Tuesday 6 December 2022

SERIKALI KUENDELEA KUTOA ELIMU YA LISHE BORA KWA JAMII

Na Frankius Cleophace Mara

SERIKALI imesisitiza utoaji wa elimu kwa jamii namna ya kuzingatia lishe bora ili kuweza kuepukana na udumavu kwa watoto na kuwa na afya bora.


Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, katika hotuba yake iliyosomwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalumu, Doroth Gwajima,kwenye ufunguzi wa mkutano wa 8 wa wadau wa lishe.

Amesema katika kutekeleza mpango jumuishi wa lishe Tanzania suala la elimu lina umuhimu wa pekee kwa kila mmoja ili kufikia malengo.


Amedai mpango huo wa miaka 5 utekelezaji wake wa hali ya lishe hauwezi kuwa na mafanikio kama hakutakuwa na elimu jumuishi ikiwa ni pamoja na kwa jamii husika.

Amesema kasi ya mapambano dhidi ya utapiamlo inaendelea kufanyika huku mbinu za kuboresha hali ya lishe hapa nchini zikifanyika.

" Yapo mambo 8 ambayo yakizingatiwa na kila mmoja ikiwemo wadau wa lishe kuhakikisha miradi inakuwa shirikishi marengo yetu yatakwenda kufanikiwa",amesema.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo, Antony Mavunde, amesema wizara imeelekeza fedha nyingi kwenye masuala ya lishe na kuimalisha kilimo cha umwagiliaji kwa ajili ya chakula.


Amesema licha ya fedha hizo kwaajili ya masuala ya lishe kuasi cha shilingi bilioni 15 zimetengwa kwaajili ya kuwawezesha maafisa ugani ili waweze kuwahudumia wakulima.

Mwenyekiti wa wabunge vinara wa lishe na mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara, Ester Matiko, amesema wabunge wataendelea kuishauli serikali juu ya masuala mazima.


Share:

MWAMALA WALIA CHANGAMOTO YA MAJI.... "TUNATUMIA MUDA MREFU KUFUATA MAJI, TENA YANA CHUMVI MATUMBO YANAUMA"


Mtoto akichota maji katika moja ya visima kitongoji cha Wela kijiji cha Mwamala B kata ya Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa kitongoji cha Wela kijiji cha Mwamala B kata ya Mwamala, Bw. Giti Singu Giti akionesha kisima cha maji kinachotumiwa na wananchi.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wakati dunia ikiadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia bado wananchi wa kata ya Mwamala katika mkoa wa Shinyanga wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa maji hali inayosababisha kutumia muda mrefu kufuata huduma hiyo ya maji ambayo pia yana chumvi.

Wakizungumza na Malunde 1 blog iliyotembelea kata hiyo, wananchi hao wamesema ukosefu wa maji safi na salama unawalazimu kutumia maji ya chumvi wenye visima walivyochimba pembezoni mwa mito ambayo si salama na wamekuwa wakitumia zaidi ya dakika 30 kufuata maji hayo kwa baiskeli na kujitwisha kichwani zaidi ya saa moja kwenda tu.

“Changamoto ya maji ni kubwa hapa Mwamala, tunalazimika kutumia maji ya chumvi kwenye visima vilivyo pembezoni mwa mto, maji haya ya chumvi siyo salama kwa afya kwani ukiyanywa tumbo linauma. Wanawake wanatumia muda mrefu sana kufuata maji badala ya kufanya shughuli zingine za kujiingizia kipato. Tunaomba serikali ituletee maji ya ziwa Victoria kwani ahadi zimekuwa nyingi sana”,amesema Bw. Nkende Mabula.

Naye Bi. Nyamizi Manoni amesema endapo serikali itawasogezea huduma ya maji wataweza kujishughulisha na kazi za kujiingizia kipato badala ya kutumia muda mrefu kutafuta huduma ya maji akieleza kuwa mfano hulazimika kuamka saa 12 kufuata maji na kurudi saa nne asubuhi kutokana na foleni kubwa ya wananchi wanaosubiri huduma ya maji hayo licha ya kwamba ni ya chumvi.

Kwa upande wake, Bi. Mhoja Masali kutokana na changamoto hiyo ya maji, wakati mwingine wanalazimika kusafiri kwa zaidi ya saa mbili kufuata maji ya Ziwa Victoria katika kata ya Mwawaza hivyo kuiomba serikali kuwaonea huruma kwani wanawake ndiyo wanahangaika zaidi na wakati mwingine kusababisha migogoro ndani ya ndoa hivyo kuchochea ukatili wa kijinsia.

“Kwa kweli maji ni shida hapa Mwamala, mimi nina umri wa miaka 77, tumekuwa tukitumia maji yasiyo salama, tunatumia pamoja na mifugo kwenye mto Wela ambako huwa tunachimba visima pembezoni mwa mto. Haya maji ni ya chumvi”,amesema Mboje Malale.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Wela kijiji cha Mwamala B kata ya Mwamala, Bw. Giti Singu Giti amekiri kuwepo kwa changamoto ya maji na kueleza kuwa wananchi wamekuwa wakihangaika kufuata maji ya chumvi kwenye visima vilivyopo kwenye maeneo yao na mtoni.

 Afisa Mtendaji wa kata ya Mwamala Halmashauri ya Shinyanga Bi. Suzana Kayange amesema ni kweli katika kata hiyo kuna changamoto ya maji na hasa kipindi cha kiangazi kumekuwa na uhaba mkubwa wa maji hali inayopelekea kufuata maji ya kunywa kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga huku wengine wakitumia maji ya chumvi na ya kwenye madimbwi.

Hata hivyo amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wanaendelea na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama kwa kuboresha visima vilivyopo pamoja kuleta Maji ya Ziwa Victoria.

“Shirika la Life Water International kwa kushirikiana na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA),wananchi wanajenga kisima kirefu cha maji katika kijiji cha Bugogo lakini pia kutajengwa mradi wa Maji ya Ziwa Victoria katika vijiji vya Mwamala B na Ibanza kupitia fedha za Benki ya Dunia”,amesema Afisa Mtendaji wa kata ya Mwamala.

Akizungumza na Malunde 1 blog, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Shinyanga Mhandisi Emael Nkopi amesema RUWASA kwa kushirikiana na Shirika la Life Water International na wananchi wanaendelea na ujenzi wa mradi wa maji ya kisima kirefu katika kijiji cha Bugogo.

“Tayari katika Kijiji cha Bugogo tumechimba kisima kirefu cha maji kwa kushirikiana na Life Water International na wananchi, mtandao wa bomba, tunatarajia Life Water International ikipata pesa mapema utajengwa kuanzia Januari 2023”,amesema Mhandisi Nkopi.

“Pia tunaendelea na ujenzi wa mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kupitia Mkandarasi Mbeso Construction unatakaonufaisha vijiji vinane katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambavyo ni Masengwa, Ishinabulandi,Mwamala B, Bubale,Idodoma, Isela, Ibingo, Ng’wanghalanga na sehemu ya kijiji cha Ibanza. Tunatajia kukamilisha ujenzi wa mradi huu katika mwaka wa fedha 2022/2023 na tayari ujenzi wa tanki la maji kijiji cha Mwamala B unaendelea”,ameongeza Nkopi.
Share:

MFANYABIASHARA AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA GARI UWANJA WA FISI MADUKA 9 MWANZA


 Mwili wa mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la Muksini, ambaye ni mfanyabiashara wa bucha umekutwa kwenye gari yake katika eneo la Uwanja wa Fisi Maduka 9 jijini Mwanza, akiwa amefariki huku ikisadikika kunyongwa na kamba ambayo ilikutwa ndani ya gari hiyo.

Wakizungumza katika tukio hilo, baadhi ya mashuhuda wamesema majira ya saa 2:00 asubuhi wamelikuta gari hilo likiwa kandokando mwa barabara huku mwili huo ukiwa ndani ya gari.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa, amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akisema bado uchunguzi unaendelea kufanyika ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

Chanzo- EATV
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 6,2022















Share:

Monday 5 December 2022

WADAU WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO ZA HAKI ZA BINADAMU, UTAWALA BORA, MAADILI NA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA


Na. Beatrice Sanga- MAELEZO

Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya Haki za binadamu na Maadili Nchini wadau mbalimbali wakiwamo Tume ya Haki za Binadamu(THBUB), Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wamekutana katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam kujadili changamoto za haki za binadamu, Utawala bora, Maadili na mapambano dhidi ya rushwa nchini ili kuleta uboreshwaji wa haki hizo.

Akizungumza katika kongamano Hilo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Ng'wilabuzu Ludigija amesema uboreshwaji wa haki za binadamu ni hatua muhimu katika kutuletea maendeleo na hatua ambazo Tanzania imepiga katika maeneo mbalimbali ni kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Taasisi zinazohusika na haki za kibinadamu kwa kushirikiana na serikali na wadau wengine.

Aidha amesema maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu na Maadili Nchini yanafanyika ili kuwakumbusha na kuwapa elimu wananchi waweze kutambua haki zao na namna wanaweza kupata msaada

" Tunapoazimisha siku hii lengo ni kuwakumbusha na kuwapa elimu wananchi kutambua kwamba serikali bado imeendelea kuvitumia vyombo hivi vitatu ambavyo ni TAKUKURU, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa sababu vyombo hivi vimekuwa vikitusaidia sana kuhakikisha haki inapatikana na inatendeka, kila mtu ambaye anahusishwa kwenye mgogoro ambao upo anapata haki yake stahiki" Amesema Bw.Ludigija

Naye, Afisa Mfawidhi THBUB Tawi la Dar es Salaam, Bi Shoma Philip amesema wadau wa Haki za Binadamu, Maadili na Rushwa wamekutana kwa lengo la kujadili changamoto ambazo wanakumbana nazo katika maeneo ya kazi ambapo zitajadiliwa na kuzipatia ufumbuzi ili kufanya kazi kwa ufanisi na kuweza kuwapatia wananchi haki zao bila upendeleo.

Share:

WAZIRI DKT. GWAJIMA APANDA BASI LA WANAFUNZI MANISPAA YA SHINYANGA...AONYA USHOGA, ATAKA MFUMO KULINDA WATOTO


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akishuka ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa hatua mbalimbali inazofanya katika kutekeleza usimamizi wa kuzuia na kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kwa kununua magari mawili yanayobeba wanafunzi kuwapeleka shuleni na kuwarudisha karibu na makazi yao.


Waziri Dkt. Gwajima ametoa pongezi hizo leo Jumatatu Desemba 5,2022 wakati akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Town baada ya kupanda gari moja na wanafunzi hao kutoka majumbani mwao kuelekea katika shule hiyo iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia


“Nawapongeza sana Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ubunifu huu wa usafiri kwa gharama nafuu shilingi 200 kutoka nyumbani hadi shuleni, nina imani wanafunzi sasa watatumia muda mfupi kwenda shuleni na kuwaepusha na vishawishi mbalimbali wawapo njiani, lakini nimeshuhudia gari hili likiwa na Msimamizi wa wanafunzi ambaye ni Afisa Maendeleo ya jamii, hii ni hatua nzuri sana, ni vyema Halmashauri zingine zikaiga mfano wa Manispaa ya Shinyanga namna ya kusaidia wanafunzi, zisisubiri matamko”,amesema Dkt. Gwajima.

Katika hatua nyingine Dkt Gwajima amezitaka halmashauri na Mikoa yote nchini kuandaa mifumo ya upatikanaji wa haraka wa taarifa za kulinda watoto utaosaidia kufahamu taarifa za watoto.

"Mtengeneze na mifumo itakayogundua iwapo mtoto hayupo shuleni, iunganishwe kuanzia wazazi, walimu, polisi na jamii nzima. Endapo tutakuwa na mfumo wa kulinda watoto itatusaidia pia kudhibiti utoro shuleni, tutaweza kutambua kama mtoto yupo shule au la! Wazazi pia watasaidia kujua mtoto yuko wapi. Mfumo wa pamoja wa taarifa utasaidia kupata sulushisho la matukio ya ukatili katika jamii", amesema.

Katika hatua nyingine amewataka wadau kuendelea kupaza sauti juu ya vitendo vya jinsia moja huku akibainisha kuwa hatakubali kuona vitendo vya ushoga na vitendo vingine vya ukatili wa kijinsia kwenye vyombo vya usafiri vinavyobeba wanafunzi lakini pia shuleni.

"Suala la mapenzi ya jinsia moja halitafumbiwa macho kwa namna yoyote ile, watoto watalindwa kwa hali zote. Nawatangazia waovu wote wanaofundisha madarasa ya ushoga waache mara moja, hata huyo mwanaume aliyekamatwa huko Geita akifundisha watoto ushoga akiwa amevaa nguo za kike ‘sidiria’ na vitu vya kike kike ni lazima achunguzwe, tutalifuatilia hili jambo haiwezekani watoto wetu waharibiwe kwa kufundishwa mambo yasiyofaa, Hili la ushoga nitalifia. Tutawalinda watoto, na hayo madarasa ya ushoga yafe huko huko",amesema Dkt. Gwajima.

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo amesema ameahidi mkoa huo kuendelea kupambana na vitendo vya ukatili na kufuata maelekezo yote yaliyotolewa na kwamba wamejipanga kukutana na wadau mbalimbali ili kutengeneza mfumo wa kutoa taarifa kwa ajili ya kuwalinda watoto.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manipaa ya Shinyanga, John Tesha ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, amesema halmashauri hiyo inaendelea kutoa elimu ya kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto mara kwa mara katika ngazi ya jamii, kwenye nyumba za ibada na Shule za msingi , Sekondari na vyuo.

“Pia halmashauri imetumia nafasi ya utoaji mikopo kwa asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kama njia nyingine za kuzuia na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto”,amesema Tesha.

“Mfano mwingine wa namna mikopo ya asilimia 10 ilivyosaidia kwenye kuzuia na kutokomeza ukatili kwa watoto ni ule ambao mwezi Aprili 2022, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ilitoa mikopo yenye thamani ya shilingi Milioni 120 kwa vikundi viwili vya vijana. Vikundi hivyo tulivisimamia na kununua magari mawili (Moja ni Basi aina ya Tata na lingine ni Basi dogo aina ya Nissan – Civilian) yanayofanya kazi ya kubeba wanafunzi”,ameongeza Tesha.

Ameeleza kuwa Vikundi hivyo vya vijana vilipewa maelekezo na kusainiana mkataba na Halmashauri kuhakikisha nyakati za asubuhi kuanzia saa 12 hadi saa 2 asubuhi magari hayo yanabeba wanafunzi kuwapeleka shuleni na nyakati za jioni kuanzia saa 10 na nusu hadi saa 12 jioni magari hayo yanabeba wanafunzi kuwarudisha karibu na makazi yao kwa bei elekezi ya shilingi 200/= / 300/=.

“Lengo la kufanya hivi ni kuwahakikishia wanafunzi usalama wao wanapoenda shuleni na wakati wa kurudi nyumbani na kuhakikisha wanafunzi wanafika shuleni kwa wakati na siku zote za masomo hivyo kuwahakikishia ufaulu mzuri katika mitihani yao”,amesema Tesha.

Amesema upatikanaji na utumiaji wa magari hayo ya mkopo kwa vijana yamewapunguzia wazazi gharama za kuwasafirisha watoto kwenda na kurudi shuleni ambapo gharama za kumsafirisha mtoto kwenda na kurudi shuleni kwa siku ni kati ya shilingi 500/= - 600/= na kwa mwezi ni kati ya shilingi 10,000/= - 12,000/=

“Hii ni gharama nafuu ukilinganisha na gharama walizokuwa wanatumia wengi wao za kutumia baiskeli ambapo huwa ni shilingi 500/= hadi 1000/= kwa safari moja ambapo kwa siku ni shilingi 1000/= -hadi 2000/= na kwa mwezi ni shilingi 20,000/= hadi 40,000/=”,ameeleza.

“Kwa kutumia mikopo ya asilimia 10 pia Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imetoa Bajaji kwa watu wenye ulemavu kwa ajili ya biashara ya usafirishaji wa abiria ambapo pia waliokopa tumewaelekeza kubeba wanafunzi popote wanapowakuta kwa bei elekezi. Pia katika mwaka huu wa fedha 2022-2023 unaoendelea tumejipanga kutoa mikopo ambayo itawezesha kununua magari/ Hiace Sita ambazo zitawajibika kufanya biashara ya abiria ndani ya Manispaa na kuhakikisha zibabeba wanafunzi kwa bei elekezi”,amefafanua Tesha.

Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa Nancy Kasembo ameshukuru uongozi wa mkoa na Manispaa ya Shinyanga kwa ubunifu huo ambao utasaidia kupunguza utoro na mimba za utotoni kutokana na ukatili.

Akiwa mkoani Shinyanga Waziri Gwajima amezungumza pia na wananchi kupitia kituo cha Redio Faraja Fm, kufanya mazungumzo na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Mhashamu Liberatus Sangu pamoja na kutembelea Kamati ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto kata ya Ibinzamata sambamba na kutoa vyeti vya pongezi kutambua mchango wa baadhi ya taasisi na watu binafsi katika kushiriki mapambano dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto.


 Baadhi ya waliokabidhiwa vyeti hivyo ni Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale, Mwandishi wa Habari wa Azam Tv Kasisi Kosta ,  Chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club -SPC), ICS na kituo cha Redio Faraja Fm.

 ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akisalimiana na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Town Manispaa ya Shinyanga kabla ya kupanda kujionea namna Basi la Wanafunzi linavyosafirisha wanafunzi Mjini Shinyanga leo Jumatatu Desemba 5,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akisalimiana na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Town Manispaa ya Shinyanga kabla ya kupanda kujionea namna Basi la Wanafunzi linavyosafirisha wanafunzi Mjini Shinyanga. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manipaa ya Shinyanga, John Tesha ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manipaa ya Shinyanga, John Tesha  (kulia) ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga. Kushoto ni Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Shinyanga Elizabeth Mweyo anayesimamia wanafunzi katika Basi la wanafunzi.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akiwa ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari  Town ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akishuhudia wanafunzi wa shule ya Sekondari wakishuka ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akiwa ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akisalimianan na Dereva wa Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akishuka ndani ya Basi aina ya Tata linalofanya kazi ya kubeba wanafunzi Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akisalimiana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manipaa ya Shinyanga, John Tesha ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manipaa ya Shinyanga, John Tesha ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga akizungumza katika shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manipaa ya Shinyanga, John Tesha ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga akizungumza katika shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akizungumza katika shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akizungumza katika shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza katika shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Tanzania, Nancy Kasembo akizungumza katika shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga wakisikiliza nasaha mbalimbali.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga wakisikiliza nasaha mbalimbali.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Town Mjini Shinyanga wakisikiliza nasaha mbalimbali.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger