Sunday 20 September 2020

UMMY MWALIMU KUWAWEZESHA VIJANA, WAKINA MAMA WAJASIRIAMALI TANGA KUPATA MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA TANGA


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akiwahutubia wananchi wa Kata ya Mabawa Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akiwahutubia wananchi wa Kata ya Mabawa Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akizungumza wakati wa mkutano huo ambapo aliwataka wananchi kumchagua Ummy Mwalimu
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati amkifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Tanga Salim Kidima
MSANII wa Mziki wa Bongofleva Jijini Tanga Mwandey akitumbuiza kwenye mkutano huo wa kampeni
Msanii wa mziki wa Bongofleva Kassim Mganga akitumbuiza kwenye kampeni hizo
Msanii wa Mziki wa Bongofleva Mchina Mweusi akitumbuiza kwenye mkutano huo
Msanii wa mziki wa Bongofleva Kassim Mganga akitumbuiza kwenye kampeni hizo
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Ummy Mwalimu wakati akinadi sera zake
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akipandisha bendera ya CCM mara baada ya kuzindua shina la Wakereketwa Wajasiriamali Womens Group

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amehaidi iwapo akichaguliwa atawawezesha kiuchumii wakina mama wajasiriamali wadogo wadogo na watu wenye ulemavu kupatiwa mikopo isiyo na riba ili waweze kufanya shughuli zao za kuzalisha mali.

Huku akiwahaidi pia vijana nao pia watapatiwa mikop  na vitendea kazi ikiwemo pikipiki alimaarufu bodaboda ili waweze kufanya biashara za bodaboda bila kulipa fedha nyingi ambazo wanapaswa kulipa

Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto alitoa ahadi hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mabawa Jijini Tanga ambapo alisema atafanya kazi usiku na mchana ili kuweza kutatua changamoto za wananchi.

Alisema dhana hizo ni kuwapatia pikipiki ili wafanya biashara ya bodaboda ambayo itawasaidi waweze kujiingizia kipato ambacho kitawasaidia kujikwamua kimaendeleo na hatimaye kukuza kipato chao.

“Ndugu zangu wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo wadogo,watu wenye ulemavu tuwapa mikopo muweza kuongeza kipato chenu na hii itawasaidia kuinuka kiuchumi kwenye biashara zenu”Alisema Ummy Mwalimu.

Aliwataka wampigia kura za ndio ili wamuweze kuwa mbunge wa Jimbo hilo ili aweze kuhakikisha anawatumikia wananchi hao ili waweze kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo.

“Lakini pia niwaombe tume kura nyingi za ndio Rais Dkt John Magufuli aendele kwani kazi yake kwenye Jiji la Tanga inaonekana kwenye sekta ya elimu amewezesha utoaji wa elimu bure,ujenzi wa madarasa nyumba vya maabara”Alisema

Hata hivyo alisema pia kazi ya Rais Dkt Magufuli kwenye sekta ya afya kwenye kata ya mabawa imeonakana kwani hamkuwa na kituo cha fya lakini leo  kumejenga majengo ya upasuaji wodi za watoto na wakina mama.

“Kwa heshima na taadhima nawaomba msifanya makosa mpeni kura za ndio Rais Dkt John Magufuli kwenye uchaguzi mkuu mwezi Octoba mwaka huu lakini pia naombeni kura zenu zote za ndio niweze kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi kwenye Jiji la Tanga”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba hakuna mgombea Urais ambaye anaweza kufikia kazi zilizofanywa na Rais Dkt Magufuli hata kwa asilimia 1 .

 

Share:

Mpango Wa Elimu Bila Malipo Wazinufaisha Shule 156 Serengeti


SHULE 156 za wilaya ya Serengeti zikiwemo 122 za msingi na 34 za sekondari zimenufaika na mpango wa elimu bila malipo kwa kupatiwa sh. bilioni 6.2 katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Hayo yamebainishwa jana jioni (Jumamosi, Septemba 19, 2020) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa alipokuwa akizungumza na wakazi wa Mugumu, wilayani Serengeti, mkoani Mara katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Sokoine.

Akiwafafanulia mambo yaliyofanywa na Serikali ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ndani ya miaka mitano, Mheshimiwa Majaliwa alisema sh. bilioni 2.9 zilitolewa kwa shule za msingi 122 kwa ajili ya ukarabati, utawala, michezo, mitihani na posho kwa maofisa elimu kata na walimu wakuu.

Kwa upande wa elimu ya sekondari, Mheshimiwa Majaliwa alisema sh. bilioni 3.3 zilitolewa kwa shule 34 ili kulipia fidia ya ada, chakula kwa shule za bweni na posho ya madaraka kwa wakuu wa shule.

Akielezea mpango mwingine ambao umezinufaisha shule nyingi za wilaya hiyo, Mheshimiwa Majaliwa alisema mfumo wa uboreshaji wa miundombinu ya shule wa Lipa Kutokana na Matokeo (EP4R) uliotekelezwa tangu 2015 hadi 2020 umewezesha sh. bilioni 2.7 zitolewe kwa ajili ya ukamilishaji wa miundombinu ya madarasa, vyoo na nyumba za walimu wa shule za msingi.

“Shilingi bilioni 1.7 zilizotolewa awali na awamu ya pili zikatolewa shilingi bilioni moja. Baadhi ya shule za msingi zilizonufaika na fedha hizo ni Wageti, Nyamakendo, Moningori, Masangura, Maburi, Kitunguruma, Itununu, Mchuri, Merenga, Mesanga, Miseke, Busawe, Musati, Monuna, Nyamburi, Nyiberekera, Motukeri, Kemugongo, Nyansurumunti, Mugumu na Nayaigabo,” alisema.

Alisema shule za sekondari zilipatiwa sh. milioni 3.076 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya shule ikiwemo maabara, madarasa, mabweni na vyoo. “Katika awamu ya kwanza zilitolewa shilingi bilioni 2.1 na awamu ya pili zikalipwa shilingi milioni 976.2.”

Alizitaja shule hizo kuwa ni Mugumu, Kitunguruma, Busawe, Nyamoko, Natta, Robanda, Serengeti, Ring’wani, Machochwe, Rigicha, Manchira, Mama Maria Nyerere, Ikongoro, Nagusi, Dkt. Omari Ali Juma na Nyambureti.

Mheshimiwa Majaliwa ametumia mkutano huo kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na kuwaombea kura mgombea ubunge wa jimbo la Serengeti, Bw. Amsabi Jeremiah Mhimi, mgombea udiwani wa kata ya Stendi Kuu, Bw. Steven Mapancha na wagombea udiwani wa kata zote za wilaya ya Serengeti.

Kuhusu maji safi na salama, Mheshimiwa Majaliwa alisema sh. bilioni 3.4 zimetumika kukarabati na kujenga miradi mbalimbali wilayani Serengeti, ikiwemo vijiji vya Natta, Motukeri, Makundusi, Nyamakobiti, Majimoto, Musati, Kebanchabancha, Kutunguruma, Kenyana na Nyamitita.

“Vilevile, shilingi milioni 62.5 zimetumika kwa ajili ya uchimbaji wa kisima kimoja kwenye kijiji cha Makundusi na ukarabati wa visima vya pampu za mikono kwenye vijiji 19,” alisema.

Kuhusu huduma ya umeme, Mheshimiwa Majaliwa alisema jumla ya vijiji 69 kati ya vijiji 78 vya Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti vimepata umeme na vijiji vilivyobaki visivyo na umeme ni tisa tu ambavyo vitapata kwa sababu mkandarasi yuko kazini.

(mwisho)


Share:

Wizara Ya Ardhi Yazindua Siku Maalum Ya Mlipa Kodi

Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imezindua rasmi siku Maalum ya Mlipa Kodi ya Pango la Ardhi itakayoendeshwa katika mikoa yote ya Tanzania.

Uzinduzi huo ambao ni mkakati maalum wa Wizara ya Ardhi kuhamasisha wamiliki wa ardhi kulipa kodi ya pango la ardhi ambapo na utekelezaji wake ulianza mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma kwa Maofisa Ardhi wa Makao Makuu kwa kushirikiana na wale wa ofisi za ardhi za mikoa na  wa jiji la Dodoma kutembelea mitaa ya Kisasa na Ilazo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Denis Masami, zoezi hilo la siku ya Mlipa Kodi ya Pango la Ardhi litakuwa likifanyika kila siku ya Ijumaa kwa Maafisa wote wa Ardhi nchi nzima kutembelea mitaa mbalimbali nyumba kwa nyumba kwa lengo la kutoa elimu na kutatua changamoto za ardhi.

‘’Zoezi hili litakuwa likifanyika kila siku ya Ijumaa na litahusisha maafisa wote wa ardhi katika mikoa ya Tanzania Bara na hapa Maafisa Ardhi hawatakiwi kujionesha wao ni nani kinachotakiwa ni kutoa elimu na leo tumeanza jiji la Dodoma kama uzinduzi rasmi wa siku hiyo’’ alisema Denis Masami.

Mkuu huyo wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi alisema, mbali na zoezi hilo la kutembelea wamiliki wa ardhi nyumba kwa nyumba kutatua changamoto za ardhi pia llitatumika kuhuisha kumbukumbu za  ardhi kwa wamiliki na kukagua uendelezaji miji.

Masami amewataka wamiliki wa ardhi nchini kuhakikisha wanaacha mawasiliano sahihi majumbani mwao ili maofisa ardhi watakapopita na kuwakosa waweze kuwasiliana kwa njia ya simu ili kupata taarifa sahihi zitakazowezesha uhuishaji kumbukumbu za ardhi kwa wamiliki.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleoi ya Makazi kwa mwaka huu wa fedha 2020/2021 imepangiwa kukusanya jumla ya shilingi bilioni 200 ya kodi ya Pango la Ardhi.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili Septemba 20













Share:

Saturday 19 September 2020

WANNE WANASWA LIVE KWENYE HARUSI WAKIMUOZESHA MWANAFUNZI WA DARASA LA 5, MIAKA 12 SHINYANGA



Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog 
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linawashilikilia watu wanne baada ya kuwanasa Mubashara 'Live' kwenye sherehe ya harusi wakimuozesha mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 12 anayesoma darasa la tano shule ya Msingi Samuye katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga aliyetolewa mahari ya ng’ombe nane na shilingi 600,000/=. 

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema watuhumiwa hao walikamatwa Septemba 14,2020 majira ya saa kumi na mbili na dakika arobaini jioni, katika kijiji cha isela, kata na tarafa ya Samuye, halmashauri ya wilaya ya Shinyanga 

“Polisi mkoa wa Shinyanga tulibaini kuwa katika kijiji cha Isela mtoto mwenye umri wa miaka 12 anafunga ndoa ndipo kikosi kazi kutoka dawati la jinsia na watoto Shinyanga wakishirikiana na Maafisa Maendeleo ya Jamii halmashauri wilaya ya Shinyanga walifika eneo husika na kukuta sherehe ya harusi ikiendelea nyumbani kwao na bwana harusi na kufanikiwa kuwakamata watu wanne”,ameeleza Kamanda Magiligimba. 

Kamanda Magiligimba amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Geni Bundala (52), Jumanne Shigimahi (54),Hawa Ramadhan (37) na Japhari Khalfan (52) wote ni wakazi wa kijiji cha Isela. 

“Watuhumiwa hawa tuliwakamata wakimuozesha mtoto (jina linahifadhiwa) , miaka 12, mwanafunzi wa darasa la tano shule ya msingi Samuye kwa kijana aitwaye Khalfan Japhari,(bwana harusi) mwenye umri wa miaka 23, mkazi wa kijiji cha Isela ambaye alitoroka na juhudi za kumtafuta zinaendelea”,amefafanua Kamanda Magiligimba. 

Amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtoto huyo wa kike mwenye umri wa miaka 12 aliozeshwa kwa kutolewa mahari ya ng’ombe 8 na pesa tasilimu laki sita za Kitanzania. 

“Mtoto huyo tayari amekabidhiwa katika kituo cha kulelea watoto ambao ni wahanga wa ukatili -ndoa za utotoni kiitwacho Agape Aids Shinyanga kwa sasa anaendelea na masomo yake”,amesema Kamanda Magiligimba. 

Kamanda Magiligimba anatoa wito kwa wananchi hususani wazazi na walezi mkoani Shinyanga kuacha kuozesha wanafunzi kwani inapelekea watoto wa kike kukatisha ndoto zao za kuendelea na masomo na hivyo kupelekea kukosa viongozi wanawake wa baadae. 

Aidha amewaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kutokemeza aina zote ukatili wa kijinsia mkoani Shinyanga. 

“Naamini kabisa wananchi wakiendelea kuunganisha nguvu ya pamoja na jeshi la polisi dhidi ya uhalifu, tutaweza kuzuia uhalifu,kupunguza uhalifu na kuufanya mkoa wetu wa shinyanga kuendelea kuwa shwari”,ameongeza.
Share:

MTATURU: KUTOICHAGUA CCM NI SAWA NA KUPISHANA NA GARI LA MSHAHARA


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Miraji Mtaturu, akiwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Tarafa ya Makiungu Wilaya ya Ikungi mkoani Singida jana.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Miraji Mtaturu, akihubia kwenye mkutano huo.

Wananchi wa Tarafa ya Makiunga wakimsubiri Mtaturu.


Waendesha boda boda wakiongoza msafara wa mgombea huo.

Wananchi wa Tarafa ya Makiungu wakiwa na mabango yenye picha za mgombea Urais wa CCM wakati wa kumpokea Mtaturu.

Wananchi wakiwa kwenye mkutano.



Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Miraji Mtaturu, akionesha upendo kwa wapiga kura kwa kusalimiana nao.

Burudani ikiendelea katika mkutano huo.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Makiungu, Daud Kinjagahi, aakizungu kwenye mkutano huo.
Kada wa CCM, Gerald Mahami akizungumza kwenye mkutano huo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Miraji Mtaturu, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa, akizungumza katika mkutano huo.
Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Ikungi, Pius Sanka, akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa, akizungumza katika mkutano huo.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida,  Alhaj Juma Kilimba, akiwanadi wagombea udiwani wa Kata ya Makiungu, John Mathias (kulia) na Gabriel Dule (katikati) wa Kata ya Mngaa.
 



Na Dotto Mwaibale, Singida.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Miraji Mtaturu amesema kutokukichagua chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu ni sawa na kupishana na gari la mshahara.

Mtaturu aliyasema hayo jana wakati akiwahutubia Wananchi na wana CCM wa Tarafa ya Makiungu na Kata ya Mngaa katika mwendelezo wa mikutano yake ya kampeni ndani ya jimbo hilo.

"CCM tumejipanga sawa sawa kwenye sekta zote hivyo kutokukichagua CCM ni sawa na kupishana na gari la mshahara." alisema Mtaturu.

Katika mkutano huo Mtaturu alikwenda mbali zaidi kwa kuwafananisha wagombea wengine wa nafasi ya Urais wa vyama vingine na mgombea Urais wa CCM kama ni kichuguu na Mlima Kilimanjaro au Mbingu na ardhi kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya mgombea wao.

"Hatuwezi kabisa kuwafananisha wagombea hao na Magufuli kwani amewaacha mbali sana." alisema Mtaturu.

Mtaturu alitumia nafasi hiyo kuomba ridhaa ya kuchaguliwa tena kwa kipindi cha Miaka 5 ili aweze kufanya makubwa ndani ya jimbo hilo na pia alimuombea kura mgombea wao wa nafasi ya Urais Dkt John Magufuli,wabunge na madiwani wa chama hicho.

Alisema kugombea ubunge sio kujaza nafasi bali ni uwakilishi wa kuwatumikia Wananchi kwa kuwapelekea maendeleo na kuacha shughuli nyingine binafsi ambazo haziwahusu wananchi.

Aidha alisema kiongozi yeyote anapoaminiwa na wananchi kwa kupewa kazi ni lazima aache alama ya utendaji wake kama alivyofanya yeye katika maeneo mbalimbali alikoaminiwa kufanya kazi na kuhakikisha jimbo hilo linakuwa la mfano kwa maendeleo katika majimbo yote Tanzania.

Akizungumzia ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 alisema ni kubwa kuliko ile ya 2015-2020 ambayo imebeba matumaini na kuwa na majibu ya kero za watanzania.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida,  Alhaj Juma Kilimba alisema uchaguzi wa mwaka huu ni wa muhimu hivyo wananchi wasifanye utani bali wamchague Rais ambaye atawafaa watanzania ambaye ni Dkt. John Pombe Magufuli.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa alisema wagombea pekee wanapaswa kuchaguliwa ni wale wanaotoka kwenye Chama hicho chenye sera na dira na sio kwa wagombea wengine ambao wamekuwa wakipitisha mabakuli kuomba wachangiwe.




Share:

KATAMBI AENDELEA KUCHANJA MBUGA JIMBO LA SHINYANGA MJINI...ATUA MWAMALILI AKIAHIDI NEEMA KWA WANANCHI



Mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Jimbo la Shinyanga Mjini,Patrobas Katambi akiwa kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Mwamalili manispaa ya Shinyanga. Picha na Suzy Luhende.
Mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Jimbo la Shinyanga Mjini,Patrobas Katambi akiwa kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Mwamalili manispaa ya Shinyanga.
Mgombea udiwani kata ya Mwamalili manispaa ya Shinyanga Paul Machela akiomba kura kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo na kuhudhuriwa na mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi.

Mgombea ubunge viti maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Christna Mzava akiwa kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Mwamalili manispaa ya Shinyanga akiomba kura za diwani, mbunge na Rais wa Chama Cha Mapinduzi CCM.

***
Na Suzy Luhende - Shinyanga 
Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Patrobas Katambi ameendelea na Kampeni zake Uchaguzi  ambapo leo alikuwa katika kata ya Mwamalili ambapo amewaomba wananchi wamchague ili aweze kuwatua ndoo kichwani akina mama kwa kuwatengenezea mtandao mkubwa wa maji ya kisima. 

Hayo aliyasema leo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Mwamalili, ambapo aliwaomba wananchi wa kata hiyo wamchague kwa kura zote ili aweze kuwatua ndoo kichwani akina mama na kuleta maendeleo mbalimbali katika kata hiyo. 

Katambi pia aliwaomba wananchi hao kumchagua John Pombe Magufuli na diwani wa Kata hiyo Paul Machela ambaye atawakilisha kero mbalimbali zilizopo na kuweza kutatuliwa. 

"Najua kuna changamoto nyingi katika kata hii zikiwemo za kilimo, nichagueni mimi na Rais Magufuli ili tuweze kuwaletea matrekta ya kulimia ambayo tutayaleta kwenye kata na mengine ya kuwakopesha",alisema Katambi. 

Alisema katika sekta ya uchumi na biashara wataangalia ni namna gani kaina mama waweze kujikwamua kiuchumi wakiwemo vijana wote,hivyo wataleta wataalamu ambao watawafundisha akina mama kutengeneza batiki na vitu vingine vya kimaendeleo. 

Pia aliwaomba wazee wamuamini waunde Baraza la Wazee ambalo litakuwa na viongozi litawasilisha kero zote zilizopo katika kata na zitafanyiwa kazi kwa wakati zikishindikana zitapelekwa bungeni na wazee watapata haki zao. 

Kwa upande wake mgombea udiwani wa kata hiyo Paul Machela alisema kuna kero ya daraja la kwenda Old Shinyanga daraja litaanza kujengwa na zahanati ya kijiji cha Bushola imekamilika, zahanati ya Mwamalili nayo imekamilika na wanajenga maabara ikiisha tu tayari itaanza kutumika. 

"Mimi ndiye diwani niliyekuwepo nawaambia ukweli, na sasa nagombea ili tumalizie yaliyobaki, hivyo kila kitu kitakamilika ndani ya uongozi wa Chama Cha Mapinduzi na kwa kufuata Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM",alisema Machela. 

"Niseme ukweli wa Machela alianza udiwani Mwaka 1995 enzi za Mkapa mpaka sasa anaendelea kusimamia miradi mbalimbali zikiwemo zahanati,maji ya ziwa Victoria na maendeleo mengi mbalimbali",alisema Kampeni Meneja wa diwani Paul Machela, Fulushi Matinde.


Share:

AHMED SALUM AWAOMBA WANANCHI WAMPE MIAKA MITANO MINGINE SOLWA...ATOA AHADI KWA WACHIMBA MADINI MWAKITOLYO


Mgombea Ubunge jimbo la Solwa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ahmed Salum akiwaomba wananchi wamchague tena kuwa Mbunge wa Jimbo la Solwa.

******
Na Victoria Robert - Michuzi blog

Mgombea Ubunge jimbo la Solwa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ahmed Salum amewaomba wananchi wamchague tena 'wampe miaka mitano mingine' ili aendelee kuwaletea maendeleo huku akiwataka wachimbaji wadogo kuendelea kuchimba madini ya dhahabu kwa kujiamini bila kubughuziwa akiahidi kuwasogezea masoko madogo madogo katika kata ya Mwakitolyo. 

Ahmed ameyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi CCM katika jimbo la Solwa ambapo alisema anazitambua changamoto zinazowakabili wananchi wa Solwa ikiwemo miundombinu ya barabara huku akidai kuwa baadhi ya barabara hizo zipo katika utekelezaji wa kiwango cha lami.

Salum aliwaomba wananchi wa Solwa wamchague kuwa Mbunge wao pamoja na Rais Magufuli na madiwani wa CCM kwani Ilani ya uchaguzi ya CCM inagusa maisha ya Watanzania na CCM imedhamiria kuwaletea maendeleo wananchi.

Akimnadi Mgombea ubunge wa jimbo hilo Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa aliwaomba wananchi kuchagua wagombea wa CCM ili waweze kuwaletea maendeleo yatakayowanufaisha wananchi.

Naye Naibu Waziri wa Ujenzi ambaye ni Mgombea Ubunge aliyepita bila kupigwa katika jimbo la Ushetu Elias Kwandikwa alisema serikali ya CCM inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara pamoja na utoaji wa maeneo kwa wachimbaji wadogo wadogo katika eneo la Mwakitolyo hivyo ni muhimu kwa wachimbaji kuchangamkia fursa hiyo. 

Kwa upande wake Mjumbe wa NEC, Gaspar Kileo ambaye pia ni Meneja kampeni wa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini. Patrobas Katambi aliwaomba kuchagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi ili waendelee kutekeleza ilani yao katika kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Solwa.

Akimuombea kura mgombea ubunge jimbo la Solwa,mgombea Ubunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga aliwaomba wanawake kumpigia kura Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania ,Wabunge pamoja na madiwani wa CCM.
Mgombea Ubunge jimbo la Solwa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ahmed Salum akiwa kwenye mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM ambapo amewaomba wananchi wamchague tena kuwa Mbunge wa Jimbo la Solwa.
Kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi ambaye ni Mgombea Ubunge aliyepita bila kupigwa katika jimbo la Ushetu Elias Kwandikwa akiwaombea kura wagombea wa CCM. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi


Share:

Alicia Keys ft Diamond Platnumz – Wasted Energy


Alicia Keys ft Diamond Platnumz – Wasted Energy


Share:

Serikali Kutokomeza Wadudu Waenezao Magonjwa Ya Mifugo


Na. Edward Kondela
Serikali imelenga kukabiliana na magonjwa ya mifugo nchini kupitia taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwa kutumia njia ya chanjo pamoja na kutokomeza wadudu wakiwemo mbung’o ambao wanaathiri afya ya wanyama.

Akizungumza katika ziara ya kikazi ya siku moja aliyofanya Mkoani Tanga mwishoni mwa wiki hii, baada ya kutembelea Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka watanzania kutambua kazi kubwa zinafonywa na taasisi za serikali katika kufanya tafiti na kutafuta tiba ya magonjwa ya mifugo nchini.

“Wito wangu kwa wafugaji ambao bado wanasumbuliwa na mbung’o, tayari kituo chetu cha TVLA Mkoani Tanga wameshapata njia nzuri na rahisi kabisa, lengo kubwa kabisa ni kuhakikisha tunatokomeza magonjwa ya mifugo kadri inavyowezekana, niombe watanzania watambue kazi kubwa zinazofanywa na taasisi zetu, ili tuondoke katika ufugaji wa mazoea bali sasa tufanye ufugaji wa kisayansi.”  Amesema Prof. Gabriel

Afisa Utafiti wa Mifugo kutoka TVLA Mkoani Tanga Bw. Peter Lucas, amemfahamisha Prof. Gabriel kuhusu njia rahisi ambazo wafugaji wanaweza kutumia katika kutokomeza mbung’o kuwa ni pamoja na mtego wa kukamata mbung’o na njia ya kuweka dawa maalum ya kuua mbung’o kwenye vitambaa vyenye rangi ya bluu na nyeusi ambazo zimekuwa zikiwavutia wadudu hao.

Akiwa katika chuo cha Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) Kampasi ya Buhuri Mkoani Tanga, Katibu Mkuu Prof. Gabriel amewataka wakufunzi wa chuo hicho wawe na upeo mkubwa ili waweze kutoa wahitimu waliopata elimu bora.

“Kikubwa wafundisheni wanafunzi kujiajiri na anayefundisha somo hilo lazima awe amejiajiri, lazima tuwajengee wanafunzi wetu kazi siyo mpaka kuajiriwa, kujiajiri pia ndiyo msingi hasa wa kuendeleza maendeleo na nchi zilizoendelea walioleta maendeleo ni wajasiriamali.” Amefafanua Prof. Gabriel.

Katika ziara hiyo ya siku moja Mkoani Tanga, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel alijionea shughuli zinazofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) mkoani humo, ambapo ameitaka taasisi hiyo kutoa taarifa ya tafiti mbalimbali za mifugo ikiwemo ya ng’ombe bora wa maziwa na kuongeza idadi ya mifugo iliyopo katika eneo hilo.

Aidha, akizungumza na watumishi wa taasisi hizo Prof. Gabriel amewataka watumishi hao kuwa wazalendo na kujituma kwa kutoa michango yenye tija katika taasisi wanazofanyia kazi.

Wakizungumza katika nyakati tofauti Kaimu Meneja wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Dkt. Oliva Manangwa amemuarifu katibu mkuu huyo kuwa TVLA imefanikiwa kufanya tafiti mbalimbali ikiwemo ya kutokomeza kabisa vimelea vya ndorobo visiwani Zanzibar kwa kuwahasi mbung’o dume.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Mkoa wa Tanga Dkt. Zabron Nziku amemweleza Katibu Mkuu Prof. Gabriel kuwa wameanzisha maabara ya kisasa kwa ajili ya kutengeneza virutubisho vya mifugo vinavyotokana na zao la muhogo ambavyo havina gharama kubwa kwa wafugaji.

Naye Meneja wa Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) Kampasi ya Buhuri Mkoani Tanga Bw. Venance Tarimo amesema chuo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu ili kupata wataalam bora wa mifugo nchini.

Akihitimisha ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Tanga katika taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Katibu Mkuu wa wizara hiyo anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amekutana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Bi. Judica Omari na kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazowakumba wafugaji katika mkoa huo na namna ya kuzitatua.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel alikuwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Tanga mwishoni mwa wiki hii ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) ambazo zote zipo chini ya wizara hiyo.

Mwisho.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger