"Wale wanawake watakaojitokeza kugombea nafasi za uongozi wapeni nafasi kwenye vyombo vya habari,angalieni michango yao,itangazeni kwa jamii ili jamii iweze kuwaona. Kuna mifano bora ya wanawake ambao wamefanya vizuri sana katika masuala ya uongozi,wale mkiwa mnawapa nafasi ,basi jamii itaona wanawake wana uwezo mkubwa sana katika kufanya kazi",aliongeza Liundi.
Aliwataka waandishi wa habari kutumia mafunzo wanayopewa kujiimarisha katika kuripoti habari kwa mrengo wa kijinsia na kuhamasisha mila na desturi chanya.
"Tuongeze nguvu katika kuondoa mawazo mgando na mitazamo hasi,tuhakikishe tunapanda mawazo chanya wezeshi ili wanawake waweze kushiriki katika nafasi za uongozi na maamuzi kwa wingi zaidi. Wanawake na wanaume wakishiriki katika ngazi za maamuzi kwa pamoja,kuna tija kwani inasaidia kuchochea maendeleo katika jamii",alisema.
"Wanawake ni zaidi ya asilimia 51 ya wananchi wa nchi za Afrika, kwa hiyo hatuwezi kuiacha hii asilimia 51 isishiriki katika kutoa maamuzi,ni muhimu sana kwa wanawake kushiriki katika michakato ya maendeleo,kushiriki katika nafasi za uongozi ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo",alisisitiza Liundi.
John alisema kupitia warsha hiyo washiriki wataweka mikakati ya namna ya kuongeza kasi ya kuripoti masuala ya kijinsia katika vyombo vya habari hasa kusambaza ilani ya uchaguzi ya wanawake na kuhamasisha mila nzuri zinazohamasisha ushiriki wa wanawake na vijana katika uongozi.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog