Saturday 29 May 2021

JAMAA MGONJWA ATIMULIWA HOSPITALI BAADA YA KUMSHIKA NESI MAKALIO

Jamaa aliyekuwa akipokea matibabu katika hospitali moja eneo la Chogoria nchini Kenya amefukuzwa wodini kabla ya kupata nafuu baada ya kushindwa kula kwa macho akaishia kunyoosha mkono na kumgusa makalio nesi mkuu.

 Inasemekena ilikuwa ni mwendo wa saa mbili usiku ambapo wagonjwa wote walikuwa wamekula wakati nesi aliyekuwa zamuni alipita katikati ya wagonjwa katika wodi kuhakikisha kila mgonjwa anashughulikiwa.

Kwa mujibu wa Taifa leo, nesi huyo alikuwa amevalia sketi fupi mno bila kujali wagonjwa.

 Duru zinaarifu kuwa alipofika alikokuwa jamaa aligundua kuwa kulikuwa na mgonjwa kando yake aliyehitaji msaada. 

Alimuonesha jamaa mgongo kisha akaninama na kufaraghua sehemu yake ya nyuma iliyompagawisha na kumzuzua jamaa. Jamaa alipoona hivyo, akili zilimsimama akawaza na kuibuka na mawazo ya kumgusa nesi bila kujali matokeo yake.

“Samahani dada. Nimeshindwa kuvumilia urembo wako nikaona ni bora niguse,” jamaa mgonjwa alisema. 

“Mjinga wewe! Umefaidi nini? Nyie nyinyi vibaka tunaoogopa usiku. Watakaje?” Nesi aliuliza.

 “Niwie radhi dada. Samahani sitarudia tena,” jamaa alizidi kujitetea.

 “Kesho utaenda nyumbani kwa maana inaonekana haufai kuwa humu wodini. Wewe ni hatari kwa wagonjwa wengine na wafanyakazi katika hospitali hii,” muuguzi mkuu alimwambia jamaa

. Siku iliyofuata mapema asubuhi, jamaa aliamuriwa kuondoka hospitalini, japo hakuwa amepona na jamaa zake walipouliza ni kwa nini waliachwa vinywa wazi walipoarifiwa kuhusu alichomfanyia nesi mkuu usiku uliotangulia. 

“Huyu ni mtu hatari kuendelea kubaki katika wodi kwa sababu anaweza kuwadhuru wagonjwa na wafanyakazi. Tamaa yake imevuka mipaka. Ondokeni naye mkamuuguze nyumbani,” waliarifiwa.

 Penyenye zinasema kuwa baadhi yao walitishia kuishtaki hospitali kwa kumfukuza mgonjwa kabla ya kupona lakini naye nesi akawaambia angemshtaki kwa kumdhulumu kimapenzi.

Jamaa hakuwa na lingine ila kuchechemea akiondoka hospitalini humo, haikubainika iwapo jamaa zake walimpeleka hospitali nyingine

Chanzo - Tuko News

Share:

RUBANI AKIRI KUANGALIA NGONO NA KUVUA NGUO MBELE YA MWANAMKE SAFARINI


Rubani wa zamani wa shirika moja la ndege la Marekani amekiri kufanya " kitendo kisichofaa" akiwa safarini mwaka jana.

Michael Haak, 60, alitoa nguo mbele ya rubani mwenzake wa kike ndani ya chumba cha marubani huku akitazama filamu za ngono (ponografia) kwenye kompyuta yake ndogo, waendesha mashtaka walisema.

Wakati ndege ya shirika la Southwest Airlines ikiendelea na safari, Haak aliendelea kufanya" kitendo kisichokuwa na staha " katika chumba cha marubani.

Jaji wa mahakama ya Maryland amemhukumu kifungo cha mwaka mmoja na kumuamuru alipe faini ya dola 5,000 sawa na (Pauni 3,500).

Tukio hilo lilitokea wakati ndege ilipokuwa safiri kutoka Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Philadelphia kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Orlando mnamo Agosti 10 mwaka 2020, mahakama ilifahamishwa.

Wakati ndege iliposhika mkondo wa safari, Haak aliondoka katika kiti cha rubani, "kimakusudi" na kuanza kutazama filamu ya ngono kwenye kompyuta yake ndogo.

"Haak aliendelea kufanya tabia mbaya, huku rubani mwenzake wa kike akiendelea na kazi," taarifa ya waendesha mashtaka ilisema.

Haak hakuwahi kukutana na rubani mwenzake kabla ya safari hiyo, waliongeza.

Wakili msaidizi Michael Cunningham alisema rubani mwenzake "alikuwa na haki ya kutofanyiwa kitendo kama hicho, bila kujali ni nini kingechochea au kilisababisha kitendo hicho", Associated Press iliripoti.

Haak alishtakiwa Maryland kwasababu ndege ilikuwa ikipaa katika anga za jimbo hilo wakati wa tukio hilo. Alikiri kufanya hatia hiyo kimakusudi, hadharani.

Katika taarifa iliyowasilishwa kupitia link ya video, Haak aliomba msamaha kwa kufanya kitendo hicho, akisema: "Ilianza kama utani kati yangu na rubani mwenzangu. Sikudhani ingeligeuka kuwa hivi ndani ya miaka elfu moja."

Jaji wa mahakama ya Marekani, J Mark Coulson alimwambia Haak kwamba tabia yake ilikuwa na athari mbaya kwa rubani mwenzake na ingeweza kuathiri usalama wa abiria.

Haak, kutoka Longwood, Florida, alikuwa rubani wa shirika la Southwest Airlines kwa miaka 27 kabla ya kustaafu mwisho wa mwezi Agosti mwaka jana.

Katika taarifa, shirika hilo lilisema haliruhusu "tabia kama hiyo na itachukua hatua mara moja endapo mwenendo kama huo utathibitishwa". Msemaji alisema kampuni hiyo ilifahamishwa kuhusu tukio hilo baada ya Haak kuacha kazi kwa hiari.

Kampuni hiyo ilisema, imesitisha kumlipa mafao yoyote ambayo alikuwa anastahili kupata kama haki ya kustaafu.

CHANZO - BBC SWAHILI
Share:

Mkuu Wa Majeshi Ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo Atembelea Ubalozi Wa Tanzania- Pretoria


Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo,ametembelea Ubalozi wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Jenerali Mabeyo yupo Nchini Afrika Kusini kuhudhuria sherehe za kumuaga Mkuu Majeshi wa Afrika Kusini Jenerali SZ Shoki zilizofanyika kitaifa Jana Mjini Pretoria. Kuhudhuria sherehe hizi,ni utaratibu uliowekwa  na nchi wanachama wa Jumuiya za SADC ya maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika kuimarisha  mashirikiano  hususan katika nyanja ya Diplomasia ya Ulinzi (Defence Diplomacy) na Amani katika eneo Ia nchi za SADC.

Jenerali Mabeyo, alikaribishwa Ubalozini na Mhe. Balozi Mej. Jen. Gaudence Milanzi (Mst) na watumishi wa Ubalozi Mhe. Balozi Milanzi alitoa taarifa fupi ya eneo la uwakilishi ya Afrika Kusini, Botswana na Falme ya Lesotho.

Mhe. Balozi alieeza kuwa hali ya uwakilishi inaridhisha kiulinzi na kiusalama, Ubalozi umeendelea kukuza mashirikiano na nchiza eneo la uwakilishi ikiwa ni pamoja na SADC. Kwa kufuata miongozo ya sera ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyoelekeza kuendeleza Diplomasia ya kisiasa na kutekeleza Diplomasia ya uchumi.


Upande wake Jenerali Mabeyo alielezea ziara yake kwa ujumla nchini Afrika Kusini imekuwa ni ya mafanikio, na pia kuna mambo kama ambayo kama Mkuu  wa Majeshi ameona yanafaa kuigwa ili kuboresha utendaji wa Jeshi la Tanzania.

Jenerali Mabeyo amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya  Muungano  wa  Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan, amelenga kuendeleza maendeleo ndani na nje ya nchi mfano katika kutekeleza Sera ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania na mwelekeo  unaelekeza kuimarisha  Diplomasia kwa  kujenga mahusiano na nchi duniani kwa   kuimarisha Diplomasia ya siasa na Diplomasia ya uchumi.

Jenerali Mabeyo alimsihi Balozi na watumishi wa Ubalozi kuhakikisha kuwa wanaielewa na kuisimamia dira ya Diplomasia kama ilivyoainishwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, ili kuweza kutelekeza majukumu yao kwa wepesi.


 



Share:

Mwongozo wa uwekezaji Mara wazinduliwa


 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Mkoa wa Mara na Watendaji katika Sekta ya Utalii wabadilike na waweke mkakati wa kuitangaza mbuga ya Serengeti ili kuweza kuvutia zaidi watalii na kuitambulisha mbuga hiyo kuwa iko mkoa humo.


Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan inaboresha mazingira ya uwekezaji na biashara ili kuvutia uwekezaji utakaoinua uchumi wa nchi na watu na mwongozo huo ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuvutia uwekezaji na kuimarisha biashara.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana(Ijumaa, Mei 28, 2021) wakati akizindua Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Mara katika Ukumbi wa Bishop Rudin uliopo katika viwanja vya Mwembeni mjini Musoma. Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaagiza viongozi wa mkoa huo wahakikishe watendaji, wataalamu na wananchi wanakuwa nyenzo ya kurahisisha kazi ya kuvutia uwekezaji.

“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa hakikisha watendaji wote wa mkoa wanausoma na kuuelewa ipasavyo mwongozo huu. Hakikisha watendaji wako wanatekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na uaminifu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa”.

Waziri Mkuu amesema mkoa huo una fursa nyingi za uwekezaji ambazo endapo zitatumika vema, zinaweza kuipaisha nchi kimaendeleo. “…Nitoe wito kwa uongozi mzima wa mkoa uhakikishe unaratibu vilivyo shughuli za uzalishaji hasa wa malighafi, bidhaa na huduma mbalimbali kwa ajili ya wananchi na mahitaji ya viwanda vya ndani.

Amesema miongoni mwa maeneo ambayo mkoa wa Mara unaweza kunufaika zaidi kwenye uwekezaji kutokana na fursa zilizopo ni kilimo, mifugo na uvuvi. Serikali ilitoa maelekezo yenye lengo la kuboresha sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ili kuzalisha malighafi za kutosha zitakazotumika kwenye viwanda.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Uwekezaji ishirikiane na mkoa ili kuwezesha Kituo cha Uwekezaji cha Kanda (TIC) kilichopo mkoani Mwanza kuanzisha Kituo cha Kutolea Huduma kwa Pamoja (One Stop Centre) ambacho kinapaswa kuwa na rasilimali za kutosha, vifaa na wataalam wote muhimu.

“Watu wote muhimu wanaopaswa kutoa huduma katika kituo wawepo, wakiwemo wataalamu wa Ardhi, Biashara, Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO), Wakala wa Vipimo, NEMC, Bodi ya Nyama, Bodi ya Maziwa”.

Pia Waziri Mkuu ameziagiza idara zote za kisekta katika ngazi ya mikoa na wilaya, zishirikiane katika kubuni njia rahisi zitakazosaidia kuondoa urasimu na kurahisisha uwekezaji katika maeneo yao ili kuongeza ajira na vyanzo vya mapato ya Serikali.

“…Viongozi na watendaji wa sekta ya umma, fanyeni vikao na sekta binafsi kupitia Mabaraza ya Biashara ili kujadili na kutatua kero za kibiashara na uwekezaji zinazowakabili kwa wakati”.

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amezitaka mamlaka husika zihakikishe zinaweka mipango ya urasimishaji sekta isiyo rasmi, kurasimisha namba msimbo, kuwapatia wafanyabiashara ndogo ndogo maeneo ya kufanyia biashara na kuongeza kasi ya upimaji ardhi na kasi ya utekelezaji wa anuani za makazi na postikodi kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuchochea fursa za kibiashara.

(Mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,



Share:

BUNGE LAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Abdallah Ulega (katikati) wakipongezana mara baada ya Bunge kupitisha bajeti ya Wizara hiyo jana(28.05.2021) jana katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Kulia kwao ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Uvuvi nchini (TAFICO) Bi. esther Mulyila.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (kushoto) akiwashukuru na kuwapongeza Viongozi, Wakuu wa idara na vitengo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo nje ya ukumbi wa Bunge jijini Dodoma mara baada ya kuhitimishwa kwa mjadala wa bajeti ya Wizara hiyo jana (28.05.2021).

Viongozi, Wakuu wa idara na vitengo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo wakifuatilia hotuba ya bajeti ilivyokuwa ikiwasilishwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mashimba Ndaki juzi (27. 05. 2021) Bungeni jiini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (kushoto) wakizungumza na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Christine Ishengoma (katikati) muda mfupi baada ya bunge kupitisha bajeti ya wizara hiyo jana (28.05.2021) jijini Dodoma.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (katikati mbele), Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Abdallah Ulega ( wa nne kutoka kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel (wa tatu kutoka kulia), katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (wa nne kutoka kushoto), Wakuu wa idara na vitengo kutoka Wizara ya Mifugo na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuhitimishwa kwa mjadala wa bajeti ya Wizara hiyo Bungeni jijini Dodoma jana (28.05.2021).


Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana (28.05.2021) lilipitisha bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyolenga kutekeleza vipaumbele 13 kwa sekta zote mbili za Mifugo na Uvuvi.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya kuhitimishwa kwa mjadala wa bajeti ya Wizara hiyo ambapo baadhi ya wabunge walitaka kupata ufafanuzi wa baadhi ya masuala yanayohusu sekta hizo mbili ikiwa ni pamoja na kutaka kujua namna Wizara hiyo ilivyojipanga kuendelea kushughulikia changamoto za wafugaji na wavuvi.

Akizungumza wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara hiyo, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai mbali na kuishauri Serikali kuibinafsisha kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) ili kuongeza ufanisi zaidi, aliwapongeza viongozi na watendaji wa Wizara hiyo kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuimarisha sekta za Mifugo na Uvuvi nchini.

“Kuongoza na kuiendesha Wizara hii sio rahisi kwa sababu inashughulikia kundi kubwa sana la Wananchi na ni miongoni mwa Wizara iliyozalisha ajira nyingi zaidi na ndio maana kutokana na umuhimu wake niliona ni vizuri tuijadili kwa mapana zaidi” Alisisitiza Ndugai.

Ndugai alisema kuwa Bunge lake limekubali kupitisha kiasi chote cha fedha kilichoombwa na Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa sababu linaamini kuwa kama Serikali ikifanya uwekezaji kwenye Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi changamoto ya ukosefu wa ajira kwa Watanzania itapungua kwa kiasi kikubwa na hatimaye kumalizika kabisa.

Awali akianisha maeneo ya kipaumbele ambayo Wizara yake imejipanga kutekeleza kwa mwaka ujao wa fedha kwa upande wa Sekta ya Mifugo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki alisema kuwa Wizara yake imejipanga kuboresha na kutafuta masoko ya mifugo na mazao yake, kuboresha kosaafu za mifugo,kuboresha malisho na upatikanaji wa maji na vyakula vya mifugo.

“Mhe. Spika Wizara yetu pia kwa mwaka wa fedha ujao imedhamiria kuendelea kuimarisha afya ya mifugo, kuwezesha utafiti na mafunzo ya ugani na kutekeleza mpango wa kopa ng’ombe lipa ng’ombe na kopa mbuzi lipa mbuzi” Aliongeza Ndaki.

Akianisha maeneo ya vipaumbele ambayo Wizara yake imejipanga kuyatekeleza kwa upande wa sekta ya Uvuvi, Ndaki alisema kuwa kwa mwaka ujao wa fedha Wizara imejipanga kujenga bandari ya uvuvi na kununua meli tatu za uvuvi, kuimarisha mialo, masoko, vichanja vya kukaushia samaki, maghala ya ubaridi na mitambo ya barafu, kuweka mazingira wezeshi kwenye uvuvi wa bahari kuu na kuanzisha mashamba darasa ya ufugaji samaki katika Halmashauri 40 kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI.

“Mhe. Spika kwa upande wa sekta ya Uvuvi pia tunakusudia kuongeza uzalishaji wa vifaranga na chakula cha samaki, kuimarisha ulinzi shirikishi na matumizi endelevu ya rasilimali za uvuvi nchini na kuweka mifumo ya TEHAMA kwa ajili ya utambuzi wa maeneo ya mavuvi” Aliongeza Ndaki.

Bunge limepitisha jumla ya shilingi Bil. 47. 8 zilizoombwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa upande wa sekta ya Mifugo na shilingi Bil. 121. 4 ambazo zitatumika kwa upande wa sekta ya Uvuvi kwa mwaka ujao wa fedha 2021/2022.

Share:

WAJASIRIAMALI WAASWA KUZALISHA BIDHAA ZENYE BORA

 

**********************

Wajasiriamali kote nchini wameaswa kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kuweza kuhimili ushindani katika soko la ndani na kimataifa.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya SIDO kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Kwaraa Babati mkoani Manyara.

Naye Meneja wa Uthibiti Ubora wa TBS Bw.Gervas Mwanjabala akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho hayo, alisema maonesho hayo yamekuwa fursa muhimu ya TBS kutoa elimu ya masuala ya viwango kwa wajasiriamali waliokusanyika kutoka sehemu mbalimbali nchini na vilevile n fursa ya kusikiliza maoni na changamoto za wajasiriamali na wananchi kwa ujumla na kutafutia ufumbuzi changamoto hizo.

.“Ushiriki katika haya maonesho umetufanya tuweze kukutana na wadau wenye viwanda,wananchi, wajasiriamali na kuweza kuwaelimisha kuhusu masuala ya viwango pamoja na kusikiliza changamoto zao”. Amesema Bw. Mwanjabala.

Aidha Meneja wa kanda ya kaskazini wa TBS, Bi. Happy Brown aliwataka wajasiriamali wote katika kanda hiyo kutosita kutoa taarifa zozote ili waweze kusaidiwa na hata kupatiwa ushauri wa kitaalam ili waweze kuzalisha bidhaaa bora.

Kwa upande wake Afisa Masoko wa TBS Bi. Deborah Haule amesema muitikio wa watu katika maonesho haya umekuwa mkubwa na wajasiriamali wengi wamejitokeza kutaka kufahamu zaidi kuhusiana na taratibu za kufuata ili kuthibitisha ubora wa bidhaa zao.

Amesema wajasiriamali wadogo nchini hawaingii gharama zozote bali wanatakiwa kupitia SIDO ili watambulike na wakipata alama ya ubora wanaweza kufikia masoko mbalimbali hasa ya Afrika Mashariki na zitaweza kuvuka mipaka ya nchi hizo bila vikwazo vyovyote.

Pamoja na hayo Bi. Deborah amesema TBS inawahimiza wahakikishe wanazalisha bidhaa zilizo na ubora hatua itakayosaidia kulinda mitaji yao na kuhimili ushindani kwenye soko la kitaifa na kimataifa.

Share:

Mawaziri Sekta Ya Biashara EAC Wakubaliana Kuondoa Vikwazo Visivyo Vya Kibiashara


Na mwandishi wetu, Arusha
Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) la Jumuiya ya Afrika Mashariki lakubaliana kuondoa vikwazo visivyo vya kibiashara na kuimarisha biashara na uwekezaji ndani ya Jumuiya hiyo.

Awali akifungua mkutano Jijini Arusha jana Ijumaa, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwani utawawezesha mawaziri kupitia na kujadili miongozo ambayo itasaidia kuboresha biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo kuondoa vikwazo visivyo vya kibiashara. 

Aidha, Mhandisi Mlote ameongeza kuwa, kwa kuzingatia kanuni na sheria ya Afrika Mashariki, vikwazo visivyo vya kibiasha baina ya nchi na nchi vimekuwa vikizuia ukuaji wa biashara hivyo ni muhimu kupitia mkutano wa baraza la mawaziri kuangalia namna ya kuviondoa ili kuwezesha ukuaji wa biashara ndani ya jumuiya.

Nae Waziri wa Viwanda na Biashara, na Mkuu wa Ujumbe wa Tanzania, Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubaliana mambo mengi ya msingi ikiwemo kuendelea kuondoa vikwazo vya biashara visivyo vya kikodi.

“Tumezungumza pia kuhusu ushiriki wetu katika kufanya biashara na Uingereza kwa kuzingatia kuwa Uingereza siyo sehemu Jumuiya ya Ulaya, lakini pia tumezungumzia suala la EAC kujiunga na jumuiya ya biashara ya Afrika ambayo sisi Tanzania tupo katika hatua kadhaa na kuona kuwa na sisi tunajiunga na jumuiya hiyo mwaka huu,” Amesema Prof. Mkumbo

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Geofrey Mwambe amesema kuwa mawaziri wamekubaliana kutoa msukumo wa biashara katika jumuiya ya afrika mashariki lizingatiwe na kupea kipaombele na kuruhusu sekta binafsi kufanya biashara katika nchi mbalimbali.

“Pamoja na mambo mengine, pi tumekubaliana kuondoa vikwazo visivyo vya kiushuru (Non-tarrif barriers) viondolewe kwani vimekuwa vikikwamisha biashara bila sababu za msingi, na kuangalia jinsi ya kuwekeza kwenye eneo la uwekezaji ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuwa na mikakati ya pamoja ya kuvutia wawekezaji” amesema Mhe. Mwambe   

Miongoni mwa maeneo yaliyojadiliwa ni pamoja na maamuzi ya ripoti ya mawaziri wa fedha, ripoti ya kamati ya forodha, ripoti ya kamati ya biashara, ripoti ya kamati ya viwango ya Afrika Mashariki, ripoti juu ya masuala ya ushindani pamoja na ripoti ya kamati ya uwekezaji.

Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara kutoka Kenya Mhe. Betty Maina, Waziri wa Viwanda na Biashara, – Tanzania, Prof. Kitila Mkumbo,  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Geofrey Mwambe, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Mhe. Omar Said Shaaban.

Wengine ni Waziri wa Biashara na Viwanda wa Rwanda, Mhe. Beata Habyarimana, Waziri wa Biashara, Viwanda na Ushirika wa Uganda, Mhe. Grace Choda, pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara, Uchukuzi, Viwanda na Utalii wa Burundi, Balozi Jeremie Banigwaninzigo.

Mkutano huu ni maelekezo ya Wakuu wa Nchi na Serikali katika ziara ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoifanya nchini Kenya tarehe 04 hadi 05 Mei, 2021.



Share:

Promosheni Supa Friday-shinda Fridge, Tv Decorder Na Safari Ya Mikumi.

 


Kampuni ya simu TECNO imezindua rasmi promosheni ya SUPA FRIDAY jana katika duka la TECNO Smart Hub lililopo Kariakoo. Uzinduzi huo uliudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali kutoka kwenye kiwanda cha Sanaa kama vile Elizabeth Michael, Idrisa Sultan, Angel Nyigu na Jihan Mark.


Promosheni ya SUPA FRIDAY itakuwa ikifanyika kila ijumaa na ambapo simu za TECNO Camon zitakuwa zikiuzwa kwa bei pungufu lakini pia zawadi mbalimbali kutolewa kama vile Fridge, Drones, DSTV Decoder na zawadi nyenginezo kama ticket yakwenda kutembelea Mbugani.

   


Wakati wa uzinduzi huo Msanii maarufu kutoka kwenye kiwanda cha filamu alisema, “simu ni kamera na TECNO wamelizingatia hilo kwenye simu hii ya TECNO Camon 17, naipenda sana simu yangu MP48 za selfie na MP 64 za kamera ya nyumba zinanifanya nionekane mrembo wakati wote ningependa nikushauri wewe mfanyabiashara kupitia mitandao ya kijamii nunua TECNO Camon 17pro kwani picha zake zinaendana na uhalisia wa bidhaa yako inavyoonekana”.
   

Lakini pia wateja walioenda kununua simu siku ya jana walikuwa na haya yakusema kuhusiana na bidhaa na promosheni ya SUPA FRIDAY, “Tunaishukuru sana kampuni ya simu TECNO imekuwa ikizingatia wateja wake wote hadi sisi wenye uchumi mdogo lakini tungetamani kumiliki simu ya TECNO Camon 17, SUPA FRIDAY imetimiza ndoto zangu kupitia ofa ya punguzo la bei na mimi sasa namiliki TECNO Camon 17  sasa nina uwezo wakuhifadhi picha, video na files nyengine kibao GB128 kwa 8ram zinanitosha kabisa sihitaji memory ya ziada alisikika akisema moja wa wateja wa TECNO Camon 17”. 


TECNO Camon 17 inapatikana katika maduka yote ya simu ikiambatana na ofa ya GB78 za bundle la internet kutoka Tigo. 


Tembelea www.tecno-mobile.com
 

 
 
 
 



Share:

Tiba Bora Ya Tatizo La Nguvu za Kiume


Baada ya kuchambua mambo yanayosababisha upungungufu wa nguvu, kukosa ham ya tendo na maumbile madogo , leo tutachambua baadhi ya dalili na tiba.

    *DALILI NI KAMA:-

1.Kukosa ham ya tendo
2.Kuwahi kufika kelele ni
3.Kushindwa kurudia tendo
4.Maumbile kusinyaa katikati ya tendo
5.Kuchoka sana baada ya raundi moja
6.Kusimama kwa ulegevu

    *TIBA SAHIHI

1.GING SENG PILLS @220,000/=
>Hivi ni vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza ham na nguvu za kiume hata kwa wenye kisukari

2.VIGRX OIL @220,000/=
>Huongeza Maumbile  kwa 6-7 inch ndani ya wiki mbili

3.BIG PENIS, VIMAX, GOOD MAN @270,000/= (Vidonge)
>Huongeza  nguvu za kiume na kuimarisha misuli hata kwa waliothiriwa na kujichua

4.HANDSOME UP @270,000/=
>Mashine hii huongeza maumbile kwa saizi unayotaka pamoja na kuimarisha misuli

5.VIGA SPRAY @180,000/=
>Huchelewesha kufika kileleni na kuongeza parfomance.

       Tiba hizi zote zimefanyiwa majaribio na zimethibitishwa. Matokeo ni uhakika na garantii.

            Fuatilia huduma na vipindi vyetu ktk mitandao ya kijamii ili kupata ushauri na tiba.

           ***YOU TUBE***
           Markson Beauty

   *GOOGLE/FACE BOOK*
Markson Beauty Products

         ***INSTAGRAM***
      @markson_beauty_pr
      @markson_beauty_pr

    Wasiliana nasi popote ulipo duniani kwa call/whatsapp no (+255)

           0767447444
                     na
           0714335378
        

                TAHADHARI:- Hakikisha ndani ya bidhaa kuna mhuri, risiti na kadi ya garantii ktk bidhaa unayonunua kwenye kampuni hii.
 
     FREE DELIVER IN:-
*D'salaam
*Arusha
*Morogoro
*Mwanza
*Moshi

#HipsNaMakalio
#BidhaaTz
#YodiPillsTz
#BotchoOg
#CosmeticsTz
#WeupeBilaDoa
#FashionsTz
        
   MARKSON BEAUTY CO
    #HOUSE OF BEAUTY#

         < WELCOME ALL>
.

Share:

IGP Sirro Awataka Askari Polisi Kutenda Haki


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka askari kuhakikisha wanaendelea kutenda haki kwa wananchi wanaowahudumia na kushirikiana nao katika kuzuia na kupambana na uhalifu nchini.

IGP Sirro amesema hayo Dar es salaam, wakati akizungumza na baadhi ya wananchi  wa eneo la Kawe wilaya ya Kinondoni ambapo aliwataka wananchi kuacha kutoa rushwa kwani kitendo hicho ni kinyume na sheria za nchi.

Aidha, IGP Sirro ameendelea kuwasisitiza viongozi wa serikali hasa watendaji wa kata na wenyeviti wa serikali za mitaa kuwashirikisha wananchi katika vikundi ya ulinzi shirikishi ili maeneo yao yaendelee kuwa salama.


Share:

Mkutano Wa Afya Wa Dunia Wajadili Umuhimu Wa Kuimarisha Mifumo Ya Ndani Ya Nchi Katika Kukabiliana na Magonjwa.


Na WAMJW- DOM.
Wataalamu wa Afya wa nchi 194 wamejadili namna ya kuboresha na kuimarisha mifumo ya ndani ya utoaji wa huduma za Afya ili kuzisaidia nchi wanachama kuwa tayari katika kukabiliana dhidi ya magonjwa mbali mbali ikiwemo magonjwa ya mlipuko.

Hayo yamejadiliwa katika Mkutano wa 74 wa Afya Duniani unaoendelea kupitia njia ya mtandao wenye lengo la kujadili mikakati mbali mbali na Sera za Afya ili kuboresha utoaji huduma za Afya kwa wananchi katika nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Katika kikao hicho jumla ya nchi 194 zimeshiriki, ikiwemo nchi ya Tanzania na kutoa mikakati mbali mbali inayotekelezwa na nchi katika mapambano dhidi ya magonjwa mbali mbali ikiwemo ugonjwa wa Corona.

Kauli mbiu ya Mkutano huo ni “Komesha ugonjwa wa COVID-19 sasa, zuia ujao, ili kujenga pamoja Ulimwengu wenye afya na salama( Ending this Pandemic, Preventing the next, Building together a healthier, safer and fairer World).

Nchi wanachama, ikiwemo Tanzania zimeonesha mikakati mbali mbali iliyochukuliwa hasa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona ikiwemo kuanzisha viwanda vya kutengeneza Barakoa (Mask), vipukusi (sanitizer) na nguo maalum za kujikinga watoa huduma wa Afya wakati wa kumuhudumia mgonjwa mwenye maambukizi ya Corona.

Mbali na hayo, nchi wanachama zimeshauriwa kuanzisha chombo cha kimataifa (International instrument) kitachoweza kusaidia kuweka mikakati mizuri katika kukabiliana dhidi ya magonjwa ya mlipuko na kutatua changamoto zitakazojitokeza hasa katika mlipuko wa ugonjwa wa Corona kwenye upatikanaji wa chanjo, vifaa vya kujikinga pamoja na teknolojia.

Aidha, Mkutano huo wa Wataalamu umependekeza nchi wanachama zitafakari faida ya kuwa na chombo hicho (International instrument) kitakacho rahisisha mapambano dhidi ya magonjwa mbali mbali ili kupeleka hoja hiyo kwa Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama zote Duniani kujadiliwa na kupitishwa.

Mkutano wa Afya wa Dunia (Word Health Assembly) hufanyika kila mwaka nchini Geneva,kutokana na janga la Corona kwa miaka miwili Sasa unafanyika kwa njia ya mtandao.Mwaka huu mkutano huo umeanza kufanyika tarehe 24 Mei Hadi 1June, 2021.


Share:

Waziri Ummy Ameagiza Kusimamishwa Kazi Kwa Wakuu Wa Idara Wanne Kupisha Uchunguzi


Angela Msimbira, SHINYANGA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu ameagiza kusimamishwa kazi wakuu wa Idara Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kushindwa kusimamia kwa weledi ukamilishaji wa ujenzi wa Machinjio ya kisasa iliyopo Ndembezi mjini Shinyanga ili kupisha uchunguzi kwa tuhuma zinazowakabili.

Akikagua mradi huo jana katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga Waziri Ummy amesema kuwa amewasimamisha kazi wakuu hao wa idara kwa kushindwa kutimiza wajibu wao wa kumshauri Mkurugenzi kuhusu mradi huo na kushindwa kusimamia ujenzi huo ili uweze kukamilika kwa wakati.

Amewataja waliosimamishwa kupisha uchunguzi kuwa ni aliyekuwa Kaimu Afisa Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji Bw. Gwakisa Mwaisyeba, Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Dkt Tito Kagize, Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi Kassim Thadeo na Mkuu wa Kitengo cha manunuzi Bw.Godfrey Mwangailo na amemuagiza Mkuu wa Mkoa Bw.Dkt Philemon Sengati kuhakikisha anaunda tume itakayochunguza ubadhilifu wa fedha ambao umesababisha kusuasua kwa ujenzi wa Machinjio hiyo.

Waziri Ummy amesema kutokamilika kwa Mradi wa Machinjio ni aibu kwa watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na inarudisha nyuma maendeleo ya Manispaa hiyo.

‘Ukamilishaji wa machinjio hii kutasaidia kuongeza mapato ya wananchi na Halmashauri kwa ujumla kwa kuwa Halmashauri ikikusanya mapato itaweza kutatua changamoto katika Sekta ya Afya, Elimu na miundombinu ya barabara’ alisema

Mbali na kuwasimamisha Wakuu hao wa Idara pia ameitaka Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuwaandikia barua Mkandarasi wa mradi huo , Kampuni ya Home Africa pamoja na Mhandisi mshauri B.J Amour nao wapelekwe bodi ya Mkandarasi ili iwawajibishe.

“ Mradi huu haukusimamiwa vizuri na tunawatesa watu wa shinyanga mpaka leo haujakamilika na fedha hazionekani, kuna shilingi milioni 800 zimelipwa kwa wakandarasi bila kuhakikiwa wala kujiridhisha. Huu mradi ni aibu kwa Shinyanga kwa hiyo nawasimamisha kazi kwa wiki mbili ili wapishe uchunguzi” amesema Waziri Ummy

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amesema kuwa mradi huo ulitengewa kiasi cha shilingi bilioni 5.7 lakini hadi sasa zimetumika kiasi cha shilingi bilioni 5.1 na shilingi milioni 600 hazijulikani zilipo wakati mradi haujakamilika, amesisitiza kuwa katika ripoti ya mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) ilieleza kuna ufisadi na mradi haukukamilika vizuri.

Hatua hiyo ya Waziri Ummy imekuja baada ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila kueleza kuwa kamati ya fedha ya halmashauri hiyo kupitia baraza la madiwani walikuwa wameanza kuchukua hatua baada ya kubaini kuwa thamani ya fedha katika mradi huo hairidhishi, huku akibainisha kuwa kupitia vyanzo vya ndani watatenga shilingi milioni 172 kwa ajili ya kukamilisha machinjio hiyo.

Machinjio hiyo ilianza kujengwa mwaka 2018 na ilitazamiwa kukamilika mwaka2019 na kuanza kutoa huduma lakini maendeleo yake yamekuwa yakisuasua na kusababisha baadhi ya viongozi kuilalamikia.


Share:

Serikali Haijaruhusu Kilimo Cha Bangi



Share:

Tangazo La Nafasi Za Kujiunga Na Masomo Chuo Cha Wanyamapori Pasiansi Jijini Mwanza Mwaka 2021/2022



Share:

Zaidi Ya Sh.bilioni 17 Kutumika Kujenga Chuo Kipya Cha Ufundi Dodoma​

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inajenga Chuo cha Ufundi katika Mkoa wa Dodoma chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 5000 ili kuongeza wigo na fursa za upatikanaji wa ujuzi na maarifa.​

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa chuo hicho uliofanyika Jijini Dodoma, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo amesema ujenzi wa chuo hicho utagharimu zaidi ya Shilingi bilioni 17 kupitia mradi wa Kukuza Ujuzi na Stadi za Kazi (ESPJ) unaosimamiwa na Wizara.​

Katibu Mkuu huyo ameitaka kampuni iliyoshinda zabuni ya ujenzi wa chuo hicho, CRJE East Africa Ltd. kuhakikisha inakamilisha ujenzi huo ndani ya miezi 18 kama Mkataba unavyoonyesha.​

“Leo tumesaini mkataba wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma, ni matarajio yangu kitakamilika kwa wakati na​ubora unaotakiwa ili malengo ya kuanzishwa kwa chuo hiki yaweze kutimia,” amesema Dkt. Akwilapo.​

Naye Meneja wa kampuni ya CRJE East Africa Ltd. tawi la Tanzania, Xu Cheng ameahidi kutekeleza mradi huo​ kwa ubora unaokubalika na kuhakikisha unakamilika kwa wakati uliopangwa.​

Mradi huo utahusisha ujenzi wa miundombinu ya Jengo la Utawala, Ofisi za Idara, nyumba za watumishi, mabweni, Zahanati, Vyoo vya wanafunzi na watumishi, karakana tatu na kituo cha kupoza umeme.​


Share:

JAMAA ACHOMA MOTO NYUMBA YA MAMA MKWE BAADA YA MKE KUTOROKA

Maafisa wa polisi eneo la Kiminini kaunti ya Trans Nzoia nchini Kenya wanamsaka jamaa mmoja mwenye umri wa makamo aitwaye Amos Wanjala ambaye anadaiwa kuvamia makazi ya mamake mkwe na kuchoma malazi yake.

Inaelezwa kuwa Amos Wanjala alitekeleza kitendo hicho baada ya mkewe kumtoroka.

Akiwa mwenye ghadhabu, Wanjala alivamia boma la Mercyline Wanyama Alhamisi, Mei 28,2021 mwendo wa saa tano usiku, alimuasha mama mkwe na kisha kuchoma malazi na baadhi ya nguo zake.

Mama huyo alisema alipoteza mali inayogharimu zaidi ya KSh 6,000 kwenye mkasa huo na hadi kwa sasa anashangaa ni nini kilichomfanya mkwe wake kumvamia.

Mshukiwa anasemekana kumtishia maisha mama huyo, hii ni kulingana na OCPD wa Kiminini Francis Tumbo.

Tumbo alisema mshukiwa akikamatwa, atashtakiwa kwa uharibifu wa mali na pia kumtishia maisha mama huyo.

"Akishakamatwa, atashtakiwa kwa kosa la kuharibu mali," OCPD huyo alisema.

Kwa mujibu wa taarifa za The Standard, mkaaji mmoja aliyetambulika kama Juma Barasa ametaka mshukiwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa ajili ya kukiuka mila.

"Ni kinyume na ukoo wa Wabukusu kwa mtu yeyote kuwashambulia wakwe zake ama kuharibu mali yao," Barasa alisema.

Mmoja wa majirani amesema kwamba Wanjala atapigwa faini ya mbuzi ambayo itachinjwa kwenye sherehe ya utakaso.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo May 29



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger