Saturday, 29 July 2023

Tazama Picha : MWENGE WA UHURU UKITOKA SHINYANGA MJINI

Tazama picha Mwenge wa Uhuru ukitoka Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwenda Halmashauri ya Shinyanga leo Jumamosi Julai 29,2023 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

MBUNGE JASON RWEIKIZA ATAKA WATANZANIA WAJIANDAE KUCHANGAMKIA BIMA YA AFYA KWA WOTE

Na Mariam Kagenda _ Kagera
Mbunge wa jimbo la Bukoba Vijijini Jason Rweikiza amewataka wananchi kujiandaa kwa ajili ya kuchangamkia bima ya afya kwa wote itakapoanza.

Dkt Rweikiza ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Buhendangabo baada ya diwani wa kata hiyo Teophily Elieza kutoa kero kwa mbunge kwa niaba ya wananchi.

Amesema   kuwa bima ya afya inasaidia pale unapoumwa wakati hauna pesa ya matibabu kwani itakuwezesha kupata matibabu

Katika hatua nyingine amewasisitiza wananchi kuendelea kuchangamkia mbolea ya Ruzuku ambayo serikali ilichangia fedha ili wakulima waipate kwa bei nafuuu.

Kuhusu ujenzi wa jengo la mama na mtoto (Kliniki) Rushaka Dkt Rweikiza amebainisha kuwa atawaongezea mchango wa shilingi milioni tano ambapo  mapema mwaka huu alitoa mchango wake ili ujenzi  uweze kuanza.

Amesisitiza kuwa daraja la Mishambwa ambalo ujenzi wake umegharimu shilingi milioni 90 likikamilika ,Barabara yake itajengwa na TARURA  kutoka Kashozi hadi  Rushaka ili wananchi waweze kupita kwa urahisi.

Aidha amechangia shilingi laki nne  kwa shule ya sekondari Kalema na shilingi laki tatu kwa  shule ya msingi Rushaka B kwa ajiili ya lishe ya wananfunzi shuleni na mipira miwili kila shule huku akitoa mipira kwa timu za vijana kwa ajili ya kujiandaa na ligi ya Rweikiza Cup 2023
Share:

WAZIRI MKENDA:TURUDISHE HUDUMA ZA MAKTABA KATIKA NGAZI ZA WILAYA NA TARAFA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akisoma  kitabu mara baada ya kutembelea Maktaba ya Taifa  jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameutaka uongozi wa Bodi ya Huduma za Maktaba kutoendelea na ujenzi wa majengo na badala yake wajikite katika ununuzi vitabu mbalimbali vya maktaba.

Prof. Mkenda ametoa agizo hilo Julai 28, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Menejimenti na watumishi wa bodi hiyo ambapo amesema kazi ya bodi hiyo ni kuhakikisha kunakuwa na maktaba zenye vitabu vya kutosha ambavyo vitawezesha watanzania kupata maarifa.

Waziri huyo ameongeza kuwa badala ya bodi hiyo kuwekeza fedha nying kwenye masuala ya ujenzi wa majengo fedha hizo zielekezwe katika kununua vitabu na kuvisambaza katika maktaba nchini ili kuwapa fursa watanzania kujisomea.

" Jukumu la kipaumbele kwenu si majengo, kazi yenu kubwa ni kuhakikisha maktaba zinakuwepo na mnanunua vitabu na vya maktaba hizo ili kutoa fursa kwa wananchi kujisomea" amesisitiza Kiongozi huyo.

Prof. Mkenda amefafanua kuwa Bodi hiyo inaweza kutafuta maeneo katika taasisi zikiwemo shule, vyuo vya maendeleo ya wananchi ama VETA vikatumika kama maktaba ambazo zitakuwa karibu na jamiii.

Ametolea mfano kwamba katika miaka ya nyuma kulikuwa na maktaba ambazo zilisambaa mpaka katika ngazi za tarafa na wala hakukuwa na majengo ya maktaba lakini wananchi waliweza kusoma na kuazima vitabu

" Mimi ni mnufaika wa maktaba hizi nimezaliwa kijijini na kusomea huko lakini kulikuwa na maktaba ambazo tulizitumia kuazima vitabu na kujisomea lakini leo hakuna maktaba kama hizo embu turudi huko, leo tunaongelea maktaba tatu tu za tarafa hapana tujitafakari" amesema Waziri huyo

Mkenda amewataka kuhakikisha Maktaba zinakuwa na vitabu mbalimbali vivyoandijwa na Watanzania waliopo nchini na nje ya nchi vikiwemo vitabu vilivyoandikwa na viongozi mbalimbali.

Mkurugrenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Dkt. Mboni Ruzegea amemwambia waziri kuwa wamepokea maelekezo na kwamba bodi hiyo ina wajibu wa kutoa fursa kwa wananchi kutumia maktaba za umma ili kujipatia elimu, maarifa na taarifa mbalimbali zitakazosaidia kujikwamua katika umasikini, ujinga na kujipatia maendeleo.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji amesema majukumu ya kisheria ya Bodi ni pamoja na kuanzisha, kuongoza, kuendesha, kutunza na kuendeleza maktaba zote za umma nchini kuanzia ngazi za wilaya, mikoa hadi Tarafa lakini pia kuupatia umma wa watanzania taarifa mbalimbali zilizokusanywa kutoka katika ulimwengu mpana wa maarifa.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiwa na Mkurugrenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Dkt. Mboni Ruzegea akikagua Ukumbi wa Mikutano wa Maktaba ya Taifa kabla ya kuzungumza  na Menejimenti na watumishi wa bodi hiyo  jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akisoma  kitabu mara baada ya kutembelea Maktaba ya Taifa  jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo,wakiangalia Vitabu kwenye Maktaba ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo,akisoma kitaba kwenye Maktaba ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiteta jambo na  Mkurugrenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Dkt. Mboni Ruzegea mara baada ya kutembelea  Maktaba ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Share:

MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MASENGWA II, RUWASA WAPONGEZWA

Mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa akishuka kwenye tangi la Maji lililopo Ishinabulandi kata ya Samuye katika Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim ameweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji Masengwa - Bubale awamu ya pili kata ya Masengwa na Samuye Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga unaotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) unaotarajia kunufaisha zaidi ya watu 24,252 ukigharimu shilingi 4,751,365,960.00

Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Abdalla Shaib Kaim ameweka jiwe la msingi la mradi huo leo Jumamosi Julai 29,2023 baada ya kukagua na kujiridhisha kuhusu ubora na gharama za mradi huo.

"Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 zimefika katika mradi huu,  tumepokea taarifa ya mradi, Mwenge wa Uhuru umefanya ukaguzi wa kina kuhusu nyaraka zinazohusiana na mradi, umetembelea na kujionea miundombinu ujenzi ulipofikia. Tunafanya haya ili kuhakikisha tunabaini ubora na viwango vinavyotakiwa katika mradi husika, thamani ya pesa iliyotumika kama inaaksi maendeleo na uhalisia  wa matokeo ya mradi. Lengo kuu ni kuhakikisha fedha zinazotolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mapenzi makubwa ya kuwaletea Watanzania maendeleo yanayolenga kuleta tija na afya kwa maslahi mapana ya Watanzania na siyo maslahi ya mtu binafsi",amesema Kaimu.

"Baada ya ukaguzi wa kina ambao Mwenge wa Uhuru umefanya, kwanza kwa upande wa nyaraka, nyaraka tumejiridhisha zote ziko vizuri hongereni sana, mradi unaendelea vizuri, kazi kubwa kazi nzuri imefanyika. Tunaamini mradi huu unaenda kutimiza dira na maono ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo wananchi kwa kusogeza kwa ukaribu zaidi upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama na unalenga kumtua mama ndoo kichwani. Tunawashukuru RUWASA kwa kazi nzuri, hongereni sana. Tunaweka jiwe la msingi",ameongeza Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim.
Akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa mradi huo, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Shinyanga, Emaeli Songelaeli Nkopi amesema lengo la mradi huu ni kutoa huduma ya maji kwa wananchi wa katika vijiji vya Ishinabulandi, Bubale, Isela, Idodoma, Ibanza, Mwamala "B", Ibingo na Ng'wang'halanga.

Amesema mradi huo hadi kukamilika unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi 4,751,365,960.00 (Bila VAT) ambapo chanzo cha fedha hizo ni Serikali Kuu kupitia mfuko wa Maji wa Taifa (NWF).

“Ujenzi wa mradi huu ulianza tarehe 25/02/2022 na unatarajia kukamilika tarehe 24/08/2023 na unatekelezwa na Mkandarasi mzawa Mbeso Construction Company wa Dar-es-Salaam. Mradi huu unahusisha ujenzi wa "off take" mbili, DP 46 za maji, matangi mawili ya maji (Ishinabuladi lita 100,000 na Mwamala lita 200,000), mtandao wa bomba za ukubwa tofauti kuanzia 32mm hadi 250mm wenye urefu wa km 71.82 na utasimamiwa na kuendeshwa na CBWSO”,ameeleza Mhandisi Nkopi.

Ameongeza kuwa mradi wa maji Masengwa II umetekelezwa kutokana na uhitaji wa huduma ya maji kwa wananchi, utekelezaji wa Sera ya Maji ya Mwaka 2002, utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Maji na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2020-2025.

Mhandisi Nkopi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutekeleza mradi huu wa kimkakati ambao utawanufaisha zaidi ya watu 24,252.

Nao wakazi wa Ishinabulandi wameishukuru serikali kwa ujenzi wa mradi wa maji hali ambayo itawasogezea karibu huduma ya maji kwani wamekuwa wakitumia maji yasiyo salama na kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma ya maji.

Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 ni "Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa ustawi wa viumbe hai na Uchumi wa Taifa”.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim akikata utepe wakati akiweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili katika kijiji cha Ishinabulandi kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga leo Jumamosi Julai 29,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim akiweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili katika kijiji cha Ishinabulandi kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga

Afisa Ustawi wa Jamii RUWASA Kishapu, Neema Mwaipopo akisoma maandishi baada ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili katika kijiji cha Ishinabulandi kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya tangi la Maji lililopo Ishinabulandi katika Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Wananchi wakiwa kwenye tangi la Maji lililopo Ishinabulandi katika Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakati Mwenge wa Uhuru ukiweka jiwe la Msingi.
Muonekano wa sehemu ya tangi la Maji lililopo Ishinabulandi katika Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa akishuka kwenye tangi la Maji lililopo Ishinabulandi katika Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa akishuka kwenye tangi la Maji lililopo Ishinabulandi katika Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Shinyanga, Emaeli Songelaeli Nkopi (kulia) akielezea kuhusu Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Shinyanga, Emaeli Songelaeli Nkopi (kulia) akielezea kuhusu Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Shinyanga, Emaeli Songelaeli Nkopi (kushoto) akielezea kuhusu Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Shinyanga, Emaeli Songelaeli Nkopi akielezea kuhusu Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Shinyanga, Emaeli Songelaeli Nkopi (katikati) akielezea kuhusu Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Shinyanga, Emaeli Songelaeli Nkopi akisoma taarifa ya ujenzi wa Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Shinyanga, Emaeli Songelaeli Nkopi akisoma taarifa ya ujenzi wa Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwenye Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum akizungumza kwenye Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim akizungumza kwenye Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga

Mmoja wa wananchi akiishukuru serikali kwa kuwajengea Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Mmoja wa wananchi akiishukuru serikali kwa kuwajengea Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Mwenge wa Uhuru ukiondoka katika Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Mwenge wa Uhuru ukiondoka katika Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Wafanyakazi wa RUWASA wakipiga picha ya kumbukumbu katika Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Wafanyakazi wa RUWASA wakipiga picha ya kumbukumbu katika Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Viongozi wa RUWASA wakipiga picha ya kumbukumbu katika Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga

Wafanyakazi wa RUWASA, CBWSO wakipiga picha ya kumbukumbu katika Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya tangi la Maji lililopo Ishinabulandi katika Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger