Sunday 2 May 2021

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo May 02



Share:

Saturday 1 May 2021

Maajabu ya Dunia : HII NDIYO MIMEA 7 INAYOKULA NYAMA NA WADUDU

Mimea mingine hukua mahali ambapo haiwezi kupata virutubisho vyote vinavyohitaji kutoka kwenye mchanga. Ili kuhakikishi mimea hii inapata madini hayo bila kupungua, mimia hiyo hutega, kukamata na kisha kuwala wadudu. Mtego wa kukamata nzi wa Venus (Venus-flytrap) ni mmea ulio na majani yaliyoumbwa mfano wa mdomo ambao hufunga wakati nzi wanapotua hapo. Majani ya mmea wenye umbo la mtungi (pitcher plant) nayo ni mtego wenye utelezi ambao una majimaji ya kumeng'enya ndani. Wadudu na wanyama wanapoanguka humo humeng'enywa.

1. Venus Mtego wa nzi (Venus Flytrap)
Mtego huu wa nzi ni moja ya mimea (jina la spishi Dionaea muscipula) inayojulikana zaidi ambayo hula nyama na hula zaidi wadudu na wale wenye miguu minane (arachnids). Mmea mdogo ulio na majani karibu manne hadi saba ambayo hukua kutoka kwenye shina fupi, na kufanya mitego. Kulingana na Listverse, mmea huo ni wa kushangaza sana kwani unaweza kutambua tofauti kati ya hai na kilichokufa na majani hayo yenye mitego huweza kufunga kwa sekunde 0.1. Ingawa kuna aina moja tu ya spishi ya Venus Flytrap, kuna aina nyingi.

2. Midumu-mwitu (Monkey cups)
Hupatikana katika maeneo ya tropiki mfano Borneo, Sumatra na Malaysia. Mmea huu (jina la spishi Nepenthes) unaokula nyama unaitwa hivyo kwa kuwa nyani wameonekana wakinywa maji yanayojikusanya kwenye vikombe vyake kwenye maeneo ya mvua nyingi misituni, kwa mujibu wa kitabu kinachoitwa Hungry Plants, majani ya mmea huu ambayo huwa mfano wa jagi la maji (pitcher) huweza kuhifadhi maji kiasi cha zaidi ya lita. Vikombe hivyo hukusanya maji ambayo hutumia kumeng'enya wadudu.

3. Umande wa jua (Sundew)
Kuna karibu spishi 200 za Sundew, na zote hutofautiana sana kwa sura, saizi na mahitaji ya kukua. Nyingi ya spishi hizo (Drosera) zimefunikwa kwenye nyuzi ambazo zina ncha zenye gundi, na ripoti ya Carnivorous Plants UK inasema kwamba nyuzi hizi zinaweza kusonga, na kusaidia kwa haraka kukamata, kunyonga na kutafuna wadudu ambao watakuwa wamekamawama.

4. Butterworts
Butterworts, au mitego ya karatasi yenye dutu za kunata zilizo na sumu unaweza kuwa hai au ya kuwa kimya na kutegemea kamasi inayonata kwenye jani kukamata mawindo. Spishi hii ya Pinguicula ambayo ipo katika orodha ya maua yanayodondoka rahisi (orchid), pia hujulikana kwa maua yake ya kupendeza kwa rangi ya manjano, nyekundu, zambarau au nyeupe. Mimea hii ya kumeng'enya hupenda kula mbu na kawaida hupatikana huko Marekani.

5. Vifuko vya kunyonya (Bladderworts)
Jina hili linatokana na vifuko vidogo vinavyopatikana kwenye mmea huu (jina la spishi genus Utricularia) na ni aina ya mmea katika jamii ya inayokula nyama na hupatikana kwenye maji wazi na hunasa wadudu kwenye kifuko mfano wa balbu inayonyonya. Kulingana na Botanical Society of America, nywele ndogo za kugusa mlangoni pa kifuko hujua wakati wadudu, mfano nzi, wanapotua kwenye mmea huo, ambao husababisha kifuko kilichosinyaa au kulegea kutanuka mara moja, kikanyonya maji, na kumfungia kisha kumla mnyama huyo.

6. Mimea yenye mtungi wa kunasia kamba (Lobster-pot plants)

Jina hili linatokana na mtungi uliotumiwa na wavuvi kunasia samaki aina ya kamba (lobsters), mmea huu (Jina la spishi ni Darlingtonia californica) hula nyama na hunasa mawindo yake yanapoingia kwenye mtego wake, ambao unafanana na mtungi wa kunasia kamba. Windo hushindwa kufahamu njia ya kujinasua, na nywele kwenye mtego huo hujikunja na kulazimisha windo kwenda chini ya jani ambapo humeng'enywa.

7. Mtengo wa manati ya kunasa nzi (Catapulting flypaper trap)
Aina hii ya mimea ambayo hula nyama ina sifa zote mbili za (kama vile Butterworts) na kunasa (kama Venus mtego wa nzi). Kuenea kwake zaidi ni Australia, mmea huu (Jina la spishi ni Drosera glanduligera) wa kula nyama hunasa mawindo yake kwa kutumia nyuzi zake za nje zenye kunata. Wakati mawindo yanapoweka shinikizo kwenye vishina hivi, chembe za chini za mmea huachia na kufanya windo lililonaswa kuelekea katikati ya mmea, ambapo huliwa.


Share:

RAIS MWINYI : TUTAPANDISHA MISHAHARA KWA WATUMISHI KADRI UCHUMI UTAKAVYOIMARIKA



Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema Serikali itapandisha mishahara kwa watumishi wa kada ya kati kadri uchumi utakapozidi kuimarika.

Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Meimosi, 2021 katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-Wakil Kikwajuni, Zanzibar.

Amebainisha kuwa wafanyakazi hao ni muhimu katika maendeleo na ndio kada yenye wataalamu wakiwemo walimu na watumishi wa sekta ya afya.

Amesema Serikali ilikuwa na nia njema ya kuimarisha mishahara kwa wafanyakazi wa ngazi zote kwa awamu tatu, hata hivyo hatua hiyo ilishindwa kutokana na kuibuka kwa ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Amesema ugonjwa huo uliathiri ukusanyaji wa mapato hivyo utaratibu huo kuishia katika kuimarisha viwango vya mishahara ya kima cha chini hadi kufikia Sh300,000.
Share:

SERIKALI YAAGIZA WENYE ELIMU YA DARASA LA SABA WALIOONDOLEWA KAZINI WALIPWE STAHIKI ZAO



Serikali imeagiza wafanyakazi wote wenye elimu ya darasa la saba walioondolewa kazini lakini hawakughushi vyeti walipwe mafao na stahiki zao zote.

Agizo hilo limetolewa leo Jumamosi Meimosi, 2021 mkoani Mwanza na Rais Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihutubia kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi iliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza.

"Wapo waliosita kutekeleza maelekezo ya malipo haya kwa kisingizio cha kutotolewa mwongozo, mwongozo ndio huo sasa nimetoa," amesema Rais Samia.
Share:

Waziri Kalemani Apiga Marufuku Uagizaji Wa Vikombe (Insulators) Kutoka Nje Ya Nchi


Na Teresia Mhagama, Dar es Salaam
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani amepiga marufuku uagizaji wa vikombe (insulators) kutoka nje ya nchi baada ya uzalishaji wa vikombe hivyo sasa kufanyika nchini.

Dkt.Kalemani ametoa agizo hilo tarehe 28 Aprili, 2021 baada ya kukagua shughuli za uzalishaji wa vikombe hivyo katika Kiwanda cha Inhemeter kilichopo wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

“Nilikuja hapa mwezi Novemba mwaka jana kukagua uzalishaji wa mita za umeme na nikatoa agizo kuwa vikombe navyo visiagizwe nje ya nchi na viwanda vya uzalishaji wa vikombe vijengwe ndani ya nchi, hivyo nimekuja kufuatilia agizo hilo na kujiridhisha kama vikombe vinazalishwa au havizalishwi.” Amesema Dkt.Kalemani

Baada ya kufanya ukaguzi katika kiwanda hicho, Dkt. Kalemani amesema kuwa, amejiridhisha kuwa kiwanda  kinazalisha vikombe takriban milioni 1.5 kwa mwaka  na pia kiwanda kingine cha Africab kinazalisha vikombe Milioni Moja kwa mwaka huku mahitaji kwa sasa yakiwa ni vikombe Milioni M1.8.

Kutokana na uzalishaji huo, Dkt.Kalemani ameeleza kuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na wakandarasi wa umeme wanunue vikombe na vifaa vingine vya umeme vinavyozalishwa ndani ya nchi, hali itakayopelekea wananchi kuunganishiwa umeme kwa kasi.

Ameeleza kuwa, kuna faida mbalimbali za kuzalisha vifaa hivyo ndani ya nchi ikiwemo vifaa husika kupatikana kwa bei nafuu kulinganisha na vifaa vinavyoagizwa kutoka nje ya nchi, vifaa hivyo kutengenezwa kwa ubora na kuongeza ajira ndani ya nchi.

Aidha, ameipongeza kampuni hiyo kwa kuzalisha vifaa hivyo na kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania takriban 150.

Ametoa wito kwa watendaji wa kiwanda hicho kuongeza uzalishaji wa vikombe hivyo ambavyo hufungwa katika miundombinu ya usafirishaji na usambazaji umeme ya uwezo tofauti ikiwemo 11kV, 33kV na 400kV.

Insulators (vikombe) hufungwa kati ya nguzo na nyaya za umeme kwa lengo la kuzuia umeme huo kusafiri kupitia kwenye nguzo na baadaye kuleta madhara mbalimbali ikiwemo ya moto.

Katika ziara yake jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nishati aliambatana na watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).


Share:

NILISEMWA SANA KUWA MIMI NI MCHAWI WA MTAA KWA MIAKA 4,ILINIUMA KUSINGIZIWA JAMBO AMBALO SIFANYI

Sisi Binadamu tunakutana na mambo mengi sana katika maisha yetu ya kila siku hapa duniani.Mimi kwa majina naitwa Mama Fatuma mkazi wa Makumbusho -Dar es salaam,umri wa miaka 50 sasa. 

Nimeweza kukutana na changamoto kubwa sana katika maisha yangu kwanza mimi najishughulisha na kupika vitumbua hapa Makumbusho. Kazi yangu imenisaidia kuweza kukuza watoto wangu,kuwasomesha,chakula na kupata mavazi.

Nimeweza kukutana na maneno mengi kutoka kwa watu mbalimbali na wengine kuniita mchawi hali ya kuwa sijawaroga au sijui kuroga mtu,jambo lolote ambalo limetokea mtaani watu kunishuku mimi hali ya kuwa mimi sijui jambo lolote.

Hali hiyo ilinikosesha raha na kujiuliza kwa nini mimi. Kwa jambo lolote baya watu wanahisi ni mimi na kibaya zaidi baadhi yao  wakaanza kuniita mchawi. Kitendo cha kuniita mchawi kiliathiri biashara yangu ya kupika vitumbua, watu waliacha  kununua vitumbua vyangu ,hivyo hali yangu ya kiuchumi ilizidi kuwa mbaya hadi watoto wangu wakashindwa masomo .

Ilinibidi niache kupika vitumbua na kuanzisha Biashara ya kutembeza mboga mboga katika mitaa mbalimbali hapa Jijini Dar .Nilifanya Biashara hiyo kwa miezi 2 ila hali ikabadilika na kuwa ile ile ya kuitwa mchawi,mtu leo akinunua kitu kwangu kesho hataki tena hata wateja ambao nilikuwa nimeisha wazoea ilifika hatua wakaanza kufunga milango yao wakiniona  nakuja na Beseni yangu ya mbogamboga.

Hali hiyo iliniumiza sana moyoni mwangu ikabidi nimwambie rafiki yangu wa karibu ambaye nilikuwa natembea nae kuuza mbogamboga kwa sababu nilihisi huenda kuna kitu ambacho siyo kizuri kwangu. Nimeacha Biashara ya kupika vitumbua kisa watu wanasema kuwa mimi ni mchawi na kukosa wateja kabisa,nimeanza Biashara ya kuuza mboga tena kwa mitaa ambayo Hata hawajui naishi wapi bado wameanza kuniita mchawi na kufunga milango yao wakiniona.

Ndipo rafiki yangu akaniambia kuwa Dr. Kiwanga anaweza kunisaidia shida gani niko nayo kwa sababu siyo hali ya kawaida na akazidi kuniambia kuwa Dr huyo huyo alimsaidia kaka yake kurudisha mke wake nyumbani baada ya kuachana kwa miaka 2. Nikamuomba mawasiliano ya Dr.kiwanga akanipatia address hii,Namba ya simu:+254 769404965 ,Website: www.kiwangadoctors.com,Email:kiwangadoctors@gmail.com

Niliongea na Dr na kumueleza kuwa maisha yangu jinsi yalivyo pia nikamwambia kuwa sina uwezo wa kufika ofisini kwake Nakuru-Kenya ila naitaji usaidizi wake kwa sababu maisha yangu kila kukicha yanakuwa mabaya sana hata jambo ambalo nafanya sipati mafanikio.

Ndipo Dr. Kiwanga akasema kuwa nitapata kisha akaniambia nisubiri kwa muda wa Dakika 35 nimtumie ujumbe WhatsApp. Baada ya dakika 35 kuisha nilifanya kama alivyo kuwa umeniambia ndipo akasema kuwa shida yangu kubwa ni Badluck,Hivyo atanisaidia na Goodluck spells na ndani ya siku 3 nitakuwa na mafanikio.

Katika maongezi na Dr. kiwanga aliniambia kuwa anatatua shida mbalimbali kama kurudisha mpenzi,kusafirisha Nyota,kuwa na mvuto wa Biashara,Kupata mtoto au mimba kwa walio kosa kwa muda mrefu,kufunga mme au mke asiende nje ya ndoa .Dr. Kiwanga alizidi kunieleza kuwa anatibu magonjwa sugu kama Kisukari,Pressure,Diabetes,TB na Syphilis kwa kutumia madawa ya miti shamba.

Baada ya siku 3 kupita nilishanga wateja wangu wamerudi tena hata wengine wakaanza kunipigia simu kuwa wanaitaji mbogamboga na kwa sasa nimefungua duka la kuuza nataka hapa Makumbusho. Asante Dr. Kiwanga kwa huduma yako leo hii napendwa mtaani kwangu,nimejenga sina mtu wa kuja mlangoni kwangu na kudai kodi,wateja ninapata

Unaweza mpata Dr.kiwanga kwa kupiga/WhatsApp +254 769404965au tembelea website yao www.kiwangadoctors.com  kwa taarifa zaid.Dr.  Kiwanga na mungu anaponya.

Share:

RAIS KENYATTA ATANGAZA KUONDOA AMRI YA KUINGIA AU KUTOKA KAUNTI 5 HATARI KWA COVID - 19



Na  Sammy Waweru 

RAIS Uhuru Kenyatta Leba Dei ametangaza kuondoa amri ya ama kuingia au kutoka kaunti tano zilizotajwa kuwa hatari katika maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19.

Machi 26, 2021, serikali iliweka amri hiyo katika kaunti ya Nairobi, Machakos, Kajiado, Kiambu na Nakuru, kufuatia kile kilisemekana kuwa hatari katika msambao wa virusi vya corona.

Katika hafla ya maadhimisho ya Leba Dei 2021 mnamo Jumamosi, Rais Uhuru Kenyatta alitangaza kuiondoa ila kwa masharti.

“Kuanzia leo (Jumamosi), usiku wa kuamkia Jumapili amri ya ama kuingia au kutoka kaunti tano zilizokuwa hatari katika maambukizi itaondolewa,” akasema Rais Kenyatta, kupitia hotuba yake katika Ikulu, jijini Nairobi.

Aidha, kiongozi huyo wa nchi pia alitathmini saa za kafyu katika kaunti hizo kutoka saa mbili jioni na kutangaza kuwa itakuwa ikianza saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri, sawa na maeneo mengine ya taifa.

“Kwa mujibu wa wataalamu, maambukizi katika kaunti tulizokuwa tumefunga yameshuka kwa asilimia 72, na sehemu zingine za nchi kwa asilimia 89 kati ya Machi 2021 na Aprili,” Rais akaelezea.

Kufungwa kwa kaunti tano zilizoathirika zaidi kulichangia wengi kuhangaika, ikizingatiwa kuwa ni maeneo yanayosaidia kupiga jeki uchumi wa nchi.
Share:

RAIS SAMIA : TUNATARAJIA KUAJIRI WATUMISHI 40,000...MISHAHARA TUTAPANDISHA MWAKANI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema jumla ya wafanyakazi zaidi ya 85,000 elfu hadi 91,000  watapanda vyeo mwaka ujao na  kuajiri watumishi  40,000 katika Idara ya Elimu na Afya.

Ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Kitaifa leo Mei 1, 2021 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

"Ndugu zangu mimi ni mama, mama ni mlezi..Dai hili ni la msingi na la kweli. Mishahara haijaongezwa muda mrefu. Kutokana na mlipuko wa ugonjwa Corona uwezo wetu kiuchumi umepungua, imekuwa vigumu kwangu kuongeza mishahara lakini tutaboresha maslahi ya wafanyakazi", amesema Rais Samia.

"Mishahara haijaongezwa kwa muda mrefu, Mimi binafsi natamani kuongeza mishahara mwaka huu ila kwasababu mbalimbali nimeshindwa, uchumi wa Tanzania umeshuka kutoka 6.9% hadi 4.7% kwasababu ya Corona, nawaahidi mwakani siku kama ya leo nitapandisha mishahara", amesema Rais Samia
 


Share:

Picha : MATUKIO MBALIMBALI KWENYE MAADHIMISHO YA MEI MOSI 2021 JIJINI MWANZA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwasili katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Kitaifa leo Mei 1, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Kitaifa leo Mei 1, 2021.
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa ukiwasili katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Kitaifa leo Mei 1, 2021.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasili kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza tayari kwa maadhimisho ya Mei Mosi.
Baadhi ya wafanyakazi walioshiriki katika maadhimisho hayo wakiwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwasili uwanjani.
Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo akiwasili kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Yustino Ndugai akiwasili kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Isdory Mpango akiwasili kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. Philip Isdory Mpango akiteta na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa.
Baadhi ya wafanyakazi wakimlaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwasili.
Wafanyakazi wa Wizara mbalimbali, Mashirika ya Umma, Taasisi za Serikali pamoja na Sekta Binafsi wakiwa kwenye maandamano wakati wa sherehe za Mei Mosi, zinazofanyika katika Uwanja wa Kirumba, jijini Mwanza.









Share:

WATUMISHI WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WASHIRIKI MAANDAMANO YA MEI MOSI JIJINI DODOMA


Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa kwenya maandamano kuelekea uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger