Saturday 26 April 2014

MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR WATIMIZA MIAKA 50


Waasisi wa Muungano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (kushoto) na Hayati,  Abeid Aman Karume (kulia waliokaa) wakisaini nyaraka za Muungano mwaka 1964.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akichanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar, huku akishuhudiwa na Rais wa Zanzibar, Abeid Aman Karume, (wa tatu kushoto) na Mhe. Rashind Mfaume Kawawa (wa kwanza kulia) wakati wa sherehe za kwanza za Muungano zilizofanyika Tarehe 26 Aprili, 1964.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (kushoto) na  Sheikh Abeid Amani Karume (kulia) wakibadilishana Hati za Muungano wa Tanganyika na  Zanzibar Aprili, 1964.
Waasisi wa Muungano, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (kushoto) na Hayati Abeid Aman Karume.
Share:

TAZAMA PICHA ZA HALFA YA KUMUAGA MZEE MSUYA BAADA YA KUSTAAFU SIASA,SHEREHE ZILIZOONGOZWA NA RAIS KIKWETE



Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiwa viongozi wengine wakuu wa serikali chama cha Mapinduzi CCM, akiwemo Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana (kushoto) katika hafla ya kumuaga aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania mara mbili katika awamu mbili tofauti, Mzee Cleopa David Msuya (wa kwanza kulia kwa Rais) ambaye amestaafu rasmi siasa baada ya kuitumikia kwa zaidi ya miaka 33.


Katibu wa CCM, wilaya ya Mwanga, akisoma historia fupi ya Mzee Msuya kabla na baada ya kujiunga na siasa


Baadhi ya Wananchi waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika katika Ofisi za CCM wilaya ya Mwanga leo

Mjumbe wa Halmashauri kuu wa CCM wilaya ya Mwanga, Joseph Thadayo akitoa salamu za marafiki na wasomi waishio nje ya Mwanga, ikiwemo salamu za Mwanasiasa maarufu na mdhamini wa CCM, Mzee Peter Kisumo ambaye aliwahi kufanya kazi pamoja na mzee Msuya katika Siasa.

Mzee Msuya akitoa pongezi zake kabla ya kuaga rasmi.

Kundi la wazee wa kimila wakiongozwa na Mzee Kasim Msemo wakimkaribisha Mzee Msuya kijijini


Mzee Msuya akiwa amekaa kwenye kiti cha jadi kama ishara ya kurudi rasmi kijijini baada kutangaza kustaafu siasa

Rais Kikwete akizungumza na wananchi katika hafla ya kumuaga Mzee Msuya katika ulingo wa siasa, uliofanyika leo katika ofisi za CCM wilaya ya Mwanga.





Mamia ya Wananchi waliokusanyika kushuhudia hafla hiyo

Share:

WATU ZAIDI YA 31 WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA BASI KILIMANJARO



Picha ya chini na juu ni baadhi ya majeruhi walikuwa kwenye basi hilo aina ya Urio lililopata ajali leo jioni katika eneo la Kia wilayani Hai mkoani Kilimanjaro



wananchi wawakiwa wanashuhudia ajali hiyo iliotokea leo jioni katika eneo la kia ambapo inasemekana watu zaidi ya 31 wamejeruliwa

Basi aina ya Urio yenye namba za usajili T 137 BCX inayofanya safari zake moshi kuelekea leguruki mkoani Arusha leo limepinduka katika eneo la kia na kujeruhi watu zaidi ya 31

kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo katika eneo la tukio walisema kuwa dereva huyo alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki iliyokuwa imejichomeka barabarani

"dereva huyu alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki ndipo gari ikamshinda na kuama barabara ndipo ilipo anguka gafla na kubiringita mara tatu apa yenyewe unavyoiyona tumeigeza ilikuwa kichwa chini matairi juu"alisema mmoja wapo wa shuhuda ambaye akutaka kutaja jina

mpaka kamera ya libeneke la kaskazini inaondoka eneo la tukio watu 31 walikuwa wamekwishwa pelekwa katika hospitali ya wilaya ya hai kwa ajili ya matibabu wakiwemo wanafunzi wa shule ya leguruki ambao walikuwa wanarejea shuleni mara baada ya kumaliza likizo yao ya sikukuu ya pasaka
Share:

SUNGUSUNGU LAWAMANI GEITA, WAMKAMATA MWANAMKE ALIYEVAA NGUO FUPI WAKAANZA KUMPAPASA MAKALIO KISHA KUMCHARAZA BAKORA


 
(picha ya maktaba)
****

Askari wa jadi maarufu kama sungusungu wa mtaa wa Mwatulole kata ya Kalangalala mjini Geita wanadaiwa kumdhalilisha na kumfanya ukatili mwanamke mmoja kwa kumkamata na kumcharaza viboko kwa tuhuma za kuvaa nguo fupi (kimini).
Inadaiwa kuwa walichukua uamuzi huo baada ya kamanda wao kuwaamuru na kutangaza sheria binafsi ya kuzuia watu kuvaa vimini kwenye mtaa huo.

Akizungumzia kwa masitikiko mwanamke huyo, Jennifa Nobo (24) alidai kuwa alishambuliwa na sungusungu hao katika mtaa huo wakati amekwenda sokoni.
Jeniffa alisema kuwa alipokwenda sokoni hapo kununua mahitaji ya nyumbani kwake, alikutana na sungusungu hao wakiwa wameongoza na kamanda wao huyo, Daud Kulola.


Alidai baada ya kukutana nao, walimkamata, kumpapasa maungoni wa kumhoji sababu za kuvaa kimini ndani na juu khanga wakati kiongozi wao amepiga marufuku kuvaa mavazi hayo katika mtaa huo.
Jeniffer alidai bila kusikilizwa utetezi wake, sungusungu hao walianza kumcharaza viboko hadharani na kumfuata kila alikokuwa akimbilia.
Alidai wakati wakicharaza viboko walimbakiza na kimini hicho. Aliendendelea kudai kuwa kamanda huyo alipochoka kumuadhibu, alimrejeshea khanga yake.


''Nlilipita kila kona akanifuata na kunicharaza kwa fimbo nililia sana na kutokwa na haja ndogo kwa hofu na kipigo ..kilikuwa kitendo cha kinyama ambacho sijawahi kutendewa katika maisha yanguna, sitakisahau, ''alidai..
Baadhi ya wakazi wa mtaa huo walidai kuwa siku moja kabla ya tukio hilo la ukatili, Kamanda huyo alisikiska akitumia kipaza sauti akitangaza kuwa vijana na wasichana wote wake kwa waume wanaovaa vimini ni marufuku kuonekana mtaani.

Walidai wengi wao walidhani huenda lilikuwa ni agizo la Serikali.
Baada ya tukio hilo Jeniffa alikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi cha Geita kufunguliwa jalada GE/RB/2033/ 2014 la shambulio la kudhuru mwili kisha kupatia PF3 kwa ajili ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Geita.
Alisema baadaye polisi walimkamata kamanda huyo wa sungusungu na kuachiwa kwa dhamana na kwamba uchunguzi dhidi yake unaendelea.
Kamanda huyo alikataa kuzungumzia madai hayo dhidi yake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa huo, Kalori Malicery amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kukataa kuzungumzia kwa undani kwa madai limeripotiwa polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph Konyo alionyesha kusikitishwa na tukio hilo na kuahidi kuzungumzia leo ofisini kwake.
Konyo alisema kuwa iwapo ushahidi utathibitika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani.
Share:

UCHUNGUZI UMEBAINI WANAWAKE WOTE WENYE MAKALIO MAKUBWA WANAONGOZA KUWA NA NYODO KISA MAKALIO YAO.. ANGALIA HAPA UONE..!






Share:

ONA UNAFIKI WA MOHAMED RAZA ALIVYOKUWA ANADAI SEREKALI TATU AKIWA ZANZIBAR


Wakuu.

Akiwa Zanzibar Mohamedi Raza alitokwa na povu la kudai serikali tatu na kusisitiza peoples power, lakini baada ya kufika Dodoma akaufyata! Wakati huo huo, gazeti la leo la Nipashe Uk 3 limemnukuu Mohamedi Raza akisema kuwa "...Njaa ndio iliyolazimisha Zanzibar kujiunga na jumuiya ya kitaifa ya kiislamu mapema miaka ya tisini...". Kwa maana hiyo aliyo yasema akiwa Zanzibar na kwenda kubadirisha msimamo baada ya kufika Dodoma nayo tuyape tafsri gani?

Bofya <HAPA >kuona Video ulivyokuwa anatetea Serekali tatu kabla ya Kuja Dodoma
Share:

VIDEO:MFANYAKAZI WA NDANI ANASWA NA KAMERA AKIJICHUA MBELE YA MTOTO MDOGO


KTN wameripoti na kuanika uchafu unaotendwa na wafanyakazi wa ndani...
Read More »
Share:

INASIKITISHA SANA: TAZAMA TUKIO LA KUAGWA KWA MWANAFUNZI ANASTAZIA LACKFORD ANAYEDAIWA KUUNGUZWA NA KUPEWA SUMU NA BABA YAKE ULIVYOAGWA SHULENI KWAO MWANZA SEKONDARI


 
Marehemu Anastazia Lackford Magafu enzi za uhai.

Wanafunzi wenzake wakisubiri kuuaga mwili wa marehemu Anastazia Lackford Magafu aliyefariki baada ya kudaiwa kuchomwa moto na baba yake kisha kupewa juisi yenye sumu.
Mwili wa Anastazia Lackford Magafu wakati ukiagwa katika Shule ya Sekondari Mwanza.

Mwili wa marehemu Anastazia Lackford Magafu juzi uliagwa katika Shule ya Sekondari Mwanza alipokuwa akisoma enzi za uhai wake.

Inadaiwa kuwa kifo cha marehemu Anastazia kimesababishwa na sumu iliyowekwa kwenye juisi aliyopelekewa na baba yake, Lackford Magafu maarufu kwa jina la DJ Lackford, wakati akiwa amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) akitibiwa majereha ya moto.
Tukio la kifo hicho liliotokea Aprili 16 mwaka huu, ikiwa ni muda mfupi baada ya kunywa juisi inayodaiwa kuwa na sumu, hivyo kuzua utata wa chanzo cha kifo hicho
Share:

Friday 25 April 2014

TITO VILANOVA AFARIKI DUNIA



hqdefault_744f4.jpg
photo_f8ce8.jpg
Kocha wa zamani wa timu ya Barcelona Tito Vilanova amefariki dunia usiku huu akiwa hospitarini alipokuwa amerazwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani ya koo
Share:

AUNTY LULU ACHEZEA KICHAPO

MSANII wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ hivi karibuni alijikuta akichezea kichapo kutoka kwa mpenzi wake anayejulikana kwa jina la Amani baada ya kutaka kwenda klabu usiku bila kumtaarifu.
Msanii wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ akipozi.
Kwa mujibu wa majirani, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo walimsikia msanii huyo akipiga mayowe na walipotoka walimuona akipigwa.
“Kwa kweli alipigwa sana na sasa amevimba uso,” alidai mmoja wa majirani aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Paparazi wetu alimtafuta Aunty Lulu lakini hawakuweza kuonana naye kwani aligoma akidai kwa hali aliyonayo hawezi kuonana na waandishi ila akasema:
“Ni kweli Amani kanipiga, kaniumiza ila siwezi kuliongelea sana suala hilo, haya ni mambo yetu binafsi.”

Share:

SNURA AGANDWA NA MAHABA NIUE

STAA wa wimbo wa Majanga, Snura Mushi anaonekana kugandwa na mahaba niue baada ya hivi karibuni kuanika hisia zake na kuonesha dhahiri kuwa amezama vilivyo kwenye penzi motomoto la jamaa yake aitwaye Hunter Sleiyum.
Staa wa wimbo wa Majanga, Snura Mushi akiwa kwenye mahaba mazito na boyfriend wake aitwaye Hunter Sleiyum.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Snura aliwataka wanaume wakware waache kumsumbua kwa sababu amempata mwanaume sahihi maishani mwake, anafurahia mapenzi na uzuri zaidi mpenzi wake anampenda yeye pamoja na mwanaye.
Snura Mushi akiwa na Hunter Sleiyum.
“Hata kuamua kufanya kazi hii ya kunengua majukwaani ni kwa sababu nilikwepa mambo ya kujiuza kwa wanaume, kazi hiyo siiwezi kabisa, niko tofauti na wengine wanaokubali kujiuza na kutothamini miili yao,” alisema Snura.
Mbali na kumzungumzia mpenzi wake huyo ambaye ni DJ wa Maisha Club, Snura alikanusha kuhusu taarifa za kutajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mchezaji wa Yanga, Mrisho Ngasa.
“Huwezi kuamini, Ngasa hajawahi kutoka na mimi, alikuwa ni mshkaji tu,” alisema Snura.

Share:

WEMA:NAJUUUUUUUTA KUMPLIPIA KAJALA MIL.13


KAMA kuna kitu kinakukwaza ndani ya moyo wako, siku zote ukikaa nacho kitazidi kukuumiza lakini ukiamua kumtafuta mtu ambaye umeshibana naye na kumsimulia, moja kwa moja utakuwa umeutua mzigo!
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akiwa Kajala Masanja.
Hicho ndicho amekifanya Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kwa kuweka kweupe chanzo cha ugomvi wake na staa mwenzake, Kajala Masanja huku akijuta kumlipia mwanadada huyo zile Sh. milioni 13 za faini ili asiende jela miaka saba.
Akizungumza na Ijumaa katika exclusive interview Jumanne iliyopita, Wema ambaye pia ni staa mkubwa wa sinema za Kibongoalisema kuwa kuna mambo mazito ambayo yamesababisha yeye kuingia kwenye gogoro kubwa na Kajala.Wema au Beautiful Onyinye alisema kwamba mambo hayo ndiyo yamemsababishia maumivu ya moyo na kutokwa machozi kila wakati.
“Leo (anataja jina la mwandishi), ngoja nikuelezee kila kitu kinachohusiana na mimi na Kajala juu ya tofauti zetu.“Naamini baada ya kusimulia kisa na mkasa nitakuwa nimeutua huu mzigo mkubwa nilionao ndani ya moyo wangu.
“Baada ya hapo sitapenda tena kuzungumzia ishu inayonihusu mimi na Kajala,” alianza kufunguka Wema.
UZINDUZI WA KIGODORO
Katika maelezo yake, cha kwanza, Wema ni uzinduzi wa Filamu ya Kigodoro uliofanyika hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar ambapo yeye alisema kuwa alianza kuyaamini yale yaliyokuwa yakisemwa na watu kuhusiana na Kajala.
Wema alisema kabla ya tukio, akiwa saluni akijiandaa kwa ajili ya uzinduzi huo, ghafla Kajala alimharibia ‘mudi’. “Unajua ile Saluni ya (anataja jina la saluni) pale Kinondoni, ina sehemu mbili, juu na chini, sasa mimi nilikuwa juu na Aunt (Ezekiel) tunatengeneza nywele.
“Niliposhuka kwa ajili ya kuosha nywele, nikamuona Kajala, kwa kuwa nilikuwa sijaonana naye siku nyingi na tayari maneno yalishaanza kuwa mimi na Kajala tuna bifu, nikaona nioneshe kuwa sina bifu naye.
“Kweli nilipiga makelele ya furaha nilivyomuona K, nikawa nakimbia kwenda kumkumbatia, kiukweli niliishiwa nguvu baada ya kunikwepa na kusema nooo...Wema usinikumbatie na kuanza kutoa maneno ya dharau eti nitamchafua.
“Kusema kweli niliishiwa nguvu na kuona kama vile kizunguzungu huku aibu ikinijaa ghafla kwani pale kulikuwa na watu wengi, basi huwezi kuamini, nilishindwa kujizuia nikajikuta namtukana, sikumbakisha.
“Wakati namtukana alikuwa amekaa kwenye kiti cha kuoshwa, nikaenda nikamsukuma na kumfukuza pale kwenye kiti ili nikae nioshwe, huwezi amini hali ya hewa iliharibika ghafla kwani sikuwa na mudi tena,” alitiririka Wema.
SAFARI YA ARUSHA KATIKA SHOO YA MIRROW
Wema alisema kuwa baada ya kutofautiana pale saluni, hakuwa na kinyongo, safari ya Arusha ilipofika walikwenda kumsapoti msanii wao wa Bongo Fleva anayesimamiwa na Kampuni ya Endles Fame Production.
Wakiwa njiani, kwa mujibu wa Wema, yeye alikuwa hana fedha taslimu za kutosha zaidi ya kubeba kadi zake saba za ATM tofauti hivyo alimwambia Kajala ampe shilingi laki tatu kwa ajili ya watu kula na kunywa njiani pamoja na matumizi madogomadogo.
Alisema Kajala hakuwa na shilingi laki tatu akampa shilingi laki mbili na elfu themanini.
Aliendelea kutoa ya moyoni: “Tulipofika Arusha Kajala alimwita ndugu yake mmoja anayeitwa Doli kisha akamwambia achukue fedha alizokuwa nazo akamuwekee benki kwa sababu sikuwa na fedha na nilianza kukopa eti nilijishaua kuandaa shoo nikitegemea fedha zake.
“Wakati K anazungumza hivyo kulikuwa na watu watatu, mimi sina hili wala lile nikamuuliza mtu mmoja mbona siwaoni, wamekwenda wapi?
“Ndipo nikafungukiwa kuwa wananikimbia kisa nimemkopa K hizo laki mbili na elfu themanini, kiukweli iliniuma sana, Kanalalamikia laki mbili? Tena hakunipa bali alinikopesha?
“Nilijiuliza amesahau mimi nilitoa Sh. milioni 13 kumlipia faini asiende jela miaka saba? Nguo nikinunua nanunua sare, nywele sare, viatu sare, mapochi sare, ninachokula na kunywa mimi ndicho hichohicho.
“Siku zote wakati akiwa gerezani nguo, viatu, hereni yaani kila kitu nilikuwa ni mimi, leo laki mbili na elfu themanini, niliyomuazima ananitangazia kwa watu (anataja jina la mwandishi)?
“Iliniuma sana basi palepale, nikaenda benki nikatoa Sh. milioni mbili, nikamlipa fedha zake, nikakaa kimya nikijifanya sijui chochote kinachoendelea kwani ningefanya chochote ningeharibu shoo na isingekuwa na maana yoyote ya sisi kwenda Arusha.”
WAREJEA DAR, MAANDALIZI YA FILAMU YAKE YAANZA
Wema alisema waliporejea Dar, alimwambia Kajala kuwa kuna mtu aliyekuwa amempa stori hivyo alimuomba wafanye filamu wawili.
Alisema kwamba Kajala alikubali na kusema kuwa atachangia Sh. milioni tano katika bajeti ya filamu hiyo.Baada ya kusikia hivyo, Wema alisema alifarijika, alipokwenda kumweleza ‘bebi’ wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, naye Diamond akasema atatoa Sh. milioni tano hivyo jumla itakuwa Sh. milioni kumi ikapita bajeti iliyokuwa imepangwa ya Sh.milioni nane.
Anaendelea: “Tukiwa katika maandalizi ya mwisho tuanze ku-shoot, K alinipigia simu akaniambia hawezi ku-shoot kwani alikuwa na safari ya kwenda China labda wa-shoot vipande vyake, nikamwambia basi aende akirudi tutatengeneza nyingine.
“Baada ya kuona hivyo ndipo nikamchukua Aunt tutengeneze filamu. K alipoona nimemchukua Aunt, akanipigia simu na kuanza kuongea shiti.“Nilijiuliza mbona mwenzangu amesahau ghafla wema wangu niliomtendea au kwa kuwa tangu aanze vijisafari vyake vya kwenda China anapata

Share:

WANAVIJIJI MBEYA WALAUMIANA UDHIBITI MIMBA KWA WANAFUNZI‏

Baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Usoha Njiapanda, Wilaya ya Mbeya Vijijini wakizungumza katika mkutano na mwandishi wa habari hizi juu ya changamoto anuai za huduma za kijamii kijijini hapo.
Baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Usoha Njiapanda, Wilaya ya Mbeya Vijijini wakizungumza katika mkutano na mwandishi wa habari hizi juu ya changamoto anuai za huduma za kijamii kijijini hapo.Mwenyekiti wa Kijiji cha Usoha Njiapanda, Willson Mwamunyila (katikati) pamoja na wanakijiji wenzake wakizungumza na mwandishi wa habari hizi. Mwenyekiti wa Kijiji cha Usoha Njiapanda, Willson Mwamunyila (katikati) pamoja na wanakijiji wenzake wakizungumza na mwandishi wa habari hizi. Mratibu wa Elimu Kata ya Tembela, Antony Mwaikwila akizungumza na mwandishi wa habari hizi. Mratibu wa Elimu Kata ya Tembela, Antony Mwaikwila akizungumza na mwandishi wa habari hizi.
WANAVIJIJI wa vijiji vya Shibolya, Usoha Njiapanda, Simambwe, Ikhoho na Ilembo Usafwa vyote vya wilayani Mbeya Vijijini wametupiana lawama kuhusiana na baadhi ya wazazi na viongozi wa vijiji kuwa wakifumbia macho watu wanaotuhumiwa kuwatia mimba wanafunzi wa msingi na sekondari na kuwakatisha masomo.
Kauli hiyo imetolewa juzi na baadhi ya wanakijiji walipokuwa wakifanya mazungumzo na mwandishi wa habari hizi Wilaya ya Mbeya Vijijini kwa vyakati tofauti alipotembelea vijiji hivyo kuangalia changamoto za elimu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wanavijiji walisema idadi kubwa ya wanafunzi wanaotiwa mimba na kukatishwa masomo ya shule za msingi na sekondari wamekuwa wakirudi vijijini na kulea watoto huku kukiwa hakuna hatua zozote za kisheria zinazochukuliwa kwa wanaotuhumiwa kuwatia mimba.
Greyson Ngolia wa Kijiji cha Shibolya alisema katika kijiji hicho wapo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambao wanalea watoto wao baada ya kutiwa mimba na kukatiswa masomo yao.
“…Hapa kijijini tunao hadi wanafunzi wa shule za msingi ambao wametiwa mimba na kukatishwa masomo, wanalea watoto wao nyumbani hakuna hatua zozote zinazochukuliwa iwe kwa mzazi wala waliowatia mimba na wengine wapo hapa hapa,” alisema Ngolia.
Eliud Mwakilasa mkazi wa Kijiji cha Usoha Njiapanda alisema katika kijiji hicho hakuna hatua zinazochukuliwa kwa wanafunzi wanaopata mimba kuanzia kwa viongozi wa kijiji, wazazi na wala uongozi wa shule husika anaposoma mtoto.
Naye Maria Kolneri wa Kijiji cha Usoha Njiapanda alisema katika kijiji hicho hakuna utamaduni wa kuwashtaki watu wanaotuhumiwa kuwatia mimba wanafunzi na suala hilo linaogopwa na kila mmoja kwa kile kuhofia kutengwa.
“…Hapa kijijini hakuna utaratibu huo wa kuwashtaki waliowatia mimba wanafunzi watu wanaogopa kulaumiwa kuanzia viongozi wa kijiji na hata wazazi wa mtoto anayekuwa ametiwa mimba, kiujumla tunaogopana,” alisema Bi. Kolneri.
Faustina Nafasi toka Kijiji cha Simambwe alisema idadi kubwa ya wanafunzi wanaopata mimba usababishwa na umbali wa shule wanazosoma, ambapo baadhi yao wamelazimika kupanga kwenye vyumba karibu na shule (yaani mageto) jambo ambalo linachangia idadi kubwa kurubuniwa kwa kukosa uangalizi wa karibu toka kwa wazazi/walezi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Usoha Njiapanda, Willson Mwamunyila alikiri kuwepo na matukio ya kesi za mimba kwa wanafunzi katika eneo lake na vijiji vinavyomzunguka lakini alisema hali ya kushindwa kuwashughulikia wanaowatia mimba wanafunzi huchangiwa na ushirikiano mdogo toka kwa wazazi wa watoto.
“…Unakuta umeletea taarifa ya mimba kwa mwanafunzi toka shuleni, ukienda kwa mzazi anasema hajui aliyemtia mimba mwanaye na vile vile mtoto anasema aliyempa mimba hamjui sasa mazingira kama hayo mnashindwa pa kuanzia, maana hakuna ushirikiano…wawazi na wanafunzi binafsi ndio nawaona kikwazo,” alisema Mwamunyila.
Kwa upande wake Mratibu wa Elimu Kata ya Tembela, Antony Mwaikwila alikiri uwepo wa matukio ya mimba katika shule anazozisimamia na takwimu zimekuwa zikitofautia kila mwaka, licha ya kesi nyingi kushindwa kushughulikiwa kwa kile kukosa ushirikiano.
Alisema kesi nyingi hata zikifika polisi huishia kituoni maana wanafunzi wengi wanaotiwa mimba hudai hawawajui waliowapa mimba hivyo kukosa ushahidi. “…Mfano mwaka 2013 Shule ya Sekondari Shibolya tulipata taarifa ya mimba tatu lakini watoto walipinga kuwa hawawajui waliowapa mimba hivyo kesi kuishia njiani, zipo kesi zinafunguliwa lakini zinaishia njiani kwa kukosa ushahidi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger