Saturday, 6 December 2025
“MAWAKILI MNA NAFASI KUBWA YA KUONDOA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZA KISHERIA KATIKA TAIFA HILI” – NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
Friday, 5 December 2025
MBUNGE MUTASINGWA AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI CHAKULA CHA PAMOJA, AHAMASISHA KALAMU ITUMIKE KULINDA JAMII
NDOTO MBAYA ZAFIKIA MWISHO: AMOS ASIMULIA MASAIBU YAKE

Kwa miaka mingi, maisha yangu, Amos, mwanakijiji wa makamo kutoka Kijiji kidogo cha Sokoine, yalikosa amani. Sikuwa mgonjwa kimwili, lakini ndani ya roho yangu kulikuwa na mateso makubwa. Usiku ulikuwa adui yangu mkubwa.
Kila nilipolala, nilikumbana na jinamizi lisiloelezeka—ndoto za ajabu, za kufisha moyo, ambazo zilinifanya niamke nikiwa nimechoka, nikiwa na hofu, na nimekata tamaa. Watu wengi waliniona kama mtu niliyepatwa na mikosi isiyokuwa ya kawaida, nilitafuta usaidizi kila kona bila kupata afadhali. Maisha yangu ya kila siku yalikuwa yameathirika sana kwa kukosa usingizi bora.
Mwezi mmoja uliopita, nilikuwa nimekaa kwenye kibaraza changu, nikivinjari mitandao ya kijamii, kujaribu kusahau uchovu wa mchana. Ghafla, jicho langu likatua kwenye tangazo la ajabu. Ilikuwa ni kuhusu Daktari Magongo, mganga wa asili maarufu kwa kusaidia watu waliokuwa wamekwama katika matatizo mbalimbali ya kiroho na kimwili. Jambo lililonivutia zaidi ni shuhuda nyingi zilizoelezea jinsi alivyomaliza matatizo ya usingizi na ndoto mbaya kwa wengine. Mwanzoni, nilisita, nikijua tayari nilitumia kiasi kikubwa cha pesa bila mafanikio. Lakini kutokana na ukweli kwamba nimekosa amani kwa muda mrefu, niliamua kujipa nafasi nyingine.
Nilituma ujumbe mfupi moja kwa moja kwa Daktari Magongo, nikieleza shida yangu kwa urefu. Alinijibu haraka sana kwa ukarimu na utulivu ulionipa tumaini jipya. Alinielekeza jinsi ya kufuata maelekezo machache, ambayo yote yaliendana na desturi na mila zetu. Sikulazimika kuondoka kijijini kwangu—utaratibu wote ulikuwa rahisi na wa kipekee.
Siku chache baada ya kuanza utaratibu wake, nilihisi tofauti. Mara ya kwanza, ndoto za ajabu zilipungua. Baadaye, zilibadilika na kuwa ndoto za kawaida. Ndani ya wiki mbili tu, jinamizi lilikuwa limeisha kabisa! Sasa ninaweza kulala fofofo, nikiwa na amani kamili usiku kucha. Ninaamka nikiwa na nguvu na furaha ya kuanza siku. Maisha yangu yamebadilika; uhusiano wangu na familia umekuwa mzuri, na kazi yangu inaendelea vizuri.
Siwezi kuelezea kwa maneno jinsi ninavyoshukuru kwa msaada wa Daktari Magongo. Magongo alinirudishia uhai na amani yangu. Kama wewe, ndugu yangu, unateseka kwa namna yoyote ile, iwe ni ndoto, bahati mbaya, au matatizo ya maisha, nakuhimiza sana umtafute Daktari Magongo. Yeye ni daktari wa asili anayeaminika na mwenye uwezo wa kusaidia wengi.
Thursday, 4 December 2025
WABEBA ZEGE WAYAKATAA MAANDAMANO YA DISEMBA 09, "TUMECHOKA"
MWIGULU AMALIZA UTATA: “WAMETENGEWA FEDHA ZA KUCHAFUA NCHI”, KAULI YAZUA HISIA KALI

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamejikita katika kuchambua chanzo cha vurugu, maslahi ya mataifa ya kigeni, na umuhimu wa busara katika kushughulikia masuala ya kitaifa.
Waziri Mkuu alisema kuwa wachochezi wamelenga kuharibu uchumi wa nchi na kurudisha nyuma maendeleo, huku lengo kuu likiwa ni kunyakua rasilimali adimu za Tanzania kama vile madini ya Uranium na maendeleo ya miradi ya gesi asilia.
Baada ya ufichuzi huo, maoni yamegawanyika kati ya wale wanaosisitiza umuhimu wa kufahamu maslahi ya Taifa na wale wanaotilia mkazo umakini wa vijana kujitambua.
Mchangiaji Oliver Kibua alikaribisha ufichuzi wa Serikali, akisisitiza umuhimu wa wananchi kujua chanzo na sababu ya vurugu hizo:"Afadhali kama inaweza kuwaambia wananchi sababu na chanzo cha yote wajue kipindi watu wanatumika na kuhadaika kuwa wapiganie haki kumbe wenzao wana wanachokitaka, na vurugu ikiwepo waumiao ni wananchi waliopo nchini na sio nje ya nchi."
Kibua pia alisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kufahamu kuwa hakuna taifa linaloingilia kati masuala ya nchi nyingine bila maslahi yao binafsi. Alihimiza, "Hao wanaojitambua waamke maana wanajitambua wao hawatambui ukweli wa mambo... think before you act."
Mchangiaji mwingine alitumia nafasi hiyo kukosoa matumizi ya lugha ya matusi na mihemko katika mijadala ya kitaifa, hasa kwa wale waliowahi kushika nyadhifa za uongozi.
"...Nikuona watu waliowahi kuwa madarakani mahali fulani wakakosana na waliowaweka madarakani wanavyokuwa hawajui kutumia lugha ya ushawishi na badala yake wanatukana... Si suala tu la kuamsha hisia bali ni suala la kusoma, kutafakari na kuona kweli katika muda sahihi na mazingira sahihi." alisema mmoja wa wachangiaji hao.
Mchangiaji huyo alitumia fumbo la kijadi kuhusu njiwa waliokosa ushauri na kufa ufukweni, akisisitiza kuwa nguvu (mihemko) bila maarifa (busara na ushauri) haisaidii. Alihimiza Watanzania kuchanganya maarifa ya kimagharibi na hekima za zamani ili kupata majibu sahihi.
Hata hivyo Rafael Valency Kwembe alionyesha imani kwa vijana wa Afrika, akisema:"Uzuri waafrika wa sasa tunajitambua sana, nyie pigeni ngonjera ila ukweli tunaujua na tunaufanyia kazi. Tunajua nani anazingua na nani yupo sahihi."
Mchangiaji mwingine aliunga mkono msimamo wa Serikali kwamba vurugu hizo zinaletwa na wanaharakati wanaolipwa na kuwahimiza Watanzania kuamka na kuchukua tahadhari, akisisitiza: "Ajira na uondoaji wa umaskini utapatikana tu nchi ikiwa na amani."
Kauli ya Waziri Mkuu inahimiza Watanzania kujiuliza maswali kuhusu maslahi na ajenda ya watu wanaotoa malipo hayo. Alionya kuwa mbinu hizi zimetumika katika nchi zingine barani Afrika, ambapo chokochoko huanzishwa ili kuruhusu uvurugaji na uchukuaji wa rasilimali, kabla ya wachochezi kuondoka baada ya rasilimali kuisha.



























