Monday 20 February 2017

MAGAZETI YA LEO JUMATATU FEB 20 2017

Share:

Sunday 19 February 2017

HII HAPA REPORT YA WANASAYANSI KUHUSU KUWEPO KWA BARA LA NANE DUNIANI



Wanasayansi wafahamisha kuwa bara la 8 lawezekana kuwa lipo chini ya bahari ya Pasifiki.


Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika jarida la Marekani la 'Geological Society of America' ni kwamba bara hilo limepewa jina la Zealandia .


Bara hilo lililokubalika na wanasayansi linasemekana kupatikana katika upande wa Kusini Magharibi mwa bahari ya Pasifiki.


Liko na ukubwa wa kilomita milioni 5 za mraba sawa na thuluthi ya ardhi ya bara la Australia .


Wanasayansi wamesema kuwa bara hilo limefinikwa na maji ya bahari .
Share:

Zijue Namba Maalum za Magari ya Viongozi, Serikali na Taasisi za Umma kwa Ujumla..!!!

Ukiona mtaani gari zimeandikwa ktk plate number kama ifuatavyo usiumize kichwa jua ni hivi:
1. Ngao-Rais, makamu wa rais na waziri mkuu
2. S-Spika wa bunge
3. JM- Jaji mkuu
4. JR- Jaji wa mahakama ya rufaa
5. JK- Jaji Kiongozi
6. J- Jaji wa mahakama kuu
7. XXXX-Mkuu wa majeshi(CDF)
8. CAG-Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali
9. CS- Katibu mkuu kiongozi
10. W mwanzoni inaashiria waziri kisha kifupi cha wizara yake hufuata
11. NW-Naibu waziri
12. DFP-Donor's Fund project
13. ST-Serikali ya Tanzania kisha herufi nyingine hufuata
14. SMZ-Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar
15. PT-Police of Tanzania
16. SM-Serikali za mitaa
17. CD- Magari ya ubalozini
18. SU-Shirika la umma.
19. gari za jeshi pia zina namba zake ambazo zina vifupi vya JW
20. MT-Magereza Tanzania
21. CGP-Commissioner General of Prison(Mkuu wa Magereza)
22. Gari nyingine za umma zina namba zaidi ya moja kwa kazi maalum
NYONGEZA:
Gari za biashara zina plate number nyeupe na zile za matumizi binafsi plate number ya njano.
Share:

MUGABE ANAWEZA KUPIGIWA KURA HATA AKIWA MAITI...


Mke wa Rais mkongwe wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amesema kuwa mumewe ni mashuhuri sana hivi kwamba anaweza kupigiwa kura hata akiwa maiti.
Bwana Mugabe, ambaye atakuwa na umri wa miaka 93 mnamo Jumanne, ametangaza mara kadhaa kuwa atagombea kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Grace Mugabe ana miaka 40 mchanga kwa mumewe.
Aliambia mkutano wa chama tawala cha ZANU-PF kuwa hata mumewe akifariki, bado jina lake litawekwa kwenye karatasi za kupiga kura.
Alisema watu wa Zimbabwe wanampenda rais wao sana, hivi kwamba wangempigia kura hata akiwa maiti.
Bi Mugabe amekuwa mkosoaji mkuu wa wakosoaji wa mumewe na kwa wale walio na tamaa ya kumrithi.
Inadhaniwa kuwa alikuwa mstari wa mbele wa kumwachisha kazi aliyekuwa makamu wa rais, Joice Mujuru mwaka 2014.
Bwana Mugabe, ambaye siku hizi haonekani sana hadharani, ametawala Zimbabwe tangu taifa hilo kuwa huru miaka 37 iliyopita.
Via>>BBC
Share:

MAELFU WAJITOKEZA KUMZIKA MCHEZAJI BONNY MWANDANJI

Maelfu ya wakazi wa mkoa wa Mbeya wamejitokeza katika mazishi ya mchezaji wa zamani Geoffrey Bonny Mwandanji aliyefariki dunia juzi na kuzikwa katika makaburi ya kanisa Katoliki Makandana wilayani Rungwe.


Akizungumza wakati wa mazishi baba mzazi wa marehemu,Bonifasi Mashamba alisema amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mwanae na kuongeza kuwa aliishi na watu vizuri jambo lililochangia watu wengi kujitokeza kumuuguza ikiwa ni pamoja na misaada mbali mbali.

Naye Mjomba wa marehemu, Innocent Sigonda alisema marehemu alikuwa akisumbuliwa na kansa ya mapafu pamoja sukari ilikuwa ikishuka mara kwa mara.


Mwenyekiti wa tawi la Yanga mkoa wa Mbeya Lusajo Kifamba alisema marehemu alikuwa mwanachama wao hivyo uongozi unasikitika kumpoteza mwanachama wake ambaye alikuwa akitoa msaada wa kiufundi kila alipotakiwa.
Naye mwakilishi wa uongozi wa yanga makao makuu Shadrack Nsajigwa alisema marehemu aliishi naye kama ndugu kwani walisaidiana na kupeana ushauri.
Alisema marehemu alikuwa na kipaji cha mpira pia alikuwa anajituma hivyo alikuwa mfano wa kuigwa kwa vijana waliopo.
Aliongeza kuwa wachezaji wa zamani ni hazina kwa taifa hivyo ni vyema wakatunzwa na kuthaminiwa.
 Aidha alitoa wito kwa wachezaji wengine kujipanga kimaisha ili baada ya kustafu wasisubiri kuomba misaada pindi wapatapo matatizo.
Alisema in vyema pia kuanzisha vyama vya kuwasaidia kama wachezaji wastaafu.
Share:

AMIRI JESHI MKUU RAIS DKT MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WAPYA WA JWTZ IKULU DAR



Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride wakati wa sherehe za Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka saini katika hati ya Kamisheni muda mfupi kabla ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka saini katika hati ya Kamisheni muda mfupi kabla ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Kikundi cha ngoma cha JWTZ kikitumbuiza kwa ngoma ya Chaso ya Pemba wakati Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipotunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Waziri wa ulinzi nja Jeshi la Kujenga taifa Dkt Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Juma Kijazi na viongozi wengine katika picha ya pamoja baada ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.PICHA NA IKULU
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI FEB TAREHE 19.2.2017

Haya hapa magazeti ya leo Jumapili,Februari 19,2017
Share:

Saturday 18 February 2017

Mwanamke asimulia alivyobakwa na askari Msumbiji

Wakati Serikali ikiahidi kufanya uchunguzi wa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika kutimua Watanzania nchini Msumbiji, mwanamke mmoja amesema alibakwa na askari watatu kabla ya kuwekwa mahabausu ambako alikaa siku tatu bila kula. 
Mwanamke huyo, aliyejitambulisha kwa jina la Halima (si jina lake halisi) ni mmoja kati ya zaidi ya Watanzania 180 ambao wamekuwa wakitimuliwa nchini Msumbiji tangu mwanzoni mwa wiki na wengi wakidai wana hati halali za kuishi nchi hiyo jirani na wengine kulalamikia vitendo vya ukiukwaji haki wakati wa utekelezaji wa operesheni hiyo. 
Tayari Serikali imesema kuwa itafanya uchunguzi wa madai hayo, ambayo yanaweza kuharibu uhusiano wa muda mrefu wa Tanzania na Msumbiji. 
Halima anasema walianza kufukuzwa usiku wa Jumamosi ya Februari 11, muda ambao askari hao waliutumia kumfanyia kitendo hicho. 
Halima anasema kuwa alisikia watu wakivunja geti la nyumba waliyokuwa wakiishi na kudhania ni majambazi, kumbe walikuwa ni askari ambao waliwalazimisha kutoa nyaraka zao zote za kuishi Msumbiji pamoja na pesa. 
“Niliwasikia wakivunja geti nikamwambia mume wangu watakuwa ni majambazi kumbe askari, mume wangu akajificha chini ya uvungu, lakini wakamtoa na baadaye kututoa ndani na kuanza kutupiga.” 
Anasema baada ya kipigo walilazimishwa kuzoa mali zao kutoka ndani na zikawekwa kwenye gari la polisi na kisha kuwafunga mikono na baadaye kuwapeleka mahabusu. 
“Cha kushangaza tulibebeshwa vitu wenyewe kuweka kwenye gari pasipo kuelezwa sababu baada ya hapo askari akanivuta nyuma ya nyumba na kuniingilia kimwili. Nikajua ni mmoja, lakini waliendelea hadi wakafikia watatu,” alisema. 
“Ninaona aibu walinibaka kwa njia ya kawaida tofauti na taarifa za wengine wanaosema tulibakwa kinyume na maumbile, si kweli. Nawaomba waelewe hatukubakwa kinyume na maumbile kama wanavyosema ilikuwa kawaida.” 
Hata hivyo anaeleza baada ya hapo waliwekwa mahabusu kwa siku tatu pasipo kula, hali iliyowalazimu kunywa maji yaliyokuwa yamewekwa chooni. 
“Tulikaa mahabusu siku tatu, hamna kula wala kunywa, chooni tulienda kwa mtutu tukalazimika kunywa maji ya chooni kwa sababu hakukuwa na jinsi na njaa ilizidi. Kwa hiyo inabidi useme unakwenda chooni ili ukanywe maji,” alisema Halima. 
Kutokana na hali hiyo, Halima anashangazwa na kauli ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Susan Kolimba kwamba waliorudishwa hawakuwa na nyaraka huku kaimu balozi wa Tanzania nchini Msumbiji akiwatangazia wengine kuondoka ndani ya siku tano. 
“Kweli mtu utathubutu vipi kuishi nchi ya watu bila kibali? Hata kaimu balozi na yeye anatukana, kwamba hatujaingia na documents (nyaraka)? Ilibidi atutetee lakini katukana. Mungu atatulipia,” alisema. 
Mwanamke mwingine aliyewekwa mahabusu kabla ya kurudishwa nchini, Mary Makundi anasema askari wa kiume walimwambia awape fedha na alipowajibu kuwa hana, walimpekua na kuzikuta. 
Anasema walizichukua fedha hizo pamoja na simu kabla ya kumpiga na kutaka kumbaka.
“Walivunja mlango wakanikuta. Wakaniambia niwape nyaraka zangu. Nikawapa nikijua wanazikagua tu na kuniacha, lakini cha kushangaza walizichana mbele yangu na kunitaka niwape pesa na simu. Nikawaambia sina wakanipiga na kunikagua hadi sehemu za siri na kuchukua pesa na simu,” alisema Mary. 
“Baada ya hapo walinipiga kwanza kabla ya kunifunga mkono. Askari mmoja akataka kunibaka, nikamwambia kuwa hata kama hawatutaki nchini kwao, hawawezi kuniingilia bila kinga. 
“Nilipoona hali imekuwa mbaya, nilisema wacha nigombane nife kwa silaha, lakini si kubakwa.” 
Mtanzania mwingine Mohamedi Said ni mmoja wa wafanyabiashara walioambiwa waondoke pasipo kuchukua chochote na anadai kuacha mali zake zote pamoja na nyumba aliyojenga. 
“Polisi walikuja ghafla wakatuambia wageni wote tunatakiwa tuondoke. Hapa nina vibali vyote mpaka leseni ya biashara, lakini imebidi niondoke kwa sababu ya usalama wangu,” alisema Said. 
“Hakuna anayejua sababu mpaka sasa. Nimekuja nyumbani kufuatilia haki yangu kwa sababu mpaka kibali cha kujengea ninacho. 
“Mpaka sasa amekuja kaimu balozi kutoka ubalozi wa Tanzania na amesema kwa ripoti aliyopewa ametupa siku tano tuondoke. Hatujui kwanini siku tano. Utahamishaje vitu kwa siku tano au kumtafuta mnunuzi wa nyumba kwa siku tano kwa sababu imenibidi niache duka kubwa na gari,” alisema Said. 
Akizungumzia tukio hilo, mwenyekiti wa Kijiji cha Kilambo kilichopo mpakani na Msumbiji, Mohamed Mkama alisema wananchi wa kijiji chake wamekuwa wakishirikiana na wanakijiji wa vijiji jirani vya Msumbiji, lakini tukio hilo limewashangaza. 
Amesema mara nyingi wamekuwa wakitembeleana na hata wengine kutoka upande wa Msumbiji kuja kutibiwa Tanzania kutokana na ujirani mwema uliopo. 
“Kijiji changu kina vitongoji vitano ambavyo tumekuwa tukishirikiana na kijiji cha upande wa pili kwa muda mrefu na wengine wana vitambulisho vya uraia mwema, lakini tunashangaa kwanini wanarudishwa pasipo kuelezwa sababu,” alisema Mkama. 
Ofisa uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama alisema idadi ya Watanzania waliorudi na kusajiliwa katika mpaka wa Kilambo ni watu 221 hadi kufikia jana mchana. 
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya February 18

Share:

Vurugu za mgambo na machinga zaibuka tena Jijini Mwanza

Share:

Thursday 16 February 2017

NECTA yasitisha mtihani wa udahili kwa kidato cha kwanza Jambo Blog 10


BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limesitisha mpango wa kuwafanyia mtihani wa udahili wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu katika shule za sekondari za serikali uliokuwa ufanyike Februari 28, mwaka huu.

Naibu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Salumu alisema hayo juzi kwenye kikao cha wadau wa sekta ya elimu Mkoa wa Morogoro alipokuwa akihitimisha mada yake kwa wajumbe wa kikao hicho kilichoongozwa na mkuu wa mkoa huo, Dk Stephen Kebwe.

Salumu alisema mpango wa kuwafanyia mtihani wa udahili wanafunzi hao ulitokana na matakwa yaliyowasilishwa Necta na baadhi ya wakuu wa shule za serikali wakipendekeza kupitia maofisa elimu wa mikoa na wilaya kuwa wanafunzi wa kidato cha kwanza waliochaguliwa na kupangiwa shule zao wengi hawana sifa na uwezo wa kumudu masomo.

Naibu Katibu Mtendaji wa Necta alisema wakuu wa shule walikuwa wakiomba kupata idhini ya kuwafanyia mtihani wanafunzi ili kubaini uwezo wao na kwamba baraza liliwasiliana na maofisa elimu mkoa na wilaya likiwataka kuwasilisha orodha ya idadi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza waliopangiwa kwenye shule ya zao.

Alisema baada ya kufahamika idadi ya wanafunzi hao, baraza ndilo litatunga maswali ya mitihani yenye kuzingatia mfumo na vigezo maalumu na kutumiwa wakuu wa shule hizo ili kuusimamia kwa lengo la kuweka uzani sawa wa mtihani huo.

Alisema moja ya masharti ni kwamba mtihani huo ulitakiwa ufanyike kwa wanafunzi wa kidato hicho kwa shule zote za serikali siku moja na kwa muda uliopangwa.

Hata hivyo, alisema baada ya kuwatumia masharti hayo, wakuu wa shule hizo walishindwa kuwasilisha orodha ya wanafunzi kwa maofisa elimu wa mikoa na wilaya ili itumwe Necta na kutokana na mazingira hayo, baraza limeamua kusitisha kuwadahili wanafunzi wa kidato cha kwanza na kuitaka mamlaka inayosimamia elimu kuendelea na utaratibu wao wa kawaida.

“Necta imewasiliana na wahusika kwa barua rasmi ya kusitisha mtihani huo ambao ulipangwa ufanyike Februari 28, mwaka huu na wanafunzi wote waliopangiwa kidato cha kwanza shule mbalimbali za serikali zikiwemo za bweni, waendelee na masomo kama yalivyopangwa,” alieleza Naibu Katibu Mtendaji wa Necta.

Novemba mwaka jana, serikali ilitangaza kuwa wanafunzi 526,653 sawa na asilimia 94.8 ya waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka jana, wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za sekondari za serikali katika awamu ya kwanza huku 28,638 wakishindwa kupangiwa shule katika awamu ya kwanza.

Kati ya wanafunzi hao, wasichana ni 268,052 sawa na asilimia 94.5 ya wasichana waliofaulu na wavulana ni 258,601 sawa na asilimia 95.2 ya wavulana waliofaulu.

Chanzo: Habari Leo
Share:

Wednesday 15 February 2017

AUDIO | YAMOTO BAND - KICHECHE | Download


Share:

NECTA: ADVANCED CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION MAY 2017


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA 
Ref. ACSEE 2017 
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL 
ADVANCED CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION MAY 2017
Share:

AUDIO | Diamomd Platnumz Ft. Sporah - Kosa Langu | Download [Extended]

Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATANO FEB 15 2017

Share:

Monday 13 February 2017

Zitto Kabwe Amtaka Rais Magufuli Avunje Bunge

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amemshauri Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli kulivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania endapo analiona ni kikwazo kwake.

Ushauri huo ameutoa jana ikiwa ni saa chache baada ya Rais Magufuli kukosoa uamuzi wa Bunge kumuita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kujieleza mbele ya Kamati ya Bunge, kutokana na kilichodaiwa na wabunge kuwa ni kauli ya kulidhalilisha Bunge.

Katika hotuba yake aliyoitoa jana wakati wa kuapishwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rais Magufuli aliwataka viongozi wengine kumuunga mkono mtu anayejitokeza kupiga vita dawa za kulevya badala ya kumdhalilisha.

"Tunapomuona mtu anajitokeza kupambana na haya madawa ya kulevya, badala ya kumdhalilisha tumuombee na kumtia moyo, hawa wanaweza hata kubadilisha maneno uliyoyazungumza wakabadilisha wakatengeneza kwenye clip wakatupa, na wakajitokeza wengine wakasema wameingilia mamlaka yao, wakati wao wanaingilia mamlaka ya kuwaita wengine, hii ni vita". Alisema Magufuli

Baada ya kauli hiyo ya Rais, Zitto kupitia ukurasa wake wa Facebook ameonesha kushangazwa na kile alichodai  kuwa Rais hakujua kuwa sheria ya kuundwa kwa mamlaka hiyo, ilitungwa, na kwamba anashangaa kuona Rais hakuwa akijua kuwa alipaswa kumteua Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo

Ujumbe wa Zitto unasema
"Wabunge walitoa Hoja Binafsi kuhusu Madawa ya kulevya ( Esther Bulaya na Faustine Ndugulile ) na kufuatia hoja hiyo Serikali ikaleta Muswada bungeni na Bunge likatunga Sheria ya Kupambana na Madawa ya kulevya mwaka 2015.

"Serikali mpya ikaingia madarakani mwezi Novemba 2015. February 2017 Ndio Kamishna Mkuu anateuliwa tena baada ya wabunge kuhoji na kushinikiza kupitia Kamati husika na pia mbunge Esther Bulaya aliyetoa Hoja Binafsi katika Bunge la Kumi.

"Rais anasema hakuwa anajua kuwa sheria hiyo ipo. Lakini Rais anapogawa Wizara huwa anatoa instruments na Hizo instruments hutaja kila sheria kwa kila Waziri. Ilikuwaje Rais akasahau sheria hii nyeti kama alikuwa na nia ya dhati ya Kupambana na Madawa ya kulevya?

Rais anaona Bunge kikwazo kwa sababu Bunge linamwongoza afuate sheria. Lakini Kama anaona Bunge linamkera turudi kwenye uchaguzi tu, alivunje".

Share:

Yusuf Manji Alivyochukuliwa na Gari la Wagonjwa Polisi na Kisha Kupelekwa Hospital

Mfanyabiashara maarufu na Mwenyekiti wa Club ya soka ya Yanga Yusuph Manji amekua akishikiliwa na Polisi kituo cha kati Dar es salaam toka Alhamisi ya February 9 2017 baada ya kwenda kuhojiwa kutokana na kutajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenye orodha ya watu 65 kwenye sakata la dawa za kulevya.

Jana jioni Mfanyabiashara huyo alichukuliwa na gari la kubebea Wagonjwa lenye namba za usajili za DFP na  alionekana akitembea na kuingia kwenye gari hilo (Land Cruise Nyeupe) yeye mwenyewe bila kubebwa au kusaidiwa huku gari lake aina ya Range Rover likitangulia mbele na watu wengine.

Baada ya gari hilo kumchukua msafara huo ulikwenda moja kwa moja kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Muhimbili Dar es salaam ambako watu mbalimbali wanaosumbuliwa na moyo hupata matibabu.
Gari la wagonjwa lililombeba Yusuf Manji na gari lake binafsi katika viunga vya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger