Saturday 26 November 2022

DIT YAANDAA KOZI MPYA ZITAKAZOWEZESHA JAMII KUENDANA NA MAPINDUZI YA NNE YA VIWANDA


Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) inaandaa kozi mpya zitakazowezesha jamii kuendana na Mapinduzi ya nne ya viwanda ambazo zitasaidia kukidhi mahitaji ya soko la ajira.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Mkuu wa Taasisi Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam Prof. Ezekiel Amri katika ufunguzi wa warsha kwa wadau iliyofanyika kampasi Kuu ya Dar es salaam yenye lengo la kukusanya maoni kwa ajili ya kuboresha mitaala ya kufundishia kozi hizo katika ngazi ya Uzamili na Stashahada.

Prof. Amiri amezitaja kozi hizo kuwa ni Uzamili katika Uhandisi Komputa, Uzamili katika Uhandisi Mawasiliano Angani, Uzamili katika Usalama wa Kimtandao pamoja na Stashaha ya Mitambo Viwandani.

Prof Amir ameeleza kuwa, DIT imeaanda warsha hiyo ili kupata maoni ya Wadau kulingana na mahitaji ya soko la ajira ambapo amesema kuwa maoni yao yatatumika katika kuandaa mitalaa itakayoendana na mapinduzi ya nne ya viwanda pia kusaidia kutatua changamoto katika jamii.

“Mapinduzi ya nne ya viwanda yanaenda kasi sana na yamejikita katika Tehama, ni muhimu kujiandaa kwa kuwa na mitaala yetu inayoendana na mapinduzi haya ili tusibaki nyuma ". Amesema Prof Amir

Ameeleza kuwa, mapinduzi hayo yana fursa na changamoto za kufanyia kazi hivyo kwa kuboresha mitaala hiyo itawawezesha vijana watakaosoma kozi hizo kuendana na mapinduzi hayo kwa kuwa wataenda kukidhi mahitaji yaliyopo viwandani na kwenye jamii.

Prof Amir ameendelea kusisitiza kuwa, taasisi imeona umuhimu na mahitaji ya kozi hizo na namna ambavyo itawawezesha vijana katika soko la ajira na hiyo ndiyo sababu iliyopelekea kuandaa mitaala itakayoendana na mabadiliko hayo.

Aidha, amewataka wadau kutoa maoni yao kutokana na wanachokiona kwenye jamii kwa sasa na mbeleni kwa kuwa maoni yakiwa mazuri ndiyo yatakayozalisha mitaala bora. Amesema “Uwepo wenu katika warsha hii ni muhimu sana, maoni yenu ni ya muhimu kwani mawazo mtakayoyatoa yatasaidia uboreshaji wa mitaala hii”.

Naye Mratibu wa program hiyo ya kuandaa mitaala, Daktari Paul Mbaga amesema kuwa kikao hicho ni muhimu kwani nia kubwa ni kuiwezesha DIT kuja na mitaala itakayotatua changamoto zilizoko katika jamii.

“Ninyi mtatusaidia kuona tunachokiandaa kama kitafaa katika jamii katika kutatua changamoto za jamii na ndio sababu kubwa iliyopelekea kuwaomba mshiriki kwenye zoezi hilo.

Warsha hiyo iliyofanyika kwa siku moja imeshirikisha wadau kutoka katika taasisi mbalimbali za serikali na binafsi.
Share:

YANGA HAIKAMATIKI, YASHINDA TENA 2-0 MBELE YA MBEYA CITY



***********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Yanga imeendelea kujiweka vizuri kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara mara baada ya kufanikiwa kuichapa Mbeya City mabao 2-0 na kuwafanya kufika pointi 32 akiwa ameshuka dimbani mara 12.

Fiston Kalala Mayele ameendelea kutikisa nyavu baada ya leo tena kupachika mabao mawili na kumfanya aendelea kushikilia usukani kwa wapachikaji wa mabao ndani ya ligi kuu akifikisha mabao 10.

Bao la kwanza Mayele alifunga dakika 24 ya mchezo kipindi cha kwanza na bao la pili akifunga dakika 79 kipindi cha pili.
Share:

DKT. TULIA ATAKA UVCCM KUACHA VIOJA,WAJIBU HOJA


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akizungumza kwenye ufunguzi wa mbio za Marathon kuelekea uchaguzi Mkuu ngazi ya UVCCM unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2022 Jijini Dodoma.

 Na Dotto Kwilasa,DODOMA

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson amewataka vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kutumia nafasi zao kubishana kwa hoja na kuendelea kudumisha amani ,umoja na mshikamano hali itakayosaidia kuwalinda Viongozi wa taifa .

Dkt.Tulia ameyasema hayo Jijini Dodoma leo Novemba 26,2022 wakati akifungua mbio za Marathon za  vijana wa UVCCM katika viwanja vya Jamhuri katika kuelekea uchaguzi Mkuu wa UVCCM ngazi ya Taifa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2022 Jijini Dodoma .

Amesema ni  jukumu la vijana hao kuacha malumbano na kubishana kwa hoja zinazojenga  na kuongeza kuwa ikiwa vijana hao wataenzi amani na mshikamano itawasaidia kuondokana na matumizi ya dawa za kulevya na kuwa na ari ya kufanya kazi kwa bidii .

Spika Tulia amesema,"Hakikisheni katika chaguzi zenu mnaenzi amani kama  ilivyo itikadi ya Chama chetu ,msianzishe vioja vinavyolenga kubomoa bali hoja zitakazoeleza maendeleo yanayofanywa na Serikali na si vinginevyo".

Pamoja na hayo ameeleza kuwa vijana hao wana jukumu kubwa la kuwalinda viongozi wao kwa hoja zinazoeleweka ikiwa ni pamoja na kuelekeza mambo mengi yanayofanywa na Serikali.

"Msikae kimya,tangazeni miradi tuliyonayo achaneni kabisa na masuala yanayowapotezea muda ambayo hayajengi,kuna wakati mnasubiri mtu atoe hoja ili muanzishe  kuleta  vioja vyenu naomba muache hiyo tabia kwani sio utamaduni wa Chama chetu ,"amesema

Pamoja na hayo ametumia nafasi hiyo kuwapongeza vijana wa hamasa wa Chama hicho kwa juhudi zao 
katika kuamsha ari kwenye matukio ya Viongozi wakuu na kueleza kuwa huo ndio uzalendo unaotakiwa kwa Kila kijana.

Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi ( UVCCM )Kenani Kihongosi amemshukuru spika Tulia kwa kukubali kuungana nao katika mbio hizo zilizoambatana na matembezi ya amani na kueleza kuwa hiyo ni fursa ya vijana kujenga Afya na kuepuka magonjwa.
Share:

MAHAFALI YA 15 YA CHUO KISHIRIKI CHA ELIMU DAR ES SALAAM (DUCE)

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwatunuku Wahitimu Digirii za Umahiri ya Elimu katika Taaluma za Mitaala kwenye Mahafali ya 15 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika chuoni hapo leo Novemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwatunuku Wahitimu Digirii za Umahiri ya Elimu katika Uongozi wa Elimu na Taaluma za Sera kwenye Mahafali ya 15 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika chuoni hapo leo Novemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwatunuku Wahitimu Digirii za Umahiri, Stashahada ya Uzamili na Digirii za Awali kwenye Mahafali ya 15 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika chuoni hapo leo Novemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapatia zawadi ya vyeti wahitimu waliofanya vizuri kwenye masomo yao kwenye Mahafali ya 15 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika chuoni hapo leo Novemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar akizungumza kwenye Mahafali ya 15 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika chuoni hapo leo Novemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof.William Anangisye akizungumza kwenye Mahafali ya 15 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika chuoni hapo leo Novemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam. Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof.Stephen Maluka akizungumza kwenye Mahafali ya 15 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika chuoni hapo leo Novemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Rasi-Taaluma, Utafiti na ushauri Elekezi, Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Dkt.Christina Raphael Isingo akizungumza kwenye Mahafali ya 15 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika chuoni hapo leo Novemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Boniventure Rutinwa akizungumza kwenye Mahafali ya 15 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika chuoni hapo leo Novemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam. Mmoja wa wahitimu waliofanya vizuri kwenye masomo yao akisoma hotuba kwa niaba ya wahitimu kwenye Mahafali ya 15 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika chuoni hapo leo Novemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya Wakuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Chuo hicho Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa katika Maandamano kwenye Mahafali ya 15 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Wahitimu wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakiwa kwenye Mahafali ya 15 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika chuoni hapo leo Novemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam. Wakuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Chuo hicho Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Mahafali ya 15 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika chuoni hapo leo Novemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam. Wakuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Chuo hicho Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi yawadau wa chuo hicho kwenye Mahafali ya 15 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika chuoni hapo leo Novemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam.Wakuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Chuo hicho Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kwenye Mahafali ya 15 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika chuoni hapo leo Novemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KUPITIA Mradi wa HEET, Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kinatarajia kutumia zaidi ya shilingi Bilioni kumi na saba kwaajili ya kuendelea kufanya ukarabati wa miundombinu ya majengo ya Chuo, kujenga majengo na miundombinu mingine mipya na kusomesha wanataaluma katika ngazi ya uzamili na uzamivu kwenye Vyuo Vikuu mbalimbali duniani.

Ameyasema hayo leo Novemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Balozi Mwanaidi Maajar katika Mahafali ya 15 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika chuoni hapo.

Amesema Baraza linaendelea kuiomba Serikali na wafadhili wengine kusaidia kuongeza miundombinu ya ujifunzaji na ufundishaji chuonii hapo kwani kumekuwa na changamoto za maabara na vifaa vingine muhimu vya kufundishia na kujifunzia.

"Neema ya ongezeko la wanafunzi kila mwaka imekuwa haiendi sambamba na ongezeko la miundombinu kama vile kumbi za mihadhara, upungufu mkubwa wa hosteli kwa wanafunzi na gharama kubwa ya kusomesha wanataaluma katika ngazi ya uzamili na uzamivu". Amesema

Nae Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof.William Anangisye ameipongeza Serikali kwa kuendelea kutoa rasilimali muhimu zinazohitajika katika uendeshaji wa Chuo.

Amesema Serikali imeendelea kujenga na kuboresha miundombinu muhimu na kutoa fedha za uendeshaji wa Chuo kwa ujumla. Ambapo pia amewashukuru wabia wao wa kitaifa na kimataifa waliochangia gharama za uandaaji na uendeshaji wa programu mbalimbali za masomo ambazo wahitimu wameshiriki na kunufaika nazo.

Kwa upande wake Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof.Stephen Maluka amesema kwa mwaka 2022/2023 Chuo kimetenga shilingi 480,035,000/= kwaajili ya mafunzo ya watumishi ambapo kati ya kisi hicho, shilingi 101,448,00/= ni kwaajili ya mafunzo ya muda mfupi na shilingi 378,587,000/= kwa ajili ya mafunzo ya muda mrefu.

Ameeleza kuwa jumla ya watumishi 54 wanatarajiwa kunufaika na mafunzo hayo kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

"Chuo kimetenga dola za Kimarekani 1,000,000 sawa na Bilioni 2.3 za Kitanzania kwaajili ya mafunzo ya muda mrefu ya watumishi kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi ambapo jumla ya watumishi 16 wanasomeshwa Digirii za Umahiri na Uzamivu katika Vyuo mbalimbali duniani". Amesema Prof.Maluka.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBA 26,2022

















Share:

Friday 25 November 2022

HUYU MWANAUME ALINITESA SANA KATIKA MAHUSIANO ILA SASA NIMEMTULIZA

Jina langu ni Brenda kutokea Mbeya nchini Tannzania, mimi ni binti wa miaka 24, niliingia katika mahusiano na kijana mmoja, nikampa kila kitu nilichoweza kwa wakati huo.

Nakumbuka kipindi kile nyumbani tulikuwa tuna ng'ombe, niliiba maziwa kila siku na kumpelekea nyumbani kwao, nilimpend sana, penzi letu likawa huru alipoanza maisha yake mwenyewe.

Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi, alinifundisha yeye, nikatengeneza maisha yangu yote kwake, akanifanya nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda ghetto kwake.

Kama haikutosha sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe, niliamini kuwa ndiye mume wangu mtarajiwa, kwa nini nikatae. Nilimkubalia kila kitu.

Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika siku zangu, kweli nilikuwa msomi na niliyajua madhara ya kufanya hivyo lakini sikutaka kumuudhi huyo niliyeamini kuwa ni mume wangu.

Nilipenda tutumie kinga lakini aliipinga sana, nikapata mimba ya kwanza!! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe. Nikachukua hela nyumbani nikafanya alivyotaka, kwa mara ya kwanza nikatoa mimba.

Haikuniuma sana, niliamini kuwa ni yeye atakuja kunioa na atanifichia aibu hii, nilitegemea sasa tutaanza kutumia kinga. Lakini hapana haikuwa hivyo.

Aliendelea kunilaghai, tayari aliujua udhaifu wangu, alinishika hapa na pale, nikishtuka tayari amefanya anavyojua, nikavumilia kwa kuwa alikuwa mume wangu mtarajiwa.

Mume asiyejulikana hata kwa wazazi, nilimfumania na mke wa mtu, niliumia sana kwa sababu nilikuwa nampenda nilimsamehe,

hivyo nilifanya jinsi anavyotaka yeye ila mwisho wa siku nilichoka na kurudi nyumbani kwetu.

Miaka ikapita, miezi ikaenda kipindi nipo mtandaoni nilikutana na maoni ya watu kuwa Dr. Kiwanga anatatua migogoro ya kimahusianpo. Nilichukua namba yake na kumpigia nikamuelezea jinsi mahusiano yangu ulivy vunjika, nashukuru akanipa tiba yake iliyokuja kubadili kila kitu.

Siku chache mbele niliona simu yake akinipigia na kuomba msamaha, kwa sababu nilikuwa nampenda bado niliweza kumsamehe tukaanza maisha mapya. Nilimshukuru sana Dr. Kiwanga kwa kunirudishia mpenzi wangu, kwa sasa amenio na tumeza kujaliwa watoto wawili.

Ukiachana na hilo, Dr. Kiwanga ana uwezo kumfanya mtu kuwa na bahati maishani mwake, kushinda katika michezo ya bahati nasibu, kukukinga na maadui zako, kukufanya ushinde migogoro kama ya ardhi, kuwa na mvuto wa kimapenzi, kuongeza mauzo katika biashara.

Vile vile anatibu magonjwa kama Kaswende, Kisonono, Kifua Kikuu, Presha na mengine mengi, kwa mawasiliano zaidi mtumie barua pepe; kiwangadoctors@gmail.com, tembelea tovuti yake; www.kiwangadoctors.com au piga simu +254 769404965.

Mwisho.
Share:

HAKIRASILIMALI WAHITIMISHA JUKWAA LA UZIDUAJI MWAKA 2022 JIJINI DODOMA, WADAU WAPONGEZA KUPANUA UELEWA SEKTA YA UZIDUAJI

Mkurugenzi Mtendaji wa HakiRasilimali Adam Anthony akizungumza wakati wa ufungaji wa Jukwaa la Sekta ya uziduaji mwaka 2022.

Na Marco Maduhu, DODOMA

JUKWAA la Sekta ya uziduaji lililoandaliwa na HakiRasilimali, limehitimishwa Rasmi leo, huku wadau wakiwamo madiwani ambao wanatoka kwenye maeneo ya uchimbaji madini, wakipongeza kupanua uelewa katika ya Sekta ya uziduaji.



Jukwaa hilo la sekta ya uziduaji lilianza jana Novemba 24, 2022 na limehitishwa leo Novemba 25, huku mada mbalimbali zikiwasilishwa pamoja na kujadiliwa kwa lengo la kuikuza Sekta ya uziduaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa HakiRasilimali Adam Anthony, akizungumza wakati wa kufunga jukwaa hilo, amewashukuru wadau wote wa Sekta ya uziduaji kwa ushiriki wao muda wote ndani ya siku hizo mbili.

Nao wadau wa Sekta ya uziduaji akiwamo Diwani Faustine Shibiliti kutoka Kata ya Igalula wilayani Sengerema mkoani Mwanza, wameshukuru kujumuika kwenye jukwaa hilo la uziduaji, ambalo wamesema limewaongezea uelewa zaidi kufahamu mambo mengi katika Sekta ya uziduaji ambayo inahusisha Madini, Mafuta na Gesi asilia.

Aidha, jukwaa hilo la uziduaji limeshirikisha wadau takribani 200 kutoka katika maeneo mbalimbali ambayo yanajihusisha na Sekta  ya uziduaji, wakiwamo wawakilishi kutoka Serikali Kuu, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Asasi za Kiraia, Makampuni ya Madini, wachimbaji wadogo wa madini, wawakilishi kutoka katika jamii inayoishi maeneo ya migodi, wanataaluma na waandishi wa habari.

Lengo la jukwaa hilo la uziduaji ni kujadili, kubadilisha uzoefu na kujifunza kutoka kwa washiriki namna ya kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika sekta ya uziduaji.


Mkurugenzi Mtendaji wa HakiRasilimali Adam Anthony akizungumza wakati akifunga Jukwaa la Sekta ya uziduaji mwaka 2022.

Diwani wa Kata ya Igalula wilayani Sengerema mkoani Mwanza Faustine Shibiliti akitoa shukrani kwa kupata elimu na kuongeza uelewa zaidi juu ya Sekta ya uziduaji.

Madiwani ambao wanatoka kwenye maeneo ya Sekta ya uziduaji wakiendelea kutoa neno la shukrani, kupata elimu katika Sekta ya uziduaji kupitia jukwaa za uziduaji.

Wadau wa Sekta ya uziduaji wakiwa kwenye jukwaa la  uziduaji mwaka 2022.

Wadau wa Sekta ya uziduaji wakiwa kwenye jukwaa la  uziduaji mwaka 2022.

Wadau wa Sekta ya uziduaji wakiwa kwenye jukwaa la uziduaji mwaka 2022.

Wadau wa Sekta ya uziduaji wakiwa kwenye jukwaa la uziduaji mwaka 2022.

Wadau wa Sekta ya uziduaji wakiwa kwenye jukwaa la  uziduaji mwaka 2022.

Wadau wa Sekta ya uziduaji wakiwa kwenye jukwaa la  uziduaji mwaka 2022.
Wadau wa Sekta ya uziduaji wakiwa kwenye jukwaa la  uziduaji mwaka 2022.

Wadau wa Sekta ya uziduaji wakiwa kwenye jukwaa la  uziduaji mwaka 2022.

Wadau wa Sekta ya uziduaji wakiwa kwenye jukwaa la  uziduaji mwaka 2022.

Wadau wa Sekta ya uziduaji wakiwa kwenye jukwaa la uziduaji mwaka 2022.

Mkurugenzi Mtendaji wa HakiRasilimali Adam Anthony akipiga picha ya pamoja na wadau wakubwa wa jukwaa hilo la Sekta ya uziduaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiRasilimali Adam Anthony, akipiga picha ya pamoja na Bodi ya HakiRasilimali.

Picha ya pamoja ikipigwa kati ya wadau wakubwa wa Jukwaa la Sekta ya uziduaji na wafanyakazi wa HakiRasilimali.
Picha za Pamoja zikiendelea kupigwa na waongoza mjadala kwenye jukwaa hilo la Sekta ya uziduaji.

Picha za Pamoja zikiendelea kupigwa.

Picha za Pamoja zikiendelea kupigwa.

Picha za Pamoja zikiendelea kupigwa.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger