Wednesday 18 November 2015

HAYA HAPA MAGAZETI YOTE YA LEO JUMATANO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO AWAMU YA NNE 2015/2016-BATCH 4

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Tokeo la picha la HESLB

AWAMU YA NNE YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA MIKOPO

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwafahamisha waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwa imetoa orodha ya AWAMU YA NNE yenye jumla ya waombaji wa mwaka wa kwanza 718 waliopangiwa mikopo.
Itakumbukwa kuwa wiki iliyopita, Bodi ilitoa orodha ya Awamu ya Tatu iliyokuwa na waombaji 6,915 waliopangiwa mikopo. Kati ya waombaji hao waliopangiwa mikopo, waombaji 4,642 ni walikua ni wale wanaojiunga na shahada ya kwanza katika vyuo mbalimbali nchini na waombaji 2,273 ni wanafunzi wanaojiunga na Stashahada (Diploma) ya Ualimu wa masomo ya sayansi na hisabati katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Kwa msingi huo, Bodi inapenda kuufahamisha umma kuwa hadi sasa imekwishawapangia mikopo jumla ya waombaji mikopo wenye sifa 48,469 wa mwaka wa kwanza. Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla ya waombaji 12,282; Awamu ya Pili wanafunzi 28,554; Awamu ya Tatu wanafunzi 6,915 na Awamu hii ya Nne wanafunzi 718 wamepangiwa mikopo.
Majina yote ya waombaji waliofanikiwa kupangiwa mikopo kutoka katika awamu zote tatu yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa olas.heslb.go.tz na tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz). Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili.

Mwisho.
Share:

Tuesday 17 November 2015

NDUGAI ASHINDA USPIKA KWA KURA 264 SAWA NA 70% YA KURA ZOTE

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mbunge wa Kongwa (CCM) Job Ndugai ashinda kiti vcha Uspika kwa kura 264 sawa na kura asilimia 70 huku mpinzani wake kupitia Chadema Goodluck Ole Medeye akipata kura 109 huku wagombea wengine wakipata kura 0.
NDUGAI anakuwa Spika wa Bunge la 11 la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBER 17 2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

I have set here headlines of various Tanzania News paper today, spend your time to read what is written here
Share:

Monday 16 November 2015

TAARIFA KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA STASHAHADA ZA UALIMU ELIMUMSINGI NA ELIMU YA SEKONDARI KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
  TAARIFA KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA STASHAHADA ZA UALIMU ELIMUMSINGI NA ELIMU YA SEKONDARI KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwataarifu wote waliochaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) baada ya Mfumo wa CAS kuonyesha kuwa umechaguliwa kwenda Chuo Kikuu cha Dodoma, utaratibu ni kusubiri UDOM na vyombo vyake vya ndani kuthibitisha majina hayo. Waliodahiliwa wanatakiwa kwenda chuoni baada ya kupata joining instructions na wito kutoka Chuo husika.

Kumekuwapo na wanafunzi waliosafiri kwenda kuripoti chuoni kabla ya taratibu hizi kukamilika na hivyo kusababisha usumbufu kwao wenyewe na kwa taasisi za NACTE na UDOM. Majina ya wanaotakiwa kwenda kuripoti na tarehe za kuripoti mara zote hutolewa na chuo husika. Kwa kuwa majina yamekwenda vyuoni kwa makundi (batches) sio makundi yote yamepitishwa na katika mchakato wa ndani ya vyuo.
Baraza (NACTE) hutoa uchaguzi wake ili kuondoa usumbufu kwa wanafunzi kuangalia tovuti za vyuo mbalimbali kusaka majina yao. Iwapo kwa sababu zozote UDOM itashindwa kuwapokea baadhi ya waliochaguliwa, Baraza litawapa nafasi katika vyuo vingine. Ikumbukwe kuwa kuna vyuo vingi ambavyo havijapata wanafunzi wa kutosha.
Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
15 Novemba 2015
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WA IFM AWAMU YA KWANZA,PILI NA TATU WALIOPATA MKOPO 2015/2016

Share:

Students Fear Impending Dropout Due to Lack of Loans

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 Scores of university students   will be forced to drop out because of prolonged delay of loans to cover tuition and other expenses.
 
The development comes in the wake of last week’s announcement by the High Education Students’ Loan Board (HESLB) that it issued loans to over 40,000 students out of 50,830 applications received in 2015/16 academic year. 
 
However, the payment only covered new students but skipped all together the majority of continuing students.
 
In separate interviews, a cross-section of students from different universities blamed the loans facility of being “too selective” and giving little consideration to continuing students.
 
Charles Alphonce, a second year student at Mzumbe University, told The Guardian that he had all the required  qualifications to secure a loan yet he had being left out.
 
“This is the third time I am applying for a loan and I have never got any luck,” he lamented.
 
“I can’t understand what’s wrong with my applications,” he said with the sad acknowledgment that, “...should I fail to get the loan this time around I will have to postpone my classes.”
 
Alphonce who comes from a poor family background said he has been struggling to raise funds for his studies but due to increasing costs he may be forced to drop out.
 
Another student from the University of Science and Technology (MUST) Mbeya Campus, Samuel Hosea shared a similar experience and appealed to the board to treat all eligible loan applicants fairly without bias.
 
Hosea also called upon the board to give special consideration to students from outside the campus regions who have to go out of pocket to survive while waiting for the  loans that may not come at all.
 
Chairman of the Ministers of Loans in High Education in Tanzania, Shitindi Venance, said the gravity of the problem is such that only 400 students of 6,000 eligible students at the University of Dar es Salaam received their loans in their first year.
 
Expressing profound dismay over the exclusion of continuing students, Venance said numerous continuing students have not being considered for the loan and remain in dilemma.
 
“The government should be transparent in issuing of loans because the money is not given to the students as an offer but as a loan which will later be repaid,” he said.
 
He challenged the 30, 000/- fees charged for every application made by students and asked the loan facility to reconsider the amount to accommodate more applications.
 
HESLB Assistant Director of Communication, Education and Information, Cosmas Mwaisoba said the continuing students who applied for loans for the first time will be treated as are the first year applicants.
 
Students who have received loans so far are 40,836 students and the loan amount is pegged at 155.2bn/-.
Share:

Opposition says no to working with new govt

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Former Chadema presidential candidate Edward Lowassa speaks to journalists in Dar es Salaam yesterday. (Photo: Mpoki Bukuku)
 The Coalition of People’s Constitution (Ukawa) said yesterday said it will not co-operate   with the fifth-phase government under President John Magufuli, citing “electoral fraud”.
 
 
The decision by Ukawa comes ten days after Magufuli was sworn-in the United Republic of Tanzania President following a 58.45 per cent victory against Chadema’s Edward Lowassa who garnered 39.97 per cent.
 
Addressing a press conference in Dar es Salaam yesterday Lowassa explained   the coalition had sufficient evidence to prove how last month’s General Election was marred  by vote rigging. 
 
 Lowassa who was supported by parties forming the Coalition of People’s Constitution (Ukawa) objected the   presidential results which were announced by National Electoral Commission,  Chairman Justice (rtd) Damian Lubuva.
 
The former prime minister, vowed to unmask what transpired during the tallying process anytime from now after getting enough evidence.
 
His statement follows a secret meeting held last Saturday in Dar es Salaam between Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD national leaders and the Zanzibar presidential candidate on CUF ticket Seif Sharif Hamad.
 
Lowassa maintained to keep a low-profile on the revelations about the ruling party’s presidential candidate victory.
 
He further explained the coalition was simply buying time to reveal what happened at the “backstage” of the presidential polls tallying exercise.
 
“We cannot at the moment reveal what had transpired,” and the coalition will not cooperate with the fifth phase government.
 
Lowassa was saddened by the country’s Constitution which bars individuals or institution to challenge the presidential elections results before the courts of law.   
 
“We are asking Tanzanian to keep on protesting the General Election results because there were rigged. No one should demonstrate as leaders were looking for other appropriate actions,” he said.
 
Referring to the Zanzibar general elections, Ukawa demanded the Zanzibar Electoral Commission (ZEC) to declare Civic United Front (CUF) presidential candidate, Maalim Seif Sharif Hamad  the winner of the elections.
 
He said: “How is it possible for one pot to cook legal and illegal things at the same time? If ZEC claims the election results were illegal then the Union results were also not legal because they all came from the same pot.”
Ukawa despite protesting the presidential results said that they would still take part during the National Assembly proceedings scheduled for tomorrow.
 
However Lowassa also called for a new constitution that would ensure free and fair elections in the country.
 
“The new constitution will ensure the country has independent election commission which is responsible to the public, without new constitution the country will continue be under the ruling Chama cha Mapinduzi dictatorship.”
 
Meanwhile Ukawa has called on the government to take immediate action over the mysterious death of former Chadema candidate for Busanda constituency in Geita Region in the recent parliamentary elections, Alfonce Mawazo.
 
NCCR-Mageuzi National chairman, James Mbatia strongly condemned the killing, calling the authority to identify culprits behind the death of Chadema’s Geita regional chairman.
Share:

Lowassa Ataja Sababu 4 Kumpinga Magufuli.....Zifahamu Hapa

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya hali ya kisiasa nchini. Wengine ni Kaimu Mwenyekiti wa Cuf, Twaha Taslima (wa kwanza kushoto), Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Prof. Abdallah Safari (wa pili kushoto) na Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia (wa kwanza kulia). PICHA: MPOKI BUKUKU
Aliyekuwa mgombea urais kupitia  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, ameeleza sababu za kutokubaliana na ushindi uliomuweka madarakani mpinzani wake kupitia CCM, Dk. John Magufuli katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Aidha, amewataka Watanzania kutoyakubali matokeo hayo na kuyapinga kwa nguvu zao zote bila ya kuandamana na kufanya fujo na kwamba umoja huo hautashirikiana na serikali ya Dk. Magufuli kwa madai haikuingia madarakani kihalali. 
 
Lowassa alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa jijini Dar es Salaam jana juu ya hali ya kisiasa nchini na mustakabali wa Zanzibar baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa visiwa hivyo.
 
ATAJA SABABU ZA KUPINGA
Lowassa alisema yeye na wenzake ndani ya Ukawa hawaukubali na ushindi alioupata Dk. Magufuli kwani wana ushahidi wa kutosha juu ya namna Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake kilivyopora ushindi wake (Lowassa) kwa kuyakachakua matokeo.
 
Hata hivyo, Lowassa hakuwa tayari kuuweka wazi ushahidi, akisema atafanya hivyo wakati muafaka ukifikaa ambao pia hakuutaja. 
 
Alitaja sababu nyingine za kutokukubali na ushindi wa Dk. Magufuli kuwa ni, matumizi makubwa ya vyombo vya dola wakati wa uchaguzi. 
 
Alisema wakati wa uchaguzi huo serikali ilitumia nguvu kubwa na vitisho vya askari wenye silaha za kivita ikiwamo kutumia magari yenye maji ya kuwasha yaliyonunuliwa kwa mabilioni ya fedha, ambayo yalikuwa yanarandaranda mitaani, ili matokeo aliyodai ya wizi huo wa kura yakubalike.
 
Sababu nyingine aliyoitoa Lowassa ni hatua ya serikali kupinga maandamano ya Ukawa na kuvitisha vyombo vya habari kufanya kazi zake kwa uhuru.
 
Nyingine alisema ni hatua ya serikali kupiga marufuku mikutano ya kisiasa iliyopangwa  kufanywa na viongozi wa Ukawa na kuwanyima viongozi hao fursa ya kuwashukuru wananchi kwa kuwapigia kura baada ya uchaguzi.
 
 “Wanatumia gharama zote hizo huku bei ya vitu mbalimbali hasa vyakula inapanda kwa kasi kubwa, kama CCM inadai imeshinda kwa nini wana hofu kubwa mpaka kuhujumu uhuru wa vyombo vya habari, kupiga marufuku mikutano ya kisiasa na kunyima viongozi wa Ukawa hata fursa ya kuwashukuru wananchi kwa kutuunga mkono katika safari yetu ya kuleta mabadiliko, hii ni aibu kwa taifa letu,” alisema Lowassa na kuongeza:
 
“Tuna ushahidi wa kutosha jinsi matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano yalivyochakachuliwa na kiasi cha kura zilizoibwa, wakati muafaka tutaweka bayana ushahidi huo ili Watanzania wajue kwa nini Ukawa inasema kwa dhati kwamba haitambui matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) na kwa nini haitashirikiana na serikali ya sasa ambayo ni batili kisheria.”
 
Lowassa alisema endapo Katiba ingekuwa inaruhusu matokeo ya urais kupingwa mahakamani wangefanya hivyo, lakini kwa kuwa hairuhusu wataendelea kutoitambua serikali hiyo, huku akiwataka wananchi kukataa matokeo hayo katika hali ya utulivu wakati Ukawa ikiendelea na harakati nyingine za kisiasa katika nyanja mbalimbali ili kutekeleza azma yao ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini.
 
ZANZIBAR
Aidha, Lowassa alisema Ukawa unamuunga mkono mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi(Cuf), Maalim Self Sharif Hamad, kama mshindi wa uchaguzi mkuu visiwani humo na kuitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) imtangaze mara moja.
 
Alisema kinyume na Tanzania Bara ambako uchaguzi uligubikwa na mizengwe, uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa wazi na wa amani, huku vyama vyote vya siasa na hata waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa walisema uchaguzi huo ulifanyika kwa amani, lakini wanashangaa Zec kufuta uchaguzi huo.
 
Alisema uamuzi huo wa Zec unalaaniwa vikali na Ukawa na kwamba uamuzi wa kutaka uchaguzi huo urudiwe  hawakubaliani nao kwa kile alichosema  hizo ni mbinu mpya ambazo zimepangwa kuhujumu uchaguzi huo na una lengo  la kuhatarisha  amani na utulivu visiwani humo. 
 
“Wakuu wa Ukawa walikataa dhana kuwa uchaguzi uleule unaodaiwa kufutwa kwa kuwa ulikuwa na mizengwe, ulizaa matokeo halali ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya urais wa Jamhuri, lakini ni batili kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Rais wa Zanzibar, dhana hii haina mantiki yeyote bali ni ubabe wa kisiasa,” alisema Lowassa na kuongeza:
 
“Haiwezekani chungu kimoja kikapika halali na haramu kwa pamoja. Kigezo cha Zec kuwa uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa batili, basi matokeo yake yote ikiwa ni pamoja na yale ya urais wa Jamhuri pia ni batili. Hii ina maana kuwa hata ushindi unaodaiwa wa Dk. Magufuli, mbali ya kuwa ni matokeo haramu ya wizi kwa kura za Tanzania Bara, pia ni batili kisheria kwani hana ridhaa ya watu wa pande zote mbili za Muungano.”
 
KATIBA MPYA
Lowassa alisema bado wataendelea kupigania kuandikwa kwa Katiba mpya ambayo watahakikisha inazingatia maoni na matakwa ya Watanzania.
 
Alisema pasipo Katiba hiyo, matatizo mengi yanayojitokeza hivi sasa hayatapatiwa ufumbuzi  ikiwamo kuwa na tume huru ya uchaguzi na serikali inayowajibika, huku akisisitiza kuwa katika mazingira ya sasa na chini ya Katiba inayotumika sasa, Tanzania haitakuwa na demokrasia na itaendelea kuwa nchi inayotawaliwa kwa mizengwe na udikiteta .
 
AELEZA HATMA YAKE 
Lowassa alisema hatarudi nyuma wala kustaafu siasa, bali ataendelea kuimarika katika nyanja hiyo kwa kuwa mstari wa mbele kupigania Ukawa na mabadiliko.
 
MBATIA
Kwa upande wake, Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia, alisema vurugu zinazoendelea hivi sasa na mauaji ya Watanzania  katika matukio tofauti na matumizi ya mabavu, itafika mahali Watanzania watakosa uvumilifu na endapo machafuko yakitokea Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete  pamoja na Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva, wote watafikishwa katika mahakama za kimataifa.
 
Mbatia  alidai Kikwete atawajibika pamoja na mambo mengine kwa kutumia nguvu kubwa kununua vifaa vya kivita vyenye thamani ya Sh. bilioni 409 katika uchaguzi wa mwaka huu, huku akimtaja Jaji Lubuva kwamba atawajibika kwa kukiuka sheria za uchaguzi kwa kuibeba CCM na Mkapa atawajibika kwa kusababisha mauaji katika uchaguzi Mkuu 2001, Zanzibar.
 
Akizungumzia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo, aliyeuawa juzi kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana, Mbatia alihusisha kifo chake na mauaji mengine ambayo yamekuwa yakihusishwa na chuki za kisiasa.
 
Lowassa aliungana na Mbatia kulaani mauaji hayo na kulitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa haraka ili kubaini waliohusika na kuwachukulia hatua.
 
MALALAMIKO VITI MAALUM
Akizungumzia malalamiko kutoka maeneo mbalimbali nchini kuhusu mgawanyo wa viti maalum kwenye nafasi ya ubunge ndani ya Chadema, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Abdallah Safari, alisema Chadema imepokea malalamiko mengi kuhusiana na mgawanyo wa wabunge wa vitihivyo na kwamba kinayafanyia kazi na yale ya msingi yatafanyiwa uamuzi na yasiyo ya msingi yataachwa.
 
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (Cuf), Twaha Taslima, alisema masuala ya wabunge wa viti maalum yanazungumzwa ndani ya chama na si katika vyombo vya habari.
 
Katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu, Nec ilimtangaza Dk. Magufuli wa CCM kuwa mshindi wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano kwa kupata  asilimia 58.46 ya kura halali zilizopigwa, huku Lowassa akipata asilimia 39.97.
 
CHANZO: NIPASHE
Share:

CHADEMA Watangaza hali hatari,Ni mauaji ya MAWAZO sasa vijana wote waagizwa kuelekea mwanza

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Katibu wa uenezi wa Baraza hilo la vijana BAVICHA Taifa Bwana EDWARD SIMBEYE akizungumza na wanahabari mapema leo juu ya hali ya mauaji ya mwenyekiti wa chama hicho mkoani Geita ALPHONCE MAWAZO na hatua ambazo watazichukua
 Na Exaud Msaka Habari
Baraza la vijana la chama cha  Demkocrasia na maendeleo chadema BAVICHA wametoa siku tatu kwa jeshi la polisi nchini kumwachia Mwenyekiti wa baraza hilo PATROBAS KATAMBI aliyekamatwa jana mkaoni mwanza pamoja na kuwakamata wahusika wote waliohusika na kifo cha Mwenyekiti cha CHADEMA mkoani GEITA Bwana ALPHONCE MAWAZO huku wakisema kuwa kama hayo hayatafanyika watalazimika kulipa kisasi.

Akizungumjza na wanahabari mchana wa leo jijini Dar es salaam katibu wa uenezi wa baraza hilo Taifa Bwana EDWARD SIMBEYE amesema kuwa kwa sasa vijana na wanachama wa chadema wamechoka na mauaji ya  viongozi wa chama hicho huku kukiwa hakuna hatua zinazochukuliwa kwa wahusika hivyo sasa wameamua kuhakikisha kuwa wanajilinda wenyewe ikiwa ni pamoja na kuwatafuta wahusika wa tukio la Geita na kuwakamata kama polisi watakuwa wameshindwa kufanya hivyo kwa muda muafaka..
BEN SAANANE ambaye ni mkuu wa Idara ya sera na utafiti wa chadema akionyesha baadhi ya picha za mauaji ya viongozi wa Chama hicho yaliyowahi kufanyika na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa hadi sasa jambo ambalo sasa wamesema wamechoka na wameamua kujilinda wenyewe kwa kuhakikisha kuwa wanawakamata wale wote walioendesha tukio la GEITA
Akizungumzia tukio la jana mkoani mwanza amesema kuwa wakati jana mwili wa marehemu MAWAZO ukiwasili katika hospitali ya BUGANDO kwa ajili ya kuhifadhiwa na kufanyiwa uchunguzi zaidi Polisi walipanga njama za kuutorosha mwili wa marehemu kwa ajili ya kwenda kuuzika kimya kimya jambo ambalo amesema wanachama na viongozi wa CHADEMA walishtuka na kuamua kulinda mwili huo na ndipo ilipotokea vurugu iliyopelekea kiongozi wa vijana taifa kukamatwa na polisi bila sababu yoyote ya msingi.

Amesema kuwa inashangaza kuona  jeshi la polisi likiwa katika mstari wambele kuhangaika juu ya mwili wa Marehemu ALPHONCE MAWAZO wakati iko wazi kuwa wakati anauawa na wananchi polisi walikuwepo eneo la tukio na kushindwa kutoa hata msaada wa gari kwa ajili ya kumpeleka hospitalini lakini jana polisi walipata gari la kuja kumtorosha katika hospitali hiyo jambo ambalo amesema limekuwa likifanywa na polisi kila mara yanapotokea matukio ya mauaji kana haya.
Kiongozi huyo amesema ni lazima jeshi la polisi sasa waeleze ukweli kama sio wao na serikali ya CCM wanaohusika na mauaji ya viongozi wa chadema Basi waweke wazi ni nani hasa anayefanya unyama huo juu ya Democrasia ya Tanzania.


Aidha katika hatua nyingine vijana hao wametangaza rasmi kuwa baada ya siku tatu na polisi kushindwa kuwaachia huru viongozi wao na kuwakamata wauaji wa MAWAZO wamewaagiza vijana wote wa Tanzania kukusanyika kwa wingi mkaoni mwanza kwa ajili ya kushinikiza kuwaachia viongozi wao pamoja na kulinda mwili wa marehemu ALPHONCE MAWAZO ambao umelazwa katika hospitali ya Bugando mkoani mwanza.

Marehemu ALPHONCE MAWAZO aliuawa na wananchi mkoani GEITA baada ya kushambuliwa na wananchi waliokuwa na sialaha za jadi ambao hadi sasa hakuna taarifa rasmi inayoeleza hali halisi ya mauaji hayo.
Share:

CCM YAMPITISHA JOB NDUGAI KUGOMBEA NAFASI YA USPIKA WA BUNGE.

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mh. Job Ndugai ameteuliwa kuwa mgombea rasmi wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM).

Wabunge wateule wa CCM wamempitisha Job Ndugai kuwania uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya wenzake wawili kujitoa.
Via>>EATV
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger