Saturday, 14 March 2026

SHUWASA YAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA, YAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA MAJI



Mkurugenzi wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) imekutana na Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Shinyanga kupitia Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) kujadili masuala mbalimbali yanayolenga kuboresha utoaji wa huduma za maji safi na usafi wa mazingira kwa wananchi.

Kikao hicho cha kazi kimefanyika leo Jumamosi Machi 14, 2026 mjini Shinyanga na kuongozwa na Mkurugenzi wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhandisi Katopola amesema SHUWASA inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha huduma za maji kwa wananchi wa Shinyanga, ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya maji, kupanua mtandao wa usambazaji na kuongeza upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Ameeleza kuwa ushirikiano kati ya SHUWASA na vyombo vya habari ni muhimu katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kuhusu huduma za maji, miradi inayoendelea pamoja na changamoto zinazojitokeza katika sekta hiyo.

Aidha amesisitiza kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kuelimisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya maji, kulinda miundombinu ya maji pamoja na kusaidia kufikisha maoni na changamoto za wananchi ili zipatiwe ufumbuzi kwa wakati.

Kwa upande wao, waandishi wa habari wameeleza utayari wa kuendelea kushirikiana na SHUWASA katika kuhabarisha umma kuhusu masuala ya maji, wakisema kuwa taarifa sahihi na kwa wakati zitasaidia kuongeza uelewa wa wananchi na kuchochea maboresho ya huduma kwa jamii.


Share:

PROF. SHEMDOE, BALOZI WA TANZANIA UFARANSA, WAJADILI MIKAKATI KUVUTIA UWEKEZAJI BONDE LA MSIMBAZI


Na OWM – TAMISEMI, Ufaransa

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amekutana na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe.Ali Mwadini, kujadili mikakati ya kuvutia na kutafuta wawekezaji katika eneo la Bonde  la Msimbazi lililopo jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamekubaliana kuwa na mpango madhubuti wa kutafuta wawekezaji wa kimataifa watakaoshiriki kuwekeza katika maendeleo ya bonde hilo, ambalo Serikali imeanza kulijenga ili kupunguza athari za mafuriko na wakati huo huo kufungua fursa mpya za uwekezaji na biashara.

Utekelezaji wa mpango huo unatarajiwa kuchochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi, kuboresha huduma za kijamii pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa wananchi wa jiji la Dar es Salaam na maeneo jirani, huku pia ukivutia wafanyabiashara na wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.

Prof. Shemdoe amefanya ziara katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa jana Machi 13, 2026, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha uwekezaji unaofanyika katika Bonde la Msimbazi unaleta manufaa makubwa kwa uchumi wa taifa na kuwawezesha wajasiriamali na wafanyabiashara wa jijini Dar es Salaam.

Uwekezaji unaotarajiwa katika bonde hilo ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya kuendeleza miundombinu ya kisasa mijini, kudhibiti mafuriko na kuifanya Dar es Salaam kuwa kitovu muhimu cha biashara na uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki.








Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MACHI 14,2026




magazeti







Share:

Friday, 13 March 2026

Video Mpya : GULI GULI - JADI

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger