Friday 27 November 2020

Hatma ya Halima Mdee na Wenzake Kujulikana Leo


 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo Ijumaa tarehe 27 Novemba 2020, kinafanya kikao maalum cha kamati kuu kuwajadili wanachama wake 19 wanaodaiwa kukisaliti kwa kukubali uteuzi wa ubunge viti maalumu.

Kikao hicho, kinafanyika jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.

  Wanachama hao 19 wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee wanajadiliwa baada ya tarehe 24 Novemba 2020 kwenda bungeni jijini Dodoma kuapishwa na Spika Job Ndugai.

Kutokana na tuhuma hizo za usaliti, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alitangaza kufanyika kwa kamati kuu leo Ijumaa na kuwataka kufika makao makuu ya Chadema, Kinondoni Dar es Salaam saa 2:00 asubuhi.


Share:

Watu 6 akiwemo Padri Sixtus Masawe wafariki dunia katika ajali ya gari


Jumla ya watu 6 akiwemo Padre Sixtus Massawe, paroko wa parokia ya Masakta Babati, mkoani Manyara, wamefariki dunia kufuatia ajali ya gari baada ya gari yao kuligonga lori kwa nyuma, maeneo ya kambi ya kijeshi ya Sofa iliyopo mkoani Arusha, wakati wakitoka kwenye msiba wilayani Rombo.

Taarifa hiyo imetolewa Novemba 26, 2020, na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Salum Hamduni, ambapo ameeleza kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 8:20 usiku wa kuamkia Novemba 26, huku akikitaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni uzembe wa dereva wa gari la kanisa kwani alikuwa anaendesha gari kwa mwendokasi pasipokuchukua tahadhari.

Aidha Kamanda Hamduni amesema kuwa waliofariki katika ajali hiyo ni wanaume 5 na mwanamke mmoja na kati ya hao aliyetambulika ni mmoja tu ambaye ni Father Sixtus Massawe, na kuongeza kuwa gari hilo lililogongwa kwa nyuma lilikuwa limesimama katika eneo hilo baada ya kupata hitilafu ya kiufundi na miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Monduli kwa ajili ya uchunguzi.

Kamanda Hamduni pia ameyataja majina ya majeruhi sita wa ajali hiyo, akiwemo Francis Gitayane (57), Muiraq na mkazi wa Masakta, Marko Slaa (56), Muiraq na mkazi wa Masakta, Patrice Faustine(34), Silas Giani, Timoth Faustine na Dismas wote wakazi wa Masakta na wote wanapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mount Meru.


Share:

WANACHAMA CHADEMA WABEBA MABANGO WAKITAKA MDEE NA WENZAKE WAFUKUZWE


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo Ijumaa tarehe 27 Novemba 2020, kinafanya kikao maalum cha kamati kuu kuwajadili wanachama wake 19 wanaodaiwa kukisaliti kwa kukubali uteuzi wa ubunge viti maalumu.

Kikao hicho, kinafanyika jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.

Wanachama hao 19 wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee wanajadiliwa baada ya tarehe 24 Novemba 2020 kwenda bungeni jijini Dodoma kuapishwa na Spika Job Ndugai.

Kufuatia hali hiyo, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alitangaza kufanyika kwa kamati kuu leo Ijumaa na kuwataka kufika makao makuu ya Chadema, Kinondoni Dar es Salaam saa 2:00 asubuhi.

Hata hivyo baadhi ya wanachama wa Chadema wakiwemo wajumbe wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha) wakiwa nje ya ofisi za makao makuu mtaa wa Ufipa, Dar es Salaam na mabango wakishinikiza chama hicho kuwafukuza uanachama makada 19 wa chama hicho ambao wameapishwa kuwa wabunge wa Viti Maalum mjini Dodoma bila idhini ya Chadema.
Share:

MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE AFANYA ZIARA DAWASA CHALINZE

Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Meneja DAWASA-Chalinze, Bw. Onest Makoi wakati wa ziara maalum alipotembelea miradi ya Maji inayoendelea jimboni humo.

Na Josephat Lazaro - Chalinze
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete amefika na kuzungumza na Meneja DAWASA-Chalinze, Bw. Onest Makoi wakati wa ziara maalum alipotembelea miradi ya Maji inayoendelea jimboni humo.

Katika ziara hiyo Mh. Mbunge amepokea taarifa ya Maendeleo ya Miradi hiyo na kuongea na watendaji wa DAWASA. 

Akizungumza Meneja wa Dawasa Chalinze, Onest Makoi alieleza kuwa Miradi yote inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Mwaka 2021 na wananchi wawe tayari kwa maboresho hayo yakiwemo upanuzi wa miundombinu ya Maji, umaliziaji wa Ujenzi wa Matenki na usambazaji awamu ya Tatu. 

Pia , Alieleza kuhusu ujenzi wa mradi wa Ruvu-Mboga ambapo Ununuzi wa Vifaa kwa ajili ya ujenzi uko hatua ya Mwisho.

Kwa upande wa Mh. Mbunge aliwashukuru DAWASA kwa hatua kubwa wanazoendelea kufanya na kumshukuru Mheshimiwa Raisi kwa kuendelea kuwaangalia wananchi wanyonge wa Chalinze kwa kuendelea kutatua kero mbalimbali ikiwemo za Maji. 

Ziara ya Kutembelea sehemu za huduma za Jamii zinaendelea na leo anaendelea kwa kutembelea Ofisi za TARURA kujua hali ya maandalizi ya marekebisho ya Miundombinu ya barabara vijijini na mijini. 
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa katika ofisi ya Meneja DAWASA-Chalinze, Bw. Onest Makoi wakati wa ziara maalum alipotembelea miradi ya Maji inayoendelea jimboni humo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akisikiliza maelezo kutoka kwa maafisa wa DAWASA Chalinze kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji.

Share:

Mawaziri SADC – Troika Wakutana Kwa Dharura Botswana

Baraza la Mawaziri wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama wamekutana katika mkutano wa dharura na kujadili masuala ya siasa, ulinzi na usalama.

Mkutano huo umefanyika  mjini Gaborone, Botswana ambapo ulitanguliwa na mkutano wa Makatibu Wakuu wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ulioanza asubuhi na kumalizika mchana.

Kupitia mkutano huo, mawaziri wameweza kujadili masuala ya hali ya siasa, ulinzi na usalama katika kanda ya SADC na kupendekeza njia mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kwenye siasa, ulinzi na usalama ndani ya ukanda wa SADC.

Pamoja na mambo mengine, Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama  inawajibika kukuza amani na usalama katika eneo la SADC na pia ina wajibu wa kuongoza na kuzipatia nchi Wanachama mwongozo kuhusu mambo ambayo yanatishia amani, ulinzi na usalama
.

Share:

Halmashauri 45 Zapewa Siku 5 Kutoa Maelezo Ya Kutoanzisha Kamati Za Watu Wenye Ulemavu


Na Angela Msimbira OR-TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt. Dorothy Gwajima amezitaka Halmashauri 45 ambazo hazijaunda kamati za watu wenye ulemavu kutoa maelezo ndani ya siku tano.

Akifungua Mkutano wa wadau wa Chama cha Wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi jana amesema hadi sasa halmashauri 140 zimeunda kamati hizo lakini nyingine bado hazijafanya hivyo, jambo ambalo linarudisha nyuma mikakati ya Serikali ya kuwasaidia watu wenye ulemavu.

Amesema kamati hizo ni muhimu kuundwa kwa kuwa zinarahisha mawasiliano kati ya jamii ya watu wenye ulemavu na serikali na kuweka mikakati bora ya jinsi ya kutatua changamoto zao wanazozipitia katika jamii kwa haraka.

“Kwa halmashauri ambazo hazijaunda kamati hizo natoa siku tano kutoa maelezo wanataka nini ili waunde kamati hizo,waliambiwa mwaka gani na sababu za kutokuunda kamati ni nini na wana mikakati gani ya kuanzisha kamati hizo”, ameagiza Dkt. Gwajima.

Hata hivyo Dkt. Gwajima amesema kuwa kutokuundwa kwa kamati hizo kumesababisha kukata mawasiliano kati ya jamii ya watu wenye ulemavu na Serikali katika suala zima la utoaji wa huduma za afya kwa jamii kwa kuwa lengo la serikali ni kuwafikia watu wenye uhitaji.

Aidha Dkt. Gwajima amewataka wadau mbalimbali nchini kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa lishe bora kabla ya Ujauzito ili kupunguza tatizo la watoto wenye mgongo wazi na vichwa vikubwa nchini.

Dkt. Gwajima amesema kuwa kuna umuhimu wa kuweka mikakati itakayosaidia kutoa elimu kuanzia ngazi ya chini ili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu umuhimu wa lishe bora kwa jamii, jambo ambalo litasaidia kumaliza au kupumguza kabisa tatizo la kupata watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi.

Dkt. Gwajima amesema Serikali imeendelea kuweka mikakati ya kuboresha huduma kwa kujenga na kukarabati vituo vya afya nchini na kupeleka vifaa tiba kwa lengo la kuhakikisha huduma bora za afya zinatolewa kwa wananchi.

Hivyo Dkt.Gwajima ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanatumia vituo vya afya hasa kwa wale watoto wenye matatizo ya mgongo wazi na vichwa vikubwa.

Pia ameitaka jamii kuacha mila potofu za kuamini kuwa mtoto anapozaliwa na tatizo la Mgongo wazi na kichwa kikubwa kuwa wamelogwa hivyo kupelekea baadhi ya wazazi kuwaficha watoto wao jambo ambalo linasababisha ucheleweshwa kwa matibabu ambayo yangemsaidia kupona kwa haraka.

“Jamii ielimishwe kuhusu chanzo cha kuzaliwa kwa watoto wenye migongo wazi na vichwa vikubwa ili waondokane na dhana potofu walizonazo ili kuwaokoa watoto wenye tatizo hilo na jinsi ya kukabiliana nalo” amesisitiza Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima ameagiza wadau wote kuhakikisha wanatoa elimu kwa kamati za vituo vya afya nchini kwa kuwa zina wananchi ambao ni wajumbe ili wajue takwimu sahihi ya watoto wenye vichwa vikubwa.

“Wekeni mikakati ya kutumia mifumo ya afya iliyopo katika jamii ili kupunguza watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi katika jamii yetu”, ameeleza Dkt. Gwajima
.

Share:

Makamu Wa Rais Mhe. Samia Amuwakilisha Rais Dkt. Magufulu Kwenye Mkutano Wa Dharura SADCS Organ Troika Botswana


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Maofisa wa Jeshi la Polisi Jijini Gaborone alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sir Seretse Khama  Nchini Botswana lep Novemba 26,2020 kwa ajili ya kumuwakilsha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  katika mkutano wa Dharura wa pamoja baina ya SADC, ORGAN TROIKA, Botswana, Malawi na Zimbabwe Nchi  Zinazochangia Vikosi vya Ulinzi  na Amani vya Umoja wa Mataifa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kwenye Kikosi cha Umoja wa Mataifa Nchini DRC  unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Novemba 2020 Jijini Gaborone Nchini Botswana. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


Share:

Trump Akubali kuondoka ikulu baada ya Biden kuthibitishwa mshindi


Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwa mara ya kwanza kwamba ataondoka ikulu ya White House iwapo rais mteule Joe Biden atathibitishwa rasmi kuwa mshindi wa uchaguzi wa Marekani.

Hata hivyo Trump bado anaendeleza madai yake kwamba uchaguzi huo kuvurugwa.

Trump alifanya majaribio kadhaa ambayo hayakutarajiwa ya kuyakataa matokeo ya uchaguzi kwa kukataa kukubali kushindwa, huku akiibua nadharia kadha wa kadha kuhusu kuibiwa kura na hata kufungua madai yasiyo na uthibitisho mahakamani, ambayo hata hivyo yalitupiliwa mbali na mahakama za Marekani.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari tangu uchaguzi wa Novemba 3, rais Trump alionekana kukaribia kukubali kwamba atahudumu kwa muhula mmoja kabla ya Biden kuapishwa Januari 20 mwakani.

Na baada ya kuulizwa iwapo ataondoka White House, kama jopo la wajumbe maalumu wa uchaguzi la Electoral College litauthibitisha ushindi wa Biden, Trump alikubali kwamba ataondoka na kuongeza kuwa hata waandishi hao wa habari wanajua kwamba ataondoka
.

Share:

DIEGO MARADONA AZIKWA NA JEZI NAMBA 10...MAELFU WAMLILIA


Baadhi ya mashabiki walipiga makofi wengine wakilia walipokuwa wakipita karibu na jeneza la Maradona
Umati mkubwa wa watu wakihudhuria mazishi ya Maradona

Mwanasoka Diego Maradona amefanyiwa mazishi katika sherehe ya kibinafsi katika mji wa Buenos Aires nchini Argentina siku moja baada ya kufariki dunia.

Jamaa na marafiki wa karibu tu ndio waliohudhuria mazishi yake.

Lakini awali, kundi kubwa la watu lilijitokeza kutoa heshima zao za mwisho wengi wakiwa wanabubujikwa na machozi na kuonesha upendo.

Maradona alifariki dunia kwasababu ya mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 60.


Kifo chake kimesababisha watu kumuombeleza kote duniani lakini hakuna walioomboleza kama raia wa nchi yake waliomchukulia kama shujaa wa taifa.

Jeneza la Maradona lilifunikwa bendera ya taifa na fulana ya mpira nambari 10 nafasi aliyocheza uwanjani - pia fulana hiyo ilikuwa inaoneshwa kwa umma katika makao ya rais.

Kufikia mchana, foleni ya waliokuwa wamekuja kutoa heshima zao za mwisho ilifika umbali wa zaidi ya kilomita moja na polisi ikakabiliana na waombolezaji walipokuwa wanajaribu kufunga kwasababu ya muda.
Wengi waliomboleza kifo cha Maradona kwa njia tofauti

Aidha, kulikuwa na taarifa za waombolezaji kurushiwa mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira.

Mmoja wa waombolezaji aliona ni kana kwamba polisi wametumia nguvu kupitia kiasi.

"Tumepanga foleni bila fujo yoyote na ghafla polisi wakaanza kurusha risasi za mpira," anasema, akinukuliwa na shirika la habari la Reuters. "Haifai, Mimi nataka tu kumuaga Diego kwa mara ya mwisho."

Na hatimaye mamlaka haikuwa na budi zaidi ya kufunga zoezi la kuruhusu raia kutoa heshima zao za mwisho ili kudumisha amani.

Gari iliyokuwa imebeba mwili wake ilielekea eneo la makaburi la Bella Vista viungani mwa mji ambapo alizikwa kando na wazazi wake.

'Alikuwa kila kitu kwetu'
Katika klabu ya Napoli ambapo Maradona alicheza kwa miaka saba na kubadilisha kabisa klabu hiyo, mashabiki walimiminika katika uwanja wa klabu hiyo kutoa heshima zao za mwisho wakiwa wanapaza sauti na kutaja jina lake "Diego, Diego!".

Kwa siku ya pili raia walikuwa wanakiuka kanuni zilizowekwa za kukabiliana na virusi vya corona ili waweze kutoa heshima zao za mwisho kabla ya mechi ya Ligi ya Europa iliokuwa imepangwa kati ya Napoli dhidi ya timu ya Rijeka ya Croatian.

Timu ya Napoli ambayo wachezaji wake wote walijitokeza uwanjani wakiwa wamevaa bangili nyeusi ya mkono na jezi nambari 10 mgongoni, ilishinda mechi hiyo mabao mawili kwa nunge.

"Alikuwa wa kipekee, aliwakilisha kila kitu, kila kitu kwetu sisi wakaazi wa Naples, shabiki Gianni Autiero amezungumza na shirika la habari la Reuters. "Maishani mwangu nimelia kwasababu ya watu chache sana na Diego ni mmoja wao."

Mmoja wa wachezaji ambaye mchezo wake ulisifika kuwa bora siku zote, Maradona, maisha yake ya kibinafsi yalikumbwa na utata wa utumiaji dawa za kulevya na pia uraibu wa pombe.

Mapema Novemba, Maradona alifanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe kwenye ubongo ambao ulifanikiwa na alikuwa amepangiwa kutibiwa tatizo la utegemezi wa pombe.

Matokeo ya awali ya uchunguzi wa kifo chake yanaonesha kuwa alipata "matatizo la moyo".
Maradona pia aliombolezwa katika mji wa Itali wa Napoli ambapo alishiriki katika mechi za Klabu kwa miaka saba

Mchezaji huyo wa Argentina aliyekuwa mshambuliaji kiungo wa kati na kocha wa timu hiyo alifariki dunia nyumbani kwake Tigre, karibu na mji wa Buenos Aires. Wa mwiso kumuona Maradona akiwa hai alikuwa mpwa wake Johnny Esposito, kulingana na taarifa za
Maradona alijaaliwa kupata watoto watano na aliyekuwa mke wake, Claudia Villafane, 58, ambaye walitengana mwaka 2004 baada ya miaka 20 ya ndoa.

CHANZO BBC SWAHILI

Share:

AJALI YA GARI YAUA WATU SITA ARUSHA..YUMO PADRE SIXTUS MASSAWE


Padre Sixtus Massawe

Jumla ya watu 6 akiwemo Padre Sixtus Massawe, paroko wa parokia ya Masakta Babati, mkoani Manyara, wamefariki dunia kufuatia ajali ya gari baada ya gari yao kuligonga lori kwa nyuma, maeneo ya kambi ya kijeshi ya Sofa iliyopo mkoani Arusha, wakati wakitoka kwenye msiba wilayani Rombo.

Taarifa hiyo imetolewa jana Novemba 26, 2020, na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Salum Hamduni, ambapo ameeleza kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 8:20 usiku wa kuamkia leo, huku akikitaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni uzembe wa dereva wa gari la kanisa kwani alikuwa anaendesha gari kwa mwendokasi pasipokuchukua tahadhari.

Aidha Kamanda Hamduni amesema kuwa waliofariki katika ajali hiyo ni wanaume 5 na mwanamke mmoja na kati ya hao aliyetambulika ni mmoja tu ambaye ni Father Sixtus Massawe, na kuongeza kuwa gari hilo lililogongwa kwa nyuma lilikuwa limesimama katika eneo hilo baada ya kupata hitilafu ya kiufundi na miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Monduli kwa ajili ya uchunguzi.

Kamanda Hamduni pia ameyataja majina ya majeruhi sita wa ajali hiyo, akiwemo Francis Gitayane (57), Muiraq na mkazi wa Masakta, Marko Slaa (56), Muiraq na mkazi wa Masakta, Patrice Faustine(34), Silas Giani, Timoth Faustine na Dismas wote wakazi wa Masakta na wote wanapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mount Meru.

Chanzo- EATV
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya leo Ijumaa Novemba 27



Share:

Thursday 26 November 2020

Stand Mpya Ya Mbezi Luis Yaanza Majaribio


Kituo kipya Cha Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi Cha Mbezi Luis kimeanza rasmi majaribio  ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amesema kwa Sasa kituo hicho kinaweza kuanza kutumika Kutokana na miundombinu muhimu ya kituo kuwa Katika Hali mzuri.


Akizungumza wakati wa zoezi la majaribio lililowahusisha Askari wa usalama barabarani na Wadau wa vyombo vya usafiri, RC Kunenge ameshuhudia Mabasi yakiingia na kutoka pasipo usumbufu wowote.


Aidha RC Kunenge amesema kwa Sasa kinachoendelea ni matengenezo madogomadogo ya umaliziaji wa jengo na miundombinu mingine ambapo Hadi Sasa Ujenzi umefikia zaidi ya 90%.


Pamoja na hayo RC Kunenge amesema Ujenzi wa barabara ya kuingia kituoni hapo nao unaendelea vizuri chini ya Wakala wa TANROAD ambapo amewahimiza kuongeza kasi ili wakamilishe mradi mapema.


 


Share:

RC Tanga Awasimamisha Kazi Watumishi 8 mpaka wa Horohoro


Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amewasimamisha kazi watumishi nane wa serikali ili kupisha uchunguzi,baada ya kubaini kuwepo kwa ubadhirifu wa fedha ulioisababishia hasara serikali.

Kati ya watumishi hao, sita wanatoka ofisi ya mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) katika kituo cha pamoja cha forodha cha mpaka wa Horohoro, mmoja anatoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na mwingine anatoka ofisi ya mifugo.

Hatua hiyo imekuja kufuatia kuwepo kwa malalamiko ya wafanyabiashara wanaopitisha bidhaa katika mpaka huo.

Kabla ya kufikia uamuzi huo, kamati ya ulinzi na usalama mkoa iliunda tume rasmi iliyoanza kazi ya uchunguzi Septemba 18, mwaka huu, na kubaini kuwepo kwa upotevu wa mapato na uzembe unaofanywa na watumishi hao ambao ni Meneja wa Forodha wa Mkoa wa Tanga Edward Ndupa, Afisa forodha mfawidhi Bakari Athumani, Danda Danda,Julia’s Asila,Bakari Ngoso. Wengine ni Afisa mifugo Nicodemus Kiharus na Michael Katanda TBS.


Share:

Diamond, Koffi waachia ngoma mpya ‘Waah!’


Msanii wa muziki wa Bongo fleva na Bosi wa Wasafi Media Naseeb Abdul maarufu ‘Diamond Platnumz’,  ameachia wimbo mpya ujulikanao ‘Waah!’ aliomshirikisha mkongwe wa muziki wa dansi kutoka nchini Congo Koffi Olomide.

Wimbo huo umeachiwa katika ofisi za Makao Makuu ya Wasafi Media ambapo Koffi Olomide amepata nafasi ya kuangalia namna ya utendaji na uzalishaji wa vipindi unavyofanyika katika Media hiyo akiongozana na mwenyeji wake Diamond Platnumz.

 

Tazama Hapo chini



Share:

Benki Ya Azania Yazindua Huduma Ya Kadi Visa Kwa Wateja Wake


Dar es Salaam Tanzania, 25 Novemba 2020
- Benki ya Azania ikiwa katika maadhimisho ya kusherehekea miaka 25 tangu kuanzishwa kwake, maadhimisho ambayo imeyaita “Mwaka wa Kifaru” kuonesha uimara wa benki hiyo kwenye soko,leo hii imezindua huduma mpya ya kisasa ya kadi za VISA kwa wateja wake.

Kadi hizo ambazo ni za aina mbili, yaani kadi za kawaida (Classic) na zile ya daraja la juu (Infinite) ambazo itatumiwa na wateja wake wa akaunti maalum, zimezinduliwa katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika ofisi za Benki hiyo zilizopo Obama Drive, Sea View- Upanga jijini Dar es salaam. Kwa kutumia Kadi hizo mbili sasa wateja wa Benki hiyo wataweza kufanya miamala popote duniani na kuweza kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao, kufanya malipo kwa kutumia kadi hizo za Visa kwenye maduka mbalimbali nk. Wateja wa kadi za daraja la juu (Infinite card) wataweza kupata huduma za ziada ikiwamo huduma katika viwanja vya ndege, hoteli za kimataifa na kadhalika.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo Bw. Charles Itembe iliishukuru bodi ya Benki hiyo kwa kuwaunga mkono katika kufanikisha safari ya Benki hiyo yenye lengo la kuifanya Benki izidi kuwa ya kisasa zaidi.

“Ikumbukwe kuwa kipindi hiki tuko katika maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Benki yetu mwaka 1995. Kwa kuwajali wateja wetu kwa kutuunga mkono kwa miaka 25 tumehakikikisha wateja wetu wanaendelea kufurahia huduma zetu zote zikiwamo za kubenki kidijitali, kwa kutumia simu zao za kiganjani kwa mobile App iliyoboreshwa, Mawakala wetu ambao wamesambaa nchi nzima, matawi yetu ambayo sasa yamefikia 24 ambapo baadhi yanatoa huduma 8-8, siku zote 7 za wiki, vituo vyetu vya kutolea huduma (Service Centres), Maduka ya kubadilishia fedha yanayojitegemea 12, na mwishoni mwa wiki hii pia tunakwenda kufungua duka jingine la 13 katika uwanja mpya wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA Terminal III), na huduma nyinginezo nyingi na za kipekee kabisa. Na sasa tumewaletea huduma hii kubwa kabisa ya kadi za VISA”, aliongeza Bw.Itembe.

“Benki yetu imewekeza katika teknolojia ya kisasa, mfumo wetu wa teknolojia ya kibenki wa Oracle Flexcube toleo la 12.4 ni wa kisasa zaidi na ndio uliotuwezesha kutuunganisha na huduma hii ya VISA inayopatikana dunia nzima na wateja wetu sasa wataweza kupata huduma kwa kutumia kadi zao za VISA popote duniani” alimalizia Bw.Itembe.

Naye Meneja wa huduma za Benki Kidijitali wa Benki hiyo Bw. Vinesh Davda aliongezea kuwa huduma hii itawapa urahisi wateja wa Benki na hivyo aliwaomba wateja wao watembelee matawi ya benki hiyo ili kuweza kupata kadi hizo mpya.




Share:

MAMA AKATA SEHEMU ZA SIRI ZA MTOTO WAKE NA KUZITUPA CHOONI

Mwanamke mmoja kaunti ya Kiambu nchini Kenya ameripotiwa kumkata mwanawe wa umri wa mwaka mmoja na miezi 8 sehemu nyeti kisha kuzitupa chooni. 

Haijabainika ni kwa nini mama huyo alitekeleza kitendo hicho ila maafisa wa polisi wameanza kufanya uchunguzi kufuatia kisa hicho.

Babake mtoto huyo aliripoti katika kituo cha polisi cha Tigoni akidai kuwa Winnie Mutheu ambaye alikuwa mkewe alitoroka baada ya kutekeleza kitendo hicho. 

Kulingana na jirani, mwanamke huyo alitupa sehemu za siri za mwanawe kwenye choo kabla ya kutorokea mafichoni.

Akithibitisha kisa hicho, OCPD wa Tigoni Mwaniki Irei alisema mtoto huyo amelazwa katika hospitali ya Kijabe akiwa hali mahututi.

Afisa anayeshughulika maslahi ya watoto eneo la Tigoni George Ngugi amesema watashikiriana na maafisa wa polisi kuhakikisha mshukiwa anakamatwa na kukabiliwa vilivyo kisheria. 

Visa vya aina hii vimekithiri nchini, mapema wiki jana mama mmoja kaunti ya Nakuru alimuua mtoto wake wa miaka mitatu baada ya kugombana na mumewe. 

Kulingana na taarifa ya polisi, mshukiwa Faith Chepkemoi Maritim alitekeleza kitendo hicho kufuatia mzozo wa kinyumbani wa mara kwa mara kati ya na mumewe Benard Maritim.

Chepkemoi aliambia polisi kwamba alikuwa amechoshwa na ndoa hiyo na ndiyo sababu aliamua kujinyakulia mpenzi mpya ambaye tayari alikuwa ameahidi kumuoa.

Via>>Tuko News

Share:

Mama Samia kumwakilisha JPM Mkutano wa SADC Organ Troika


Na Nelson Kessy, Gaborone-Botswana
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwenye Mkutano wa dharura wa pamoja baina ya SADC Organ Troika (Botswana, Malawi na Zimbabwe), na nchi zinazochangia Vikosi vya ulinzi na amani vya Umoja wa Mataifa, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwenye Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC utakaofanyika tarehe 28 Novemba 2020, mjini Gaborone, Botswana.

Akithibitisha kuhusu ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kuwa ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo utaongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye atakuwa anamwakilisha Mhe. Rais.

Kwa mujibu wa Prof. Kabudi, mkutano huu utatanguliwa na mkutano wa Maafisa Waandamizi/Makatibu Wakuu wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama na kufuatiwa na mkutano wa Dharura wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama tarehe 26 Novemba 2020.

"Pamoja na Mambo mengine, mkutano huo utajadili hali ya siasa, ulinzi na usalama katika kanda ya SADC na kuweza kuona changamoto mbalimbali zilizojitokeza na kupata majibu ya kutatua changamoto hizo," Amesema Prof. Kabudi

Makamu wa Rais ataambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi Dkt. Faraji Mnyepe pamoja na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda na Mratibu Kitaifa wa Masuala ya SADC, Bibi Agnes Kayola.

ASASI ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika) ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) inawajibika kukuza amani na usalama katika eneo la SADC na pia ina wajibu wa kuongoza na kuzipatia nchi Wanachama mwongozo kuhusu mambo ambayo yanatishia amani, ulinzi na usalama.



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger