Saturday 25 January 2020

Nafasi Mpya 650 za Kazi TANAPA...Mwisho wa Kutuma Maombi ni Tarehe 31 Mwezi huu

Nafasi Mpya  650 za Kazi TANAPA...Mwisho wa Kutuma Maombi ni Tarehe 31 Mwezi huu
__________________________

1. Conservation Assistant II- Wildlife Management-tourism 

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Holder of Ordinary Diploma either in Wildlife Management, Conservation Science, Wildlife Tourism or equivalent qualifications from a recognized institution. 
 
_______________________________

2.Conservation Officer II- Geographical Information Systems 

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Bachelor of Science Degree in Geo–informatics or Geomatics majoring in GIS or equivalent qualification from a recognised institution. 

_______________________________

3. Conservation Officer II- Information Communication Technology 

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Bachelor Degree either in Computer Science, Information Technology, Computer Engineering or equivalent qualifications from a recognized institution.

_______________________________

4. Conservation Ranger III- Wildlife Management-driving - 15 Post 

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with Certificate of Vehicle Driving from a recognized institution and valid Driving License Class E, D and C. A holder of Basic or Technician Certificate in Wildlife related fields or One-year National Service Certificate will be an added advantage.

_______________________________

5. Conservation Assistant II – Clinical Service 

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Diploma in Clinical Medicine or equivalent qualification from a recognized institution and must be a holder of valid licence of registration by the Medical Council of Tanganyika (MCT).

_______________________________

6. Conservation Assistant II- Animal Health 

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Ordinary Diploma in Animal Health and Production or equivalent qualification from a recognized Institution.

_______________________________

7. Conservation Ranger III-Wildlife Management- Law Enforcement  – 589 Post  

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with Basic or Technician Certificate in Wildlife Management or One-year National Service Certificate.

_______________________________

8. Conservation Ranger III- Plant Operation  – 2 Post  

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with Class “F” Plant Operators Licence.

_______________________________

9. Conservation Assistant II-Wildlife Management-Ecology- 4 Post  

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Diploma either in Wildlife Management, Conservation Science or equivalent qualification from a recognized institution.

_______________________________

10. Conservation Ranger III- Boat Operator

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with Basic Certificate in Marine Operations. A holder of Basic or Technician Certificate in Wildlife Management or One-year National Service Certificate will be an added advantage.

_______________________________

11.Conservation Ranger III- Nursing  – 4 Post  

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Certificate in Nursing. Must be licensed and Enrolled Nurse (EN) by the Tanzania Nurses and Midwives Council (TNMC).


_______________________________

12. Conservation Ranger III- Artisan - 6 Post  

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with Trade Test Grade III or Relevant CBET Level in Motor Vehicles Mechanics or Auto mobile or any other relevant fields from a recognized training Institution.


_______________________________

13. Conservation Officer II-Wildlife Management - 32 Post 

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Bachelor Degree in either of the following fields; Wildlife Management, Conservation Science, Wildlife Ecology or equivalent qualification from a recognized institution.

_______________________________

14. Conservation Officer II-veterinary  – 2 Post 

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Bachelor of Science Degree in Veterinary Medicine or equivalent qualification from a recognized institution and must be registered by the Veterinary Council of Tanzania.

_______________________________

15. Conservation Officer II- Civil Engineering

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Bachelor Degree in Civil Engineering from a recognized Institution and must be registered by the Engineers Registration Board (ERB) as a “Graduate Engineer.”

_______________________________





Share:

MEMBERSHIP OFFICER III – 7 POST | Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)

POST DETAILS POST MEMBERSHIP OFFICER III – 7 POST POST CATEGORY(S) BANKING, ECONOMICS AND FINANCIAL SERVICES HR & ADMINISTRATION STATISTICS AND MATHEMATICS TAXATION AND SOCIAL PROTECTION EMPLOYER Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) APPLICATION TIMELINE: 2020-01-22 2020-02-05 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.Assist with Correspondences with employees and employers   on matters concerning enrolment, registration and… Read More »

The post MEMBERSHIP OFFICER III – 7 POST | Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Mamia ya Wananchi wa IRAQ Waandamana Kulitaka Jeshi la Marekani Liondoke Nchini Mwao

Mamia ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad, wakidai vikosi vya Marekani viondoke Iraq.

Kiongozi mwenye ushawishi wa dhehebu la Shia Iraqi, Moqtada al-Sadr awali alitoa wito kwa mamilioni ya raia kushiriki maandamano ya Ijumaa, karibu na ubalozi wa Marekani nchini Iraq.

Vikosi vinavyoungwa mkono na Iran ni miongoni mwa wanaondamana.

Hatua ya Marekani ya kumuua kamanda wa kijeshi wa Iran, Jenerali Qasem Soleimani, Januari 3 katika uwanja wa Baghdad uliongeza uhasama

Pia aliyeshambuliwa kwa ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani ni Abu Mahdi al-Muhandis, mmoja wa makamanda wa Iraq ambaye kundi lake la Kataib Hezbollah linaloungwa mkono na Iran pia aliuawa katika shambulio hilo.

Iran ilijibu shambulizi la mauaji ya Jenerali Soleimani kwa kutekeleza shambulizi la kombora dhidi ya kambi mbili za kijeshi za Marekani nchini Iraq.


Share:

Akina Mbowe na Vigogo Wengine CHADEMA Wafunga Ushahidi, Hakimu Amuonya Halima Madee na Ester Bulaya

Shahidi namba 13 katika kesi ya jinai inayowakabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe & wenzake ambaye ni mwanafunzi wa DIT, Lumola Kahumbi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa polisi walichukua fedha zake na kumlazimisha kuimba wimbo wenye maneno Dola si lelemama.

Katika kesi hiyo mawakili wa upande wa utetezi Peter Kibatala, Profesa Abdallah Safari na upande wa mashtaka wanaongozwa na wakili wa serikali mkuu, Faraja Nchimbi.

Akiongozwa na Kibatala, shahidi huyo amesema katika kituo cha daladala cha Kinondoni Studio wakati akielekea kwa shangazi yake, polisi waliwakamata watu kadhaa na kuwapeleka kituo cha polisi cha Oysterbay.

Amesema akiwa kituoni hapo, waliulizwa kama wanataka kwenda msalani na wakati anakwenda polisi wawili walimsindikiza na mmoja alimtaka ajiongeze.

Amebainisha kuwa askari mmoja alimsachi mfukoni na kuchukua Sh12,700 huku akimtaka aondoke bila kugeuka nyuma. Amesema alibaki na Sh200 mfukoni na alilazimika kutembea kwa miguu kutoka kituoni hapo hadi zilipo hosteli za chuo hicho.


Baada ya Maelezo ya shahidi huyo, upande wa utetezi katika kesi hiyo ulisema umefunga ushahidi baada ya kuwaleta mahakamani mashahidi 15 badala ya 200 walioahidi.

Sasa kinachosubiriwa ni majumuisho ya kesi hiyo yatakayowasilishwa na upande wa utetezi na ule wa mashtaka Februari 24, 2020 siku ambayo itapangwa tarehe ya hukumu ya kesi hiyo.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba baada ya kusikiliza maelezo hayo aliwaonya washtakiwa, Halima Mdee (Kawe) na Ester Bulaya (Bunda)  kwa kukiuka masharti ya dhamana yao baada ya kutoka nje ya Tanzania bila kibali cha mahakama.

Hakimu huyo ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 24, 2020 siku ambayo pande zote mbili zitawasilisha majumuisho yao kabla kupangwa tarehe ya hukumu.


Share:

Market and Gender Value Chain Assessment Job Vacancy at VSO Dar Es SalaamTanzania

Market and Gender Value Chain Assessment Location: Dar Es Salaam, Tanzania Salary: Competitive Contract type: Consultant Agreement Contract length: 30 Days Full Time: 35 hours per week Application Closing Date: 5 Feb 2020 Interview date: TBBC Start date: Feb 2020 VSO is the world’s leading international development organisation that works through volunteers to fight poverty. Working in 24… Read More »

The post Market and Gender Value Chain Assessment Job Vacancy at VSO Dar Es SalaamTanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Naibu Waziri Ulega Asisitiza Utengenezaji Zaidi Wa Bidhaa Za Ngozi Hapa Nchini

Na. Edward Kondela
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema wizara yake itahakikisha matamanio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ya nchi kuuza ngozi na bidhaa zake kwenda nchi za nje yanafikiwa.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati alipotembelea Kiwanda cha kuchakata ngozi cha Ace Leather kilichopo katika Manispaa ya Morogoro na kujionea maboresho makubwa ya kiwanda hicho kwa kufungwa mashine za kisasa, Mhe. Ulega amesema wizara itahakikisha pia uwezekano wa kupunguza gharama kununua bidhaa za ngozi kutoka nchi za nje kuja hapa nchini zinapunguzwa.

“Matamanio ya serikali ya Rais Magufuli kila mara amekuwa akizungumzia kuhusu zao la ngozi, nchi yetu ina mifugo mingi sana na kila mara matamanio yake kuona Tanzania haitumii tena gharama kubwa kununua bidhaa za ngozi kutoka katika mataifa ya nje bali sisi ndiyo tuwauzie ngozi na bidhaa zake.” Amesema Mhe. Ulega

Aidha Mhe. Ulega amesema ameridhishwa na mitambo ya kisasa inayofungwa katika Kiwanda cha Ace Leather ambacho kinatarajiwa kufunguliwa tena hivi karibuni baada ya kusitisha shughuli zake ili kupisha maboresho ya kiwanda hicho kwa kufungwa mitambo hiyo ya kisasa.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa makampuni ya Taifa Group of Companies inayomiliki kiwanda hicho Bw. Abdulkarim Shah amesema mara baada ya kiwanda hicho kukamilika maboresho yake kitakuwa ni moja ya viwanda vikubwa katika ukanda wa kusini mwa janga la sahara.

Bw. Shah amesema mara baada ya kiwanda hicho kukamilika kinatarajiwa kuajiri takriban wafanyakazi 250 hadi 300 na nia ya kiwanda hicho katika siku zijazo ni kuanza kutengeneza bidhaa za ngozi.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amekagua pia ujenzi wa kiwanda cha kuchakata nyama cha Nguru Hills kilichopo katika Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro ambapo amesema ameridhishwa na ujenzi wa kiwanda hicho.

Kufuatia ujenzi wa viwanda vya kuchakata nyama vinavyojengwa maeneo mbalimbali hapa nchini, Naibu Waziri Ulega amehamasisha wananchi kufanya biashara ya kunenepesha mifugo kwa kuwa viwanda hivyo mara vitakapokamilika vitahitaji mifugo mingi kwa ajili ya uchakataji.


Share:

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI YA MBUNGE RWEIKIZA MADAI YA SH BIL. 1 NA MIL 216 KUDHALILISHWA NA KIONGOZI WA CCM


Mdaiwa Mjumbe wa halmashauri ya Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Mkoa wa Kagera Novatus Nkwama (mwenye suti katikati) akiwa nje ya jengo la mahakama baada ya hukumu kutolewa

Na Ashura Jumapili - Malunde 1 blog Bukoba
Mahakama  Kuu kanda ya Bukoba Mkoani Kagera imetupilia mbali kesi ya madai namba 12 ya mwaka 2016 ya fidia ya shilingi bilioni 1 na milioni 216 iliyofunguliwa na Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Jasson Rweikiza dhidi ya Mjumbe wa halmashauri ya Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Mkoa wa Kagera Novatus Nkwama kuwa alimdhalilisha.

Akisoma hukumu mahakamani hapo jana Jaji wa mahakama hiyo Dk. Ntemi Kilekamajinga ,alidai kuwa baada ya kuzingatia ushahidi wa pande zote mbili kwanza msingi wa kisheria ni wajibu mdai kuthibitisha madai yake mahakamani.

Jaji Dk. Kilekamajinga alisema katika kesi hiyo aliangalia hoja nne za kesi hiyo ambavyo ni:

1.Je mdaiwa alimdhalilisha mdai?.

2.Maneno yaliyosemwa yalikuwa na udhalilishaji?.

3.Je maneno hayo yalisababisha madhara yoyote ya udhalilishaji/.

4.Maneno ya kushusha hadhi kwa jamii yajulikane na mtu Zaidi ya mmoja.

“Nimechambua ushahidi uliotolewa na mdai yeye hakuwahi kuyasikia maneno ingawa alisikia kupitia kwa watu wakati huo huo anasema alisikia kipindi kikirudiwa katika radio ,anasema kama yeye hakusikia kupitia masikio yake ushahidi wake unaleta ukakasi”,alisema Jaji Dk.Kilekamajinga.

Alisema kifungu cha 62 kifungu kidogo cha (1)cha sheria za ushahidi alitakiwa kuijumuisha Radio Karagwe kwenye ushahidi mahakamani hapo.

Aliieleza mahakama kwamba mdai hakumpeleka mahakamani mtangazaji wa radio hiyo ,wala uthibitisho wowote toka radio Karagwe kwamba ilirusha matangazo yaliyomdhalilisha.

Alisema kuhusu madai kuwa Rweikiza alitukanwa kwenye nyumba ya Nazir Karamagi wakati wa dua mtu anaalikwa kusalimia halafu anaanza kuropoka na kuanza kutukana hilo jambo pia linaleta ukakasi.

Alisema shahidi mwingine wa mdai aliieleza mahakama kuwa akiwa njiani kuelekea bukoba mjini alipita Itawa akasikia mdaiwa anamtukana mdai ,sijui kilichomsimamisha kwa kweli sasa nimejiuliza alitumia usafiri gani kwanza hakuwa pale na ajenda ilikuwa moja ya kujadili wizi katika Kitongoji pia ushahidi wale ni wa ukakasi.

Alisema mashahidi walioileza mahakama kuwa waliacha kazi kwa mdai baada ya kusikia maneno ya udhalilshaji walishindwa kuithibitishia mahakama kama kweli waliacha kazi hawakuleta barua.

Alisema mdai alishindwa kuithibitishia mahakama madai yake ya watoto 50 wa kiislamu waliokuwa wanasoma kwenye shule yake ya ( Rweikiza primary school )walihama baada ya kusikia maneno kuwa anawabagua waislam na kumsababishia hasara kwa sababu hakuleta idadi ya wanafunzi waliokuwepo shuleni kabla ya maneno na waliohama baada ya maneno.

Alisema cha msingi ni uthibitisho wa jambo linalosemwa kwa msingi wa kisheria hivyo kesi hii imejaa msuguano wa kisiasa Zaidi mdai na mdaiwa wanaongalia kugombea mwaka 2020.

Alidai kuwa kwa kutengeneza kesi sababu ya kumuumiza mwingine mahakama haiwezi kuliacha jambo hilo,mahakama imeshindwa kujiridhisha kama kweli maneno hayo yalitolewa na mdaiwa na kama yalitolewa yanaweza kuwa yalikuzwa Zaidi kwa sababu mdai hakusikiliza kwa masikio yake mwenyewe.

Alisema mahakama imeona madai hayana msingi wowote hivyo pande zote mbili ziweze kubeba gharama zake za kesi.

Awali kabla ya kutoa hukumu hiyo jaji ,huyo alisema kesi hiyo ilishasuluhishwa na chama cha mapinduzi ,viongozi wa serikali na mahakama pia ilisuluhisha ikashindikana ndio ikafunguliwa kesi.

Kesi hiyo ilifunguliwa na mbunge wa jimbo la Bukoba Vijijini Jasson Rweikiza ,akidai fidia ya shilingi bilioni 1 na milioni 216 akidai alidhalilishwa na Novatus Nkwama aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Wilaya Bukoba Vijijini.

Rweikiza ,alisema alitukanwa kuwa yeye ni mwizi alimuibia mdaiwa gari lake,yeye ni mbaguzi anawabagua waislamU na aliiba kura wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015ndiyo akashinda kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Upande wa mdai ulikuwa na mashahidi 7 na mdaiwa mashahidi 4.

Kwa upande wa mawakili wa upande wa mdaiwa ambao ni Dastan Mujaki na Jovin Rutainulwa walisema wamepokea hukumu kama ilivyotolewa kwa sababu imezingatia haki.

Wakili Mujaki,alisema mahakama hiyo imezingatia misingi ya kisheria kwa kuchambua ushahidi uliotolewa na pande zote mbili na kubaini kuwa kesi hiyo ilitengenezwa.

Alisema liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia za kutengeneza kesi na kuwashtaki watu.

Wakili wa upande wa mdai Nyikiza Seth,alitoweka mahakamani hapo bila kuongea chochote hivyo haijajulikana kama wanampango wa kukata rufaa.
Share:

Marekani Yasema Wanajeshi wake 34 Walijeruhiwa na Wanapatiwa Matibabu baada ya Shambulizi la Makombora la Iran

Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imesema makumi ya Wanajeshi wa nchi hiyo walijeruhiwa na kupatwa na matatizo ya kisaikolojia kufuatia shambulizi la makombora la Iran dhidi ya kambi mbili za kijeshi za nchi hiyo huko Iraq mapema mwezi huu, licha ya utawala wa Washington hapo awali kudai kuwa hakuna askari wake hata mmoja aliyeuawa au kujeruhiwa katika shambulizi hilo

Katika kikao na waandishi wa habari mjini Washington jana Ijumaa, Jonathan Hoffman, msemaji wa Pentagon alisema, "askari 34 hivi sasa wanapatiwa matibabu kutokana na kukabiliwa na matatizo ya kisaikolojia, msongo wa mawazo na madhara mengine ya ubongo kufuatia shambulizi la Iran la Januari 8. Wanane waliopelekwa Ujerumani wameletwa katika Hopitali ya Kijeshi ya Walter Reed (karibu na Washington) na wengine tisa wamebaki huko Ujerumani."

Maafisa wa Marekani wanaendelea kukiri hatua kwa hatua juu ya kujeruhiwa wanajeshi wa nchi hiyo na makombora ya Iran, licha ya hapo awali kukataa 

Awali Kamandi ya Jeshi la Marekani Asia Magharibi (CENTCOM) ilidai kuwa  askari 11 wa nchi hiyo waliojeruhiwa Iraq katika makombora ya Iran wanatibiwa mjini Landstuhl nchini Ujerumani na katika kambi ya Arifjan nchini Kuwait.

Masaa machache baada ya Iran kuvurumisha makombora na kupiga kambi mbili za Marekani nchini Iraq, Rais Donald Trump alijitokeza mbele ya vyombo vya habari na kudai kuwa, "ni furaha kuwatangazia Wamarekani kuwa hakuna askari wetu hata mmoja aliyeuawa au kujeruhiwa katika shambulizi la makombora la Iran nchini Iraq."


Share:

World Food Programme (WFP) PD Summer Paid Internship Programme 2020 | Dar es Salaam, Tanzania

PD Summer Internship Programme 2020 – Innovation at WFP – World Food Programme, Dar es Salaam, Tanzania World Food Programme (WFP) PD Summer Paid Internship Programme 2020 | Dar es Salaam, Tanzania Programme Unit, Dar es Salaam, Tanzania The World Food Programme (WFP) is the leading humanitarian organization saving lives and changing lives, delivering food assistance in emergencies… Read More »

The post World Food Programme (WFP) PD Summer Paid Internship Programme 2020 | Dar es Salaam, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Waziri Kairuki: “Kila Mtanzania Anaweza Kuwekeza, Tumieni Fursa Zilizopo”

MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe. Angellah Kairuki amewaasa wananchi kuthubutu uwekezaji katika maeneo yenye tija kwa kuzitumia fursa za uwekezaji zilizopo ili kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo yao na nchi kwa ujumla.

Ametoa kauli hiyo tarehe 23 Januari, 2020 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika kiwanda cha kuchakata maziwa ya mtindi cha Mather Dairies kilichopo Kijiji cha Ikwiriri Wilaya ya Rufiji katika Mkoa wa Pwani alipotembelea kiwandani hapo ikiwa ni eneo la mwisho kutembelea katika ziara yake ya siku 6 Mkoa wa Pwani.

Akiwa katika kiwanda hicho kilichowekeza mtaji wa zaidi ya milioni 300 chenye uwezo wa kuchakata zaidi ya lita 2000 kwa siku ambazo hutengeneza maziwa ya mtindi aina ya Yogurt Full Manyonyo, waziri alitoa hamasa hiyo kwa Watanzania kuzichangamkia fursa na kuwatoa shaka kuwa hakuna Mwananchi asiyeweza kuwekeza kikubwa ni kuwa na nia na uthubutu.

“Ni ukweli kuwa, kila uwekezaji Mtanzania anaweza kuufanya muhimu kuwa na ujuzi, teknolojia pamoja na mtaji pasipo kutia shaka na kujiamini,”alifafanua Waziri Kairuki

Aliongezea kuwa, ikiwa uwezo wa kuwekeza ni mdogo kwa kuzingatia ukosefu wa ujuzi wananchi wanapaswa kutumia fursa za mafunzo ya ukuzaji ujuzi unaotolewa katika vyuo mbalimbali na kutumia watu wenye uzoefu inapofaa kulingana na aina ya uwekezaji unaotaka kuufanya.

Aliwaasa watanzania kuacha tabia ya kukatishana tamaa na kuona namna ya kushikamana kuweza kuwekeza katika sekta mbalimbali.

“Kumekuwa na tabia ya kukatishana tamaa pindi mtu anapothubutu kuona fursa na kuichangamkia, ni rai yangu kwa wananchi kuona watanzania tunawekeza kufanya mambo makubwa katika maeneo yote yenye fursa, na kuzitumia vyema mamlaka zilizopo kwa kupata msaada ya ushauri elekezi na miongozo ya namna bora ya kuwekeza,”alifafanua

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Mzee Abdallah Nyarando alieleza namna alivyoanza uwekezaji wake mwaka 2010 kwa mtaji wa shilingi milioni 20 na hadi kukamilika kwa kiwanda hicho ametumia jumla ya shilingi Milioni 300, na kuweza lengo ni kuongeza thamani ya maziwa, kuzalisha ajira na kujipatia kipato.

 “Kiwanda hiki kimeweza kusaidia zaidi ya vijana 12 ambao wamekuwa wa msaada katika kuzalisha na kuuza maziwa maeneo mablimbali nchini ikiwemo; Masasi, Kibiti, Rufiji, Mtwara na Dar es Salaam,”alisema Mzee Nyarando.

Alitoa wito kwa wananchi kuondokana na hofu za kuwekeza katika maeneo mbalimbali na kueleza zipo faidi za kuwekeza katika nchi yao na kujipatia kipato ili kujikwamua kiuchumi.

Akiwasilisha taarifa yake kwa Waziri Kairuki Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mhe. Juma Njwayo alieleza kuwa Tanzania ina fursa nyingi za kusaidia kundi kubwa la vijana katika kujikwamua kiuchumi kwa kuangalia maeneo muhimu ya uwekezaji katika Nyanja mbalimbali.

Aliongezea kuwa, wananchi hawana budi kujiajiri kwa kutumia nguvu kazi walizonazo na kuzichangamkia fursa za Wilaya yake ambazo alizibaini ni pamoja na shughuli za kilimo, ufugaji, uvuvi na biashara na kuwataka kuzitumia kwa kuzingatia uwepo wa miundombinu muhimu ya kuvutia uwekezaji.

“Wilaya yetu ina vivutio vingi ikiwemo ardhi inayokubali mazao mbalimbali kama mahindi, mpunga, korosho, mazao jamii ya mikunde na mbogamboga  na matunda aina ya matikiti hivyo zitumieni kwa tija na kuhakikisha tunaondokana na ukosefu wa ajira,”alieleza Juma

Alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa wawekezaji kuona maeneo yenye rutuba na kuwekeza katika mazao hayo na kubainisha fursa zilizopo katika ufugaji kwa kuzingatia uwepo wa mabwawa ya asili maji katika wilaya hiyo.


Share:

Waziri wa Kilimo: Bodi Za Mazao Ya Kilimo Wekezeni Katika Utafiti

Na Revocatus Kassimba, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ameagiza wakurugenzi wakuu wa bodi za mazao chini ya wizara ya kilimo kutenga fedha kwa ajili ya kufanya utafiti ili kuongeza tija ya uzalishaji.

Waziri Hasunga ametoa maelekezo hayo tarehe 24 Januari 2020 jijini Dodoma ikiwa ni siku ya pili ya kikao kazi cha Menejimenti ya Wizara, bodi za mazao na taasisi kinacho tathamini utendaji kazi wa nusu mwaka kufikia Disemba 2019.

“Bila kuwekeza fedha za kutosha kwenye utafiti kilimo kitaendelea kukua kwa kasi ndogo, hivyo nawaagiza watendaji wakuu wa bodi  kuweka bajeti ya utafiti mwaka 2020” alisema Waziri wa Kilimo

Katika kikao hicho wajumbe walionesha kutoridhishwa na mwenendo wa hali ya uzalishaji kwenye mazao ya kimkakati ya biashara kama tumbaku, mkonge,kahawa, pareto na chai.

Akitoa taarifa ya hali utendaji kazi  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Stanley Mnozya alieleza katika mwaka 2019/20  jumla ya tani 70,087 zilinunuliwa zenye thamani ya shilingi Bilioni 230.3

Mnozya aliongeza kusema licha ya zao la tumbaku kuwa la pili kwa kuingiza mapato zaidi nchini linakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa uhakika wa soko na uwezo kidogo wa wakulima kuzalisha kutokana na mfumo wa kilimo mkataba kutoeleweka vizuri.

“Bodi  inaendelea na majaribio ya aina mpya nne za mbegu ya tumbaku ya mvuke toka China ili kuongeza tija kwa mkulima “  alisema Mkurugenzi Mkuu huyo.

Kwa upande wa Bodi ya Kahawa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo  Prof Jamal Adam imeonyesha uzalishaji wa kahawa kufikia Disemba 2019 ulifikia tani 55,979 kati ya lengo la tani 50,000.

Prof Jamal ametaja aina za kahawa zilizouzwa kuwa ni Robusta tani 22,320 Arabika laini (Mild Arabica) 32,057 na  Arabika ngumu (Hard Arabica) tani 1,602 na kuingiza mapato  yenye thamani ya Dola za kimarekani 87,527,779 mwaka 2019.

Alitaja sababu ya kufikia mafanikio haya kuwa ni bei nzuri katika soko la dunia  na kuongezeka kuwa ubora wa kahawa ya Tanzania iliyokusanywa toka vyama vya ushirika.

Prof Jamal alitaja changamoto inayoikabili bodi ya kahawa  ni  uzalishaji mdogo wa  miche bora ya kahawa nchini, ambapo mwaka 2019 walizalisha miche milioni 3.6 kati ya lengo la kuzalisha miche milioni 8.

“Tutaendelea kushirikiana watafiti hususani TARI kuwekeza katika utafiti wa miche ili kufikia lengo la  Wizara  kuongeza wigo wa wakulima kupanda kahawa bora ” alisema Prof Jamal

Wakati huo huo Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ameagiza watafiti wa madawa na viuatilifi nchini kutumia zao la pareto kuzalisha viuatilifu bora kwa matumizi ya wakulima.

Hasunga alisema hayo kufuatia taarifa iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pareto Lucas Ayo kusema Tanzania inashika nafasi ya kwanza Afrika na ya pili duniani kwa uzalishaji wa pareto.

‘’Ni wakati sasa wataalamu kutumia pareto kuzalisha madawa na viutilifu bora kwenye viwanda vya ndani ili kukidhi soko la wakulima na kuepusha uwepo wa viuatiflifu visivyo na ubora”alisisitiza Hasunga

Taarifa hiyo ya Bodi ya Pareto ilionesha kuwa hadi kufikia Desemba 2019 tani 1,627 kati ya lengo la tani 2,600 za pareto zilizalishwa nchini na kuliingiza taifa mapato ya shilingi Bilioni 4.28 kufikia Disemba 2019.

Akitoa mchango kuhusu umuhimu wa utafiti, Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) Dkt Geofrey Mkamilo alisema “ tupo tayari kushirikiana na bodi zote za mazao kufantya tafiti zitakazokuja na suluhisho la tija ya mazao kuongezeka” hivyo akashauri bodi za mazao kujipanga kifedha .

Takwimu za uzalishaji mazao nchini zinaonesha kupungua kwa uzalishaji na ubora kwenye mazao ya biashara nchini hali inayopelekea nchi kukosa mapato ya kutosha, hivyo kuhitaji utafiti.

Waziri wa Kilimo anaendelea na vikao vya Menejimenti kupitia taarifa za utendaji kazi wa Bodi za Mazao na Taasisi zote zilizo chini ya Wizara yake na kuweka malengo na mikakati ya kuimarisha utendaji kazi kwa mwaka 2020/2021.


Share:

Senior Specialist, Learning & Talent Development Job at NMB Tanzania

Senior Specialist, Learning & Talent Development Reporting Line: Head, HR Center of Expertise  Job Purpose Partner with HRBPs to support the analysis, scoping of development needs, identify solutions, monitor and evaluate different learning solutions put in place. Main Responsibilities Prepare consolidated HQ/Zonal training plans, training needs assessment and training budgets. Support stakeholders by providing various training programs options… Read More »

The post Senior Specialist, Learning & Talent Development Job at NMB Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Finance Officer Job vacancy at Seedstars Dar es Salaam, Tanzania

Finance Officer Job vacancy at Seedstars Dar es Salaam, Tanzania Are you looking to join a fast-growing international and impact-driven startup, work in a flexible environment, and be surrounded by a young and diverse team? Who We Are Seedstars is a global organization with headquarters in Switzerland and a presence in 70+ emerging markets. We are on a… Read More »

The post Finance Officer Job vacancy at Seedstars Dar es Salaam, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Senior Supply Chain Officer Job at International Rescue Committee Tanzania Dar es Salaam

Senior Supply Chain Officer Job at International Rescue Committee Tanzania Dar es Salaam Job Summary Job Description The International Rescue Committee (IRC) is an International Non-Governmental Organization working in 40 countries, responding to the world’s worst humanitarian crises and helps people to survive and rebuild their lives. With funding from donor governments, institutions, companies and individual supporters we… Read More »

The post Senior Supply Chain Officer Job at International Rescue Committee Tanzania Dar es Salaam appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi January 25













Share:

Admin Officer Job Vacancy at Seedstars Dar es Salaam, Tanzania

Admin Officer Job Vacancy at Seedstars Dar es Salaam, Tanzania Are you looking to join a fast-growing international and impact-driven startup, work in a flexible environment, and be surrounded by a young and diverse team? Who We Are Seedstars is a global organization with headquarters in Switzerland and a presence in 70+ emerging markets. We are on a… Read More »

The post Admin Officer Job Vacancy at Seedstars Dar es Salaam, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Tanzania Program Associate at One Acre Fund Morogoro

Tanzania Program Associate We are seeking an exceptional candidate with 5+ years of consulting, project management or entrepreneurial experience and a demonstrated passion for poverty alleviation.   ABOUT ONE ACRE FUND Founded in 2006, One Acre Fund supplies smallholder farmers with the agricultural services they need to make their farms vastly more productive. We provide quality farm supplies… Read More »

The post Tanzania Program Associate at One Acre Fund Morogoro appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger