Monday 2 March 2020

Video Mpya : BEXY - BORA IWE

Ninao wimbo mpya wa Msanii Bexy unaitwa Bora Iwe.. 
Tazama video hapa chini

Share:

WAANDISHI WA HABARI WASHAURIWA KUWA WAZALENDO, KUTUMIA VYEMA KALAMU NA MIDOMO YAO KATIKA USTAWI WA TAIFA


Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Arusha, Bw. Charles Yamo, akisoma hotuba ya ufunguzi wa semina kwa waandishi wa habari za uchumi na fedha kwenye ukumbi wa BoT jijini Arusha Machi 2, 2020.
****
WAANDISHI wa habari nchini wameshauriwa kuwa wazalendo kwa taifa kwa kutumia vyema kalamu zao, midomo yao na vyombo vyao vya habari kwa kuhabarisha umma vyema bila kuharibu uelekeo wa ustawi wa taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Arusha wakati akifungua semina kwa wanahabari kuhusiana na habari za Uchumi na Fedha Mkurugenzi wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) tawi la Arusha Charles Yamo amesema kuwa umuhimu wa vyombo vya habari katika ujenzi wa taifa ni mkubwa sana hivyo ni lazima Wanahabari wawe chachu ya maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

"Kupitia mafunzo haya tunaamini umma utaelewa zaidi ni nini benki kuu inafanya na nini wategemee kutoka kwetu" Ameeleza.

Amesema kuwa kupitia mafunzo hayo wanahabari watapata fursa ya kufahamu zaidi kuhusiana na sera za fedha, masoko ya sekta ya fedha, usimamizi wa fedha na huduma za kibenki na kupitia maarifa hayo wananchi watapata fursa ya kupata elimu zaidi kuhusiana na majukumu yanayotekelezwa na benki kuu ya Tanzania.

Aidha Yamo amewashauri waandishi wa habari kujiendeleza kielimu ili kwenda sambamba na maendeleo ya sayansi na teknolojia.

"Dunia imebadilika teknolojia inakua kwa kasi ni vyema wanahabari mkajiendeleza zaidi kielimu ili kuweza kutayarisha na kuandika habari zitakazowafikia wananchi kwa urahisi zaidi" Ameeleza.

Pia amesema kuwa umahiri kwa wanahabari ni jambo lisiloepukika hivyo ni vyema kwa kila mwanahabari kubobea katika sekta fulani kiuandishi na kuimakinikia.

"Ukiwa na sekta ambayo umeibobea utaitendea vyema kazi yako na sio kuandika kila kitu, ukiwa mahiri na mweledi katika sekta ya uchumi au kilimo itakupa nafasi zaidi ya kuitendea kazi vyema" amesema.

Mafunzo hayo kwa waandishi wa habari yatakwenda sambamba na kutembelea miradi mbalimbali ya kiuchumi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano jijini Arusha.

Kwa upande wake Meneja Msaidizi wa Uhusiano na Itifaki, BoT, Bi. Vicky Msina mwanzoni mwa semina hiyo, alieleza kuwa washiriki wa semina hiyo wanatoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vya televisheni, radio, magazeti na mitandao ya kijamii na kwamba semina hiyo itadumu kwa siku tano ambapo wataalamu wa BoT watatoa elimu kuhusu shughuli za BoT.
Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Arusha, Bw. Charles Yamo, akisoma hotuba ya ufunguzi wa semina kwa waandishi wa habari za uchumi na fedha kwenye ukumbi wa BoT jijini Arusha Machi 2, 2020.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Misango, akiendelea kutoa ufafanuzi kuhusu ukuaji wa Uchumi nchini kwenye semina ya Waandishi wa Habari za Uchumi na Fedha inayofanyika jijini Arusha.
Meneja Msaidizi wa Uhusiano na Itifaki BoT, Bi. Vicky Msina (katikati) akitoa maelezo ya awali kuhusiana na semina hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa BoT tawi la Arusha, Bw. Charles Yamo na kulia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Misango.
Meneja Msaidizi wa Uhusiano na Itifaki BoT, Bi. Vicky Msina akitoa maelezo ya awali kuhusiana na semina ya Waandishi wa Habari za Uchumi na Fedha inayofanyika jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Misango, akifafanua moja ya mada iliyohusu mapitio ya maendeleo ya uchumi nchini, kikanda na dunia na matarajio kwa mwaka 2020,Kwenye Semina ya Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali ikiwemo mitandano ya Kijamii iliyohusu Habari za Uchumi na Fedha,inayofanyika jijini Arusha
Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye semina hiyo inayoendelea jijni Arusha
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Misango, akitoa mada kuhusu mapitio ya maendeleo ya uchumi nchini, kikanda na Dunia na matarajio kwa mwaka 2020.
Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Misango kuhusu mapitio ya maendeleo ya uchumi nchini, kikanda na dunia na matarajio kwa mwaka 2020.
Share:

TMA YATOA TAHADHARI YA MVUA KUBWA KUNYESHA LEO HADI JUMATANO TANZANIA ...."MJIANDAE MAJI"

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini(TMA), imetoa tahadhari ya mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha Machi 2 - 3, 2020, katika Mikoa ya Mara, Simiyu, Arusha,Kilimanjaro, Manyara, Singida,Dodoma, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Tanga, Dar es Salaam,Pwani pamoja na Visiwa vya Mafia,Unguja na Pemba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo pia imeeleza kuwa mvua hizo pia zitanyesha Machi 4 kwa baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Njombe, Iringa, Arusha, Kilimanjaro,Manyara, Dodoma, Tanga, Morogoro, Dares Salaam, Pwani pamoja na Visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.

Mvua hizo zinatarajiwa kunyesha kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo Machi 2 hadi Jumatano ya Machi 4, 2020.

TMA pia imeeleza athari ambazo zinaweza kujitokeza kuwa ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri,kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii na kuwataka wananchi kuzingatia na wajiandae.

Share:

TAASISI ZA KIFEDHA NCHINI ZATAKIWA KUACHA URASIMU KATIKA MIKOPO

Na Salvatory Ntandu - Kahama

Serikali imezitaka Taasisi za kifedha nchini kuacha urasimu katika utoaji wa mikopo kwa wawekezaji wa viwanda wa ndani ili kuwasaidia kukuza mitaji yao hali ambayo itachangia kuongeza ajira.

Kauli hiyo imetolewa Machi mosi na Makamu wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Ali Idd wilayani, Kahama mkoani Shinyanga katika ziara yake ya kwanza baada ya kutembelea na kukagua eneo la ujenzi wa viwanda vitatu katika eneo la Chapulwa vinavyojengwa na KOM GROUP OF COMPANIES.

Alisema kuwa baadhi ya taasisi hizo zimekuwa zitoa masharti magumu kwa wawekezaji wa ndani pindi wanapohitaji kukopeshwa fedha kwaajili ya kukuza biashara zao na kusababisha wengi wao kushindwa kuwekeza kwa tija.

“Nizitake taasisi hizi zitambue umuhimu wa wawekezaji wetu wa ndani kama vile kampuni hii ya KOM ambayo inaendelea na uwekezaji katika eneo hilo la Chapulwa,riba zikipungua nina imani watanzania wengi watanufaika kwa kupata mikopo ambayo itasaidia kukuza uwekezaji wao”,alisema Balozi Idd.

Alifafanua kuwa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk John Pombe Magufuli imejikita katika uanzishwaji wa viwanda hivyo ni budi kwa taasisi hizo kuunga mkono juhudi za kuelekea katika uchumi wa kati na kuwawezesha wananchi wengi kupata ajira za kudumu sambamba na kuongeza uchumi wa taifa.

“Mkoa wa shinyanga mmetia fora katika uhamasishaji wawekeza wa ndani katika ujenzi wa viwanda nimekagua eneo hili ambako kunajengwa viwanda zaidi ya vitatu ambapo watanzania zaidi ya 2000 watapata ajira”,alisema Balozi Idd.

Naye mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack alitoa rai kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza katika mkoa wa Shinyanga kutokana na wingi wa fursa mbalimbali zilizopo katika mkoa huo.

“Katika eneo hili la Chapulwa mkoa wa Shinyanga tumetoa viwanja bure kwa wawekezaji huyu wa kampuni ya KOM kama kuwapa motisha ya kuwahamasisha kuwekeza katika mkoa wetu sambamba na kuandaa mazingira rafiki kwao”,alisema Telack.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya KOM GROUP OF COMPANIES,Braison Edward alisema kuwa gharama za uwekezaji wa kiwanda hicho ni zaidi ya dola milioni 10 za Kimarekani na viwanda vitakavyojengwa ni vya maji,soda na kusaga nafaka.

Balozi Seif Alli Idd yupo mkoani Shinyanga katika ziara ya siku tano akiwa ni mlezi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga ,akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM.
Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na kwa kutowapa mikono viongozi kutekeleza agizo la Waziri wa Afya Ummy mwalimu kuhusu Virusi vya Corona.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga  Mabala Mlolwa akiwa amekiti na mgeni wake Balozi Seif Ali Idd katika sofa katika eneo la Bukondamoyo
Mkuu wa mkoa wa shinyanga zainabu telack akiwa ameketi kwenye sofa na Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika eneo la viwanda vidogo la bukondamoyo katika eneo la halmashauri ya mji wa kahama.
Share:

Raia wanne wa kigeni walioingia na mafua Uganda watengwa Kwa Hofu Ya Virusi Vya Corona

Raia wanne wa kigeni waliowasili nchini Uganda na dalili za virusi vya corona wametengwa katika hospitali ya Entebbe, Waziri wa afya amethibitisha.

Bila ya kutaja uraia wao, afisa mahusiano wa waziri wa afya bwana Emmanuel Ainebyoona alisema kuwa raia hao wamechukuliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe.

"Sampuli ya vipimo vyao vimepelekwa katika kituo cha utafiti wa virusi nchini humo (UVRI). Na tutaitaarifu umma " gazeti la Daily Monitor limemnukuu

Wizara ya afya imewataka wananchi kuwa watulivu na kufuata hatua za kujikinga na ugonjwa wa corona kwa sababu hakuna udhibitisho wa kuwa virusi hivyo vimeingia nchini humo.

-BBC


Share:

Korea Kaskazini Yafyatua Makombora Mengine Mawili

Korea Kaskazini  leo imefyatua makombora mengine mawili kuelekea baharini

Vyombo vya habari kutoka Korea Kusini vimeinukuu wizara ya ulinzi ya nchi hiyo ikitangaza kuwa, makombora hayo mawili yamefyatuliwa mapema leo katika mji wa Korea Kaskazini wa Wonsan kuelekea baharini.

Tarehe mosi Januari, Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alitangaza kuwa, miradi ya nyuklia na majaribio ya makombora ya nchi yake yataanza tena endapo mazungumzo ya nchi hiyo na Marekani hayatoanza tena.

Mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini hivi sasa yameingia kwenye mkwamo baada ya kuvunjika mazungumzo kati ya pande hizo mbili yaliyofanyika Hanoi, Vietnam mnamo mwezi Februari mwaka 2019.


Share:

Uturuki yawauwa wanajeshi 19 wa serikali ya Syria

Mashambulizi ya angani ya ndege za Uturuki zisizoruka na rubani yamewauwa wanajeshi 19 wa serikali ya Syria katika mkoa wa kaskazini magharibi wa Idlib, wakati mvutano ukiendelea kati ya Syria na Uturuki. 

Shirika linalofuatilia haki za binaadamu nchini Syria limesema wanajeshi hao waliuawa baada ya msafara wao kushambuliwa katika eneo la Jabal al-Zawiya na kituo cha kijeshi karibu na mji wa Maaret al-Numan. 

Ripoti hiyo imekuja saa chache baada ya Uturuki kuzidungua ndege mbili za kivita za Syria, katika operesheni kali inayofanywa dhidi ya serikali ya Syria mkoani Idlib, ambako wanajeshi waasi wakisaidiwa na Uturuki wanaweka kizingiti kwa serikali ya Damascus kuchukua udhibiti wa nchi nzima. 

Uturuki imethibitisha kuanzisha operesheni kamili dhidi ya wanajeshi wa Syria wanaoungwa mkono na Urusi baada ya wanajeshi 34 wa Uturuki kuuawa wiki iliyopita katika shambulizi la angani lililodaiwa kufanywa na serikali ya Syria.


Share:

Watanzania Watakiwa Kuchangamkia Fursa Kili Marathon.

Na. Aron Msigwa - WMU, Moshi.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla ametoa wito kwa Watanzania hususani vijana wajitokeze kushirikimashindano mbalimbali  yanayofanyika nchini Tanzania yakiwemo ya Kilimanjaro Premium Lager  Marathon ili wanufaike wanufaike kiuchumi.

Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo mjini Moshi wakati  akizungumza na wakazi wa mji wa Moshi na maelfu ya wakimbiaji waliojitokeza kushiriki  Mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon mwaka 2020 katika uwanja wa Michezo wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.

Dkt. Kigwangalla ambaye alikua mgeni rasmi na miongoni mwa washiriki wa mbio hizo kwa upande wa Kilometa 21 amesema ushiriki wa Watanzania katika mbio za KILI Marathon unachangia kuimarisha afya za washiriki na kutoa fursa ya ajira kwa wakimbiaji, kukuza kipato kwa wenyeji kufanya  biashara na kuuza huduma mbalimbali kwa wageni.

Dkt. Kigwangalla amewashukuru waandaji wa mbio hizo ambazo zimejumuisha washiriki zaidi ya elfu kumi na mbili (12,000) kutoka nchi zaidi ya 56.

Amesema ujio wa wageni hao kutoka mataifa mbalimbali ni fursa ya kiuchumi kwa Watanzania pia ni moja ya mkakati wa kukuza na kutangaza vivutio mbalimbali vya Utalii.

" Unapopata wageni kutoka nchi zaidi ya 56 kwa wakati mmoja ni jambo la kujivunia, sio jambo dogo sisi kama wizara tumelichukulia kwa uzito mkubwa na ndio maana niko hapa leo pamoja na watendaji kutoka Taasisi mbalimbali kama vile Bodi ya Utalii , TANAPA, KINAPA , Ngorongoro na wadau wengine wa utalii ili kwa pamoja tutangaze utalii uliopo nchini kwetu" Amesema Dkt. Kigwangalla.

Ameeleza kuwa washiriki wa mbio hizo pamoja na mambo mengine wanapata fursa ya kuzuru vivutio vya utalii ikiwemo kupanda Mlima Kilimanjaro , kutembelea eneo la Ngorongoro, Zanzibar, Mikumi Ruaha, Nyerere na maeneo mengine yenye vivutio vya utalii na kuchangia katika kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa.

" Watalii hawa hufanya matumizi mbalimbali wanapotembelea vivutio vyetu na hii hukuza biashara mbalimbali, ni jambo la kuungwa mkono kwa nguvu zote natoa rai kwa waandaaji tuendelee kushirikiana pamoja na Wizara ya Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo ili tusukume gurudumu hili" Amesisitiza Dkt.Kigwangalla.

Dkt.Kigwangalla ametoa wito kwa watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii.

" Tumeshusha viingilio kwa kiasi kikubwa ili Watanzania wengi zaidi wapate fursa ya kutembelea vivutio hivi na hii ni pamoja na wanafunzi kuanzia shule za msingi hadi vyuo, Tutumie fursa hii vizuri na Wizara yangu itagakikisha vivutio vyote vinakuwa katika hali ya ubora unaotakiwa " Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Aidha, amewataka waandaaji wa mbio mbalimbali zinazovutia watalii wajitokeze na kuishirikisha Wizara ili isaidie kuweka mikakati mizuri ya matumizi ya fursa zilizopo.

Amesema Serikali itaendelea kuunga mkono mashindano hayo na kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara ili mashindano hayo yaendelee kuwa kivutio miongoni mwa washiriki, yakuze utalii na kuwa chanzo kikubwa cha mapato.

Kwa Upande wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa utoaji wa Nishani na  zawadi mbalimbali kwa Washindi wa mbio hizo ametoa wito kwa waandaji wa mbio hizo wawahamasishe vijana wa Kitanzania washiriki mashindano hayo na kushinda Tuzo na zawadi mbalimbali zinazotolewa badala ya kuachia wageni.

Dkt. Mwakyembe ametoa rai hiyo kufuatia idadi kubwa ya washindi wa nafasi za juu katika mashindano hayo kuwa wageni kutoka nchi za jirani za Kenya na Uganda.

Amesema Tanzania ina vijana wazuri wenye uwezo wa kukimbia na kupeperusha bendera ya Tanzania Kimataifa akibainisha kwamba jambo hilo la ushiriki hafifu wa Watanzania katika mashindano ya Marathoni lazima litafutiwe ufumbuzi.

" Haiwezekani, Tanzania tunao vijana wazuri sana na wenye uwezo wa kukimbia kwa spidi kama ya pikipiki, hatuwezi kuendelea kuwaachia wageni ndio wakawa wanashika nafasi za kwanza na kuchukua fedha wakati vijana wa kitanzania miguu mnayo na uwezo wa kukimbia mkachukua fedha hizi upo" Amesisitiza.

Kufuatia hali hiyo ametoa agizo kwa viongozi wa mchezo wa riadha kutoka maeneo mbalimbali nchini kukutana naye mjini Dodoma ili waweze kufanya maamuzi juu ya hiyo hilo.

Aidha amesema kuwa Wizara yake itaendelea kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii ili kuweka miundombinu na mazingira wezeshi ya kuongeza idadi ya washiriki wanaojitokeza katika mashindano hayo ikiwemo ujenzi wa miundombinu na njia maalum zitakazoongeza idadi kubwa ya  wakimbiaji wa Kili Marathon kutoka katika mataifa mbalimbali.

MWISHO


Share:

Taasisi Za Kifedha Nchini zatakiwa Kuacha Urasimu Katika Mikopo

NA SALVATORY NTANDU
Serikali imezitaka Taasisi za kifedha nchini kuacha urasimu katika utoaji wa mikopo kwa wawekezaji wa viwanda wa ndani ili kuwasaidia kukuza mitaji yao hali ambayo itachangia kuongeza ajira.

Kauli hiyo imetolewa Machi mosi na Makamu wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,  Balozi Ali Idd  wilayani, Kahama mkoani Shinyanga katika ziara yake ya kwanza baada ya kutembelea na kukagua eneo la ujenzi wa  viwanda vitatu katika eneo la chapulwa vinavyojengwa na KOM GROUP OF COMPANIES.

Alisema kuwa baadhi ya taasisi hizo zimekuwa zitoa masharti magumu kwa wawekezaji wa ndani pindi wanapohitaji kukopeshwa fedha kwaajili ya kukuza biashara zao na kusababisha wengi wao kushindwa kuwekeza kwa tija.

“Nizitake taasisi hizi zitambue umuhimu wa wawekezaji wetu wa ndani kama vile kampuni hii ya KOM ambayo inaendelea na uwekezaji katika eneo hilo la Chapulwa,riba zikipunguwa naimani watanzania wengi watanufaika kwa kupata mikopo ambayo itasaidia kukuza uwekezaji wao”alisema Balozi Idd.

Alifafanua kuwa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk John Pombe Magufuli imejikita katika uanzishwaji wa viwanda hivyo ni budi kwa taasisi hizo kuunga mkono juhudi za kuelekea katika uchumi wa kati na kuwawezesha  wananchi wengi kupata ajira za kudumu sambamba na kuongeza uchumi wa taifa.

“Mkoa wa shinyanga mmetia fora katika uhamasishaji wawekeza wa ndani katika ujenzi wa viwanda nimekagua eneo hili ambako kunajengwa viwanda zaidi ya vitatu ambapo watanzania zaidi ya 2000 watapata ajira”alisema Balozi Idd.

Nae mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack alitoa rai kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza katika mkoa wa shinyanga kutokana  na wingi wa fursa mbalimbali zilizopo katika mkoa huo.

“katika eneo hili la chapulwa mkoa wa Shinyanga tumetoa viwanja bure kwa wawekezaji huyu wa kampuni ya KOM kama kuwapa motisha ya kuwahamasisha kuwekeza katika mkoa wetu sambamba na kuandaa mazingira rafiki kwao”alisema Telack.

Kwa upande wake meneja wa kampuni ya KOM GROUP OF COMPANIES,Braison Edwad alisema kuwa gharama za uwekezaji wa kiwanda hicho ni zaidi ya dola milioni 10 za kimarekani na viwanda vitakavyojengwa ni vya maji,soda na kusaga nafaka.

Balozi Seif Alli Idd yupo mkoani shinyanga katika ziara ya siku tano akiwa ni mlezi wa chama cha mapinduzi mkoa,akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM.

Mwisho.


Share:

Waziri Mkuu Majaliwa Afungua Kitengo Cha Kuchuja Damu Katika Hospitali Ya Bombo-Tanga

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua mradi wa huduma ya kuchuja damu  katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga ya Bombo na kupunguza gharama ya kuwasafirisha wagonjwa wenye matatizo ya figo kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  kufuata hiduma hiyo.

Pia, Waziri Mkuu amefungua mradi wa ujenzi wa barabara ya Makorora-Msambweni (km nne) iliyojengwa kwa thamani ya sh. bilioni 5.9 ambayo itarahisisha mawasiliano kwa wakazi wa kata za Msambweni, Makorora, Mzingani na watumiaji wengine wa barabara hiyo.

Waziri Mkuu amezindua miradi hiyo kwa nyakati tofauti jana (Jumapili, Machi 1, 2020) wakati akiwa katika siku ya kwanza ya ziara  ya kikazi mkoani Tanga, ambapo alisisitiza azma ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwaletea maendeleo wananchi wote.

Alisema sekta ya afya imepiga hatua kubwa ukilinganisha na miaka minne iliyopita na Serikali inaendelea kuboresha huduma za afya ikiwa ni pamoja na maboresho ya stahili za watumishi. Amewataka watumishi waendelee kuwa watulivu wawe na Imani na Serikali yao.

Alisema ni vema kwa watumishi wa hospitali hiyo kuhakikisha wanafanyakazi kwa uaminifu na uadilifu ili wagonjwa wenye matatizo ya figo pamoja na matatizo mengine ya kiafya wapate huduma bora  bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Pia, Waziri Mkuu aliwataka watumishi hao kuandaa utaratibu wa kutoa elimu kila siku asubuhi juu ya umuhimu wa kujikinga na magonjwa yanayoambukiza na  yasiyoambukiza ambayo ni hatari na ya gharama kubwa.

“Suala la mazoezi ni tiba muhimu na nyie wataalamu ambao mnajua ugonjwa huu tunautibu vipi ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi, hivyo  andaeni nafasi ya dakika tano hadi kumi za kutoa elimu na kuhamasisha watu wajenge tabia ya kufanya mazoezi. Magonjwa mengine yanaweza kutibika kwa kufanya mazoezi na kubadilisha mitindo ya maisha.”

Waziri Mkuu alisema Serikali imeboresha utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi wake zikiwemo za afya, hivyo aliwaagiza viongozi katika ngazi mbalimbali wahakikishe hakuna mwananchi anayekwenda kwenye maeneo ya kutolea huduma na kukosa dawa au vipimo.

Akizungumza kuhusu barabara ya Makorora-Msambweni, Waziri Mkuu alisema mbali na kurahisisha mawasiliano pia itaboresha usalama na mazingira ya wananchi kutokana na uwepo wa taa za barabarani jambo litakaloongeza thamani ya makazi.

Awali, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema huduma za figo nchini zilikuwa zinatolewa katika vituo 19 vya binafsi na hospitali tano za Serikali ambazo ni Hospitali za Kanda za Rufaa Muhimbili, Mbeya, Bugando, KCMC na Benjamin Makapa.

Waziri Ummy alisema hadi 2016 asilimia 90 ya huduma za kusafisha figo zilikuwa zinatolewa na sekta binafsi na asilimia 10 taasisi za umma. “Hali hii inasababisha huduma za usafishaji figo kuwa na gharama kubwa na kukosa uwiano wa huduma hasa kwa wananchi waishio mikoa ya pembezoni.”

Alisema Serikali imepanga kutanua huduma hizo ili ziweze kutolewa katika hospitali zote za rufaa za mikoa, ambapo awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mpango huo imeanza kwa hospitali za rufaa za mikoa ya minane ambazo ni Bombo-Tanga, Meru-Arusha, Mtwara, Iringa, Bukoba-Kagera, Maweni-Kigoma na Sekoutoure-Mwanza.

Waziri Ummy alisema uanzishwaji wa kituo kimoja cha kutolea huduma ya kuchujia damu hadi kuanza kufanya kazi kama kilivyo cha Bombo kinagharimu sh milioni 574,794,177, hivyo kwa vituo hivyo nane ambavyo mwezi huu vinataanza kutoa huduma vitagharimu sh. bilioni 4.5.

Kwa upande wao,wagonjwa wenye matatizo ya figo waliishukuru Serikali kwa kuwasogezea huduma ya kuchuja damu katika hositali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga kwa kuwa awali walilazimika kutumia gharama kubwa kufuata huduma hiyo katika hospitali ya Muhimbili.

Pia, Wagonjwa hao licha ya kuishukuru Serikali kwa kuwasogezea huduma, pia wameiomba iangalie uwezekano wa kupunguza gharama ili watu wengi waweze kumudu matibabu hayo kwani kwa sasa gharama ya session moja ni sh. 250,000.

(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne March 2


















Share:

Sunday 1 March 2020

Mechi Imeisha.....Manchester City watwaa Ubingwa wa Carabao Cup Kwa kuichapa Aston Villa 2-1

Dakika 90 za Mchezo  Kati ya Manchester City  na Aston Villa kwenye Uwanja wa Wembley  zimemalizika ....Manchester City Wamebeba Ubingwa wa Carabao Cup kwa msimu wa tatu mfululizo baada ya kuichapa Aston Villa 2-1

Hata hivyo, Mtanzania Mbwana Samatta amekuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kuifunga goli Manchester City  na amekuwa mchezaji wa tano kutoka Bara la Afrika kufunga kwenye Kombe la Ligi, wengine ni Didier Drogba , Joseph-Désiré Job, Obafemi Martins na Yaya Touré.


Share:

Mbwana Samatta Avunja Rekodi Kwa Kufunga Goli Moja Matata...Mechi ni Mapumzo, Manchester City Inaongoza

Mbwana Samatta amefunga bao lake la kwanza kwenye Uwanja wa Wembley  kunako Dakika ya 41 wakati Aston Villa ikivaana na Manchester City katika fainali ya Kombe la Carabao..

Nahodha huyo  wa Tanzania ameanza katika kikosi cha kwanza cha Aston Villa na kazi yao ni moja tu.... kuhakikisha wanawazuia Manchester City kutetea ubingwa wake wa Kombe la Carabao.

Villa mara ya mwisho kutwaa ubingwa ilikuwa msimu wa 1995/96 .

Mechi ni Mapumziko;  Manchester City inaongoza 2-1 dhidi ya Aston Villa.


Share:

Nafasi za Kazi 21 Benjamin William Mkapa Foundation (BMF)

Overview
The Benjamin William Mkapa Foundation (BMF) is a non- profit Trust, established in 2006 with the vision towards healthy lives and well-being for all, in Tanzania and the rest of Africa. Its strategic focused results areas include to combat HIV and AIDS, TB, Malaria and Reproductive, Maternal New Born, Child and Adolescent Health coupled with Health Systems Strengthening including Human Resource for Health. The Foundation addresses the above health challenges through innovative design and implementation of sustainable programs such as the Mkapa Fellows Program.

Achievement of the BMF’s vision can be achieved through empowered workforce, which is self-motivated, committed to growth and integrity, and seeks excellence in execution. BMF seeks for innovative, self-driven, dynamic and competent qualified candidates to fill various vacancies as described in PDF file:

BMF is an equal opportunity employer and we value diversity.
For more information please Download attached PDF file to get full details of all jobs requirements.

The deadline for application is on Monday, 09th March 2020



Share:

Majeshi Ya Uturuki Yadungua Ndege Mbili za Kivita za Syria

Vikosi vya Uturuki vimedungua ndege mbili za kivita za serikali ya Syria katika mkoa wa kaskazini-maghribi wa Idlib siku ya Jumapili, baada ya Ankara kutangaza operesheni ya kijeshi ndani ya mipaka ya Syria.

Shirika la uangalizi wa haki za binadamu la Syria lenye makao yake nchini Uingereza, lilisema ndege hizo mbili chapa ya Sukhoi zilianguka katika maeneo yanayodhibitiwa na vikosi vya utawala, baada ya kushambuliwa na ndege za Uturuki aina ya F-16.

Shirika la habari la serikali ya Syria SANA, lilisema vikosi vya Uturuki "vimelenga" mbili kati ya ndege zake kaskazini-magharibi mwa Syria. T

angu Desemba, vikosi vya utawala vikiungwa mkono na Urusi vimeongoza operesheni ya kijeshi dhidi ya ngome ya mwisho ya waasi ya Idlib, ambako Uturuki inayaunga mkono baadhi ya makundi ya waasi.

Wizara ya ulinzi ya Uturuki pia iliripoti kudunguliwa kwa ndege hizo siku ya Jumapili, lakini haikuthibitisha juu ya nani alihusika. "Ndege mbili za utawala za SU-24 zilizokuwa zinashambulia ndege zetu zimeangushwa," ilisema.
 
Hatua hiyo ilikuja baada ya Uturuki kutangaza operesheni ya kijeshi kaskazini-magharibi mwa Syria baada ya mashambulizi ya ndege za utawala wa Syria kuuwa wanajeshi  zaidi ya 30 wa Uturuki siku ya Alhamisi.

Mashambulizi ya kisasi ya ndege zisizo na rubani na mizinga yameuwa wanajeshi 74 wa Syria na wapingaji 14 washirika tangu siku ya Ijumaa, limesema shirika la uangalizi wa haki za binadamu. Pia Jumapili jeshi la Syria lilianguisha ndege ya Uturuki isiyo na rubani kaskazini-magharibi mwa Syria.

Shirika la SANA lilisema ndege isiyo n rubani ilidunguliwa karibu na mji wa Saraqeb, na kuchapicha picha za ndege ikiporomoka kutoka angani ikiwaka moto. 

Shirika la haki za binadamu pia lilithibitisha tukio hilo. Jeshi la Syria lilikuwa limeonya kwamba lingedungua ndege yoyote inayokiuka anga yake kaskazini-magharibi mwa Syria.

-DW


Share:

Tanzania Yatajwa kuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki na ya nne Afrika kwa kuweka mazingira wezeshi ya ufanyaji biashara ndogondogo.

Na Mwandishi Wetu
Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki na ya nne Afrika kwa kuweka mazingira wezeshi ya ufanyaji biashara ndogondogo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma, Msemaji mkuu wa Serikali  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa kidunia Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika Nyanja mbalimbali ambapo katika suala hilo anasema kidunia imekuwa ya 21.

“Taasisi za Kimataifa zinatambua juhudi za Serikali yetu katika kuwaletea wananchi maendeleo, Baadhi ya masuala yaliyofanyika  kwa wajasiriamali wadogo ni  kupewa vitambulisho maalum vya kuwatambulisha, tozo mbalimbali zimefutwa ili kuwesesha ukuaji wa  sekta ya biashara hapa nchini”,Alisistiza Dkt. Abbasi

Akifafanua  Dkt. Abbasi amesema kuwa Kituo cha Kimataifa cha Televisheni cha CNBC Africa kimerusha makala maalum inayoonesha mafanikio ya Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo na kuoneshwa na zaidi ya nchi 100 Duniani.

Katika makala hiyo iliyoakisi sekta za utalii, miundombinu, nishati, madini, kilimo na uzalishaji, Dkt. Abbasi amesema kuwa hatua hiyo ni moja ya ishara kuwa Taasisi za Kimataifa zinaendelea kutambua hatua zinazochukiliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Katika hatua nyingine Dkt. Abbasi amesema kuwa Waziri wa  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi aliwasilisha ripoti ya Tanzania katika Baraza la Dunia la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu  na kusisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuheshimu na kulinda haki za binadamu kama ilivyokawaida yake.

“ Haki za Binadamu sio siasa, kama nchi tumeendelea kusisitiza na tutaendelea kuzienzi haki zote za Binadamu kwa maslahi ya watu wote” , alisisitiza Dkt. Abbasi

Tanzania imetajwa kwa nyakati tofauti na Taasisi mbalimbali za Kimataifa kuwa Taifa la kupigiwa mfano kwa namna inavyochukua hatua za kuwaletea wananchi maendeleo, kupiga vita rushwa, kujenga uchumi na ustawi wa wananchi.


Share:

Ujenzi wa SGR Waendelea kwa Kasi, Trilioni 2.957Zatumika hadi Sasa

Na Frank Mvungi- MAELEZO
Serikali imetumia kiasi cha Shilingi Trilioni 2.957 kutekeleza mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) huku kasi ya utekelezaji ikiongezeka.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma , Msemaji Mkuu wa Serikali  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo unaendelea kama ulivyopangwa.

“Mradi  wa SGR kwa kipande cha Dar es Salaam na Morogoro umefikia asilimia asilimia 75 wakati kipande cha Morogoro Makutopora Singida kimefikia takribani asilimia 28”, Alisisitiza Dkt. Abbasi

Akifafanua Dkt. Abbasi amesema kuwa watanzania wataanza kutumia usafiri huo wa kisasa kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro mwaka huu wa 2020 hivyo ile ahadi ya Serikali kwa wananchi itatimia kama ilivyopangwa na kwa wakati.

Kwa upande wa kipande cha Mwanza-Isaka  Dkt.Abbasi amesema kuwa wakati wowote tenda itatangazwa ili kumpata mkandarasi atakayejenga reli hiyo kwa kipande hicho ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa mwezi Desemba 2019 Jijini Mwanza kwa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano.

Akizungumzia baadhi ya wanasiasa wanaobeza juhudi za Serikali kuwaletea wananchi maendeleo kupitia miradi kama SGR Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali haitarudi nyuma katika kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuwa hata wanaobeza watanufaika na miradi hiyo ikiwemo ndege na umeme.

Kwa upande wa utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere(JNHPP) , ujenzi wa eneo la kuchepusha maji ya mto Rufiji ili ujenzi wa ukuta wa bwawa uanze limekamilika kwa asilimia mia moja,  Aidha bwawa hilo linatajwa kuwa kati ya mabwawa makubwa 70 ya kuzalisha umeme wa maji Duniani na kwa Afrika litakuwa la nne kwa ukubwa.

Kwa upande wa kiwango cha fedha kilicholipwa hadi hasa Dkt. Abbasi amesema kuwa Shilingi Trilioni 1.275 kati ya Trilioni 6.5 zimeshalipwa ambapo kazi zote zinaendelea kama ilivyopangwa.

Katika hatua nyingine Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara zote kesho Machi 2, 2020 na watatembelea mradi wa SGR  ili kujionea utekelezaji wake.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi wa Chelezo katika Ziwa Victoria Dkt. Abbasi  amesema kuwa umekamilika kwa asilimia 100 na Shilingi Bilioni 32.8 zimeshalipwa na katikati ya mwezi Machi Itaanza kufanya kazi , huku ukarabati wa MV Victoria umefikia asilimia 89 na Bilioni 14 zimeshalipwa, Wakati MV Butiama ukarabati wake umefikia asilimia 86 na Bilioni 3 zimeshalipwa kati ya Bilioni 4 zilizotengwa kwa ajili ya mradi huo.

“ Ujenzi wa meli mpya  na ya kisasa katika Ziwa Victoria itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1200 na Tani 400 za mizigo umefikia asilimia 52 hadi sasa na unaendelea kutekelezwa kwa kasi kama ilivyopangwa.

Utaratibu wa Msemaji Mkuu wa Serikali kukutana na vyombo vya habari unalenga kuileta Serikali kwa pamoja na wananchi kwa kueleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa maslahi yao katika maeneo mbalimbali hapa nchini


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger