Friday 2 September 2022

WAZIRI JAFO AMPONGEZA RC MAKALLA KWA OPERESHENI YA KUKAMATA MIFUKO YA PLASTIKI.

Afisa Mazingira NEMC Bw.Erick Fussi akimuonesha Waziri Jafo baadhi ya Mifuko ambayo wameikamata katika kiwanda cha Swallow investment Ltd mara alipofanya ziara katika kiwanda hicho kilichopo Tegeta Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Amos Makalla wakati alipofanya ziara katika kiwanda cha Swallow investment Ltd kilichopo Tegeta Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo akimisikiliza Afisa Rasilimali Watu wa kiwanda cha Swallow investment Ltd kilichopo Tegeta mara baada ya kutembelea kiwanda hicho leo Septemba 2,2022, ambacho kinazalisha Mifuko iliyokatazwa ambapo zaidi ya Tani 41 za Mifuko hiyo zimekamatwa.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake kwenye Kiwanda Swallow investment Ltd kilichopo Tegeta leo Septemba 2,2022 Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Waziri Jafo kwenye Kiwanda Swallow investment Ltd kilichopo Tegeta Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla wakati walipotembelea kiwanda cha Swallow investment Ltd ambacho kinazalisha mifuko ambayo imepigwa marufuku.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo ametoa muda wa siku 7 kwa Wafanyabiashara na Wananchi Wenye Mifuko ya plastiki iliyokatazwa kuisalimisha kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kupitia kikosi kazi au Kwenye Kiwanda walichochukulia Mzigo.

Pia Waziri Jafo amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Amos Makalla kwa Operesheni ya kukamata Mifuko hiyo.

Waziri Jafo ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara kwenye Kiwanda Swallow investment Ltd kilichopigwa faini ya Shilingi Milioni 100 kwa kosa la kuzalisha Mifuko iliyokatazwa ambapo zaidi ya Tani 41 za Mifuko hiyo zimekamatwa.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Waziri Jafo amempongeza RC Makalla kwa kufanikisha kukamatwa kwa Shehena ya Mifuko hiyo kupitia Operesheni aliyotangaza na kuelekeza Mikoa mingine kuiga mfano wa Mkoa wa Dar es salaam.

Aidha Waziri Jafo amemtaka Mmiliki wa Kiwanda hicho kulipa faini aliyopigwa ndani ya siku 14 na kuhakikisha anatoa gharama zote za uteketezaji wa mzigo uliokamatwa na Mifuko iliyoingizwa sokoni ahakikishe anaikusanya.

Pamoja na hayo Waziri Jafo ameelekeza Kiwanda hicho kuanza mchakato wa kupata cheti Cha tathimini ya athari za mazingira na kuzitaka Mamlaka za TRA, TBS, NSSF na Taasisi nyingine kufika kiwandani hapo kuona Kama wanazingatia taratibu.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) alipozungumza amewataka wawekezaji kuzingatia Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004, pamoja na Kanuni zake ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea ikiwemo kutozwa faini au kuchukuliwa hatua.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amemshukuru Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango na Waziri wa Mazingira kwa kumuunga mkono kwenye Operesheni hiyo.

Share:

RAIS SAMIA AFUNGUA MIRADI MBALIMBALI KIZIMKAZI, ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni wakati akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Polisi Kizimkazi, Zanzibar tarehe 02 Septemba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Abdulmajeed Nsekela wakati akifungua Maabara katika Skuli Kizimkazi, Zanzibar tarehe 02 Septemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maabara katika Skuli ya Kizimkazi Zanzibar tarehe 02 Septemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ngoma ya asili ya Watoto wadogo mara bada ya kufungua Maabara ya Skuli ya Kizimkazi Mkunguni Zanzibar tarehe 02 Septemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kufungua Ofisi za Kizimkazi Saccos Mkunguni, Zanzibar 02 Septemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kama ishara ya kufungua Ofisi za Kizimkazi Saccos Mkunguni, Kizimkazi Zanzibar 02 Septemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ukumbi wa Mitihani wa Skuli ya Kizimkazi Dimbani leo tarehe 02 Septemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni wakati akivuta kitambaa kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Polisi Kizimkazi, Zanzibar tarehe 02 Septemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati akipigiwa Wimbo wa Taifa na ule wa Afrika Mashariki kabla ya kufungua Kituo cha Polisi Kizimkazi, kwenye hafla iliyofanyika Mkunguni Zanzibar tarehe 02 Septemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa Tawi la Chama la Miwaleni, Makunduchi Zanzibar tarehe 02 Septemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kama ishara ya kufungua Ofisi ya Sheha ya Tasani, Zanzibar tarehe 02 Septemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia Wananchi wa Kizimkazi mara baada ya kufungua Kituo cha Polisi Kizimkazi, Zanzibar tarehe 02 Septemba, 2022.
Share:

RC MJEMA AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI UTEKELEZAJI MKATABA WA LISHE, CHANJO YA UVIKO -19 NA POLIO SHINYANGA...AGEUKA MBOGO UPATIKANAJI TAKWIMU

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akifungua kikao cha Tathmini ya  Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha 2021/2022 na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema ameziagiza Halmashauri za wilaya katika mkoa huo zitoe shilingi 1000 kwa kila mtoto aliye chini ya miaka mitano kila mwezi na kufanya vikao vya tathmini ya lishe ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe.

Mjema ametoa agizo hilo leo Ijumaa Septemba 2,2022 wakati wa Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha 2021/2022 na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano iliyoanza Septemba 1,2022.

Mjema amesema kikao hicho cha tathmini ni fursa ya kujipima na kuchukua hatua kwa kila halmashauri kubaini changamoto zinazokwamisha ili wazifanyie kazi na kuondokana na hali isiyoridhisha ya utekelezaji wa afua za lishe.

“Tukumbuke kuwa Lishe bora na Chanjo ya Polio ni msingi wa maendeleo ya taifa letu, nawatakia Utekelezaji mwema wa Kampeni ya Polio na shughuli za lishe ili kufikia lengo la uchanjaji na utekelezaji wa mkataba wa lishe”,amesema Mjema.

“Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea na utekelezaji wa mkataba wa Lishe kupitia Mikoa, Halmashauri, kata na Vijiji/mitaa tangu mwaka 2018, utekelezaji huu wa mkataba wa Lishe umewezesha kuboresha utoaji wa huduma za lishe kwa wananchi”, ameongeza.

Amesema lengo la Mkataba wa Lishe ni kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya serikali ya kutenga na kutumia shilingi 1000 kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano kwa ajili ya kutekeleza afua za lishe ngazi ya halmashauri.

“Katika utekelezaji wa Mkataba wa Lishe ngazi ya halmashauri kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2022, mkoa wa Shinyanga umetoa fedha kwa asilimia 76.56 ambapo Manispaa ya Shinyanga imeongoza kwa utoaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa afua za lishe kwa kutoa fedha kwa asilimia 100”,amefafanua.

Mkuu huyo wa Mkoa amewapongeza Wakuu wa Wilaya na viongozi wengine kwa kusimamia mkataba wa lishe na kufanya vikao vya tathmini kila baada ya miezi mitatu kama mwongozo unavyoelekeza.

Akizungumzia kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio kwa awamu ya tatu iliyoanza Septemba 1,2022 , Mjema amesema Kampeni hiyo itafanyika hadi Septemba nyumba kwa nyumba ambapo walengwa kimkoa ni 445,681 walio chini ya miaka mitano.

Amesema Chanjo zinazotolewa na Serikali ni salama na zimedhibitishwa na Wizara ya Afya pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) hivyo kuwaomba wadau wa afya kukanusha upotoshaji wowote unaoweza kujitokeza katika jamii kuhusu kampeni za chanjo pamoja na kuhamasisha wananchi kupata chanjo na kusimamia shughuli zote za utekelezaji wa kampeni za chanjo.

“Kwenye eneo la utoaji wa Chanjo za UVIKO 19, Mkoa unaendelea na utoaji wa chanjo hizo. Walengwa wa chanjo za UVIKO -19 ni watu walio chini ya umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea ambao kimkoa ni 1,011,085 na hadi kufikia Agosti 31,2022 wateja wapatao 735,844 wamepata kinga kamili dhidi ya ugonjwa wa UVIKO – 19 ambao ni sawa na asilimia 73 na kufanya mkoa wetu kushika nafasi ya tano kitaifa”, ameeleza Mjema.

“Kwa upande wa dirisha la dawa kwa wazee, tuhakikishe wazee wanapata dawa, malalamiko yapungue, wazee wapate dawa”,amesema.

Mjema pia ameziagiza halmashauri za wilaya kuhakikisha zinatoa takwimu kwa wakati

“Nimeona kuna tatizo kubwa la Takwimu kwenye Halmashauri zetu, hili donda ndugu nataka liondoke, kwenye kutoa taarifa naona kuna tatizo,unakuta kazi imefanywa vizuri sana lakini changamoto inakuja kwenye takwimu”,amesema

“Mimi sitaki kuona tena tatizo la takwimu, takwimu zikihitajika nataka tuzipate haraka, hili tatizo la taarifa sitaki kulisikia, zikitakiwa mkoani lazima tuzipate, hii iwe mwisho. Haiwezekani Mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya , kamati ya usalama inahangaika kutafuta takwimu…. Wafichueni wanaokwamisha, ukijiona wewe ni Slow Learner tuambie tukusaidie.

“Nataka takwimu ziwe zinakuja kwa wakati na zinaenda kwa wakati, hatuhitaji kugombana kuhusu takwimu, Mhe, RAS Ondoa mtu anayekwamisha, hatutaki kurudishwa nyuma” ,amesema Mjema.

“Siyo kazi ya Mkuu wa Mkoa, Kamati ya Usalama, Mkuu wa Wilaya kwenda kuhangaika kutafuta takwimu.. Unapochelewesha takwimu unakwamisha mambo, RAS niondolee watu wanaokwamisha upatikanaji wa takwimu. Tunataka kila mmoja afanye kazi, hatutawavumilia wanaoturudisha nyuma, ni lazima tumsaidie Mhe. Rais Samia Suluhu ambaye anafanya jitihada kubwa za kuleta fedha kwa ajili ya maendeleo”,ameongeza Mjema

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza leo Ijumaa Septemba 2,2022 wakati akifungua kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha 2021/2022, Chanjo ya UVIKO - 19 na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza leo Ijumaa Septemba 2,2022 wakati akifungua kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha 2021/2022, Chanjo ya UVIKO - 19 na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha 2021/2022, Chanjo ya UVIKO - 19 na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akizungumza kwenye kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha 2021/2022, Chanjo ya UVIKO - 19 na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akiongoza kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha 2021/2022, Chanjo ya UVIKO - 19 na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza kwenye kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha 2021/2022, Chanjo ya UVIKO - 19 na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano.

Wadau wa afya wakiwa kwenye kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha 2021/2022, Chanjo ya UVIKO - 19 na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

RAIS SAMIA AZINDUA MAABARA YA SAYANSI SKULI YA KIZIMKAZI ILIYOJENGWA NA BENKI YA CRDB

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suhuhu Hassan (watatu kushoto) kwa pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Mohammed Musa (wapili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Maabara ya Sayansi katika Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi yenye thamani ya Sh. Milioni 50 iliyojengwa kwa msaada wa Benki ya CRDB  leo Agosti 02, 2022. Wengine pichani kutoka kulia ni Waziri wa Utumishi na Utawala bora Zanzibar, Haroun Ali Suleiman, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Sadala pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadid Rashid.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suhuhu Hassan kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakifungua kitambaa kwenye jiwe la msingi  kuashiria uzinduzi rasmi wa Maabara ya Sayansi katika Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi yenye thamani ya Sh. Milioni 50 iliyojengwa kwa msaada wa Benki ya CRDB  leo Agosti 02, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suhuhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Mohammed Musa (kulia), wakati wa uzinduzi rasmi wa Maabara ya Sayansi katika Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi yenye thamani ya Sh. Milioni 50 iliyojengwa kwa msaada wa Benki ya CRDB  leo Agosti 02, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suhuhu Hassan akifurahia burudani kutoka kwa wanafunzi wa Skuli ya maandalizi Kizimkazi wakati wa uzinduzi rasmi wa Maabara ya Sayansi katika Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi yenye thamani ya Sh. Milioni 50 iliyojengwa kwa msaada wa Benki ya CRDB  leo Agosti 02, 2022. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suhuhu Hassan akipata maelezo ya mradi wa maabara kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, wakati wa uzinduzi rasmi wa Maabara ya Sayansi katika Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi yenye thamani ya Sh. Milioni 50 iliyojengwa kwa msaada wa Benki ya CRDB  leo Agosti 02, 2022. 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger