Wednesday 28 September 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI SEPTEMBA 29,2022















Share:

MADIWANI HALMASHAURI YA SHINYANGA WABARIKI TAARIFA ZA HESABU ZA MWISHO KWA MWAKA 2021/2022


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje akiongoza Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kujadili na kupitisha Taarifa za Hesabu za Mwisho za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022 uliofanyika leo Jumatano Septemba 28,2022 katika ukumbi wa makao makuu ya halmashauri hiyo Iselamagazi. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Nicodemus Simon.

Katika mkutano huo, Waheshimiwa Madiwani wameruhusu Mchakato wa ufungaji wa Ripoti za Hesabu za Mwisho za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022 zilizoishia Juni 30,2022 uendelee kwa ajili ya kuwasilisha katika Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje akizungumza kwenye Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kujadili na kupitisha Taarifa za Hesabu za Mwisho za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje akizungumza kwenye Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kujadili na kupitisha Taarifa za Hesabu za Mwisho za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Stewart Makali akizungumza kwenye Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kujadili na kupitisha Taarifa za Hesabu za Mwisho za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Mweka Hazina wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Rumoka akitoaa Taarifa za Hesabu za Mwisho za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022
Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kujadili na kupitisha Taarifa za Hesabu za Mwisho za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ukiendelea
Madiwani wakiwa kwenye Mkutano Maalumu wa kujadili na kupitisha Taarifa za Hesabu za Mwisho za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022
Madiwani wakiwa kwenye Mkutano Maalumu wa kujadili na kupitisha Taarifa za Hesabu za Mwisho za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022
Mkutano ukiendelea
Madiwani wakiwa kwenye Mkutano Maalumu wa kujadili na kupitisha Taarifa za Hesabu za Mwisho za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022
Madiwani wakiwa kwenye Mkutano Maalumu wa kujadili na kupitisha Taarifa za Hesabu za Mwisho za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022
Madiwani wakiwa kwenye Mkutano Maalumu wa kujadili na kupitisha Taarifa za Hesabu za Mwisho za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022
Madiwani wakiwa kwenye Mkutano Maalumu wa kujadili na kupitisha Taarifa za Hesabu za Mwisho za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022
Madiwani wakiwa kwenye Mkutano Maalumu wa kujadili na kupitisha Taarifa za Hesabu za Mwisho za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi akitoa salamu kwenye Mkutano Maalumu wa kujadili na kupitisha Taarifa za Hesabu za Mwisho za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini, Erinestina Richard akitoa salamu kwenye Mkutano Maalumu wa kujadili na kupitisha Taarifa za Hesabu za Mwisho za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini, Edward Ngelelaakitoa salamu kwenye Mkutano Maalumu wa kujadili na kupitisha Taarifa za Hesabu za Mwisho za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022
Wadau na wakuu wa Idara na Vitengo  Halmashauri ya Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano Maalumu wa kujadili na kupitisha Taarifa za Hesabu za Mwisho za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

NDEJEMBI AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUJITOA KIKAMILIFU KATIKA KUWAHUDUMIA WANANCHI


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, wakati wa ziara yake ya kikazi katika halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili.

Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao, wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili.


Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Meatu, Bw. Msoleni Dakawa, akitoa taarifa ya utelezaji wa majukumu ya halmashauri yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (Wakwanza kulia), wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi katika halmashauri hiyo.


Mkuu wa Shule ya Kimali, Bw. Marco Ng’wendamunkono wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu (aliyesimama) akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa halmashauri hiyo.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi (Wakwanza kushoto) akijibu hoja iliyokuwa imewasilishwa na mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri hiyo. Kulia Kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Fauzia Ngatumbura na kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Oscar Maduhu.


Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Thomas Shishwa akitoa neno la shukurani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi, wakati wa ziara yake ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.

***************************

Na. Veronica E. Mwafisi-Meatu

Tarehe 28 Septemba, 2022

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka watumishi wa umma nchini kujituma na kujitoa kikamilifu katika kuwahudumia wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa huduma zinazotolewa na Serikali kupitia taasisi zake.

Mhe. Ndejembi ametoa wito huo kwa watumishi wa umma, wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu akiwa katika ziara ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamozo zinazowakabili watumishi wa umma katika Wilaya hiyo.

Mhe. Ndejembi amesema, watumishi wa umma ni mabalozi wa serikali hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa uadilifu, weledi, kujituma na kujitoa kwa ajili ya serikali katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

“Mtumishi wa umma ni mwakilishi wa serikali mahali anapofanya kazi, hivyo hana budi kutambua kuwa serikali imemuajiri ili kuwatumikia wananchi kwa kuwapatia huduma bora kama ambavyo serikali imekusudia,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Meatu, Bw. Msoleni Dakawa amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ajira mpya 104 katika Halmashauri hiyo zikiwemo kada za elimu na afya ili kuwahudumia wananchi wilayani humo.

Aidha, Bw. Msoleni ameishukuru ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kutoa kipaumbele cha kuwapatia stahiki watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.

Naye, Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Thomas Shishwa kwa niaba ya watumishi wengine, amemshukuru Mhe. Ndejembi kwa kutenga muda wake kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi papo kwa hapo, ikiwa ni pamoja na kuwapatia ufafanuzi wa hoja za masuala ya kiutumishi walizoziwasilisha.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi anaendelea na ziara ya kikazi Mkoani Simiyu yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani humo.

Share:

NAIBU WAZIRI MASANJA AFUNGUA WARSHA YA WADAU WA UHIFADHI MFUMO WA IKOLOJIA WA HEWA YA UKAA


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akifungua warsha ya siku mbili ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani) akifungua warsha ya siku mbili ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (kulia) na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jeroen Verheul (kushoto) wakikata utepe kama ishara ya kufungua warsha ya siku mbili ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.


Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jeroen Verheul akizungumza katika warsha ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.


Kaimu Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii,Deusdedit Bwoyo akitoa maneno ya utangulizi katika warsha ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.


Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo akizungumzia namna taasisi yake inavyoshiriki katika utunzaji wa misitu ya mikoko katika warsha ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (katikati)katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

…………………………………………….

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amefungua warsha ya siku mbili ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini.

Warsha hiyo imefunguliwa Septemba 27,2022 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika ufunguzi huo, Mhe. Masanja amesema misitu ya mikoko na majani ya baharini inatarajiwa kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa bluu kwa kuhifadhi hewa ya ukaa mara tano zaidi ya misitu ya kawaida.

Ameelekeza washiriki wa warsha hiyo kuibua masuala muhimu yatakayoisaidia Serikali kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya biashara ya hewa ya ukaa.

Ametaja faida nyingine za misitu ya mikoko kuwa ni kusaidia kukabiliana na athari za kimazingira kama mabadiliko ya tabia ya nchi, mmomonyoko wa udongo na vimbunga baharini, kusaidia uwepo wa mazalia ya samaki, chanzo cha kuni, mbao na milunda ya kujengea.

Aidha, amesema uwepo wa shughuli za kibinadamu katika misitu ya mikoko, hupelekea kupotea kwa mikoko na kuathiri ukuaji wa uchumi wa bluu.

Mhe. Masanja amefafanua kuwa ili kukabiliana na changamoto za upotevu wa misitu ya mikoko Serikali itatoa elimu kwa wananchi namna bora ya kutunza mikoko hiyo na kushiriki moja kwa moja katika uhifadhi wa mikoko kwa kushirikiana na sekta binafsi.

Naye, Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu za Misitu Tanzania, Prof Dos Santos Silayo amesema wananchi wanatakiwa wawe na mifumo endelevu ya kupata kipato itakayowawezesha kukidhi mahitaji yao bila kukata mikoko.

“Mifumo hii itawawezesha wananchi kuvuna hewa ya ukaa na kujipatia fedha bila kuathiri mikoko kwa mfano kufanya shughuli za ufugaji nyuki na utalii” amefafanua Prof. Silayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uvuvi, Wizara ya Uchumi wa Bluu Zanzibar, Dkt. Salumu Hemedi amesema kuna uhusiano mkubwa wa uchumi wa bluu na biashara ya hewa ya ukaa.

Amesema biashara ya hewa ya ukaa inafanyika sana katika mataifa mengi duniani ambayo yana viwanda yanatumia hewa ya ukaa katika nchi ambazo zina misitu ambazo zinalipwa ili kutunza misitu.

Warsha hiyo imehudhuriwa wa Maafisa kutoka Serikali ya Tanzania na Kenya, Wawakilishi wa Sekta Binafsi, Wadau wa Uhifadhiwa Mifumo Ikolojia ya Bluu pamoja na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger