Monday 22 July 2019

Rais Magufuli aagiza kigogo aliyesimamishwa kazi mwaka 2016 arejeshwe kazini

Rais Magufuli ameagiza Dkt. James Mataragio  arejeshwe katika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), baada ya kusimamishwa kazi tangu Agosti 2016.

Agizo hilo amelitoa leo Julai 22, 2019 kupitia taarifa ya Ikulu ambayo imeeleza kuwa Rais, ameitaka Wizara ya Nishati kumrejesha kazini Mkurugenzi huyo Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania.



Share:

NAPE NNAUYE : KAKA JANUARY KARIBU BACK BENCH, HONGERA KWA UTUMISHI WAKO


Baada ya mawaziri, George Simbachawene na Hussein Bashe kuapishwa asubuhi ya leo, Julai 22, 2019 na Rais Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mbunge wa Mtama, Nape Moses Nnauye amewatumia salamu za pongezi viongozi hao.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Nape amesema kuwa uteuzi wa viongozi hao ni bora na kuwatakia mafanikio mema katika kazi yao mpya, huku akieleza sifa aliyoiacha Waziri aliyeondolewa katika nafasi yake, January Makamba.

"Uteuzi wa Mhe. Hussein Bashe na Mhe. Simbachawene ni katika teuzi bora kabisa. Ninawapongeza na kuwatakia majukumu mema!. Kaka January karibu 'back bench', hongera kwa utumishi wako!", amesema Nape.

Jana Jumapili, Rais Magufuli aliwateua George Simbachawene kuwa Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, akichukua nafasi iliyoachwa na January Makamba. Pia alimteua Hussein Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo, ambapo wawili hao wameapishwa leo, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Share:

MHANDISI WA MELI AJINYONGA BAHARINI KATIKATI YA SAFARI

Mhandisi msaidizi katika meli ya Mv Mapinduzi, Haji Abdalla Khatib (55) amefariki dunia baada ya kujinyonga wakati meli hiyo ilipokua inatoka Unguja kwenda Pemba.
Tukio hilo limetokea leo Jumatatu Julai 22, 2019, Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, Mustafa Aboud Jume amesema baada ya kupata taarifa hiyo walilazimika kusitisha safari na kuamuru meli hiyo irudi Unguja.
Amesema Khatib amejinyonga katika chumba cha Injini, sehemu aliyokuwa anafanyia kazi na kwamba, hadi sasa bado hawafahamu sababu za kujinyonga kwake.
“Marehemu alikuwa fundi umeme wa miaka mingi tangu enzi za meli ya ukombozi, hivyo ni mtu muhimu sana,” amesema.
Amesema pamoja na hayo, uchunguzi wa kifo hicho umefanyika na tayari jeshi la polisi linaanza kazi zake mara moja kwa lengo la kubaini sababu zilizomfanya injinia huyo kujitoa uhai wake.
Na Muhammed Khamis, mwananchi 
Share:

Naibu Waziri Bashe Atua Wizarani, Waziri Wa Kilimo Agawa Majukumu

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 22 Julai 2019 ameongoza kikao kazi cha uongozi wa juu wa Wizara ya Kilimo ili kutoa taswira ya muelekeo wa Wizara hiyo.

Kikao hicho kilichotuama kwa masaa kadhaa katika Ofisi ndogo za Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam na kuongozwa na Mhe Hasunga, kimehudhuriwa pia Naibu Maziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) na Mhe Hussein Bashe kadhalika katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Mathew Mtigumwe.

Katika kikao hicho Waziri Hasunga amewataka Naibu Mawaziri hao kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa bidii na ushirikiano ili kutimiza adhma ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli akiwa na muktadha wa kuimarisha uchumi wa wananchi kadhalika maendeleo kwa ujumla wake.

Waziri wa Kilimo Mhe Hasunga ametoa taswira ya muelekeo wa wizara hiyo katika mipango ya muda mfupi na muda mrefu ili kuwa na weledi na utendaji uliotukuka katika utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020.

Rais Magufuli amemteua Naibu waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe akishika nafasi ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa ambaye sasa ni waziri wa Viwanda na Biashara.

Moja ya mambo aliyoyabainisha Mhe Hasunga ni pamoja na haja ya kuanzishwa kwa Sheria ya Kilimo itakayotoa suluhisho la changamoto zinazamkabili Mkulima na Sekta hiyo kwa ujumla.

“Kuna kila sababu ya kuanzishwa haraka sheria ya kilimo na tayari tupo katika hatua za mwisho, kwa sababu hatuna Sheria ya Kilimo na inayotumika sasa ni Sera ya Kilimo, iliyotungwa mwaka 2013 ambayo pia inahitaji kupitiwa upya” amesema

Mhe. Hasunga ameongeza kuwa Sheria zinazotumika kwa sasa ni za Bodi za Mazao mbalimbali, ambazo pia zinachangamoto zake na kuna mazao ambayo hayana Bodi kiasi kwamba kuwatetea Wakulima wa mazao hayo inakuwa vigumu.

Mazao yaliyo katika utaratibu wa Bodi ni pamoja na zao la Pamba, Kahawa, Chai, Korosho, Pareto na Tumbaku kwa upande wa mazao ya biashara, mazao ambayo hayana bodi ni yale ya chakula ambayo nayo yana mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa.

Kadhalika ameeleza kuhusu usajili wa wakulima wa mazao yote na ambapo Bodi hizo ziliagizwa kuwapatia vitambulisho kwa ajili ya kuwatambua wakulima hao na wanapofanyika kazi zao ili iwe rahisi kuwahuduma.

Pamoja na mambo mengine Mhe Hasunga ametaja umuhimu wa Wizara ya Kilimo kuanzisha Bima ya Mazao itakayokuwa suluhisho kwa wakulima nchini ambao kwa muda mrefu wamekosa utetezi pindi wanapopatwa na majanga kutokana na uchache wa mvua ama vinginevyo, jambo linalopelekea kukoseka kwa mazao ya kutosha.

MWISHO.


Share:

RC GAGUTI AAGIZA MAWAKALA WANAOPOTOSHA WAKULIMA WA KAHAWA WAKAMATWE


Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog Kagera
Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Elisha Marco Gaguti ameagiza kukamatwa mara moja mawakala wa kampuni binafsi wanaopita vijijini katika wilaya za Karagwe na Kyerwa mkoani Kagera na kuwalaghai wakulima wa kahawa wasikubaliane na mfumo wa serikali wa kukusanya Kahawa katika vyama vya msingi na kuziuza kwa mfumo wa ushirika ulioanzishwa na serikali.

Mh.Gaguti ametoa maelekezo hayo Julai 21 2019 katika mkutano wa vyama vya msingi,watendaji wa kata na viongozi wa chama kikuu cha ushirika cha KDCU LIMITED wilayani Karagwe Mara baada ya kukagua viwanda vitatu vya kukoboa Kahawa vya Karim Amri, ASU Company limited na KDCU Limited kuona namna gani vinavyoendelea kuchakata kahawa.

"Nimeona nije kujionea msimu unaendeleaje na kama kuna changamoto yoyote tuitatue kwa pamoja na si kusubiri msimu umeisha.

"Nia ninazo taarifa kuwa kuna mawakala wawili wa kampuni binafsi wamekuwa wakipita vijijini kupotosha wakulima wasifuate mfumo wa serikali ili baadaye wanunue kahawa yao kwa bei ndogo tu, namuagiza kamanda polisi mkoa mawakala hao wakamatwe mara moja", amesema Gaguti.

Amesema maelekezo ya serikali yako wazi kuwa kama kuna mfanyabiashara yeyote anataka kununua Kahawa awasiliane na ofisi yake lakini awe na bei inayomnufaisha mkulima huku akidai kuwa mpaka sasa hakuna mfanyabiashara aliyekidhi vigezo.

Mkuu huyo wa mkoa ameagiza wakuu wa wilaya mkoani hapa kubuni maeneo yenye changamoto ya mtandao kuhakikisha wakulima wanalipwa malipo yao ya awali na wakulima ambao malipo yao yako chini ya laki moja hawatalipwa kwa njia ya mtandao watachukua fedha zao kwa simu za mkononi.

Vyama vikuu vya ushirika mkoani Kagera vya KCU 1990 LTD na KDCU LIMITED tayari vimekusanya Kahawa kilo milioni 8.5 sawa na asilimia 20% ya malengo ya ukusanyaji katika msimu huu wa mwaka 2019/20 na jumla ya shilingi bilioni 6.2 tayari zimelipwa kwa wakulima.

Aidha KDCU LIMITED tayari kimekusanya Kahawa ya maganda kilo 5.8 na shilingi Bilioni 5.3 zimelipwa kwa wakulima sawa na asilimia 15% ya matarajio ya makusanyo.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Elisha Marco Gaguti akizungumza.

Share:

Rais Magufuli aeleza sababu ya kumuondoa January Makamba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amebainisha baadhi ya matatizo yaliyokuwa yakipatikana kwenye Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, ikiwemo ucheleweshwaji wa utoaji wa vibali kutoka NEMC, pamoja na kupokea malalamiko ya wawekezaji kuhusu taasisi hiyo.

Akizungumza wakati akiwaapisha Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, George Simbachawene na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, leo Julai 22, 2019, Ikulu jijini Dar es salaam, Rais amesema kuna baadhi ya wawekezaji walikuwa wakikwamishwa na NEMC.

Magufuli amesema kuwa, "nataka kusiwe na ucheleweshaji wa kutoa vibali vya NEMC kwa wawekezaji wa Viwanda hapa Tanzania, vibali hivi vitoke kwa wakati kwa sababu tunahitaji viwanda ikiwezekana wawekeze kwanza na vibali vije baadaye."

Audha Rais ameongeza kuwa "Nakumbuka suala la mifuko ya plastiki lilichukua karibia miaka 4, nilisaini lakini halikutekelezwa mpaka hapa mwishoni nilitoa amri ya lazima, ndiyo likatekelezwa." ameongeza Rais Magufuli.

Julai 21, 2019 Rais Magufuli alifanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, kwa kumuondoa Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba, na kumteua George Simbachawene kuongoza Wizara hiyo.


Share:

TCU unbanned 6 universities and ban three universities from enrolling new students

TCU have banned 3 universities in the country from enrolling new students after a report blacklisted them for providing poor quality education , also unbanned 6 universities. Download the pdf below to check the full list of banned and unbanned universities

Download pdf>> TCU Yarejesha Udahili kwa Vyuo Vikuu Sita na Kufuta Usajili wa Chuo Kikuu kimoja

The post TCU unbanned 6 universities and ban three universities from enrolling new students appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Dakika mbili za Bashe akizungumzia matarajio yake Wizara ya Kilimo

Naibu waziri wa kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa atajitahidi kadri ya uwezo wake kutimiza  majukumu aliyopewa

Bashe ametoa kauli hiyo leo wakati wa hafla ya kuapishwa kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam, huku akisema Sekta ya kilimo ina changamoto na anaahidi kuzishughulikia.

"Nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kwa yale niliyopewa ili kusukuma gurudumu la maendeleo mbele, Sekta ya kilimo ina changamoto na ninaahidi kuzishughulikia, sitokuangusha na nitatimiza wajibu wangu.

"Mh. Rais nakushukuru kwa imani yako juu yangu na Wananchi wa Nzega, nalifahamu sana suala la Kilimo nafahamu changamoto hizi ambazo zimeajiri 70% ya Watanzania nilizoea kuzisikia tu sasa ntazipata field.

"Sekta ya kilimo tumekuwa tunaita tu kilimo cha kujikimu, ila nafahamu kilimo ni biashara na kilimo ni maisha, uchumi wa nchi hii ambapo ndoto yako ni kujenga uchumi wa viwanda ni lazima wakulima wawe na uwezo na yapaswa tuwatendee haki" -Amesema Bashe.

==>>Msikilize hapo chini


Share:

Waziri Lugola Aipongeza Jkt Ujenzi Nyumba Za Askari Magereza Ukonga, Jijini Da Es Salaam

 Na Felix Mwagara, MOHA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba za askari magereza unaofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Ukonga jijini Dar es Salaam.

Waziri Lugola amesema Jeshi hilo linastahili pongezi kutokana na kasi ya ujenzi wa nyumba hizo ambao umefikia asilimia 70 kukamilika.

Akizungumza mara baada ya kumaliza ukaguzi wa ujenzi huo, Lugola amesema, atazungumza na Rais John Magufuli ili aweze kutoa kiasi cha fedha kilichobaki kwa ajili ya kukamilisha asilimia thelathini zilizobaki ili mradi huo ukamilike.

Lugola amesema, Jeshi la Kujenga Taifa lilikabidhiwa mradi huo zaidi ya miezi miwili iliyopita kutoka kwa Wakala wa Majengo (TBA) kufuatia agizo Rais Dkt. John Magufuli baada ya kuonekana kusuasua kwake.

Waziri Lugola amesema, amefurahia kuona ujenzi huo ukiendelea vema na kwa kasi kubwa na kuwapongeza askari hao kwa kazi kubwa wanayoifanya na kusisitiza kuwa anataka kuona zaidi kauli ya Mkuu wa Ujenzi huo akisema Jeshi halishindwi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu, alisema amefurahishwa na kasi hiyo, na ana uhakika JKT ipo vizuri na matumaini yake makubwa ujenzi huo utakamilika hivi karibuni.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Phaustine Kasike, amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutawezesha jumla ya familia 172 za askari Magereza kuishi eneo katika makazi hayo huku ujenzi huo ukikadiriwa mpaka sasa kutumia zaidi ya shilingi bilioni.


Share:

Waziri Mkuu: Tumieni Fursa Za Utalii Kuboresha Maisha Yenu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Bashay, wilayani Karatu watumie fursa zinazojitokeza kwenye sekta ya utalii kuboresha maisha yao.

“Tumieni fursa ya uwepo wa eneo hili. Halmashauri wakishajenga vizimba vya biashara, leteni bidhaa zenu kama vile picha za tingatinga, mapambo, vinyago na vyakula vya asili ili watalii wakija hapa wapate huduma kutoka kwenu,” alisema.

Ametoa wito huo jana jioni (Jumapili, Julai 21, 2019) wakati akizindua mradi wa ujenzi wa vituo vya polisi vya kupunguza changamoto kwa magari ya utalii barabarani na kukabidhi gari la polisi kwa ajili ya patrol ya watalii katika eneo la Bashay, wilayani Karatu, mkoani Arusha.

Waziri Mkuu alizindua kituo cha kutolea huduma za usalama kwa watalii wilayani Karatu ikiwa ni ishara ya kuwakilisha vituo vingine vitatu vinavyoendelea kujengwa mkoani Arusha katika maeneo ya Kikatiti (Arumeru), Makuyuni (Monduli) na Engikaret (Longido).

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwasihi wakazi hao wawalinde watalii ili waitangaze vema nchi ya Tanzania pindi wakirudi makwao. “Ili kukuza na kutangaza utalii, tunapaswa tuwe na mapenzi mema kwa watalii lakini kikubwa zaidi ni usalama wao.”

Aliwataka wakazi hao waendelee kuiamini Serikali ya awamu ya tano na waendelee kumuombea Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili apate nguvu ya kuleta maendeleo zaidi.

Pia aliwashukuru viongozi wa Tanzania Association of Tour Operators (TATO) kwa kuchangia ujenzi wa vituo hivyo na kutoa gari jipya la polisi kwa ajili kituo hicho cha Karatu. Gari hilo aina ya Toyota Landcruiser lililogharimu dola za Marekani 45,000, limepewa namba za usajili za PT 4190.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wakazi wa Bashay waliohudhuria hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo alisema ujenzi wa vituo hivyo umetokana na malalamiko aliyopokea kwamba watalii wakitoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) hadi kufika Karatu wanakuwa wamesimamishwa njiani zaidi ya mara 20.

“Tulijiuliza hawa watalii wamekuja kutalii, wanataka kupumzika, sasa ni kwa nini wasumbuliwe kiasi hicho? Tuliamua kuanzisha vituo vya aina hii, ili watalii wafanyiwe ukaguzi kwenye check-points maalum,” alisema.

Aliomba Jeshi la Polisi liwapange barabarani askari ambao ni weledi na wana uelewa wa masuala ya utalii na kutolea mfano wa wiki iliyopita ambapo alikuwa akitokea mjini kwenda Karatu na kukuta magari ya watalii zaidi ya 10 yamesimamishwa njiani.

“Niliona baadhi yao wakiwa wamelala kwenye magari kwa uchovu, nilipowauliza wamekalishwa kwa muda gani, walisema ni kwa zaidi ya dakika 45. Nilipomuuliza askari aliyewasimamisha ni kwa nini anafanya hivyo, akanijibu kwamba dereva amemjibu vibaya. Hivi ni kwa nini watalii wateseke juani wakati mwenye makosa ni dreva?”

Naye, Makamu Mwenyekiti wa TATO, Bw. Henry Kimaro aliishukuru Serikali kwa jitihada inazofanya za kupambana na ujangili na kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini. “Tumeona hivi karibuni watalii wengine kutoka Israel, China na sasa ndege yetu imeanza kwenda India kuwafuata hukohuko,” alisema.

Alisema wameanza na vituo hivyo vinne mkoani Arusha lakini tatizo hilo liko maeneo mengi nchini na wao hawawezi kufika nchi nzima kutoa huduma kama hiyo. Hivyo, alimuomba Waziri Mkuu awahimize Wakuu wa Wilaya ambao wilaya zao zinajihusisha na sekta ya utalii, waige mfano wa wilaya ya Karatu ili kuhakikisha usalama wa watalii wawapo nchini.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Waziri Mkuu: Watoto Wa Kike Msikubali Kudanganywa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watoto wa kike wasikubali kudanganywa na wanaume na badala yake wakazanie masomo hadi wahitimu elimu ya juu.

“Wasichana wote mliopo hapa, mwanaume yeyote akikufuatafuata mwambie usinusumbue; mwambie niache nisome. Kamwe msikubali kudanganyika, someni hadi mmalize Chuo Kikuu,” alisema.

Ametoa wito huo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wakazi wa wilaya za Same na Mwanga akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa na ziara ya siku nne mkoani humo, amewaonya vijana na wazee ambao wana tabia ya kuweka mahusiano ya kimapenzi na watoto wa kike kwamba waache mara moja la sivyo wataishia jela.

“Wanaume msisahau kwamba mtoto wa mwenzio ni wako. Nataka niwakumbushe kuwa ukimuona mtoto wa kike, muache. Huyo ni moto wa kuotea mbali. Ukimchumbia, ukimuoa, au kumpa mimba mtoto wa kike, ujue kuwa miaka 30 jela ni yako.”

“Serikali ya awamu ya tano, imeamua kuwekeza kwa mtoto wa kike, kwa hiyo tunataka watoto wa kike wakianza shule ya awali, wasome shule ya msingi, waende sekondari hadi wamalize Chuo Kikuu,” alisisitiza.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,  


Share:

Hice na Land Cruiser za gongana uso kwa uso kahama na kusababisha vifo vya watu wanne na kujeruhi wengine 12 usiku huu

NA SALVATORY NTANDU
Watu wanne wamefariki dunia na wengine 12 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea jana majira ya saa mmoja usiku    katika eneo la nyambula kata ya Ngogwa Wilayani  Kahama mkoani Shinyanga baada ya gari aina ya Totoya hice yenye namba za usajili T 710  AZZ na Gari aina ya Land cruiser  yenye namba za usajili T 477 ATC.

Mpekuzi Blog  imezungumza na kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga (ACP) Richard Abwao ambaye alikuwa katika hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama kuhusiana na tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa hice iliyokuwa na abiria ikitokea kakola kwenda kahama.

Amesema barabara ya kakola kahama imekuwa na  vumbi nyingi kutokana na kutumika na magari mengi baada ya kuibuka kwa machimbo mapya ya kakola namba 9 na kuwataka madereva wote kuchukua tahadhari kwa kutoendesha kwa mwendo kasi ili kuzuia ajali.

Amefafanua kuwa leo RTO atakuwa na operation maalum katika barabara hiyo ili kubaini madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani pamoja na kuyaondoa magari mabovu yote barabarani.

Kamanda Abwao Amesema leo  atatoa taarifa rasmi  za ajili hiyo ikiwemo majina ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo.

Boniface Makoye shuhuda wa tukio hilo amesema baada ya ajali hiyo kutokea abiria wengi walijeruhiwa na aliweza kuwaokoa baadhi yao ambao walikuwa wamenaswa na vyuma katika hice hiyo.

Taarifa kamili zaidi kuhusiana na ajali hii endelea kufuatilia mpekuzi blog


Share:

Katibu Mwenezi Wa Chadema Akutwa Amejinyonga Kwa Kutumia Kamba Ya Katani Kwenye Mti.

NA AVITUS BENEDICTO KYARUZI, KAGERA.
Katibu mwenezi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema katika kata ya Igurwa Wilayani Karagwe mkoani Kagera amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani huku sababu za kujinyonga  zikiwa hazijafahamika.
 
Akizungumza katika eneo la tukio Diwani wa kata ya Igurwa Bwana WILBAD ABDALA amesema kuwa katibu huyo NURUBET BAKAISHUMBA (35) ambaye pia alikuwa mjumbe katika serikali ya kijiji cha  Bwera amekutwa amejinyonga kwenye mti jilani na nyumba yake.
 
Amesema kuwa mwili wa marehemu umegunduliwa na baadhi ya wanakijiji july 20 mwaka huu huku akiacha ujumbe wa maandishi unaoeleza kuwa familia yake haihusiki na kifo chake na kumtaka mke wake atunze watoto aliowaacha na kuonesha mali zake zilipo
 
Bwana Abdala amesema kuwa ujumbe huo aliouacha marehemu amesema kuwa uamuzi huo wa kujinyonga ni wake mwenyewena kwamba wazo hilo alikuwa nalo kwa muda wa mwezi mmoja.
 
Kwa upande wake katibu wa Chadema Wilaya ya Karagwe bwana AMON MINYANGO amesema kuwa chama hicho kimepoteza mtu muhimu ambaye mchango wake katika maendeleo ya chama hicho ulikuwa mkubwa.


Share:

Mhandisi Mtigumwe Akerwa Na Kusuasua Kwa Mradi Ya Erpp Hususani Katika Ujenzi Wa Maghala

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Morogoro
KATIBU mkuu wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe amefanya ziara katika Mradi wa kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga-ERPP) unaotekelezwa katika Wilaya za Kilosa, Kilombero na Mvomero Mkoani Morogoro na kutorishwa na kasi ya wakandarasi katika ujenzi wa Maghala ya kuhifadhia Mpunga.

Mradi wa ERPP unatekelezwa na Wizara ya Kilimo ukiwa na lengo la kuongeza tija katika uzalisha wa zao la Mpunga kwa kutoa mbegu  bora za zao hilo, ukarabati wa skimu za umwagiliaji ujenzi wa Maghala pamoja na utafutaji wa masoko.

Aidha Mradi wa ERPP  unatekelezwa katika Visiwa vya Zanzibar huku Tanzania Bara  ukitekelezwa katika Maeneo matano ya Mkoa huo.

Akiwa katika ziara hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe ametembelea ujenzi wa Maghala katika Kijiji cha Mvuha Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, ghala la Kijiji cha Msolo ujamaa Kilombero, Kijiji cha Njage Kilombero pamoja maghala ya  Kijiji cha Kigugu na Mbogo katika Halmashauri ya Wilaya Mvomero.

Mhandisi Mtigumwe amesema kuwa serikali haitosita kuwachukulia hatua wakandarasi hao kwa kuchewesha kazi wanazopatiwa pasina kuwa na sababu za msingi.

Amesema kuwa hatua zitakazochuliwa ni pamoja kupeleka mapendekezo katika bodi za wakandarasi ili kampuni hizo ziweze kufutiwa usajili nchini kutokana na kutotimiza matakwa ya serikali katika ujenzi wa maghala hayo ikiwemo kutokukabidhi kazi kwa wakati pamoja na ujenzi chini ya Kiwango.

Akiwa katika Kijiji cha Mbogo Katibu Mkuu huyo wa wizara ya Kilimo ametaka kuchunguzwa kwa Mkandarasi wa kampuni ya Skemu ya Mkoani Morogoro kutokana kuwa nyuma ya kazi tofauti na Mkataba wa kazi hiyo unavyoelekeza.

Amesema kuwa Mkandarasi huyo pia ameshindwa kuweka uzio mzuri katika eneo la ujenzi kutokana kutumia mabati mabovu hivyo kumtaka aubomoe kisha kujenga mwingine kama alivyoekezwa katika mkataba.

Awali  Viongozi wanaosimami mradi huo katika Mkoa wa Morogoro walimueleza katibu Mkuu wa Kilimo kuwa Baadhi wa wakandarasi wamekuwa wazito katika ujenzi hali inayotia wasiwasi wa kushindwa kukabidhi kazi kwa wakati.

Nao Baadhi ya wananchi wakizungumza kwa nyakati tofauti wameishukuru serikali kwa kuwaletea mradi huo na kueleza kuwa utakuwa chachu ya kuongeza uzalisha wa zao la Mpunga hali itakayofanya waweze kuongeza pato lao pamoja na kuchangia uchumi wa Taifa

kwa Upande wao wakandarasi hao wamesema kuwa awali walikuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali huku pia wakimuahidi katibu Mkuu huyo kukamilisha kazi kwa wakati na kiwango kinachotakiwa na serikali.

MWISHO


Share:

LIVE: RAIS JPM Akiwaapisha MAWAZIRI Aliowateua

LIVE: RAIS JPM Akiwaapisha MAWAZIRI Aliowateua


Share:

AJALI YA HIACE,LAND CRUISER YAUA WANNE NA KUJERUHIWA WATU 12 KAHAMA


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao 
Na Salvatory Ntandu- Malunde1 blog Kahama
Watu wanne wamefariki dunia na wengine 12 wamejeruhiwa katika eneo la nyambula kata ya Ngogwa Wilayani Kahama mkoani Shinyanga baada ya gari aina ya Totoya hiace yenye namba za usajili T 710 AZZ na Gari aina ya Land cruiser yenye namba za usajili T 477 ATC.

Ajali hiyo imetokea jana Jumapili Julai 21,majira ya saa moja usiku.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao ambaye alikuwa katika hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa hiace iliyokuwa na abiria ikitokea Kakola kwenda Kahama Mjini.

Amesema barabara ya Kakola Kahama imekuwa vumbi nyingi kutoka na kutumika na magari mengi baada ya kuibuka kwa machimbo mapya ya Kakola Namba 9 na kuwataka madereva wote kuchukua tahadhari kwa kutoendesha kwa mwendo kasi ili kuzuia ajali.

Kamanda Abwao amesema leo atatoa taarifa rasmi za ajili hiyo ikiwemo majina ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo.

Boniface Makoye shuhuda wa tukio hilo amesema baada ya ajali hiyo kutokea abiria wengi walijeruhiwa na aliweza kuwaokoa baadhi yao ambao walikuwa wamenaswa na vyuma katika hiace hiyo.

Taarifa kamili zaidi kuhusiana na ajali hii endelea kufuatilia Malunde 1 blog
Share:

Bashe, Simbachawene Kuapishwa Leo

Rais Magufuli atawaapisha mawaziri wateule ambao ni Mh. George Simbachawene kuwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na Mhe. Hussein Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo, leo Julai 22, 2019, kuanzia saa 2:30.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger