Tuesday, 3 March 2026

FCC KUADHIMISHA SIKU YA HAKI YA MLAJI KWA KUTOA ELIMU KWA UMMA



Na Emmanuel Mbatilo, Dar es Salaam

Tume ya Ushindani (FCC) imetangaza kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Haki ya Mlaji Duniani kwa kuendesha kampeni maalum ya utoaji elimu kwa walaji na wafanyabiashara ili kuongeza uelewa wa haki na wajibu wao katika soko.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Khadija Ngasongwa amesema maadhimisho hayo yanalenga kuwawezesha walaji kufanya maamuzi sahihi wanaponunua bidhaa au huduma, pamoja na kuwahamasisha kuchukua hatua pale wanapobaini ukiukwaji wa sheria.

Amesema elimu hiyo pia itawalenga wafanyabiashara kwa kuwajengea uelewa kuhusu wajibu wao wa kumlinda mlaji na kuzingatia matakwa ya sheria katika utoaji wa bidhaa na huduma.

Kwa mujibu wa FCC, kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika Machi 31, 2026 katika Hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam, ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga.

Amesema katika maadhimisho ya mwaka huu, Tume hiyo imejikita kutoa elimu kupitia vipindi vya redio na televisheni, pamoja na majukwaa ya mitandao ya kijamii ili kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, FCC itaendesha kliniki za walaji katika mikoa ya Pwani, Dodoma, Musoma, Njombe na Tanga kwa lengo la kupokea na kushughulikia hoja, malalamiko na changamoto zinazowakabili walaji.

Sambamba na hilo, Machi 10, 2026 Tume hiyo itaendesha semina kwa wafanyabiashara na taasisi zinazotumia mikataba ya walaji (Standard Form Consumer Contracts) katika ofisi zake za Dar es Salaam, ili kuwajengea uelewa kuhusu umuhimu wa mikataba inayozingatia haki za mlaji.

Vilevile, Machi 11, 2026 kutafanyika semina kwa wadau wa sekta ya ujenzi wakiwemo wazalishaji wa nondo, bati, nyaya za umeme na rangi za majumbani, pamoja na vyama vya kibiashara na wadhibiti wa kisekta.

Mbali na semina hizo, FCC itatumia magari ya matangazo (road shows) kufikisha elimu kwa wananchi moja kwa moja katika maeneo yao.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo amewahimiza wananchi wenye changamoto zozote zinazohusiana na bidhaa au huduma kufuatilia vipindi vya elimu vitakavyorushwa na vyombo vya habari, kuhudhuria kliniki za walaji na kutumia fursa hiyo kuwasilisha malalamiko yao kwa ajili ya kupatiwa ufafanuzi au hatua stahiki.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MACHI 3,2026

Magazeti
 




Share:

Monday, 2 March 2026

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MACHI 2, 2026



Magazeti
Share:

MFANYABIASHARA AELEZA MBINU ALIZOTUMIA KULIPA MADENI YOTE KIBABE

 

Mfanyabiashara kutoka Nairobi ameelezea jinsi alivyohama kutoka deni kubwa hadi utulivu wa kifedha ndani ya kipindi kifupi cha kushangaza. Kwa miaka mingi, alipambana na mikopo mingi iliyochukuliwa ili kupanua biashara yake. Kwa bahati mbaya, changamoto za soko na malipo ya kuchelewa kutoka kwa wateja yalimfanya asiweze kulipa kwa wakati. Riba iliongezeka haraka, na wadai walimpigia simu kila mara. Baadhi hata walitishia kuchukua hatua za kisheria.

Shinikizo liliathiri biashara yake na maisha yake binafsi. Hakuweza kulala vizuri, akijua kwamba kila mwezi uliokuwa ukipita uliongeza mzigo wake wa kifedha. 

SOMA ZAIDI HAPA

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger