Saturday 15 January 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 16,2022

 


Dkt.Shoo:Huyu ndiye Spika anayehitajika




Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo January 15



Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JANUARI 15,2022

Magazetini leo Jumamosi January 15 2022









Share:

Friday 14 January 2022

TBS YASHIRIKI TAMASHA LA NANE LA BIASHARA VISIWANI ZANZIBAR, YATOA ELIMU YA VIWANGO

Afisa Masoko TBS Bi. Rhoda Mayugu akitoa elimu ya viwango kwa mjasiriamali aliyeshiriki katika wa Tamasha la 8 la Biashara liliofanyika visiwani Zanzibar

Afisa Masoko TBS Bi. Rhoda Mayugu akitoa elimu ya viwango kwa wanafunzi waliotembelea Banda la TBS na ZBS wakati wa Tamasha la 8 la Biashara liliofanyika visiwani Zanzibar.

********************

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu ya Viwango kwa wazalishaji, wasamabazaji waagizaji wa bidhaa nje ya nchi na Wafanyabishara visiwani Zanzibar .

Elimu hii imetolewa wakati wa Tamasha la 8 la Biashara Zazinbar lililofanyika kuanzia tarehe 2/1/2022 hadi 15/1/2022.

Akizungumza wakati wa Tamasha hilo Afisa Masoko (TBS) Bi Rhoda Mayugu amesema shirika limetumia Tamasha hili kutoa elimu kuhusu majukumu yake ikiwa ni uthibitishaji wa bidhaa na mifumo, usajili na majengo na bidhaa za chakula na vipodozi, upimaji, uandaaji wa viwango na udhibiti wa bidhaa kwa bidhaa zinanotoka nje ya nchi.

“TBS ni shirika lililopewa dhamana ya kusimamia ubora wa bidhaa zinazozalishwa nchini na zile zinatoka nje ya nchi hiyo basi wazalizaji, wasambazaji, waagizaji wa bidhaa nje ya nchi na wafanyabiashara wanatakiwa kuhakikisha bidhaa wazaozalisha na zile zinazotoka nje ya nchi zimethibishwa na kukidhi matakwa ya viwango kabla ya kuingizwa sokoni” alisema Mayugu

Aliongeza kuwa wananchi kama watumiaji wa bidhaa wao wananafasi kubwa ya kufanya katika kuhakikisha bidhaa zilipo sokoni zimekidhi matakwa ya Viwango kwani wao ndio wanofanya maamuzi ya kununua au kutokununua bidhaa

“Wananchi kama watumiaji wa mwisho wa bidhaa ndio waathirika wakubwa wa bidhaa hafifu na endapo watajenga utamaduni wa kununua bidhaa zile tu ambazo zimethibitishwa ubora wake taratibu lakini kwa hakika soko la Tanzania litajazwa na bidhaa zilizokidhi matakwa ya viwango tu na kwa pamoja kama Taifa tutakuwa tumeishinda vita ya bidhaa hafifu.

Jukumu la kuhakikisha Tanzania inakuwa na bidhaa zilizokidhi matakwa ya Viwango si la TBS pekee yake bali ni jukumu la kila Mtanzania kuanzia mzalishaji wa bidhaa, muagizaji wa bidhaa nje ya nchi,msambazaji wa bidhaa, muuzaji wa bidhaa na mtumiaji wa bidhaa. Hiyo basi tukiamua kwa pamoja tutajenga Taifa salama na kukuza uchumi wa nchi kwani bidhaa zetu zitakubalika katika masoko ya kitaifa na kimataifa. Alisisitiza Bi Mayugu

Share:

MTANGAZAJI MASHUHURI ZUHURA YUNUS ATANGAZA KUONDOKA BBC SWAHILI




MTANGAZAJI mashuhuri wa BBC Zuhura Yunus anaondoka kutoka shirika hilo baada ya kulitumikia kwa takriban miaka 14.

Zuhura atatangaza kipindi chake cha mwisho cha Dira ya Dunia leo Januari 14, 2022 majira ya saa tatu Afrika mashariki. Hata hivyo taarifa kutoka shirika hilo imeabinisha kuwa Zuhura amebakiza siku kadhaa za likizo kabla ya kuondoka rasmi.

Mtangazaji huyo aliyejiunga na BBC Swahili mwaka 2008 amesema anataka kuutumia muda wake sasa kuendelea na uandishi na mambo mengine nje ya BBC.


Taarifa ya Zuhura kuondoka BBC inakuja miezi kadhaa baada ya kuandika kitabu chake cha wasifu wa Biubwa Amour Zahor mwanaharakati mwanamke wa kisiasa wakati wa mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.


Zuhura alianza kama mtangazaji wa redio na mzalishaji wa vipindi mwaka 2008. Mwaka 2014 alihamia Swahili TV na akawa mwanamke wa kwanza kutangaza Dira ya Dunia TV.
Share:

GGML KUANZA KUTUMIA RASMI UMEME WA TANESCO MWISHONI MWA 2022

Shughuli za uchimbaji zikiendelea ndani ya Mgodini wa GGML
***


 

NA MWANDISHI WETU

 

MKUU wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule amesema mpango wa kuunganisha umeme wa gridi ya taifa kuelekea katika mgodi wa Geita Gold Mine Limited (GGML) unaendelea ambapo ujenzi wa laini maalumu za kwenda mgodini zimekamilika kwa asilimia 90. 

 

Hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa kituo kubwa cha kupoozea umeme cha Mpomvu kilichopo Mjini Geita ambapo kinauwezo wa Megawatt 90.

 

Mkuu huyo wa mkoa ametoa kauli hiyo jana mjini Geita kutokana na taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limeshindwa kupeleka umeme unaohitajika na mwekezaji Geita Gold Mine.

 

Akifafanua zaidi Senyamule alisema kwa upande wa Mgodi (GGML) wanaendelea na hatua za ujenzi wa kituo cha kupooza umeme cha msongo wa Kilovolt 33 kuwa Kilovolt 11 ndani ya mgodi wa GGML chenye uwezo wa Megawatt 40. 

 

“GGML wanatumia voltage level tofauti na inayosambazwa na TANESCO hivyo tunategemea shughuli zote mpaka December 2022 zitakamilika,” alisema.

 

Mgodi wa GGML unatumia zaidi ya MW 40 zinazozalishwa kwa kutumia jenereta zinazotumia mafuta ya dizeli tangu mwaka 2018.

 

Hata hivyo, katika mipango ya TANESCO imekuwa ikitekeleza mradi huo wa Mpovu kuhakikisha inapeleke umeme wa zaidi ya MW 20 katika mgodi huo.

 

Kituo hicho cha Mpomvu chenye eneo lenye ukubwa wa takribani heka tano kitapokea umeme wa Msongo wa Kilovolt 220 na kutoa Kilovolt 33 kisha kuvinufaisha vijiji 11 vitakavyopitiwa na mradi na wakazi 1,424 walio jirani. 

 

Mikoa jirani kama Mwanza na Kagera itaweza kunufaika na umeme huu kwani ni wa kutosha.

 

Mradi huo mkubwa wa umegharimu zaidi ya Sh bilioni 50 ili kuwezesha wananchi wa Mkoa wa Geita na maeneo ya jirani kupata umeme wa uhakika na gharama nafuu.

 

Aidha, mkuu huyo wa mkoa aliongeza kuwa, kukamilika kwa kituo cha kupooza umeme cha Geita kitawezesha Mkoa wa Geita kuwa na umeme wa uhakika utakaowezesha uwekezaji katika sekta mbali mbali hususan  uchimbaji wa Madini na Viwanda.

 

Kwa upande wake, Kampuni ya GGML imethibitisha kuwa utaratibu wa mananuzi ya mitambo ya kupoozea umeme yaani transformers uko katika hatua ya manunuzi na ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kukamilika kufika November 2022.

 

Makamu Rais wa Kampuni hiyo, Simon Shayo amesema GGML imekamilisha majadiliano na kuandaa rasimu ya mkataba wa kuuziana umeme (power selling agreement) na TANESCO ili kuhakikisha kampuni hiyo inapata umeme wa uhakika na kwa ubora unaotarajiwa ili kuepuka kuathiri shughuli za uzalishaji kwa Kampuni.


Shughuli za uchimbaji zikiendelea ndani ya Mgodini wa GGML
Share:

“WEWE NI WANGU MILELE” ...NILISIKIA AKINONG’ONEZA

 “Umdhaniaye ndiye siye” kwa miaka nane nimekuwa kwenye ndoa na mpenzi wangu niliyempenda kama chanda na pete.

 Sikujua siku moja angefanya alichokifanya, kweli asante ya punda ni mateke. Naishi katika mtaa wa Embakasi jijini Nairobi, hapo awali nilikuwa naishi pamoja na familia yangu kule Kakamega magharibi mwa Keny. Kwa kuwa nilikuwa nafanya kazi kule Magharibi, kwa kawaida kwa shughuli za kikazi, niliweza kupata uhamisho wa pahala pa kazi kuenda kuifanya kazi hiyo mjini Nairobi.

 Kwa kuwa sikuwa na hela za kutosha niliamua kuiacha familia yangu mashambani kuenda kwa shughuli za utaftaji wa kila siku, niliamua kufanya hivyo kwa huwa sikuwa na hela za kutosha kuweza kukimu mahitaji yetu yote mjini. 

Hivyo nikaamua wasalie nyumbani, mara kwa mara nilipopata nafasi niliwatembelea na kuwajulia hali na kurudi mjini baada ya siku mbili tatu hivi. Kando na hayo mara kwa mara ningeweza kumpigia mke wangu simu na kuzungumza naye kwa kuwa nilimpenda sana na nilitamani kuwa karibu naye mara kwa mara ila shughuli za kikazi hazikuniruhusu.

 Kwa upande mungine muke wangu naye hakuachwa nyuma, mara kwa mara angenitumia jumbe za mapenzi kwenye simu yangu na kunieleza jinsi anavyonipenda sana, nikikumbuka yalivyokuwa mapenzi yetu kabla ya yaliotokea kutokea naeza sema yalikua mapenzi yasikuwa na kifani.

 Jambo hilo lilinifanya mwenye furaha kila wakati na hivyo nilitia bidii kazini kuweza kumtimizia chochote alichohitaji kwa kuwa nilimuahidi kuwa ningemuweka vyema na furaha kila wakati, baada ya mwaka moja hivi mambo yalianza kubadilika, mapenzi aliyokuwa ananionesha mke wangu Sarah yalibadilika, ujumbe na simu alizokuwa akinipigia mara kwa mara zilisitishwa.

 Nilipompigia simu hakuzichukua zote, zingine zilienda bila kujibiwa kwa vyovyote vile, jambo hilo lilinipa kiwewe, na kushidwa nini mke wangu alikuwa anakifikiria kila wakati , nilishuku kulikuwa na kitu fiche. Kwa bahati nzuri niliweza kupata mapumziko ya wiki moja kazini, hivyo nikafunga safari ya kwenda nyumbani bila ya kumfahamisha mke wangu.

Nilipofika kwangu nilipata lango kuu limefungwa, nilimpigia simu haukuchutua hata! Alivyozoea , hivyo nikapenyeza kwenye ua na kuingia kwa boma langu bila yeyeto kugundua, niliubisha mlango mara kadhaa, lakini haukufunguliwa, nilishikwa na hofu kwa kudhani mke wangu alikua ameaga kumbe sivyo, niliposonga kwenye dirisha la chumba chetu cha kulala, nilisikia watu wakinong’onezana, Niliiskia sauti ya mwanaume mle chumbani na kushtuka nini kilichokuwa kinaendelea, Niliupiga mlango teke na kuingia chumbani mle ghafla nilimpata mwanaume akiwa chumbani mwangu nisijue nini alichokuwa anafanya chumbani mle, ghafla mume huyo alijihami kwa kisu na kutishia kuniua, nilipoenda kumpiga mke wangu nilimpata ametoweka kwa kutumia mlango wa nyuma, nilibaki wenye mafikira tele nisijue la kufanya.

 Kwa bahati nzuri nilipiga akili ya kuweza kupata usaidizi kutoka kwa “Kiwanga doctors” waliokuwa wamenisaidia hapo awali, nilimpigia daktari huyo simu na kumweleza kilichotokea, aliahidi kuyashughulikia kwa haraka, siku tatu baaadaye, mke wangu alirejea nyumbani na kupiga magootii na kuomba msamaha kwa aliyoyatenda, Mume huyo vile vile alinipigia simu na kuniomba msamaha , kwa uchungu aliniambia mrija wake ulikuwa umefura na angeomba urudi salama, nilimsamehe na kumpigia daktari kiwanga kumwarifu aurudishe salama, namshukuru daktari kiwanga kwa kulinda penzi langu na mke wangu.

 Pia Dkt. Kiwanga anatibu magonjwa kama Kifua kikuu, kifafa na mengine mengi kwa upande mungine anatatua mizozo ya familia, ndoa na pia kulinda mali katika boma lako. Kwa mengi tembelea wavuti www.kiwangadoctors.com ama waweza kutuma barua pepe kwa kiwangadoctors@gmail.com. Pia waweza kumpigia simu/WhatsApp kwa nambari +254769404965.
Share:

Video Mpya : AGGY BABY Ft STOMPION - KAMNYWESO


Aggy Baby
Malkia kwenye muziki wa Bongo fleva Agness Suleiman maarufu Aggy Baby anakualika kutazama video ya wimbo wake mpya wa Kamnyweso aliomshirikisha msanii Stompion.
.
Tazama video hapa chini, usisahau ku Share ,comment , like & Subscribe
Share:

WAZIRI BASHUNGWA AZINDUA KALENDA ZA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU YA AWALI, MSINGI, SEKONDARI NA MAFUNZO JIJINI DODOMA


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda hafla iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu anayeshughulika Elimu OR-TAMISEMI, Gerald Mweli ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda hafla iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.


Katibu wa TSC Bi.Paulina Nkwama,akielezea malengo ya mkutano wakati wa uzinduzi wa kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda hafla iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.


Muwakilishi wa Kamishna wa Elimu Bw.Venance Manoni,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda hafla iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.


Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.


Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Alhaji Abdul Maulid akitoa neno la shukrani kwa niba ya washiriki kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa (hayupo pichani) mara baada ya kuzindua kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.



WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa,akizindua kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda.Wengine Pichani ni Katibu Mkuu TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe (wa pili Kulia),Naibu Katibu Mkuu anayeshughulika Elimu OR-TAMISEMI, Gerald Mweli (Kushoto).Muwakilishi wa Kamishna wa Elimu Venance Manoni (wa Kwanza Kulia) hafla ya uzinduzi huo umefanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa akisoma maandishi baada ya kuzindua kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda hafla iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa akiwa katika picha mbalimbali za pamoja na washiriki mara baada ya kuzindua kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.

.......................................................................

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa ametoa maelekezo saba kwa viongozi wa Mikoa na Halmashauri ikiwemo kuhakikisha hakuna mwanafunzi wa elimu ya awali, darasa la kwanza au kidato cha kwanza anayetozwa mchango wowote kama sharti la mwanafunzi kuandikishwa.

Maagizo hayo ameyatoa leo Januari 14,2022 Jijini Dodoma wakati akifungua Mafunzo kwa Maafisa Elimu Mikoa, Maafisa Taaluma Mikoa na wathibiti ubora wa shule kanda pamoja na kuzindua kalenda za utekelezaji wa Mitaala ya elimu ya Awali,Msingi na Sekondari.

Waziri Bashungwa amesema wakati shule za msingi na sekondari zinatarajiwa kufunguliwa tarehe 17 Januari, 2022, kumeanza kutokea malalamiko toka kwa wananchi, kuhusu kutozwa michango mbalimbali, bila kufuata utaratibu.

“Wanafunzi kupelekwa kuandikishwa shule, na kisha kuambiwa shule zimejaa, au wazazi kuwapeleka shule wanafunzi, na kukuta shule haina mwalimu anayetakiwa kuwandikisha shule, kwa maana wanakuta shule zimefungwa,”amesema.

Amesema changamoto hizi, zimekuwa zikileta usumbufu kwa wazazi na wanafunzi pamoja na kuleta usumbufu usio wa lazima kwa wananchi.

Amesema vikwazo na kero hizi zimefifisha kwa kiasi kikubwa, uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza na elimu ya awali.

Kutokana na hali hiyo Waziri Bashungwa amewaelekeza viongozi wa Mikoa, Halmashauri na Shule, kuhakikisha hakuna mwanafunzi wa elimu ya awali, darasa la kwanza au kidato cha kwanza anayetozwa mchango wowote kama sharti la mwanafunzi kuandikishwa.

Pia,kila shule kuwepo na mwalimu mmoja kwa ajili a kuandikisha watoto katika kipindi hiki ambacho wanafunzi wapo likizo.

“Viongozi wote wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa Mwongozo wa utoaji wa Elimumsingi Bila Malipo. Mheshimiwa Rais ameongeza fedha zinazotolewa kila mwezi, kwa ajili ya kugharimia elimu bila malipo, kutoka shilingi bilioni 23 kwa mwezi hadi kufikia bilioni 26 kwa mwezi,”amesema.

Pia amewaelekeza Maafisa elimu wa kata kwa kushirikiana na watendaji wa kata,mitaa na vijiji, wabainishe watoto wote wanaotakiwa kuandikishwa shule na wawasisitize wazazi/walezi kufanya hivyo.

“Viongozi wote wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuendelea kufafanua utekelezaji wa Waraka wa Elimumsingi Bila Malipo kwa wazazi, jamii na wanafunzi,”amesema.

Pia,kila kundi litimize wajibu wake ili watoto wote waandikishwe, na kuendelea na masomo, katika ngazi husika.

“Kufanya zoezi la utambuzi wa watoto wenye mahitaji maalum ni suala endelevu hapa nchini. Mwaka 2018 na 2021 Ofisi ya Rais – TAMISEMI ilifanya ubainishaji wa watoto hao, nakuwaandikisha shule,”amesema.

Waziri Bashungwa pia ameelekeza Mikoa yote iimarishe na kutumia vituo vya Uchunguzi Education Service Resource Assessment Centre (ESRAC) ili visaidie katika kubainisha wanafunzi wenye mahitaji maalum, na kushauri wapelekwe katika shule maalumu, vitengo vya elimu maalum au shule jumuishi.

Kuhusiana na kalenda,Waziri Bashungwa amesema kusudi la kuandaa kalenda ni kuhakikisha kuwa, kunakuwepo na ulinganifu na usawa, wa ukamilishaji katika utekelezaji wa mitaala wa ngazi husika, katika maeneo yote ya nchini.

“Kalenda hii ni ya kwanza kuandaliwa na Serikali. Kalenda hii itawezesha wasimamizi wa elimu kufanya usimamizi, ufuatiliaji, na tathmini ya utekelezaji wa mitaala kwa urahisi,”amesema

Vilevile, kalenda hiyo itawapa fursa wanafunzi wanaohama kutoka shule moja kwenda nyingine kuwa na mwendelezo wa aina moja wa mada zinazofundishwa.

Waziri Bashungwa amewaagiza Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya, kuwasimamia Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na Walimu wa Masomo, kuzingatia kalenda ya utekelezaji wa mtaala, ili wawe na ufundishaji na ujifunzaji wenye tija na mahiri, badala ya kuwekamsisitizo katika ukaririshaji wa mada.

“Hivyo, natumia fursa hii kuwaagiza Maafisa Elimu Mikoa, kutoa mafunzo ya matumizi ya Kalenda ya Utekelezaji, katika Halmashauri zenu zote, kabla au ifikapo tarehe 1 Februari, 2022,”amesema.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger