Friday 29 May 2020

BREAKING: Zitto Kabwe Kaachiwa Huru Kwa Sharti La Kutotoa Maneno ya Uchochezi

Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo Zitto Kabwe ameachiwa huru  na Mahakama ya Kisutu kwa sharti kwamba asitoe matamshi ya uchochezi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Katika kesi hiyo   ya uchochezi,  Zitto Kabwe  alikuwa anatuhumiwa kutoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki  akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika katika makao makuu ya ofisi ya Chama cha ACT –Wazalendo Oktoba 28, 2018


Share:

PICHA: Zitto Kabwe Kawasili Mahakamani Kusikiliza Hukumu Yake Huku Tayari Akiwa Ameshanyoa Kipara

Mbunge wa Kigoma ambaye ni Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amewasili Mahakamani pamoja na Mawakili wake, kusubiri hukumu dhidi ya kesi yake ya uchochezi huku akiwa tayari amesha nyoa kipara.

Hukumu hiyo ya kesi ya uchochezi, inayotarajiwa kuvuta hisia za watu mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania, itatolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Kesi hiyo iliyofunguliwa tarehe 2 Novemba 2018 na Jamhuri, itahitimishwa leo kwa Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, ama kutupwa gerezani, kupigwa faini, au kuachiwa huru

Katika kesi ya msingi, Zitto anadaiwa Oktoba 28, 2018 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika katika makao makuu ya ofisi ya Chama cha ACT –Wazalendo, alitoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki.


Share:

Waziri Kairuki “Changamkieni Fursa Za Uwekezaji Wa Mafuta Ya Alizeti”.

NA MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe. Angellah Kairuki ametoa rai kwa Watanzania kuwekeza katika sekta ya mafuta ya kula kwa kuzingatia uhitaji na soko lililopo ndani na nje ya nchi.

Ametoa rai hiyo Mei 28, 2020 alipotembelea na kukagua kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kula cha SUNSHINE kinachozalisha mafuta yanayotengenezwa kwa kutumia malighafi ya alizeti yanayoitwa Sunbelt kilichopo katika eneo la Zuzu Jijini Dodoma.

Akiwa katika ziara hiyo, yenye lengo la kukagua, kusikiliza na kutatua changamoto za wawekezaji nchini.Waziri Kairuki alipongeza uwekezaji katika kiwanda hicho chenye uwezo wa kuzalisha tani 25 kwa siku na kilichowekeza zaidi ya shilingiBilioni 230.

“Niwapongeze kwa uwekezaji mkubwa mlioufanya katika eneo hili tangu mwaka 2015 na hii inaleta chachu kwa wawekezaji wazawa kuona fursa na soko la malighafi wanazozalisha hasa zao la alizeti,”alisema Waziri Kairuki

Aliongezea kuwa, ni vyema watanzania wakaendelea kuchangamkia fursa ya kilimo cha zao la alizeti kwa kuzingatia uhitaji mkubwa wa mafuta ya kula nchini kwani nchi imekuwa ikipoteza zaidi ya shilingi bilioni 443 kwa mwaka kwa kuagiza mafuta nje ya nchi.

Aidha Waziri alibainisha kuwa  uwekezaji huo ni miongoni mwa fursa muhimu na kuwataka wenye uwezo kulima zao hilo kwa wingi kuchangamkia  fursa hiyo kwa vile zao hilo linastawi katika ukanda huo.

Alitumia fursa hiyo kuendelea kuwasihi wataalam wa masuala ya kilimo kutoa elimu kwa umma kuhusu kilimo bora cha zao hilo ili kuwa na utaalam wa kutosha kuhusu kilimo cha zao hilo  ili kutumia mbinu za kisasa na zenye kuzingatia viwango vinavyotakiwa.

Akitoa taarifa ya kiwanda hicho, Meneja Biashara na Maendeleo wa kiwanda hicho Bw. Krishna Urs alieleza changamoto wanayokabiliana nayo ni uhaba wa malighafi kwa ajili ya uzalishaji na kuendelea kutoa wito kwa wadau kuitumia fursa ya kilimo cha zao hilo ili kuendana na mahitaji halisi.

“Ni muhimu kuwekeza zaidi katika alizeti kwa sababu soko lake lipo na hii itatatua changamoto ya kuzalisha kwa uchache na kuwafikia wananchi  wengi na kuapata soko la nchi za nje”, alisema Krishna.

Naye Afisa Viwango wa kiwanda hicho, Upendo Mganda alipongeza uwekezaji huo kwa kuwa, umesaidia kutoa ajira  na vibarua  kwa wananchi walio wengi.

“Tunashukuru uwepo wa kiwanda umetusaidia kupata ajira na wazawa wameweza kuuza malighafi zao kiwandani hapa kwa bei yenye tija,” alisema Upendo

Aidha aliongezea kuwa, ni kiwanda chenye tija kwa kuzingatia uwezo wake wa uzalisha tani 24 hadi 25 kwa siku na kinafanya vizuri sokoni kwa kuzingatia kuwa mafuta yanayozalishwa hayana kemikali zenye athari kwa watumiaji.

“Uzalishaji ni wa kuridhisha japo kuna changamoto ya uchache wa malighafi unaochangia kusuasua kwa uzalishaji na kusababisha kuzalisha kwa msimu si ya mavuno pekee inayochangia kutolifikia mahitaji halisi nchini,”alisema Upendo.

=MWISHO=


Share:

Hukumu Ya Zitto Kabwe Kusomwa Leo Ambapo Ndipo Hatima Yake Itajulikana Kama ni Faini, Kifungo au Kuachiwa Huru

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo  Ijumaa, tarehe 29 Mei, inatarajia kusoma hukumu ya kesi inayomkabili Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe

Hukumu hiyo ya kesi namba 327/2018 ya uchochezi, inayotarajiwa kuvuta hisia za watu mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania, itatolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi. 

Kesi hiyo iliyofunguliwa tarehe 2 Novemba 2018 na Jamhuri, itahitimishwa leo kwa Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, ama kutupwa gerezani, kupigwa faini, kufungwa au kuachiwa huru
 
Katika kesi ya msingi, Zitto anadaiwa Oktoba 28, 2018 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika katika makao makuu ya ofisi ya Chama cha ACT –Wazalendo, alitoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alinukuliwa “…watu ambao walikuwa ni majeruhi katika tukio la mapambano baina ya wananchi na polisi wakiwa wamekwenda hospitali kupata matibabu katika kituo cha afya Nguruka, polisi wakapata taarifa kuwa kuna watu wanne wamekwenda hospitali kituo cha afya Nguruka kupata matibabu wakawafuata kule wakawaua…”

Katika shitaka ya pili ilidaiwa Oktoba 28, 2019 eneo la Kijitonyama katika makao makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam, alitoa maneno ya uchochezi dhidi ya Jeshi la Polisi akisema “…lakini tumefuatilia kwa kina jambo hili, taarifa ambazo tumezipata kutoka kijijini Mpeta-Nguruka, Uvinza ni mbaya, ni taarifa ambazo zinaonyesha wananchi wengi sana wameuawa na jeshi la Polisi pamoja na kwamba afande Sirro amekwenda kule, haijatoa taarifa yoyote kuhusu wananchi…kama hawa Wanyantuzu walivamia eneo la Ranchi kuna taratibu za kisheria za kuchukua na sio kuwauwa, wananchi wengi sana wamekufa…”

Ilidaiwa kuwa katika tarehe hiyo hiyo, Zitto alitoa maneno ya uchochezi dhidi ya Jeshi la Polisi akisema “… Tumekuwa tukifuatilia kwa kina yanayojiri yote huko Uvinza tunasikitika kusema kuwa taarifa tunazozipata kutoka Uvinza zinaogofya mno, kwani tunaambiwa kuwa wananchi zaidi ya 100 wa kabila la Wanyantuzu wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi na polisi, wengine wakisema kuuawa hata wakiwa kwenye matibabu hospitalini baada ya kujeruhiwa kwenye purukushani na jeshi la polisi…’’

Katika shauri hilo, upande wa mashitaka uliwasilisha mashahidi 15, huku Zitto akiwasilisha mashahidi nane.

Upande wa mashtaka uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka akisaidiwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga; huku Zitto akitetewa na mawakili watatu wakiongozwa na Jebra Kambole.

Mawakili wengine waliomtetea Zitto, ni Frank Mwakibolwa na Bonifacia Mapunda.



Share:

Ufaransa Yaipongeza Tanzania Mapambano Dhidi Ya Virusi Vya Corona

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Pamalagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Frederic Clavier ambapo pamoja na mambo mengine, Balozi Clavier ameipongeza Tanzania kwa hatua ilizochukua kupambana na janga a virusi vya corona nchini.

Balozi Clavier pia amemhakikishia Mhe. Waziri kuwa Ufaransa inaiunga mkono Tanzania kwa asilimia 100 kwa hatua ilizochukua kupambana na janga la virusi vya corona na kusema Ufaransa itaipatia Tanzania Euro milioni 30 ikiwa ni mkopo wenye masharti nafuu na riba ndogo kwa ajili ya kupambana na janga la virusi vya Corona pamoja na kusaidia kuinua uchumi.

Katika mazungumzo yao, Mhe. Waziri Kabudi amemuelezea Balozi wa Ufaransa jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kupambana na Janga la Corona nchini na kumhakikishia utayari wa Tanzania katika kupambana na janga hilo na kuongeza kuwa Serikali ya Tanzania ilichukua hatua hizo kulingana na hali halisi ya maisha ya watanzania.

Prof. Kabudi amesema hatua zilizochukuliwa na Tanzania zililenga kuwafanya watanzania kuendelea na maisha yao bila ya kuathiriwa kiuchumi huku wakijilinda na kuchukua tahadhari ambazo zilikuwa zikitolewa na wataalamu wa afya nchini na duniani.

Balozi Clavier amemuambia Mhe. Waziri Kabudi kuwa Ufaransa pia imetoa msaada wa Dola 500,000 ambazo watapewa wakulima wadogowadogo 6,000 nchini kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha kilimo chao na maghala ya kuhifadhia mazao yao.

Ameongeza kuwa Rais wa Ufaransa ameziandikia nchi za G20 na Paris Club kuzishawishi kuahirisha ulipaji wa madeni na riba zake na pia kufuta kabisa madeni hayo ili kuimarisha uchumi ambao umeathiriwa na janga la corona katika nchi zinazoendelea.

Katika hatua nyingine Waziri Kabudi amekutana na kuagana na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Ali Davutaglu ambaye amemaliza muda wake wa utumishi na amemtakia maisha mema na kumwambia kuwa ni matarajio yake kuwa atakuwa Balozi wa hiari wa Tanzania nchini uturuki na kwingineko duniani.

Naye balozi Davotaglu ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano ambao imekuwa ikimpatia alipokuwa akitekeleza majukumu yake nchini na kuahidi kuwa ushirikiano uliopo utaendelezwa hasa ikizingatiwa kuwa. 


Share:

Wafungwa Vifungo Vya Nje Watakiwa Kufanya Kazi Zinazoonekana Na Wadau

Na Veronica Mwafisi, MOHA-Morogoro
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Chritopher Kadio, ameitaka Idara ya Huduma za Uangalizi kuhakikisha wafungwa wenye vifungo vya nje wanafanya kazi zinazoonekana kwa wadau.

Alisema kutekelezwa kwa agizo hilo, wadau wataona faida ya wahalifu kutumikia adhabu zao nje ya Magereza badala ya kufanya usafi kwenye maofisi.

Kadio aliyasema hayo Mjini Morogoro jana wakati akifungua mkutano wa siku mbili unaoshirikisha Maafisa Wafawidhi wa idara hiyo kutoka mikoa 23 nchini.

Alitoa wito kwa idara hiyo kuandaa mpango mkakati ambao utaiwezesha Serikali kupunguza mzigo wa kuwahudumia wahalifu waliopo gerezani.

Alisema baadhi ya wahalifu wanaweza kutumikia adhabu zao nje ya Magereza hivyo ni wakati muafaka kwa idara hiyo kuwa na suluhisho ili changamoto hiyo iweze kupatiwa ufumbuzi.

“Lipo tatizo kubwa ambalo linaukabili mpango huu hasa fikra za kizamani kuwa adhabu ya kila mhalifu ni kwenda jela, dhana ya adhabu mbadala bado haijakolea katika fikra za wengi.

“Fikra hizo zipo kwenye sekta zote za jamii yetu kuanzia katika mahakama, baadhi ya Mahakimu wana kigugumizi cha kutoa adhabu za kutumikia jamii nje ya jela,” alisema.

Alifafanua kuwa, pia kwenye jamii vijijini na mitaani bado hawajaona umuhimu wa kutekeleza jukumu la kuwarekebisha na kuwalea jamaa zao wnaojiingiza katika uharifu.

Kadio alisema viongozi wa kisasa nao hawajalichangamkia jambo hilo na kulipigia debe kwa nguvu zote.

“Ni imani yangu kuwa idara pamoja na Wizara tunalo jukumu la kuhamasisha na kutoa elimu kwa wadau tukianzia mikoani, kila kiongozi wa Mkoa awe na mpango kazi wa kuelimisha.

“Mbali ya kuhamasisha matumizi ya adhabu mbadala pia ni jukumu letu kuhamasisha jamii ijiepushe na vitendo vya uhalifu, kuheshimu utawala wa sheria unaozingatia haki,” aliongeza.

Alisema pamoja na changamoto nyingi zinazoikabili idara hiyo katika utendaji kazi wao, aliwataka wakuu wa idara watafute ufumbuzi wake badala ya kuitegemea serikali izitatue.

Kadio alisema Wizara hiyo itaendelea kuwawezesha kadri inavyoweza ndio maana kila mwaka inaboresha bajeti yao.

“Ni vema mkafahamu kuwa, dhamira na dira ya Wizara yetu ni kudumisha utulivu, usalama na amani kwa Watanzania na ili dhamira hii ikamilike, idara imepewa jukumu la kusimamia utekelezwaji wa adhabu mbadala ya kifungo gerezani.

“Mnalo jukumu la kuchangia mafanikio ya Wizara iweze kufikia dhamira yake kwa Taifa,” alifafanua.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara hiyo, Aloyce Musika, alisema lengo la mkutano huo ni kufanya tathmini ya shughuli zilizofanyika mwaka mzima, kupanga mipango ya mwaka ujao.

Alimshuruku Kadio kwa kufungua mkutano huo ambao unashirikisha Maafisa Wafawidhi kutoka mikoa 23 ambayo wameifikia nchini isipokuwa mikoa mitatu ya Katavi, Lindi pamoja na Ruvuma.

“Miaka yote tumekuwa tukifanya mkutano kama huu kwa mafanikio makubwa mbali ya ugumu wa bajeti lakini Wizara imekuwa karibu na sisi, kukaa pamoja,” alisema.

MWISHO.


Share:

HALMASHAURI YA JIJI YAMPONGEZA RAIS JPM KWA HATUA ALIZOCHUKUA KUKABILIANA NA COVID 19



 Kaimu Ofisa Afya wa Jiji la Tanga Hamza Maulidi akizungumza wakati akitoa elimu katika semina ya siku mbili
inayotolewa kwa Wasaidizi wa msaada wa kisheria (Paralegals) kutoka halmashauri 11 zilizopo mkoani Tanga,

 Kaimu Ofisa Afya wa Jiji la Tanga Hamza Maulidi akizungumza wakati akitoa elimu katika semina ya siku mbili
inayotolewa kwa Wasaidizi wa msaada wa kisheria (Paralegals) kutoka halmashauri 11 zilizopo mkoani Tanga

 Programu Meneja wa Shirika la TEWOREC Halima
Jabiri Saguti akisisitiza jambo jana wakati akitoa elimu ya msaada wa kisheria kwa wasaidizi wa kisheria Mkoani Tanga yaliyoendeshwa na Shirika hilo Jijini Tanga kwa kushirikisha wilaya zote za mkoa huo
 AFISA wa Tathimini na Ufuatiliaji wa Taasisi ya TEWOREC akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo
 Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira Mashaka Mhando akitoa uzoefu wake wakati wa semina hiyo

 Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akichangia


HALMASHAURI ya Jiji la Tanga, imempongeza Rais John Magufuli, kwa hatua alizochukua kukabiliana na ugonjwa wa Corona nchini.

Sambamba na pongezi hizo, ugonjwa huo katika Jiji la Tanga unapungua kwa kasi kutokana na wananchi wengi kuchukua tahadhari zinazotolewa na Serikali pamoja na wataalamu wa afya.

Akizungumza kwenye semina ya siku mbili inayotolewa kwa Wasaidizi wa msaada wa kisheria (Paralegals) kutoka halmashauri 11 zilizopo mkoani Tanga, Kaimu Ofisa Afya wa Jiji la Tanga Hamza Maulidi alisema wananchi hawana budi kumpongeza Rais kutoka na kututoa hofu tangu alipogundulika mgonjwa mmoja hapa nchini.

Alisema kweli ugonjwa huo bado upo nchini na wananchi waendelee kuchukua tahadhari zote pamoja na kwamba maambukizi yanashuka kwa kasi kubwa Jijini hapa, lakini pia wanampongeza Rais kwa hatua alizochukua hadi ugonjwa unaendelea kupungua.

"Ugonjwa upo na Tanga pia upo, tuchukue hatua tunazoelekezwa na wataalamu wetu wa afya, lakini kwa kweli tunampongeza mheshimiwa Rais kwa kututia faraja tangu ugonjwa huu umeanza," alisema Maulidi.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo walisema yametolewa wakati muafaka ambao shughuli za kiserikali nyingi zimeanza kufanyika baada ya mikusanyiko kuzuia hivyo itawasaidia kupata uelewa mkubwa wa ugonjwa huo na taadhari zake.

Awali akifungua mafunzo hayo Meneja wa Shirika la kutoa msaada wa kisheria mkoani Tanga (TAWOREC) Halima Saguti alisema lengo la kutoa mafunzo kwa Paralegal hao ni kutaka wanapotoa huduma kwa wananchi huko vijijini waweze kujiinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

Alisema kazi za wasaidizi hao wa kisheria zimekuwa zikiendelea huko vijijini na hivyo kupewa elimu hiyo kutasaidia kupunguza kusambaa kwa ugonjwa huo kwa watu wengine.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa May 29



















Share:

Thursday 28 May 2020

Nafasi Mpya Za Kazi Zilizotangazwa Wiki Hii...Bofya Hapa

Share:

Ugonjwa Wa Malaria Wazidi Kupungua Nchini

Na.WAMJW,Chunya
Takwimu za kitaifa za viashiria vya malaria kwa mwaka 2017 (Malaria Indicator Survey) inaonesha kuwa upatikanaji wa vyandarua (access) kwa wananchi kitaifa ni asilimia 63 na matumizi ya vyandarua kwa wanajamii kitaifa ni asilimia 52.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa vyandarua kwa kila kaya uliofanyika wilayani Chunya.

Waziri Ummy amesema kuwa Mkoa wa Mbeya, upatikanaji wa vyandarua ni asilimia 62 na kiwango cha matumizi ya vyandarua kwa Mkoa ni asilimia 32 tu.

“Nchi yetu imepiga hatua kubwa na kupata mafanikio katika mapambano dhidi ya Malaria ambapo kiwango cha maambukizi kimepungua kwa karibu asilimia 50, kutoka asilimia 14.8 mwaka 2015 hadi asilimia 7.3 mwaka 2017. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema hiyo ni kutokana na takwimu za matokeo ya utafiti wa viashiria vya Malaria katika jamii (MIS 2017) ambapo visa vipya vya Malaria vimepungua kwa asilimia 19 kutoka visa 150 kati ya watu 1000(2015) hadi visa 122 kati ya watu 1000(2019).

Ameongeza kuwa idadi ya vifo vitokanavyo na Malaria vimepungua kwa asilimia 67 kutoka vifo 6311 mwaka 2015 hadi vifo 2079 mwaka 2019.

“Kwa mkoa wa Mbeya pia maambukizi yapo kwa kiasi cha asilimia 4 kiwango hiki ni kidogo ukilinganisha na wastani wa kitaifa wa asilimia 7.3

Aidha, Waziri Ummy amesema kila mwanafamilia mwenye dalili za Malaria ahakikishe kuwa anawahi kwenye kituo cha kutolea huduma za afya ili kupimwa kabla ya kutumia dawa kwani sio kila homa ni Malaria na endapo atagundulika kuwa na vimelea vya malaria ahakikishe anatumia dawa kulingana na maelekezo ya mtoa huduma za afya na kumaliza dozi ili kuepuka usugu wa dawa mwilini.

Ugawaji wa vyandarua unafanyika kwa awamu tatu kupitia Bohari Kuu ya Dawa(MSD) ambapo awamu ya kwanza inajumuisha mikoa ya Mbeya,Songwe,Njombe na Rukwa

Awamu ya pili ni mikoa ya Iringa, Dodoma na Singida na awamu ya tatu na ya mwisho itahusisha mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Manyara.

Hata hivyo mikoa mingine iliyobaki itaendelea kupata vyandarua kupitia kliniki ya afya ya uzazi (wajawazito) na watoto chini ya mwaka mmoja na pia kupitia wanafunzi wa shule za msingi.


Share:

MBUNGE WA KAHAMA MJINI AOMBA SERIKALI IFUNGUE 'CHUO CHA WIZI'



Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba.

Mbunge wa Kahama Mjini kupitia CCM Jumanne Kishimba, ameiomba Serikali ifungue chuo cha wizi kwa kuwa matukio ya wizi katika sekta za umma na Halmashauri nyingi umeshamiri kwa kiasi kikubwa na kwamba chuo hicho kitasaidia wale watu wanaoenda kuchunguza wezi, kuzijua mbinu zao na kuwabaini.

Hayo ameyabainisha leo Mei 28, 2020, Jijini Dodoma wakati wa mkutano wa 19, kikao cha 39, wakati wa uchangiaji wa hoja ya Kamati ya Kudumu ya Huduma za Serikali za Mitaa, na kueleza kuwa ni vyema chuo hicho kikawekwa japo kwa kutumia jina lingine ili kukomesha suala hilo.

"CAG na Waziri wa Fedha yuko hapa hawa vijana wanaoajiriwa lazima wanatoka shule inayofundisha maadili mema na uaminifu, sasa wanaenda kupambana na wizi wengine wamesoma Seminari, kwanini serikali haifikirii sasa kuanzisha chuo cha wizi, kwa maana mtu anapochaguliwa kwa sifa ya uaminifu kwenda kupambana na wezi anaenda kupambana nao namna gani? afadhali apite kwenye chuo hicho kwa miezi mitatu ili ajue akili ya wizi, hawa vijana wetu tutawamalizia magerezani na hali ya wizi ni mbaya sana", amesema Mbunge Kishimba.
Via >>EATV
Share:

Riwaya Kali ya Kusisimua....SIN- Sehemu Ya Tano (05)

Mwandishi- EDDAZARIA G.MSULWA
Age-18+
Simu-0657072588(whatsapp) au 0768516188


ILIPOISHIA
“Kwa nini kaka?”
“Kuna watu wana wateka watu na wanavishwa jina.... Yaani nashindwa hata kuelewa, tunaelekea wapi?”
“Nani mwengine ametekwa?”
“Si yule nabii Sanga wa kanisa la Heaven light ministry”
Mapigo ya moyo wa Magreth, yakasimama kwa sekunde kadhaa, kisha yakaanza kumuenda kasi, mwili mzima ukaanza kumtetemeka na jasho likimtiririka usoni mwake, hadi muendesha bajaji akabaki akiwa ameshikwa na butwaa kwa nini hali ya abiria wake imebadilika gafla mara ya kusikia taarifa hiyo.


ENDELEA   
“Dada upo salama?”
Dereva wa bajaji aliuliza huku akimtazama Magreth kwa macho ya kuiba iba kwani anahitajika kuwa makini katika barabara hiyo yenye magari mengi sana.
“Dada”
“Beee”
“Upo salama?”
“Umesema wamemteka nani?”
“Nabii Sanga, “
“Wamemuaa?”
“Hapana, hakuna taarifa kama hiyo, ila polisi wana dai kwamba gari lake kwenye kioo cha mbele kilipigwa kwa risasi moja”
Magreth akazidi kutetemeka kwa woga huku hali ya kukata tamaa ikiendelea kumtawala. Akataka kupiga namba ya nabii Sanga na kujikuta nafsi yake ikiendelea kusita na kushindwa kabisa kufanya hivyo. Akafikishwa hospitalini, akamlipa muendesha bajaji kiasi cha pesa anacho kihitaji, kisha akashuka kwenye bajaji hiyo, huku mwili mzima ukiwa umeishiwa na nguvu. Akaanza kutembea kwa mwendo wa taratibu, huku akihisi kukata tamaa, ndoto zake zote ambazo kwa siku hiyo zilikuwa zinakwenda kutimia, zote zimepotea. Akaingia ndani ya chumba alicho lazwa Evans. Wakatazamana na Evans kwa sekunde kadhaa kisha akaanza kuangua kilio kizito, kilicho mfanya Evans kushangazwa.
“Hei Mage kwa nini unalia?”
“Mchungaji?”
“Mchungaji amefanya nini?”
“Ametekwa na watu wasio julikana”
Habari hii hakika haikuwa nzuri kwa Evans.
“Mchungaji gani lakini, au yule uliye kuja naye hapa jana usiku?”
“Huyo huyo, ohoo Mungu wangu. Ni kina nani wamemfanyia mambo hayo jamani”
Magreth alizungumza huku akiendelea kulia kwa uchungu sana, hadi ikamlazimu, Evans kuanza kumbembeleza.
                                                                                                                                ***
    Majira ya saa mbili asubuhi, watekaji wawili wakaingia kwenye chumba walicho muhifadhi nabii Sanga. Wakamfungua kamba walizo mfunga na kumkalisha kwenye kiti. Wakamfungua kitambaa usoni mwake. Nabii Sanga akakutana na wanaume hao ambao wameendelea kufunika sura zao. Mbele yake kuna meza iliyo wekwa kikombe cha chai ya maziwa pamoja na vipande vinne vya mkate ulio pakwa blueband vizuri.
“Pata kifungua kinywa”
Mtekaji mmoja alizungumza huku mkononi mwake akiwa na bastola.
“Vijana, ninaomba tuweze kuzungumza. Kama ni pesa ambayo mumelipwa kwa ajili ya kuniteka. Tafadhali, nipo tayari kuhakikisha kwamba nina walipa mara mbili ya pesa hiyo ambayo mume pangiwa kunilipa”
“Mzee acha siasa, unahitaji kula au unahitaji kufa?”
Mtekaji wa pili alizungumza kwa ukali sana, mwezake akamnyooshea mkono kwa ishara ya kumuomba aweze kutulia.
“Una weza kutupatia ofa gani?”
“Mkuu unakosea?”
“Hapa, tuna fanya kazi hii kwa pesa. Upo tayari kutupa ofa gani?”
Mtekaji huyo alizugumza huku akisimama mbele ya nabii Sanga.
“Semeni aliye wapa hii kazi amewalipa kiasi gani?”
“Milioni ishirini”
“Nipo tayari kuwapa milioni hamsini by cash”
“By cash, unazo hapo ili uweze kutupatia?”
“Mukikubali na mukiniamini basi nita hakikisha kwamba nina wapatia hicho kiasi. Ila kabla sijafanya hivyo, nina waomba muweze kunisaidia jambo moja”
“Jambo gani?”
“Ninahitaji kumfahamu mtu aliye weza kutoa kazi hii”
“Siku zote huwa tuna linda siri za wateja wetu. Hatuto weza kukuambia ni nani ambaye ametupatia kazi hiyo.”
“Milioni sabini nawapatia”
“Hatuwezi kutoa siri”
“Milioni themani”
“Mzee hatuto weza kukuambia siri kwa ajili ya pesa”
“Milioni mia moja cashe munazipata katika siku hii hii ya leo”
Watekaji hawa wakatazamana usoni. Hapakuwa na kazi kubwa walio ifanya kwenye maisha yao, ambayo walihi kulipwa milioni mia moja. Uchu wa pesa ukawajaa mioyoni mwao, wakavutana pembeni ya chumba hicho na kuanza kunong’onezana.
“Mkuu tukubali hiyo ofa, milioni mia moja ni kubwa sana”
“Kawaite wezako”
“Sawa”
Mtekaji huyo akatoka na baada ya dakika moja akarudi akiwa ameongozana na wezake ambao nao sura zao wamezifunika. Mkuu wao akawaeleza ofa iliyo wekwa mezani na nabii Sanga.
“Mkuu ni pesa nyingi, kama ana uhakika wa kutupatia hicho kiasi hakuna haja ya sisi kuendelea kumshikilia. Yaani hapo ni sawa una ambiwa uchague Vitz na Hammer”
Hapakuwa na mtekaji yoyote ambaye aliweza kukataa ofa hiyo.
“Natambua kwamba muna fanya kazi hii kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya maisha yenu, ikiwemo familia zenu. Nipo tayari kuwalipa kiasi hicho cha pesa na nyinyi mkawa ni watu wa mkono wangu wa kushoto”
Nabii Sanga aliendelea kuwashawishi watekaji hawa.
“Una maanisha nini kusema tuwe watu wa mkono wako wa kushoto?”
“Haya ni maisha, kesho na kesho kutwa nami nitakuwa na kazi ya kuwapatia, je mtashindwa kuifanya?”
Watekaji hawa wakatazamana huku sura zao wakiwa wamezifunika na kubakisha macho tu.
“Tutafanya”
“Basi kwa leo nipatieni hiyo nafasi ya kuwalipa na muweze kuniambia ni nani ambaye ameifanya kazi hiyo.”
Ushawishi wa nabii Sanga ukazidi kuwapagawisha watekaji hawa.
“Sawa tupo tayari ila kwa sharti moja”
“Niambieni”
“Pesa tuna ihitaji iweze kuletwa hapa”
“Ndio iletwe hapa, hatuwezi kurudi mjini. Polisi wapo makini kukutafuta nchi nzima. Changanua akili yako kisha hakikisha kwamba hiyo pesa ina letwa hapa na huyo atakaye ileta hapa awe ni mtu ambaye una muamini na asije akafanya kosa lolote la kipumbavu, kuwaeleza polisi. Akifanya hivyo nina apia kwa MUNGU. Nitakuchinja kama kuku”
Mkuu wa kikosi hicho cha watekaji alizungumza huku akimtazama nabii Sanga usoni mwake. Nabii Sanga akaanza kuchanganua akilini mwake ni nani ambaye ata muamini. Akili ikatua kwa mke wake, ila akajikuta akipata ukinzani mkubwa sana moyoni mwake.
‘Kwa nini nafsi yangu ina kataa kwa mke wangu. Kuna nini?’
Nabii Sanga alizungumza kimoo moyo huku akiendelea kutafuta ni nani ambaye anaweza kumuamini na kumkabidhi kazi hiyo. Akafikiria baadhi ya wachungaji wa kanisani kwake, ila hapo napo hakuweza kupata mtu wa uhakika wa kuwaamini.
“Mzee una dakika moja ya kutujulisha ni nani utakaye muamini”
Mtekaji huyo alizungumza na kumfanya nabii Sanga kuongeza umakini wa kuwachanganua watu wake wa karibu na kujua ni nani anaweza kuwaamini. Akili ikaangukia kwa Magreth, mwanamke aliye tokea kumpenda na kumjali kwa kipindi cha hivi karibuni. Moyo wake katika kumuamini Magreth haukuwa na wasiwasi hata kidogo.
“Nimempata”
“Nani?”
“Ahaa ni muumini wangu wa karibu ana itwa Magreth”
“Muumini, hato weza kutoboa siri kwa askari?”
“Hapana. Nina muamini sana.”
Watekaji hawa wakatazamana kisha mkuu wao akamsogelea nabii Sanga. Akamtazama machoni mwake kwa sekunde kadhaa kisha akatoa simu yake na kuiweka mezani.
“Endapo utafanya kosa lolote, nitakufumua ubongo wako. Mpigie na uweke loud speaker”
“Sawa sawa”
Nabii Sanga akaichukua simu hiyo, akafumba macho yake kwa sekunde kadhaa, huku akijaribu kuikumbuka namba ya Magreth na kwa bahati nzuri akafanikiwa kuikumbuka, akaiingiza katika simu hiyo kisha akaipiga na kwa bahati nzuri akakuta ina patikana hewani.
                                ***
    Mlio wa taratibu unao ita katika simu yake, ukamfanya Magreth kuitazama simu yake. Evans aliye lala pembeni yake, naye akamtazama Magreth kwa sekunde kadhaa anaye endelea kuitazama simu yake inayo ita.
“Mbona hupokei simu?”
“Hii namba yangu ni mpya na hakuna mtu yoyote anye ifahamu”
“Mmmm sasa inakuwaje watu wameifahamu?”
Evans aliuliza, taratibu Magreth akaipokea simu hiyo na kuiweka sikioni mwake.
“Haloo”
Magreth alizungumza kwa umakini sana huku akisubiria kusikilizia ni nani huyo aliye mpigia.
“Ni mimi Magreth, usijaribu kutaja jina langu wala kuonyesha dalili yoyote ya kuweza kunifahamu, kwa maana nina hisi upo na watu”
Sauti ya nabii Sanga ikamfanya Magreth macho kumtoka. Akasimama huku akiwa amejawa na tabasamu.
“Nisikilize kwa umakini mkubwa sana, kwanza upo wapi?”
“Hospitali”
“Simama sehemu ambayo hakuna mtu anaye weza kusikiliza mazungumzo yetu”
Magreth kwa haraka akatoka ndani humo pasipo hata kumuaga Evans. Akatafuta eneo lisilo na mtu na akasimama.
“Unaweza kuendelea”
“Nipo chini ya watekaji, wanahitaji kiasi cha milioni mia moja.”
“Mungu wangu!!”
“Nisikilize, wewe ndio mtu wa pekee ambaye ninakuamini na unaye weza kunisaidia mimi kutoka katika kifungo hichi”
Nabii Sanga alizungumza kwa msisitizo mkubwa sana.
“Ehee”
“Nenda pale kanisani, password ya mlango wa ofisini kwangu ni tisa, moja, moja tisa moja, sifuri. Fungua mlango wa ofisini kwangu, kuna shelf kubwa imo mule ofisini, fungua hiyo shelf kwa kutumia password hizo hizo nilizo kutajia. Kuna pesa za kimarekani. Chukua dola alfu sitini, weka kwenye begi, ukifanikisha kufanya hivyo hakikisha kwamba una piga namba hii, kwa ajili ya maelekezo zaidi. Ninakuomba Magreth usimuambie mtu wa aina yoyote. Ukifungua kinywa chako, basi tambua mimi huku nina kufa”
Magreth mwili mzima ukamtetemeka, akashusha pumzi huku akifikiria ni wapi anapo weza kuanzia.
“Baba mchungaji lakini upo salama”
“Ndio yupo salama na endapo utafungua kinywa chako kwa askari. Tutamuua na wewe tutakutafuta na kukuua”
Sauti hiyo nzito ya mwanaume, ikamstua sana Magreth. Mwili mzima ukazidi kutawaliwa kwa woga. Simu ikakatwa na kumfanya aishiwe hata nguvu za kusimama. Akakaa chini kwa sekunde kadhaa huku akitafakari ni wapi kwa kuanzia.
‘Lazima nimsaidie, ndio lazima nimsaidie’
Magreth alizungumza kimoyo moyo huku akinyanyuka eneo hilo. Wazo la kurudi chumbabini kwa Evans wala hakuweza kuwa nalo kabisa. Akakodisha pikipiki na akarudi nyumbani kwake, akatoa nguo zilizomo kwenye begi lake la mgongoni. Alipo hakikisha begi hilo halina nguo akalivaa na kutoka ndani humu. Akapanda pikipiki nyingine na kufikishwa kanisani. Kutokana mlinzi wa kanisa hilo wana fahamiana, hapakuwa na tatizo la yeye kufunguliwa geti.
“Mage una habari yoyote ya kupatikana kwa nabii?”
Mlinzi aliuliza huku akiwa amejawa na unyonge mkubwa sana.
“Hapana kaka. Nimekuja kumuomba MUNGU japo aweze kulete rehema yake”
“Sawa Mage ila huko hakuna mtu yoyote”
“Hakuna shaka”
Magreth akamuongopea mlinzi huyo. Akaingia kwa mlango wa mbele wa kanisa hilo, ili kumdanganya mlinzi asiweze kufahamu kwamba lengo na nia iliyo mleta hapo kanisani ni kuingia katika ofisi ya nabii Sanga. Magreth akatoke katika mlango mwingine wa kanisa hilo na kuelekea ilipo ofisi ya mchungaji. Akasimama mlangoni hapo na kuchunguza eneo hilo kwa umakini. Alipo hakikisha hakuna mtu wa aina yoyote akaingiza namba hizo za siri alizo tajiwa na mchungaji. Mlango ukafunguka na kuzama ndani na huku nyuma mlango ukajifunga.
Magreth akaanza kuangaza macho yake huku na huku na kufanikiwa kuona shelf kubwa iliyomo ofisini hapo, akaisogelea na akaingiza namba hizo za siri. Mlango mzito wa shelf hiyo ukafunguka. Magreth macho yakamtoka mara baada ya kukuta vibunda vya pesa za kimarekani(USD DOLLARS) vikiwa vimepangwa vizuri. Akaanza kuvihesabu kwa haraka haraka. Alipo hakikisha kwamba ni dola elfu stini, akaziingiza kwenye begi lake na kulivaa mgongoni. Akaanza kutembea kuelekea mlangoni, ila kabla hajaufungua mlango, akasikia hatua za miguu ya watu zikija katika mlango huo. Akatazama eneo hilo na kwa haraka akakimbilia kwenye moja ya sofa iliyomo ndani humo. Akajificha nyuma ya sofa ambapo sio rahisi kwa mtu kuweza kumuona.
“Yaani mpenzi wangu, nimewakimbia maaskari nyumbani kwa ajili yako. Nimeona tusikutanie kwako kwa maana una weza kufaatiliwa na ukakamatwa bure”
Sauti ya mama chungaji ikamstua sana Magreth aliye jibanza nyuma ya sofa hilo.
“Usijali mpenzi wangu, acha nikupe chap chap tuondoke kwa maana nina hamu na wewe sasa”
Sauti ya Tomas haikuwa ngeni kabisa masikoni mwa Magreth, kwani mtu huyo ni jana tu ametoka kuonana naye uso kwa uso.
“Ila vijana wako walio mteka huyo mpuuzi, una waamini au ni watu wa ajabu ajabu?”
Magreth akazidi kujawa na mshangao ulio sababisha mapigo yake ya moyo kuanza kumuenda kasi sana. Siri ya Mrs Sanga na Tomas, imevuja masikioni mwake.
“Nina waamini sana, tena hakuna ambaye ana weza kuenenda kinyume na mimi. Unacho paswa ni wewe kunipatia milioni arobaini za kuwalipa tu”
“Usijali pesa sio tatizo kwangu, jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba wana mshikilia hadi wiki ijayo, na akiondoka kuelekea nchini Nigeria, yule kimada wake aliye panga kumnunulia nyumba na kumfungulia mgahawa nitamuua kwa mikono yangu mimi mwenyewe.”
Maneno hayo ya Mrs Sanga yakamfanya Magreth kuhisi haja ndogo ikianza kumtoka. Kama mwana mama huyo amefanya maamuzi ya kumteka mume wake bila ya huruma na yeye ndio anaye faatia kuuwawa, je itakuwaje endapo wata muona nyuma ya sofa hilo.
                                                                                                   ITAENDELEA
Haya sasa Magreth ametambua siri ambayo hakuna mtu mwingine ameweza kuifahamu huku akiwa na mzigo mkubwa sana wa kumsaidia nabii Sanga.Je ataweza kumsaidia nabii huyo?. Nini kitatokea? Endelea kufatilia kisa hiki cha kusisimua, usikose sehemu ya 06

 


Share:

Kenya Yaendelea Kurekodi Maambukizi Makubwa Zaidi Ya Wagonjwa Wa Corona

Idadi ya maambukizi ya corona nchini Kenya imefikia watu 1618, hii ni baada ya watu 147 zaidi kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo katika muda wa saa 24 zilizopita baada ya sampuli 2831 kufanyiwa uchunguzi.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema  kuwa miongoni mwa maambukizi hayo mapya 147, 90 ni jijini Nairobi na 41 ni huko Mombasa.

Vilevile idadi ya waliofariki imefikia 58 baada ya watu wengine watatu kufariki,wawili huko Mombasa na mmoja huko Kiambu.

Idadi ya waliopona imefikia 421 baada ya watu 13 zaidi kupona na kuondoka hospitalini.


Share:

Mpangaji Anayelipa Kodi Ya Zuio Anapaswa Kurejeshewa Na Mwenye Nyumba

Na. Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Serikali imesema kuwa Sheria ya Kodi ya Mapato inaruhusu mpangaji wa nyumba ya biashara kusajiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania na kuwa Wakala wa ukusanyaji wa Kodi ya Zuio (Withholding Tax) hivyo kuwa sehemu ya mlipaji wa kodi ya pango.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Pauline Gekul, aliyetaka kujua lini Serikali itabadili utaratibu wa kumtoza mpangaji wa nyumba ya biashara Kodi ya Zuio ya asilimia 10 badala ya mpangishaji.

Dkt. Mpango alisema kuwa, Kodi ya Zuio siyo ya mpangaji, na kwa kuwa Sheria ya Kodi ya Mapato inamtambua mpangaji kama Wakala, kiasi cha kodi ya pango ambacho kimelipwa na mpangaji huhesabiwa kama sehemu ya fedha ambazo anapaswa kurejeshewa na mwenye nyumba.

“Kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Mapato, mpangaji ambaye sio mfanyabiashara na hajasajiliwa na TRA kama mlipakodi hapaswi kukusanya kodi hii”, alieleza Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango alisema kuwa utaratibu wa ukusanyaji Kodi ya Zuio kupitia Wakala ambaye ni mpangaji umewekwa ili kurahisisha ukusanyaji wa kodi hiyo, kwa kuwa inarahisisha ukusanyaji wa kodi hasa ambapo mpangishaji hajasajiliwa na TRA kama mlipa kodi.

Sheria ya Kodi ya Mapato inamtaka mmiliki wa nyumba ya biashara mwenye mapato yanayozidi shilingi laki tano kulipa Kodi ya Zuio kutokana na mapato yanayotokana na upangishaji wa pango (rental tax) kwa kiwango cha asilimia 10 ya mapato ya kodi ya pango husika.

Mwisho.


Share:

Jakaya Kikwete: Hostel za Magufuli Ziko Salama na tayari kwa matumizi, Vijana Njooni Muendelee na Masomo

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jakaya Kikwete amesema hosteli za chuo hicho maarufu hostel za Magufuli ambazo zilibadilishwa matumizi na kuwa karantini kwa watu waliokuwa wakitoka nchi za nje ikiwa ni hatua ya kupambana na corona, ziko salama na tayari kwa matumizi. 

Kikwete ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Mei 28, alipotembelea hosteli hizo kwa ajili ya kukagua mazingira kabla ya wanafunzi kuanza kupokelewa kwa ajili ya kuendelea na masomo yao kuanzia Juni Mosi mwaka huu. 

"Tulitaka waliochukua ile hosteli watangaze rasmi kwamba wameshafanya yale yote waliyoahidi, ya kutayarisha hii hosteli kuwa salama kwa ajili ya kupokea wanafunzi wetu.  Kauli hiyo hatutakiwi kutoa sisi, wala DVC, tunataka watoe wenyewe waliochukuliwa hizo hosteli na waeleze walichokifanya kuhakikisha wanafunzi na jamii yetu kwamba hapa mahali pako salama, kwa hiyo Neema ( kwa niaba ya mganga mkuu wa mkoa Dar) nikushukuru kwa kauli uliyotoa, wamekusikia

"Niliposikia wanawaleta wasafiri kutoka nje na kukaa hapa kwa siku 14, shaka yangu kubwa ilikuwa, itakuwaje kama hao watu watakuwa na maradhi, je, wakiondoka hawataacha mbegu? Na vijana wetu wakija wakaja kupatia maradhi hapa?

"Lakini tukazungumza sana na uongozi wakanihakikisha kwamba serikali imechukua tahadhari zote kuhakikisha panakuwa  sterilized, disinfected kiasi cha kutosha ili wakija vijana pasiwe na shaka yoyote. Waliponieleza hivyo nilipata matumaini. Lakini nikawaeleza kuwa lazima tuhakikishe hilo limefanyika kwa sababu hatutaki hii kambi tukufu sana yenye jina la Rais… iwe ndio kitovu cha ugonjwa.

"Maana watu walikwenda makwao, isije ikatokea watakaporudi wakaugua wakasema si unaona serikali imewaleta na wametuachia mbegu za virusi. Hata tulipopata agizo la vyuo vifunguliwe mazungumzo yangu na DVC yslikues ni  kwamba tumejiandaaje. Akaniambia tumeshajiandaa vya kutosha ndipo siku ya pili yake ikatoka kwamba vyuo vifunguliwe Juni mosi

"Kwa maeleo yake ni kwamba hakuna hata mmoja miongoni mwa 426 waliogusana wale waliokutwa na maambukizi, 418 wametoka, kati ya hao hakuna hata mmoja aliyekutwa na virusi, kwa maana waliokuwepo hapa walikuwa salama ina maana kuwa hapa ni salama, ila makubaliano yetu ni lazima kufanya disinfection na wamefanya mwezi moja uliopita.

"Kwa hiyo tunaichukua kauli yenu kwamba pako salama, niwahakikishie vijana kwamba pako salama njooni, wale tuliowakabidhi wamefanya vile tulivyokubaliana, basi likitokea la kutokea tutawasiliana

"Lakini kwa upande wenu mmefanya tuliyoahidiana, kwa niaba ya uongozi wa chuo niwashukuru. Mmetimiza ahadi yenu, ndio uungwana. Ada ya mja hunena muungwana ni vitendo, mmenena lakini pia mmetenda." Amesema Kikwete


Share:

Taarifa Kwa Umma Kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete-JKCI Kuhusu Kutohusika Kwa Njia Moja au Nyingine na Mashindano ya Mbio za Heart Marathon 2020

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuujulisha Umma kuwa haihusiki kwa njia moja au nyingine na mashindano ya mbio za Heart Marathon 2020 yaliyokuwa yafanyike  tarehe 19 Aprili mwaka huu jijini Dar es Salaam na Zanzibar na kuahirishwa kutokana na kuwepo kwa ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona (COVID – 19).

Mbio hizo za Heart Marathon ambazo zimepangwa kufanyika siku za mbeleni zimeandaliwa  na Asasi ya kiraia ya Tanzania Health Summit na siyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Aidha Taasisi inatoa rai kwa wananchi watakaopenda kushiriki katika mashindano hayo kuwasiliana moja kwa moja na waandaaji  kama matangazo yao yanavyoonesha.

Hata hivyo kama unapenda kuchangia sehemu ya gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo mdogo kiuchumi wanaotibiwa katika Taasisi yetu unakaribishwa. Unaweza kuchangia kiasi chochote cha fedha kupitia  namba ya malipo ya Serikali 994830000022.


Share:

Kutana na Mtabibu wa Nyota za Binadamu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH

Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Adam shariff Mtabibu wa Nyota za Binadamu  Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo fanya mawasiliano kupitia wasaa Husika.

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasiliana nae sasa atatue tatizo lako.
.
Adam shariff Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
 
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu. Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI
.
Nguvu za KIUME, Kesi .... Kwa mawasiliano piga simu namba(+255 )715971688 au (+255 )756914036
.+255 712921834
.

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger