Tuesday 3 December 2019

Picha : KIVULINI YAENDESHA KIKAO CHA KUJADILI MATOKEO YA UTAFITI KUHUSU UPATIKANAJI WA HAKI KWA WAHANGA WA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO SHINYANGA

Imeelezwa kuwa kuahirishwa kwa kesi za ukatili wa kijinsia hususani mimba za utotoni mara kwa mara mahakamani na idadi ndogo ya kesi zilizofika mahakamani na kufanikiwa imewafanya wananchi waone hakuna haja ya kupeleka kesi kwa vyombo vya sheria matokeo yake matukio ya ukatili kuendelea kuwepo katika jamii. 
Hayo yamesemwa na Afisa Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Shirika la Kivulini,Godfrey Paschal leo Jumatatu Desemba 3,2019  kwenye kikao cha wadau wakati akiwasilisha taarifa matokeo yaliyopatikana kutokana na utafiti mdogo uliofanywa na Shirika la Kivulini kuhusu upatikanaji wa haki kwa wahanga wa ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilaya ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia. 

Alisema kutokana na utafiti mdogo walioufanya katika wilaya ya Shinyanga na Kishapu wamebaini kuwa changamoto hizo zinazopatikana mahakamani zinawafanya wananchi wakati tamaa wakati wanatumia rasilimali zao nyingi kwenda kwenye kesi mara kwa mara ambazo mwisho wake hauwanufaishi.

Alisema kitendo cha Polisi kuchukua muda mrefu kufanya uchunguzi/upelelezi kwenye kesi hususani kesi za mimba za utotoni mpaka mtuhumiwa wa kesi anakimbia bado ni changamoto.

“Tumebaini pia kuwa Wanawake wengi hawatoi taarifa kwa sababu ya kuogopa kuachwa na mume wake na kuwaacha watoto wake wakiteseka lakini pia kwa taratibu na utamaduni wa wasukuma hawapendi kutoa taarifa/ kumshtaki mume kwa watoa huduma kama Maafisa ustawi, polisi, na mahakama, badala yake wanataka kesi iishie ngazi ya familia tu”,alieleza Paschal. 

Paschal alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia kutokana na kwamba wanajamii wengi wamekuwa wakitoa taarifa tu pale wanaposhindwa kuelewana wao kwa wao hususani kwenye kesi za mimba.

Aidha alisema pamoja na kuwepo ongezeko la kuripotiwa kwa kesi lakini bado kesi nyingi za mimba za utotoni haziripotiwi.

Afisa huyo wa aliwataka wadau kwa kushirikiana na serikali kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kutoa taarifa mapema ndani ya masaa 72 na kuacha kumaliza kesi nyingi na kutengeneza sheria ndogo ndogo zitakazo wasaidia wanajamii watoe taarifa mapema au kuacha ukatili kabisa.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika kikao hicho,Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Hoja Mahiba alisema ukatili dhidi ya wanawake na watoto bado lipo katika halmashauri yake hivyo kuwataka wadau na jamii kwa ujumla kushiriki kutokomeza vitendo hivyo.

“Nawapongeza Kivulini kwa kufanya utafiti huu. Naomba kila mmoja ashiriki kwa nafasi yake katika kupiga vita ukatili wa kijinsia.Kila mtu ana familia yake,asimame katika nafasi yake ili jamii iwe salama kwani vitendo vya ukatili vinaathiri maendeleo ya taifa”,alisema Mahiba.

Kikao hicho cha kuwasilisha taarifa matokeo yaliyopatikana kutokana na utafiti mdogo uliofanywa na Shirika la Kivulini kuhusu upatikanaji wa haki kwa wahanga wa ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilaya ya Shinyanga umefanyika katika ukumbi wa zamani wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa haki za wanawake na watoto.

Washiriki wa kikao hicho wametumia fursa hiyo kujadili mikakati mbalimbali ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia huku washiriki wakisisitiza zaidi suala la elimu kwa wananchi kuachana na vitendo vya ukatili.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba akizungumza wakati wa kufungua kikao cha kujadili matokeo yaliyopatikana kutokana na utafiti mdogo uliofanywa na Shirika la Kivulini kuhusu upatikanaji wa haki kwa wahanga wa ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Desemba 3,2019 katika ukumbi wa zamani wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba alilishukuru shirika la Kivulini kwa kufanya utafiti kwenye halmashauri hiyo huku akibainisha kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani kwa watoto bado ni kubwa katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.Alisema ili kukomesha vitendo hivyo ni jukumu la kila mmoja kushiriki kupiga vitendo vitendo vya ukatili katika jamii.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba aliitaka jamii kuendelea kuwaelimisha watoto waache kujihusisha na mapenzi katika umri mdogo huku akivitaka vyombo vya dola ikiwemo polisi na mahakama kuacha kuchelewesha kesi za matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Shirika la Kivulini,Godfrey Paschal akiwasilisha taarifa matokeo yaliyopatikana kutokana na utafiti mdogo uliofanywa na Shirika la Kivulini kuhusu upatikanaji wa haki kwa wahanga wa ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilaya ya Shinyanga. Alisema wamefanya utafiti katika kata tatu za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambazo ni Nsalala,Nyida na Itwangi na kwa upande wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu,utafiti umefanyika katika kata za Kishapu,Talaga,Lagana,Uchunga,Ukenyenge na Shagihilu.
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Shirika la Kivulini,Godfrey Paschal alisema Kivulini ilifanya utafiti mdogo kwa wanajamii na watoa huduma mbalimbali kujua kwanini wahanga wengi wa ukatili hawatoi taarifa pale wanapofanyiwa ukatili na kuna changamoto gani zinawakumba ambapo baadhi ya matokeo yaliyopatikana ni Wanajamii wengi wanapenda kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia kwa wenyeviti wa vitongoji wenyeviti wa vijiji na wanamabadiliko kuliko kwa watoa huduma wengine.Pia ujuzi na uwezo wa wenyeviti wa vitongoji na vijiji wa kusuluhisha kesi ni mdogo sana.
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Shirika la Kivulini,Godfrey Paschal akiendelea kuwasilisha taarifa ya utafiti. Alisema utafiti wao umebaini kuwa wanajamii wengi hawatoi taarifa kwa watoa huduma ndani ya masaa 72 (siku 3) na kwamba kwa taratibu na utamaduni wa wasukuma hawapendi kutoa taarifa/ kumshtaki mume kwa watoa huduma kama Maafisa ustawi, polisi, na mahakama, badala yake wanataka kesi iishie ngazi ya familia tu. Pia alisema Wanawake wengi hawatoi taarifa kwa sababu ya kuogopa kuachwa na mume wake na kuwaacha watoto wake wakiteseka.Godfrey Paschal pia alieleza kuwa kuahirishwa kwa kesi mara kwa mara mahakamani, wakati wananchi wanatumia rasilimali zao nyingi kwenda kwenye kesi mara kwa mara na 
Polisi kuchukua muda mrefu kufanya uchunguzi/upelelezi kwenye kesi hususani kesi za mimba mpaka mtuhumiwa wa kesi anakimbia imekuwa ni changamoto kubwa.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba akiwasikiliza taarifa ya utafiti iliyofanywa na shirika la Kivulini. Utafiti huo umebaini kuwa idadi ndogo ya kesi zilizofika mahakamani na kufanikiwa imewafanya wananchi waone hakuna haja ya kupeleka kesi kwa vyombo vya sheria. 
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Hoja Mahiba akiongoza mjadala namna ya kumaliza vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani matukio ya mimba na ndoa za utotoni.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Hoja Mahiba akiongoza mjadala namna ya kumaliza vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani matukio ya mimba na ndoa za utotoni.
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Shirika la Kivulini,Godfrey Paschal akichokoza mada wakati wa mjadala namna ya kumaliza vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani matukio ya mimba na ndoa za utotoni.
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Shirika la Kivulini,Godfrey Paschal akichokoza mada wakati wa mjadala namna ya kumaliza vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani matukio ya mimba na ndoa za utotoni.
Mratibu wa Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto mkoa wa Shinyanga, unaotekelezwa na Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT), Glory Mbia akichangia hoja wakati wa mjadala wa namna ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ambaye ni diwani wa kata ya Iselamagazi, Isack Sengerema akichangia hoja wakati wa mjadala wa namna ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia ambapo alipendekeza wanafunzi wanaopewa mimba nao washughulikiwe badala ya kuwafunga jela wanaume wanaowapa mimba wanafunzi pekee.
Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Claude Kanyorota kutoka kitengo cha polisi na Jamii alishauri wenyeviti wa serikali za mitaa wapewe elimu ya kuhamasisha kuelekeza wananchi kupeleka kesi za ubakaji kwenye vyombo vya dola.Aliwasisitiza wananchi kutoa taarifa pindi wanapobaini kuwepo kwa dalili ama vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Diwani wa kata ya Nyida,Seleman Segeleti akichangia hoja wakati wa mjadala wa namna ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mchungaji Ibrahim Robert kutoka kanisa la CCT Shilabela kata ya Pandagichiza akichangia hoja wakati wa mjadala wa namna ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Diwani wa kata ya Itwangi Sonya Mhela akichangia hoja wakati wa mjadala wa namna ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mwakilishi wa BAKWATA Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Hemed Rashid akichangia hoja wakati wa mjadala wa namna ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mwakilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT) linalohusika na utetezi wa haki za wanawake,watoto na ujenzi wa tapo ya wanawake nchini Tanzania,Zainab Ally kutoka Iselamagazi akichangia hoja wakati wa mjadala wa namna ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mzee wa mila kutoka kijiji cha Welezo kata ya Nsalala ,Kapaya Sosoma akiwasisitiza Wasukuma kuacha tabia ya uoga kupeleka kwenye vyombo vya dola kesi zinazohusu matukio ya ukatili wa Kijinsia.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Mwakilishi wa Afisa Ustawi wa jamii mkoa wa Shinyanga Nyanjula Kiyenze akichangia hoja wakati wa mjadala wa namna ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga Ngwale Tedson akichangia hoja wakati wa mjadala wa namna ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Elizabeth Mweyo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) katika halmashauri hiyo.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kutoka Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Shinyanga,Victoria Maro akitoa taarifa ya Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Shinyanga juu ya matukio ya ukatili wa kijinsia. Alisema makosa yanayoripotiwa mara kwa mara katika ofisi za dawati ni kubaka,kulawiti,kutelekeza familia na mashambulio.
Afisa Elimu kata ya Nyida,Martin Kingu akiwasilisha taarifa ya matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo mimba za wanafunzi kwenye kata ya Nyida.
Afisa Elimu kata ya Nsalala,Ilioza Kakusa akiwasilisha taarifa ya matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo mimba za wanafunzi kwenye kata ya Nsalala.
Afisa Elimu kata ya Itwangi,Essero Ashery akiwasilisha taarifa ya matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo mimba za wanafunzi kwenye kata ya Itwangi.
Mratibu wa Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto mkoa wa Shinyanga.Glory Mbia akielezea namna wanavyotekeleza mradi huo kupitia Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT) linalohusika na utetezi wa haki za wanawake,watoto na ujenzi wa tapo ya wanawake nchini Tanzania.
Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Deus Mhoja akizungumza wakati wa kikao hicho.
Wadau wakiwa ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Wiki Hii....Zipo zaTANESCO, Umoja wa Mataifa, WHO, Benki Mbalimbali za Tanzania Na Zingine

Share:

CCM Yawaonya Walioanza Kampenzi za Urais na Ubunge Kabla Ya Wakati

Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amewaonya wanachama wa chama hicho tawala walioanza mikakati ya kutaka kupitishwa kuwania udiwani, ubunge na urais akibainisha kuwa kufanya hivyo ni makosa.

"Watu wa namna hiyo(walioanza mapema mikakati ya kutaka kupitishwa kuwania udiwani, ubunge na urais) hawatavumiliwa kwa kuwa taratibu za kuwania uongozi, nafasi mbalimbali katika chama hicho zipo wazi na zina muda wake" Dk. Bashiru Ally, Katibu mkuu wa CCM

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Desemba 3, 2019 katika ziara yake kisiwani Pemba, Zanzibar wakati akizungumza na kamati ya siasa Wilaya ya Chakechake.


Share:

DC Sabaya Aaamuru Kapteni mstaafu John Mushi Akamatwe

Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, ameagiza kukamatwa kwa Kapteni Mstaafu mkoani Kilimanjaro John Mushi, kwa madai ya kumiliki kwa mabavu eneo la TANESCO kwa zaidi ya miaka 35, huku akiwa halipii kodi ya ardhi anayodaiwa ambayo ni zaidi ya Milioni 20.

Eneo hio lenye ukubwa wa mita za mraba 3,371 mali ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) linadaiwa kumilikiwa na Mushi tangu mwaka 1984 huku kodi ikilipwa na Tanesco. Anadaiwa hana nyaraka zozote zinazomruhusu kufanya hivyo.

Sabaya pia ameagiza mali zilizokuwepo katika eneo hilo vikiwamo vifaa vya ujenzi kuzuiwa na mashine ya kufyatua matofali kupelekwa katika eneo la ofisi yake mpaka  Mushi atakapolipa kodi ya miaka 35 aliyolipiwa na Tanesco

Sabaya ametoa agizo hilo jana Jumatatu Desemba 2, 2019 baada ya kutembelea eneo hilo, kutoa siku 30 kwa Tanesco kuhakikisha wanazungusha ukuta eneo lote na siku 60 kuanza ujenzi wa jengo la kisasa.


Share:

VIDEO : Harmonize – Kushoto Kulia

VIDEO :  Harmonize – Kushoto Kulia


Share:

VIDEO : Rayvanny Ft. Patoranking, Zlatan & Diamond Platnumz – Tetema Remix

VIDEO :  Rayvanny Ft. Patoranking, Zlatan & Diamond Platnumz – Tetema Remix


Share:

Tanzania na Namibia Zajizatiti kukuza Biashara baina yao




Share:

Maswali 15 Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kwenye Usaili ( Interviews ) na Namna ya Kuyajibu

Usail wa ajira (interviews) husababisha hofu na msongo wa mawazo kwa vijana wengi kabla au baada ya kutoka chumba cha usaili.

Tatizo hilo hutokana na hofu inayojenga wakati wa kujibu maswali unayoulizwa  na watu ambao wamekuzunguka wakati wa kufanyiwa usaili.

Njia moja ya kuzuia hii kutokea ni kufuatilia mfumo wa kujibu maswali.

Ifuatayo ni orodha yetu ya maswali 15 yanayoulizwa mara kwa mara kwenye interviews( Usaili) na namna ya kuyajibu;

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

1.Jitambulishe(Wewe ni Nani?)
Mara nyingi hili ni swali ambalo mtahiniwa huulizwa mara tu aingiapo kwenye chumba cha usaili. Kwa bahati mbaya watahiniwa wengi hudhani kuwa waajiri hutamani kujua majina yao. Hapana, majina yako wanayafahamu na pengine hata taarifa za ziada. Katika swali hili waajiri uhitaji kujua sifa zako zihusianazo na ajira zitakazo dhihirisha kuwa wewe ni mtu sahihi.

Mfano mtu anaweza kujibu hivi, “Jina langu ni Mti Mkavu, ni Mhitimu wa Shahada ya Masoko ya Chuo Kikuu Dodoma. Ni mtu makini, mbunifu, mchapa kazi na ninayependa watu. Pamoja na hayo ninao ujuzi usio na shaka kwenye masuala ya mawasiliano. Uwezo wangu unadhihirishwa na mrejesho ambao huwa na upata kwa kila mtu ninaye fanya naye kazi”.

Katika swali hili ni muhimu kujua kuwa halihitaji wewe kuzungumzia mambo yasiyo husiana na kazi na ajira. Kwenu mpo wa ngapi,jina la mama yako, mkoa unaotoka, kabila, kazi ya baba au mama yako havihitajiki katika taarifa unazotakiwa. 


2.Kwanini upewe ajira kwetu? | au unaweza ukaulizwa Kwa nini unahisi wewe ni mtu sahihi kwa kazi hii na siyo mwingine?

Kumbuka kuwa usaili wa kazi unahusisha ushindani hivyo swali hili linataka uoneshe utofauti ulionao. Katika kujibu swali hili zingatia mahitaji ya kazi husika kujenga hoja kwani hata kama una utofauti wa aina gani kama hautasaidia katika kufikia  malengo ya taasisi bado itakuwa ni kazi bure.

Mfano, “ Siyo kwamba mimi ni mchapakazi na mbobezi katika uhasibu pekee lakini pia ni mtu ambaye ninaweza kufanya shughuli zangu bila kusimamiwa. Mimi ni mtu wa matokeo hivyo kwa kila ambacho hufanya hulenga kutimiza malengo kwa wakati na kufikia viwango stahiki. 


"Ubora wangu unathibitishwa na tuzo kadhaa nilizowahi kupata ikiwemo mfanyakazi bora wa mwezi mara nne nilipokuwa nikifanya kazi na na Magogo Media. Hii inathibitisha kuwa mkinipa fursa hii hamtakuwa mnajaribu bali mtakuwa mnafanya maamuzi sahihi”.

3.Unajua nini kuhusu sisi?
Siku zote maandalizi ya usaili yanaenda sambamba na kutafuta taarifa sahihi za taasisi husika. Hivyo ni vyema kuhakikisha kuwa taarifa unazotoa hapa ni sahihi na muhimu katika kudhirisha kuwa ulishafanya utafiti wa kutosha kuhusu taasisi husika.

Mfano, “ Benki yenu ilianzishwa mwaka 1987 ina maono ya kuwa benki bora kuliko zote nchini kwa kutoa huduma za kifedha zinazo aminika na kufikia maeneo mengi nchini. Kwa sasa benki yenu ina matawi 700 na ATMs 500 huku ikiwa na mpango wa kufungua matawi mengine Kigoma hivi karibuni. 


Endapo mtanipa fursa ya kufanya kazi na nyinyi nitahakikisha natumia vyema uwezo wangu katika masuala ya masoko ili kuongeza wateja na kuhaikisha huduma bora mnayotoa inafahamika kwa watu wengi.”

4. Ni vitu gani unavyojivunia?
Katika swali hili waajiri huhitaji kujua mambo kadhaa ambayo unayaona kama mtaji mkubwa katika utendaji kazi. Ni vyema kukumbuka kuwa mambo utakayo yataja hapa ni yale yenye umuhimu katika kuongeza ufanisi au ubora katika kazi husika kwani kila kazi inamahitaji yake ya tofauti na kazi nyingine.

Kwa mfano, “mambo makuu mawili ninayojivunia ni ujuzi na uwezo katika huduma kwa wateja na kujisimamia katika majukumu yangu. Kila ninapowahudumia wateja huwa napokea mrejesho chanya juu ya namna wanavyoridhishwa na huduma yangu hivyo kutamani kuhudumiwa nami tena.


Hii hunifanya nijione kuwa mtu muhimu sana katika taasisi yoyote ninayofanya nayo kazi. Pia, uwezo wangu katika kufanya shughuli bila kusimamiwa au chini ya usimamizi mdogo unanifanya niwe mtu wa kuaminiwa na kutegemewa katika kufanya shughuli zangu.Haya ni baadhi ya mambo mengi yanayonifanya mimi kuwa mtu wa tofauti. Nina amini hamtaacha fursa ya kufanya kazi nami”
 

5.Udhaifu wako ni upi?
Hili ni moja ya maswali ambayo watainiwa wengi huyachukia na kuyaona kama yana lengo la kuwatafutia sababu za kuwanyima kazi. Wengine kwa lengo la kuonesha ukamilifu huthubu kusema kuwa hawana udhaifu wowote-usithubutu kusema hivyo. Kila mtu ana udhaifu wake kwani hakuna aliye mkamilifu.

Suala la msingi ni kujua namna ya kujibu suali hili. Mambo ya kuzingatia ni pamoja na kuchagua udhaifu ambao hauta athiri utendaji wako na pili hakikisha udhaifu huo unahusiana na ujuzi na sio tabia. 


Ujuzi ni rahisi kuutafuata lakini kubadilisha tabia ni ngumu zaidi hivyo usiseme kuwa wewe ni mvivu,mdokozi, na mengineyo ya kitabia. Na unapotaja udhaifu wowote kumbuka kuonesha jitihada ambazo umeshazifanya ili kudhibiti udhaifu huo.

Kwa mfano, kwa kazi ya uhasibu mtu anaweza sema, “Udhaifu nilio nao ni masuala ya ‘graphic designing’ niligundua hili nilipohitaji kuandaa tangazo kwa ajili ya ofisi niliyokuwa nikifanya nayo kazi. Hata hivyo, nimeanza kujifunza mwenyewe kupitia mtandao wa internet na naona napata mabadiliko chanya kila leo”.

Kwa jibu hili ni dhahiri kabisa graphic designing siyo mahitaji muhimu ya kazi ya uhasibu hivyo haita athiti utendaji wa kazi.


6. Kwa nini uliacha kazi yako ya mwanzo?
Hapa unahitajikua makini sana, kumbuka na epuka kuzungumza vibaya kuhusu muajiri yeyote kabla au sasa au uwezo wa muajiri. 


Hapa unaweza ukawajibu tu kwamba;" Kwa sababu ya kuboresha na kuongeza ujuzi, pia natafuta fursa bora zaidi."

7.Unatarajia kupata nini kutokana na kufanya kazi hapa? au unaweza ukaulizwa | Baada ya miaka mitatu wewe mwenyewe utakua wapi?
Ongelea unachotumaini kutimiza ila kuwa mkweli. Pia usiongee kwa ujumla. Chagua kitu maalum ambalo ni muhimu kwa kampuni alafu ilenge. Ila, uwe wazi kwa kusema itachukua muda kujifunza zaidi kuhusu kampuni ili kufanikiwa zaidi.

Kwa mfano; “Nikiwa mwalimu wa kiingereza, lengo langu ni kuongeza asilimia ya wanafunzi wanaofaulu mtihani wa taifa kuwa 85% ya darasa yangu. Najua itachukua muda kujua vizuri changamoto za wanafunzi ila, naamini nitafanikiwa”


Ni vizuri kusema kwamba unatumaini kuona uwajibikaji zaidi  katika kampuni hiyo na kuongeza thamani katika kampuni kwa mchango wako. 

8.Kwanini umekaa muda mrefu bila kupata ajira?

Wajibu kwamba; "Nilikuwa najiendeleza katika taaluma yangu "


9. Eleza namna unavyoweza kujisimamia mwenyewe
Wajibu kwamba: Nitakuwa nafanya kazi niliyopewa nikishirkiana na wasimamizi wangu na viongozi juu ya namna ya kumaliza kazi kabla ya muda uliopangwa.


10. Kitu gani kinakukera miongoni mwa wafanyakazi wenzako?

Wajibu kwamba; "Naamini katika kufanya kazi kwa pamoja. Hata kama nikikerwa na kitu chochote, huwa najaribu kuepuka isipokuwa kama ni kitu cha binafsi."

11.Unategemea kufanya kazi kwa muda gani kama ukipewa ajira?

Wajibu:Kwa muda mrefu kama nitaendelea kuongeza kitu katika taaluma yangu.

12:Je, mwenyewe unajiona kufanikiwa?

Wajibu: Ndio, ukiachana na uwezo wa taaluma yangu, nadhani nimepata watu sahihi wa kufanya nao kazi.

13. Uwezo wako ni upi katika kazi?
Wajibu: Mimi huwa naelewa na kufundishika kwa haraka na ni mchapakazi wa kweli.

14,Unapenda nafasi au cheo gani katika timu unayofanya nayo kazi?
Wajibu: Haijalishi hadi nitakapojifunza kitu kipya kwa kila mradi au kazi.

15.Je, unaswali lolote kwetu? 

Mwishoni wa interview, ni kawaida kwa mwajiri kuuliza kama una maswali kwao. Ukipewa nafasi hii, usiulizie mshaara na faida zingine. Badala yake, uliza:
  1.     Maadili ya kampuni
  2.     Aina ya uongozi
  3.     Wafanyakazi wenzako
  4.     Chochote ambacho hukuelewa kuhusu kazi hiyo.
  5.     Watakupa jibu baada ya muda gani?
==>>USIFANYE HAYA MAKOSA KATIKA SWALI HILO:
- Je, kuna fursa ya kukua / kupandishwa ngazi?
- Nitapata siku ngapi za likizo?

- waajiliwa wanafaidika vipi na kampuni hii. 

==>Tiba bora ya msongo wa interview ni kujiandaa
Ingawa interview inaweza ikakupa misongo mingi, ukijiandaa vizuri Utashangazwa na mafanikio yako.

Interview ni nafasi yako ya mwisho kumvutia mwajiri, na vidokezo vilivyoelezwa hapo juu vitakusaidia na hilo.

Kumbuka, hamna haja ya kuwa na wasiwasi ukiwa umejiandaa. 


Nakutakia Mafanikio mema kwenye Interview
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

👉Sasa, kwa kuwa umeshajua jinsi ya kujibu vizuri maswali ya Interview, anza kutafuta kazi unayoitaka kwa kubofya hapo chini. 


Hilo ni Jukwaa Maalumu la Ajira zote za Serikali, Makampuni Binafsi n.k. Kuna Nafasi za Kazi zaidi ya 7000 kwa ajili yako.

👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
http://ajirazote.com/jobs


▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬


Share:

Serikali Kuzalisha Zaidi Ya Tani Elfu Hamsini Tatu Za Mbegu Mwaka 2019/2020

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Morogoro
Serikali nimewema kuwa katika msimu wa kilimo wa mwaka 2019/20 kwa kushirikiana na sekta binafsi, imejipanga kuzalisha jumla ya tani 53,608.2 za mbegu mbalimbali.

Wazalishaji hao ni pamoja na Wakala wa Taifa wa Mbegu (ASA), Vituo vya Utafiti, Magereza na Sekta binafsi. Aidha, Wizara kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) inaendelea na ujenzi wa Mradi wa Kuongeza Uwezo wa Kuhifadhi Nafaka.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 2 Novemba 2019 wakati akifunga mradi wa ubia kwa maendeleo ya mifumo ya uzalishaji endelevu wa mpunga Afrika chini ya jangwa la Sahara wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.

Amesema kuwa Sanjali na jitihada hizo, Wizara ya Kilimo imeanzisha kitengo cha masoko ya mazao ya kilimo ambacho kinahusika na kutafuta masoko ndani na nje ya nchi kwa mazao mbali mbali yanayozalishwa hapa nchini ili mbegu zitakazozalishwa na kuwa na mafanikio makubwa katika kilimo uweze kuimarisha kipato cha wananchi.

Takwimu zinaonesha kwamba wastani wa kitaifa wa matumizi ya zana bora za kilimo umeongezeka hadi kufikia asilimia 20 kwa matrekta na asilimia 27 kwa wanyama kazi ikilinganishwa na asilimia 14 ya  matrekta na asilimia 24 ya wanyama kazi mwaka 2013.

Amesema kuwa Kutokana na ongezeko hilo, matumizi ya jembe la mkono yamepungua na kufikia asilimia 53 kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na asilimia 62 kwa mwaka 2013.  Aidha, kupitia Mfuko wa Taifa wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) Wizara imeendelea kutoa mikopo ya pembejeo na zana za kilimo.

Mhe Hasunga amesema kuwa pamoja na hayo, Wizara kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika imeendelea kuimarisha Sekta ya Ushirika kwa kusimamia na kuhamasisha maendeleo yake hapa nchini ili wakulima waweze kunufaika na matunda ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika usimamizi madhubuti wa sekta ya ushirika.

Ameongeza kuwa Wizara ya Kilimo imeendelea kuratibu utekelezaji wa mikakati ya maendeleo ya kilimo hapa nchini kwa kuimarisha huduma za utafiti, upatikanaji na utumiaji wa pembejeo na zana za kilimo, udhibiti wa visumbufu vya mazao, huduma za ugani, uongezaji wa thamani na upatikanaji wa masoko.

Waziri Hasunga amesema kuwa Serikali imeendelea na jitihada mbalimbali za kuhakikisha inaongeza tija na uzalishaji wa mazao mbalimbali nchini. Jitihada hizo ni pamoja na Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kukamilisha mapitio ya Mpango Kabambe wa Taifa wa Umwagiliaji ili kubaini maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji kwa kuzingatia Mipango Shirikishi ya Maendeleo ya Rasilimali za Maji.

Aidha, Wizara ya Kilimo imeendelea kuanisha maeneo ya kipaumbele ya kuongeza tija kwa kuimarisha upatikanaji wa pembejeo za kilimo, udhibiti wa visumbufu, matumizi ya zana bora za kilimo na huduma za ugani; ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji; ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhi mazao ya kilimo na masoko; kufanya utafiti wa kilimo na kuzalisha teknolojia kwa mazao mbali mbali ukiwemo mpunga.

Amesema, Wizara imeanza na itaendelea kuipitia Sera ya Taifa ya Kilimo ya mwaka 2013 na sheria mbalimbali kwa lengo la kubaini maeneo ambayo yatapaswa kuhuishwa ili kwenda na hali halisi ya sasa na mwelekeo wa Serikali wa kubadili kilimo chetu kuwa kilimo cha kibiashara. 

Ameongeza kuwa Mtazamo wa Wizara ni kuwa na Sheria moja itakayosimamia rasilimaliwatu, matumizi bora ya pembejeo, ardhi ya kilimo na maeneo mengine muhimu.

Aidha, Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa serikali inatambua na kulipongeza Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa-FAO, Serikali ya Venezuela, Halmashauri za Wilaya za Kilosa, Mvomero na Kilombero kwa utekelezaji wa mradi wa ubia wa maendeleo ya mifumo ya uzalishaji endelevu wa mpunga Afrika chini ya jangwa la Sahara.

Kwa upande wake Muwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO nchini Tanzania Ndg Fred Kafeero ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuimarisha ushirikiano na Taasisi za kimataifa katika kuimarisha sekta ya kilimo.

Ameongeza kuwa mradi huo kwa upande wa Tanzania ulilenga kujenga mifumo yenye tija na endelevu katika Afrika ili kuboresha uhakika wa chakula na kuwezesha maendeleo endelevu kupitia mnyororo wa tahamani wa zao la mpunga miongoni mwa wakulima watoto hususani vijana.

Aidha amesema kuwa mradi huo ulilenga kukabiliana na changamoto zinazosababisha uzalishaji mdogo wa mpunga hapa nchini kwa kutambulisha na kusambaza teknolojia ya kilimo shadidi cha mpunga kwa kutumia njia kadhia ambazo FAO imetumia katika nchi nyingine.

Mkutano huo umehudhuriwa pia na Balozi wa Venezuela kwa Kenya na Tanzania Mhe Jesus Manzanilla Puppo, Naibu waziri wa kilimo na Ardhi wa serikali ya Venezuela Mhe Jose Gregorio Aguilers Contreras, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Loata Erasto Olesanare.

MWISHO



Share:

9 Vacancies at Dar Es Salaam Development Corporation (DDC)

9 Vacancies at Dar Es Salaam Development Corporation (DDC) December 2019 PRESIDENT’S OFFICE  PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT  Ref.No.EA.7/96/01/K/126 2nd December, 2019  VACANCIES ANNOUNCEMENT  On behalf of The Dar Es Salaam Development Corporation (DDC) President’s  Office, Public Service Recruitment Secretariat invites competent, experienced, highly organized and self- motivated Tanzanians to fill 9 vacant posts mentioned below;  CIVIL ENGINEER; – 1 POST… Read More »

The post 9 Vacancies at Dar Es Salaam Development Corporation (DDC) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Marufuku Uchimbaji Holela Wa Madini Ya Ujenzi Kahama

NA SALVATORY NTANDU
Wachimbaji na wamiliki wa maeneo yenye  madini ya ujenzi wilayani kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuwa leseni za uchimbaji ambazo zitawasaidia kuepukana na kutaifishwa kwa madini hayo pindi yanapokamatwa  na kubainika kutolipiwa kodi ya serikali.

Kauli hiyo imetolewa jana na Kamishina wa madini wa mkoa wa Shinyanga Mhandisi Joseph Kumburu kwenye mkutano maalumu na wamiliki wa maeneo ya uchimbaji, wachimbaji, wasafirishaji mjini kahama kuhusiana na kuwa na leseni za uchimbaji wa madini ya Ujenzi.

Amesema kwa mujibu wa sheria ya Madini ya mwaka 2010 kifungu cha sita na marekebisho ya kifungu cha 30 ni kosa la kufanya shughuli za madini bila kibali hivyo wanapaswa kuwa na leseni na hawatakubali kuendelea na  uchimbaji holela wa madini ya ujenzi katika mji wa kahama.

“Tumekuja kutoa elimu kwa kundi hilo linalojihusisha na shughuli za madini ili waitambue sheria hii na namna inavyofanya kazi endapo tukiacha uchimbaji huu holela ukaendelea katika wilaya ya kahama maeneo mengi yatabaki kuwa na mashimo”alisema Kumburu.

Naye mwenyekiti wa Wachimbaji wa madini ya Ujenzi katika wilaya ya kahama Martine Clemency amesema bado wanakabiliwa na changamoto nyingi katika uchimbaji wa madini hayo kutokana na mrundikano wa tozo pindi wanaposafirisha madini ya ujenzi.

“Msafirishaji wa madini haya anatozwa kodi shilingi 2500 kwa kila gari na wakati mwingine hutozwa zaidi ya mara mbili kutokana na kuwepo kwa mageti mengi kabla ya kufikisha mzigo kwa mteja wake jambo ambalo limekuwa likisababisha usumbufu kwa madereva wangu”alisema Martine.

Kwa upande wake ofisa Mazingira wa halamshauri ya mji wa Kahama Johanes Mwebesa amesema halamshauri ya mji imetenga maeneo ya uchimbaji wa madini katika kata ya Ngogwa  na wachimbaji wote wa madini ya Ujenzi waliopo mjini watalazimika kwenda huko ili kuzuia uharibifu wa mazingira.

“Tumefanya tahimini na kujiridhisha kuwa maeneo ambayo tumeyatenga yanafaa kwaajili ya shughuli hizo na muda si mrefu mtalazimika kwenda huko na kuondoka hapa mjini kwaajili ya shughuli hizo za uchimbaji madini Ujenzi”alisema Mwebesa.

Mkutano huo umejumusha wachimbaji,wamiliki wa magari na madereva wapatao 100 na madini ujenzi ambayo yanapaswa kulipiwa ushuru ni pamoja na kokoto,mchanga na moramu.


Share:

Jamii yaombwa kuwashika mkono watoto yatima

Na Amiri kilagalila-Njombe
Jamii nchini inaombwa kuendelea kutoa mchango katika vituo vya kulea watoto yatima pamoja na kusaidia watoto katika malezi,ili kuendelea kupunguza changamoto zinazovikabili vituo vya kulea watoto nchini.

Ombi limetolewa na baadhi ya walezi wa vituo vya kulea watoto yatima Njombe mjini mara baada ya hafla ya chakula cha mchana baina ya vituo vya kulea watoto mjini humo pamoja na viongozi wa ustawi wa jamii na maendeleo ya jamii wa mji wa Njombe iliyofanyika katika kituo cha kulea watoto yatima cha St.Anne kilichopo Uwemba mjini humo.

Sista Maria Mgeni ni msimamizi wa shule ya watoto yatima mtakatifu Donbosco iliyopo Unewa kijiji cha Madobole kata ya Luponde,anasema licha ya serikali na baadhi ya wahisani kutoa michango ya hali na mali ili kuendeleza vituo hivyo lakini bado wanaiomba jamii kuendelea kujitoa kwa kuwa bado changamoto zinaendelea kukabili vituo.

“Ningeomba msaada jamii iendelea kuchangia chochote iwe mavazi,chakula,vitanda, hata Magodoro na kwa upande wa serikali hasa maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii kwa kweli tunawashukuru sana kwa kuendelea kuwa pamoja na sisi”Alisema Maria Mgeni

Naye Sista Maria Mwinuka kutoka kituo cha kulea watoto yatima St.Anne,amesema wameweza kupata mafanikio makubwa ikiwemo kuokoa maisha ya watoto wengi wanaofika kituoni wakiwa na hali mbaya huku akiomba jamii ijifunze kuwajibika katika kuwalea watoto.

“Wito wetu jamii ijifunze kuwajibika kulea mtoto,katika familia za kiafrika watoto hulelewa na jamii kwa hiyo mama akifariki,ndugu pande zote mbili wahusike kumlea kwa karibu mtoto katika mazingira ya nyumbani”alisema Sista Maria Mwinuka

Enembora Lema ni afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya mji wa Njombe,amesema serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na vituo kwa ajili ya malezi ya watoto hivyo ametoa pongezi kwa kazi zinazofanywa na walezi.




Share:

Serikali inaandaa sheria ya kulinda na kuhifadhi urithi wa Ukombozi wa Afrika

Na Eleuteri Mangi, Kongwa
Serikali inaendelea kubainisha maeneo yaliyotumiwa na wapingania uhuru wa nchi za Kusini mwa Afrika ambayo yanasimamiwa kupitia Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika iliyopo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
 
Akiwa katika ziara ya kikazi wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma wakati akitembelea maeneo ya historia ya Ukombozi wa Afrika, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema kuwa Serikali kupitia wizara hiyo inaandaa sheria ya kulinda na kuhifadhi urithi wa ukombozi wa Afrika unaopatikana nchini.
 
“Lengo kubwa ni kuhakikisha maeneo haya yanalindwa kisheria ili yaweze kutumika kama vivutio vya utalii wa kiutamaduni pamoja na utalii wa kihistoria kwa sababu huu ni urithi muhimu wa historia nzuri ya nchi yetu, haya ni maeneo yaliyotumika kusaidia ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika” alisema Naibu Waziri Shonza.
  
Katika kutekeleza Programu ya Uhifadhi na Uendelezaji wa historia ya Ukombozi wa Afrika, Wizara inaendelea kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo, ukarabati wa jengo lililokuwa la Kamati ya Ukombozi ya iliyokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) ambayo kwa sasa ni Umoja wa Afrika (AU).
 
Kazi nyingine ambazo Serikali imekamilisha ni uandaaji wa tovuti ya Programu, ubainishaji wa maeneo yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi, utambuzi wa nyaraka na vitu mbalimbali vinavyohusiana na harakati hizo pamoja na kufanya mahojiano na watu walioshiriki au kushuhudia harakati za ukombozi wa Afrika ambayo yamehifadhiwa kwa njia ya kidigitali.
 
Mji wa Kongwa kihistoria ni kitovu cha harakati za Ukombozi wa Afrika kwani harakati zote za mapambano ya kutafuta uhuru zilianzia Kongwa na baadaye zikaendelea katika maeneo mengine nchini kama sehemu ya kupanua wigo wa harakati hizo na huduma kwa Wapigania Uhuru.
 
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Deogratius Ndejembi amesema kuwa Kongwa ni eneo kongwe lililotumiwa na Wapigania uhuru kutoka vyama mbalimbali vya Ukombozi kutoka nchi za Kusini mwa Afrika. 
 
Aidha, Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa eneo hilo lilitumika kwa ajili ya mafunzo kwa wapigania uhuru ambapo kwa sasa lina vielelezo muhimu vya kihistoria vilivyopo katika eneo hilo yakiwemo maeneo ya Handaki alilokuwa akilitumia Samora Mashel, nyumba za Makazi kwa wapigania uhuru, majengo ya shule ya sekondari Kongwa, eneo la Mafunzo ya kijeshi, kiwanja cha ndege na makaburi ya wapigania uhuru. 
 
Maeneo mengine ya kihistoria ni makaburi ya mashujaa wa harakati za ukombozi ambayo jumla yake ni 11; makaburi matano ya wapigania uhuru kutoka Msumbiji, makaburi matatu ya wapigania uhuru kutoka Afrika Kusini na makaburi matatu ya wapigania uhuru kutoka Namibia.
 
Naibu Waziri Shonza yupo katika ziara ya kikazi kutembelea maeneo ya ya historia ya ukombozi wa Afrika katika mikoa ya Dodoma wilaya ya Kongwa, Morogoro wilaya Kilosa, Manispaa ya Morogoro pamoja na Mkoa wa Pwani wilaya za Chalinze na Bagamoyo.  
 
Mwisho


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne Disemba 3





















Share:

Monday 2 December 2019

Uchaguzi CHADEMA: Heche Asema Kura Hazikutosha, Matiko Aomba Ushirikiano

Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amewashukuru wanachama wenzake waliompigia kura ijapokuwa hazikumpa ushindi, katika kinyang'anyiro cha kumtafuta Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti, uchaguzi uliofanyika usiku wa kuamkia leo Desemba 2,

Katika uchaguzi huo wa ndani Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko, aliibuka mshindi kwa kupata kura 44 dhidi ya kura 38 alizopata Mbunge Heche na kumfanya Matiko kuwa Mwenyekiti wa Kanda hiyo.

"Nawashukuru sana wanachama wenzangu na wajumbe kwa kura mlizonipa japo hazikutosha, nawapongeza wengine wote waliotumia Demokrasia yao kuchagua wagombea wenzangu, nawatakia kila la kheri walioshinda katika majukumu magumu mbele yetu" ameandika Mbunge Heche.

Kwa upande wake  Ester Matiko ambaye pia ni mbunge wa Tarime mjini amesema kura alizopata zinaonyesha imani kwake na kuahidi kufanya kila lililo ndani ya uwezo wake kuijenga Chadema katika kanda hiyo.

Matiko aliwaambia wajumbe wa mkutano huo wa uchaguzi uliosimamiwa na Meya wa Ubungo, Boniface Jacob kuwa umoja na ushirikiano miongoni mwa viongozi, wanachama na wananchi ndiyo siri ya mafanikio na kuwaomba wagombea wote kuvunja makambi kwa sababu baada ya uchaguzi kambi inayosalia ni ya Chadema.


Heche ambaye pia ni mbunge wa Tarime vijijini ndiye alikuwa mwenyekiti wa kanda hiyo tangu mwaka 2014.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger