Sunday 1 September 2019

FAIZA ALLY AFUNGUKA BAADA YA SUGU KUOA MWANAMKE MWINGINE


Mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya Mjini Sugu, Faiza Ally amesema amependezwa na tukio la kufunga ndoa kwa Joseph Mbilinyi, na anaamini sasa Mbunge huyo anaenda kuwa na maisha ya furaha zaidi.

Faiza ametoa kauli hiyo ikiwa saa chache baada ya Mbunge Sugu kufunga ndoa na mkewe Happines Msonga, ambapo kupitia mtandao wake wa Instagram, amesema licha ya Sugu kuoa bado ana mapenzi na yeye.

"Kuna mtu anayenipemnda sana alinipa ratiba nzima mwezi mmoja kabla ya ndoa na kabla ya hapo nilijua kama wataoana ila siku ya tukio ni siku ya tofauti, hata mwanzoni nilipotaka kufanya jambo nilijikuta nakosa hisia za kufanya kwa sababu sina tena majonzi juu ya baba Sasha.", amesema Faiza.

Ameendelea kusema, "nikimwangalia baba Sasha na mke wake sioni mtu wa kuniliza na najiuliza nilikosea wapi, kwa sababu nilikuwa mpenzi bora, nilikuwa mama bora kwahiyo sijapata mwanaume tu wa kunielewa mimi. Anaoa lakini najua bado ananipenda mimi".

Mapema jana Agosti 31, 2019 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi 'Mr.II Sugu' alifunga ndoa na mpenzi wake Happiness Msonga, katika kanisa Katoliki, Ruanda jijini Mbeya.
Share:

ALIYENASWA AKIFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI NDANI YA CHUMBA CHA MAMA YAKE ATUPWA JELA MIAKA 30


Mkazi wa Kata ya Mikumbi, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Abdull Mohamedi (30) amehukumiwa kifungo cha miaka (30) Gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na hatia ya kujihusisha kimapenzi na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahakama ya Mkoa huo, James Karymaha baada ya kuthibitisha bila shaka na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Hakimu Karyamaha akitoa hukumu katika kesi hiyo namba 08/2019 kupitia kifungu cha Sheria namba 130 kifungu kidogo (1) na (2) na 131 kifungu cha (2) amesema kutokana na kubanwa na Sheria amemuhukumu kifungo cha miaka 30 gerezani.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na Mwanasheria wa Serikali Abdulaha Madi Mohamedi kuwa mshitakiwa alikamatwa na mama mzazi wa mwanafunzi huyo Salma Salum, Julai 05, 2019, akiwa chumbani ndani ya nyumba yake na mtoto wake akishiriki mapenzi.

Mwanasheria huyo wa Serikali, amesema baada ya Mama mzazi kumkuta mshtakiwa akiwa na mtoto wake alitoa taarifa kwa uongozi wa Serikali ya Mtaa na Kata yao na majirani, ambao walifika na kufanikiwa kumkamata na kumfikisha kituo cha Polisi.

Kabla ya Jaji Ngwembe hajatoa adhabu hiyo, mshtakiwa alipewa nafasi ya kujitetea na kuomba imuonee huruma kwa kutompa adhabu kali, kwa madai ni mkosaji wa mara ya kwanza na pia shetani mbaya wa mapenzi alimpitia.
Chanzo - EATV
Share:

TAZAMA PICHA ZA BARABARA YA KYAKA-BUGENE


Picha zikionesha Sehemu mbalimbali za Barabara ya Kyaka-Bugene mkoani Kagera. Barabara hiyo yenye Urefu wa Kilometa 59.1 ni kichocheo kikubwa cha Uchumi katika Mikoa ya Kanda ya ziwa pia huunganisha nchi ya Tanzania na nchi jirani za Rwanda na Burundi. PICHA NA IKULU
Sehemu ya Barabara ya Kyaka- Bugene katika eneo la Kishoju Karagwe mkoani Kagera. 
Share:

WAZIRI LUGOLA AAGIZA BODABODA ZOTE ZISAJILIWE..., AWATAKA TRAFIKI KUACHA VISINGIZIO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akimsikiliza Katibu wa Chama cha Wamiliki na Waendesha Bajaj na Bodaboda Mkoa wa Kilimanjaro (CWBK), Rashid Omary, alipokuwa anatoa pongezi kwa Waziri huyo, kuwasaidia kupata eneo la maegesho ya Bajaj na Bodaboda Shairifu, Mjini Moshi, leo. Mwezi uliopita, Lugola alitatua mgogoro uliopo kati ya Manispaa ya Moshi na CWBK kuhusiana na maeneo ya maegesho. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Khamis Issa, na wapili kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani humo, Zauda Mohammed. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (aliyevaa Kaunda suti), akikagua eneo la maegesho ya Bodaboda na Bajaj, Sharifu, Mjini Moshi, leo. Lugola aliambatana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Khamis Issa (kulia), kukagua maeneo ya Aghakan na Shairifu ambalo lilileta mgogoro kati ya Manispaa ya Moshi na Chama cha Wamiliki na Waendesha Bajaj na Bajaj Mkoani humo (CWBK), na kutatuliwa na Waziri huyo mwezi uliopita, mjini humo. Wapili kushoto ni Katibu wa CWBK, Rashid Omary. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimuaga Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki na Waendesha Bajaj na Bodaboda Mkoa wa Kilimanjaro (CWBK), Rashid Omary, mara baada ya kumaliza kukagua vituo vya Sharif una Aghakan vya maegesho ya Bodaboda na Bajaj, Mjini Moshi, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimuaga Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kilimanjaro, Zauda Mohammed (kushoto), mara baada ya Waziri huyo, kumaliza kukagua vituo vya Sharif una Aghakan vya maegesho ya Bodaboda na Bajaj, Mjini Moshi, leo. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa huo, Khamis Issa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
…………………………………………………..
Na Felix Mwagara, Moshi (MOHA).

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amelitaka Jeshi la Polisi Kikosi Usalama Barabarani washirikiane na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuzisajili bodaboda na bajaj zote nchini ili ziweze kudhibitiwa katika ukusanyaji wa faini pamoja na matukio mbalimbali ya kiuhalifu zinapofanya makosa.

Lugola alisema ushirikiano kati ya viongozi au askari waliopo chini ya halmashauri nchini ipo ndani ya sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi Wasaidizi Sura namba 322, hivyo Jeshi lake linapaswa kushirikiana na Polisi Wasaidizi waliopo chini ya halmashauri ya Miji, Wilaya, Manispaa na Jiji kwa mujibu wa sheria. 

Waziri Lugola ameyasema hayo Mjini Moshi, leo, wakati alipokuwa anakagua vituo vya bodaboda na bajaj mjini humo ambapo mwezi uliopita alifanya mkutano na wamiliki na waendesha bodaboda na bajaj mkoani humo kwa lengo la kutatua migogoro mbalimbali waliokuwa wanailalamikia Manispaa ya Moshi kuwanyanyasa pamoja na kuwafukuza kuegesha kituo cha Sharif una Aghakan mjini humo ambapo Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabara Mkoani humo aliwaelekeza wawepo katika eneo hilo. 

“Askari wa usalama barabarani, muache visingizio kuwa ukamataji wa bodaboda ni mgumu hasa mnapowaandikia makosa walipe baada ya siku saba, mara usingizia bodaboda hazipo katika mfumo wa TRA kama magari, tukiziachia tuzipate wapi, nilishawaelekeza mshirikiane na viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijijini, Miji, Manispaa na Jiji kuanzisha kanzi data, kwenye mfumo wa kuwasajili waendesha bodaboda wote sehemu mbalimbali nchini, na taarifa za bodaboda hizo endapo zinafanya makosa inakua rahisi kuzikamata kwasababu zipo kwenye mfumo,” alisema Lugola.

Lugola aliongeza kuwa, lengo la usajili wa bodaboda huo, ni kutokana na kuepuka kuzikamata hovyo na kuziweka vituoni jambo ambalo analipinga kuepusha mlundikano wa boaboda vituoni na pia kuwasababishia bodaboda hao kuwaongezea umaskini zaidi.

“Naomba niendelee kurudia tena agizo hili, bodaboda zinazopaswa kuwepo vituo vya polisi ni za aina tatu, moja bodaboda zilizotumika katika matukio ya uhalifu, mbili zilizohusika katika ajali, na tatu bodaboda zilizookotwa, mbali na makundi hayo zinapaswa kulipwa faini,” alisema Lugola. 

Pia Lugola aliwataka baadhi askari na wananchi kuacha tabia ya kuwatuhumu viongozi wanapowatetea waendesha bodaboda wanaambiwa kuwa wanasiasa ndiyo wanasababisha ajali kuongezeka.

Amesema kauli hiyo sio sahihi, kwani wanaosababisha ajali asilimia 76 kwa mujibu wa utafiti wa ajali zinazotokea barabarani zinasababishwa na makosa ya wanadamu na sio bajaj na bodaboda peke yao, na asilimia 24 za ajali zinatokea zinasababishwa na ubovu wa miundombinu.

“Kumekuwa na dhana potofu kwamba wanasiasa kama mimi tunasababisha ajali za bodaboda, kwasababu tunawatumia bodaboda kwa mgongo wa siasa, sasa nataka niwaambie, wanaosababisha ajali barabarani ni asilimia 76 ni makosa ya wanadamu ambao ni wanadamu watembea kwa miguu, waendesha baiskeli, wenye mikokoteni, wanafuga mifugo barabarani na madereva ndio wanasababisha ajali, na sio bodaboda wala bajaj peke yao,” alisema Lugola.

Lugola amesema hakuna mahali popote ambayo tumesema baodaboda wakifanya makosa wasikamatwe, tunachosema na kusimamia nikupunguza umaskini kwa mujibu wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo inaelekeza Bodaboda na Bajaj wafanye biashara ili wapunguze umaskini. 

Aidha, Lugola amesema Serikali ya Magufuli inataka wananchi Watanzania wajiajiri hivyo sekta ya bodaboda lazima iheshimika kwakua nao wanatafuta ridhiki kama ilivyo kwa watanzania wengine.
Share:

OPARESHENI YA KIJANI YATUA KIGOMA..... WAZEE WATAKIWA KUPISHA VIJANA NAFASI ZA UONGOZI

Na Rhoda Ezekiel - Malunde1 blog Kigoma
Wazee wametakiwa kutoa nafasi kwa vijana waweze kugombea katika nafasi za uongozi na kuacha tabia ya kuwatisha na kuwazuia vijana ili kuwajengea msingi mzuri na kuwapima katika nafasi mbalimbali ili kujenga viongozi watakaoongoza kwa hekima na busara.

Rai hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi taifa (UVCCM) Kheri James  mkoani Kigoma wakati wa uzinduzi wa  'Oparesheni ya Kigoma ya Kijani'.

James alisema nchi inahitaji utayari wa vijana na uongozi wa vijana hivyo lazima wazeee wawaachie vijana kugombea na wasiwanyime nafasi ili waweze kuwapima na kuwajengea weledi wa uongozi na busara kwa kipindi hiki ambacho bado kuna wazee wenye busara ili waweze kuwapa busara hizo na waweze kubaki viongozi wazuri.

Alisema vijana wakipewa nafasi kwa kipindi hiki ambacho bado kuna wazee wa kuwapima kutokana na busara zao namna gani ya kuongoza, itasaidia kutengeneza taifa lenye uongozi ulio bora na unaozingatia misingi ya waasisi wa Taifa la Tanzania na kuepuka kuacha taifa la watu wanaofanya maamuzi bila kutumia busara.

Aidha James aliwataka wananchi wa mkoa wa Kigoma kuwapuuza wanasiasa wanaotumiwa na watu wa nje kuivuruga nchi, kwa kusema kwamb Tanzania kuna matatizo na hakuna kilichofanyika jambo ambalo sio kweli kwa kuwa mambo yaliyofanywa na Serikali iliyopo madarakani yanaonekana.

Alisema Siasa hazifai kutweza juhudi zinazofanywa na serikali kwa maslahi ya Taifa letu,  hivyo wanasiasa wanatakiwa kujua kazi yao ni kukosoa pale jambo linapoonekana haliendi sawa na kupongeza pale serikali inapofanya vizuri na sio kutumiwa na watu wa nje kuwakatisha tamaa viongozi wanaoifanya nchi isonge mbele kwa kuwa uchumi. 

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma, Amandus Nzamba alisema watajitahidi kutoa  nafasi kwa vijana,  ili na wao waweze kujifunza namna ya kuongoza  na kuiletea nchi maendeleo.

Aidha aliwaomba vijana kujitokeza kwa wingi kugombea uongozi kuanzia ngazi ya serikali za mitaa hadi uongozi wa juu, kwa kuwa vijana wengi wanaogopa kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali  hivyo sasa ni wakati wao.

Nae katibu wa Umoja wa Vijana(UVCCM) Kigoma Rashidi  Semindu alisema Vijana Kigoma wamejipanga katika chaguzi zinazokuja ikiwa ni pamoja na kulirudisha jimbo la kigoma mjini kwa chama cha mapinduzi na kuhakikisha vijana wote  wanajitokeza na kupambana na upinzani kwa Mkoa wa Kigoma.

Alisema wamefanikiwa kuwarudisha kwenye Chama Cha Mapinduzi vijana 82 wakiwemo waliokuwa Viongozi wa chama cha ACT wazalendo, wataendelea kuwashawishi vijana kutokana na mambo Makubwa yanayofanywa na viongozi wa CCM Kwa kuleta maendeleo Tanzania.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM)Taifa Kheri James pembeni ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kigoma Silvia Sigula  akikaribishwa Mkoani Kigoma.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM)Taifa Kheri James pembeni ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kigoma Silvia Sigula  akikaribishwa Mkoani Kigoma.

Share:

RAIS MAGUFULI NA MKEWE WAMESHIRIKI MISA TAKATIFU DOMINIKA YA 22 MWAKA 'C' KATIKA KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU PETRO PAROKIA YA OYSTERBAY DAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli, Mama Marry Majaliwa (Mke wa Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa) pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 22 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Dkt. Alista Makubi, Septemba 01,2019. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli, Mama Marry Majaliwa (Mke wa Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa) pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 22 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Dkt. Alista Makubi, Septemba 01,2019. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika Misa Takatifu Dominika ya 22 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Dkt. Alista Makubi, Septemba 01,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika Misa Takatifu Dominika ya 22 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Dkt. Alista Makubi, Septemba 01,2019.
Picha zote na IKULU
Share:

TAASISI NUNUZI ZASISITIZWA KUJIUNGA NA MFUMO WA MANUNUZI YA UMMA KWA NJIA YA MTANDAO (TANePS)


Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo akikabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo kwa mmoja wa washiriki.
Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo akiwahutubia washiriki wa mafunzo kuhusu matumizi ya mfumo wa TANePS yaliyofanyika jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika mafunzo kwa vitendo kuhusu matumizi ya mfumo wa TANePS .

Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) imetoa wito kwa Taasisi nunuzi kuwaruhusu watumishi wa vitengo vya usimamizi wa manunuzi pamoja na mifumo ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kushiriki kwenye mafunzo kuhusu matumizi ya Mfumo wa Manunuzi ya Umma kwa njia ya Mtandao ili ziweze kuunganishwa na kufanya manunuzi yake kwa kutumia mfumo huo. 

Wito huo umetolewa jijini Arusha na Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo, alipokuwa akifunga mafunzo ya siku sita kuhusu matumizi ya Mfumo huo unaojulikana kwa jina TANePS (Tanzania National e-Procurement System) kwa maafisa 110 wa vitengo vya usimamizi wa manunuzi na Tehama kutoka Taasisi 44. 

Mhandisi Kapongo amezisisitiza Taasisi nunuzi kuhakikisha zinaunganishwa na kisha kufanya manunuzi yake kwa kutumia mfumo huo wa TANePS ili kukidhi matakwa ya sheria ya manunuzi ya umma pamoja na uamuzi wa Serikali kutaka taasisi zote za umma kuunganishwa na TANePS ili ziweze kufanya manunuzi yote kupitia mfumo huo kwa lengo la kurahisisha michakato ya manunuzi kufanyika kwa ufanisi na tija zaidi na kuhakikisha upatikanaji wa thamani halisi ya fedha. 

Amezitaja baadhi ya faida za mfumo wa TANePS unaosimamiwa na PPRA kuwa ni kupunguza gharama na muda kwenye michakato ya manunuzi serikalini pamoja na kuongeza uwazi, ushindani na usawa kwa wazabuni na watoa huduma wanaoshindania zabuni mbalimbali zinazotangazwa na Taasisi za Umma. 

“TANePS inawezesha mchakato wote wa manunuzi serikalini kufanyika kielektroniki ambapo hakutakuwa na sababu ya wazabuni kutumia muda mwingi kutembelea ofisi za Taasisi za Umma pale wanapotaka kushindania zabuni, pia hawawezi kukutana ana kwa ana na watumishi wa taasisi za umma kwa kuwa kila kitu kinafanyika mtandaoni,”alisema Mhandisi Kapongo. 

Aidha, Mhandisi Kapongo ametoa wito kwa wafanyabiashara, wazabuni na watoa huduma kuhakikisha wanajisajili kwenye mfumo huo ili waweze kushiriki au kushindania zabuni mbalimbali zinazotangazwa na taasisi za umma. 

Tangu mwanzoni mwa mwezi Agosti, 2019, wataalamu kutoka PPRA wamepiga kambi jijini Arusha kwa ajili ya kutoa mafunzo kuhusu matumizi ya TANePS kwa awamu tofauti, programu inayotarajiwa kuwa endelevu ili kutoa fursa kwa wataalamu wa manunuzi kwenye taasisi zote za umma kupata fursa ya mafunzo hayo. Tangu kuanza kwa programu hii kabambe jumla ya watumishi 204 kutoka taasisi za umma 75 wameshapatiwa mafunzo hayo, ambapo wahusika wanapaswa kutembelea tovuti ya mfumo (www.taneps.go.tz) au tovuti ya PPRA (www.ppra.go.tz) ili kupata zaidi maelezo ya namna kujisajili kushiriki. 

Mafunzo haya yanagharamiwa na Serikali pamoja na ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB).
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEPTEMBA 1,2019






































Share:

Saturday 31 August 2019

UDOM- certificate and diploma selection 2019/20- Majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Udom (Cerificate na Diploma) 2019/2020

UDOM-SELECTED APPLICANTS FOR NON-DEGREE PROGRAMMES ROUND ONE FOR 2019/2020, UDOM- certificate and diploma selection 2019/20, UDOM- certificate and diploma selection 2019/20- Majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Udom (Cerificate na Diploma) 2019/2020, udom third round selection, diploma in pharmacy udom, udom second selection, udom diploma courses, diploma udom 2019/2020, udom diploma courses 2019 2020, udom diploma courses in health,… Read More »

The post UDOM- certificate and diploma selection 2019/20- Majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Udom (Cerificate na Diploma) 2019/2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

HALMASHAURI YA BUKOBA YAKUSANYA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI MOJA MWAKA WA FEDHA 2018/2019


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Murshid Hashim Ngeze.
Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Zaidi ya shilingi bilioni moja na Milioni mia tatu zimekusanywa na Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera Kwa Mwaka fedha 2018/2019 ambazo ni zaidi ya asilimia 97 za mapato kwa mwaka mzima.

Akizungumza leo Jumamosi Agosti 31,2019  katika kikao cha halmashauri hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo kilicholenga kufunga robo ya nne ya mwaka wa fedha 2018/2019,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Murshid Hashim Ngeze,amesema  mafanikio hayo yamekuja kutokana na kasi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kusimamia vizuri rasilimali mbalimbali za nchi.

"Mafanikio hayo yamekuja kutokana na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DkT. John Pombe Magufuli katika kusimamia vizuri rasilimali mbalimbali za nchi na ndo sababu kila kiongozi amewajibika kwa nafasi yake kuanzia ngazi ya juu mpaka ya chini kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote ujumla",ameeleza.
 

Ngeze amesema Halmashahuri hiyo imepiga hatua kubwa na kudai kuwa wakati wanaingia madarakani walikuwa wakikusanya zaidi ya shilingi milioni mia sita kwa mwaka lakini mpaka sasa wamevuka malengo kwa 100% kwa miaka minne wakiwa kwenye uongozi.

"Ni jambo la kumshukuru mungu nikikumbuka tulipoanzia hadi sasa ni hatua kubwa hii ni kutokana na juhudi kubwa za Rais wetu za mapambano yenye kuleta maendeleo amesema’’ ,amesema.


Mwenyekiti huyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Rukoma amesema tayari ujenzi wa shule ya sekondari umeanza kwenye kata ya Rukoma ili kutatua changamoto inayowakabili wanafunzi wa kata hiyo wanaohangaika kufuata huduma ya elimu umbali mrefu na kulazimika kutembea takribani kilometa 38.

Hata hivyo Ngeze ametoa wito kwa wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla
Share:

WAHUNI WADUKUA AKAUNTI YA TWITTER YA MWANZILISHI WA TWITTER

Wadukuzi walichukua kwa muda udhibiti wa akaunti ya Twitter ya mwanzilishi na mkurugenzi wa mtandao wa kijamii wa Twitter.

Kundi la wadukuzi linalojiita Chuckling Squad limedai kuhusika na udukuzi wa akaunti ya Twitter ya Jack Dorsey.

Akaunti hiyo iliyo wa mashabiki zaidi ya milioni nne ilianza kutumiwa kusambaza taarifa za chuki na kibaguzi kwa kutumia lugha chafu kwa karibu dakika kumi na tano.

Twitter inasema mitambo yake haikufikiwa na wadukuzi na badala yake kulaumu kampuni ya mawasiliano ambayo haikutaja jina lake kwa kusababisha hitilafu hiyo.

"Nambari ya simu inayohusishwa na akaunti hiyo ilivamiwa kutokana na hitilafu ya kiufundi iliyosababishwa na kampuni hiyo ya mawasiliano ," ilisema taarifa iliyotolewa na Twitter.

"Hali hiyo ilitoa fursa kwa watu wasio na idhini ya kutumia nambari hiyo kuanza kutuma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter."

Chanzo cha habari kutoka Kampuni hiyo ilithibitishia BBC kuwa wadukuzi walitumia mfumo unaojulikana kama "simswapping" kuchukua udhibiti wa akaunti ya Twitter ya Bw. Dorsey.

Huu ni mfumo ambao inatumiwa kuhamisha nambari halisi ya simu ya Dorsey katika laini nyingine- na kuanza kuitumia.

Wadukuzi mara nyingine hutoa hongo kwa wahudumu wa kampuni za mawasiliano au kuwapotosha kupata namabari halisi.

Kwa kuchukua udhibiti wa nambari hiyo wadukuzi waliweza kuandika ujumbe moja kwa moja katika akaunti ya Twitter ya Bw. Dorsey.

Japo siku hisi watumiaji wengi wa mtandao huo wanatumia programu tumishi kwenye simu zao kutuma ujumbe, awali Twitter ilibuniwa katika mfumo wa kutuma ujumbe mfupi- hali inayoisaidia kudhibiti idadi ya maneno mtumiaji anastahili kuandika.

Wadukuzi waliandika nini?

Ujumbe wa chuki na wa kibaguzi - ulitumwa moja kwa moja kwa kutumia akaunti ya @jack, na wengine wakasambaza ujumbe huo kwa kutumia akaunti zingine.

Ujumbe mmoja uliashiria kuna bomu limetegwa katika makao makuu ya kampuni hiyo.

Chuckling Squad imedai kuhusika na udukuzi wa Twitter za watu mashuhuri,kama vile mwanablogu wa masela ya urembo James Charles miongoni mwa watu wengine.

Japo tukio hilo linaonekana kufanyika nje ya kampuni hiyo, linasalia kuwa aibu kwa mtandao wa kijamii wa Twitter, unaotoa huduma kwa viongozi wenye nguvu zaidi ulimwenguni.
Chanzo- BBC
Share:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akutana Na Waziri Mkuu Wa Japan, Rais Wa JICA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe na kuishukuru Serikali ya Japan kwa ushirikiano inaoutoa kwa Tanzania.

Amekutana na kiongozi huyo leo (Jumamosi, Agosti 31, 2019) katika hoteli ya The New Otani, Tokyo Japan. Amesema Tanzania inaheshimu uhusiano mzuri uliopo kati yake na Japan

Mazungumzo yao yalihusu masuala mbalimbali yakiwemo ya kidiplomasia pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayofanywa kwa ushirikiano kati ya Japan na nchi yetu.

Waziri Mkuu ameishukuru Japan kwa misaada mbalimbali ya maendeleo inayoitoa nchini ambayo imesaidia katika kujenga uchumi na kuwaondolea wananchi kero mbalimbali

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji hususan wenye viwanda wawekeze nchini ili washirikiane na Watanzania kukuza uchumi.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kukuza uchumi na kufikia wa kati ifikapo 2025 kupitia sekta ya viwanda.

“Japan imepiga hatua kubwa katika tekinolojia hivyo naamini kuwa  wafanyabiashara na wenye viwanda  kutoka Japan wakiwekeza Tanzania wataleta tekinolojia yao pia.”

Awali, Waziri Mkuu alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Shinichi Kitaoka.

Katika mazungumzo hayo kiongozi huyo wa JICA alisema wameridhia kuwa wataendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutia saini mikataba mbalimbali yenye lengo kuinua maisha ya watanzania na kujenga uchumi.

Waziri Mkuu aliishukuru JICA kwa ushirikiano unaoutoa nchini likiwemo suala la kuendelea kuwapokea wanafunzi wa Kitanzania na kuwasomesha katika taaluma mbalimbali. Amesema Tanzania inathamini sana mchango unaotolewa na JICA katika ujenzi wa barabara, huduma za Afya na elimu.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,        
JUMAMOSI, AGOSTI 31, 2019.


Share:

Waziri Lugola Awataka Maafisa Uhamiaji Kuepuka Rushwa na Kutokuwanyanyasa Wawekezaji Nchini

Na Felix Mwagara, Moshi (MOHA).
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amewataka Maafisa Uhamiaji nchini, kuepuka rushwa na kutokuwanyanyasa wageni na hasa wawekezaji nchini.

Akizungumza katika kikao cha Maafisa Uhamiaji Waandamizi kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Uhamiaji (Trita), Mjini Moshi, leo, Lugola alisema wawekezaji ni watu muhimu katika maendeleo ya nchi, hivyo wanaposumbuliwa kwa kunyanyaswa bila sababu za msingi ni kuvunja misingi ya uadalifu.

Pia Waziri Lugola aliwataka maafisa hao waache kutoa PI (tangazo la kuondolewa mtu asiye raia nchini) zenye utata kwa maslahi binafsi bila kuzingatia athari ambazo nchi inazipata.

“Yapo malalamiko kwamba kuna wageni wanaingia nchini na kuwekeza kwa ubia na Watanzania, biashara inapokuwa inaendelea Watanzania huwazunguka wageni na kuwatengeneza mazingira ya kuwafukuza ili wapate fursa ya kumiliki hizo biashara na hapo ndipo Idara ya Uhamiaji hutumika, acheni hayo mambo kwa kuwa yanatuchafua kama taifa letu,” alisema Lugola.

Aliongeza kuwa, Rais John Magufuli anatafuta wawekezaji kwa nguvu na kuwahakikishia usalama wao na biashara zao lakini baadhi ya watumishi wa umma badala ya kusaidia jitihada hizi wao wanatumika kuwafukuza kwa dhuluma.

Alisema wageni hao wakishafukuzwa na wanaacha uwekezaji wao nchini ambao wanadhulumiwa huko waliko wanaisema nchi vibaya na kwa uzoefu huo wageni wengine hawawezi kuja nchini.

“Tujitathimini, tuzingatie sheria, kanuni, taratibu na miongozo yetu kwa kuzingatia maslahi ya taifa, pia nawasihi sana mumsaidie mheshimiwa Rais kutimiza ahadi zake kwa Watanzania ambazo amezitoa kupitia Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na ahadi zake nyingine mbalimbali ambazo amekuwa akiahidi na kuzitekeleza,” alisema Lugola.

Aidha, Waziri Lugola kabla ya kukifungua kikao hicho kilichojumuisha Maafisa kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, alisema kikao hicho kitakuwa chachu ya kudumisha maadili ya kazi, nidhamu, utii, na ushirikiano katika maeneo yao ya kazi ili kwenda sambamba na kauli mbiu ya Idara hiyo ya Upendo, Mshikamano, Uwajibikaji na Kukataa Rushwa.

“Ni imani yangu kuwa, mtaendelea kutekeleza majukumu yenu kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma katika utoaji wa huduma bora kwa Wananchi,” alisema Lugola.

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala, alisema kikao hicho zitatolewa mada mbalimbali zitakazowasilishwa kuhusu rushwa na Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018 ambazo ndio mwongozo wa utendaji kazi wa  Idara ya Uhamiaji.

“Kwa kuwa Idara yetu ya Uhamiaji inatoa huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo pasipoti, vibali vya ukaazi, pasi pamoja na viza, hivyo kupitia kikao hiki tutazingatia kikamilifu mada hizo kwa kuwa zitatusaidia katika kutoa huduma bora kwa maslahi ya Idara yetu, Wizara na taifa kwa ujumla,” alisema Dkt. Makakala.


Share:

Taarifa Kwa Umma: Kuhusu Mwenendo Wa Mlipuko Wa Ugonjwa Wa Ebola Ulioripotiwa Nchi Jirani Za Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo Na Uganda.




Share:

Jeshi la Polisi Latoa Onyo Kwa Watakaofanya Vurugu Wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mtaa

Jeshi la Polisi nchini limewatahadharisha wale wote watakaoleta vurugu wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa  na kusema watachukuliwa hatua kali za kisheria

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime, ambaye amesema kuwa watu wakifuata sheria chaguzi zote nchini zitabaki kuwa na amani.

“Wale ambao wanahisi watatingisha kiberiti kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa, sisi tumejipanga vizuri kukabiliana nao kwa nguvu zote kwa jinsi ambayo tutazidi kupokea nguvu toka kwao au ubishani toka kwao” amesema Misime.


Share:

Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ afunga ndoa rasmi

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mhe.Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la SUGU, leo Agosti 31, 2019 amefunga ndoa na Happiness Msonga katika  Kanisa la Katoliki Ruanda, jijini Mbeya.


Share:

Jipatie Tiba ya Asili ya Ngiri, Vidonda vya Tumbo,Kisukari na Nguvu za Kiume


Super nzoka  IKEMEKO   TRDITONAL clinic ;

Ni dawa ya Asili  iliyotengenezwa kwa techknojia ya kisasa na ubora wa hali ya juu 
 
Huongeza nguvu za kiume maradufu hata kwa wale wasiojiweza kabisa kufanya tendo la ndoa na wapo abao hata wakifanya hushindwa kutoa maji maji  ambayo ndani yake kuna mbegu za kiume zinazotakitakiwa kurutubisha yai

Dawa hii huboresha na tunatibu nakumaliza matatizo haya kwa muda mfupi tu na haina madhara.

Huanza kufanya kazi baada ya dakika 60 tu na kufanya uchelewe kufika kileleni dakika 20 .
 
Tiba hii ni ya kudumu.Pia tunatibu ngiri ya kupanda na kushuka,tumbo kuuguruma chini ya kitovu ,kaswende kisukari ,maumivu ya mgongo, kiuno, kutopata choo vizuri na uvimbe kupitia njia ya mkojo, presha, vidonda vya tumbo

Wasiliana Nasi kwa namba;  0789289945.Au whasap/0716343218 TUNAPATIKANA MBAGALA ZAKIEM STENDI ya mustang


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger