Friday 1 October 2021

NHIF TANGA YASHEHEREKEA MIAKA 20 KWA KUTOA MASHUKA 80 KITUO CHA AFYA PONGWE

Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa akipokea zawadi ya mashuka 80 katika kituo cha Afya Pongwe kilichopo Kata ya Pongwe Jijini Tanga yaliyotolewa na NHIF kulia ni Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO) Dkt Charles Mkombe akifuatiwa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto ni Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sady
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo
Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO) Dkt Charles Mkombe
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa kulia akipokea msaada wa mashuka 80 kutoka kwa Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally  Mwakababu  kushoto ikiwa ni katika kusherehekea miaka 20 katikati anayeshughudia ni Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO) Dkt Charles Mkombe

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa kulia akiangalia shuka alizokabidhiwa na  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) kushoto ni Meneja wa Mfuko huo Ally  Mwakababu  ikiwa ni katika kusherehekea miaka 20 

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa kulia akiwa ameshika moja ya  shuka zilizokabidhiwa na  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) kushoto ni Meneja wa Mfuko huo Ally  Mwakababu  ikiwa ni katika kusherehekea miaka 20
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa  katika akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Pongwe  kulia ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Ally Mwakababu
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mngandilwa katika kulia ni Msimamizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga Dinna Mlwilo

NA OSCAR ASSENGA,TANGA

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Tanga katika kusherehekea miaka 20 wamekabidhi zawadi ya mashuka 80 katika kituo cha Afya Pongwe kilichopo Kata ya Pongwe Jijini Tanga.

Akizungumza wakati akipokea mashuka hayo Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa aliwataka wananchi kuchangamkia fursa za kujiunga na Bima ya Afya ili kuweza kupata uhakika wa kupata matibabu kutokana na kwamba siku zote magonjwa hayabishi hodi yanapokuja .

Alisema kwa sababu huja muda wowote hivyo ni muhimu waweze kuwa na bima ya afya kwani wakifanya hivyo watakuwa wamejitengenezea utaratibu wa uhakika wa matibabu kwa mwaka mzima na kuondosha changamoto ambazo wangekumbana nazo.

“Kwanza niwashukuru NHIF kwa namna mlivyoonyesha umuhimu kwenye sekta ya afya na kuamua kutoa msaada huo na niwaombe muendelee kutusaidia katika kuhakikisha tunamaliza changamoto mbalimbali zilizopo”Alisema

Alisema duniani kote moja ya jambo muhimu la kuwekeza kuliko chochote ni sekta ya afya kutokana na wao wenyewe ni watanzania mazingira yao wanayajua na maisha yao na magonjwa hayapigi hodi yanakuja siku ambayo ukiwa hauna fedha.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kutokana na hilo Serikali ikaona kuna kila sababu ya kufikia hatua kila mtanzania kuwa na bima ya afya ili kuweza kupata matibabu.

“Serikali imeona kuna sababu ifike hatua iwe ni sheria kila mtanzania anapozaliwa ana miliki bima ya afya ili aweze uhakika kupata matibabu kutokana na kwamba fedha haitunziki na matatizo yanakuja pale kwenye changamoto”Alisema

Alisema sasa inaweza kutokea unapata shida unapokwenda hospitali huna fedha na kupelekea kukaa nyumbani na mgonjwa wako na hivyo kupelekea kupoteza maisha.

“Niwapongeze NHIF na niwaombe wananchi maisha yetu tunayajua na sisi tunaotegemea shughuli za kilimo fedha zetu ni za msimu kutokana na wakati mwengine hatuna sasa kama tutajenga utamaduni ya kujiunga na mpango huo utatusaidia kupata matibabu “Alisema DC Mgandilwa.

Awali akizungumza wakati wa sherehe hizo,Meneja wa NHIF Ally Mwakababu alisema katika miaka 20 mfuko huo umepitia hatua mbalimbali na wameamua kutoa msaada huo kituo cha Afya Pongwe kwa sababu ya idadi ya watu wanaohudumiwa eneo hilo na uhitaji.

Alisema mfuko huo umeamua kurudisha kidogo kwa wananchi na wametoa mashuka ili kuwawezesha wagonjwa kuweza kulala mahali pazuri na kupata huduma bora.

“Pongwe inahudumia kata mbili na baadhi ya wilaya nyengine hivyo tunatamani watu wapate mahali pazuri na tunajivunia miaka 20 ya NHIF mfuko mkoa wa Tanga huduma zimeimarika na wameweza kuboresha huduma mbalimbali”Alisema

Alisema huduma hizo ni pamoja na kutoa mikopo kwa vituo,mikopo ya ukarabati na ununuzi na vifaa tiba na kulipa kwa wakati madai ya wanachama wanaotibiwa na vituo hivyo na hivi sasa NHIF tumeingia kwenye mfuko wa Kidigitali”Alisema .

Naye kwa upande wake Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO) Dkt Charles Mkombe alishukuru kwa msaada huo wa mashuka 80 ambao wameupata kutoka kwa wadau wao NHIF.

Alisema kwa kiasi kikubwa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya kuna changamoto nyingi wanazokutana nazo hasa bidhaa za afya na shirikishi kwenye kutuo huduma na mashuka ni bidhaa muhimu kwa maisha ya wagonjwa wanaolazwa .

“Niwashukuru NHIF kwa maada huu mkubwa kwani tuna upunguza vifaa mbalimbali ikiwemo mashuka ambayo yanatumika kwenye vitu vikubwa na bado tunaupungufu wa mashuka watakaoguswa wajitokeze watuwasaidie”Alisema

Share:

Nutrition Advisor at TechnoServe

For more than 20 years, TechnoServe has been working in Tanzania with farmers, cooperatives, suppliers and processors to strategically develop competitive industries around key crops, including cash crops such as cocoa, horticulture and coffee, and staples such as maize. We are helping farmers make the transition from subsistence to commercial production, assisting processors to improve […]

This post Nutrition Advisor at TechnoServe has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

 Sustainable Horticulture Lead at TechnoServe

For more than 20 years, TechnoServe has been working in Tanzania with farmers, cooperatives, suppliers and processors to strategically develop competitive industries around key crops, including cash crops such as cocoa, horticulture and coffee, and staples such as maize. We are helping farmers make the transition from subsistence to commercial production, assisting processors to improve […]

This post  Sustainable Horticulture Lead at TechnoServe has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

 Monitoring, Evaluation & Learning (MEL) Manager at TechnoServe

For more than 20 years, TechnoServe has been working in Tanzania with farmers, cooperatives, suppliers and processors to strategically develop competitive industries around key crops, including cash crops such as cocoa, horticulture and coffee, and staples such as maize. We are helping farmers make the transition from subsistence to commercial production, assisting processors to improve […]

This post  Monitoring, Evaluation & Learning (MEL) Manager at TechnoServe has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

 Inclusion Advisor at TechnoServe

For more than 20 years, TechnoServe has been working in Tanzania with farmers, cooperatives, suppliers and processors to strategically develop competitive industries around key crops, including cash crops such as cocoa, horticulture and coffee, and staples such as maize. We are helping farmers make the transition from subsistence to commercial production, assisting processors to improve […]

This post  Inclusion Advisor at TechnoServe has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

. Partnerships and Small and Medium Enterprise (SME) Development Lead at TechnoServe

For more than 20 years, TechnoServe has been working in Tanzania with farmers, cooperatives, suppliers and processors to strategically develop competitive industries around key crops, including cash crops such as cocoa, horticulture and coffee, and staples such as maize. We are helping farmers make the transition from subsistence to commercial production, assisting processors to improve […]

This post . Partnerships and Small and Medium Enterprise (SME) Development Lead at TechnoServe has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Consultant at UNESCO

Parent Sector : Education Sector (ED)   Duty Station: Multiple Job Family: Education Type of contract : Non Staff Duration of contract : From 1 to 6 months Recruitment open to : External candidates Application Deadline (Midnight Paris Time) : 07-OCT-2021 UNESCO Core Values: Commitment to the Organization, Integrity, Respect for Diversity, Professionalism OVERVIEW OF THE FUNCTIONS OF THE POST Terms of […]

This post Consultant at UNESCO has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Human Resource Manager at CVPeople Tanzania

Human Resource Manager   CVPeople Tanzania | Full time Nairobi , Kenya | Posted on 09/29/2021 Job Description To lead the HR team and take ownership of all HR matters across the company from recruitment to performance reviews, wage reviews, disciplinary action, and learning and development and Strategic Contribution to the Company.   Consistently recruiting […]

This post Human Resource Manager at CVPeople Tanzania has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Hukumu Kesi ya Lengai Ole Sabaya na Wenzake Kutolewa Leo

Mahakama  ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, leo inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya jinai namba 105 ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34).

Washtakiwa wengine katika shauri hilo ni Silvester Nyegu(26) na Daniel Mbura(38), ambao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya unyang'anyi kwa kutumia silaha.

Kesi hiyo ilinguruma kwa siku 35 mfululizo mbele ya Hakimu Mwandamizi wa mahakama hiyo, Odira Amworo hadi kufikia tamati.

Upande wa Jamhuri ulikuwa na mashahidi 11 na vielelezo 10 vya ushahidi na viliwasilishwa mahakamani kama sehemu ya ushahidi.

Mashahidi wa upande wa utetezi, walikuwa watatu na walijitetea kwa njia ya kula kiapo na kuwasilisha baadhi ya nyaraka kama vilelezo vya ushahidi.

Share:

Member of The Board of Directors at CVPeople Tanzania

Member of the Board of Directors (2 Females, 2 Males)   CVPeople Tanzania | Full time Dar es salaam , Tanzania | Posted on 09/29/2021 Job Description Mission WIMA Nonprofit’s mission is to close the gender gap for for women in leadership across Africa through training, mentoring and  honoring them for their achievements For more information, […]

This post Member of The Board of Directors at CVPeople Tanzania has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Head of Enterprise Risk at Bank of Africa Tanzania

Head of Enterprise Risk    Location: Head Office Reporting to Managing Director Summary of Responsibilities: To facilitate the execution of Enterprise Risk Management (ERM) processes and infrastructure as a key enabler to achieving the business objectives of the bank sustainably. Scope of Duties:   To integrate risk management within the strategy development process of the […]

This post Head of Enterprise Risk at Bank of Africa Tanzania has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Ufafanuzi Kuhusu Magari Ya Mizigo Ya Tanzania Yaliyokwama Nchini Malawi

Share:

Head of Finance at Bank of Africa Tanzania

Head of Finance Location: Head Office Reporting to Managing Director Summary of Responsibilities: Manage the Bank’s Finance function in accordance with the established professional standards, policies and procedures and give a general strategic and operational guidance on all financial matters of the bank to continuously improve the financial Position of the bank. Scope of Duties: […]

This post Head of Finance at Bank of Africa Tanzania has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo October 1

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA OKTOBA 1,2021

Magazetini leo Ijumaa October Mosi 2021

Share:

WANAWAKE WAKERWA TABIA YA WANAUME KULALA NA WAKE ZAO WAKIWA WAMEVAA SURUALI

Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela, Bi. Rahabu Nkwabi akielezea namna tabia ya wanaume kulala na wake zao huku wamevaa suruali inavyochangia ukatili wa kingono.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wanawake katika kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wamewaomba wanaume kubadilika na kuacha kuwafanyia ukatili wa kingono wake zao kwa kutowapatia haki yao ya ndoa kwa kulala wakiwa wamevaa suruali.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Septemba 30,2021 na Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela kinachosimamiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Rahabu Nkwabi wakati wa mkutano wa hadhara katika kata hiyo kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia.

Rahabu alisema matukio ya ukatili wa kijinsia katika familia nyingi yamekuwa yakisababishwa na tabia za wanandoa kuanza kusaliti wenza wao matokeo yake wanashindwa kuwapatia haki ya ndoa wake zao hali inayosababisha nao kuanza kuchepuka ili kukidhi haja zao za kimwili.

“Wanawake vunjeni ukimya, fungukeni kuhusu akina baba wanaolala na suruali kwani wanawafanyia ukatili wa kingono kwa kuwanyima haki yenu ya ndoa", amesema Rahabu.

“Mwanaume kwanini ulale na mke wako huku umevaa suruali? ulioa kwa ajili ya nini,huoni kuwa unamnyima haki yake mkeo na kumfanya awaze kuwa unamsaliti kwa kufanya ngono na wanawake wengine nje ya ndoa. Kwanini ulale na suruali wakati mwenzako anataka, umeshiba huko nje ndiyo maana ndani hutaki?”,amehoji Rahabu.

Katika hatua nyingine Rahabu aliwataka akina mama kuwapatia haki ya ndoa waume zao na kuepuka visingizio na sababu za mara kwa mara kuwa hawawezi kushiriki tendo la ndoa kwani kitendo cha kunyimana tendo la ndoa kinasababisha migogoro hali inayopelekea kupigana ndoa kuvunjika na kusababisha watoto kuteseka, kutelekezwa na kuacha shule,kuolewa wangali wadogo au kuzurura tu mtaani.

“Wanawake wapeni tendo la ndoa waume zenu, acheni visingizio. Mkiwanyima ndiyo maana wengine wanaamua kuanza kuchepuka matokeo yake wanalala na suruali. Wanaume nanyi na msipowapa haki yao wake zenu inafikia wanawake wanachoka kuvumilia wanatafuta wanaume wa pembeni kisha mnaanza kuvurugana humo ndani ya nyumba”,ameongeza Rahabu.

Aidha amewashauri akina mama kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia badala ya kukaa tu kimya huku akiishauri jamii kuacha tabia ya kuozesha watoto wadogo.

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Shilela Shiminzi Ngeleja amesema suala la wanandoa kunyimana tendo la ndoa limekuwa chanzo cha matukio ya ukatili ndani ya familia hali inayojenga chuki na kusababisha migogoro ya hapa na pale hivyo ni vyema pande zote (mke na mme) kukaa chini na kutatua changamoto zao.

"Hili suala la kunyimana tendo la ndoa lipo pande zote mbili, tunapokea kesi kwa baadhi ya wanaume wanalala na wake zao huku wakiwa wamevaa suruali, wanawake nao wanakwepa tendo kwa visingizio vingi na wapo wanalala huku wamevaa suruali/ Skin tight (Jeans za kubana) kiasi kwamba huwezi kumvua, huu ni ukatili wa kingono na wanapata sana athari za kisaikolojia matokeo yake ugomvi ndani hauishi", amesema Ngeleja.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Shilela Bi. Mwanaidi Mustapha Mzee amesema amekuwa akipata kesi mbalimbali kwa baadhi ya wanandoa kunyimana tendo la ndoa ambapo kesi hizo huwa wanazipeleka kwenye Baraza la usuluhishi la kata.

“Nimekuwa nikipokea kesi za wanandoa kunyimana tendo la ndoa. Hivi karibuni nimepata kesi kuhusu mwanaume kulala na mke wake huku akiwa amevaa suruali kwa muda wa miezi miwili mfululizo,mwanamke akavumilia. Lakini cha kushangaza mwanaume huyo akaanza kumpiga mkewe ili aondoke aoe mwanamke mwingine”,amesema Mwanaidi.

Amesema matukio ya wanaume kuwapiga na kuwafukuza wake zao yamekuwa yakitokea hasa katika kipindi cha mavuno ambapo baadhi ya wanaume wanaanza kufanya vituko ili kutumia peke yao mali walizochuma na wake zao.

Hata hivyo amesema wanaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu Ukatili wa kijinsia ili watu wabadilike, waishi kwa amani na upendo ili kuchochea maendeleo katika jamii sambamba na namna ya kupata haki zao pindi zinapopotea au zinapotaka kupotea.

Kwa upande wake, Mkazi wa Shilela Simon Masolwa amesema tabia ya watoto kusindikiza Harusi inasababisha ukatili wa kijinsia kwani watoto wanaanza kujifunza mambo ya wakubwa na kujikuta wanaolewa au kupata mimba wangali wadogo.

Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela, Joseph Samwel Mbunge amesema miongoni mwa mafanikio yaliyofikiwa na kituo hicho ni pamoja na kupunguza ndoa za utotoni na kurudisha shuleni watoto walioacha masomo yao.

Msaidizi wa Kisheria Esther Mwampashi kutoka kata ya Bulige amewashauri wanajamii kuvunja ukimya juu ya matukio ya ukatili wa kijinsia na kuibua matukio mbalimbali yaliyofichwa ili yaweze kutatuliwa na wasaidizi wa kisheria na waragbishi na wana vituo vya taarifa na maarifa.

Naye Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika la linalotoa msaada wa kisheria mkoani Shinyanga Paralegal Aid Centre (PACESH), Henerico Masasi amewataka wanajamii kuwatumia wana vituo vya taarifa na maarifa na wasaidizi wa kisheria kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo mimba na ndoa za utotoni na migogoro ya ndoa na ardhi.

Mkutano huo wa hadhara uliolenga kutoa Matokeo ya Utekelezaji wa Shughuli za Mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake kiuchumi unaotekelezwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kupitia shirika la Watu na Makazi Duniani (UNFPA tangu mwezi Julai 2020.
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela kinachosimamiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Rahabu Nkwabi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata hiyo kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia Septemba 30,2021.Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela kinachosimamiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Rahabu Nkwabi akiwasihi wanawake na wanaume kuvunja ukimya kwa kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ukatili wa kingono kwa kunyimana tendo la ndoa.
Wananchi wa kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala wakiwa kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia
Wananchi wa kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala wakiwa kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia
Afisa Mtendaji wa Kata ya Shilela Bi. Mwanaidi Mustapha Mzee akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Mkazi wa Shilela Simon Masolwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Shilela Shiminzi Ngeleja akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Msaidizi wa Kisheria Esther Mwampashi kutoka kata ya Bulige akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika la linalotoa msaada wa kisheria mkoani Shinyanga Paralegal Aid Centre (PACESH), Henerico Masasi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Wananchi wa kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala wakiwa kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia
Igizo kuhusu Ukatili wa Kisaikolojia likiendelea kwenye mkutano wa hadhara ambapo jamaa amenaswa mubashara akimchungulia mwanamke anayeoga bafuni hali inayomfanya mwanamke huyo aathirike kisaikolojia kuchunguliwa
Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela, Joseph Samwel Mbunge
Wasaidizi wa Kisheria halmashauri ya wilaya ya Msalala wakiwa kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia
Wananchi wa kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala wakiwa kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

Thursday 30 September 2021

SEMA SINGIDA YAZINDUA MRADI WA KILIMO BIASHARA

Mkuu wa Wilaya ya  Manyoni Rahabu Mwagisa akizindua mpango wa uboreshaji wa maisha ya jamii kupitia mradi wa "Kilimo Biashara" unaosimamiwa na Shirika la SEMA mkoani Singida.

Na Edina Malekela,Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amesema Mkakati wa kitaifa wa kuondoa umaskini ni jukumu la Serikali,Sekta binafsi,Asasi zisizo za kiserikali (NGO'S) na washirika mbalimbali wa maendeleo ambapo unahitaji kuzingatia na kushughulikia kwa usahihi changamoto zinazowakabili wakulima wadogo.

Dkt. Mahange alisema hayo jana alipowakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa katika uzinduzi wa mpango wa uboreshaji wa maisha ya jamii kupitia mradi wa "Kilimo Biashara" unaosimamiwa na Shirika la SEMA mkoani Singida.

Alisema tafiti kadhaa zilizofanywa kuhusu umasikini zimebaini watu wengi masikini wanaishi vijijini na ni wakulima wadogo hivyo mikakati ya kitaifa ya kuondoa umasikini huo unahitaji kutatua kwa usahihi changamoto zinazowakabili wakulima hao.

Alisema mradi huo umeanza wakati muafaka ambapo mkoa kwa sasa unafikiria kuanzisha utekelezaji wa mpango wa kukuza uzalishaji wa zao la Alizeti unaolenga kuongeza uzalishaji wa mafuta yatokanayo na zao hilo kutoka tani 90,000 hadi tani 242,500 sawa na 54% ya jumla uagizaji wa mafuta hayo hapa nchini.

"Mpango huu wa uzalishaji utajumuisha washikadau wakiwemo wakulima wadogo,Vyama vya ushirika, Asasi za kiraia, wakulima wakubwa,Wizara ya Kilimo na Sekta binafsi." alisema na kuongeza.

"Matarajio yetu Mkoa na Wizara ya Kilimo katika utekelezaji wa mpango wa uboreshaji wa maisha ya jamii kupitia mradi wa Kilimo cha kibiashara ambao SEMA wanautekeleza utainua Uchumi wa wakulima wadogo wadogo kupitia kuongeza kwa tija ya mazao yatakayowezeshwa na mradi huu." alisema Dkt Mahenge.

Awali kabla ya kuzungumza Mkuu wa Mkoa Meneja Mkuu wa SEMA Ivo Manyaku alisema lengo la mradi huo ni kuwajengea uwezo wakulima waweze kujiunga kwenye vikundi vya kuweka na kukopa waweze kutunza mazao yao ili waje kuyauza kwa pamoja jambo litakalo wasaidia kuwa na sauti moja ya soko.

"Wakulima wengi wanauza mazao yao yakiwa shambani ili kukidhi mahitaji yao kutokana na kutokuwa na akiba hivyo ili wapate mahitaji wanayoyahitaji wanajikuta wanauza kwa bei ya hasara." alisema Manyaku.

Alisema kupitia mradi huo wanalenga kuyaongezea thamani mazao yanayozalishwa na wakulima,kuongeza mnyororo wa thamani ambapo mikakati ni kuwa na mashamba darasa,maonyesho ya Vijiji ya kibiashara ambapo watawaunganisha wasambazaji wa pembejeo ,maafisa Kilimo, wakulima na wanunuzi ili waone kila mmoja anahitaji nini jambo litakalosaidia mkulima kuwa na uhakika wa soko.

Meneja alisema mradi huo umewapa kipaumbele Wanawake na Vijana kwa zaidi ya 70% na utatekelezwa katika Wilaya tatu za mkoa huu ambazo ni Iramba, Ikungi na Manyoni huku ukitarajiwa kuboresha maisha ya wakulima wadogo 6,000 kwa kuimarisha miundombinu ya kusaidia biashara na mnyororo wa thamani wa mazao ya Mahindi,Mbaazi,Mtama pamoja na Alizeti.
Mkuu wa Wilaya ya  Manyoni Rahabu Mwagisa katikati  akiwa na viongozi wengine wakitembelea mabanda ya wajasiliamali kabla ya kuzindua mapanho wa uboreshaji wa maisha ya jamii kupitia mradi wa  kilimo biashara.

Meneja Mkuu wa SEMA Ivo Manyaku akizungumza kwenye ghafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya  Manyoni Rahabu Mwagisa akizungumza kabla ya kuzindua mradi huo.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger