Saturday, 31 July 2021

BROTHERHOOD SURVEY SERVICES YATUMIA MAONESHO SHINYANGA KUTANGAZA MCHONGO WA VIWANJA IBADAKULI

Afisa Masoko wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Victoria Mahindi akionesha ramani mahali ulipo mradi wao wa uuzaji wa Viwanja ‘Diamond City Project’ katika kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited ya Mjini Shinyanga imeshiriki Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga kwa kuonesha huduma wanazotoa pamoja na kuwatangazia wananchi kuhusu mradi wao wa uuzaji wa Viwanja ‘Diamond City Project’ unaopatikana katika kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayoongozwa na kauli mbiu “Uwekezaji wa Madini na Viwanda Shinyanga kwa Uchumi Endelevu” yameanza tarehe 23 Julai, yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 1 Agosti, 2021 katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza leo Jumamosi Julai 31,2021 Afisa Masoko wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Victoria Mahindi amesema Kampuni yao inajihusisha na Uendelezaji wa ardhi, ushauri kuhusu masuala ya ardhi, usimamizi wa mali yakiwemo majengo, magari na viwanja, ukusanyaji wa ushuru na mikopo, udalali, uchoraji wa ramani za majengo, uuzaji wa vifaa vya ujenzi pamoja na kufanya tafiti mbalimbali.

Amesema Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Ltd imeshiriki kwenye Maonesho hayo kwa ajili ya kuonesha huduma wanazozitoa.

“Kwenye maonesho haya pia tumekuja kuwatangazia wananchi kuhusu mradi wetu wa uuzaji Viwanja unaojulikana kwa jina la Diamond City Project unaopatikana katika kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga",amesema.

“Mradi huu wa viwanja upo Kilomita 8 kutoka Mjini Shinyanga na mita 500 kutoka barabara kuu ya Shinyanga - Mwanza. Katika mradi huu tunauza viwanja kwa bei nafuu kuanzia shilingi 540,000/= na unaweza kulipa kidogo kidogo hadi miezi sita. Viwanja vimepimwa na pia Kampuni yetu itafuatilia upatikanaji wa Hati Miliki ya Kiwanja chako kama utahitaji”,ameongeza Victoria.

Eneo la mradi huo wa uuzaji viwanja lipo jirani na mahali patakapojengwa Stendi Kuu ya Mabasi Mkoa wa Shinyanga, Ibadakuli eneo ambalo ni zuri kwa uwekezaji wa biashara na viwanda vidogo vidogo lakini rafiki kwa makazi na tayari kuna huduma ya umeme ,maji na zahanati ya Ibadakuli.

Ofisi za Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited zipo Mjini Shinyanga jengo la NSSF Mafao ghorofa ya Pili Wasiliana nao zaidi kwa simu namba 0746633364 ,0768992606, 0754 763263,0757462260 au Email
 info@brotherhoodsurveyservices.com
Afisa Masoko wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Victoria Mahindi akionesha ramani mahali ulipo mradi wao wa uuzaji wa Viwanja ‘Diamond City Project’ katika kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga leo Julai 31,2021 kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Masoko wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Victoria Mahindi akionesha ramani  ya nyumba kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Victoria Mahindi akielezea kuhusu huduma zinazotolewa na Kampuni yao kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Victoria Mahindi akiwakaribisha wananchi kuchangamkia fursa ya viwanja wanavyouza kupitia mradi wao wa uuzaji wa Viwanja ‘Diamond City Project’ unaopatikana katika kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Ofisi za Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited zipo Mjini Shinyanga jengo la NSSF Mafao ghorofa ya Pili Wasiliana nao zaidi kwa simu namba 0746633364 ,07689926060754 763263,0757462260 au Email
 info@brotherhoodsurveyservices.com


Share:

Maelekezo 10 ya Waziri Ummy kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu ametoa maelekezo 10 kwa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya ya kuimarisha ukusanyaji mapato na upelekaji wa fedha za maendeleo kwenye  miradi inayogusa wananchi.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu matumizi na mapato ya ndani ya Halmashuari hizo kwa mwaka 2020/21, Mhe.Waziri Ummy amezitaka Halmashauri ziendelee kubuni vyanzo vipya vya mapato ya ndani ambavyo haviitakuwa kero kwa wananchi ili kuongeza uwezo wa utoaji huduma kwa wananchi hususani huduma bora za Afya, Elimu na Miudombinu ya Barabara.

Pia, amesema Halmashauri ziimarishe usimamizi wa ukusanyaji wa mapato ya ndani ikiwa ni pamoja na matumizi ya mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa mapato ili kuondoa mianya ya uvujaji wa mapato na kusisitiza kila chanzo kikusanywe kwa kutumia POS machine ili kudhibiti upotevu huo.

BONYEZA HAPA KUJUA VITUO VITAKAVYOTOA CHANJO YA CORONA TANZANIA

“Halmashauri zihakikishe kuwa fedha za makusanyo ya ndani zinazokusanywa zinapelekwa benki ndani ya masaa 24 baada ya kuzikusanya. Ni marufuku na ni kosa la kisheria kwa Halmashauri kutumia fedha zilizokusanywa kabla ya kuzipeleka benki (fedha mbichi) kwa sababu yoyote ile,”amesema.

Amesisitiza Halmashauri zihakikishe zinapeleka na kutumia angalau asilimia 40 ya mapato yaliyokusanywa (kwa Halmashauri zinazokusanya chini ya Shilingi bilioni 5 kwa mwaka) na asilimia 60 (kwa Halmashauri zinazokusanya zaidi ya Shilingi bilioni 5 kwa mwaka) kwenye miradi ya maendeleo ili kutatua kero za wananchi hususan kuboresha huduma za Afya, Elimu na miundombinu ya barabara. Fedha hizi zitumike kwenye miradi yenye tija na inayogusa moja kwa moja wananchi na sio kugharamia semina, vikao, safari na mambo mengine yasiyogusa wanananchi moja kwa moja.

 Aidha, amesema kwa Halmashauri zenye makusanyo kuanzia bilioni 5 na zaidi kwa mwaka, zihakikishe zinatumia angalau asilimia 10 ya sehemu ya fedha zao za maendeleo kwenye uboreshaji wa Miundombinu ya barabara kupitia TARURA.

“Ninazitaka Halmashauri kuhakikisha fedha za mapato ya ndani zinatumika kutekeleza na kukamilisha miradi kwa asilimia 100 ili wananchi waweze kuona faida za mapato ya ndani na hatimaye kuongeza mwamko wa ulipaji wa kodi na ushuru,”amesema.

Mhe. Waziri Ummy amesema Halmashauri zihakikishe zinapeleka asilimia 10 ya fedha za mikopo ya Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kwenye shughuli zenye tija kama ilivyoelekezwa na Mh.Rais Samia Suluhu Hassan na katika hilo Halmashauri zihakikishe angalau asilimia 60 ya fedha za mikopo zinatolewa kwenye Vikundi hivyo.

“Halmashauri zihakikishe zinakamilisha miradi ambayo haijakamilika (viporo) kabla ya kuanzisha miradi mipya, Halmashauri zitumie sehemu ya fedha za matumizi ya kawaida kutoka kwenye mapato ya ndani ili kulipa madeni na hatimaye kuondoa malimbikizo ya madeni yasiyokuwa na msingi,”amesema.

Amehimiza Mabaraza ya Madiwani yahakikishe yanasimamia ipasavyo matumizi ya fedha za Halmashauri ili kupata thamani halisi ya fedha zinazotumika na kwamba yana wajibu wa kuhakisha fedha zinatumika kwenye miradi ya maendeleo yenye tija na manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi.

 Kuhusu maelekezo kwa Mikoa, Mhe.Waziri huyo amesema Sekretarieti za Mikoa zifanye ufuatiliaji wa ukusanyaji wa mapato ya ndani na matumizi ya mapato hayo kwa Halmashauri zilizo ndani ya Mikoa yenu mara kwa mara ili kujiridhisha na ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri pamoja na matumizi yake na kuwasilisha taarifa za utekelezaji Ofisi ya Rais – TAMISEMI kila robo mwaka kabla ya tarehe 20 baad ya robo husika kuisha.

“Sekretarieti za Mikoa zifanye ufuatiliaji wa fedha za miradi inayotekelezwa kwa mapato ya ndani iliyopo kwenye Halmashauri zao ili kujiridhisha na ubora wa Miradi inayotekelezwa. Aidha Sekretariat zifanye ufuatiliaji wa kina wa miradi inayotekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu na wadau wengine,”amesema.



Share:

AFARIKI AKILALA NA JIKO LA MKAA KIBANDANI KUWAHI WATEJA




Na Amiri Kilagalila,Njombe
Editha Mangita (40) mkazi wa mtaa wa Matema kata ya Maguvani mjini Makambako amefariki dunia baada ya kujifungia na jiko la mkaa katika kibanda chake cha biashara.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amesema tukio hilo limetokea Julai 28,2021 ambapo marehemu Editha aliamua kubaki na kulala katika kibanda chake cha biashara ili kuwahi wateja wake wa asubuhi.

Aidha Kamanda Issa amewataka wananchi wa mkoa wa Njombe kuacha kulala na majiko ya mkaa ndani huku akitoa wito kwa wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu kuhusu madhara hayo Ili jamii.

Hivi karibuni mjini Njombe kulitokea kifo cha watu wawili wapenzi baada ya kulala na jiko la mkaa ili kupunguza baridi katika chumba chao.

Kamanda Issa ametaja tukio lingine la mwanamke mmoja Imelda Mgeni ametelekeza mtoto mwenye umri wa miezi mitatu kwa mume wake naye kwenda kusikojulikana.

Share:

TAZAMA HAPA ORODHA YA VITUO VYA KUTOLEA CHANJO YA CORONA KATIKA MIKOA YOTE TANZANIA

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Prof.Abel Makubi akionesha chanjo aina ya Jonson Jonson kwa Wana habari.
**
Baada ya taasisi tano zilizo chini ya wizara ya afya kufanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa chanjo za Johnson & Johnson ni salama kutumika kwa Watanzania, zimeanza kusafirishwa  katika mikoa 26 kwa ajili ya makundi matatu yaliyopewa kipaumbele wakiwemo watoa huduma za afya, wazee na wenye magonjwa sugu.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 31,2021











Share:

Friday, 30 July 2021

WANANCHI WAMIMINIKA BANDA LA CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO KUPIMA AFYA MAONESHO SHINYANGA


Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kinachomilikiwa na Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga kimeshiriki Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga kwa kuonesha shughuli wanazofanya chuoni hapo, kutoa elimu ya afya pamoja na kutoa huduma kwa jamii  kwa kupima afya ikiwemo upimaji wa  Sukari, Shinikizo la damu na malaria.

Wananchi waliotembelea banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto  kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yaliyoanza Julai 23,2021 na kutarajiwa kuhitimishwa Agosti 1, 2021 katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga, wamechangamkia fursa zinazotolewa na chuo hicho ikiwa ni pamoja na kupima afya zao bure.

Akizungumza leo Ijumaa Julai 30,2021 , Mkuu wwa Idara ya Famasi katika Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Paschal Marusu amewahamasisha wananchi kutembelea banda lao ili wapime afya zao bure.

"Tunashiriki maonesho haya kwa kuonesha shughuli zetu za kawaida chuoni na aina ya mafunzo tunayotoa, tunatoa elimu ya afya pamoja na kutoa huduma kwa jamii za upimaji wa Sukari, Shinikizo la damu na kipimo cha haraka cha Malaria",amesema Marusu.

"Huduma hii ya upimaji afya bure katika banda letu ni Ofa maalumu katika kusherehekea Mahafali ya 9 kwenye Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto yatakayofanyika Siku ya Ijumaa Agosti 6,2021",ameongeza Marusu.

Marusu ametumia fursa hiyo kuwakaribisha watu wote wanaotaka kusoma mafunzo ya Sayansi za Afya katika kada za Nursing, Maabara, Utabibu, Famasia na Mafunzo ya Maabara Viwandani.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI 
Mkuu wwa Idara ya Famasi katika Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Paschal Marusu akizungumza kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wwa Idara ya Famasi katika Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Paschal Marusu akizungumza kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. Kushoto ni Naibu Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Michael Henerco. Kulia ni Mteknolojia Maabara za Afya katika Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Daniel Mapungu Shija.
Mteknolojia Maabara za Afya katika Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Daniel Mapungu Shija akionesha kipimo cha haraka cha Malaria kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Kulia ni Muuguzi wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto,Peris Nderitu akionesha namna ya kumsaidia kupumua mtoto baada ya mama kujifungua halafu mtoto anashindwa kupumua kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.  
Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Wananchi wakiwa nje ya banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Naibu Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Michael Henerco na Muuguzi wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto,Peris Nderitu wakiwa kwenye banda la chuo chao kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Shinyanga.
Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu katika Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto akiwaonesha wanafunzi hatua za kufuata ukiwa unanawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Wanafunzi wakijifunza masuala ya afya kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

RAIS SAMIA AMTEUA MATIVILA KUWA MTENDAJI MKUU WA TANROADS, PROF. MGAYA MWENYEKITI TAFICO




Rais Samia leo Julai 30, 2021 amemteua, Rogatus Hussein Mativila kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na amemteua, Prof. Yunus Daudi Mgaya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uvuvi la Tanzania (Tanzania Fisheries Corporation-TAFICO) Uteuzi huo umeanza leo Julai 28, 2021
Share:

TANZANIA U-23 MABINGWA CECAFA 2021



Timu ya Taifa ya Tanzania imtwaa Ubingwa wa Michuano ya Kombe la Chalenji ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kwa vijana chini ya umri wa miaka 23 kwa mwaka 2021.

Tanzania ilikuwa ikipepetana na Burundi ambapo matokeo yalikuwa suluhu ya bilabial katika dakika 90 hivyo kwenda kwenye matuta ya penalty ndipo Tanzania ikabuka na ushindi wa penalti 6 kwa 5 za Burundi.

Mara ya mwisho Tanzania kuchukua kombe hilo ni mwaka 2010 huku Burundi ikiwa haijawahi kuchukua zaidi ya kuishia nafasi ya pili mwaka 2013.

Timu tisa zilishiriki michuano hiyo ambazo ni Tanzania, Burundi, Kenya, Uganda, Ethiopia, Eritrea, DR Congo, Sudan Kusini na Djibouti zilizogawanywa kwenye makundi matatu yenye timu tatu tatu kila moja.

Stori na Sifael Paul


Share:

WAZIRI KALEMANI AAGIZA WAKANDARASI KUPELEKA UMEME KATIKA MAENEO YA VIWANDA VIJIJINI

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani(Kulia) akizungumza na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango(kushoto) wakati wa uzinduzi wa Mradi wa umeme wa Ujazilizi Fungu la Pili A Ngazi ya Mkoa uliofanyika wilayani Same, Julai 29,2021.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Kalemane baada ya kuwakabidhi kifaa cha UMETA kwa ajili ya kuunganishiwa umeme katika shule yao wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Ujazilizi Fungu la Pili A ngazi ya Mkoa uliofanyika katika kitongoji cha Mheza wilayani Same, Julai 29,2021.
Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa umeme wa Ujazilizi Fungu la Pili A ngazi ya Mkoa uliofanyika wilayani Same, Julai 29,2021 uliozinduliwa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani.
Baadhi ya wanafunzi na wananchi wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati akizundua Mradi wa umeme wa Ujazilizi Fungu la Pili A ngazi ya Mkoa uliofanyika wilayani Same, Julai 29,2021.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiwa na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango,wanafunzi pamoja na viongozi wa wilaya ya Same wakikata utepe kuwasha umeme katika Kijiji cha Kifaru wakati wa ziara ya uzinduzi wa Mradi wa umeme wa Ujazilizi Fungu la Pili ngazi ya Mkoa wa Kilimanjaro uliofanyika wilayani Same, Julai 29,2021.
Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango akisoma maelezo ya jiwe la msingi baada ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani kuzindua Mradi wa umeme wa Ujazilizi Fungu la Pili ngazi ya Mkoa uliofanyika wilayani Same, Julai 29,2021.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akipongezwa na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango mara baada ya kuzindua Mradi wa umeme wa Ujazilizi Fungu la Pili A Ngazi ya Mkoa Uliofanyika katika kitongoji cha Mheza, Julai 29,2021.

...............................

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani amewaagiza wakandarasi wanaojenga miundombinu ya kusambaza umeme vijijini kupeleka umeme katika maeoneo maalum ambayo yametengwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda.

Dkt. Kalemani alitoa agizo hilo wakati akizindua Mradi wa Ujazilizi Umeme Vijijini Fungu la Pili A ngazi ya mkoa uliofanyika Julai 29,2021 katika kijiji cha Mheza wilaya ya Same Mkoa wa Kilimanjaro.

Aidha, amewakumbusha viongozi wa Serikali za Mitaa katika ngazi ya kata na vijiji kutenga maeneo maalum ya uwekezaji wa viwanda ili yaweze kupelekewa miundombinu ya umeme wakati wa utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini. “Tumieni umeme kufanya biashara muongeze thamani ya mazao ya kilimo na mifugo kwa kuanzisha viwanda” alisisitiza.

Waziri Kalemani amesema Mradi huo utatekelezwa kwa muda miezi 12 na Serikali imetenga kiasi cha takribani Shilingi Bilioni 8.59 kwa ajili ya kuvifikishia umeme vitongoji ambavyo havina umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro katika fedha hizo Wilaya ya Same imetengewa zaidi ya Shilingi Bilioni 3.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Mhe. Anne Kilango Malecela ameishukuru Serikali kwa kupelekewa miradi hiyo ya kusambaza umeme vijijini na kuomba maeneo ambayo bado hayajafikishiwa umeme yapatiwe nishati hiyo.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger