Friday 14 January 2022

WAANDISHI WA HABARI MWANZA WAKUTANA KWA MAJADILIANO BAADA YA AJALI ILIYOGHARIMU MAISHA YA WAANDISHI WA HABARI


TAARIFA YA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI 

Leo Tarehe 14 Januari 2022, MPC imefanya Mkutano wa Waandishi wa Habari katika Ukumbi Mdogo wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel pamoja na Viongozi wa klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari aliwajulisha Waandishi wa habari juu ya taratibu za mazishi ya Waandishi ambao walipata ajali walipokua na ziara ya kiserikali kuelekea wilayani Ukerewe

Soko alieleza kuwa taratibu za mazishi zilienda vizuri na kuupumzisha miili ya Waandishi wa habari salama

Pia aliwashukru madaktari wa hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa jitihada nzuri za kunusuru maisha ya majeruhi wa ajali kwani ndani ya siku mbili au tatu wataweza kuinuka na kuanza mazoezi hivyo  madaktari wanaandaa utaratibu mzuri kwa majeruhi kuhakikisha Hali zao zinazidi kuimarika.

Pia Mwenyekiti wa MPC aliwaeleza Waandishi wa habari  kuwa usalama wa Waandishi wa habari ni muhimu hivyo taasisi/ wadau watakaofanya kazi na Waandishi waweke utaratibu mzuri na mikakati maalumu kwa ajili ya kufatilia weledi wa vyombo vya usafiri watakavyotumia

Kama kutakua na tukio linalohitaji Waandishi kuhakikisha wanajipanga siku kabla ya tukio Ili kupata logistics nzuri na kujiepusha na matukio yanayoweza kuzua taharuki

Mwenyekiti wa kamati ya maafa ya MPC Bw Charles Nyamasiriri alizungumza pia katika Mkutano huo juu ya michango ya rambirambi inayoendelea kutolewa na wadau mbalimbali.

Nyamasiriri alisema fedha zote zitakazopatikana zitatumwa kwa familia za marehemu Waandishi wote waliopata ajali. 

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza alizungumza na Waandishi na kuwashukuru sana kwa ushirikiano waliotoa juu ya kuwastili Waandishi waliopata ajali

Alizungumza kwa kutoa ushirikiano wa kina kwa familia za wafiwa na kusema Bado wanaendelea kuzungumza na familia zao na kuweka baadhi ya mambo katika utaratibu mzuri.

Mhandisi Gabriel aliwakaribisha Sana wanahabari na kutoa Rai yake kuwakaribisha Sana Nyumbani kwenye ofisi yake endapo kutakua na changamoto yoyote ya kitaaluma wasisite kumueleza.

 Mratibu 
 MPC 
 14.01.2022
Share:

Video : BHUDAGALA MWANAMALONJA - WALE WALE


Hii hapa ngoma matata ya Gwiji wa Nyimbo za asili Bhudagala Mwanamalonja inaitwa Wale Wale...Wimbo huu umebeba ujumbe mzito kuhusu watu wetu wa karibu wanaobadilika na kufanya unafiki/usaliti... Katika wimbo huu Bhudagala anasikika akisema :

👉Kumbe na wewe ni wale wale, wale wale niliowathamini, Tunakula pamoja, tunakunywa pamoja,tunacheka pamoja kumbe mwenzangu unanizunguka

👉Nilijua ni rafiki wa kweli, kumbe adui wa kweli unayeniombea nifeli niishi maisha ya ukata

👉Kilichopangwa na mwenyezi binadamu utabaki kukienzi, wivu, tamaa vitakwisha ushushe saluti za kutosha

👉Changu ni changu nimepewa, cha kwako kama hujapewa, tamaa za nini wewe shetani, kimya ushenzi kikapuni

Tazama Video hii hapa chini
 
Share:

CHAMA ATAMBULISHWA RASMI SIMBA SC



Klabu ya Simba leo Januari 14, 2022 imethibitisha kukamilisha usajili wa kwa kiungo mshambuaji wa Zambia Clatous Chota Chama.

Chama amejiunga na Simba akitokea Rs Berkane ya Morocco kwa mkataba wa miaka miwili.
Share:

MHADHIRI ANAYEFAULISHA WANAFUNZI WA KIKE KWA NGONO ATUPWA JELA


Picha

Mhadhiri wa Chuo Kikuu kimoja nchini Morocco aliyekuwa anatuhumiwa kufaulisha wanafunzi wa kike kwa kufanya nao ngono amehukumiwa kifungo cha jela miaka miwili.

Hukumu hiyo ni ya kwanza kutolewa nchini Morocco kwa mtumishi mwandamizi wa kada hiyo kwenye vyuo vikuu vya Morocco.

Mhadhiri huyo wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Hassan, kilichopo karibu na Casablanca, alitiwa hatiani kwa tabia chafu pamoja na makosa mengine.

Wahadhiri wengine wanne wanafikisha mahakamani hii leo kuhusiana na kashfa hiyo ya ufaulu kwa kutoa ngono.

Kesi hiyo iliibuliwa na chombo cha habari cha Morocco mwaka jana baada ya waandishi wake kunasa meseji za mapenzi baina ya wanafunzi na wahadhiri.
Share:

Thursday 13 January 2022

Rais Samia akutana na kuzungumza na Mawaziri na Naibu Mawaziri



Share:

Ashikiliwa Na Jeshi La Polisi Kwa Tuhuma Za Kumuua Baba Yake Mzazi Kwa Kisu


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia MUSSA EDWARD NDONDE @ SANGA MAPESA [31] Askari wa JWTZ MT.109772 Kikosi cha Ruvu JKT mkoani Pwani na Mkazi wa Mlandizi kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi aitwaye EDWARD NDONDE [75] Mwalimu Mstafuu, Mkazi wa Lumbila Jijini Mbeya kwa kumkatakata visu sehemu mbalimbali za mwili wake.  

Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 12.01.2022 majira ya saa 09:00 asubuhi huko Mtaa wa Lumbila uliopo Kata ya Iwambi, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya ambapo mtuhumiwa aliuawa EDWARD NDONDE [75] ambaye ni baba yake mzazi kwa kumchoma kisu sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha kumkata kiganja cha mkono.

Chanzo cha tukio ni tuhuma za ushirikina kwani inaelezwa kuwa mtuhumiwa anadai kuwa marehemu ambaye ni baba yake mzazi ni mchawi anamloga ili hasifanikiwe kwenye mambo yake. Awali  mtuhumiwa alifika nyumbani kwa marehemu majira ya 09:00 asubuhi pasipo kutoa taarifa  yoyote ya  kuja Mbeya na kuingia moja kwa moja sebuleni na kuanza kumshambulia kwa kisu na stuli na kupelekea kifo chake.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa uchunguzi wa kitabibu. Mtuhumiwa anaendelea kupatiwa matibabu chini ya ulinzi Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya baada kushambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi kutokana na tukio alilofanya.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linalaani tukio hili baya kutokea na litahakikisha mtuhumiwa anafikishwa kwenye mamlaka husika ya sheria kwa hatua zaidi. Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa rai kwa wananchi kuachana na Imani potofu za kishirikina hasa kuamini waganga wapiga ramli chonganishi kwani ni hatari kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya Taifa.

Imetolewa na:

[CHRISTINA A. MUSYANI – ACP]

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.



Share:

Rais Samia amuapisha Balozi wa Tanzania Nchini Kuweit na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Ndugu. Aisha S. Amour kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma leo tarehe 13 Januari 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Ndugu. Said Shaibu Mussa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma leo tarehe 13 Januari 2022.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Ndugu. Aisha S. Amour Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) kushoto na Ndugu. Said Shaibu Mussa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait kulia, mara baada ya kuwaapisha katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma leo tarehe 13 Januari 2022.



Share:

KATIBU MKUU UJENZI BALOZI MHANDISI AISHA AMOUR AWASILI RASMI WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI


Katibu Mkuu Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour (Kushoto), akipokea zawadi ya maua wakati akiwasili katika ofisi za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma


Katibu Mkuu Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour akisalimiana na watumishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), mara baada ya kuwasili katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dododma. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Ujenzi, Ludovick Nduhiye.


Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kumpokea Katibu Mkuu Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour (hayupo pichani), katika ofisi za wizara hiyo, zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Gabriel Migire - Katibu Mkuu Uchukuzi, Ludovick Nduhiye - Naibu Katibu Mkuu Ujenzi pamoja na Richard Mkumbo - Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango (Sekta Ujenzi).


Katibu Mkuu Ujenzi Balozi Mhandisi Aisha Amour akisaini kitabu cha wageni, mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu Ujenzi, Ludovick Nduhiye (aliesimama), akizungumza jambo wakati wa kikao cha mapokezi na utambulisho baada ya kuwasili kwa Katibu Mkuu Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour (aliyeketi kushoto kwa Naibu Katibu Mkuu Ujenzi), Katika ofisi za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi zilizopo mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Wakimsikiliza Katibu Mkuu Ujenzi, wakati wa kikao cha Mapokezi na Utambulisho, kilichofanyika leo katika ofisi za Wizara hiyo, zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Share:

Wednesday 12 January 2022

RAIS SAMIA AKUTANA NA JOB NDUGAI IKULU



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kuzungumza na aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) aliyefika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Share:

KAMERA KUFUNGWA BUIGIRI KUKABILI AJALI BARABARA KUU DAR-DODOMA


Diwani wa Kata ya Buigiri Mhe Kenneth Yindi,akimueleza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka jinsi walivyojipanga kufunga Kamera ili kuzuia ajali zinazotokea kwa wanafunzi wakati wa kuvuka barabara katika eneo la Buigiri wakati wa uzinduzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Buigiri yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.


MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akimpongeza Diwani wa Kata ya Buigiri Mhe Kenneth Yindi,kwa wazo la kufunga Kamera ili kuzuia ajali zinazotokea kwa wanafunzi wakati wa kuvuka barabara katika eneo la Buigiri wakati wa uzinduzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Buigiri yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.


Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga,akizungumza wakati wa uzinduzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Buigiri yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.


MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akiwa amekaa ndani ya darasa mara baada ya kuzindua vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Buigiri yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

................................................................

Na.Alex Sonna,Chamwino

KUTOKANA na idadi kubwa ya wanafunzi kugongwa na magari na kupoteza maisha katika Barabara kuu ya Dodoma - Dar es Salaam halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma anapanga kufunga kamera katika eneo la Buigiri kwa ajili ya kunasa magari yanayopita kwa mwendo kasi.

Hayo yameelezwa na Diwani wa Kata ya Buigiri Mhe. Kenneth Yindi,mbele ya Mkuu wa Mkoa Dodoma wakati akizindua vyumba vya madarasa yaliyojengwa kwa fedha za UVIKO-19, katika shule ya sekondari wa Buigiri.

Yindi, amesema kuwa kata hiyo ina shule sita na barabara kuu imepita katika vijiji vitatu.

"Wanafunzi wengi wanagongwa, magari yanakimbia sana hasa yale ya serikali, wanafunzi na hata wananchi wanapoteza maisha kutokana na ajali za barabarani" amesema Yindi

Aidha, amesema alitembelea maeneo mbalimbali nchini yaliyopitiwa na barabara kuu ili kuona namna gani wataweza kuepukana na ajali hizo.

"Tumeshafanya kikao na kamanda wa kikosi cha usalama barabarani na kupeleka ombi rasmi kwa kutumia wataalam wa ICT tutafunga kamera nne” alisema

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka, amesemasuala la kufungwa kamera ni jambo zuri kwani litasaidia kuokoa maisha wanafunzi katika shule hizo pamoja na watu wote wanao itumia barabra hiyo.

"Fungeni hizo kamera huenda tukapata suluhisho la ajali ambazo zimekuwa zikijitokea katika eneo hili mara kwa mara na kukatisha uhai wa vijana wetu" amesema.

Aidha alimtaka mkuu wa wilaya ya Chamwino Gift Msuya na vyombo vya ulinzi na usalama kuona jinsi gani jambo hilo linatekelezwa kwa haraka.

Awali akipokea taarifa ya ujenzi wa madarasa ilielezwa kuwa Buigiri Sekondari ilipokea jumla ya Sh. milioni 60 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa matatu na ofisi ya walimu.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbanga, amesema Chama hicho kinawashukuru wote waliohakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati.
Share:

WATATU WAFARIKI KWA KULIPUKIWA NA KINACHODAIWA KUWA NI BOMU


Watu watatu wamefariki dunia baada ya kulipukiwa na kile kinachodaiwa kuwa bomu mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 8:00 mchana katika kijiji cha Pongwe Msungura, Kata ya Msata.

Wankyo alisema watu hao waliokota chuma kinachodhaniwa kuwa ni bomu ambacho kililipuka mikononi mwao na kusababisha vifo vyao.

Kwa mujibu wa Kamanda Wankyo, watu hao waliokota kitu hicho kwa lengo la kwenda kukiuza kama chuma chakavu, lakini kiliwalipukia muda mfupi baada ya kukiokota.

Aliwataja waliofariki dunia katika tukio hilo kuwa ni Athumani Ramadhani (20), Maneno Hamis (23) na Abdallah Rajabu (21), wote wakazi wa Msata.

Kamanda Wankyo alitoa angalizo kwa wananchi wanaojihusisha kuuza na kununua vyuma kuwa waangalifu wanapokusanya na vitu vingine kwa lengo la kwenda kuviuza.
Share:

Tuesday 11 January 2022

RAIS SAMIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MWINYI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo.11-1-2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo.11-1-2022.
(Picha na Ikulu)
Share:

WAZIRI JAFO AFANYA ZIARA YA KIKAZI KATIKA MSITU WA PUGU KAZIMZUMBWI, AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA TFS

Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Seleman Jafo akizungumza jambo mara baada ya kutembelea Msitu wa Pugu Kazimzumbwi ulioko wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani, kuona namna ambavyo Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) ilivyojidhatiti kuendeleza msitu huo kama sehemu ya kuhifadhi mazingira. Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Seleman Jafo akiwa katika Msitu wa Pugu Kazimzumbwi ulioko wilayani Kisarawe MKOA wa Pwani kwenye ziara yake ya kikazi.Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Seleman Jafo (kulia) akimsikiliza Kamanda wa Kanda ya Mashariki TFS, Kamishna Msaidizi Caroline Malundo mara baada ya kutembelea Msitu wa Pugu Kazimzumbwi ulioko wilayani Kisarawe MKOA wa Pwani, kuona namna ambavyo Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) ilivyojidhatiti kuendeleza msitu huo kama sehemu ya kuhifadhi mazingira. Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Seleman Jafo (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka mara baada ya kutembelea Msitu wa Pugu Kazimzumbwi ulioko wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani, kuona namna ambavyo Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) ilivyojidhatiti kuendeleza msitu huo kama sehemu ya kuhifadhi mazingira. Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Seleman Jafo akipata mti katika eneo la hifadhi ya Pugu Kazimzumbwi lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kupanda miti ili kukabiliana na hewa ukaa.

Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Seleman Jafo akinawishwa mikono na Kamanda wa Kanda ya Mashariki TFS, Kamishna Msaidizi Caroline Malundo mara baada ya zoezi la Upandaji wa miti katika eneo la hifadhi ya Pugu Kazimzumbwi lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kupanda miti ili kukabiliana na hewa ukaa.

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka akipanda mti katika eneo la hifadhi ya Pugu Kazimzumbwi lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kupanda miti ili kukabiliana na hewa ukaa. Kamanda wa Kanda ya Mashariki TFS, Kamishna Msaidizi Caroline Malundo akipanda mti katika eneo la hifadhi ya Pugu Kazimzumbwi lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kupanda miti ili kukabiliana na hewa ukaa. Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Seleman Jafo akizungumza katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya kisarawe kabla ya kutembelea Msitu wa Pugu Kazimzumbwi ulioko wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani, kuona namna ambavyo Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) ilivyojidhatiti kuendeleza msitu huo kama sehemu ya kuhifadhi mazingira. Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Seleman Jafo akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kabla ya kutembelea Msitu wa Pugu Kazimzumbwi ulioko wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani, kuona namna ambavyo Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) ilivyojidhatiti kuendeleza msitu huo kama sehemu ya kuhifadhi mazingira.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**************************

NA EMMANUEL MBATILO, KISARAWE PWANI

Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Seleman Jafo amewataka wananchii wanaoishi pembezoni mwa hifadhi za misitu kuendelea na utamaduni wa utuzaji wa mazingira katika maeneo hayo ili kuendana na mabadiliko ya Tabianchi.

Ameyasema hayo leo Waziri Jafo baada ya kutembelea Msitu wa Pugu Kazimzumbwi ulioko wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani, kuona namna ambavyo Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) ilivyojidhatiti kuendeleza msitu huo kama sehemu ya kuhifadhi mazingira.

Aidha ameelekeza kila halmashauri ianze programu ya kutumia mvua zinazoendelea kunyesha nchini kupanda miti ili kuweza kufikia lengo la miti milioni 276 kwa mwaka mzima hivyo Wakuu wa Mikoa na Wilaya watasiimamia zoezi hilo.

"Tunafahamu kila halmashauri imepewa muongozo wa uwekaji wa vitalu kwa lengo la kusaidia katika maeneo mbalimbali hasa katika taasisi, tunataka tuone katika shule zetu zote, vituo vya afya, hospitali maeneo hayo yote yanapandwa miti". Amesema

Amesema upandaji wa miti kwa wingi kwenye mazingira ni njia moja wapo itakayosaidia kukabiliana na changamoto ya hewa ukaa inayoweza kuhatarisha maisha ya mwanadamu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka amesema kuna umuhimu wa utunzaji wa mazingira hivyo watanzania wanatakiwa kuweka mazingira yao kama yalivyookuwa awali na vilevile watanzania wakiendelea kupanda miti kwa wingi basi nchi itakuwa imejawa na misitu na tutaweza kupunguza athari kubwa tunazozipata kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Nae Kamanda wa Kanda ya Mashariki TFS, Kamishna Msaidizi Caroline Malundo amesema Pugu Kazimzumbwi moja ya hifadhi ya msitu muhimu uliopo hapo Wilayani Kisarawe ambao umekuwa ukichochea Utalii ndani kutokana na mikakati iliyowekwa na Wakala wa Misitu TFS.

Share:

MBUNGE DODOMA APONGEZA TEUZI ZA RAIS SAMIA


Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile

MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile amempongeza Rais Samia Suluhu kwa kuteuwa mawaziri, manaibu mawaziri na makatibu wakuu ambapo amesema kuwa ni wazi Rais Samia amekusudia kuboresha maisha ya watanzania.

Akizungumza leo Januari 11,2022 mbunge huyo amesema kuwa viongozi hao wapya ni wazi kuwa ni wachapakazi na wazalendo ambapo wataweza kwenda na kasi katika kutatua changamoto za wananchi.

"Rais Samia ameendelea kuthibitisha kwa vitendo anayo nia ya dhati ya kuboresha maisha ya Wananchi kwa kuteua wasaidizi wachapakazi, Wazalendo na Vijana wengi ambao binafsi naamini watakwenda speed kukimbizana na matatizo na changamoto za wananchi", amesema Mariam Ditopile.


Aidha, amewapongeza viongozi hao kwa kuaminiwa na kuteuliwa katika nafasi hizo ambapo amesema kuwa "Nichukue Nafasi hii kuwapongeza Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu walioaminiwa na kuteuliwa.”

Amesema Watanzania wana imani kubwa na Serikali ya Rais Samia ambapo katika kipindi kifupi uchumi umeimarika, huduma za jamii zimeendelea kuboreshwa na kipato cha mtu mmoja mmoja kinaongezeka.
Share:

MPC YATAJA MAJINA YA WAANDISHI WA HABARI WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA GARI, YUMO HUSNA MILANZI... MAJERUHI WAWILI AKIWEMO VANY CHARLES

Waandishi wa habari waliofariki dunia kwenye ajali

Taarifa kamili juu ya ajali iliyohusisha waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza. 
............................................
Ndugu waandishi wa habari na wadau wa habari , asubuhi ya leo tuliwataarifu taarifa ya awali juu ya ajali ya waandishi wenzetu wa Mkoa wa Mwanza.

Baada ya kufika kwenye Zahanati ya Busenga nilipewa jukumu la kuwataambua  marehemu.

Waliofariki ni 
1.Husna Milanzi - ITV
2.Johari Shani - Uhuru Digital
3.Antony Chuwa - Freelancer 
4.Abel Ngapenda - Afisa Habari ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza
5.Steven Msengi - Afisa Habari Ukerewe.

Majeruhi.
1.Tunu Heman - Freelancer
2 Vany Charles  - Icon TV

Kwa sasa tupo njiani na miili ya wapendwa wetu kuelekea hospitali ya Mkoa ya Seketoure Mwanza.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Simiyu chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa magari yote mawili na amethibitisha vifo hivyo.

Taarifa nyingine za uratibu wasibu wa msiba  tutawajuza.

Mwanza press club tumepokea kwa masikitiko makubwa msiba huu.

Kazi ya Bwana haina makosa, jina lake lihidimiwe.

 Edwin Soko 
 Mwenyekiti 
 Mwanza Press Club 
 11.01.2022


UTPC 
It with a great sadness that we have received information about the death of five journalists caused by a tragedy accident occurred in Busega Simiyu today. 

Among the dead are;
1. Johari Shani -Uhuru Digital
2. Husna Milanzi - ITV
3. Abel Ngapemba - Mwanza Regional Information Officer
4. Antony Chuwa - Habari Leo Digital
5. Steven Msengi - Ukerewe Information Officer

Journalists who were injured in this accident are:
1. Tunu Hermany - Freelance Journalist
2. Van Charles - Icon TV
We offer our sincere and deepest condolences to all journalists, friends and relatives for this tragedy. May their soul rest in peace. Amen
More information will be provided later.
Share:

Video : BHUDAGALA - TULEBHALYO....NGOMA YA HUZUNI SANA

Huu hapa wimbo wa Maombolezo wa Gwiji wa nyimbo za asili,Bhudagala Mwanamalonja inaitwa  Tulebhalyo.  Imetengenezwa katika studio za Asili Yetu Africa ikiongozwa na Gooder / Mong


Tazama hapa  chini video hii ya huzuni


UPDATES ZOTE

Pakua / Download App ya Malunde 1 blog Tuwe tunakutumia taarifa zote moja kwa moja kwenye simu yako bure kabisa 

Bofya <<HAPA>> Mara Moja Tu


Share:

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE AJALI ILIYOUA WATU 14, WAKIWEMO WAANDISHI WA HABARI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameeleza kushtushwa na ajali iliyosababisha vifo vya watu 14 mkoani Mwanza.

Mheshimiwa Rais Samia ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter huku akimuomba Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema na majeruhi wapone haraka.

"Nimeshtushwa na vifo vya Watu 14 wakiwemo Wanahabari 6 vilivyotokea leo asubuhi baada ya gari lililokuwa katika msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kugonga na Daladala. Poleni Wafiwa, Wanahabari na jamaa wote. Mungu aziweke mahali pema roho za Marehemu na Majeruhi wapone haraka,"ameeleza Mheshimiwa Rais Samia.

Ajali hiyo imehusisha magari mawili likiwemo la abiria aina ya Toyota Hiace na jingine lenye namba za usajili STK 8140 mali ya Serikali lililokuwa limebeba waandishi wa habari mkoa wa Mwanza wakitokea Mwanza kuelekea Ukerewe kupitia Bunda, Mara baada ya kugongana uso kwa uso leo Janauri 11, 2022.


Tayari Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, Bw. Emmanuel Luponya Sherembi, ameahirisha ratiba ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhandisi Robert Gabriel kwa ajili ya kukabidhi miradi baada ya ajali hiyo.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger