Thursday, 28 February 2019

MAKUBWA YAIBUKA KIFO CHA RUGE MUTAHABA

Wengi walimfahamu Ruge Mutahaba kama mdau mkubwa wa burudani, lakini kifo chake kimeibua mengi makubwa aliyofanya nje ya nyanja hiyo.

Kutoka siasa, ujasiriamali, michezo, afya, mazingira, uchumi, utafutaji fursa hadi kujenga fikra chanya za maisha ni mambo yaliyoibuka baada ya kifo chake kilichotangazwa juzi jioni.

Hayo yamo katika salamu za rambirambi, mahojiano na watu mbalimbali waliofika nyumbani kwao Mikocheni kuomboleza, taarifa za vyombo tofauti vya habari na watu walioandika katika mitandao ya kijamii kuhusu maisha ya Ruge.


Ruge, mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, alifariki akiwa hospitalini nchini Afrika Kusini alikopelekwa kutibiwa takriban miezi minne iliyopita. Awali alipata matibabu nchini India.


Miongoni mwa waliotuma salamu na kufika nyumbani kutoa pole ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye amemtaja Ruge kuwa nguzo iliyosimamisha uelekeo wa vijana wa sasa.


Alisema Ruge aliwasaidia vijana kwa kuwapa mwanga wa kutimiza ndoto zao.


Hivyo ndivyo anavyomzungumzia January Makamba, ambaye ni Waziri wa Mazingira, Hamisi Kigwangalla (Maliasili na Utalii), Antony Mtaka (mkuu wa Mkoa wa Simiyu) na wengine waliowahi kufanya kazi na Ruge.


Waziri Mkuu alisema Ruge amefanya kazi kubwa tangu wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete ya ujenzi wa Taifa, hasa katika kunyanyua vijana.


“Pia ametoa mchango wake wa mali kuwasaidia Watanzania hasa vijana,” alisema Waziri Mkuu.


“Tumempoteza kijana wetu na wito wangu kwa Watanzania wote tuungane kwa pamoja kumuombea ndugu yetu Ruge.”


Naye Kigwangalla amemsifu kwa kujitoa kwake katika shughuli za ujenzi wa Taifa, akisema ingawa alikuwa mgonjwa, Ruge alishiriki kikamilifu kuiandaa programu maalumu ya utalii inayoitwa Tanzania Unforgettable.


“Ni mtu ambaye alijijengea jina kubwa katika tasnia ya habari, maendeleo, uchumi na burudani kwa ujumla,” amesema.


Alisema heshima hiyo ameipata kutokana na uwezo wake wa kubuni vitu mbalimbali, kiasi cha watu kudiriki kusema alikuwa injini ya Clouds.


“Ruge alifanya kazi kwa bidii usiku na mchana hata alipokuwa anaumwa,” alisema.


“Siku moja kabla ya mimi kupata ajali (Agosti 3,2018), tulikuwa Arusha na licha ya yeye kuwa India anaumwa, aliporejea nchini hata kabla hajaripoti kazini kwake alikuja Arusha na alishiriki kikamilifu.


“Ruge alikuwa mtetezi sana wa hoja mbalimbali zilizotolewa na wadau wa utalii. Alijitoa sana kwa kufanya kazi kwa bidii, kushirikiana na wadau na kwa kiasi kikubwa ameshiriki Tanzania Unforgettable kikamilifu.”


Naye Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson alimmwagia Ruge sifa kutokana na ubunifu, akisema asilimia kubwa ya mawazo ya kuanzishwa kwa taasisi ya Tulia Trust ni yake.


Alisema ni mtu aliyekuwa akiwapa moyo vijana na kuwataka watu wanaomlilia, waishi katika maneno yake.


“Nimepokea msiba wake kwa shukrani na huzuni kwa kuwa ni mtu ambaye alikuwa na mchango kubwa kwa watu wengi,” alisema Dk Tulia.


“Ni mtu ambaye ulikuwa unampigia simu na kumuomba mawazo yake, hivyo unafikiria leo mtu kama huyo hayupo, unawaza namna ya kutafuta rafiki mwingine wa aina yake.”


Waziri Ummy alisema amepata pigo kwa kuwa mikakati aliyokuwa nayo Ruge katika kuiboresha sekta ya afya nchini ni mikubwa.


Ummy alisema Ruge aligusa maisha ya wengi hasa vijana katika masuala mbalimbali hususani kufikisha ujumbe katika jamii hasa katika masuala ya afya ya uzazi kwa vijana na mapambano dhidi ya VVU.


Alisema katika kipindi cha uhai wake, Ruge alishirikiana na Serikali katika kufanya kampeni za masuala ya afya, kama ya Malaria na Nyumba ni Choo.




Pengo lake katika siasa


Mbali na masuala hayo, Ruge amezungumziwa kwa mtazamo chanya na vyama vya siasa, akielezewa kama mtu aliyeweka jukwaa la kukuza demokrasia na kupigania uhuru wa habari nchini.


Katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ali alisema Ruge alirahisisha shughuli za ujenzi wa chama hicho kupitia majukwaa mbalimbali ya vijana.


“Hata wakati wa kampeni za uchaguzi, mchango wake ulikuwa mkubwa kwa sababu vipindi vilivyokuwa vinaandaliwa vilikuwa vinaboresha demokrasia,” alisema Dk Bashiru.


“Kwa kuwa kipindi cha uchaguzi huwa kuna hamasa kubwa, tukikosa watu wabunifu inaweza kuwa balaa. Kwa hiyo aliunganisha watu na sera.”


Naye katibu mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji alisema Ruge alithubutu kuweka usawa katika jukwaa kwa vyama vya siasa kuuza sera zao katikati ya mazingira magumu ya uhuru wa vyombo vya habari.


“Pamoja na hali ya kidemokrasia na uminyaji wa vyombo vya habari, Ruge aliweza kutukaribisha na kutupatia jukwaa la kutangaza ajenda zetu kwa wananchi, tofauti na vyombo vingine vingi tu. Nilishiriki kipindi cha live 360. Ni uaminifu mkubwa sana alioonyesha kwa chama,” alisema.


“Kwa hiyo tumepata msiba, tasnia ya habari hususani upande wa vijana, itakuwa imeyumba sana. Kama chama tumepokea kwa masikitiko sana kifo chake, tunamwombea kwa Mungu ampumzishe kwa amani.”


Dk Mashinji amesema Ruge alitamani kuona wanasiasa wakishiriki siasa safi.


Ruge alitamani kuona uhuru wa habari ukiheshimiwa nchini.


“Nakumbuka hadi Clouds inavamiwa studio zake, alionyesha ujasiri na akaonyesha msimamo wa kutoyumbishwa katika uhuru wa habari. Kwa hiyo ni pengo kubwa sana kwa Taifa na tasnia ya wanahabari,” alisema.




Wanamichezo wamlilia


Ruge hajaliliwa na wanasia na wasanii pekee; bali hata wanamichezo.


Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah (Try Again) amemuelezea Ruge kuwa alikuwa mwanachama na mchezaji wa timu ya kundi la Friends of Simba na Simba Veterans.


“Amewahi kushiriki kuandaa sherehe ya Simba Day, vilevile niliwahi kumshauri aanzishe kampuni akanisikiliza na ndiye alinipa jina la Try Again ambalo linanitambulisha katika soka,” alisema Try Again.


“Ruge alikuwa na mchango mkubwa sana kwenye klabu yetu, alikuwa mjumbe wa kamati ya Masoko na Uwekezaji ya Simba,” alisema.


“Nikiwa mwenyekiti wa hiyo kamati, tumefanya naye mambo mengi ikiwamo kuandaa moja ya sherehe za Simba Day.”


Naye kaimu mwenyekiti wa Yanga, Samwel Lukumay alisema kifo cha Ruge ni pigo kwa Taifa kwa kuwa alikuwa na ushawishi na mchango mkubwa kwa vijana.


“Nakumbuka kuna mechi moja ya Simba na Yanga, Ruge alikuwa mstari wa mbele katika kuitangaza na ikateka nchi,” alisema.


Alisema mbali na mechi hiyo, Yanga ilikuwa ikishirikiana na Clouds Media katika matangazo na kupewa ushirikiano mkubwa na Ruge.


Naye bingwa wa zamani wa dunia wa mbio za mita 1500 na mshindi wa medali ya fedha ya Olimpiki ya 1980, Filbert Bayi alisema vijana wanapaswa kujifunza kutokana na kile alichokifanya Ruge katika tasnia tofauti.


“Wakiendeleza yale mazuri ambayo Ruge ameyafanya enzi za uhai wake, itakuwa ni shukrani tosha katika kumuenzi kwa mazuri yake, kwa kuwa alikuwa ni mtu ambaye alijitoa,” alisema Bayi ambaye ni Katibu Mkuu wa TOC.


Upande wa masumbwi pia walikuwa na kilio chao.


“Binafsi Ruge amenisimamia mapambano yangu kama matatu, hakuishia hapo hata mdogo wangu Mbwana ameandaliwa mapambano mengi tu na Ruge,” alisema nyota na bingwa wa zamani wa dunia wa WBU, Rashid Matumla.


“Alikuwa kijana mwenye mipango mingi ya maendeleo katika tasnia mbalimbali.” Bondia Francis Cheka alisema kwa mara ya kwanza pambano alilopigana kwenye ngumi za kulipwa na kupata fedha nyingi liliandaliwa na Prime Time Promotions ambako Ruge alihusika.


Chanzo- Mwananchi
Share:

MAPYA YAIBUKA HUKUMU YA WALIOTUPWA JELA MAISHA KWA KUCHOMA MOTO KITUO CHA POLISI


Baadhi ya watuhumiwa nane waliohukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kuchoma moto kituo cha polisi.

Wakili wa kujitegemea nchini Jebra Kambole amebainisha kusudio la kuwakatia rufaa baadhi ya waliohukumiwa kifungo cha maisha kwa kukutwa na hatia ya makosa 6 ikiwemo kuchoma moto kituo cha polisi Bunju A Jijini Dar es Salaam.

Licha ya Jebra Kambole, mawakili wengine watano wanakusudia kukata rufani kupinga hukumu ya kifungo cha maisha jela iliyotolewa wiki iliyopita na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, dhidi ya washtakiwa wanane.

Akizungumzia uamuzi huo Wakili Jebra Kambole amesema "kwa sasa tumeshatoa notisi ya kusudio la kukata rufani maana kikawaida inatakiwa utoe notisi ndani ya siku 10, baada ya hapo, utaratibu mwingine utafuata".

Mbali na kosa la kuchoma moto kituo cha polisi, vijana hao walihukumiwa kwa makosa sita yakiwamo ya kufanya mkusanyiko usio halali, kuharibu mali, kumwagia petroli na kuchoma moto Kituo cha Polisi cha Bunju A, mwaka 2015.

Awali kesi hiyo ilikuwa na washtakiwa 35, lakini baadaye Mahakama iliwaachia huru washtakiwa 17 na kati ya 18 waliobakia, wanane ndiyo walitiwa hatiani Ijumaa iliyopita, huku 10 wakiachiwa huru.

Waliokutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha ni Ramadhan Said (22), Veronica Ephraim (32), Yusuph Sugu (40), Juma Kozo (32), Rashid Liwima (29), Baraka Nkoko (23), Abuu Issa (36) na Abraham Mninga (23).
Share:

HUU HAPA WIMBO MAALUMU KUHUSU RUGE MUTAHABA

Wimbo Maalumu kutoka THT Group kwa Ajili ya Ruge Mutahaba unaitwa Asante Baba.
Advertisement
Share:

KIWANDA CHA VIATU CHA BORA CHATEKETEA KWA MOTO

Sehemu ya kiwanda cha viatu cha Bora kinawaka moto katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam. 

Chanzo bado hakijajulikana, lakini Kikosi cha zimamoto tayari kiko eneo la tukio na juhudi za kudhibiti moto huo zinaendelea.
Share:

Wednesday, 27 February 2019

Picha : MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AKIWA MKOANI SHINYANGA LEO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa haamini macho yake kuona uchafu uliokithiri mara baada ya kutembelea jiko la kupikia chakula cha wanafunzi wa Chuo Cha Ualimu SHYCOM wengine pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Taleck (kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho John Nandi. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Mwanafunzi wa Chuo Cha Ualimu SHYCOM Happyness Kasuku akimueleza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) changamoto ya maktaba ya kusomea ambayo ni ndogo na ina vitabu vichache.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akkizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu SHYCOM mkoani Shinyanga mara baada ya kutembelea chuo hicho na kukagua ukarabati na ujenzi wa miundombinu. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Edward K. Mulumba (kulia) wa Wizara ya Maji yanayohusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ofisi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Shinyanga (KASHWASA).
Picha ya Jengo la Madarasa ya Chuo cha Ualimu SHYCOM ambalo Makamu wa Rais alitembelea na kutaka kujua kwa nini ujenzi wake umesimama. Makamu wa Rais yupo mkoani Shinyanga katika ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo.
Wanafunzi Nchambi Nsile (kulia) anayesoma darasa la 7 akiwa amempakata mwenzake Nyazobe Sembe darasa la 4 wa Shule ya Msingi Jumuishi Buhangija wakati wa kumsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alitembelea shule hiyo na kufungua Bwalo. Makamu wa Rais yupo ziara ya kikazi mkoani Shinyanga. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Share:

Helb : The 2nd & Subsquent Application open Now 2019/2020

Helb : The 2nd & Subsquent Application open Now 2019/2020

HELB – Higher Education Loans Board is a state owned corporation established in 1995 and have grown to become the leading financiers of higher education in Kenya. Our mandate is to source funds and lend them as affordable loans, bursaries and scholarship to students pursuing higher education in recognized institution; which we have successfully done for the past 2 and a half decades

Moving to your next year in campus? Make your transition easier with the subsequent HELB loan. Apply today!

APPLY /REGISTER HERE

The post Helb : The 2nd & Subsquent Application open Now 2019/2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

SERIKALI YASIMAMISHA LESENI YA UCHAPISHAJI NA USAMBAZAJI WA GAZETI LA THE CITIZEN


Serikali imesimamisha leseni ya uchapishaji na usambazaji wa gazeti la The Citizen kwa siku saba kuanzia leo Jumatano, Februari 27, 2019.


Uamuzi huo uliotolewa na Idara ya Habari (Maelezo) unatokana na madai ya gazeti hilo la Kiingereza kuandika habari iliyohusu maoni ya wataalamu walioelezea kuporomoka kwa shilingi ya Tanzania na kuchapishwa Februari 23, 2019.

Barua ya Februari 27, 2019 ya kusimamishwa kwa The Citizen iliyosainiwa na msajili wa magazeti, Patrick Kipangula kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) inaeleza kuwa adhabu hiyo inahusu pia mtandao wa gazeti hilo.

“Katika habari hiyo kwa makusudi uliandika habari za uongo na upotoshaji kwa kuaminisha umma wa Watanzania na kwamba thamani ya Shilingi ya Tanzania imeporomoka ikilinganishwa na miaka mitatu iliyopita pasipo kufuata utaratibu wa kisheria na kanuni za fedha ambapo viwango vya fedha ya Tanzania hutolewa na Benki Kuu ya Tanzania,” inasema aya mmojawapo ya barua hiyo.

“Uamuzi wa kusimamisha kwa muda leseni hiyo unatokana na mwenendo na mtindo wa habari na makala ambao kwa kiasi kikubwa unakiuka misingi ya maadili ya taalamu ya habari kwa upotoshaji wa mara kwa mara wa taarifa zinazohusu Serikali na uchochezi bayana unaokiuka masharti ya leseni,” inasema aya nyingine katika hiyo iliyotumwa kwenda kwa Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications Limited (MCL).

Katika barua hiyo, Serikali imeeleza kuwa licha ya gazeti la The Citizen kuomba radhi mara kwa mara bado limeendelea na uandishi ule ule wenye utata na ikalitaka lijirekebishe na kuzingatia misingi ya taalamu ya habari na sheria za nchi.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari amesema licha ya habari hiyo, The Citizen limewahi kuchapisha habari nyingine inayokiuka misingi na maadili ya uandishi wa habari Julai 22, 2018. 

Habari hiyo iliyokuwa na kichwa cha habari ‘US Senator Raises Alarm on Tanzania” ilimnukuu seneta wa Jimbo la New Jersey nchini Marekani, Bob Menendez alieleza kuhusu mwelekeo wa ukuaji wa demokrasia nchini Tanzania.

Kufungiwa kwa gazeti la The Citizen, ambalo ni gazeti dada la Mwananchi, kwa siku saba kunamaanisha kuwa litarejea tena sokoni Alhamisi ijayo ya Machi 7, mwaka huu.

Mhariri Mtendaji Mkuu wa MCL, Bakari Machumu amesema wamepokea barua hiyo kwa mshtuko, lakini watafuata maelekezo ya Serikali.

“Tumepokea agizo hilo la Serikali kwa masikitiko, lakini kama kampuni daima tunaamini katika kufanya kazi kwa mujibu wa sheria, hivyo tutatumikia adhabu hiyo kama tulivyoelekezwa,” alisema Machumu.

Chanzo - Mwananchi

Share:

Picha : KIGWANGALLA AHANI MSIBA WA RUGE

Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefika nyumbani kwa familia ya Ruge Mutahaba na kutoa pole za msiba ambapo pia ameweza kumwelezea marehemu Ruge kama mtu mwenye uthubutu kwa jamii.

Dk. Kigwangalla ameweza kuonana na kutoa pole kwa wafiwa ndugu,jamaa na marafiki akiwemo Baba mzazi Mzee Mutahaba pamoja Mama wa Ruge Bi. Cristina Mutahaba na kutoa pole zake hizo pamoja na rambirambi alizokabidhi kwa Mama mzazi.

Dk.  Kigwangalla amemuelezea marehemu kama mtu wa kuigwa kwani alijituma katika kuhakikisha anatimiza malengo yake aliyopangiwa ama kujipangia. 

"Ruge alikuwa mtu wa watu na alisimama katika mipango sahihi hata nikamchagua kwenye Kamati za kuendeleza masuala ya Utalii ikiwemo ile ya Tanzania Unforgettable." alieleza Dk Kigwangalla. 

Aidha, Dk Kigwangalla ameweza kuungana na viongozi wengine pamoja na ndugu na jamaa.

Awali taaifa ya Msemaji wa Familia Bw. Anic Kashasha amesema kama mipango itakwenda kama ilivyopangwa mwili wa marehemu Ruge Mutahaba utawasili Ijumaa na utaagwa rasmi siku ya Jumamosi jijini Dar es salaam, Baada ya kuagwa utasafirishwa kwenda Bukoba siku ya jumapili na kuzikwa siku ya jumatatu huko Bukoba mkoani Kagera.

Na Andrew Chale  - Dar es salaam
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa pole kwa Mama mzazi wa Ruge Mutahaba alipoenda kutoa pole mapema leo Februari 27.2019.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Andrea Kigwangalla akiteta jambo na Mbunge pole wa Kigoma Zitto Kabwe katika msiba wa Ruge Mutahaba alipoenda kutoa pole mapema leo Februari 27.2019.
Share:

MWAKYEMBE AMLILIA RUGE


Share:

AZAM FC YAWAFUNGIA WACHEZAJI WAKE


Wachezaji wa Azama FC
Uongozi wa klabu ya Azam FC imesema kuwa kuanzia sasa haitoruhusu wachezaji wake kwenda kufanya majaribio katika klabu zingine na kama itawahitaji basi zinatakiwa kufuata utaratibu maalum.

Hayo yameelezwa na Afisa Habari wa klabu hiyo, Jaffar Iddy Maganga, akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa uongozi wa klabu hiyo hautaruhusu mchezaji yeyote wa timu yake hasa kutoka timu za vijana kwenda kufanya majaribio katika timu nyingine.

"Kwanza kabisa wanafahamu kuwa wachezaji wanaotoka hapa ni Superior kwasababu kuna kila kitu. Kwahiyo hatuwezi kupeleka timu ambayo tunajua kabisa uwezo wake ni mdogo, na sisi tunafuatilia lakini tunajua wenyewe jinsi gani tunafuatilia", amesema Jaffar Idd Maganga.

Hatua hiyo imefikiwa ili kuweza kujenga umara wa kikosi chake na kupoteza muda kwa wachezaji hao.

Kikosi cha Azam FC hivi sasa kipo chini ya kocha wa vijana chini ya miaka 20, Meja mstaafu Abdul Mingange na Idd Cheche wa timu ya vijana chini ya miaka 17, baada ya Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm kutimuliwa hivi karibuni baada ya mfululizo wa matokeo mabovu.
Share:

SERIKALI YATANGAZA NAFASI ZA AJIRA ZA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI..SOMA HAPA


Kuomba ajira bofya hapa 
Share:

SHIRECU YAPUNGUZA WATUMISHI NA KUWALIPA STAHIKI ZAO

Share:

BOSI WA CLOUDS : MSIBA WA RUGE HAUTAKUWA WA MAJONZI


Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga amesema kwamba msiba wa Ruge hautakuwa wa majonzi kama ilivyozoeleka, bali itakuwa ni kusherehekea maisha yake kama ambavyo mwenyewe alitaka iwe.

Kusaga amezungumza hayo akisema kwamba kabla Ruge hajafariki, aliwahi kusema kuwa ikitokea siku amekufa, basi watu wasihuzunike sana, bali washerehekee maisha yake na vile alivyo vifanya wakati yupo hai.

“Kuna kitu alikuwa akisisitiza, kwamba ikitokea bahati mbaya Mwenyezi Mungu amemchukua, tu-'celebrate' maisha yake, tu-'celebrate' alivyovifanya, kwa hiyo tutaanza maombolezo lakini yatakuwa ku-'celebrate' mazuri aliyoyafanya, hii alisisitiza wazi kabisa, na mimi kumpa heshima hiyo ni lazima tu-'celebrate' mengi mazuri aliyoyafanya”, amesema Kusaga.

Akiendelea kuzungumzia hilo Joseph Kusaga amesema kwamba Ruge amefanya mengi mazuri ambayo yalifaa kutunukiwa, huku akitoa shukrani kwa serikali kwa kuwa nao bega kwa bega, kwenye kipindi hiki kigumu kwao.

“Inaweza ikawa sio wakati mzuri wa kusema mengi, lakini Watanzania inabidi tujifunze kutoa tuzo au kitu chochote kizuri kwa mtu aliyefanya mambo mazuri, amefanya mengi mazuri kwenye tasnia hii na burudani, naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa serikali na viongozi wote ambao wamekuwa kwa kiasi kikubwa wamekuwa wako karibu sana kutu suport, ili kuhakikisha tunamponya na maisha yake yanaendelea”, amesema Kusaga.

Ruge Mutahaba amefariki jioni ya Februari 26 huko Afrika Kusini, akipatiwa matibabu ya figo aliyokuwa akisumbuliwa nayo.
Share:

WAZIRI MAKAMBA AANDIKA WARAKA MZITO KUHUSU RUGE MUTAHABA

Na January Makamba
Ndugu yangu Ruge, najua ndio umewasili huko upande wa pili na si ajabu una mambo mengi na bado unasalimiana na jamaa zetu wengi waliotangulia.

Lakini naomba uchukue muda wako kidogo kunisikiliza. Nimeumia sana na nimelia peke yangu kwamba umetuacha namna hii. Sawa, umeitwa kwa wakati wako na sisi hatuna kauli kwenye suala la wakati wa kuitwa lakini nilitegemea, na sikuwa na shaka kabisa, kwamba tutakamilisha yale mawazo yako mengi mazuri uliyoniambia. Sikuwa na shaka kwasababu nilishuhudia pale Hospitali ya Kairuki kabla hujaenda India, ulivyorudi kutoka India, na siku nimekuona Afrika Kusini, ulivyokuwa unapigana kupona — hadi madaktari wa Afrika Kusini wakakupa jina “Ruge, The Fighter”. Jina sahihi kabisa lililotafsiri harakati za maisha yako.

Unajua nini? Nilikuwa nangoja urudi Dar nikwambie nilichogundua mara ya mwisho nilivyokuona hospitali. Lakini ngoja tu nikwambie kabla sijaja huko uliko. Ile kiu kubwa ya kupona niliyoiona kwenye macho yako haikuwa kwa ajili yako wewe, bali kwa ajili ya kutoiangusha familia yako nzima iliyosimamisha kila kitu kukuuguza na Watanzania wote waliokuwa wanakuombea. Ulipigana kupona, sio kwa ajili yako, bali kwa ajili yetu. Hukuamka kitandani lakini hukushindwa mapambano kwasababu umeamkia ndani ya mioyo ya Watanzania. Huku tuliko karibu watu wote tunakumbuka ulivyotugusa. Jamaa yangu, tunakuomboleza wakati huu, halafu tutabaki tunafurahia nuru yako katika maisha ya wengi kwa urefu wa uhai wetu. Umekimbia mbio njema, umemaliza safari yako vyema.

Majonzi yangu ni kwamba umeondoka kabla sijalipa kwa ukamilifu deni langu kwako. Deni la upendo na urafiki wa kweli. Ulinipa heshima kubwa ya kuwa msiri wako — kwa kuniamini na kunielezea wasiwasi wako, ndoto zako, matumaini yako, harakati zako, mipango yako. Ulinipa heshima ya kunipa fursa ya kubishana nawe kuhusu mawazo na fikra zako.

Majonzi yangu ni kwamba kuna vitu fulani vikubwa na vizuri tulivipanga — mimi na marafiki na wadogo zako, kwa ajili yako, kwa staili yako — mapema mwezi Machi, ambavyo naamini vingekupa tabasamu. Kama unaweza, hapo ulipolala, tupe ishara tufanyeje.

Nafarijika kidogo kwamba nilipata nafasi ya kukukumbatia kwa mara ya mwisho. Sikujua kwamba tunaagana. Ulinishika mkono kwa nguvu, hukutaka kuuachia, na ulitabasamu niliposema nakungoja Dar tukae pale THT, kama kawaida yetu, kujadili mawazo na mipango yako mingi.

Ingawa umeshawasili huko upande wa pili, familia yako na watu wengi watauaga mwili wako kwa heshima kubwa. Utajengewa kaburi. Nadhani litawekwa marumaru. Lakini tukitaka kukusalimia tena hatutakutafuta kaburini kwako. Tutakutafuta kwenye nyoyo za watu uliowagusa na kuwasaidia. Na ni wengi kweli. Kumbukumbu yako itabaki kwenye nyoyo zao na kwenye mafanikio yao. Watoto wako hawapo peke yao. Watalia sana, lakini ni kwa muda tu; kwasababu watafunikwa kwa upendo wetu sote na watafarijika, na watakuwa na fahari, kwa jinsi unavyosemwa na unavyokumbukwa.

Ndugu yangu, nisikuchoshe. Mengine tutaongea tutakapokutana tena kwasababu kwa hakika sisi sote, mmoja mmoja na kwa wakati wetu, kwa kadri ya mipango ya yeye aliyetuumba, tutakufuata huko. Miaka yote nimekujua, sijawahi kukuona umepumzika. Pumzika kwa amani kwa sasa — na milele.

Ndimi, rafiki yako,
January Makamba
27 Februari 2019
Share:

WAZIRI MKUU : RUGE ALIKUWA TAYARI KUHAMASISHA VIJANA WAJITAMBUE

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Taifa limepoteza kijana aliyekuwa msatari wa mbele kuwahamasisha vijana wajitambue wawe wazalendo kwa nchi yao na watambue fursa za maendeleo zilizopo na wasiwe walalamikaji.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 27, alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema vijana nchini walikuwa na kiongozi aliyekuwa akiwaongoza kwa kuwafungua kimawazo na kuwaonesha fursa mbalimbali zitakazowawezesha kuwakwamua kifikra na kiuchumi ili waweze kujitegemea.

Waziri Mkuu amesema msiba huo ni wa wote kwani marehemu amefanya kazi kubwa ya kushirikiana na Serikali kuhamasisha vijana kujitambua na kutambua fursa zilizpo na kuzifanyia kazi. “Ruge ametoa mchango mkubwa kwa Taifa

Amesema marehemu Ruge katika kipindi cha uhai wake amefanya kazi kubwa kwa upande wa Serikali, kuanzia awamu ya nne hadi ya tano hususani katika suala la kuhamasisha vijana kujikwamua na kutokuwa wategemezi.

Pia, Waziri Mkuu amesema historia yake inaeleza namna alivyozunguka nchi nzima na kukutana na makundi ya vijana mbalimbali na kuwaelimisha namna ya kutambua fursa zilizopo nchini huku akiwahamasisha wawe wazalendo.

"Marehemu alikuwa akitoa hadi fedha zake binafsi kwa ajili ya kuwawezesha vijana hasa wale ambao hawakuwa na uwezo wa kiuchumi ili nao washiriki katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali na hatimaye waondokane na utegemezi.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wazazi, watoto wa marehemu pamoja na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa na subira na watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao. 

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, FEBRUARI 27, 2019.
Share:

SHIRIKA LA YOUNG WOMEN LEADERSHIP LATOA MAFUNZO KWA WALIMU KUHUSU AFYA YA UZAZI NA UKATILI WA KIJINSIA

Meneja Miradi wa shirika la Young Women Leadership (YWL),Veronica akizungumza wakati wa mafunzo kwa walimu wa Manispaa ya Shinyanga kuhusu afya ya uzazi kwa vijana na ukatili wa kijinsia -Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
*** 

Shirika la Young Women Leadership (YWL) limetoa mafunzo kwa walimu kutoka shule tisa za sekondari na msingi za Manispaa ya Shinyanga kuhusu afya ya uzazi kwa vijana na ukatili wa kijinsia kwa lengo la kuimarisha masuala ya usawa wa kijinsia na huduma za afya uzazi kwa wanafunzi.

Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza Februari 26 hadi 27,2019 yamefanyika katika ukumbi wa Simej Hoteli Mjini Shinyanga na
kukutanisha walimu 40 kutoka shule za sekondari Kizumbi,Mwawaza,Old Shinyanga,Town,Ibinzamata na shule za msingi Mwantini,Bugayambelele,Mwadui na Azimio.

Meneja Miradi wa shirika la YWL linalojihusisha na masuala ya uongozi kwa mabinti,kutokomeza mimba na ndoa za utotoni na kuimarisha uchumi kwa kaya, Veronica Massawe alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa ustawi wa wanafunzi shuleni na jamii kwa ujumla.

“Walimu wanakaa muda mwingi na watoto shuleni kuliko wazazi nyumbani,mafunzo haya yatasaidia kuimarisha usalama na afya za watoto wawapo shuleni na hata kwenye jamii”,
alieleza.

“Walimu hawa tuliowajengea uwezo katika masuala ya usawa wa kijinsia na huduma za afya ya uzazi wanatoka kwenye shule zenye wanafunzi tuliowalenga kuwafikia na wanapatiwa elimu hii, wanafunzi hao wengi wao wanatoka kwa wazazi na walezi wao ambao tunawapatia stadi za malezi na makuzi bora ya watoto na kuimarisha uchumi wa familia”,alifafanua Massawe.

Alisema YWL inatekeleza mradi wa Kutokomeza Mimba na Ndoa za Utotoni ulioanza Januari 2019 na utamalizika mwezi Desemba mwaka huu ukiwa na lengo la kuwafikia walimu,wazazi, wanafunzi na wahanga wa ndoa za utotoni ili kuwapa elimu kuhusu masuala ya afya ya uzazi,stadi za malezi na makuzi bora ya watoto na kuimarisha uchumi wa familia.

Nao washiriki wa mafunzo hayo waliwaomba viongozi wa serikali kutumia mikutano ya kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia huku walilishauri ngoma na jeshi la sungusungu vitumike kukusanya watu ili wapewe elimu hiyo.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja Miradi wa shirika la Young Women Leadership (YWL),Veronica Massawe akizungumza wakati wa mafunzo kwa walimu wa Manispaa ya Shinyanga kuhusu afya ya uzazi kwa vijana na ukatili wa kijinsia katika kumbi wa Simej Hoteli Mjini Shinyanga  -Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog


Meneja Miradi wa shirika la Young Women Leadership (YWL),Veronica Massawe akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

Walimu wakiwa ukumbini.

Mafunzo yanaendelea.

Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Agnes Ginethon akitoa mada kuhusu Mpango Mkakati wa Kupinga Ukatili kwa wanawake na watoto (MTAKUWWA).

Kulia ni Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Agnes Ginethon akieleza kuhusu sababu zinazochangia ukatili wa kijinsia kuwa ni umaskini,mila na desturi,ulevi kupindukia na madawa ya kulevya pamoja na mmomonyoko wa maadili katika jamii.

Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada ukumbini.
Mwalimu Jovini Bartholomew kutoka shule ya sekondari Ibinzamata akichangia hoja kuhusu masuala ya afya ya uzazi.
Mwalimu Grace John Bunga kutoka shule ya msingi Azimio akichangia hoja wakati wa mada kuhusu afya ya uzazi.
Mwalimu Dismas Humay kutoka shule ya msingi Bugayambelele akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.
Mwalimu Neema Mcharo kutoka shule ya sekondari Town akizungumza wakati wa mafunzo hayo na kuwahamasisha walimu kuwa na muda wa kuwajenga kusaikolojia wanafunzi.
Mwalimu Robert Mlela kutoka shule ya msingi Mwadui akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Picha ya pamoja washiriki wa mafunzo hayo.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Share:

RUGE MUTAHABA KUAGWA DAR JUMAMOSI, KUZIKWA JUMATATU BUKOBA


Familia ya Ruge Mutahaba imetoa utaratibu wa mazishi ya ndugu yao, ambayo yanatarajiwa kufanyika wiki ijayo mkoani Kagera.

Kwa mujibu wa Clouds Media Group, taarifa hizo zimetolewa na Ndugu Kashasha ambaye ni msemaji wa familia ya Ruge Mutahaba. Amesema kwamba kama mambo yakienda kama yalivyopangwa, mwili wa Ruge Mutahaba utafika Dar es salaam kutokea Afrika Kusini siku ya Ijumaa na iwapo ratiba itaenda sawa basi wakazi wa Dar es Salaam watatoa heshima za mwisho na kumuaga siku ya Jumamosi katika viwanja vya Karimjee.

Baada ya hapo familia imeamua kwamba Ruge atakwenda kuzikwa nyumbani kwao huko Bukoba siku ya Jumatatu.

Ruge amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 49, huku akiwa mmoja wa waasisi wa Clouds Media Group
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger