Wednesday 23 September 2020

Dr Mwinyi Aahidi Neema Kwa Wajane

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Hussein Mwinyi, amekutana na Jumuiya ya Wanawake Wajane na kuahidi kuwatambua kwa kuwaingiza katika mfuko wa hifadhi ya jamii na kupata mikopo itakayowasaidia kujikwamua kimaisha na kupata maendeleo ya kiuchumi.
Akizungumza na wanawake hao mjini Unguja jana, Dk Mwinyi alisema akichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar atayatambua rasmi makundi maalumu ikiwamo walemavu, wazee na wajane na kuwasaidia kuzitumia fursa mbalimbali za kiuchumi.

Alisema katika serikali yake, makundi hayo yatapatiwa mikopo isiyokuwa na riba, ambapo serikali itachukua jukumu la kulipa riba katika taasisi za fedha.

“Nazitambua changamoto kubwa zinazowapata wanawake walioachwa na waume zao na kuishi katika mazingira magumu, nikichaguliwa nitalichukua suala hilo kwa kuyaingiza makundi maalumu katika mfumo wa kupata mikopo isiyokuwa na riba ili kupata fedha kwa ajili ya kufanya miradi midogo na kuondokana na hali ngumu ya maisha,'' alisema.

Mgombea huyo wa urais wa Zanzibar kupitia CCM, alisema akichaguliwa pia anakusudia kuangalia mfumo mzuri wa sheria za kupambana na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake hasa wanaoachwa na kuachiwa mzigo wa familia ikiwemo watoto.


Share:

Ofisi ya Rais -TAMISEMI yatangaza majina ya madaktari walioitwa kazini.


Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inapenda kuwataarifu waombaji wa nafasi za ajira ya Madaktari zilizotangazwa na Serikali mwezi Agosti, 2020 kuwa zoezi la uchambuzi wa maombi yaliyopokelewa limekamilika.

Aidha, waombaji wa nafasi za ajira ya Madaktari waliokidhi vigezo wamepangiwa kazi katika Vituo vya Afya na Hospitali mbalimbali za Wilaya/Halmashauri nchini.


Madaktari wote waliopangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
1. Kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa kuanzia tarehe 23 Septemba, 2020 hadi 30 Septemba, 2020. Aidha, waombaji watakaoshindwa kuripoti kwenye vituo vya kazi kwa tarehe hizo bila ya taarifa, nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine wenye sifa haraka iwezekanavyo.


2. Kuwasilisha kwa waajiri wao (Wakurugenzi wa Halmashauri walizopangiwa) vyeti halisi (Originals Certificates) kwa ajili ya kuhakikiwa na waajiri kabla ya kupewa barua za ajira. Vyeti hivyo ni kama ifuatavyo:
(i) Cheti cha kuzaliwa;
(ii) Cheti cha Kidato cha Nne na Sita/Diploma;
(iii) Cheti cha Kuhitimu Shahada ya Udaktari;
(iv) Cheti cha Usajili wa Baraza la Madaktari Tanzania (MCT); na
(v) Uthibitisho wa Kumaliza Mazoezi kwa Vitendo (Internship).


3. Kwa Madaktari waliosoma nje ya nchi wanatakiwa kuwasilisha vyeti vya ithibati (Accreditation Certificates) kutoka NACTE/TCU.


Orodha ya Madaktari waliopangiwa vituo vya kazi katika Halmashauri mbalimbali nchini inapatikana kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI: www.tamisemi.go.tz.


Limetolewa na:-
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais - TAMISEMI,
DODOMA.
22 Septemba, 2020

Kuona majina ya waliochaguliwa bofya <<HAPA>>


 



Share:

Majaliwa: Dkt. Magufuli Ni Kiongozi, Anastahili Kupewa Nchi


MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amesema Dkt. Magufuli ni kiongozi anayestahili kupewa nchi kwa sababu ana uwezo wa kuongoza.

“Dkt. Magufuli ana uwezo wa kupewa nchi kwa sababu suala la kupewa nchi siyo la mzaha. Wamejitokeza wengi lakini siku ya kupiga kura ni lazima uwe makini, umpe mtu unayemjua historia yake. Dkt. Magufuli amekuwa Waziri kwa miaka 20. Ameongoza wizara nyeti na kubwa na amekuwa na uwezo wa kuzisimamia na kuleta maendeleo,” alisema.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Septemba 22, 2020) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wakazi wa kata za Lubuga na Ilungu, wilayani Magu, mkoani Mwanza kwenye mikutano ya kuwanadi wagombea wa CCM iliyofanyika akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza.

Mheshimiwa Majaliwa ambaye amemaliza ziara yake mkoani Mara, ameingia Mwanza kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli. Alitumia fursa hiyo kumwombea kura mgombea ubunge wa jimbo la Magu, Bw. Kiswaga Destery na madiwani wengine wa jimbo hilo.

Alisema Dkt. Magufuli anastahili kupewa nchi kwa sababu ana uwezo wa kuisimamia nchi yake na kuongeza: “Tanzania imekosa maendeleo ya haraka kwa sababu kulikuwa na tabia ya watu wachache ya kula rushwa na kuwaathiri wananchi wa chini wasipate mafanikio. Tunataka kiongozi wa nchi anayeweza kupambana na rushwa na mafisadi. Na huyo ndiye kiongozi tunayemtaka.”

Kuhusu uboreshaji kwenye sekta ya afya, Mheshimiwa Majaliwa alisema sera ya tiba kwa mama mjamzito na watoto na wazee ni bure. “Huduma ya mama mjamzito kujifungua ni bure. Tumeleta fedha wilayani Magu, sh. bilioni 10.8 za kuhudumia wote hawa.”

“Tunayo Bima ya Afya na sasa tunataka tuiimarishe ili iwe ya Kitaifa. Na leo tayari tunao muswada wa Bima ya Afya, tunataka tuunganishe wafanyakazi na wananchi wa kawaida ili Watanzania wote wawe na Bima ya Afya.”

Akielezea ni kwa nini bima hiyo inapaswa kusambaa nchi nzima, Mheshimiwa Majaliwa alisema si kila mara mtu anakuwa na pesa taslimu wakati anapopata mgonjwa kwenye familia, na ndiyo maana inasisitizwa Watanzania wote wawe na Bima ya Afya.

“Unapata kadi wewe na mkeo au mumeo, na wategemezi wanne. Leo tuna watoto wanatoka Magu lakini wanasoma Chuo Kikuu cha Dodoma. Una mtoto yuko hapa lakini anasoma Chuo Kikuu Dar es Salaam, una mtoto mwingine anasoma Bwiru. Akiugua huko na kuulizwa kitambulisho, anatambulika kuwa ni mtoto wa fulani, anatibiwa.”

“Haya yote niliyoyasema, yamefanyika katika kipindi cha miaka mitano chini ya uongozi wa Dkt. John Pombe Magufuli na ndiyo sababu leo namuombea kura ili awe Rais wa nchi hii,” alisema.

Akitoa ufafanuzi kuhusu sekta ya afya, Mheshimiwa Majaliwa alisema sh. bilioni 1.4 zimetolewa kwa Wilaya ya Magu kwa ajili ya ujenzi wa vituo vitatu vya afya ambapo kituo cha afya Kahangara kilipata sh. milioni 500 na ujenzi umekamilika, kituo cha afya Lugeye kilipatiwa sh. milioni 500 na ujenzi umekamilika na kituo cha afya Kabila kilipatiwa sh. milioni 400, na ujenzi uko katika hatua za mwisho.

Kuhusu fedha zilizotolewa kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi, Mheshimiwa Majaliwa alisema sh. bilioni 10.1 zimetolewa kwa ununuzi wa dawa na vifaa tiba na kwamba kila mwezi, wilaya hiyo imekuwa ikipokea wastani sh. milioni 108. “Pia kuna magari mawili ya kubebea wagonjwa yaliletwa, moja liko Hospitali ya Wilaya na jingine liko katika kituo cha afya cha Kahangara,” alisema.

Kuhusu ujenzi wa barabara, Mheshimiwa Majaliwa alisema sh. bilioni 10 zimetolewa kupitia TARURA na TANROADS kwa ujenzi, matengenezo ya kawaida, matengenezo ya sehemu korofi na madaraja kwa barabara za Halmashauri ya Wilaya ya Magu ikiwemo ujenzi wa barabara ya lami ya Magu mjini yenye urefu wa km. 5.7 ambayo tayari imekamilika kwa sh. bilioni 2.7.

Alizitaja barabara nyingine kuwa ni ya Kisesa-Bujora yenye urefu wa km. 0.4 kwa kiwango cha lami ambayo imekamilika kwa sh. milioni 360, barabara ya Usagara-Kisesa (km. 16.14) kwa kiwango cha lami, na usanifu wa kina wa barabara ya Magu-Ngudu-Hungumalwa (km. 70). Pia alisema fedha zimetengwa kwa ajili ya usanifu wa kina wa babarara ya Mabuki- Jojiro-Ngudu (km. 28).

(mwisho)


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano September 23





















Share:

Tuesday 22 September 2020

Waziri Wa Kilimo Azindua Utoaji Mikopo Ya Zana Za Kilimo, Asema Wakulima Zaidi Ya Mil 1.2 Wa Mazao Ya Biashara Wamesajiliwa

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Katika kuboresha sekta ya kilimo na kuongeza uzalishaji wa mazao, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeendelea kuimarisha upatikanaji wa mbegu bora, mbolea na viatilifu kwa ajili ya kudhibiti visumbufu vya milipuko.

Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya upatikanaji wa masoko ya uhakika kwa mazao ya kilimo ndani na nje ya nchi. Katika kufikia azma hiyo, Wizara ya kilimo imeanzisha Kitengo cha Masoko ya Mazao (Agricultural Marketing Unit) katika Idara ya Maendeleo ya Mazao inayosimamia utafutaji wa masoko, kufanya tafiti za masoko na bei za mazao pamoja na kufuatilia/kusimamia mifumo ya uuzaji wa mazao.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ameyasema hayo tarehe 22 Septemba 2020 wakati wa uzinduzi wa mikopo ya zana za kilimo inayotolewa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na ETC Agro, LoanAgro na Agricom hafla iliyofanyika katika viwanja vya Posta Jijini Dar es salaam.

Pamoja na hayo amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa huduma za Bima ikiwemo Mamlaka ya Kudhibiti Shughuli za Bima nchini (TIRA), Shirika la Bima la Taifa (NIC), kampuni binafsi tano (5) za bima zimeanzisha Bima ya Mazao kwa lengo la kumsadia mkulima kujikinga na athari za majanga ya asili na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kupata dhamana ya mikopo.

Kuhusu usajili wa wakulima - Waziri Hasunga amesema kuwa Serikali imefanya zoezi la kuwatambua, kuwasajili na kuwapatia vitambulisho wakulima. Zoezi hilo lilifanywa kupitia Bodi za Mazao. Hadi sasa, wakulima 1,279,884 wa mazao ya biashara wamesajiliwa na kutengeneza kanzidata/database kwa lengo la kuwatambua na kusaidia katika utoaji wa huduma za kilimo ikiwemo huduma ya bima ya mazao.

Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, Mkurugenzi Mtendaji wa LoanAgro Kashyap Godavarthi, Mkurugenzi Mtendaji wa ETC Agro, Shashi Gupta, Mkurugenzi Mtendaji wa Agricom, Angelina Ngalula, Viongozi na Wafanyakazi wa Benki ya CRDB, ETC Agro na LoanAgro, waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ameipongeza Benki ya CRDB kwa kutambua umuhimu wa sekta ya kilimo na kuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali.

Kadhalika, Hasunga ameipongeza benki hiyo kwa kuwa kinara wa uwezeshaji sekta ya kilimo ambapo takwimu zinaonyesha asilimia 40 ya mikopo yote ya kilimo nchini imetolewa na Benki ya CRDB.

Amesema kuwa Kilimo ni sekta muhimu sana kwa maendeleo ya taifa letu kutokana na mchango wake katika uchumi. Takwimu zinaonyesha sekta ya kilimo inachangia zaidi ya asilimia 28 katika Pato la Taifa, huku ikitoa ajira kwa takribani asilimia 75 ya Watanzania.

Pia amesema kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo vinavyoweka mkazo kwenye mapinduzi ya viwanda, kwa pamoja vanaitambua Sekta ya Kilimo kama mhimili imara utakaowezesha upatikanaji wa malighafi za viwanda na kukuza uchumi wa taifa letu.

Waziri Hasunga amesema kuwa Takwimu zinaonesha ni asilimia 8 ya mikopo yote iliyotolewa na taasisi za fedha katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 ilielekezwa katika sekta ya kilimo. Kiwango hicho kinajumuisha mikopo ya fedha pamoja na pembejeo za kilimo. Hiki ni kiwango kidogo ukilinganisha na umuhimu wa sekta hii katika uchumi wa taifa letu.

Hivyo basi, ili kuweza kufikia malengo serikali iliyojiwekea taasisi za fedha na wadau wengine wa sekta ya kilimo wanahitaji kuwekeza zaidi katika ubunifu wa huduma na bidhaa zenye vigezo na masharti nafuu ili kuwawezesha wakulima kufanya kilimo cha kisasa na chenye tija zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema kuwa katika kuunga mkono juhudi za kuboresha kilimo nchini, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita,  Benki ya CRDB imetoa mikopo ya zaidi ya shilingi 1.6 trilioni kwa wadau wote katika mnyororo wa thamani katika kilimo.

Amesema Benki ya CRDB ndio inayoongoza nchini kwa kutoa mikopo kwenye sekta ya kilimo kwa kutoa asilimia 40 ya mikopo yote ya kilimo nchini. "Kama unavyofahamu Mheshimiwa kuna taasisi za fedha zaidi ya 58 nchini na kwa ujumla wao wanatoa asilimia 60 wakati Benki ya CRDB pekee inatoa asilimia 40. Hii inadhihirisha adhma ya Benki ya CRDB ya kuunga juhudi za serikali za kuwaletea watanzania maendeleo kwa vitendo" Amesisitiza Nsekela

Ameongeza kuwa Mikopo ya kilimo toka Benki ya CRDB imeelekezwa katika maeneo kama vile: Pembejeo na uendeshaji, Zana za kilimo Ujenzi wa maghala, Uunganishwaji na masoko, Uwekezaji kwenye viwanda, Elimu ya mambo ya fedha ili kutoa ufahamu wa uwekezaji na kuwajengea wakulima uwezo Ufugaji wa mifugo, nyuki na samaki.

MWISHO


Share:

Picha : BENKI YA CRDB, WADAU WA KILIMO WAZINDUA HUDUMA YA MIKOPO YA ZANA ZA KILIMO 'MATREKTA' KWA WAKULIMA


Kushoto ni Afisa Masoko wa Kampuni ya ETC Agro, John Joseph na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui wakimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko mfano wa funguo ya trekta wakati wa uzinduzi wa za huduma ya mikopo ya zana za kilimo. Wa pili kulia Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney.


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya kilimo ‘ETC Agro,Agricom na Loan Agro wamezindua huduma ya Mikopo ya zana za kilimo yakiwemo matrekta kwa wakulima ili kuwawezesha kukopa kwa riba nafuu bila kuweka dhamana ya ziada ili kuboresha kilimo chao.

Uzinduzi wa Mikopo ya zana za kilimo umefanyika leo Jumanne Septemba 22,2020 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa mikopo ya zana za kilimo, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko aliipongeza Benki ya CRDB kwa ubunifu wao wa mara kwa mara katika kurahisisha uboreshaji wa maisha ya Watanzania kiuchumi na hasa katika kuunga mkono juhudi za serikali kuondoa umaskini wa kipato kwa wananchi wake.

“Benki ya CRDB mmetia fora katika sekta ya kilimo,wakati wa msimu wa pamba napo mlishiriki kikamilifu kutoa fedha na leo mmekuja na mikopo ya zana za kilimo,yakiwemo matrekta haya tena bila dhamana za ziada”,alisema. 

Mboneko alieleza kuwa matrekta hayo yatawasaidia wakulima kuboresha kilimo chao badala ya kutumia jembe la mkono na majembe ya kukokotwa na ng’ombe ili kuongeza uzalishaji hivyo kilimo kuwa na tija zaidi.

"Naomba wakulima mchangamkie fursa ya kununua matrekta yaliyotolewa na Benki ya CRDB kupiti wadau ambao ni ETC Agro (wauzaji wa matrekta ya Mahindra), Agricom (wauzaji wa matrekta ya Swaraj na Kubota) na Loan Agro (wauzaji wa matrekta ta John Deer)”,alisema Mboneko.

“Hongereni sana Benki ya CRDB,Mara zote CRDB mmekuwa wabunifu wa kushiriki kwa karibu katika miradi mbalimbali ya kimkakati ya serikali yetu hasa kwa kipindi hiki ambacho Tanzania ipo katika uchumi wa kati”,aliongeza Mboneko.

Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wakulima,vyama vya msingi vya mazao (AMCOS),wakulima binafsi hususani wa zao la pamba,mpunga na alizeti kuchangamkia fursa ya mikopo ya zana za kilimo ili kuhakikisha kilimo chao kiwe na tija zaidi.

Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui alisema benki ya CRDB kwa kushirikia na Makampuni ya uuzaji matrekta ‘ETC Agro,Agricom na Loan Agro’ wameboresha taratibu za utoaji wa mikopo ya zana za kilimo kupitiaa benki ya CRDB ili kuwawezesha wakulima kukopa bila kuweka dhamana ya ziada kwa riba nafuu.

Alieleza kuwa benki ya CRDB imeamua kuleta wadau wa maendeleo ya kilimo ili kuwapunguzia wakulima riba kubwa na kupata mikopo ya dhana za kilimo bila kutumia hati za nyumba ambapo pia matrekta yatakuwa yanafanyiwa matengenezo na wauzaji hao wa matrekta.

“Benki ya CRDB ni benki ya Kimkakati inayounga mkono jitihada za serikali kuwaongezea kipato wananchi na imekuwa ikishirikiana na serikali bega kwa bega kutekeleza miradi ya kuwaletea maendeleo wananchi na imechangia nchi kufikia uchumi wa kati”,alisema Pamui.

Aidha alisema benki ya CRDB, ni benki ya wananchi na inaongoza kuwa karibu wakulima na kwamba hatarajii kuona wakulima wanaendelea kulima kizamani kwa kutumia majembe ya mikono ama ya kukokotwa na ng’ombe.

Naye Afisa Masoko wa Kampuni ya ETC Agro, John Joseph alisema kupitia mikopo ya zana za kilimo,kinachotakiwa kufanywa na wakulima ni kutoa mchango wao katika ununuzi wa trekta usiopungua 25% ya bei ya trekta.

Katika uzinduzi huo wa huduma ya mikopo ya zana za kilimo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko amekabidhi matrekta kwa wakulima wawili kutoka Bariadi mkoani Simiyu ambao ni Njobola Ng’weleja Mome na Malugu Masanja Shashi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa Uzinduzi wa huduma ya Mikopo ya zana za kilimo kutoka Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya kilimo ‘ETC Agro,Agricom na Loan Agro uliofanyika katika benki ya CRDB tawi la Shinyanga leo Jumanne Septemba 22,2020.  Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui, kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB, Luther Mneney. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akiwahamasisha wakulima kuchangamkia fursa ya mikopo ya zana za kilimo ili kuboresha kilimo chao.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akiwakaribisha wakulima binafsi,kutoka kwenye vikundi kukopa zana za kilimo kwani hakuna masharti magumu kama dhamana.
Afisa Masoko wa Kampuni ya ETC Agro, John Joseph akizungumza wakati wa Uzinduzi wa huduma ya Mikopo ya zana za kilimo kutoka Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya kilimo ‘ETC Agro,Agricom na Loan Agro
Mwalikishi wa Kampuni ya Agricom Guninja Gaspar akizungumza wakati wa Uzinduzi wa huduma ya Mikopo ya zana za kilimo kutoka Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya kilimo ‘ETC Agro,Agricom na Loan Agro
Muonekano wa sehemu ya Matrekta ambayo wakulima wanaweza kukopa 
Muonekano wa sehemu ya Matrekta ambayo wakulima wanaweza kukopa 
Muonekano wa sehemu ya Matrekta ambayo wakulima wanaweza kukopa 
Muonekano wa sehemu ya Matrekta ambayo wakulima wanaweza kukopa 
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui (katikati)  akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (wa pili kulia) kuhusu matrekta ambayo wakulima wanaweza kukopa kupitia Benki ya CRDB
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikata utepe wakati wa uzinduzi wa mikopo ya zana za kilimo. Kushoto ni Afisa Masoko wa Kampuni ya ETC Agro, John Joseph. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akifuatiwa na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikata utepe wakati wa uzinduzi wa mikopo ya zana za kilimo. Kushoto ni Afisa Masoko wa Kampuni ya ETC Agro, John Joseph. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akifuatiwa na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwasha trekta wakati wa uzinduzi wa mikopo ya zana za kilimo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwa amepanda trekta wakati wa uzinduzi wa mikopo ya zana za kilimo. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akijaribu kuendesha trekta wakati wa uzinduzi wa mikopo ya zana za kilimo. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui wakifurahia jambo baada ya kupanda kwenye matrekta wakati wa uzinduzi wa huduma ya mikopo ya Zana za Kilimo.Katikati ni Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui wakifurahia jambo baada ya kupanda kwenye matrekta wakati wa uzinduzi wa huduma ya mikopo ya Zana za Kilimo.Katikati ni Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney akiwa amepanda juu ya trekta.
Afisa Biashara Benki ya CRDB, Mwanahamis Iddi akiwa amepanda juu ya trekta
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkabidhi funguo ya Trekta Mkulima kutoka Bariadi mkoani Simiyu Malugu Masanja Nshashi (kushoto) aliyenunua trekta kwa njia ya mkopo kupitia Benki ya CRDB.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkabidhi funguo ya Trekta Mkulima kutoka Bariadi mkoani Simiyu Manjobola Mome (kulia) aliyenunua trekta kwa njia ya mkopo kupitia Benki ya CRDB.
Meneja Mahusiano Kilimo Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Anselm Mwenda akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko kuhusu aina za matrekta
Meneja Mahusiano Kilimo Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Anselm Mwenda akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko kuhusu aina za matrekta
Wadau wa kilimo wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa huduma ya mikopo ya zana za kilimo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya kumbukumbu na viongozi wa benki ya CRDB, Kampuni ya ETG Agro na wakulima kutoka Bariadi mkoani Simiyu walionunua matrekta kwa njia ya mkopo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya kumbukumbu na viongozi wa benki ya CRDB, Kampuni ya ETG Agro na wakulima kutoka Bariadi mkoani Simiyu walionunua matrekta kwa njia ya mkopo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya kumbukumbu na wadau wa kilimo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya kumbukumbu na wadau wa kilimo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya kumbukumbu na viongozi wa benki ya CRDB.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akifurahia jambo na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui (kushoto) na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia).

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger