“Mdogo wangu Seth alikuwa anasumbuliwa na uvimbe kwenye uti wa mgongo akafanyiwa upasuaji na tukawa tunamuuguza nyumbani kwa Mama hapa Kimara Temboni, Jana jioni akalalamika maumivu yanazidi tukampeleka Muhimbili akapata afadhali tukarudi nae nyumbani
“Tuliporudi nyumbani kutokea Muhimbili alikuwa yuko vizuri tu, akaomba alale kidogo kisha tumuamshe aangalie TV kuna kipindi anakipenda, akiwa kitandani akafariki, tulikuwa na Daktari nyumbani anasema Seth alipata shida ya kupumua, pumzi zilimuishia
“Mwili wa Seth kwa sasa umehifadhiwa Muhimbili na shughuli zote za Mazishi zinafanyika hapa Kimara Temboni DSM, nyumbani kwa Mama Kanumba” - Amesema Abela (Dada wa Maremu)