Thursday 5 May 2022

BAKWATA MWANZA YAWAKUTANISHA WANANDOA KONGAMANO LA 'USIKU WA RAHA'... KIVULINI YATAKA WAONGEZE MAHABA NYUMBANI

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa Mwanza limewakutanisha wanandoa kupitia kongamano maalum la 'Usiku wa Raha' lengo likiwa ni kuimarisha mahusiano miongoni mwa wanandoa.

Akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika Mwanza Hotel Mei 04, 2022, Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke alisema BAKWATA inalenga kuresha misingi ya ndoa kama ilivyokuwa zamani ambapo ndoa zilidumu jambo ambalo siku hizi imekuwa ni changamoto kubwa kwani ndoa zimekuwa na migogoro na huvunjika kwa muda mfupi na kusababisha hatari ya watoto kukosa malezi kutoka kwa wazazi.

Ili kudumisha misingi ya ndoa, Sheikh Kabeke aliwahimiza wanandoa kila mmoja kutimiza wajibu wake ambapo alitaja baadhi ya mambo muhimu ambayo mme na mke kila mmoja anapaswa kuyatimiza ili kulinda ndoa yake.


"Kwa mwanaume lazima awe na uwezo wa kumhudumia mke wake kwa kumlisha/ chakula, kumvisha, kumsikiliza mkewe na kukubali kufanya mashauriano naye inapotokea changamoto. Lakini pia mke anapaswa kuzingatia usafi wa mwili, mazingira kama vile chumba cha kulala na choo pamoja na kutumia vyema ulimi wake anapozungumza na mmewe kwa kuwa na matamshi yenye heshima kwa mmewe", alidokeza Sheikh Kabeke.


Hata hivyo Sheikh Kabeke aliwatahadharisha wanaume hususani waislamu ambao imani yao inawaruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja kwamba wanapaswa kuwa na uwezo wa kuwahudumia kwa usawa wake zao kwa chakula, mavazi na tendo la ndoa lakini pia kuwapa makazi kwani hairuhusiwi wote kukaa nyumba moja labda kama wamekubalina wenyewe huku akijiepusha kuwafitinisha.


Akitoa mada ya ndoa kwenye kongamano hilo la Usiku wa Raha kwa wanandoa, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally alisema :
"Wanandoa wengi wakiwa ndani hawataniani kama wanavyofanya wakiwa nje. Unakuta mwanaume anamtania mama ntilie lakini akirudi nyumbani ni mwendo wa kipolisi polisi, hiyo inapunguza mahaba ndani ya ndoa".


"Hivi lini umesema ahsante kwa mkeo ama mmeo kwa kukupa vyema tendo la ndoa? Ama lini umekuwa muwazi kwake na kumwambia leo umenibip? Lazima wanandoa wazungumze na kutaniana ili kuimarisha mahusiano yao huku kila mmoja akitimiza wajibu wake", Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally aliwahoji wanandoa kwenye kwenye kongamano hilo la Usiku wa Raha, na kuzua vicheko ukumbini.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
"Tumefanya kampeni Mkoa wa Mwanza ya kupeleka ujumbe wa malezi bora, tabia njema na misingi ya ndoa tukishirikiana na Shirika la KIVULINI chini ya Mkurugenzi wake Yassin Ally. Tumesaidia kurejesha misingi na maadili kwa wanandoa" alisema Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke.
"Wanandoa wengi wakiwa ndani hawataniani kama wanavyofanya wakiwa nje. Unakuta mwanaume anamtania mama ntilie lakini akirudi nyumbani ni mwendo wa kipolisi polisi, hiyo inapunguza mahaba ndani ya ndoa" alisema Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally wakati akitoa mada ya ndoa kwenye kongamano hilo la Usiku wa Raha kwa wanandoa.
"Hivi lini umesema ahsante kwa mkeo ama mmeo kwa kukupa vyema tendo la ndoa? Ama lini umekuwa muwazi kwake na kumwambia leo umenibip? Lazima wanandoa wazungumze na kutaniana ili kuimarisha mahusiano yao huku kila mmoja akitimiza wajibu wake" Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally aliwahoji wanandoa kwenye kwenye kongamano hilo la Usiku wa Raha, na kuzua vicheko ukumbini.
Wanandoa wakifuatilia kongamano la 'Usiku wa Raha' jijini Mwanza.
Share:

MISA-TANZANIA, TAMWA ZAANDAA MKUTANO WA WADAU WA HABARI ARUSHA


Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, akiongea katika mkutano na wadau wa habari Arusha Mei 5, 2022, ambao imeandaliwa na MISA-Tanzania na TAMWA kwa ufadhili wa International Media Support (IMS).
Mwenyekiti wa MISA-Tanzania, Salome Kitomari, akiongea katika mkutano na wadau wa habari na serikali jijini Arusha Mei 5, 2022, ambao umeandaliwa na MISA-Tanzania na TAMWA kwa ufadhili wa International Media Support (IMS)
Mwenyekiti wa TAMWA, Joyce Shebe, akiongea katika mkutano na wadau wa habari na serikali jijini Arusha Mei 5, 2022, ambao umeandaliwa na MISA-Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA kupitia ufadhili wa International Media Support (IMS)
(Kutoka kushoto) Meneja Programu wa International Media Support (IMS), Fausta Musokwa, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, Mkurugenzi wa Tanzania Media Fund, Dastan Kamanzi, wakishiriki kwenye mkutano na wadau wa habari na serikali jijini Arusha Mei 5, 2022, ambao umeandaliwa na MISA-Tanzania na TAMWA kwa ufadhili wa IMS
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wadau wa habari na serikali jijini Arusha Mei 5, 2022, wakifuatilia mada kutoka kwa wazungumzaji. Mkutano huo umeandaliwa na MISA-Tanzania na TAMWA kwa ufadhili wa International Media Support (IMS)
**


TAASISI ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Kusini (MISA-Tanzania) kwa kushirikiana na Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) imeandaa mkutano leo Mei 5, 2022, kati ya wadau wa vyombo vya habari na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Zaidi ya washiriki 50 kutoka taasisi mbalimbali za vyombo vya habari na sheria nchini Tanzania wanashiriki mkutano huo kwenye hoteli ya Four Points by Sheraton leo Alhamisi Mei 5,2022.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amemuwakilisha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, pamoja na timu yake amehudhuria mkutano huo wa siku moja uliofadhiliwa na taasisi ya International Media Support (IMS).

Wakifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa MISA-Tanzania, Salome Kitomari, na Mwenyekiti wa TAMWA, Joyce Shebe, wamesisitiza umuhimu wa mahusiano mazuri kati ya serikali na vyombo vya habari nchini.

Naye Msemaji Mkuu wa Serikali , Gerson Msigwa aliwataka waandishi kuheshimu maadili na kuepuka "tug-of-war" au mvutano na serikali.

Mkutano huu unakuja siku moja baada ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani iliyohudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan hapa jijini Arusha.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni Uandishi wa Habari na Changamoto za Kidijiti.

Mashauriano kati ya wadau wa vyombo vya habari na serikali ni sehemu ya kutafuta maridhiano ya kurekebisha sheria kadhaa kandamizi zinazoathiri uhuru wa vyombo vya habari nchini, ikiwemo  Sheria ya Huduma ya Habari, 2016.
Share:

UWT NJOMBE WATOA PONGEZI KWA UONGOZI WA CCM TAIFA KAULI YA RAIS SAMIA NYONGEZA YA MISHAHARA



MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Njombe Scolastika Kevela ameunga mkono hatua ya uongozi wa CCM Taifa kwa kuwapongeza wafanyakazi kwa tamko lao la kuunga mkono kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa kuhusu nyongeza ya mshahara.

Ametoa kauli hiyo wakati wa akiwatakia salamu za Idd wananchi wa Mkoa wa Njombe na watanzania wote ambapo alisisitiza kuwa kitendo kilichofanywa na Chama chake kupitia kwa Katibu Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka kinaonesha namna gani chama hicho kinazingatia masuala ya utu.

"CCM ni Chama cha watu na chenye kujali Utu, kitendo cha uongozi wa juu kuwapongeza wafanyakazi kwa kuunga mkono kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu suala la Ongezeko la mishahara kinastahili pongezi" amesema Mama Kevela

Awali chama hicho kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wake wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka iliwapongeza wafanyakazi hao chini ya Shirikisho la wafanyakazi(TUCTA) kwa tamko lao la kuunga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan juu ya nyongeza ya mshahara alilolitoa katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Mkoani Dodoma 1 Mei 2022.

"Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA amesema walikutana na Rais siku moja kabla ya sherehe za Mei Mosi na kukubaliana juu ya ajenda hiyo ambapo Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliwahakikishia kuwa serikali itapiga mahesabu na nyongeza hiyo itapatikana katika mwaka mpya wa fedha unaoanza mwezi wa Julai 2022" alisema Shaka kupitia taarifa yake.

Katika taarifa yao TUCTA pia imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa hatua hiyo lakini hatua yake ya kukubali wafanyakazi waliyofukuzwa kazi baada ya kukutwa na vyeti bandia walipwe stahiki zao, kitendo ambacho kimedhihirisha wazi namna Rais Samia Suluhu Hassan alivyokuwa muumini wa Haki, huruma na mapenzi mema kwa kila mtanzania.

Aidha akizungumzia hilo, Mwenyekiti huyo wa UWT Mkoa wa Njombe amesema Chama Cha Mapinduzi siku zote kimekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha maslahi ya wananchi wake na haki zao zinasimamiwa na kulindwa hatua iliyomfanya Rais Samia umuhimu wa waliokuwa watumishi hao kulipwa stahiki zao.

Shaka katika taarifa hizo alisistiza kuwa majibu hayo ya TUCTA kuwa ni sahihi kwa wanasiasa wasio na maslahi na wafanyakazi wala nchi yetu ambao wanaumizwa na mazuri yanayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na wao hupenda kubadili mazuri kuwa mabaya ili wajijengee umaarufu na ushawishi wa kisiasa kwa wananchi.

Katika kipindi cha miaka mitano (2020-2025) Chama Cha Mapinduzi kiliahidi kupitia ilani yake ya uchaguzi ibara ya 130 kuwa serikali itakazoziunda zitaendelea kuweka mazingira rafiki ya utendaji wa vyama vya wafanyakazi ili viendelee kuwa nguzo muhimu katika kujenga mahusiano mahala pa kazi na kuboresha masilahi na haki za wafanyakazi ikiwemo uboreshaji wa mishahara ya watumishi wa umma ili waweze kumudu gharama za Maisha kwa kuzingatia ukuaji wa uchumi wa Taifa na tija ya wafanyakazi.

Hivyo anachokifanya Rais Samia Suluhu Hassan siyo maneno bali ni vitendo ikiwa ni utekelezaji wa ilani, Chama Cha Mapinduzi kinampongeza sana kwa umakini wake katika kuitekeleza ilani kwa vitendo.
Share:

BENKI YA CRDB KUENDELEA KUTOA MIKOPO YA WAFANYAKAZI KWA RIBA YA CHINI


Wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ikiboresha maslahi ya wafanyakazi nchini pia kushusha tozo mbalimbali katika mishahara, Benki ya CRDB imepandisha kiasi cha mkopo wanachoweza kuchukua wafanyakazi pia kuongeza muda wa marejesho hadi kufikia miaka saba ili kufanikisha shughuli zao za kiuchumi.

Kwenye maadhimisho ya Mei Mosi mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema, benki itaendelea kutoa mikopo kwa wafanyakazi (personal loan) kwa riba ya chini ili kuwaongezea kiasi wanachoweza kukopa. Alisema benki imeshusha riba hiyo kutoka 16% hadi 12% hivyo kuongeza kiwango cha kukopa hadi Sh200 milioni kitakachorejeshwa mpaka kwa miaka saba.

“Maboresho haya ni sehemu ya mkakati wa Benki ya CRDB kusaidia jitihada za Serikali kuboresha maisha ya wafanyakazi nchini,” amesema Nsekela.

Maboresho mengine Nsekela amesema yamefanyika kwenye Salary Account ambayo ni akaunti maalaum kwa ajili ya wafanyakazi inawawezesha kupokea mshahara kwa urahisi. Akaunti hii imeunganishwa na huduma za kidijitali za SimBanking na Internet banking ili kumwezesha mfanyakazi kupata taarifa na kufanya miamala kwa urahisi kutoka mahali popote alipo ndani hata nje ya nchi.

“Huduma hizi zimekuwa mkombozi mkubwa kwa wafanyakazi hususani waliopo maeneo ambako hakuna matawi yetu kwani husaidia kupata huduma zote kiganjani ikiwamo huduma ya mkopo wa kidijitali wa Salary Advance ambao hivi karibuni kiwango cha kukopa kiliongezwa hadi Sh3 milioni,” amefafanua Nsekela.

Kwa kushirikiana na taasisi za Serikali, Nsekela amesema Benki ya CRDB imejipanga vyema kuhakikisha mipango ya wafanyakazi inakamilishwa kwa wakati kupitia mtandao wake mpana wa huduma.

Amesema Benki ya CRDB inaongoza katika hilo kwani inao mtandao mpana wa kutolea huduma ikiwa na matawi 268 na mawakala (CRDB Wakala) zaidi ya 20,000 waliosambaa kila kona ya nchi, kuanzia mjini mpaka vijijini hivyo kuwawezesha wafanyakazi kupata huduma katika maeneo yao ya kazi hali inayowasiaidia kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za benki.

Kwa wateja wanaopata matatizo ya kifamilia, Nsekela amesema Benki ya CRDB inayo Kava Assurance, huduma ya bima ya maisha ambayo imeunganishwa na akaunti ya mteja inayomwezesha kupata mkono wa pole kuanzia Sh2 milioni hadi Sh15 milioni pindi mwenza wake anapofariki au kuwafariji warithi wake yeye mwenyewe akifariki.

Benki ya CRDB kwakushirikiana na Serikali ya mkoa wa Dodoma chini ya Mkuu wa Mkoa ilifanikisha sherehe hizo kwa kuwa mzamini mkuu ikitekeleza kauli mbiu yake ya Tupo Tayari, kufanya kazi Bega kwa Bega na Serikali katika kufanikisha maendeleo ya Taifa letu.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akifurahi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela mara baada ya kumalizika kwa sherehe za Mei Mosi zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri-Dodoma.


Tawi linalo tembea(Mobile Branch) likipita mbele ya Mgeni Rasmi katika kusindikiza maadamano ya wafanyakazi.
Share:

Wednesday 4 May 2022

SERIKALI YAVIKUMBUKA VITUO VYA WALIMU 'TRC' KWA KUBORESHA MIUNDOMBINU NA KUVIPA VITENDEA KAZI

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Seleman Msumi akikabidhi vitendea kazi hivyo kwa waratibu elimu


Rose Jackson,Arusha

Serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Rais Samia Suluhu, kupitia Wizara ya Elimu, imevikumbuka vituo vya walimu 'Teacher's Resources Center (TRC)', kwa kuanza kuboresha miundombinu na kuvipa vitendea kazi.

Wizara hiyo ya Elimu, imetoa seti tano za mashine za kudurufia karatasi kwa vituo vitano vya walimu, halmashauri ya Arusha, lengo likiwa ni kuviwezesha vituo hivyo, kuanza kufanya kazi upya, kwa ajili ya kuwaendleeza walimu kitaaluma wawapo kazini.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mashine hizo, mkurugenzi Mtendaji, halmasahuri ya Arusha, Seleman Msumi, amethibitisha kupokea seti tano za mashine na wino, kutoka Wizara ya Elimu, kwa ajili ya kutumiwa na vituo vitano vya TRC vya halmashauri hiyo.

Mkurugenzi Msumi, amesema serikali katika kuboresha sekta ya elimu, inajikita pia katika kuboresha mazingira bora kwa kuwapa walimu fursa ya kupata mafunzo kazini, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo katika stadi za ujifunzaji na ufundishaji unaoendana na mabadiliko ya kiteknolojia.

"Kazi ya kufundisha inatakiwa kujifunza mara kwa mara, serikali kupitia vituo vya TRC, imeona umuhimu wa kuvihuisha vituo hivyo, ili walimu waweze kupata mafunzo kazini wakati wote, hivyo niwatake walimu kutumia fursa hiyo adhimu kwa kujinoa kitaaluma, pamoja na kubadilishana uzoefu wa mbinu za ufundishaji na ujifunzaji, unaoendana na wakati na mabadiliko ya kiteknolojia", amesisitiza Mkurugenzi Msumi.

Naye Kaimu Afisa Elimu Msingi, Ruth Sumari, amefafanua kuwa, lengo la serikali kutoa vifaa kwenye vituo vya TRC, ni kuhakikisha walimu wanapata elimu wakiwa kazini, inayowajengea uwezo wa kuendeleza mbinu mbalimbali za ufundishaji ili kuwasaidia wanafunzi kujifunza stadi tatu za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu, maarufu kama KK tatu.

Amefafanua kuwa, halmashauri ina jumla ya vituo vitano vya TRC, na kuvitaja vituo hivyo ni pamoja na Kiutu, Mlangarini, Mateves, Oloirien na Lengijave, vituo ambavyo vitahudumia shule zote 132 za serikali za msingi na sekondari za halmashauri.

Hata hivyo, Wasimamizi wa vituo hivyo vya TRC, halmashuri ya Arusha, licha ya kuishukuru na kuipongeza serikali ya awamu ya sita, kwa kuvihuisha vituo vya TRC, wameweka wazi kuwa vituo hivyo ni muhimu kwa walimu kwa kuwa vinawapa fursa ya kupata mafunzo, mafunzo ambayo yanawezesha walimu kujifunza na kufundisha, kunako endana na wakati, na kuahidi kutumia vituo hivyo kwa maendeleo ya walimu na kupandisha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi.

Msimamizi wa TRC Kiutu, na Mratibu wa Elimu kata ya Kiutu, Mwalimu Evaline Mosha, amesema kuwa, TRC ni muhimu sana kwa walimu, kwa kuwa ni kituo kinachowakutanisha walimu kujiendeleza kitaaluma, kwa kujifunza moduli mbalimbali za ualimu zinatolewa na wizara, pamoja na kubadilishana uzoefu katika nyanja za ufundishaji na ujifunzaji wawapo kazini.
Share:

APELEKWA MOCHWARI AKIWA HAI..MADAKTARI WAFUKUZWA KAZI


Mwili wa mtu aliyedhaniwa kufariki na kupelekwa Mochwari ukirudishwa baada ya kugundulika kuwa yupo hai
 **

RAIA mmoja katika Jiji la Shanghai nchini China amepelekwa mochwari kwa bahati mbaya akidhaniwa ni maiti kumbe bado yupo hai.


Katika Jiji ambalo limeshmbuliwa na tatizo kubwa la Uviko -19, limetokea tukio hilo la kustua ambapo mwili wa mzee mmoja mkazi wa jiji la Shaghai uliwekwa katika begi maalum la kuhifadhia maiti na kupelekwa mochwari ambapo mhudumu wa Mochwari aligundua kuwa mtu alikuwa hajafa.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Utangazaji la CNN ni kwamba picha za video za tukio hilo zilichukuliwa na Jirani ambaye alikuwa ghorofani huku akipaza sauti akisema manesi wanamchukua mtu aliyehai na kumpeleka mochwari.

Madaktari wa zamu wakifuatilia sakata la mtu ambaye alipelekwa mochwari akiwa hai

Serikali ya Shanghai tayari imechukua hatua kuhusu tukio hilo ambapo kwanza imethibitisha kuwa hali ya mtu hiyo kwa sasa imeimarika lakini tayari imemnyang’anya Cheti Daktari aliyehusika katika Sakata hilo ambaye pia yupo chini ya uchunguzi, Maafisa watatu wa afya wameshaondolewa katika nafasi zao lakini pia Mkuu wa Idara ya Uuguzi naye ameondolewa katika nafasi yake.


Tayari kumekuwa na mtazamo mbalimbali kutoka kwa wananchi wa China na wengi wao wameonesha kukerwa huku wakiishutumu Serikali kutokuwa makini na Maisha ya raia hasa wa Jiji la Shanghai ambako mamilioni ya wakazi wamepigwa Lock Down.


Kupitia mtandao maarufu wa kijamii unaofanana na Twitter huko nchini China wa Weibo mmoja wa raia wa Shanghai amesema:

Gari la wagonjwa ambalo limebeba mwili wa mtu aliyedhaniwa kufariki

“Hili linaonekana kama tukio la mauaji ya kudhamiria.”


Nchi ya China hasa katika Jiji la Shanghai inakabiliwa na tatizo kubwa sana la Uviko-19 kiasi kwamba kume kuwa na Lock Down ambayo imeathiri mamilioni ya wtu katika Jiji hilo.
Share:

JAMII YAKUMBUSHWA KUWAJALI WATU WENYE ULEMAVU


Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda (katikati) akizungumza na wanafunzi pamoja na viongozi mbalimbali wa Chuo cha Ufundi Stadi kwa watu wenye ulemavu Yombo kilichopo Dar es Salaam alipotembelea chuo hicho akiambatana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Adam Katundu (hayupo pichani), kwa lengo la kujumuika na wanafunzi wa chuo hicho katika kusherekea Sikukuu ya Eid El-fitr.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Adam Katundu, (aliyesimama) akizungumza na wanafunzi pamoja na viongozi mbalimbali wa Chuo cha Ufundi cha watu wenye ulemavu Yombo alipotembelea chuo hicho akiambatana na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda (katikati). Wakwanza kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Bi Mariam Chelangwa.


Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi cha Watu Wenye Ulemavu Yombo, Bi Mariam Chelangwa (wakwanza kulia), akifanya utambulisho wa wanafunzi na viongozi mbalimbali wa chuo hicho wakati Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Adam Katundu, (hayupo pichani) pamoja na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda (katikati) walipotembelea chuo hicho kwa lengo la kujumuika na jamii ya wanafunzi na watumishi wa chuo hicho katika kusherekea sikukuu ya eid el-fitr


Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda (wakwanza kulia), akishiriki katika zoezi la kugawa chakula kwa wanafunzi wa Chuo cha Ufundi cha Watu Wenye Ulemavu Yombo alipotembelea chuo hicho akiambatana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Jamal Adam Katundu (hayupo pichani) kwa lengo la kusherehekea sikukuu ya Idd El Fitr pamoja na wanafunzi na watumishi wa chuo hicho.


Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi kwa Watu Wenye Ulemavu Yombo wakiwasikiliza viongozi mbalimbali wakati wa ziara ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Adam Katundu pamoja na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda katika chuo chicho.

**************************

Na Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Jamal Katundu, ametoa wito kwa jamii kuwakumbuka na kuwajali watu wenye ulemavu ambapo amesema kundi hilo lina nafasi muhimu katika kuleta maendeleo ya Taifa.

Ametoa wito huo, aliposhiriki chakula cha mchana na jamii ya wanafunzi na watumishi wa Chuo cha Ufundi Stadi kwa watu wenye ulemavu Yombo cha jijini Dar es Salaam katika kusherekea sikukuu ya Idd el Fitr.

“Nitoe wito kwa jamii kwa ujumla kutenga muda wao kwa ajili kujumuika na watu wenye ulemavu ili kuendelea kuwapa faraja na kuwatia moyo wa kuendelea kujituma na kutoa mchango wao katika ujenzi wa Taifa letu kwa kadri inavyowezekana,” amesema Prof. Katundu na kuongeza:

“Kwa upande wetu sisi kama serikali tunaendelea kutimiza wajibu wetu wa kuwahudumia Watanzania wote bila kujali hali zao na ndio maana leo tumeona ni vema kujumuika na vijana wetu wenye ulemavu ambao wanapatiwa mafunzo katika chuo hiki ambacho ni miongoni mwa vyuo vyetu vilivyopo katika kanda mbali mbali kwa ajili ya kuwalea na kuwapa ujuzi vijana wenye ulemavu wa aina tofauti ikiwemo uziwi, ulemavu wa ngozi, ulemavu wa viungo nakadhalika.”

Aidha, Katibu Mkuu huyo amesema serikali imeanza kufanya maboresho ya miundombinu katika vyuo vya ufundi vya watu wenye ulemavu nchini ili kuliwezesha kundi hilo maalum kupata ujuzi muhimu utakaoliwezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli mbali mbali za uzalishaji mali.

“Nadhani mmeshaliona lile gari kubwa ambalo limekuwa likija hapa chuoni, mnajua linaleta nini?” Aliwauliza wanafunzi wa chuo hicho ambao waliitikia “maru maru”.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu, Prof. Jamal Katundu na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Bi. Mariam Chelangwa, serikali imetenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu mbali mbali yakiwemo mabweni na vyumba vya madarasa katika chuo hicho na vingine vilivyopo Singida, Tabora, Mwanza, Tanga na Mtwara ambapo tayari baadhi ya vifaa vya ujenzi vimeshaanza kufikishwa katika vyuo husika.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu huyo ameambatana na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda, ambaye amesema lengo la kuandaa na kushiriki chakula cha pamoja na jamii hiyo ya wanafunzi na watumishi wa chuo ni kuendelea kutoa faraja kwa kundi hilo muhimu katika jamii ambalo mara nyingi limekuwa likisahaulika.

“Tumekuja hapa kwasababu tunatambua kuwa watu wenye ulemavu ni sehemu ya jamii lakini kwa muda mrefu watoto hawa wanakuwa pekee yao pamoja na walezi wao tu hivyo wanatuhitaji sana kwa ajili ya kuendelea kuwatia moyo na kuwafariji. Hivyo, sisi kama Ofisi ya Waziri Mkuu tumeona leo tuje tujumuike nao kwa kula pamoja, kuongea na kucheza nao kama namna ya kuendelea kuwapa faraja na kuwahamasisha kuendelea kujibidiisha katika masomo yao. Na si hivyo tu, kuja kwetu hapa kunatuwezesha kufahamu changamoto zao na kupata mrejesho zaidi wa maendeleo ya vyuo vyetu,” amesema Mtendaji Mkuu wa OSHA.

Kwa upande wao, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Mariam Chelangwa na mmoja wa wakufunzi wa chuo hicho, Bw. Aloyce Nkuna, wamewashukuru viongozi waliowatembelea na serikali kwa ujumla kwa jitahada mbali mbali zinazochukuliwa katika kuwezesha chuo kuendelea kutekeleza wajibu wake kikamilifu.

Aidha, baadhi ya wanachuo wakiwemo Joseph Baraza na Asia Bashiri wametoa shukrani zao za dhati kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuendelea kuwakumbuka ambapo viongozi wa Ofisi hiyo wamekuwa wakiwatembelea na kujumuika nao mara kwa mara.

“Tunawashukuru wageni wetu wote mliotutembelea katika siku hii ya leo, tumefurahi, tumekula pamoja nanyi katika sikukuu hii ya Idd El Fitr na tuwaombea kwa Mungu azidi kuwabariki,” amesema Joseph Baraza, Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Yombo.

Chuo cha Ufundi Stadi Yombo cha watu wenye ulemavu ambacho kipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kilianzishwa mwaka 1973 kwa malengo ya kutoa mafunzo ya ufundi kwa vijana wenye ulemavu nchini. Chuo kinatoa kozi mbali mbali za ufundi zikiwemo; Ufundi Umeme, Uwashi, Ushonaji, Uchomeleaji Vyuma pamoja na Kilimo na Ufugaji.
Share:

SERIKALI YATANGAZA BEI MPYA ZA MAFUTA YA PETROLI NA DIZELI...SOMA HAPA


 
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na EWURA, bei hizi zitaanza kutumika kuanzia leo Mei 4, 2022. Pamoja na kutambua bei hizo, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:-


(a) Bei za rejareja za petroli ni Shilingi 3,148 kwa lita kwa Dar es Salaam, Shilingi 3,161 kwa lita kwa Tanga na Shilingi 3,177 kwa lita kwa Mtwara;


(b) Bei za rejareja za dizeli ni Shilingi 3,258 kwa lita kwa Dar es Salaam, Shilingi 3,264 kwa lita kwa Tanga na Shilingi 3,309 kwa lita kwa Mtwara;


(c) Bei za rejareja za mafuta ya taa ni Shilingi 3,112 kwa lita kwa Dar es Salaam na bei za bidhaa hiyo kwa mikoa yote nchini zimekokotolewa kulingana na gharama za kupokelea mafuta hayo kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka miji husika.


(d) Mabadiliko ya bei yanatokana na ongezeko la bei za mafuta katika soko la dunia zinazochangia takribani asilimia 93 ya ongezeko la bei hizo na gharama za uagizaji (premium) ambazo zinachangia takribani asilimia 4. Vilevile, bei za mafuta hapa nchini zina uwiano na bei za bidhaa hizo katika nchi jirani.


(e) EWURA inapenda kuukumbusha umma kwamba bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana pia kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo. Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.


(f) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi
stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.


(g) Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani mradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo (Price cap) au kushuka chini ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama ilivyokokotolewa kwa kutumia fomula na Kanuni za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2022 zilizotangazwa kupitia Magazeti ya Serikali Na. 2A na 57 ya tarehe 3 Januari 2022 na 28 Januari 2022, sawia.


(h) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.


Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani.


Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.


(i) Wauzaji wa mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa risiti za mauzo kutoka kwenye mashine za EFPP (Electronic Fiscal Pump Printers) na Wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita.


Stakabadhi hizo za malipo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya aidha kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora kinachofaa, na pia, risiti hizo zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mauzo ya mafuta ya petroli.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 4,2022


Magazetini leo Jumatano May 04,2022


Share:

Tuesday 3 May 2022

RAIS SAMIA ASHIRIKI SWALA YA EID EL FITRI KATIKA MSIKITI MKUU WA BAKWATA KINONDONI DAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa anatoka katika Msikiti Mkuu wa BAKWATA uliopo Kinondoni Muslim mara baada ya kushiriki Swala ya Eid El Fitri pamoja na Waumini wengine wa dini ya Kiislamu Jijini Dar es Salaam tarehe 3 Mei, 2022.


Waumini wa dini ya Kiislamu wakishiriki Swala ya Eid El Fitri iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa BAKWATA Kinondoni Muslim Jijini Dar es Salaam tarehe 3 Mei, 2022.

Share:

Video Mpya : GUDE GUDE - SHULE

Hii hapa video Mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Gude Gude inaitwa Shule
Share:

Video Mpya : GUDE GUDE - TINGINAGA NSI

Msanii wa nyimbo za asili maarufu Gude Gude kutoka Segese Kahama ameachia wimbo mpya unaitwa Tinginaga Nsi..
Share:

Video Mpya : BHULEMELA - SHIKOLO

Hii hapa video mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Bhulemela inaitwa Shikolo
Share:

Video Mpya : BAHATI BUGALAMA - TAMADUNI

Msanii wa nyimbo za asili Bahati Bugalama anakualika kutazama video yake mpya inaitwa Tamaduni
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger