Tuesday 28 June 2016

Magazeti ya Leo Jumanne ya June 28, 2016


Share:

Monday 27 June 2016

Afariki Dunia Baada ya Kunywa GONGO Kupita Kiasi


MKAZI wa Mondo katika Kijiji cha Kitumba wilayani Magu, Wilson Magola (45), amekufa baada ya kunywa pombe haramu ya gongo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoani Mwanza, Ahmed Msangi alisema jana kuwa, tukio hilo lilitokea Juni 23, mwaka huu, saa 8:00 mchana kitongojini humo.

Msangi alieleza kuwa, baada ya kufika nyumbani kwa Daudi Mtula anayeuza gongo kwa siri Magola alikunywa pombe hiyo kupita kiasi akaishiwa nguvu na kupoteza maisha.

“Mtu huyo pia alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifafa,” Kamanda Msangi alisema na kuongeza kuwa, baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alitoroka na kuuacha mwili wa marehemu nyumbani kwake.

Alisema kuwa Polisi inamtafuta kwa ajili ya kumchukulia hatua za kisheria. 
“Tulipata taarifa kutoka kwa raia mwema na tulipofika nyumbani kwa mtuhumiwa tuliupata mwili na tayari umekwishafanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa familia kwa ajili ya maziko,” alisema.

Alitoa wito kwa wananchi kuiunga Polisi mkono kudhibiti biashara ya pombe hiyo haramu.
Share:

Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo

Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo kuanzia jana. 
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa ikimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema Rais amemteua Dk Charles Mlingwa ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Siha kujaza nafasi hiyo. 
Mulongo anakuwa mkuu wa mkoa wa pili kutimuliwa kazi na Rais Magufuli baada ya Anne Kilango Malecela aliyekuwa Shinyanga.

Hata hivyo, tofauti na Kilango ambaye alitimuliwa kutokana na kutoa taarifa potofu kuhusu watumishi hewa mkoani mwake, Ikulu haikutoa sababu za kutenguliwa kwa uteuzi wa Mulongo.

Mulongo ameondolewa madarakani miezi sita baada ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Dk Faisal Issa baada ya kutofautiana na Mulongo wakati huo akiwa mkuu wa mkoa huo.

Baada ya kumwondoa Dk Issa na nafasi yake kujazwa na aliyekuwa Kamishna wa Polisi, Fedha na Utawala (CP) Clodwig Mtweve, miezi miwili baadaye Rais alimbadilisha Mulongo kituo cha kazi akimhamishia Mara.

Alipoulizwa jana jinsi alivyoipokea hatua hiyo iliyochukuliwa dhidi yake Mulongo alisema: “Sina taarifa rasmi.” 

Kabla kuhamishiwa Mara akitokea Mwanza, Mulongo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Alishika nafasi hiyo baada ya kupandishwa cheo akiwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo.
Share:

CHADEMA Watafakari Hatua za Kuchukua Baada ya Rais Magufuli Kutaka Siasa Zifanywe 2020 ( wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao )


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pwani kimesema kinatafakari hatua gani ya kuchukua baada ya Rais John Magufuli kutaka siasa za nguvu zifanywe wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao, kauli inayotafsiriwa kuwa ni kupiga marufuku shughuli za kisiasa. 
Rais alitoa kauli hiyo mapema wiki iliyopita wakati akipokea taarifa ya Uchaguzi Mkuu kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kuisisitizia juzi wakati wa hafla ya kuzindua mpango wa polisi wa kuboresha huduma za usalama wa jamii. 
Akizungumza jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam, katibu wa Chadema wa kanda hiyo, Casmir Mabina alisema wamefikia azimio la kupinga unyanyasaji na ukandamizaji kwa vyama vya siasa unaofanywa na Serikali ya Dk Magufuli. 
Mabina alisema Rais Magufuli anavunja Katiba na Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 ambayo inaviruhusu vyama vya siasa kuendesha shughuli mbalimbali za kisiasa. 
Alisema vyama haviwezi kukaa kimya mpaka mwaka 2020 wakati kazi yao ni kukutana na wananchi. 

“Tunamshauri Rais Magufuli aache kutawala nchi kwa woga na ubabe ... afuate misingi ya Katiba na sheria, na kuwaongoza Watanzania badala ya kuwatawala,” alisema Mabina. 
 
Mabina aliongeza kuwa Jeshi la Polisi liache kutumiwa na Serikali kufinyanga sheria za nchi na kukandamiza upinzani kwa kutumia vibaya Sheria ya Jeshi la Polisi, kifungu cha 43 (3) kwa kusingizia habari za ‘kiintelijensia’ na ‘hali ya uvunjifu wa amani’. 
Mwenyekiti wa Chadema wa Kanda ya Dar es Salaam Kuu, Mwita Waitara alilalamikia kitendo cha mameya wa Dar es Salaam kunyimwa vibali vya kwenda nje ya nchi kutafuta fedha ili kusaidia maendeleo ya halmashauri zao. 
Alisema fedha za safari hizo zinatolewa na washirika wa maendeleo, lakini Serikali imekuwa ikizuia safari hizo kwa kisingizio cha kubana matumizi. 
Alisema safari nyingine za nje ni muhimu kwa sababu zinawawezesha mameya kukutana na wadau wa maendeleo ili kupata misaada. 

 “Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob alikuwa na safari ya kwenda Afrika Kusini kukutana na mameya wengine duniani, lakini alizuiliwa kwa maelekezo. 

"Hatuwezi kuendelea kama tutashindwa kukaa na wenzetu ili kujifunza mambo ya maendeleo,” alisema.

Mwita alidai kuwa huo ni mpango wa Serikali kudhoofidha halmashauri zinazoongozwa na upinzani ili wasiweze kufanya mambo makubwa ambayo hayajawahi kufanywa na CCM. 
Alisema yeye pia alizuiliwa kwenda Marekani akiwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii. 

Ushauri mwingine ulitolewa na mwenyekiti wa Kanda ya Ilala, Dk Makongoro Mahanga ambaye alimtaka Rais kufuata Katiba kwa sababu aliapa kuilinda na kuitetea kwa masilahi ya Taifa. 
Dk Mahanga alimtaka Rais akumbuke ahadi mbili alizozitoa wakati wa kampeni na wakati anaapishwa, ambazo ni kuilinda Katiba na kuwaletea wananchi maendeleo. 
“Kinachowaogopesha CCM ni upinzani kupata kura zaidi ya milioni sita wakati wa uchaguzi. Wanajua kwamba wanaweza kuchukua nchi, ndiyo maana wameanza kudhibiti vyama vya siasa ili visiwe na nguvu,” alisema Dk Makongoro ambaye aliwahi kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne.
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNE TAREHE 27.6.2016

Share:

Sunday 26 June 2016

BREAKING NEWS:RAIS MAGUFULI ATEUA WAKUU WA WILAYA 139 NA NAFASI ZA WAKUU WA MIKOA ZILIZOKUWA WAZI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60 ameamua wastaafu.
Mhe. Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.
Katika uteuzi huo, Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya kutokana na utendaji wao mzuri.
Aidha, nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali.
Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa)
ARUSHA
  1. Arusha           -           Mrisho Mashaka Gambo
  2. Arumeru        -           Alexander Pastory Mnyeti
  3. Ngorongoro  -           Rashid Mfaume Taka
  4. Longido         -           Daniel Geofrey Chongolo
  5. Monduli         -           Idd Hassan Kimanta
  6. Karatu                        -           Therezia Jonathan Mahongo


DAR ES SALAAM
  1. Kinondoni     -           Ally Hapi
  2. Ilala                -           Sophia Mjema
  3. Temeke         -           Felix Jackson Lyaviva
  4. Kigamboni     -           Hashim Shaibu Mgandilwa
  5. Ubungo          -           Hamphrey Polepole

DODOMA
  1. Chamwino     -           Vumilia Justine Nyamoga
  2. Dodoma        -           Christina Solomon Mndeme
  3. Chemba         -           Simon Ezekiel Odunga
  4. Kondoa          -           Sezeria Veneranda Makutta
  5. Bahi                -           Elizabeth Simon
  6. Mpwapwa      -           Jabir Mussa Shekimweli
  7. Kongwa          -           John Ernest Palingo

GEITA
  1. Bukombe      -           Josephat Maganga
  2. Mbogwe         -           Matha John Mkupasi
  3. Nyang'wale     -           Hamim Buzohera Gwiyama
  4. Geita               -           Herman C. Kipufi
  5. Chato             -           Shaaban Athuman Ntarambe

IRINGA
  1. Mufindi          -           Jamhuri David William
  2. Kilolo             -           Asia Juma Abdallah
  3. Iringa              -           Richard Kasesela

KAGERA
  1. Biharamulo   -           Saada Abraham Mallunde
  2. Karagwe         -           Geofrey Muheluka Ayoub
  3. Muleba          -           Richard Henry Ruyango
  4. Kyerwa           -           Col. Shaban Ilangu Lissu
  5. Bukoba          -           Deodatus Lucas Kinawilo
  6. Ngara             -           Lt. Col. Michael M. Mtenjele
  7. Missenyi         -           Lt. Col Denis F. Mwila

KATAVI
  1. Mlele              -           Rachiel Stephano Kasanda
  2. Mpanda         -           Lilian Charles Matinga
  3. Tanganyika    -           Saleh Mbwana Mhando

KIGOMA
  1. Kigoma           -           Samsoni Renard Anga
  2. Kasulu                        -           Col. Martin Elia Mkisi
  3. Kakonko       -           Col. Hosea Malonda Ndagala
  4. Uvinza                        -           Mwanamvua Hoza Mlindoko
  5. Buhigwe         -           Col. Elisha Marco Gagisti
  6. Kibondo        -           Luis Peter Bura

KILIMANJARO
  1. Siha                -           Onesmo Buswelu
  2. Moshi             -           Kippi Warioba
  3. Mwanga         -           Aaron Yeseya Mmbago
  4. Rombo           -           Fatma Hassan Toufiq
  5. Hai                 -           Gelasius Byakanwa
  6. Same              -           Rosemary Senyamule Sitaki

LINDI
  1. Nachingwea   -           Rukia Akhibu Muwango
  2. Ruangwa        -           Joseph Joseph Mkirikiti
  3. Liwale             -           Sarah Vicent Chiwamba
  4. Lindi               -           Shaibu Issa Ndemanga
  5. Kilwa              -           Christopher Emil Ngubiagai


MANYARA
  1. Babati             -           Raymond H. Mushi
  2. Mbulu                        -           Chelestion Simba M. Mofungu
  3. Hanang'         -           Sara Msafiri Ally
  4. Kiteto              -           Tumaini Benson Magessa
  5. Simanjiro       -           Zephania Adriano Chaula

MARA
  1. Rorya              -           Simon K. Chacha
  2. Serengeti        -           Emile Yotham Ntakamulenga
  3. Bunda                        -           Lydia Simeon Bupilipili
  4. Butiama         -           Anarose Nyamubi
  5. Tarime           -           Glodious Benard Luoga
  6. Musoma        -           Dkt. Vicent Anney Naano

MBEYA
  1. Chunya          -           Rehema Manase Madusa
  2. Kyela              -           Claudia Undalusyege Kitta
  3. Mbeya                        -           William Ntinika Paul
  4. Rungwe          -           Chalya Julius Nyangidu
  5. Mbarali          -           Reuben Ndiza Mfune

MOROGORO
  1. Gairo              -           Siriel Shaid Mchembe
  2. Kilombero     -           James Mugendi Ihunyo
  3. Mvomero       -           Mohamed Mussa Utali
  4. Morogoro      -           Regina Reginald Chonjo
  5. Ulanga                        -           Kassema Jacob Joseph
  6. Kilosa             -           Adam Idd Mgoyi
  7. Malinyi           -           Majula Mateko Kasika

MTWARA
  1. Newala           -           Aziza Ally Mangosongo
  2. Nanyumbu    -           Joakim Wangabo
  3. Mtwara           -           Dkt. Khatibu Malimi Kazungu
  4. Masasi                        -           Seleman Mzee Seleman
  5. Tandahimba -           Sebastian M. Walyuba

MWANZA
  1. Ilemela           -           Dkt. Leonald Moses Massale
  2. Kwimba          -           Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon
  3. Sengerema     -           Emmanuel Enock Kipole
  4. Nyamagana    -           Mary Tesha Onesmo
  5. Magu              -           Hadija Rashid Nyembo
  6. Ukerewe        -           Estomihn Fransis Chang'ah
  7. Misungwi       -           Juma Sweda

NJOMBE
  1. Njombe          -           Ruth Blasio Msafiri
  2. Ludewa                      -           Andrea Axwesso Tsere
  3. Wanging'ombe          -           Ally Mohamed Kassige
  4. Makete                       -           Veronica Kessy

PWANI
  1. Bagamoyo      -           Alhaji Majid Hemed Mwanga
  2. Mkuranga      -           Filberto H. Sanga
  3. Rufiji               -           Juma Abdallah Njwayo
  4. Mafia              -           Shaibu Ahamed Nunduma
  5. Kibaha           -           Asumpter Nsunju Mshama
  6. Kisarawe        -           Happyness Seneda William
  7. Kibiti               -           Gulamu Hussein Shaban Kifu

RUKWA
  1. Sumbawanga -           Dkt. Khalfan Boniface Haule
  2. Nkasi              -           Said Mohamed Mtanda
  3. Kalambo        -           Julieth Nkembanyi Binyura

RUVUMA
  1. Namtumbo    -           Luckness Adrian Amlima
  2. Mbinga           -           Cosmas Nyano Nshenye
  3. Nyasa             -           Isabera Octava Chilumba
  4. Tunduru        -           Juma Homela
  5. Songea           -           Polet Kamando Mgema

SHINYANGA
  1. Kishapu         -           Nyambonga Daudi Taraba
  2. Kahama         -           Fadhili Nkulu
  3. Shinyanga      -           Josephine Rabby Matiro


SIMIYU
  1. Busega           -           Tano Seif Mwera
  2. Maswa                        -           Sefu Abdallah Shekalaghe
  3. Bariadi           -           Festo Sheimu Kiswaga
  4. Meatu             -           Joseph Elieza Chilongani
  5. Itilima             -           Benson Salehe Kilangi


SINGIDA
  1. Mkalama       -           Jackson Jonas Masako
  2. Manyoni        -           Mwembe Idephonce Geofrey
  3. Singida           -           Elias Choro John Tarimo
  4. Ikungi             -           Fikiri Avias Said
  5. Iramba           -           Emmanuel Jumanne Luhahula

SONGWE
  1. Songwe           -           Samwel Jeremiah
  2. Ileje                -           Joseph Modest Mkude
  3. Mbozi             -           Ally Masoud Maswanya
  4. Momba          -           Juma Said Irando


TABORA
  1. Nzega             -           Geofrey William Ngudula
  2. Kaliua             -           Busalama Abel Yeji
  3. Igunga                        -           Mwaipopo John Gabriel
  4. Sikonge          -           Peres Boniphace Magiri
  5. Tabora           -           Queen Mwashinga Mlozi
  6. Urambo         -           Angelina John Kwingwa
  7. Uyui                -           Gabriel Simon Mnyele

TANGA
  1. Tanga             -           Thobias Mwilapwa
  2. Muheza          -           Mhandisi Mwanaisha Rajab Tumbo
  3. Mkinga           -           Yona Lucas Maki
  4. Pangani          -           Zainab Abdallah Issa
  5. Handeni        -           Godwin Crydon Gondwe
  6. Korogwe        -           Robert Gabriel
  7. Kilindi                        -           Sauda Salum Mtondoo
  8. Lushoto         -           Januari Sigareti Lugangika

Wakuu wote wa Wilaya walioteuliwa wanapaswa kufika Ikulu Dar es salaam siku ya Jumatano tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi kwa ajili ya kiapo cha maadili ya uongozi na maelekezo mengine kabla ya kuapishwa na wakuu wa mikoa watakaporejea katika mikoa yao.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
26 Juni, 2016

Share:

USHAURI WA BURE NINI CHA KUFANYA KWA WANAFUNZI WOTE MLIOKOSA NAFASI ZA KUJIUNGA KIDATO CHA 5 2016

Image result for ngao ya tanzania 


Habari zenu wadau wa BLOG PENDWA YA MASWAYETU
,namshukuru allah kwa kuniwezesha kuiona siku hii ya leo tena.
Mada ambayo napenda kuiongelea hapa ni kuhusu vijana wote waliokosa nafasi za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano july 2016,lakini wanasifa za kujiunga na kidato cha tano,Basi kama wewe au ndugu yako ni mmoja wapo fanya yafuatayo kwa kuangalia lipi linakufaa kwa sasa;

1.SUBIRI SECOND SELECTION
Endapo bado una nia ya kwenda kidato cha tano na umefaulu vizuri,mara nyingi serikali yetu imekuwa sikivu katika kuhakikisha kuwa kila kijana aliefaulu anachaguliwa kujiunga kidato cha tano,huwa inatoa second selection kwa wanafunzi wwenye sifa za kujiunga na kidato cha tano,kwa hiyo kama wewe GPA YAKO ni kuanzia 1.6 au div 3 pts 25  na unahamu na kidato cha tano tafadhali subiri utachaguliwa.

NOTE:usibweteke na kusubiri tu hizo second selection fanya yafuatayo kwani kidato cha TANO sio maisha ,maisha ni popote pale,basi fanya yafuatayo;

2.APPLY UALIMU KUPITIA NACTE
Nacte inahusika na vyuo vya ualimu kwa ngazi ya diploma na kushuka chini,basi naomba ufanye hima uombe ualimu haraka mara tu watakaofungua application,Kama una sifa zifuatazo omba ualimu fasta wakifungua.

EDUCATION PROGRAMS 
The Ministry of Education and Vocational Training in collaboration with the National Council for Technical Education (NACTE) would like to inform the public that Central Admission System (CAS) is now open for new applicants into Teacher Training Institutions for academic year 2016/17
Minimum Entry Requirements:

  1. Ordinary Diploma (Pre Service): Division I – III OR GPA of 1.6 in O’Level
  2. Ordinary Diploma (In Service): Grade IIIA Certificate
  3. Higher Diploma: Two (2) principle passes in A’Level or Ordinary Diploma (NTA 6).
  4. Ordinary Diploma in Laboratory Technology: Passes (D) in Physics, Chemistry, Biology and Mathematics
NOTE:KUNA UWEZEKANO MKUBWA NACTE WAKAFUNGUA APPLICATION UPYA,PLEASE WAKIFUNGUA FANYIA KAZI USHAURI WANGU.

MWISHO:
Endapo utaufanyia kazi ushauri wangu nina imani kubwa malengo yako yatafanikiwa mbele kwa mbele,nakutakia mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Wako,
Share:

AJALI: Meli ya mizigo iitwayo HAPPY yazama eneo la Chumbe, Unguja ikitoka Dar kuelekea Zanzibar

Meli ya mizigo iitwayo Happy ikitokea Dar es salaam kwenda Zanzibar imezama eneo la Chumbe, Unguja.

Taarifa zimedai kwamba Meli hiyo ilianza kuzama saa 10 alfajiri baada ya kuingiza maji ndani na kukosekana kwa vifaa kama motor ya kutolea maji hayo kufikia saa 1 asubuhi hii Meli hiyo ilizama kabisa ndani ya maji.


Meli hiyo ilikuwa imebeba Dengu gunia 450 pamoja na Mbao zaidi ya 1000 huku wafanyakazi sita waliokuwa ndani ya Meli hiyo wakiokolewa.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa ni meli ya mizigo mitupu na mabaharia mpaka sasa imeripotiwa kwamba wote ni wazima.

13502130_1070396369720352_3702524120513408319_n.jpg 13495064_500820163444320_103952615715841024_n.jpg
13529254_500820133444323_9094812653178131848_n.jpg
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger