Thursday 24 September 2020

NITAPIGANIA AWAMU YA PILI YA MABORESHO YA BANDARI YA TANGA ILI KUFUNGUA FURSA ZA AJIRA-UMMY MWALIMU

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi wa Kata ya Duga Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi wa Kata ya Duga Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akimnadi mgombea udiwani wa Kata ya Duga (CCM)
MWENYEKITI wa UWT Mkoa wa Tanga Dkt Aisha Kigoda akimuombea kura kwa wananchi wa Kata ya Duga mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
Mkuu wa Mkoa Mstaafu Mwatumu Mahiza akimuombea Kura mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM)Ummy Mwalimu
KATIBU Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga Lupakisyo kapange akimuombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wakati wa mkutano huo
MGOMBEA Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Mhandisi Mwanaisha Ulenge
Umati Mkubwa wa wananchi wakimsikiliza mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu(CCM)
Umati Mkubwa wa wananchi wakimsikiliza mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu(CCM)
Msanii wa mziki wa Bongofleva Kassim Mganga akitumbuiza wakati wa mkutano huo
Msanii wa mziki wa Bongofleva Kassim Mganga akitumbuiza wakati wa mkutano huo


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema iwapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atapigania maboresho ya awamu ya pili ya Bandari ya Tanga ili kuongeza fursa za ajira na kuongeaza vipato vya wakazi wa Jiji hilo.

 

Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto aliyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi wa Kata ya Duga Jijini Tanga katika mkutano wake wa kampeni alisema huo ni mkakati wake wa kutaka kuona meli kubwa zinatia nanga kwenye bandari hiyo.

 

“Ndugu zangu wana Duga naombeni kura zenu niweze kulibadilisha Jiji la Tanga kwa kuhakikisha tunasukuma maboresho ya awamu ya pili ya Bandari ya Tanga kuweza kuongeza fursa za ajira kwa vijana”Alisema

 

Alisema pia licha ya uwepo wa fursa za ajira kwa vijana lakini pia vipato vya wakazi wa mji wa Tanga vitaongezeka kutokana na mzunguko mkubwa wa biashara .

 

“Katika hili tunamshukuru Rais Dkt John Magufuli kwa kutuwezesha milioni 372 kwa ajili ya maboresha ya awamu ya kwanza ya Bandari hiyo lengo langu ni kutaka bandari ya Tanga meli kubwa zote ziweze kutia nanga kwenye bandari”Alisema

 

Alisema meli hizo kubwa zikitia nanga kwenye Bandari hiyo itawawesha vijana waweze kupata ajira wanaume na wanawake na mji utachangamka na hivyo kuchochea kipato cha mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.

 

“Nitumeni Bungeni ninaaminika ninaweza kupiga hodi kwa kiongozi yoyote, waziri yoyote ili bandari ya Tanga iweze kuboreshwa na kuweza kufungua fursa za ajira kwa vijana wanawake na wanaume “Alisema

 

Hata hivyo alisema kwamba amedhamiria kupigania mizigo yote inayokwenda mikoa ya kanda ya kaskazini ishushwe kwenye bandari ya Tanga badala ya Dare s Salama ili mji huo uweze kuchangamsha .

 

“Hili nitalipigania usiku na mchana ili kuweza kurejesha heshima ya Jiji la Tanga nataka kuona mji huu unapata mafanikio makubwa na kuwa kama Singapori.

Share:

KONGWA YAANZA MKAKATI WA KILA KAYA KULIMA EKARI MOJA YA KOROSHO


Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Suleiman Serera akizungumza na Maafisa Ugani na Wakulima wakati akifungua mafunzo ya kilimo bora cha korosho yanayotolewa na Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele Mtwara, wilayani humo mkoani Dodoma. Kushoto ni Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Kongwa, Jackson Shija na Mratibu wa Kitaifa wa Zao la Korosho kutoka  TARI Naliendele, Dkt.Geradina Mzena.

Mratibu wa Kitaifa wa Zao la Korosho kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele, Dkt.Geradina Mzena, akitoa mada kwenye mafunzo ya kilimo bora cha korosho yaliyotolewa kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kwa Maafisa Ugani na Wakulima mkoani Dodoma. 

Mtafiti Mwandamizi na Mdhibiti wa Visumbufu vya wadudu na magonjwa kwenye zao la korosho, kutoka Tari- Naliendele  Dkt.Wilson Nene, akitoa mada kwenye mafunzo hayo.

Mtafiti  kutoka Tari- Naliendele Programu ya Zao la Korosho, Kasiga Ngiha, akitoa mada kuhusu 'Agronomia' ya korosho.

Meneja wa Bodi ya Korosho Kanda ya Kati na Magharibi, Ray Mtangi, akizungumzia masoko ya zao hilo.

Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo.
Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Kongwa, Jackson Shija, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo.
Afisa Kilimo wa Kata ya Mkoka, Marcelin Chingilile, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mkulima wa Korosho wa Kata ya Mkoka, Rajab Singo, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa Kilimo wa Kata ya Mlali, Markusi Wongo, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mkulima wa Korosho, Sospeter Chiwuyo, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa Kilimo wa Kata ya Songambele, Asha Malekela, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa Kilimo wa Kata ya Zoissa, Emmanuel Mongi, akizungumza kwenye mafunzo hayo.


Godwin Myovela na Doto Mwaibale, Kongwa 

WILAYA ya Kongwa ipo mbioni kuanza kutekeleza mpango wa kuhakikisha kila kaya 
inalima ekari moja ya zao la miche ya mikorosho bora azma ikiwa ni kuongeza kipato sambamba na kusaidia kurejesha hali ya uoto wa asili na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo yalibainishwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Suleiman Serera, wakati akifungua mafunzo ya Kilimo Bora cha Korosho yanayoendelea kutolewa na Kituo cha Utafiti wa Kilimo Tari Naliendele kwa wakulima na Maafisa Ugani wa Halmashauri wilayani hapa.

“Mkakati wa Wilaya ya Kongwa ni kuhakikisha angalau kila kaya inakuwa na ekari moja ya zao la korosho bora sababu ni zao la kudumu la kibiashara lenye manufaa kiuchumi, lakini tunataka kuikijanisha Kongwa yetu kupitia mbegu bora za mikorosho kutoka Tari Naliendele ,” alisema Serera.

Alisema ili kukamilisha mpango huo ambao hata hivyo tayari umeanza kutekelezwa kwa awamu itahitajika miche zaidi ya milioni 2 ili kuzifikia kaya zote 74,000 zilizopo ndani ya wilaya hiyo.

Serera alisema kilimo cha zao la Korosho katika Wilaya ya Kongwa kilianza rasmi msimu wa kilimo wa 2007l2008 na mpaka sasa kuna jumla ya mikorosho mikubwa 75,591 na midogo 231,295, hivyo kuwa na jumla ya mikorosho 306,886 sawa na ekari 10229.5.

“Naamini baada ya mafunzo haya maafisa ugani mtaendelea kutoa mafunzo ya kilimo bora cha korosho kwa wakulima kwenye maeneo yenu ili kuongeza tija na uzalishaji kwa ustawi wa wilaya yetu,” alisema Serera.

Kwa upande wake, Mratibu wa zao la Korosho Kitaifa kutoka Tari Naliendele, Dkt.Geradina Mzena alisema mafunzo hayo ya nadharia na vitendo yana lengo la kuongeza ujuzi kwa wakulima na maafisa ugani ili kuinua tija kwenye zao la korosho.

“Kwenye mafunzo haya pamoja na mambo mengine tutajikita katika kuangalia namna 
bora ya kuanzisha shamba jipya, ‘agronomia ya Korosho’ na namna bora ya kudhibiti wadudu na magonjwa ya zao hilo,” alisema Mzena. 
 
Share:

VIWANDA VYA KATI NA VIDOGO YAHIMIZWA KUJITOKEZA KUSHIRIKI KWA WINGI SHINDANO LA 15 LA TUZO ZA RAIS ZA MZALISHAJI BORA (PMAYA)

 

Afisa wa masoko kutoka ALAF Ltd. Bi. Theresia Mmasy akielezea jinsi Tuzo za Raisi za Mzalishaji Bora wa Viwanda(PMAYA) zilivyo za haki na huru.

Waandishi mbalimbali walioshiriki katika kuunga mkono uzinduzi wa shindano la 15 la Tuzo za Raisi za Mzalishaji bora wa mwaka(PMAYA)Afisa wa masoko kutoka ALAF Ltd. Bi. Theresia Mmasy akielezea jinsi Tuzo za Raisi za Mzalishaji Bora wa Viwanda(PMAYA) zilivyo za haki na huru. Waandishi mbalimbali walioshiriki katika kuunga mkono uzinduzi wa shindano la 15 la Tuzo za Raisi za Mzalishaji bora wa mwaka(PMAYA)

Mkurugenzi mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Bwana. Leodegar Tenga akisisitiza ushiriki wa viwanda vidogo na vya kati kushiriki katika mashindano ya Tuzo za Raisi za Mzalishaji Bora (PMAYA)

*************************************

Dar Es Salaam, Septemba 23 2020.

Kwa miaka 15 mfululizo, shindano la tuzo la Rais za mzalishaji bora wa mwaka wa viwandani linalofanyika kila mwaka maarufu kama “PMAYA” limepangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.

Dhumuni la shindano la PMAYA ni kutambua makampuni yanayojihusisha na uzalishaji wa bidhaa na huduma nchini Tanzania katika sekta mbalimbali kwenye vipengele vya viwanda vikubwa, vya kati na vidogo.

Akitangaza rasmi shindano la PMAYA kwa mwaka huu wa 2020, mkurugenzi wa Shirikisho la viwanda Tanzania (CTI) Bw. Leodegar Tenga alikaribisha viwanda kushiriki na kuungana na mlezi wa Shirikisho la viwanda Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Joseph Magufuli katika jitihada zake za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

“Kwa kipindi chote tumepata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wadau mbalimbali, na kwa mwaka huu tumekwisha pokea idadi kubwa ya washiriki kutoka viwanda mbalimbali kote nchini. Tunahamasisha makampuni mengi ya uzalishaji kushiriki na hususani tunahamasisha ushiriki wa viwanda vya kati na vidogo” alisema Bw. Tenga.

“Mbuyu ulianza kama mchicha , hivyo ni muda mwafaka kwa viwanda vya kati na vidogo kutumia jukwaa hili kama nafasi kwao kuongoza kwenye nyanja tofauti, kutambulika, kuchangia ukuaji wa biashara zao na kutambulika” aliongeza Bw. Tenga.

Shindano la PMAYA linaloandaliwa kwa heshima ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania akiwa kama mlezi wa Shirikisho la viwanda Tanzania, linadhamiria kutambua mchango wa sekta ya viwanda , kutangaza umuhimu wa sekta ya viwanda nchini, kuongeza tija kwenye viwango vya ufanyaji biashara pamoja na kukuza utawala bora wa makampuni nchini.

Meneja masoko wa kampuni ya ALAF Ltd iliyokuwa mshindi wa kiwango kikubwa kwenye kipengele cha chuma na bidhaa za chuma kwenye shindano la mwaka jana Bi. Theresia Mmasy alisema, “ALAF imekua ikishiriki kwenye PMAYA na tumekua washindi wa vipengele mbalimbali kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo kwenye kipengele cha chuma na bidhaa za chuma.

Kwetu ALAF tumeona umuhimu wa PMAYA na ni kwa sababu taratibu zote za ushiriki na mchakato wa kutafuta washindi unafanyika kwa haki na huru jambo linalotoa nafasi sawa kwa kila mshiriki kushinda. Sambamba na hilo, PMAYA ndio tuzo pekee za viwanda ambapo makampuni ya uzalishaji yanapata kutambulika.

Nayasihi makampuni mengine kuchangamkia fursa hii na kushiriki waweze kushinda.

Mashindano ya PMAYA yamekuwa moja ya njia fasaha kwa makampuni kuongeza ubora wa bidhaa na huduma zao kwa jamii. Tathmini ya shindano inafanywa na jopo huru la wakaguzi, na mwishoni hutoa taarifa na majibu ya tathmini iliyofanywa.

Washiriki hupewa taarifa ya tathmini ili waweze kufahamu mapungufu na umahiri wao kiutendaji kwa maendeleo yao kama kampuni

Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya PLASCO Ltd waliokua washindi kiwango kikubwa kwenye kipengele cha plastiki na mipira, meneja wa masoko na mauzo Bi. Edith James alisema,”Tuzo za PMAYA zimetoa fursa nzuri na ya kipekee kwa viwanda vya ndani. Zimesaidia pia katika kukuza ufahamu juu ya umuhimu wa kuhakikisha ubora kwenye sekta zote kwa mtazamo wa kuhamasisha mchango wa viwanda vya ndani kwenye miradi mikubwa ya miundombinu. Kampuni ya PLASCO imekua ikishiriki kwenye mashindano haya ya PMAYA na tumekuwa washindi katika vipengele mbalimbali jambo linalotupa nafasi kuongoza na pia kukuza biashara yetu. Nahamisisha Viwanda vyote Tanzania haswa ya kati na vidogo kushiriki na kuitumia kwa ufasaha nafasi hii kujitangaza kibiashara”

Uzinduzi wa shindano hili linafungua milango kwa wadau mbalimbali kwenye sekta ya viwanda kujisajili ili kushiriki kwenye shindano hili. Kujisajili tafadhali tembelea toviti ya shirikisho www.cti.co.tz. Mwisho wa kuwasilisha maombi ya kushiriki ni tarehe 12 Oktoba 2020.

Tuzo za Rais za mzalishaji bora wa viwandani PMAYA mwaka huu zinaandaliwa na Shirikisho la viwanda Tanzania (CTI) kwa kushirikiana na GIZ – Kuunda mitazamo: kwa maendeleo ya Afrika Mashariki

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Septemba 24





















Share:

Wednesday 23 September 2020

NDUGAI AFUNGUA SHINA LA WAKEREKETWA CCM LA WAFANYA BIASHARA IPEMBE SINGIDA

Mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa Ndugu Job Ndugai Akihutubia wanachama na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi wa shina na 3 la Ipembe mkoani Singida.
 Eneo la Shina la wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi CCM  Mbacho Guest ambalo lipo kata ya Ipembe Manispaa ya Singida.
 Mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa Ndugu Job Ndugai akiwakabidhi kadi za CCM wanachama wapya waliohamia Chama Cha Mapinduzi CCM kutoka vyama vingine vya upinzani.
Mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa Ndugu Job Ndugai akiwakabidhi kadi za CCM wanachama wapya waliohamia Chama Cha Mapinduzi CCM kutoka vyama vingine vya upinzani.

Na Ismail Luhamba, Singida.


MJUMBE wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Job Ndugai amesema Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania linatarajia kuboresha sheria kwa wafanyabiashara nchini ili wafanye biashara zao kwa tija.


Mjumbe huyo ambaye pia ni Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyasema hayo jana wakati akizindua shina la wakereketwa wa CCM ambao ni wafanyabiashara kata ya Ipembe Wilaya ya Singida mjini. 

Ndugai alitumia nafasi hiyo kuwaomba wanachama wote na wasio wanachama siku ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura na kukipigia chama cha CCM kwani kina mambo makubwa ya kimaendeleo kwa wananchi wake.

Awali akisoma taarifa fupi ya shina hilo kabla ya kuzinduliwa, atibu msaidizi wa shina hilo Florian Malya alisema wafanyabiashara hao wanaiomba serikali kuwawekea mazingira mazuri ya kufanikisha biashara zao ili waweze kujipatia kipato na kuweza kulipa kodi mbalimbali kwa mujibu wa sheria.

"Sisi wafanyabiashara tunakiunga mkono chama cha Mapinduzi na tutahakikisha kinashinda kwa kishindo kwa ngazi zote kuanzia diwani,mbunge na Rais",alisema Malya.

Shina hilo ambalo lipo eneo la Mbacho Guest kata ya Ipembe lina wanachama 50 likiwa linaongozwa na mwenyekiti wake Philipo Masawe, katibu ni Mark Kimboka na katibu msaidizi akiwa ni Florian Malya.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger