Tuesday 17 May 2022

SERIKALI YAZITAKA TAASISI KUWAJENGEA UWEZO WAKAGUZI WA NDANI

Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Bw. Athumani Mwituka alipokuwa akizungumza kwenye warsha ya wakaguzi wa ndani iliyoandaliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa Ndani nchini (IIA), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uelewa wa Wakaguzi wa ndani duniani.
Baadhi ya washiriki kwenye warsha ya wakaguzi wa ndani iliyoandaliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa Ndani nchini (IIA), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uelewa wa Wakaguzi wa ndani duniani.
Viongozi wa Meza kuu kwenye warsha ya wakaguzi wa ndani iliyoandaliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa Ndani nchini (IIA), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uelewa wa Wakaguzi wa ndani duniani, iliyofanyika mkoani Tanga.

Mwandishi Wetu, Tanga

SERIKALI inategemea kuwa na Wakaguzi 300 wa Mifumo kote nchini katika sekta za Umma ifikapo Mwaka 2026 ili kuhakikisha inaweka udhibiti wa mapato kwenye shughuli zinazofanywa na taasisi zake mbalimbali.

Wakati huo huo imezitaka sekta binafsi kuhakikisha zinatambua umuhimu wa wakaguzi wa ndani na kuwajengea uwezo wakaguzi wao ili waweze kufanya ukaguzi wa mifumo kwa ufanishi, huku wakiwa na vyeti vinavyotambulika kimataifa.

Kauli hiyo, imetolewa juzi jijini Tanga na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Bw. Athumani Mwituka alipokuwa akizungumza kwenye warsha ya wakaguzi wa ndani iliyoandaliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa Ndani nchini (IIA), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uelewa wa Wakaguzi wa ndani duniani.

Katika warsha hiyo Serikali imeweka wazi mapungufu ambayo hung'amuliwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG na nini kifanyike ili kupunguza hoja za mashaka ndani ya taasisi zao, amewataka wakaguzi hao kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na miongozo ya kimataifa, hivyo wana kila sababu ya kuongeza ujuzi wao kwa manufaa ya taasisi na taifa kwa ujumla.

Alisema kwa kuanzia aupande wa Serikali imeanzisha mifumo mingi ya ukusanyaji mapato ambayo inachangia katika udhibiti matumizi mabaya na pia imechangia kurahisisha utendaji kazi wa shughuli zake.

" Upande wetu serikalini tumejipanga ifikapo Juni 2026 tuwe na wakaguzi wa mifumo kwa sekta za umma takribani 300. Tunatoa wito kwa sekta binafsi nao kuhakikisha inawajengea uwezo wakaguzi wao ili waweze kufanya ukaguzi wa mifumo kwa ufanishi, huku wakiwa na vyeti vinavyotambulika.

Serikali itaendelea kuongeza uwezo wa wakaguzi wa ndani ikiwemo kufanya ukaguzi wa miradi na tayari Waziri wa Fedha na Uchumi, ametoa maelekezo ya kuwa kila unapobuniwa mradi ndani ya taasisi zake itengwe fedha kwa ajili ya kufanikisha mkaguzi wa ndani kufanya ukaguzi wake.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya IIA, Bi. Zelia Njeza akizungumza alisema taasisi hiyo ya wakaguzi inaungana na wakaguzi wengine duniani kote kusherekea mwezi huu wa wakaguzi wa ndani, na umejipanga kusherehekea kitofauti zaidi kwa kuhakikisha tunawajengea uwezo wakaguzi wa ndani.

Alisema maadhimisho ya mwaka huu pamoja na kuwajengea uwezo wanachama wao, lakini wamelenga zaidi kujumuika na kusherekea mafanikio ya ukaguzi wao ndani ya taasisi wanazofanyia kazi.

Alisema bado kunachangamoto ya uelewa wa kazi za wakaguzi wa ndani katika jamii na changamoto hii ya uelewa haipo katika jamii ya Watanzania tu bali hata katika nchi zingine.

"...Kwa ujumla ukitofautisha na fani zingine kama udaktari, mtu yeyote ukimuuliza kuhusu daktari atakujibu ni nani...tumekubaliana mwezi huu wa tano uwe ni mwezi maalum kuweza kusherehekea mafanikio yoyote tuliyoyaleta kwa kutumia kazi zetu.

"...Na ni kipindi ambacho tunatumia fursa hii kuweza kuwaelimisha wadau wetu kuhusu umuhimu wa wakaguzi wa ndani na ni kitu gani wategemee kutokana na kazi zetu, kutoa elimu kwa wadau ni muhimu kwani kama hawatajua nini tunakifanya wanaweza wakawa na kigugumizi hata kuitaji huduma zetu," alisema.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 17,2022

Magazetini leo Jumanne May 17 2022

Share:

SIMBA SC YAKUTANA NA RUNGU KUTOKA CAF KWA KOSA LA KUWASHA MOTO UWANJANI

************************

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika (CAF) limeipiga faini ya dola za Kimarekani 10,000 (zaidi ya shilingi milioni 22.8) Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Ni baada ya kupatikana na hatia kuwasha moto katika uwanja wa Orlando katika mchezo dhidi ya Orlando Pirates.

Kabla ya mchezo huo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho,wachezaji wa Simba walionekana kukusanyika katikati ya uwanja na baadaye moshi kutokea katikati ya kundi hilo.

Taarifa kutoka CAF imesema, maafisa wa mchezo walionesha katika ripoti zao kwamba, wachezaji wa Simba waliwasha moto katikati ya uwanja wakati wakijifanya kuomba kabla ya mechi.

"Ilitubidi kumwaga maji ili kuuzima moto,”wameeleza huku wakibainisha kuwa, malipo hayo yanapaswa kufanyika ndani ya siku 60 kuanzia sasa.
Share:

Monday 16 May 2022

Tazama Picha : MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI MKOA WA SHINYANGA..RC MJEMA AWAPONGEZA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema amefungua Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga huku akiwapongeza waandishi wa habari mkoani humo kuendelea kufanya kazi kwa weledi mkubwa pamoja na kushirikiana na serikali.

Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani mkoani Shinyanga yamefanyika leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga.

“Sijawahi kupata tatizo na waandishi wa haabari wa mkoa wa Shinyanga, wanafanya kazi vizuri, wanafanya kazi kwa weledi. Nimeona wana uweledi, wana balance story, naomba tuendelee kushirikiana. Tunawashukuru waandishi wa habari kwa kuendelea kushirikiana na serikali, endeeleni kuripoti mambo mazuri yanayofanywa na serikali”,amesema Mjema.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akifungua Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga  leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga. Picha na Kadama Malunde & Marco Maduhu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akifungua Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga  leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru akisoma hotuba kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga  leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga  leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru akisoma hotuba kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga  leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru akisoma hotuba kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga  leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga
Wadau wa habari wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga  leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga

Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde akiwasilisha mada kuhusu Mitandao ya Kijamii na Uandishi wa Habari na Changamoto za Kidigiti kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga  leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga
Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde akiwasilisha mada kuhusu Mitandao ya Kijamii na Uandishi wa Habari na Changamoto za Kidigiti kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga  leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga 

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Mwanza, Edwin Soko akiwasilisha mada kuhusu Usalama Mtandaoni na umuhimu wa Klabu za waandishi wa habari na wadau katika maendeleo ya mikoa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga  leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga

Mkurugenzi wa Radio Faraja Padre Anatoly Salawa akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga  leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga
Katibu wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Ali Lityawi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga  leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga  leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga  leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga

Mjumbe wa kamati Tendaji SPC, Michael Mipawa akitoa neno la shukrani kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga  leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga
Mwandishi wa Habari Stephen Wang'anyi akiwashukuru wadau na waandishi wa habari waliomsaidia kipindi chote tangu alivyopata ajali ya pikipiki mwaka 2019 na sasa anaweza walau kutembea japo hawezi kufanya kazi yoyote leo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger