 2022 kuwa ni kwa Midahalo na Makongamano mbalimbali yatakayofanyika katika Wilaya zote hapa nchini kujadili, kutafakari kwa pamoja na kukumbuka tulikotoka, tulipo na tunakoelekea kuhusu Maendeleo Endelevu ambayo Nchi yetu adhimu Tanzania imeyafikia"amesema.  

"Kwa muktadha huu, Mheshimiwa Waziri Mkuu ameniagiza nishirikiane na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI kufanya usimamizi, ufuatiliaji na tathmini ya Midahalo na Makongamano hayo ili kujiridhisha na matokeo yake hivyo katika kutekeleza maelekezo haya ofisi hizi zimetoa Maelekezo mahsusi na ratiba kwa ajili ya kurahisisha uendeshaji mzuri wa shughuli kwa Mikoa na Wilaya zote nchini,"amesema.
 
Amesema kuwa Katika kukuza uzalendo na kusherehekea Maadhimisho hayo pamoja na maadhimisho mengine ya Kitaifa kama vile sherehe za Muungano, Ofisi zote za Serikali hapa nchini zipambwe kwa mapambo ya rangi za Bendera ya Taifa pamoja na picha ya Rais. 
 

Share:

ANAYECHEZEA MTIHANI AFUNGWE JELA-PROF.MKENDA






Na Mathias Canal, WEST-Dar es salaam

Serikali imeweka bayana dhamira yake ya kuchukua hatua kali za uwajibikaji kwa Maafisa Elimu wa Mikoa, Wilaya, Walimu na maafisa wengine wote wakiwemo askari ambao wamepewa jukumu la kusimamia mitihani na kufanya udanganyifu.

Hatua hizo dhidi ya wasimamizi hao wa mitihani zitahusisha kusimamishwa kazi, kufukuzwa pamoja na kufikishwa mahakamani ili wafungwe jela.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 5 Disemba 2022 wakati akizungumza na uongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mlongazila katika Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja.

Amesema kuwa ili kuimarisha sekta ya elimu lazima kushughulika na watu wanaofanya udanganyifu ikiwemo kuwachukulia hatua kali na kuwajibika huko sio tu kufukuzwa kazi kama ilivyozoeleka au kupewa onyo pekee bali wafungwe jela ili iwe fundisho kwa wengine.

Waziri Mkenda amesema kuwa Baraza la Mitihani Tanzania (NACTE) limeongeza mikakati ya kupambana na watu ambao wanafanya udanganyifu kwenye vituo vya mitihani ambapo serikali imewakamata na kuwachukulia hatua wasimamizi wote kwa kushirikiana kufanya ubadhilifu wa mitihani.

Amesema kuwa serikali imechunguza na kubaini kuwa watumishi wa serikali na watumishi wa sekta binafsi wamehusika kwenye udanganyifu wa elimu na kuwachukulia hatua.

"Sasa nisisitize kuna kauli inasema ukitaka kuuwa Taifa basi uwa elimu, sasa tunafanya mageuzi ya elimu nchini kwenye sera na mitaala lakini haiondoi jukumu la kusimamia elimu tunayoitoa sasa hivi inatolewa kwa taratibu zinazokubalika" Amesisitiza Waziri Mkenda

Waziri Mkenda amesema kuwa udanganyifu katika mitihani una madhara ya kumuwezesha mtu kufaulu ambaye hakustahili kufaulu kwani akiwa daktari ataleta athari kubwa katika jamii.

"Hasara mojawapo kubwa kwa Taifa letu ya kuvujisha mitihani ni kuwafundisha watoto katika umri mdogo kwamba ili uendelee ni lazima ufanye udanganyifu, tunaanza kujenga rushwa mapema mno na serikali haitakubali kitu kama hicho" Amekaririwa Waziri Mkenda

"Wale waliohusika hasa watumishi wa serikali, Maafisa elimu na watu wote waliohusika mahali pao kwa kweli ni jela, tunaongea na mamlaka husika kwamba tusije tukawafukuza tu kazi, wanachokifanya ni jinai, ukiangalia gharama za kuendesha mitihani ni kubwa sana kwahiyo mtu anayevuruga mitihani ashitakiwe mahakamani wahukumiwe na waende jela" Amesisitiza Waziri Mkenda

Waziri Mkenda ameeleza kuwa serikali itapitia sheria ili kama kuna mwanya wa kuwawezesha watu kufanya udanganyifu na wakatoka bila kuchukuliwa hatua yoyote kuwe na namna ya kufanya mabadiliko.

Amesema anayechezea mtihani afungwe jela na ametoa onyo kwa wote wanaofanya hivyo kuacha mara moja udanganyifu huo.


Share:

MASHINDANO YA BULYANHULU HEALTHY LIFESTYLE MARATHON YAVUTIA WENGI


Meneja Mkuu wa Mgodi wa wa Bulyanhulu, Cheick Sangare akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa wa Bulyanhulu, Cheick Sangare akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya, akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa wa Bulyanhulu, Cheick Sangare, akikabidhi zawadi ya baiskeli kwa mshindi wa mbio ndefu Elias Charles.
Mtaalamu wa Afya wa Mgodi wa Bulyanhulu,Dk. Nolask Kigodi akiongea katika hafla hiyo (kulia) ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa wa Bulyanhulu, Cheick Sangare.
Baadhi ya washiriki baada ya kumaliza mbio hizo
Baadhi ya washiriki baada ya kumaliza mbio hizo
Baadhi ya washiriki wa mbio hizo wakikimbia kuwania ushindi
Baadhi ya washiriki wa mbio hizo wakikimbia kuwania ushindi
Baadhi ya washiriki wa mbio hizo wakikimbia kuwania ushindi
**

Mashindano ya mbio ya kilomita 42 ya Bulyanhulu Healthy Lifestyle Marathon yaliyoandaliwa na Mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu yamefanyika jana ambapo Elias Charles, ameibuka mshindi wa jumla wa mbio ndefu na kujishindia zawadi ya baiskeli ya kisasa ya kupanda milima aina ya La Ruta 29+.

Mashindano hayo ya mbio zenye urefu wa aina mbalimbali yamewashirikisha washiriki zaidi ya 250 ambao ni wafanyakazi wa Mgodi, wakandarasi wa Mgodi na wananchi wanaoishi kwenye vitongoji vinavyozunguka Mgodi.

Zawadi nyingine ambazo wamejinyakulia washindi katika mbio za Kilometa 21, 15, 10 na 5, ni pamoja na jokofu, simu janja, saa ya kisasa, mikeka ya mazoezi ya yoga na mashine za kutengeneza salasi na kukamua juisi.

Mgeni rasmi katika hafla alikuwa ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya, ambaye pamoja na kuwapongeza washiriki hao alisema kuwa ofisi yake itashirikiana na Mgodi katika kuhakikisha watumishi na wakandarasi wake wanapata miongozo ya lishe ya taifa ambayo kwa sasa imeanza kutumika katika ngazi zote kuanzia Serikali kuu hadi kwenye kata na vijiji. "Unene na kasi ya magonjwa yatokanayo na mifumo ya maisha yanaongezaka hivyo Serikali imeamua kulivalia njuga changamoto hii".

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Mgodi wa wa Bulyanhulu, Cheick Sangare, alisema kuwa kampuni imejipanga kuhakikisha kuwa suala la afya za wafanyakazi inalipa kipaumbele kwa kuwa inaamini kuwa kuwa na nguvu kazi yenye afya bora kunaleta tija zaidi.


Naye mtaalamu wa afya kutoka Mgodi huo, Dk. Nolask Kigodi, alisema mgodi ulikuwa na lengo la kupunguza uzito wa jumla wa kilo 1,500 kwa wafanyakazi wapatao 2,500 ikiwemo wakandarasi mbalimbali waliopo mgodini hapo. “Tumejipanga kuhakikisha suala la mazoezi linapewa kipaumbele sambamba na kuwa na sehemu za kufanyia mazoezi zenye vifaa mbalimbali na kuzingatia lishe bora.


Share:

BENKI YA CRDB, VISA WATAMBA KOMBE LA DUNIA


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akiwa uwanjani kushuhudia mechi ya Kombe la Dunia kati ya Argentina na Poland ikiwa ni sehemu ya mwaliko kutoka Visa International, washirika rasmi wa malipo wa FIFA. Benki ya CRDB imekuwa na mahusiano ya muda mrefu na Visa kupitia mifumo yake ya malipo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulamajid Nsekela (katikati) akiwa na Afisa Mkuu Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile (kushoto), na Mkurugenzi wa Mawasiliano Benki ya CRDB, Tully Mwambapa wakati wa mkutano maalum uliondaliwa na kampuni ya Visa International nchini Qatar kujadili ushirikiano katika mifumo mipya ya malipo.
Mwakilishi wa Visa nchini Qatar akielezea juu ya mwenendo wa huduma za malipo na biashara kote duniani katika kipindi cha mwaka 2022




Kampuni ya Visa ambayo ndio mwezeshaji mkuu wa malipo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa), imeikaribisha Benki ya CRDB kushuhudia maboresho ya huduma zake kwenye michuano ya kombe la dunia yanayoendelea nchini Qatar.


Ili kurahisisha malipo kwa mashabiki na washiriki waliohudhuria michuano hiyo, Visa imefanya maboresho kadhaa kuondoa usumbufu kwa wateja wake.


Maboresho yaliyofanyika yanamruhusu mteja anaweza kuidhinisha malipo kwa kutumia sura yake bila kulazimika kutumia kadi au simu baada ya kukamilisha usajili, kutumia kadi za kidijitali pamoja na kulipia teksi kidijitali.


Katika kusherehekea mafanikio hayo, Visa imezialika benki kubwa inazoshirikiana nazo kutoka kila pembe ya dunia huku Tanzania ikiwakilishwa na Benki ya CRDB.


Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema mashabiki wa mpira nchini ambao wameenda kujionea michukuano hiyo wanaweza kulipia huduma na bidhaa wanazozitaka iwe hotelini, dukani au katika chombo cha usafiri.


“Michuano hii ya kombe la dunia ni fursa kwa Benki ya CRDB na Visa kuonyesha na kudhihirisha ubora wa huduma zetu za malipo.


Kadi zetu za TemboCard Visa zinatumiwa na Watanzania wengi wlaiokuja kushuhudia michuano inayoendelea hapa Qatar,” amesema Nsekela.


Ushirikiano wa Benki ya CRDB na Visa umekuwa na mchango mkubwa katika kuwawezesha Watanzania kupata huduma bora za benki hata kushiriki kwenye uchumi wa kidijitali.


Tangu mwaka 2014 ulipoanza kwa kuitambulisha Tembocard Visa, ushirikiano huo umewawezesha Watanzania kupata huduma za fedha ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.


"Benki ya CRDB inajisikia fahari kuwa mbia wa Visa kuwawezesha mashabiki wa mpira wa miguu kufurahia mchezo huku wakilipa kwa namna rafiki kwa kutumia kadi zetu za TemboCard Classic, Gold, Platinum, na Infinite zenye huduma zinazokidhi mahitaji ya mteja,” amesema Abdulmajid Nsekela.


Wakati wote, Nsekela amesema benki imekuwa ikitumia juhudi kubwa, kwa kushirikiana na Visa, kuboresha na kuongeza ujumuishaji wa wananchi kwenye huduma za fedha.


Kutokana na uwezo wake, Nsekela amesema TemboCard Visa zinaweza kutumiwa kwenye mashine za kutolea fedha (ATM), vituo vya mauzo hata majukwaa ya mtandaoni yanayomruhusu mteja kufanikisha muamala akiwa mahali popote duniani.


"Mpaka sasa tuna zaidi ya wateja milioni 4 wanaotumia huduma kupitia kadi zetu, wengi wanamiliki TemboCard Visa. Malengo yetu ni kuhakikisha mteja anaweza kupata huduma aitakayo kutoka popote alipo na wakati wowote anaoihitaji.


Mwanzon wateja hawakuwa tayari kufungua akaunti kutokana na ulazima wa kwenda kwenye tawi la benki watakapohitaji kuzitumia fedha zao lakini ushirikiano wetu na Visa umeondoa ulazima huo,” amesema Nsekela akisistiza kuwapo kwa CRDB Wakala nako kumeongeza maeneo ambako wateja wa benki wanaweza kupata huduma.


Kwa sasa kuna zaidi ya CRDB Wakala 25,000 wanaosaidia kufikisha huduma hata maeneo yasiyona tawi huku mifumo ya kidijitali ya benki ikiongeza fursa za kulipia bili za Serikali kwani imezijumuisha zaidi ya taasisi 4,000 za umma.


Huduma za kidijitali ni kati ya vipaumbele vya Visa hata Benki ya CRDB kwani teknolojia hiyo siyo tu imerahisisha miamala ya wateja bali ukusanyaji mapato kwa mamlaka za serikali.


Katika kampeni iliyoizindua mapema mwaka huu kuhamasisha uchumi wa kidijiti, wateja wanne wa Benki ya CRDB wanaotumia TemboCard Visa walilipiwa nauli ya ndege na tiketi za kuingia uwanjani kushuhudia mechi za kombe la dunia, visa ya kuingia Qatar pamoja na malazi ili kuwapa nafasi ya kufurahia michuano hiyo inayoendelea kutokana na matumizi ya kadi zao.


Ujumbe wa Benki ya CRDB ulioenda Qatar ulipata fursa ya kutembelea vituo vya ubunifu kama sehemu ya mwaliko wa kuhudhuria michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022.


Vilevile, ulishuhudia mtanange wa makundi uliozihusisha Argentina na Poland, pamoja na ule wa Japan na Hispania.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU DESEMBA 5,2022






Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger